MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU'

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU'
#1
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'AIBU'

Neno aibu katika lugha ya Kiswahili ni nomino: [Ngeli: i-/zi-] yenye maana zifuatazo:

1. Jambo la kumtia mtu fedheha, jambo la kumvunjia mtu heshima.

2. Hali ya mtu kuvaa mavazi yasiyomsitiri vyema.

Kuna nahau: jitia aibu, tia mtu aibu: Alivua nguo mbele ya watu bila kuona aibu.

Kuna methali: Aibu ya maiti aijuaye mwosha: mtu anayezifahamu siri za mtu fulani ni yule aliyenaye karibu.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili aibu( soma: aybun/ayban/aybin عيب ) ni nomino ya Kiarabu yenye maana zifuatazo:

1. Kasoro, upungufu wa sifa: bidhwaa-atun laa aiba fiihaa بضاعة لا عيب فيها bidhaa isiyo kasoro yoyote.

2. Fedheha. Kuna msemo: Alfaqru Laysa Bi Aybin الفقر ليس بعيب ufukara si aibu.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili aybun/ayban/aybin lilipoingia katika  Kiswahili na kutoholewa kuwa neno la Kiswahili ' aibu ' halikubadili maana yake katika lugha yake asili - Kiarabu.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)