MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  

Password
  





Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 97 online users.
» 0 Member(s) | 95 Guest(s)
Bing, Google

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

 
  KISWAHILI NA UTANGAMANO WA AFRIKA MASHARIKI
Posted by: MwlMaeda - 09-07-2021, 03:29 PM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Dhima ya Kiswahili Afrika Mashariki katika Ujenzi wa Utangamano
Makala hii imejikita katika kuangalia nafasi ya kiswahili katika ujenzi wa utangamano wa nchi za Afrika Mashariki. Marejeleo ya makala haya ni mapitio ya kimaktaba ambayo yametokana na makala, tasnifu, kamusi elezi-huru na vitabu. Lugha ya kiswahili katika utendaji wa dhima ya kimawasiliano katika Afika Mashariki, imefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuwaunganisha wanajamii.  Lugha hii ya Kiswahili ni lugha yenye wazungumzaji wengi katika bara la Afika na imekuwa ikitumika katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile dini, harusi, sherehe na hata misiba. Hali kadhalika katika shughuli za kiuchumi kama biashara na masuala ya kidiplomasia. Pia shughuli za kidini kama vile nyimbo za kanisani kwa wakristo na Kaswida kwa Waislamu. Vilevile shughuli za kielimu, siasa na kiutamaduni kama jando, unyago na maombolezo.
Shughuli hizi ziliwaunganisha wanajamii katika mwingiliano wao wa majukumu ya kila siku. Kulikuwepo na taratibu mbalimbali zilizolinda mienendo na tabia za wanajamii hao. Taratibu hizo zimekuwa zikifuatwa na watu wote kwa kuwa waliziridhia. Jamii za Afrika Mashariki zilipoongezeka wazungumzaji wa Kiswahili waliongezeka pia na kuifanya lugha kusambaa. Katika Afrika, licha ya kuwepo kwa lahaja tofauti za Kiswahili lakini haikuwa kikwazo katika masikilizano na maelewano. Na ndio maana watu waliweza kuhusiana katika shughuli mbalimbali na kujenga utangamano baina yao.
Shughuli mbalimbali za kijamii, uchumi, biashara, elimu na nyinginezo zimeifanya jamii ya Afrika Mashariki kuwa na maridhiano na utangamano kwa sababu ya matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Pamoja na Kiswahili kuenea miongoni mwa jamii za Afrika Mashariki; ubinafsi, chuki, upendeleo katika baadhi ya mambo vimekuwa changamoto katika mahusiano ya mataifa ya Afrika Mashariki. Hata hivyo upendeleo, ubabe, ubaguzi na ukabila hautegemewi kuwa mfumo wa kudumu.
Katika katiba ya jumuia ya Afrika Mashariki Ibara ya 119 inayohusu utamaduni na michezo, nchi wanachama zimehimizwa kukuza ushirikiano na kuimarisha utamaduni na  michezo ikiwemo lugha ya Kiswahili kutumika kama lugha ya mawasiliano baina ya watu.  (Ripoti ya tume ya Blair kuhusu Afrika (Rasimu ya tafsiri) 2005
Maitaria & Monyanyi 2005 katika makala yao wanasema ‘hata hivyo, ni jambo mustahili kujaribu kujenga amani hiyo chini ya vivuli vya ukabila, ubahili na ufisadi. Mfano, katiba ya nchi ya Kenya, utangamano pia huhusisha kukuza na kulinda haki za binadamu kama zinavyofafanuliwa ili kuhakikisha uwiano mzuri miongoni mwa jamii mbalimbali.’
Aidha wasanii mbalimbali katika Afrika Mashariki wamekuwa wakitumia fasihi kueleza njia za ujenzi wa utangamano katika kazi zao za kisanii. Baadhi wamekuwa wakiandika mada mbalimbali ambazo zimeshughulikiwa na zilizokuwa zikihusiana na ujenzi wa jamii ya mshikamano.  Mfano wa kazi zilizoandikwa ni pamoja na uzindushi wa jamii, umoja katika jamii, masuala ya kisiasa, nafasi ya mwanamke katika jamii, umuhimu wa subira na matumizi ya kauli zinazofaa. Jamii haiwezi kuwa na utangamano unaofaa iwapo kuna mazonge na figisufigisu  zinazopingana na amani na upendo miongoni mwa wanajamii.
Lugha ya Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na waafrika walio wengi katika nchi za Tanzania, Kenya, Burundi, Rwanda Zambia, Sudani kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya kongo. Kutokana na idadi kubwa ya wazungumzaji wa Kiswahili mataifa ya ulaya huona sababu ya kuwafundisha watu wao Kiswahili ili waweze kuwekeza na kufanya tafiti katika nchi zinazozungumza lugha hii. Katika utafiti wake Ababaker, (2003) anaeleza kuwa mmoja wa wasailiwa wake walikiri kuwa lugha ya kiswahili inapendwa na wageni na ni rahisi kueleweka pindi wanapoamua kujifunza. (Ababaker E.A. 2003). Suala hili linaonesha dhima ya lugha katika hitaji la kukidhi mawasiliano.
Hata hivyo, ni jambo mustahili kujaribu kujenga amani hiyo chini ya vivuli vya ukabila, ubahili na ufisadi. Utangamano pia huhusisha kukuza na kulinda haki za binadamu kama zinavyofafanuliwa katika katiba za baadhi ya nchi za Afrika Mashariki ili kuhakikisha kunakuwepo na uwiano na maelewano mazuri miongoni mwa jamii mbalimbali.
Maitaria na Momanyi (2012) wanaeleza kuwa katika, kuhakikisha usalama wa mtu binafsi popote pale anapoishi na usalama wa umma kwa ujumla ni nguzo muhimu katika kujenga utangamano miongoni mwa watu wa asili mbalimbali. Utangamano mzuri pia ni ule unaotokana na uimarishaji wa uhuru wa kijamii na kisiasa utakaochangia kuwepo kwa jamii tulivu inayojiamini.
Attafuah (2012:89) kama alivyonukuliwa na Maitaria na Momanyi (2012) utangamano wa kitaifa unahusu uhusiano mzuri wa kijamii uliojengwa juu ya mhimili mkuu wa amani. Nakubaliana na hoja hii kwa vile ithibati ya kuwepo kwa utangamano mzuri miongoni mwa jamii za Afrika Mashariki ni amani. Uwepo wa amani utaleta ushirikiano na mahusiano yenye tija.
 
Athari zinazoweza kuharibu utangamano mzuri
Wakati mwingine mapingamizi ya utangamano mzuri na wenye manufaa huathiriwa na Utashi wa kisiasa.  Kwa mujibu wa Post na wenzake (2008) utashi wa kisiasa ni uungwaji mkono na viongozi wa kisiasa ambao husababisha mabadiliko ya kisera.
Charney (2009) naye anaelezea kuwa vikundi vinavyoongoza vyama vya siasa au serikali huweza kuwa na nguvu isiyoonekana nguvu hii ndiyo tunayosema ni utashi wa kisiasa amabayo husukuma na kusababisha maamuzi ya kisiasa. Maamuzi yanaweza kuwa na nguvu na kusababisha kutokuwepo kwa utangamano mzuri baina ya jamii za Afrika Mashariki.
MAREJELEO
Ripoti ya tume ya Blair kuhusu afrika (Rasimu ya tafsiri) 2005
https://repositories.lib.utexas.edu/bits.../5029/2389. pdf Dar es Salaam 2002 © Friedrich Ebert Stiftung East African Community 2002 ISBN 9987 22 036 3
Emad Ahmed Ababaker(2003) Chimbuko na Maendeleo ya Kiswahili na athari zake kwa jamii ya kiarabu: mtazamo wa vilughawiya jamii
 
Maitaria& Monyanyi 2005
Charney (2009)

Print this item

  HADHI NA NAFASI YA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI KITAIFA NA KIULIMWENGU
Posted by: MwlMaeda - 09-07-2021, 08:35 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Utangulizi
Kadri jamii inavyobadilika ndivyo na historia inavyobadilika. Yote haya yanakwenda katika usambamba sawia. Hivyo kilichopo leo kinaweza kuwa sawa au tofauti na cha jana na ukweli wa jana waweza kuwa ukweli au uongo wa leo au kesho, kwa maana hiyo jamii na historia yake si tuli (static).
Vivyo hivyo hata katika fasihi ya Kiswahili hususani fasihi andishi. Jinsi jamii inavyobadilika kifikra, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni ndivyo na fasihi inavyobadilika. Kwa mantiki hiyo ni dhahiri kwamba, hata hadhi na nafasi ya fasihi andishi ya leo yaweza kuwa sawa au tofauti na fasihi andishi ya jana, juzi au kesho.
Hivyo basi, fasihi andishi ya Kiswahili tunaweza kuifananisha na kinyonga kutokana na tabia zake za kubadilika badilika kulingana na mazingira fawafu. Mabadiliko hayo huleta tija kubwa sana kwa taifa na jamii kwa ujumla.
===================================================================
Fasili mbalimbali:
Awali ya yote ni vyema kujua fasili ya dhana za msingi zilizojitokeza katika mada tajwa. Dhana hizo ni pamoja na fasihi ya Kiswahili na fasihi andishi. Kwa kuanza na fasili ya fasihi ya Kiswahili;
Kwa mujibu wa Mulokozi (1996) akiwanukuu Syambo na Mazrui (1992); fasihi ya Kiswahili ni ile iliyoandikwa kwa Kiswahili tu, iwapo inazungumzia utamaduni wa Kiswahili au utamaduni mwiningineo. Maadam fasihi hiyo imetumia lugha ya Kiswahili na imefuata mbinu za ufasaha wa lugha hiyo, basi kwa tafsiri yao ni fasihi ya Kiswahili.
Fasili hii ina mapungufu yafuatayo:
o   Kwanza wanadai kuwa, fasihi ya Kiswahili ni lile tu iliyoandikwa yaani fasihi andishi. Kitu ambacho si cha kweli, kwani ipo fasihi simulizi ya Kiswahili. Hivyo fasili yao inashindwa kufafanua uwepo wa fasihi simulizi ya Kiswahili. Fasihi ambayo ndiyo kongwe kabisa ukilinganisha na fasihi andishi.
o   Pili wanadai kuwa kazi yoyote ile ikiandikwa kwa Kiswahili basi ni fasihi ya Kiswahili hata kama ikaelezea utamaduni wa watu wengine.
Hivyo basi, kutokana na mapungufu hayo, tunaweza kusema kwamba; fasihi ya Kiswahili ni ile ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili na inahusu au inaelezee utamaduni wa waswahili. Kwa mantiki hiyo, tunaweza kuhitimisha kuwa kuna fasihi ya Kiswahili na fasihi kwa Kiswahili.
Dhana ya pili ambayo nayo ni muhimu kufasili ni fasihi andishi ya Kiswahili. Hii tunaweza kuifasili kama ifuatavyo: Ni sanaa ya lugha iliyotungwa kwa lugha ya Kiswahili na kuwasilishwa kwa hadhira (wasomaji) kwa njia ya maandishi yenye kuelezea utamaduni na jadi wa waswahili.
Maana ya Hadhi na Nafasi ya fasihi andishi ya Kiswahili:
Hivyo basi, baada ya kuangalia fasili hizo sasa tuangalie kwa kina hadhi na nafasi ya fasihi ya Kiswahili kupitia mifano mbalimbali kutoka katika fasihi andishi ya Kiswahili.
Ili tuweze kujua hadhi ya fasihi ya Kiswahili ni vyema kwanza kujua nini maana ya hadhi. Hadhi katika maana ya kawaida ni ile hali inayomfanya mtu ajiheshimu na aheshimiwe; heshima.
Katika muktadha wa kifasihi tunaweza kusema kuwa, hadhi ya fasihi ya Kiswahili ni ile hali au namna ambavyo fasihi ya Kiswahili inavyochukuliwa/inavyoonekana. Je ina hadhi ya juu kati au chini?
Nadharia ya Msambao na hadhi ya fasihi andishi ya Kiswahili kitaifa na kiulimwengu:
Hivyo basi, tunapoizungumzia hadhi ya fasihi ya Kiswahili hususani fasihi andishi ya Kiswahili ni vyema kuhusianisha dhana hii na nadharia ya msambao “Diffusionism Theory”
 iliyoongozwa na mawazo ya ushawishi wa Grimms na Thompson.
Wanamsambao wanaamini kuwa, pale ambapo kazi mbili za fasihi toka jamii mbili tofauti zikifanana kimuundo au kimaudhui sababu ya ufanano huo ni kuwa, katika kipindi fulani hapo zamani, jamii hizo mbili ziliwahi kukutana kwa namna fulani na makutano baina ya jamii hizo yalisababisha hali ya kuazimiana kwa baadhi ya mila na desturi. Kwa hiyo uwepo wa fasihi andishi katika jamii ya waswahili  ulitokana na mwingiliano baina ya wageni na wenyeji.
Hiyo basi, uingiaji huu wa fasihi andishi katika jamii ya waswahili huonesha kuwa, hapo awali hakukuwa na fasihi andishi ya Kiswahili wala hadhi yake. Hadhi ya fasihi andishi ya Kiswahili imeanza kujitokeza baadaye na kujidhihirihsa kupitia nyanja mbalimbali kama vile elimu, utamaduni, jamii na hata siasa.
Kwa mantiki hiyo, tunaweza kuitazama hadhi ya fasihi andishi ya Kiswahili katika nyanja ya elimu kuanzia ngazi ya astashahada (cheti), stashahada, shahada, uzamili mpaka uzamifu.
Katika ngazi ya cheti yaani shule za msingi, sekondari na vyuo vya daraja la tatu fasihi andishi ya Kiswahili inahadhi kubwa sana. Kwa mfano, katika elimu ya msingi zipo kazi mbalimbali za fasihi andishi ya Kiswahili kama vile ushairi; mfano “Sizitaki Mbichi Hizi”, “Mama wa Kambo ni Mama”, “Karudi baba mmoja” na “Shairi la Moto na Maji”. Vilevile hata katika hadithi fupi kuna hadithi ya “Tola ala Gizani”, “Manenge na Mandawa”, “Nikiwa mkubwa” nk.
    Kwa upande wa elimu ya sekondari, kidato cha kwanza mpaka cha sita kazi nyingi za fasihi andishi ya Kiswahili zinajidhihirisha kama ifuatavyo: kwa mfano; ushairi, (Mashairi ya Chekacheka, Wasakatonge, Kimbunga, Mapenzi Bora, Diwani ya Mloka, nk.), riwaya (Kiu ya Haki, Takadini, Vuta Nkuvute, nk.), tamthilia (Kwenye Ukingo wa Thim, Orodha, Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe, Kivuli Kinaishi, Mfalme Juha, nk.)
    Pia hata katika ngazi ya elimu ya juu bado kazi hizi za fasihi andishi ya Kiswahili zina hadhi kubwa na umuhimu mkubwa sana katika jamii ndio maana tunaona zinajitokeza kata huku. Kwa mfano; kuna kazi za ushairi kama vile Dhifa, Tenzi tatu za kale, Insha na Mashairi, nk.
      Pia kuna riwaya kama vile: Moto wa Mianzi, Rosa Mistika, Nagona, Adili na Nduguze, Mzingile, Ufunguo Wenye Hazina nk.
      Vilevile kuna tamthilia kama vile; Amezidi, Aliyeonja Pepo, Jogoo Kijijini na Ngao ya Jadi,Ngoma ya Ng’wanamalundi, Lina Ubani, Mkutano wa Pili wa Ndege, nk.
   Licha ya hayo, pia tunaweza kuitazama hadhi ya fasihi andishi ya Kiswahili katika nyanja ya kijamii; fasihi andishi ya Kiswahili inahadhi kubwa sana. Hii ni kutokana na kazi mbalimbali zinazosomwa na jamii kupitia vitabu, majarida na hata magazeti. Kupitia kazi hizi hadithi mbalimbali zinasomwa na watu wanajipatia maarifa tofauti tofauti.
     Vilevile hadhi ya fasihi inajibainisha hata katika utamaduni kupitia kazi mbalimbali, kwa mfano; fasihi andishi imepiga hatua kubwa sana katika kuenzi na kuendeleza utamaduni na historia ya makabila mbalimbali kitaifa. Mfano; zipo kazi za fasihi andishi ya Kiswahili kama vile vitabu ambavyo huelezea utamaduni pamoja na historia ya waswahili. Kwa mfano; Moto wa Mianzi (historia ya wahehe), Utenzi wa Nyakirukibi (historia ya wahaya) nk.
     Licha ya fasihi ya Kiswahili kuwa na hadhi kubwa kitaifa kupitia nyanja hizo bado fasihi hii inaonesha juhudi za maendeleo yake na kuzidi kujipatia umaarufu katika shughuli mbalimbali kama ifuatavyo:
  Katika kuhitimisha maadhimisho ya miaka 50 ya Chuo Kikuu cha DSM tarehe 25/10/2012 waandishi mbalimbali wa fasihi andishi ya Kiswahili walitunukiwa tuzo ya uandishi bora. Kwa mfano; Ibrahimu Hussein, S. Mohammed Ahamed, Luhumbika, Penina Muhando na E. Kezilahabi.
      Vilevile katika kongamano la kimataifa la Kiswahili lililofanyika Blue Peal Hotel tarehe 04 hadi 06 /10/2012 waandishi mbalimbali walipata tuzo kutokana na kazi zao za uandishi. Pia robo tatu ya kazi zilizowasilishwa zilikuwa za fasihi andishi ya Kiswahili. Vilevile Balozi wa Kenya nchini Tanzania, alizindua kitabu chake alichokiandika kwa lugha ya Kiswahili kwenye Kongamano hilo.
   Pia fasihi imepelekea kupanuka kwa idara ya Kiswahili ambapo kumekuwa na idara mbili ambazo ni Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu pamoja na Idara ya Fasihi Mawasiliano na Uchapishaji. Maendeleo mazuri ya Idara ya Kiswahili yamechangiwa na wingi wa kazi za fasihi andishi, kwani robo tatu ya machapisho yote ni fasihi andishi.
v  Hadhi ya fasihi ya kiswahili kiulimwengu. Kwa kweli si jambo rahisi sana kusema kuwa fasihi ya Kiswahili hususani fasihi andishi ya Kiswahili inahadhi ya chini au juu. Ila kwa ujumla tunaweza kusema kwamba hadhi ya fasihi ya Kiswahili kiulimwengu haiko nyuma sana imepiga hatua kidogo japo si kwa kiasi kikubwa.
  Kwa mfano hadhi ya fasihi ya kiswahili kiulimwengu; fasihi andishi ya Kiswahili inafundishwa katika mataifa mbalimbali kama vile Korea, Afrika Kusini, Ujerumani, Marekani, Botswana, China, Italia nk.
      Vilevile wanafunzi wa kigeni kutoka katika mataifa mbalimbali wanaokuja kwa lengo la kusoma lugha ya Kiswahili, wanasoma kazi mbalimbali za fasihi andishi ya Kiswahili kama vile hadithi fupi nk.
    Pia zipo kazi mbalimbali za fasihi andishi ya Kiswahili zilizochapishwa nje ya nchi na bado zinaonekana kuwa na thamani sana. Mfano; baadhi ya kazi za mwandishi mashuhuri S. Robert.
v  Nafasi ya fasihi ya Kiswahili kiulimwengu na kitaifa:
Nadharia ya sosholojia na nafasi ya fasihi andishi ya Kiswahili kitaifa na kiulimwengu
Katika kuangalia nafasi ya fasihi ya Kiswahili kitaifa na kiulimwengu tutazingatia nadharia ya wanasosholojia ambayo waasisi wake ni pamoja na Bronislaw Malinowski, A.R. Radcliffe- Brown na Franz Boaz. Wataalam hawa wanaweka mkazo zaidi katika utendaji na msisitizo juu ya dhima ya fasihi katika jamii. Nafasi ya fasihi andishi kitaifa na kiulimwengu ni kama ifuatavyo:
      Kitaifa: fasihi ya Kiswahili kitaifa inanafasi kubwa sana, kwani dhima zake zina halisika katika jamii ya Tanzania na zinaendana na wakati uliopo. Miongoni mwa dhima hizo ni pamoja na kuelimisha, kuburudisha, kukuza uchumi nk.
  Kiulimwengu: kupitia fasihi andishi ya Kiswahili tunao waandishi maarufu ambao ni kama chachu ya maendeleo ya Kiswahili nje na ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile E. Kezilahabi, F. Nkwera, J. Madumulla, I. Husseni, T.Sengo, Kingo, Chachage, Penina Mlama, S. Shaffi, Wamitila, E. Mbogo, Asha Kunemah, nk.
Waandishi hawa wametoa changamoto kubwa sana katika kukikuza na kukieneza Kiswahili pamoja na fasihi andishi ya Kiswahili.
Vilevile kupitia fasihi andishi ya Kiswahili wameonesha mafanikio makubwa katika kazi zao kiuchumi na hata katika ukombozi wa fikra za wanajamii.
Hitimisho:
Pamoja na kwamba, fasihi ya Kiswahili inahadhi na nafasi ya juu kitaifa bado inakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile; watanzania wengi hawana utamaduni wa kusoma vitabu vya fasihi andishi ya Kiswahili, vilevile hata serikali haithamini sana mchango wa watunzi mbalimbali wa kazi za fasihi andishi na hii inatokana na kasumba kuwa lugha ya Kiswahili bado inahadhi ya chini hivyo, inapelekea hata kazi zake kutosomwa na watu wengi.
Marejeo:
BAKITA, (2004), Makala ya siku ya Kiswahili Kiswahili na Utandawazi, Dar es salaamu
Mulokozi, M. M. (1996) Utangulizi wa Fasihi ya Kiswahili. Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria.
TUKI, (2003) Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III: Fasihi Dar es Salaam.
TUKI, (2004) Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Wamitila, K.W. (2003) Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi-Kenya: Focus                                           Publications Ltd.
Wamitila, K. W. (2004) Kichocheo cha Fasihi Simulizi na Andishi. Focus Publications Ltd.

Print this item

  NGUVU YA KAMATI YA LUGHA NA ITHIBATI
Posted by: MwlMaeda - 09-07-2021, 07:33 AM - Forum: Taasisi za kukuza lugha - No Replies


.pdf   Makampuni ya kuchapisha vitabu hayakusita kuchapisha kitabu baada ya ithibati ya kamati kupatikana.pdf (Size: 530.73 KB / Downloads: 0)

Print this item

  ULINGANISHI NA ULINGANUZI WA MASHAIRI YA EUPHRASE KEZILAHABI NA HAJI GORA HAJI
Posted by: MwlMaeda - 09-07-2021, 07:17 AM - Forum: Ushairi - No Replies


.pdf   USHAIRI_WA_KISWAHILI.pdf (Size: 424.8 KB / Downloads: 0)

Print this item

  SHAIRI : BUSITANI NI MWANANA, WACHENI KUIHARIBU
Posted by: MwlMaeda - 09-07-2021, 07:14 AM - Forum: Ushairi - No Replies

SHAIRI : BUSITANI NI MWANANA, WACHENI KUIHARIBU
———————————————————————
1.
Busitani hino wazi, imefika mashakani,
jamii ya zama hizi, kwake haina thamani.
Mnaichimba mizizi, kwani kuiharibuni?
mwapandikiza magugu,yanayochafua shamba
2.
Busitani tumerithi, toka kale ya mababu,
ni wa jamii urithi, muwache kuuharibu.
Isibakie hadithi, isokuwa na sababu,
kama vile Kilatini, ile lugha ya Warumi.
3.
Busitani ni mwanana, matundaye mubashara,
kwayo twajadiliana, tukifanza biashara.
Ndani ye tunakutana, kwa kheri si masihara,
Visiwa na mwambaoni, hadi bara mbali sana.
4.
Ni shamba linatufaa, kwalo twawasiliana,
hili limekuwa taa, kwazo fani nyingi sana.
Ni mbali limetandaa, kwalo tunashikamana,
busitani ni mwanana, wacheni kuiharibu.
5.
Msione vyaelea, vinakuwa vimeundwa,
inajitoshelezea, busitani ilokuzwa.
Acheni kuichezea, kwa mambo yasiyo sawa,
mnapoivangavanga, kuichanga na kimombo.
6.
Inakuwa ni hatari, hata wetu viongozi,
jopo la wanahabari, wasanii welekezi,
pasi na kutafakari, kuwa huu upuuzi,
mnapozivanga ndimi, Kiswahili kwa kimombo.
7.
Viongozi yetu taa, Kiswahili msivange,
wanahabari ni nyota, ulimi wetu mchunge.
Wasanii wetu nyota, lugha msivangevange,
Kiswahili chajitosha, kimombo hakihitaji.
8.
Fikiri upo Ulaya, unalonga Ki’ngereza,
huku unagwayagwaya, Kiswahili kuongeza,
niambie pasi haya, aonaje Mungereza?
hata hapa Afurika, wenzio watakupu’za.
9.
Kiswahili laazizi, ni busitani mwanana,
tusikichimbe mizizi, kwacho tunaelewana.
Ni gundi ya pande hizi, yatufanya kushikana,
ni ulimi mtukuka, tuwache kuuharibu.
10.
Shukurani Subukhana, kalamu chini naweka,
umeniwezesha tena, beti hizi kuandika.
Kwako naamini sana, tungo litaeleweka,
busitani ni mwanana, wacheni kuiharibu.
————————————


Rwaka rwa Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda)
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, RWANDA.

Print this item

  SHAIRI: NA TUTENDE KWA UMOJA
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 10:33 PM - Forum: Ushairi - No Replies

NA TUTENDE KWA UMOJA
Nabutadi kutunga, kwa jinale Subuhana,
Ndiye kanipa kutunga, kwa marefu na mapana,
Sana napenda kupanga, Mashairi yenye vina,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Wetu umoja ni kinga, adui awe hakuna,
Ni hasara kujitenga, mwenda peke mwendo hana,
Matata yatamzinga, hata akimbie sana,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Wadudu pia hupanga, pamwe husaidiana,
Siafu hutangatanga, wenyewe wakisongana,
Mizigo wakiifunga, vinywani kushikizana,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Nyuki umoja huchunga, daima wakipishana,
Wanaolinda mzinga, hawana kutegeana,
Kwenye mashine za unga, wadudu hutanguzana,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Ijapo mchwa humanga, kucha hao hupishana,
Kichuguu kukijenga, anayebisha hakuna,
Mtaka peke ni mwanga, hendi mbele kuuona,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Umoja huleta mwanga, siende kupapasana,
Ni Nani atatutinga, na madhila kusongana?
Tuwache kuvungavunga, vema tukikamatana,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Beti kadha nazifunga, nawasihi kushikana,
Moja jambo kulilenga, Kulifanya kwa mapana,
Msijitie uchanga, muende kwa kutengana,
Na tutende kwa umoja, tushikaneni insia.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item

  UFUNDISHAJI WA LUGHA YA PILI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 06:02 PM - Forum: Nukuu - No Replies

Utangulizi

Kuna mikabala/ mikondo mbalimbali katika historia ya ufundishaji wa lugha ya pili  ambayo  imewahi  kutumiwa.  Baadhi  ya  mikabala  hiyo,  mpaka  sasa  imeendelea kuathiri ufundishaji wa lugha ya pili. Ujuzi wa mikabala hiyo ni jambo muhimu kwa mwalimu wa Kiswahili kwa sababu unaweza kumsaidia kupata fununu kuhusu asili ya mbinu  tofauti  tofauti  zinazotumiwa  kufundisha  lugha  ya  pili. Hapo  awali  mbinu  hizi zililenga hasa ufundishaji wa lugha ya Kingereza kama lugha ya pili. Hata hivyo, baadhi ya  mambo  ambayo  hupendekezwa  katika  mbinu  hizo  yanaweza  kumsaidia  mwalimu ambaye anajishughulisha na ufundishaji wa Kiswahili kama lugha  ya pili.
Madhumuni Ya Somo
Kufikia mwisho wa somo hili utaweza kutoa mifano ya mbinu za kufundishia lugha na kueleza jinsi kila mojawapo ya mbinu hizo inaweza kutumiwa katika ufundishaji wa Kiswahili.
Mbinu Ya Kimapokeo
Hii ni mbinu ambayo hapo awali ilitumika kama njia ya kufundishia lugha za kijadi  kama  vile  Kiyonani  na  Kilatini.  Ilitawala  ufundishaji  wa  lugha  za  kizungu  na kigeni kati ya miaka 1840 na 1940. Lengo kuu la mbinu hii ni kufanikisha ufahamu wa sarufi  pamoja  na  uwezo  wa  kuandikia  kwa  usahihi  katika  lugha  inayolengwa.  Pia inalenga kuwezesha mwanafunzi kuwa na upeo mpana wa msamiati unaotumika sana katika lugha ya uandishi katika lugha husika, ili hatimaye aweze kuthamini umuhimu pamoja na thamani ya nakala zinazohusika.
Katika mazingira ya darasani, mwalimu anatazamiwa kutekeleza malengo haya kwa kushirikisha wanafunzi katika kazi ya kutafsiri mara kwa mara kutoka lugha zao hadi  katika  lugha  inayofunzwa.  Kabla  ya  kutafsiri,  wanafunzi  wanapaswa  kwanza kijifunza maneno ya lugha inayolengwa ili waweze kutafsiri katika lugha mpya. Pamoja na  hayo,  wanafunzi  wanapewa  maelezo  marefu  kuhusu  sheria  za  kisarufi.  Kisha wanapewa zoezi la kutunga sentensi ili kubainisha ufahamu wao wa sheria hizo. Uwezo wa  mwanafunzi  katika  kutafsiri  huwa  ndicho  kigezo  muhimu  kinachotumiwa  kama chombo cha kupima ustadi wake katika kipengele cha sarufi na msamiati.
Udhaifu hasa wa mbinu hii ni kwamba haitilii mkazo juu ya matamshi sahihi pamoja na stadi za kimawasiliano. Inasisitiza sana ujuzi wa sheria za kisarufi bila kupatia wanafunzi nafasi ya kutosha kujieleza kutokana na nafsi zao. Matokeo ya kujishughulisha sana na ufundishaji wa kanuni na vighairi ni kwamba waalimu huishia kwa kufundisha wanafunzi lugha ya ulimwengu wa vitabu, lugha isiyokuwa na uhai, na ambayo mara nyingi haina manufaa katika ufanikishaji wa mawasiliano ya kawaida.
Utumiaji wa mbinu hii unalifanya somo la lugha kukosa ubunifu unaotakikana. Wanafunzi hawapati nafasi ya kutumia lugha kama chombo wanachoweza kukitegemea kutekeleza mahitaji yao ya kimawasiliano. Shughuli ya kujifunza lugha inageuka kuwa zoezi la kukariri maneno chungu nzima na kanuni kemkem za kisarufi. Hakuna hakikisho kwamba baada ya kukariri maneno na kanuni wanafunzi watakuwa na uwezo wa kutumia kanuni  na  maneno  vilivyokaririwa  katika  mawasiliano  ya  nje  ya  darasa.  Shughuli  ya kufundisha na kujifunza lugha inakuwa kama zoezi la kuchemsha bongo tu.
Mbinu Ya Moja Kwa Moja
Hali ya kutoridhika na mbinu ya kimapokeo ni miongoni mwa mambo ambayo yalichangia kuibuka kwa mbinu ya moja kwa moja. Iliibuka katika karne ya 19 kuchukua mahali  pa  mbinu  ya  kimapokeo.  Wanaopendelea  mbinu  hii  hushikilia  kwamba  njia mwafaka ya kujifunza lugha ya pili ni kukabiliana nayo moja kwa moja na kuitumia kama vile mtoto mdogo anavyofanya anapojifunza lugha ya mama. Kulingana na mbinu hii ni marufuku kutumia lugha ya wanafunzi au lugha nyingine yo yote ile.
Mbinu hii husisitiza umilisi wa lugha bila tafsiri wala maelezo rasmi juu ya sheria za kisarufi. Wanafunzi wanatakiwa kijifunza lugha kwa kushirikishwa kikamilifu kama wahusika watendaji katika matumizi tofauti tofauti ya lugha. Inasisitizwa kwamba ikiwa maana inaweza kuwasilishwa moja kwa moja kwa kushirikisha maono au vitendo hakuna haja ya kutafsiri.
Kwa upande wa sarufi, mbinu hii inashikilia kwamba njia bora ya kuendeleza ufahamu wake ni kutokana na uzoefu wa kutumia mara kwa mara lugha inayohusika. Mwanafunzi akipewa fursa ya kutosha kukumbana na matumizi ya lugha, itakuwa rahisi kwake kutambua na kujifunza sheria zinazotawala sarufi ya lugha hiyo. Mbinu hii inasisitiza haja ya kutoa nafasi kwa mwanafunzi ya kujifunza lugha kama vile mtoto anavyojifunza lugha yake ya kwanza. Mtoto anajifunza na kuimudu lugha kwa kukumbana nayo moja kwa moja katika mkutadha maalum wa mawasiliano.
Hakuna mtu anayemfafanulia kanuni za kisarufi za lugha yake. Hata hivyo anazing’amua kanuni hizo yeye mwenyewe baada ya kushuhudia matumizi yake katika vielelezo vya sentensi. Huwa anajifunza lugha ya jamii yake katika mazingira yanayoshirikisha vitendo na maono. Ushirikishaji wa maono na vitendo unachangia kujenga hali ambayo husaidia mtoto  kukisia  maana  ya  kile  kinachosemwa. Anajifunza  lugha  ya  jamii  yake  kwa kusikiliza kwanza na baadaye kuigiza yale anayosikiza.
Kwa mujibu wa mbinu hii mwalimu anapofundisha lugha ya pili anashauriwa kutotegemea  tafsiri.  Anashauriwa  vile  vile  kutofundisha  moja  kwa  moja  sheria  za kisarufi.  Ana  wajibu  wa  kuambatanisha  ufundishaji  wake  na  vitendo,  uigizaji  na mazungumzo. Lakini ikiwa mwalimu hana budi kufundisha sarufi, inafaa ufundishaji wa sarufi uzingatie kiwango cha matumizi ya lugha huko mkazo ukitiliwa juu ya madondoo ya kisarufi yanayotumika sana sana hasa katika mazungumzo.
Kwa mujibu wa mbinu hii, dhima ya mwalimu ni kupanga na kufanikisha utumizi wa lugha badala ya kujishughulisha na ufafanuzi pamoja na uchambuzi wa kanuni za kisarufi. Ili mwalimu aweze kufaulu kutumia mbinu hii anapaswa kuwa na ujuzi wa kiwango cha hali ya juu katika lugha anayofundisha. Ni lazima pia awe na ubunifu wa kumwezesha kuwasilisha maana bila kutumia lugha nyingine yo yote zaidi ya ile ambayo anafundisha.  Anatarajiwa  pia  kujitahidi  kujenga  mazingira  ya  kufundishia  ambayo yanakaribia kufanana yale ya lugha ya kwanza. Mazingira hayo yanatarajiwa kufanikisha ufahamu wa lugha kupitia mazoezi ya kusikiliza pamoja na mazungumzo. Lazima yawe mazingira   ambayo   yanaweza   kuchangia   katika   kuhamasisha   mwanafunzi   kutaka kujifunza lugha inayohusika.
Kwa kawaida mtoto anapojifunza lugha yake ya kwanza anakuwa na hamu ya kujifunza lugha hiyo ili aweze kutangamana na jamii ya watu wanaomzunguka. Jamii hiyo pia humsaidia kuendelea kwa kumtia shime. Pamoja na hayo mtoto huwa na muda mwingi wa kusikia na kutumia lugha hiyo. Lugha inakuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku.
Mbinu Ya Uzungumzi
Mbinu hii ilizuka na kukita mizizi katika miaka ya 1950 kutokana na mwamko mpya nchini Amerika wa kujishughulisha na ufunzaji wa lugha za kigeni. Tukio muhimu ambalo lilichangia pakubwa kuamsha ari ya Wamerika katika lugha za kigeni ilitokea mnamo mwaka wa 1957. Mwaka huo Warusi walifaulu kupeleka chombo chao (sputnik) angani. Jambo hili lilikuwa changamoto kubwa kwa taifa la Amerika. Kufuatia tukio hilo, serikali ya Amerika iliamua kujishughulisha kikamilifu katika ufundishaji wa lugha za kigeni ili isiachwe nyuma katika maendeleo ya kisayansi. Jambo ambalo linapewa kipaumbele katika mbinu hii ni ufasaha wa kuzungumza.
Ufasaha unaotarajiwa unahusu matamshi bora, sarufi, pamoja na uwezo wa kuitikia upesi na kwa urahisi katika hali tofauti zinazohusisha utumizi wa lugha katika mazungumzo.
Ufahamu  sikizi,  matamshi,  sarufi  na  msamiati  vinapofundishwa  huwa  kama  njia mojawapo   ya      kufanikisha ufasaha       wa     kuzungumza. Vilevile wanafunzi wanaposhirikishwa katika kuandika na kusoma mambo haya yanaambatanishwa na ustadi wa kutumia lugha ya mazungumzo. Kulingana na mbinu hii, stadi za lugha zinastahili kufundishwa kwa kuzingatia mfuatano huu: Kusikiliza, Kuongea, Kusoma na Kuandika.
Katika hatua za mwanzo mwanzo, kusoma na kuandika vinachukuliwa tu kama mambo  ambayo  yanaweza  kuchangia  kuimarisha  ustadi  wa  kusikiliza  na kuongea.
Vinatiliwa mkazo zaidi katika viwango vya juu wakati ambapo wanafunzi wana uzoefu unaofaa ili kuweza kukabiliana na mitindo zaidi ya lugha ya kimaandishi. Madondoo ya lugha yanapofundishwa kwa   kutumia      mbinu         hii      huwa yanawasilishwa  kupitia  mjadala  ambao  ni  chombo  muhimu  cha  kutoa  mkutadha  wa kufundishia  kile  kinacholengwa.  Zaidi  ya  kushiriki  katika  mjadala,  wanafunzi  huwa wanatakiwa, mara kwa mara, kukariri vielelezo vya sentensi.
Mbinu Ya Mawasiliano
Msingi  wa  mbinu  hii  ni  imani  kwamba  kazi  kuu  ya  lugha  ni  kufanikisha maingiliano   pamoja   na   mawasiliano   katika   jamii.   Lugha   ni   chombo   ambacho kinamwezesha binadamu kushirikiana na watu wengine na pia kutekeleza mahitaji ya maisha yake. Kwa hivyo, kulingana na waasisi wa mbinu hii, lengo kuu la kufundisha lugha  ni  kuwezesha  mwanafunzi  kuwa  na  uwezo  wa  kuwasiliana  akitumia  lugha inayohusika.
Njia moja ya kuhakikisha kuwa mwanafunzi anakuwa na uwezo wa kuwasiliana ni, kwanza, kumpa fursa ya kushiriki kama mhusika mpokezi. Mwanafunzi  anapata fursa ya kupanua upeo wake wa lugha kupitia kusikiliza na kusoma. Baada ya kushiriki katika matumizi ya lugha akiwa mhusika mpokezi mwanafunzi anashirikishwa kama mhusika mwanzilishi wa mawasiliano. Kulingana na waasisi wa mbinu ya mawasiliano, lugha ambayo ni ya maana / manufaa kwa wanafunzi inatilia nguvu juhudi za kujifunza. Kwa hivyo ni muhimu kwa walimu kuhakikisha kwamba wanapochagua kazi ya wanafunzi wanatilia  maanani  uwezo  wa  kazi  hiyo  wa  kuwashirikisha  katika  matumizi  ya  lugha yenye maana na uhalisi.
Kwa kawaida, mawasiliano hufanyika katika mazingira ya watu wakiwa katika vikundi. Pia, aghalabu, mawasiliano huchukua mkondo wa mazungumzo (conversation) na  majidiliano  (discussion).  Wakizingatia  ukweli  huu,  wanaounga  mkono  mbinu  ya kimawasiliano wanapendekeza kugawanya  wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo. Hii ni njia bora ya kuendeleza uwezo wa wanafunzi wa kuwasiliana kwa kutumia lugha inayofundishwa. Wakiwa katika vikundi vya watu wachache, wanafunzi wanakuwa na fursa bora ya kutumia lugha halisi. Pia wanapata nafasi ya kujieleza kwa ufasaha bila wasiwasi.  Ustadi  katika  kusoma  na  kuandika  unaweza  kukuzwa  kutokana  na  msingi imara wa kutumia lugha kwa uhalisi.
Je  jukumu  hasa  la  mwalimu  ni  nini?  Kwa  mujibu  wa  waasisi  wa  mbinu  hii, jukumu la mwalimu ni kuhamasisha wanafunzi na kutoa kwao nafasi ya kujieleza katika lugha  inayohusika.  Ana  wajibu  wa  kuhamasisha  wanafunzi  kutumia  lugha  kwa  njia mbalimbali. Anapaswa pia kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi anapata fursa ya kujieleza.
Pamoja na hayo, mwalimu ana wajibu kuhakikisha kwamba wanafunzi wanaelewa vizuri kwa nini wanafundishwa kile wanachofundishwa. Hivi ndivyo watakavyoweza kushiriki kwa  njia  ya  maana  na  manufaa  kwao.  Vilevile  ni  lazima  mwalimu  ahakikishe  kuwa wanafunzi wake wanahusika zaidi kuliko vile anavyohusika mwenyewe.
Aidha,  mwalimu  anashauriwa  kushirikisha  wanafunzi  katika  vitendo  ambavyo vinaweza   kuwalazimisha   kuwasiliana   kwa   kutumia   lugha   inayofaa   kulingana   na mkutadha. Kwa maneno mengine, mwalimu anapaswa kubuni hali na mazingira ambamowanafunzi  hawawezi  kukidhi  mahitaji  na  matarajio  yao  bila  kuwasiliana.  Wakijikuta katika  mazingira  ya  namna  hii  hawatakuwa na  budi  kutafuta  ufumbuzi  kwa  kutumia lugha.  Kwa  ufupi,  mwalimu  anaweza  kusaidia  kuendeleza  uwezo  wa  wanafunzi  wa kuwasiliana wakitumia lugha kwa kuzingatia mfuatano wa hatua zifuatazo:
  1. Mapokezi ya lugha.
  2. Ufafanuzi / Maelezo
  3. Majaribio ya matumizi ya lugha
  4. Mawasiliano huru
Katika hatua ya mapokezi wanafunzi wanashiriki kama wahusika wapokezi. Kazi yao katika hatua hii ni kupokea ujumbe unaowasilishwa na watu wengine na kupata maana  ya  ujunbe  unaowasilishwa.  Wanaweza  kutekeleza  jambo  hili  kupitia  zoezi  la kusikiliza au kusoma. Zoezi la kusikiliza husaidia wanafunzi kupata nafasi ya kupanua upeo  wa  lugha.  Kupitia  zoezi  hili  wanaweza  kujifunza  msamiati  mpya  na  miundo mbalimbali  ya  kisarufi.  Vilevile  wanafunzi  wanaimarisha  ujuzi  wao  wa  yale  ambayo wamejifunza tayari.
Kwa upande mwingine, katika hatua ya ufafanuzi (maelezo) mwalimu anaweza kudondoa madondoo fulani ya lugha ambayo wanafunzi wamewahi kukumbana nayo, katika zoezi la kusikia na kusoma. Kisha anatoa maelezo kuhusu madondoo hayo ili wanafunzi   wayatilie   maanani   zaidi   kuliko   mengine   kwa   wakati   huo.   Baada   ya kuhakikisha   kwamba   wanafunzi   wanafahamu   kiini   cha   somo   mwalimu   anawapa wanafunzi  nafasi  ya  kujaribu  kutumia  madondoo  hayo  katika  vielelezo  vya  sentensi wakizingatia maagizo yaliyotolewa.
Katika hatua ya mawasiliano huru wanafunzi wanapata fursa zaidi ya kujieleza bila kufuata maagizo ya mwalimu. Wanaweza kujieleza kwa njia halisi kulingana na mahitaji  ya  mawasiliano  katika  mkutadha  unaohusika.  Wanafunzi  watateua  lugha kulingana na hali halisi inayowakabili wakati huo. Mawasiliano huru huwapa wanafunzi fursa ya kutambua kuwa lugha siyo somo ambalo linajikita katika mipaka ya mazingira ya  darasani  tu,  lakini  pia  ni  chombo  cha  mawasiliano  nje  ya  mipaka  ya  darasa.
Mawasiliano huria huwapa wanafunzi nafasi ya kutumia lugha kwa njia ya ubunifu katika miktadha tofauti tofauti ya kijamii. Wanatumia lugha bila usimamizi wa mwalimu, lakini kulingana  na  hali  halisi  katika  mazingira  ya  mawasiliano.  Huwa  wajitegemea  wao wenyewe. Kadiri wanavyoshiriki katika mikutadha tofauti ya mawasiliano na kushuhudia jinsi lugha inavyotumiwa, ndivyo wanavyoendelea kukuza na kuimarisha uwezo wao wa kimawasiliano (communicative competence). Uwezo huu ni muhimu kwa mwanafunzi kwa sababu akiwa nao anaweza kufasiri lugha kwa njia iliyo sahihi akizingatia mkutadha unaohusika.  Na  akifanya  hivyo  anaweza  kuitikia  kama  inavyotarajiwa.  Kwa  mfano mwalimu  akiingia  darasani  ambamo  mna  joto  jingi  na  agundue  kuwa  madirisha yamefungwa,  anaweza  akasema:  Mbona  joto  limezidi  sana  humu  ndani.  Mwanafunzi mwenye  uwezo  wa  kimawasiliano  atatambua  kuwa  mwalimu  angetaka  madirisha yafunguliwe, na ataitikia kwa kuyafungua. Yule asiyekuwa na uwezo huo atachukulia usemi wa mwalimu kama kauli ya kawaida tu.
Msingi wa Mbinu ya Kimawasiliano
Asili ya mbinu ya kimawasiliano ni imani inayoshikilia kwamba:
(a) Lugha ni mfumo wa kueleza maana.
(b) Jukumu kuu la lugha ni kufanikisha maingiliano na mawasiliano baina ya watu.
© Shughuli  ambazo  zinachangia  kufanikisha  ufahamu  wa  lugha  ni  zile ambazo  zinatoa  kwa  wanafunzi  nafasi  ya  kushiriki  katika  mawasiliano halisi (real communication).
(d) Vitendo  vinavyohusisha  matumizi  ya  lugha  ili  kutekeleza  shughuli  za maana (meaningful tasks) husaidia kufanikisha ujuzi wa lugha.
(e) Lugha yenye maana kwa wanafunzi inaimarisha hali ya kujifunza.
(f) Mawasiliano hufanyika ikiwa wale wanaohusika wana hamu (motisha) ya
kuwasiliana.

Print this item

  MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 05:59 PM - Forum: Kiswahili kwa wageni - No Replies

MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
  1. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni
Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha ile
Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja na:-
1)      Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.
2)      Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika
LUGHA YA KWANZA
Stern (1983) anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga.
LUGHA YA PILI
Stern (1983) anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi
LUGHA YA KIGENI
Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania
MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI
Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:
1)      Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika
2)      Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali
3)      Kwa ajili ya kufanya biashara
4)      Kukidhi vigezo vya masomo
5)      Kufanya utafiti katika taaluma husika
6)      Ili kupata ajira nchi za ng’ambo
KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?
Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako
W      Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.
MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI
a)      Ili mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:
i.            Aweze kumudu lugha ya Kiswahili
ii.            Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili
iii.            Ili wanafunzi waweze kung’amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo gani? Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa nini aseme? Kwa nani aseme? Mazingira gani aseme?
iv.            Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha
v.            Wanafunzi wang’amue umuhimu wa lugha wanayojifunza
b)     ili wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima wape wanafunzi:
kuchunguza®kugundua®kutalii kuhusu lugha ya Kiswahili
c)      wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi
d)     wape nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao
e)      wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi
f)       wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya Kiswahili
NADHARIA KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA
Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili wanapaswa kujua
1)      mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu wengi
2)      manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema kwamba “ wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”
kuna nadharia kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:
1)      NADHARIA YA UHULKA
ü  Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)
ü  Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na uwezo lugha. Yaani kwenye ubongo wake ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)
ü  Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga mkono ni Ellis (1997) walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa lugha husika. Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu wa wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote katika ujifunzaji lugha.
2)      NADHARIA YA UTABIA
ü  Kwa mara ya kwanza ilidokezwa na E.Thonilke(1935). Kwa mujibu wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo
ü  Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni B.F SKINNER , Huyu alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali huichota kutoka kwa wazazi wake
  • Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika ujifunzaji lugha
  • Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha? Jibu unalo wewe mwenyewe!
3)      NADHARIA YA UTAMBUZI
ü  Nadharia hii iliasisiwa na Jean Hajet (1954)
ü  Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha
ü  Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha
ü  Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.
ü  Arth(2003) anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18
ü  Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji lugha
4)      NADHARIA YA UUMBAJI/ MAUMBILE
ü  Iliasisiwa na Jerome Brunner
ü  Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama katika upataji lugha ya kwanza
ü  Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano ambayo mama yake anayatumia
ü  Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo yatimizwe
  • Muktadha
  • Tajiriba (experience)
  • Upangilifu (organization)
  • Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_
ü  Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji lugha
NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI
Njia za ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia hizi itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa zitumike.
  1. Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa mara ya kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri kwa mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
  2. Njia ya mahojiano. Mfano mwalimu aandae maswali, awaambie wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine anakuwa mgonjwa n.k
  3. Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani? Watajibu na kujipatia msamiati kibao
  4. Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa maigizo
  5. Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni, wewe ni nani?
  6. Njia ya uwandani. Mfno ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi wapeleke sokoni.
  7. Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu anataka kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
  8. Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini mbalimbali wanafunzi
  9. Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili vitu ambavyo vimewekewa mipaka
Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na kazi zao!
HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA
Wanafunzi hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo ya wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi kusahihishwa, mkimya nk
ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA
Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya mambo yanayoathiri ni kama vile
i.            Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo
ii.            Jinsia
iii.            Umri
iv.            Mazingira
v.            Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo
Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:
i.            Kuwatia motisha wa kujifunza lugha
ii.            Kumsaidia kuondokana na hasira
iii.            Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba Kiswahili ni lugha ya kiislamu
iv.            Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi
v.            Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika
Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa awaeleze mambo yafuatayo
i.            Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini
ii.            Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia
iii.            Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa
iv.            Namna ya kusimama na kuelezea jambo
Ili kutimiza hayo yote mwaimu lazima awe na sifa zifuatazo:
i.            Awe muwasilishaji mzuri
ii.            Awe na mpangilio mzuri
iii.            Awe mstahimilivu
iv.            Awe na ujuzi wa kufundisha
v.            Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi
vi.            Awe na maarifa ya somo
SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA
a)      Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa
b)     Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo
c)      Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo ambayo jamii Fulani inayafanya
d)     Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
e)      Awe na ratiba ya kujifuza
f)       Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza
g)      Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika
h)     Awe mtendaji
i)        Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi
MOTISHA
Ni tabia au msukumo katika kutimiza malengo Fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni kitu kama fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.
Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya sio hasi. Mfn hutakiwi kuchapa fimbo
Brown (1994) anasema kuwa motisha:
a)      Ni kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
b)      Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo
SKINNER &WATTSON-hawa wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali Fulani
AINA ZA MOTISHA
  1. Mwamko wa mjifunzaji mwanyewe
  2. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k
  3. Jamii inayomzunguka ni motisha pia
  4. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
  5. Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha
  6. Motisha wa ndani-
MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI
ü  Haitegemei vitu vya nje ya yenyewe
ü  Hiki ni kile kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe
ü  Hii haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule
  1. Motisha wa nje
ü  Ni aina ya motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona
ü  Hivi vitamsaidia katika kujifunza lugha
Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha kulingana na muktadha. Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-
a)      Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili zao ili kujifunza lugha
b)     Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha
c)      Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha
d)     Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka kuliko wanaume
UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO
ü  Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano
ü  Ni mbinu ya kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili
ü  Husisitiza mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha
KAZI ZA LUGHA
ü  Van (1975) anasema kuwa kazi ya lugha ni:
a)      Kutoa habari
  • Kusimulia
  • Kuuliza
  • Kutoa taarifa
b)      Kutafuta taarifa za kitaaluma
c)      Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko
d)     Kuelezea masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc
e)      Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha nk
Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha hiyo ni lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha
MASHARTI YA KUZINGATIA
a)      Azingatie majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu asiyemjua? Watu wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya kuzungumza nao
b)      Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn CHADEMA CUF na CCM
c)      Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka wanatumiaje?
Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha mawasiliano, hivyo inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi
MUKTADHA WA UFUNDISHAJI LUGHA
ü  Haya ni mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia wadau wakuu watatu
a)      Mwanafunzi
b)      Mwalimu
c)      Jamii
ü  Pamoja na motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:
  • Utoaji wa kazi na mazoezi mengi
  • Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye stadi nne za lugha
  • Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha
  • Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha, katuni. Nk
  • Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina yako mwalimu
  • Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)
  • Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi
  • Ajue maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk
  • Kuunda mazingira ya utani darasani
UFUNDISHAJI WA DARASA MSETO
ü  TUKI (2013) Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutengeneza kitu fulani
ü  Hapa ni mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na wenye umri tofauti, malengo tofauti nk
ü  Hivyo mwalimu inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili usije ukawakwaza wanafunzi wengine
NAMNA YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO
a)      Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn utamaduni wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao
b)     Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua
c)      Tumia vitendo halisi, ishara nk
d)     Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na mazingira
e)      Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi
f)       Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima ufungamane na muktadha husika
SIFA ZA MPATAJI LUGHA
Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili tu:
  1. Umilisi wa kiisimu
ü  Ni uwezo alio nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha
ü  pia kuweza kutamka lugha ile.
  1. Umilisi wa kiisimujamii
ü  Ni umilisi ambao mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na kuzingatia muktadha
NADHARIA /MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI
ü  Nadharia ni mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo
ü  Mtesigwa(2009) anasema “ nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi
®kuna mambo mawili ambayo lazima tujikumbushe:
a)      Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo wengi
b)      Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani, usitumie njia moja tu.
ü  Rogers&Richards (2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza maswali yafuatayo:-
a)      Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.
b)      Upi ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfn kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?
c)      Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
d)     Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni, mfano salamu nk
e)      Je lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
f)       Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
g)      Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?
NADHARIA ZA KUJIFUNZA
  1. Mbinu ya tafsiri sauti
  2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method
  3. Mbinu ya usomaji(reading approach method)
  4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
  5. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
  6. Mbinu ya ukimya (silence method)
  7. Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)
  8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
  9. Mbinu ya utambuzi (communitive code method)
  10. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
  1. Mbinu ya tafsiri sarufi
ü  wakati mwingine hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao ufundishaji wa lugha ya kigeni umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa na Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya kiratini ndiyo lugha pekee.
ü  Nafasi ya lugha mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini, na hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na vipengele vingine vilipuuzwa
ü  Huu ulikuwa ni mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na sivyo wanajamii wanavyotumia lugha hiyo
  1. Mbinu ya moja kwa moja(direct method)
ü  Iliasisiwa na Gouin(1880)
ü  Nadharia hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika
ü  Mbinu zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfn mbinu ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi
ü  Masomo yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.
ü  Matumizi ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k
ü  Kipengele vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha inatumika
ü  Kipengele cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana
  1. Mbinu ya usomaji (reading approach method)
ü  Mbinu hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni ambao hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo inatumika
ü  Malengo yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha
ü  Vipengele vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.
ü  Mbinu hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika bali ni kuisoma tu.
  1. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
ü  Nadharia hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.
ü  Iliasisiwa na Bloomfield (1942) na Fries (1945)
ü  Msingi mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa
ü  Maandishi hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield alisema kuwa lugha si katika maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.
ü  Inahusisha kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia
ü  Walipenda sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji
ü  Walisisitiza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
ü  Waliongeza kitu kingine chakuona
  1. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
ü  Iliasisiwa na curran (1976)
ü  Dai la nadharia hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi kutenga jamii na lugha
ü  Walidai kwamba ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda kwenye jamii husika
ü  Walidai pia kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa lako lifanye angalau lifanane fanane na jamii ya lugha husika
ü  Ili uweze kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha hiyo.
ü  Mwanafunzi atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni mambo gani yanafaa na mambo gani hayafai
ü  Nadharia hii inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika kujifunza lugha
  1. Mbinu ya ukimya (silence method)
ü  Nadharia hii inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha anayojifunza
ü  Nadharia hii inadai kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu viwili.
Kichocheo®     Mwitikio®       mgeuko
(Mwalimu)     (mwanafunzi)-(anabadilika)
ü  Ili kuweza kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani katika darasa jambo ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha husika
ü  Nadharia hii inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi wake ili kubaini kama kuna badiliko
  1. MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)
ü  Nadharia hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya sarufi na ile ya moja kwa moja
ü  Ilianzishwa mwaka 1970
ü  Wanadai kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana kuhusu lugha, kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe kulingana na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.
ü  Uwafundishe kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni lazima ujue ngeli za majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza kukaa peke yake kama sentensi
  1. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
ü  Nadharia hii pia hujulikana kama mkabala asilia.
ü  Iliasisiwa na James na Asher
ü  Inatilia mkazo mfumo na muundo wa lugha.
ü  Kama ilivyo nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu mazungumzo kama sehemu ya umilisi wa lugha
ü  Ufundishaji uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi kumudu anachojifunza
ü  Nadharia hii inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo katika kujifunza lugha.
  1. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
ü  Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)
ü  Nadharia hii inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo katika kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia lugha ni lazima yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake
ü  Wanaelezea namna ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa uwe ni wa kutazamana, maana yake vikae kwa duara.
ü  Wanasisitiza matumizi ya mziki laini na mziki nyororo
  1.                 MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE LANGUAGE APPROACH)
ü  Inasisitiza maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii
ü  Wanakaza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.
ü  Kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika
ü  Ni nadharia ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky
ü  Hii ndiyo nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha
VIWANGO VYA WANAFUNZI
  • Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.
  • Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali liitwalo Interagence Language Round Table (ILRT)
  • Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango vitatu
a)      Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
b)      Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)       Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
a)                  Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
Daraja limegawanyika katika viwango hivi
  • Kiwango cha 0-®mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugha
  • Kiwango cha +0-®mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu akibadilishiwa tu basi Amepotea
  • Kiwango cha 1-®mwanafunzi anaweza kusitahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
  • Kiwango cha +1-®huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake
INTERMIDIATE
  • Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi
  • Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma
  • Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma
b)            Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)            Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level

Print this item

  USANIFISHAJI WA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 04:21 PM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Usanifishaji Wa Kiswahili

Usanifishaji wa lugha ni mchakato unaowezesha kupatikana kwa lugha moja yenye namna moja ya uzungumzaji na uandishi. Usanifishaji hutokea katika mazingira yenye vilugha (lahaja) vingi. Ulinganifu wa vilugha hivyo ili kupata lugha moja itakayotumiwa kirahisi katika mawasiliano. Historia ya mchakato wa usanifishaji wa Kiswahili iligubikwa na malumbano juu ya lahaja ipi iwe ya msingi kati ya Kiamu, Kimvita na Kiunguja ambapo ilikubalika kwa sauti moja kuteua Kiunguja kuwa ndio msingi wa ‘Kiswahili Sanifu’ katika kikao kilichofanyika mjini Mombasa mnamo mwaka 1928 na kufuatiwa na uundwaji wa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki mwezi Januari mwaka 1930. Kamati ilitumia muda mwingi kwenye kipindi cha miaka ya 1930 hadi 1947 katika kuweka ithibati katika mtindo wa tahajia, na sifa bainifu za kisarufi za Kiswahili Sanifu (angalia Whiteley 1969, Massamba 1996). KKAM ilifanya kazi yake kama chombo chenye sauti moja kwa Afrika ya Mashariki yote na ilitunga kamusi mbalimbali, ilipitisha vitabu vya shule, sheria na uandishi wa habari chini ya kamati ya KKAM (Gibbe 1983, Mbaabu 1991, 2007, Maganga 2008).
Umuhimu wa usanifishaji wa Kiswahili
  • hutambulisha utamaduni wa mtanzania nje ya nchi yake
  • husaidia kusawazisha matamshi ili lugha iwe na namna moja ya uzungumzaji na uandishi mf; kilolo-kioo, niumba-nyumba
  • kuifanya lugha itumike kwa namna moja kwa watumiaji wake wote
  • hukuza msamiati wa lugha kwa kuchukua maneno toka lahaja mbalimbali
  • hurahisisha mawasiliano miongoni mwa watumiaji wa lugha inayohusika
  • huondoa tofauti za kikabila zinazoleta migogoro ndani ya jamii
  • hukuza sanaa ya jamii pana ya kitanzania.
Hatua za usanifishaji wa Kiswahili
  • Uteuzi wa lahaja ya usanifishaji miongoni mwa lahaja zilizokuwepo mf. Katika Kiswahili lahaja ya Kiunguja ndio iliyoteuliwa.
  • Kurahisisha matamshi ili yawe ya aina moja nchi nzima
  • Kuundwa kwa chombo cha usanifishaji mf. Kamati ya lugha ya Afrika Mashariki (Interterritorial Language –swahili Committee,1930)
  • Kutayarisha kamusi na vitabu vya sarufi ya lugha inayohusika
  • Kuitangaza lahaja iliyosanifishwa ili itambulike kwa watu wengine
  • Kuandaa wataalam wenyeji wa usanifishaji watakaoshughulika na usanifishaji baada ya wageni kuondoka
Wataalamu wa kizungu ndio walioshughulika na usanifishaji wa Kiswahili. Baada ya uhuru TUKI (TATAKI), BAKITA na vyombo vingine vya ukuzaji wa lugha ndivyo vinavyoshughulika na usanifishaji wa lugha.
Usanifishaji wa lugha ya Kiswahili ulifanywa na Waingereza wakati wakitawala makoloni ya Tanganyika, Kenya na Uganda. Walilenga kupata lugha ya kufundishia katika makoloni yote ya Afrika Mashariki kwa hiyo mwaka 1925 Gavana wa Tanganyika Sir Donald Cameroon aliitisha mkutano Dar es Salaam, mkutano huo ulihusisha wakuu wa elimu wa nchi za Afrika Mashariki ili kujadili jinsi ya kupata lugha moja ya kufundishia kutokana na kuwepo kwa lahaja nyingi. Katika mkutano huo wajumbe waliteua lugha ya Kiswahili itumike kufundishia katika hatua za awali.
Mwaka 1928 mkutano mwingine uliitishwa mjini Mombasa ambapo lahaja ya kiunguja iliteuliwa kuwa lahaja ya usanifishaji.
Matukio wakati wa usanifishaji wa Kiswahili
  1. Kuitishwa kwa mkutano na Gavana wa Tanganyika (1925) ulioshirikisha nchi zote za Afrika Mashariki mjini Dar es Salaam ili kujadili na kuchagua lugha moja ambayo ingetumika shuleni katika nchi zote nne.
  2. Kuchagua lahaja ya Kiunguja kuwa lahaja ya usanifishaji ili itumike katika shughuli rasmi katika Afrika Mashariki, mkutano ulifanyika (1928) mjini Mombasa na wajumbe kutoka nchi zote nne akiwemo Prof Carl Meinholf mwanaisimu mashuhuri alihudhuria.
  3. Kuundwa kwa kamati ya ukuzaji na usanifishaji wa lugha ya Kiswahili (1930) iliyoitwa The Inter-Territorial Language (Swahili) Committee.
  4. Kuundwa kwa shirika la uchapaji wa miswada lililoitwa The East African Literature Bureau (EALB, 1948)
  5. Kuiweka kamati ya lugha chini ya Chuo cha Afrika Mashariki cha uchunguzi wa jamii (East African Institute of Social Research) cha Makerere (1952).
  6. Kuanzishwa kwa vyombo vya habari kama redio na magazeti. Magazeti kama vile: Mambo Leo, Habari za Mwezi, Tazama, Barazani, Kiongozi, Afrika Kwetu, n.k. Redio ilianza rasmi matangazo mwaka 1950 kwa lugha ya Kiswahili ikijulikana kama Sauti ya Dar es Salaam na baadaye Sauti ya Tanganyika.
  7. Kuundwa kwa chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanganyika (UKUTA, 1959) ili kushughulika na sanaa ya ushairi na ngonjera.
Kipimo cha Lahaja ya usanifishaji/Sababu za kuteuliwa kwa Lahaja ya Kiunguja
  1. Lahaja ya usanifishaji ilipaswa kuwa na ulinganifu katika eneo kubwa kimsamiati na hati za maandishi.
  2. Iwe inaandikika
  3. Iwe na mawanda mapana kimatumizi
  4. Iwe ni kipimo cha kutambulisha matumizi sanifu na yasiyosanifu
  5. Iwe na historia ndefu kimatumizi
  6. Iweze kubadilika kulingana na mazingira na wakati
  7. Ipokee msamiati toka lahaja/lugha nyingine
Kuundwa kwa kamati maalumu ya lugha
Mkutano wa Mombasa ulipendekeza kiundwe chombo maalumu ambacho kingesimamia na kuratibu utumizi wa Kiswahili na kutilia mkazo usanifishaji wake. Mnamo tarehe 1 Januari 1930 kamati ya kukuza na kusanifisha Kiswahili iliundwa na kuongozwa na Fredrick Johnson kama Katibu wake wa kwanza. Kamati hiyo ilijulikana kama The Inter-Territorial Language (Swahili) Committee, ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya nchi zote za Afrika Mashariki, yaani Tanganyika, Zanzibar, Kenya na Uganda.
Majukumu ya kamati ya Lugha
  1. Kueneza mtindo mmoja wa lugha ya Kiswahili katika nchi zote za Afrika Mashariki
  2. Kuleta ulinganifu wa kisarufi kwa kuchapisha vitabu vya sarufi vitakavyokubalika
  3. Kuwatia moyo kwa makusudi waandishi ambao ni wenyeji wan chi hizi ili waweze kuandika vitabu vya lugha ya Kiswahili
  4. Kuleta ulinganifu wa matumizi ya maneno yaliyopo na maneno mapya yatakayoundwa kwa kusimamia uchapishaji wa kamusi za shule na nyinginezo
  5. Kutoa ushauri juu ya utunzi wa vitabu kwa watu wote wenye hamu au nia ya kuwa waandishi wa vitabu vinavyokusudiwa
  6. Kuhariri vitabu vya Kiswahili vinavyotarajiwa kutumika shuleni pamoja na vitabu vya hadithi za kuburudisha
  7. Kutafsiri katika Kiswahili vitabu vya lugha ya Kiingereza vilivyochaguliwa kutumika shuleni kama vitabu vya kiada au vya ziada au kutunga moja kwa moja vitabu hivyo
  8. Kujibu maswali mbalimbali yanayohusu lugha ya Kiswahili na fasihi yake
  9. Kila mwaka kutoa vitabu vya Kiswahili vya kiada na ziada
  10. Kutoa kamusi na kuandaa vitabu vya shule vya Kiswahili sanifu
     Mafanikio ya kamati
Katika jitihada za utekelezaji wa majukumu yake, kamati ilipata mafanikio mbalimbali kama vile:
  1. Iliweza kuchapisha kamusi ya Kiswahili sanifu iliyojulikana kama Standard Swahili – English Dictionary pamoja na Standard English – Swahili Dictionary
  2. Iliweza kutoa jarida lenye makala mbalimbali kuhusu lugha ya Kiswahili lililoitwa Bulletin of Inter – Territorial Language (Swahili) Committee.
  3. Ilipitia miswada mbalimbali ya vitabu vya Kiswahili ili kutoa vibali vya uchapishaji wake
  4. Ilifanya uchunguzi wa lahaja mbalimbali za Kiswahili
  5. Kurahisisha mawasiliano miongoni mwa jamii za Afrika mashariki kwa kutumia lugha moja ya Kiswahili
Matatizo yaliyojitokeza wakati wa usanifishaji wa Kiswahili
Kazi ya usanifishaji wa Kiswahili wakati wa Waingereza haikupita kirahisi tu, ilikumbana na matatizo mbalimbali kama vile:
  1. Kutokubaliwa kwa lahaja ya usanifishaji: Kuchaguliwa kwa Kiunguja na kuachwa kwa Kimombasa kuliletata mgogoro mkubwa uliofanya Kiswahili sanifu kikataliwe na kuonekana kuwa ni njama za kudhoofisha na kudhalilisha Kimombasa kilichokuwa na historia ndefu kuliko Kiunguja.
  2. Kutoshirikishwa wenyeji: kutokana na mchakato mzima wa usanifishaji kufanywa na wageni wenyeji walijiona wamedharauliwa mno na hivyo wakapinga muelekeo wa kugeuza lugha ya Kiswahili toka tabia na asili yake wakapendekeza sarufi iimarishwe kwa kuangalia vilugha au lahaja nyingine.
  3. Tatizo la fedha za kuendeshea kamati: serikali ya kikoloni ilitoa fedha kidogo sana kwa ajili ya usanifishaji wa Kiswahili hali iliyofanya kamati ya lugha ishindwe kufanya kazi zake ipasavyo na matokeo yake yakawa ni kulegalega kwa maendeleo ya lugha hasa maeneo ambayo hayakushawishi kwa shughuli za uzalishaji mali.
  4. Tatizo la vitabu: kamati ya usanifishaji ilimudu kutoa vitabu vichache ambavyo havikutosheleza mahitaji ya watumiaji wa lugha ya Kiswahili, hali hii ilifanya kazi ya usanifishaji iwe ngumu mno.
  5. Kutothaminiwa kwa machapisho ya usanifishaji: wazawa wengi hawakuthamini machapicho yaliyotolewa na kamati ya lugha kwa sababu yalikuwa na kasoro nyingi zilizotokana na matumizi ya sarufi ya Kiingereza kusanifishia Kiswahili. Hali hii ikafanya baadhi ya maneno kuandikwa tofauti na yanavyotamkwa hasa na wabantu. Mf:
  Kibantu        Matamshi   Kiswahili sanifu
   Inge                 nnge               nge
   Umbwa           mmbu             mbu
   Inzi                  nnzi                nzi
   Umbu              mmbu             mbu
  1. Matumizi duni ya Kiswahili: Kiswahili hakikupewa hadhi na nafasi ya kutosha kama ilivyo kwa lugha ya Kiingereza, mathalan Kiswahili kilionekana kama lugha ya makabwela tu kutokana na kutumiwa na manamba, madarasa ya chini shuleni, pamoja jumbe,akida na liwali walioonekana kama vibaraka wa wazungu.
Kuteuliwa kwa kiunguja kulivyodumaza lahaja nyingine
  1. Lahaja teule hupata hadhi ya juu, hivyo matumizi ya lahaja nyingine yanaonekana kama ni ya watu wa hali ya chini.
  2. Lahaja sanifu huandikwa katika vitabu vya sarufi sanifu na kamusi, hivyo kutumika katika mifumo rasmi kama elimu.
  3. Lahaja rasmi huteka mawasiliano yote ndani ya jamii husika na kufanya lahaja nyingine kupoteza idadi kubwa ya wazungumzaji.
  4. Lahaja sanifu huweza kupitishwa kuwa lugha ya taifa kama ilivyo kwa Kiswahili na matokeo yake lahaja nyingine hukosa utambulisho mpana kitaifa na hata nje ya taifa.
  5. Lahaja sanifu huchukua maneno ya lahaja nyingine na kufanya lahaja nyingine zikose sifa ya usiri katika mawasiliano na kufanya wenye lahaja zao wasiache.

Print this item

  MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA NA LUGHA YA TAIFA (KISWAHILI)
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 03:59 PM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA NA LUGHA YA TAIFA (KISWAHILI)
USULI WA LUGHA YA KISWAHILI
Kabla ya kuingia kwa undani kuangalia lugha hii ya Kiswahili baada ya uhuru. Tunaweza kutalii dhana ya lugha na usuli wa lugha ya Kiswahili.
Dhana ya lugha
Wanaisimu wamekuwa wakitazama dhana ya lugha kwa mitazamo mbalimbali. Mitazamo hiyo huweza kutoa taswira ya maana ya lugha inavyo weza kuwa.
Lado (1964) Lugha ni chombo cha mawasilianoa baina ya binadamu katika jumuia Fulani.
Potter (1960) Lugha ni utaratibu wa alama za sauti zilizopangiliwa kutokana na mazoea au matamshi ya watu kwa njia ya sauti ambazo wanadamu wanapelekeana habari na wanasikilizana
TUKI (2004)  Lugha ni mpangilio wa sauti na maneno unaoleta maana ambao hutumiwa na watu wa taifa au kundi fulani kwa ajili ya kuwasiliana.
Kutokana na mitazamo hiyo lugha ya weza kufasiliwa kuwa  ni sauti za nasibu za binadamu zinazobeba maana na zilizokubaliwa na jamii ya watu ili zitumike katika mawasiliano yao ya kila siku.
LUGHA YA KISWAHILI
Kama zilivyo lugha nyingine za kitaifa na kimataifa, Lugha ya kiswahili ina tabia ya kusemwa, kuzungumzwa na kuandikwa kwa nia ya kukamilisha mawasiliano miongoni mwa wanajamii wa kiswahili. Lugha ya kiswahili ni lugha rasmi na Lugha ya Taifa kwa upande wa Tanzania ingawa kwa Watanzania ni lugha ya Pili. Lugha ya kiswahili ina watumiaji wanaokadiliwa  kuwa ni zaidi ya milioni 37 kwa Tanzania. Kiswahili kinafundishwa katika shule za msingi, sekondari na vyuoni. Hivi sasa kiswahili kimeteuliwa na kupewa baraka zote  kuwa  lugha ya Umoja wa Afrika na Kiswahilli kina hadhi ya nafasi ya sita kimataifa kikitanguliwa na na Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, na Kireno. Pia inakadiriwa kuwa Kiswahili kina wazungumzaji zaidi ya Milioni 160 Duniani. Kuna vituo mbalimbali vya redio na luninga vinayotangaza kwa kiswahili Ndani na nje ya bara la Afrika kama vile Sauti ya Amerika, BBC London, Sauti ya uajemi, KBC, na vingine vingi.Pia kuna vyuo vingi duniani vinavyofundisha lugha ya kiswahili mfano katika bara la Afrika, Asia, Ulaya, na Marekani. Vyuo hivyo ni pamoja na Chuo Kikuu cha Minesota, Vyuo vikuu mbalimbali duniani mfano Ujerumani, Uingereza kwa kutaja baadhi.
HISTORIA YA LUGHA YA KISWAHILI
Kuna nadharia mbalimbali zinazoeleza historia ya lugha ya kiswahili, mfano wa nadharia hizo ni nadharia ya kihistoria, na nadharia ya kiisimu
Katika nadharia ya kihistoria inaeleza historia ya kiswahili kwa ujumla. Mfano historia ya Kilwa, ushahidi wa marco Polo na Ushairi wa Fumoliyongo unaosemekana ni ushairi wa Kiswahili ulioandikwa karne ya kumi na tatu BK. Nadharia ya kiisimu inaeleza taratibu na kanuni za lugha. Mfano upatanisho wa kisarufi, maumbo ya maneno (umoja na wingi), muundo wa tungo (kiima na kiarifu) mnyumbuliko wa maneno (kitenzi) na tabia ya vitenzi vya lugha ya kiswahili.. Hivyo lugha ya kiswahili inaweza kutazamwa kwa mtazamo ya kiisimu na kihistoria katika kupata historia ya lugha ya kiswahili kwa usahihi wake. Pamoja na kuwa wananadharia hawa hutofautiana, huweza kukubaliana kwa kutojua au kwa kujua kuwa kiswahili kimetokana na Kibantu.
            Kutokana na shahidi mbalimbali Mfano Shihabuddin Chiraghdin na Mathias Mnyapala (1988) wanaeleza kuwa asili ya lugha ya kiswahili ni kibantu ambacho kinazungumzwa zaidi katika upwa wa Afrika Mashariki mfano Pate, Unguja, Lamu, Comoro, Pemba, Mombasa, Kilwa, Tanga kwa kutaja baadhi. Wageni walikuja hususani Waarabu walikuta lugha hii ya kiswahili ikiwa inazungumzwa na wenyeji wao wa mwambao wa upwa wa Afrika mashariki kwa Lahaja tofauti tofauti kulingana na maeneo mfano kimakunduchi, kimtang`ata (Pangani na Tanga), Kingozi, (Pate na Kisumayu) Kitumbatu, Kimrima(Dar es salaamu na Tanga) Kimvita (Mombasa) Chimiini (Mogadishu/ Somalia) kwa kutaja baadhi. Lugha hizi zinafanana. kutokana na kufanana huko walipokuja Waarabu wakaziita lugha zote zilizokuwa zikizungumzwa upwa wa mashariki mwa Afrika ni Sahil. Kutoka na sababu kadha wa kadha na athari za matamshi ikatokea swahili na baadaye ikapatikana lugha ya kiswahili
Katika ujio wa waingereza ndipo shughuli za usanifishaji zilipoanza. Katika shughuli za usanifishaji shughuli mbalimbali zilifuatwa ikiwa ni pamoja na uteuzi wa lahaja moja miongoni mwa lahaja nyingi zilizokuwepo. Lahaja ya kiunguja ikateuliwa na kufanyiwa mchakato wa usanifishaji. Ndipo tukapata kiswahili sanifu. mfano wa maneno yaliyosanifiwa ni kama :-
Kiunguja                                 Kiswahili sanifu
Cai                                           Chai
Cumba                                     Chumba
Ceza                                        Cheza.  Kwa kutaja baadhi
KISWAHILI BAADA YA UHURU
Baada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kukiendeleza na kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na kupendekezwa kuwa lugha rasmi 1962.
1964 kiswahili kilipendekezwa kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumika katika shughuli zote za kiserikali na kitaifa mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.
Kundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza maendeleo ya kiswahili, kutayaricha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na fasihi ya lugha ya kiswahili na kuandaa wataalamu watakaoshughulikia usanifishaji wa kiswahili
Pia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya kiswahili. Mfano:- BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo Kikuu Cha Dar es salaamu.
Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa nchini. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha ya Taifa, Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia katika shule za msingi. kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza kiswahili, Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa, shughuli mbalimbali za kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala na shughuli za kiutamaduni na uchapishaji wa vitabu na majarida mbalimbali.
KISWAHILI KUWA LUGHA YA TAIFA
Baada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia kiswahili katika shughulizote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi. Pia kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili kilihimizwa kutumika katika mawasiliano yote hususani katika mawasiliano yote hasa katika shughuli za umma na Wizara zote, Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupanda hadhi zaidi wakati wa Azimio la Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa na kuandikwa kwa lugha ya kiswahili.
KUUNDWA KWA VYOMBO VYA UKUZAJI NA UENEZAJI WA KISWAHILI
Tanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya kukuza na kueneza kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo ni UWAVITA BAKITA TUMI TUKI Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu Dar es salaam.
KUTUMIKA KATIKA ELIMU
Kiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali, kilipendekezwa kutumika katika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya sekondari kama somo na katika vyuo vikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazima ambao hawakujua kusoma na kuandika. Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengi kujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwa nchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya, Siasa, Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengi kuzungumza kiswahili sanifu.
VYOMBO VYA HABARI
Tangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa. Vyombo hivi hutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu wengi licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti na majarida mbalimbali ambayo huandikwa kwa lugha ya kiswahili lakini kuna redio na runinga ambazo matangazo yake hutangazwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.
BIASHARA
Shughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na kuwepo kwa makabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika katika biashara hizo.
SHUGHULI ZA SIASA NA UTAWALA
Tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo muhimu kuwaunganisha wananchi. Shughuli nzima za kisiasa zimetumia lugha hii katika kujiimarisha; mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha  na Mfumo wa vyama vingi Kiswahili kimetumika kama njia kuu ya mawasiliano. Pia katika utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli katika nyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote za kiutawala. Hivyo shughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza, kukieneza na kukiendeleza kiswahili.
UANDISHI NA UCHAPISHAJI WA VITABU
Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi ambavyo vilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili na utamaduni wake, mfano :- F Nkwera, Shabani Robart, Mathias Mnyapala na  Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.
SHUGHULI ZA KIUTAMADUNI

Shughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya kiswahili. Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe mbalimbali za kijamii ambazo zimesaidia kukiendeleza kiswahili kwa kuwa huwakutanisha watu tofautitofauti katika shughuli hizo, ambapo huwalazimu kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahili kuendelea. Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya kiswahili kutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza kiswahili Mfano;-(    ) Pia katika sherehe mbalimbali za kiserikali na kisiasa hususani vyama mbalimbali vya kisiasa mfano bendi ya TOT  inayoongozwa na kepteni Komba.

MAFANIKIO YA KISWAHILI WAKATI WA UHURU MPAKA SASA
Kiswahili kimeweza kujizolea na kinendelea kujizolea sifa kemkem ndani ya  Miaka  50 ya uhuru wa nchi yetu hatuna budi kukitolea mifano ili tuone kwa namna moja au nyingine jinsi kilivyofanikisha kuwaunganisha Watanzania katika mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni na kusababisha matokeo hasi kwao ambapo kubwa zaidi ni kujipatia uhuru. Kwa maana nyingine, Kiswahili kiadhimishwe kama lugha ya ukombozi wa nchi yetu wa mwaka  1961.
            Mpaka sasa kiswahili kimefanikiwa kuwaunganisha watanzania wote na kwa maneno yake yaliyojaa faraja na matumaini, kimeweza kudumisha amani ya Tanzania (nchi yetu) kwa miaka hamsini sasa. Bado kinaendelea kuwaweka pamoja watanzania na kuwafanya kuwa kitu kimoja. Pia kimetoa mchango mkubwa katika kuipa sifa kubwa nchi yetu ya Tanzania na kuwa mfano wa kuigwa duniani kote. Tanzania imepewa sifa ya kisiwa cha amani kutokana na amani ya muda mrefu iliyopo nchini ambayo inasimamiwa vilivyo na lugha yetu ya kiswahili.
Katika nyanja ya fasihi, Kiswahili kimeweza kuelezea utamaduni wa nchi nyingine kama vile Kongo Afrika kusini, Uganda n.k . Kwa kutumia muziki kwani sasa kuna wanamziki wengi wanaotoka katika nchi hizo wanaotambulisha utamaduni wao kwa lugha ya kiswahili. Baadhi yao ni Mbili Abel Kutoka kongo, Ivon Chakachaka kutoka Afrika Kusini, Marehemu Miriam Maakeba Kutoka Afrika Kusini pamoja na Jose Kamilion kutoka nchini Uganda. Pia kuna baadhi ya wanamziki kutoka Korea waliweza kuonesha hisia zao kwa kutumia lugha ya kiswahili katika uimbaji wao.
Lugha ya kiswahili ina utajiri wa maneno (msamiati) ambao katika lugha nyingi za kimataifa hazina msamiati huo kama Kiingereza hakina msamiati wa aina hiyo, Mfano wa misamiati hiyo ni pamoja na Shangazi, Baba mdogo, Baba mkubwa, Ugali nk. Kutokana na tafiti zilizofanywa kiswahil kinaonekana kuwa ndiyo lugha pekee kwa sasa ambayo inakubarika kwa kasi zaidi duniani kote kuliko lugha nyingine zinazokua. Hii ni kutokana na ongezeko la watu wanaohitaji kujifunza na kuzungumza kiswahili duniani kote.
Pia kiswahili kimeweza kufikia kiwango cha juu sana cha kusikika kwani sasa kinasikika dunia nzima. Hii ni kutokana na mashirika makubwa ya habari yanayorusha matangazo kwa kutumia lugha ya kiswahili. Mfano BBC, Sauti ya Ujerumani. (Deutsche Welle ) Sauti ya Amerika, Pamoja na shirika la utangazaji la Tanzania TBC kupitia kituo cha runinga kinachorusha matangazo yake kupitia kituo cha DSTV kilichopo nchini Uingereza, kinachorusha matangazo kwa njia ya setilaiti.
Mafanikio mengine ya kiswahili ni kufanikiwa katika sayansi mbalimbali katika jamii ambapo kiswahili kimetumika kuandika vitabu mbalimbali kwa kutungwa au kufasiriwa na wataalamu mbalimbali. mfano  kitabu kinachohusu afya ya binadamu kilichotafsiriwa ambacho hata sasa hutumika katika kufundishia wataalamu wa afya katika vyuo vikuu. kitabu hiki kimefasiliwa na Daktari(….)
Pia Watanzania wanaoishi katika nchi za dunia ya kwanza  wameonyesha nia ya dhati  ya kuwasaidia vijana wakitanzania  kutambua thamani kubwa   ya lugha yao ya Kiswahili. Kwa mfano, Freddy Macha, Mtanzania aishiye Uingereza  kwa kushirikiana na watanzania wengine waliopo barani Ulaya. Wamedhamiria kwa dhati kulifanikisha hilo kwa vitendo, ambapo hivi karibuni wanatarajia kufanya semina na vijana wa Tanzania hapahapa nyumbani. Kwa kushirikiana na Mtandao wa Maendeleo ya Vijana Tanzania (MMVT) na vijana wengine na kujadili mada mbalimbali ikiwamo mada ya Kiswahili inayohusu umuhimu wa kujua lugha mbalimbali kikiwamo Kiswahili na namna ya kukitumia kama nyenzo ya maendeleo na biashara.
Nao Watanzania waliopo Denmark  wamepongeza juhudi zinazofanywa na wadau wa Kiswahili nyumbani  (Tanzania) kwa namna moja au nyingine katika kukikuza na kukieneza Kiswahili na wanakubaliana na misingi iliyowekwa na waasisi wa taifa letu, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume  katika kuitumia lugha ya Kiswahili kama kitambulisho cha taifa, ambapo Kiswahili kinatumika kama lugha ya taifa.
Pia wanawapongeza viongozi waliofuata kwa kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili   katika nyanja ya muhimu za elimu, uchumi na utamaduni wa taifa letu la Tanzania
            Pia, watanzania na wadau wote wa lugha ya Kiswahili wanampongeza  Rais mstaafu wa awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Rais wa awamu ya tatu Mh.Benjamini Willium Mkapa wamekuwa Viongozi hodari wa kukisimamia na kukieneza Kiswahili. Hawakuwa nyuma kumpongeza  Raisi  Kikwete kwa  kuhakikisha Watanzania wanafahamu umuhimu wa lugha ya kiswahili  nchini na duniani kote yeye alitia msisitizo kwa kuhutubia mkutano wa Umoja wa Afrika kwa Kiswahili .
Kituo cha runinga cha TBC 1 nacho kwa nafasi na mchango wake katika lugha, kimekuwa kikirusha kipindi cha Lulu za Kiswahili pamoja na kipindi cha Ulimwengu wa Kiswahili na kujadili masuala ya lugha ya  Kiswahili nchini na nje ya nchi. Pia vituo vingine vya runinga ni kama star TV na ITV Ambayo havipo nyuma katika kukieneza na kutangaza Kiswahili.
            Vilevile, kuingizwa Kiswahili katika mtandao ni hatua kubwa inayoonyesha kwamba, Kiswahili kinaendana na hali ya utandawazi ambapo watu wamekuwa wakipata taarifa ambazo zimetafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili. Na kufanya watu wengi hususani wanaojua Kiswahili kusoma makala mbalimbali katika matandao na kupata habari kwa kina.
            Kuwapo kwa kamusi za lugha katika tovuti ambazo huwezesha watu kujifunza lugha kupitia njia ya mtandao.
Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Skuli ya Sanaa na Lugha  pamoja na kuongezeka kwa vyuo vinavyofundisha shahada ya lugha ya  Kiswahili nchini kama vile vyuo vikuu vya SAUT, Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro, Chuo Kikuu cha Serikali Zanzibar (Suza), Tumaini na pia Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM) hatua hiyo imesababisha kuwa na wasomi wengi wenye taaluma ya Kiswahili, licha ya  changamoto ya wanafunzi hao wa Kiswahili kuwa na upungufu wa maeneo ya kufanya  mafunzo ya vitendo, ni changamoto inayopaswa kuangaliwa na kufanyiwa kazi.
Kuongezeka kwa istilahi za lugha ya Kiswahili ni jambo linaloashiria kupanuka kwa matumizi ya Kiswahili na ndiyo maana kumekuwapo na machapisho ya kamusi mpya mara kwa mara ili kukidhi mahitaji na matumizi ya lugha ya kila siku katika mawasiliano . Istilahi hizo zinaongezeka kutokana na sababu mbalimbali za kijamii, kiutamaduni, kisiasa, kiuchumi lakini pia maendeleo ya sayansi na teknolojia Mfano wa istilahi hizo ni kamazifuatazo;-
Chakachua, ngangali, ng`atuka, ngamizi.
            Vilevile, kuingia katika mfumo wa mawasiliano kwa njia ya setelaiti (digitali) kumehamasisha zaidi matumizi ya Kiswahili hasa katika tasnia ya utangazaji hususani redio na runinga, mfano TBC na ATN. Hivyo hufanya mawasiliano kuwa rahisi miongoni mwa wasikilizaji wao.
Mafanikio menginie ni kuongezeka kwa watu kutoka mataifa mbalimbali ikiwemo Ulaya, Amerika, Asia na kwingineko kuja Tanzania kujifunza Kiswahili. Pia kufanya tafiti kuhusiana na lugha ya Kiswahili
Kuongezeka kwa nchi nyingi dunia zinazotumia lugha Kiswahili katika mawasiliano na kuhitaji wataalamu wa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya watu wao kujifunza Kiswahili mfano Botswana, Libya, Malawi na Afrika Kusini.
Kiswahili kimekuwa kama sehemu ya ajira katika taasisi na mashirika mbalimbali ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali. Mfano katika tafsiri na ukalimani, pia katika kutoa Elimu Kiswahili kinatumika. Hii inawafanya watumiaji wa lugha hii kuongezeka kwa kasi kubwa.
Kuwepo kwa machapisho mengi ya Kiswahili na kuwepo kwa waandishi wengi wanaoandika kazi mbalimbali za Kiswahili mfano katika fasihi na sarufi ya Kiswahili.
Mfano wa waandishi maarufu walio kama chachu ya maendeleo ya Kiswahili ni              F. Kezilahabi, F. Nkwera, J. Madumulla, I. Huseni, T.Sengo, Kingo, Chachage, Penina Mlama, S. Shaffi na Asha Kunemah. Ambao wametoa changamoto kubwa katika kukikuza na kukiensza Kiswahili. Pia wameonesha mafanikio makubwa katika kazi zao.
Kiswahili kimekuwa maarufu sana na kukubarika katika nchi za Afrika Mashariki. Mfano nchini Uganda, Rwanda, Burundi na Kenya, mathalani nchini Kenya Kiswahili kimekuwa lugha ya Taifa. Kuandikwa kwa katiba ya Kenya kwa lugha ya Kiswahili na kuwa lugha ya Taifa katika nchi za Afrika Mashariki. Hivyo kukifanya kiswahili kuwa na hadhi kubwa ndani na nje ya bara la Afrika
KISWAHILI NA UTANDAWAZI
Utandawazi ni dhana pana ambayo imeenea na kugusa nyanja mbalimbali ikiwemo ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Kiswahili ikiwa ni sehemu ya utamaduni kimeguswa na kuathiriwa na utandawazi.
Dhana ya utandawazi inaweza kuangaliwa kwa mitazamo mbalimbali. Miongoni mwa dhana hizo ni aina ya tabaka jipya la kibepari lililojitutumua kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi, kisiasa, na kiutamaduni. Kujiinua huku hudhihirika katika taaluma na  vyombo vya habari mfano matangazo  na kufanya kuwa dhana inayoenea kwa kasi na kugusa nyanja mbalimbali duniani. Hivyo utandawazi unaweza kuifanya dunia kuwa kama  kijiji . Utandawazi una muonekano wa mradi wa kiitikadi na ajenda ya kujenga mahusiano ya kibinadamu na ambayo ni ngumu kueleweka kwa wanazuoni mbalimbali na kuonekana kuwa ni dhana mpya.
UTANDAWAZI KATIKA UTAMADUNI
Utandawazi huendana na mambo mbalimbali kama vile Lugha, Sanaa, Mavazi, na namna ya kula na hivyo jamii kuathirika kwa sehemu kubwa. Jamii huweza kuathirika kwa kupoteza amali za jamii kwa kupokea mambo ya jamii nyingine hususani mambo ya kimagharibi. Hivyo kiswahili kama sehemu ya utamaduni wa Taifa letu imeathirwa kwa sehemu kubwa.
KISWAHILI NA UTANDAWAZI.
Utandawazi ulianza kuingia katika lugha ya kiswahili wakati wa utawala wa kikoloni. Ambao ulisababisha mabadiliko mbalimbali katika lugha ya kiswahili. mfano Dini, biashara, utawala na elimu vilisaidia kukuza na kueneza lugha ya kiswahili. Utawala wa kikoloni uliambatana na kuanzishwa kwa vyombo vya habari kama vile magazeti, redio. Runinga, tovuti na simu ambapo kuliimarisha utandawazi na kiswahili kupata matumizi makubwa.
Kutokana na utandawazi kumekuwa na ushindani mkubwa katika mambo mengi ikiwemo Lugha. Lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa lugha zilizo kwenye ushindani huo. Lugha hii inakubalika na watu wengi wanaoitumia katika mawasiliano, na kukifanya kiswahili kuingia katika utandawazi kwa lengo la kuiunganisha jamii.
Katika utandawazi ajira inaongezeka, Mathalani mtu anayetumia lugha nyingine nje ya kiswahili anakuja nchini  kwa lengo la uwekezaji hulazimika kujifunza kiswahili ili kudumisha mahusiano na wenyeji wake. Hivyo huongeza walimu wa lugha kwa ajili ya kufundisha lugha ya kiswahili pia huweza kueneza lugha kwa njia ya ukalimani.
Watanzania wengi huchukuliwa na nchi mbalimbali kwa lengo la kufundisha lugha ya kiswahili katika nchi zao.
Utandawazi huweza kusaidia kuongeza msamiati wa lugha. Kiswahili ni miongoni mwa lugha inayopokea maneno kutokana na matumizi yake yanayotokana na utandawazi hususani katika maendeleo ya sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni na uchumi. Mfano katika maendeleo ya sayansi na teknolojia, kuna istilahi nyingi za kimtandao.
Utandawazi umeweza kuongeza idadi ya watumiaji wa lugha ya kiswahili. Ambapo ikadiliwa kuwa katika nchi za maziwa makuu idadi ya watumiaji wa lugha kiswahili ni zaidi ya milioni 60.
MADHARA YA UTANDAWAZI
Kila kitu kina pande mbili, kadharika utandawazi nao una pande mbili faida na hasara. Baada ya kuangalia upande mmoja wa shilingi uzuri wa utandawazi katika kiswahili. Sasa tuangalie madhara ya utandawazi katika lugha ya kiswahili
Mosi kutokana na utandawazi kumekuwa na kudharau lugha ya kiswahili. ambapo lugha hii ya kiswahili inaonekana kuwa ni lugha ya watu wa tabaka la wasionacho. Pia Watu huiona lugha ya kiswahili kuwa ni lugha ya watu wasiojua kitu chochote duniani. Kiswahili kinaonekana kuwa si lugha ya sayansi na teknolojia na kwamba haiwezi kutumika katika shughuli zote za kisayansi  hususani katika taaluma ya ufundi.
CHANGAMOTO  KATIKA LUGHA YA KISWAHILI
Pamoja na hadhi na umaarufu wa kiswahili, bado lugha hii inakumbana na matatizo makubwa ya dhana na matumizi ya lugha ya kiswahili.
Katika dhana ya kiswahili bado kuna baadhi ya watu wanaonasibisha kiswahili na dini ya kiislam hili limekuwa ni tatizo kubwa miongoni mwa watumiaji wa lugha hii.
Pia upinzani mkubwa kutoka katika lugha ambazo zimekwisha jitanua katika dunia Mfano:- Kiingereza, Kifaransa, Kireno na Kiarabu. Watumiaji au watu wenye asili na lugha hizo wanakipiga vita kiswahili wakihofia kuwa wasipofanya hivyo kitazimeza lugha zao.
Kudharauliwa kwa lugha ya Kiswahili na kupigiwa chapuo kwa lugha za kigeni kwamba ndio pekee zinazofaa kutumika katika shughuli mbalimbali za kiuchumi. Hivyo kiswahili kuonekana kuwa hakifai kutumiwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi.
Kasumba mbaya na mtazamo hasi wa Watanzania katika lugha ya Kiswahili ambao unawafanya watanzania kukitukuza zaidi kiingereza na kutojua kuwa kiingereza ni sawa na lugha nyingine tu.
Kucheleweshwa kwa maamuzi ya sera ya kukipa hadhi kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika nyanja zote za elimu, na kiingereza kuwa somo tu. Hivyo inarudisha nyuma maendeleo ya kiswahili.
Watanzania kuwa nyuma katika kufanya tafiti mbalimbali juu ya lugha ya kiswahili ili kuona ni jinsi gani tunaweza kufunguka kiakili na kufahamu umuhimu wa kuwa na lugha ya kiswahili
Uchumi mdogo wa nchi yetu unakwamisha kwa sehemu kubwa maendeleo ya haraka ya lugha ya kiswahili duniani. Kwa kuwa nchi inashindwa kuzalisha wataalamu wengi wa lugha hii, pia inashindwa kufasiri maandiko kutoka lugha nyingine kuwa katika lugha ya kiswahili kwa sababu ni ghari mno.
Watanzania wanakosa moyo wa kuthamini na kujali tamaduni zao ambapo kiswahili ni lugha inayotangaza utamaduni wao lakini wao wanathamini sana utamaduni wa kimagharibi. Kwa hakika hii ni changamoto kubwa ambayo inakikumba kiswahili katika harakati zake za kujitanua duniani kote.
Pia kuna dhana kuwa Kiswahil ni lugha ya watu duni kitaaluma mathalani watu walioishia darasa la saba. Hivyo hufanya watu kutaka kujifunza Kiingereza. Hii ni dhana ya watu potofu kabisa ambayo inajitokeza kwa watu ambao ni wasomi kabisa.
Kwa upande wa matumizi ya lugha ya Kiswahili, kumekuwa na matatizo makubwa ya kutumiwa isivyosahihi na matumizi yasiyofasaha katika nyanja zake za kimatamshi, kimaandishi na kimaana.  Matatizo hayo ndiyo yanayopelekea kutokuwa na kiswahili sahihi na fasaha. Jambo la kusikitisha na kushtua zaidi ni kuwa kwa muda mrefu, kumebaini na kuwa na kiswahili sanifu nchini lakini kiswahili hiki kinazungumzwa na kuandikwa kimakosa mno. Makosa haya hutendwa na taasisi mbalimbali zikiongozwa na vyombo vya mawasiliano. Mfano katika magazeti waandishi wanatumia lugha inayokiuka misingi na kanuni za kiswahili sanifu tunachokielewa au wanachofundishwa wanafunzi.
MAKOSA YANAYOFANYWA NA UMMA WA WATANZANIA
Makala hii inadokeza na kubainisha makosa ya matumizi ya kiswahili yanayofanywa na umma wa Watanzania, Vyombo vya mawasiliano na Walimu katika shule na vyuo. Pia inaeleza sababu za msingi na athari na matumizi yasiyosahihi  kwa jamii ya watumiaji wa Kiswahili hususani Watanzania wote. Baadaye kutakuwa na mapendekezo ya nini kifanyike ili kupunguza au kuondoa kabisa matatizo hayo ya makosa ya matumizi yasiyosahihi ya lugha hii kwa vyombo vyote vya umma na watu binafsi watumiaji wa kiswahili.
Kabla ya kuangalia makosa ya matumizi yasiyosahihi ya Kiswahili sanifu ni afadhali kwanza kudokeza maana ya umma wa Watanzania, maana ya matumizi yasiyokuwa sahihi ya Kiswahili na maana ya mawasiliano sahihi na fasaha.
MAANA YA UMMA WA WATANZANIA
Umma wa Watanzania kwa muktadha wa makala hii ni watu wengi wenye kutumia stadi ya kusema na kuandika kwa lugha ya kiswahili. Kwa upande wa kusema au kuzungumza makosa hayo hutokea katika shughuli zisizo rasmi na zile zisizorasmi katika mazingira tofautitofauti ya mawasiliano ya kila siku, kama vile mitaani, nyumbani, ofisini, shuleni na kazini. Kwa upande wa uandishi makosa hayo hutokea katika vitabu, magazeti, majarida na vipeperushi vya matangazo mbalimbali.
MAANA YA MAKOSA YA MATUMIZI YA KISWAHILI SANIFU
Maana ya makosa ya matumizi  ya kiswahili sanifu kwa upana wake ni yale matumizi ya kiswahili ama ya kuzungumzwa au kuandikwa ambayo yanakiuka taratibu na makubaliano ya kimawasiliano ya kisarufi ambayo ni sahihi na fasaha na kusababisha karaha au upotofu wa mawasiliano rasmi kwa wazawa na wajuzi wa kiswahili fasaha.
MAAN A YA MAWASILIANO SAHIHI NA FASAHA
Mawasiliano sahihi na fasaha ni yale mawasiliano ya kuitumia lugha ya yenye kufuata taratibu za maneno, miundo ya kisarufi pamoja na maana na kuweza kukubalika na wazawa na wajuzi wa lugha hiyo. Ikiwa inasemwa au kimaandishi, bila kuwa na uvulivuli, ukakasi au chukivu kwa wasikilizaji au wasomaji. Kigezo kikubwa cha lugha sahihi na fasaha ni ile lugha ya mazungumzo au maandishi ambayo ikisemwa au ikiandikwa haitagunwa na wazawa au wajuzi mahiri wa lugha ile. Mfano wa lugha ya Kiswahili isiyosahihi na isiyofasaha ni kama mtu akisema au kuandika hivi
 “Tuende wote pale tulikuwa juzi”
Sentensi hii ina makosa ya taratibu za kisarufi, katika upatanisho wa vipashio na muundo unaokubalika kwa wajuzi wa lugha hii na kuleta ukakasi na uvurivuri na  kusababisha kukosa ufasaha. Sentensi hii ilitakiwa kusemwa au kuandikwa hivi “Twende sote pale tulipokuwapo jana”
Hivyo ni uandishi na usemaji wa lugha ya kiswhili ni dhahiri kuwa huwa na taratibu wa kisarufi, muundo na upatanishi wa vipashio unafuatwa na unapelekea sentensi hiyo kuwa na mawasiliano sahihi na fasaha mbele ya wajuziz wa lugha
MAKOSA YA KISWAHILI YANAYOFANYWA NA UMMA WA WATANZANIA
Makosa hayo ya kimatumizi yanabainika kutawala katika maeneo ya matamshi, maumbo, miundo na maana; ama kimazungumzo au kimaandishi. Makosa makuu ya mawasiliano ya umma yanabainika katika nyanja zifuatazoa;-
1                    Matamshi na maandishi mfano thamani badala ya zamani, arubaini badala ya arobaini, samanini badala ya themanini. sambi badala ya Dhambi na sahabu badala ya dhahabu. Wngine pia hushindwa kutofautisha kati ya kula na kura hii inatokana na watu hawa kuwa wamawameathiliwa na lugha mama. Hivyo hata wakati wa kujifunza au kufunza lugha hufunza kwa makosa hayo.
2                    Maumbo ya maneno  ambayo kwa sehemu kubwa huendana na maana za maneno.
mfano:- Zoezi (kazi), zoezi (jaribio)
3                    Miundo ya sentensi, miundo mingi ya sentensi zinazotolewa huwa si sahihi na huleta ukengeushi mkubwa kwa wajuzi wa lugha mfano:- hadi hapo nawaageni, nachukua nafasi hii, kwa niaba yangu. Pia katoka muundo wa sentensi za Kiswahili huanza na nomino na kufuatwa na aina nyingine za maneno Mfano:- Mtoto mzuri anacheza jikoni
  N        V          T           E
                  Tena katika muundo kuna makosa ya upatanishi wa kisarufi ambapo watu wanapotosha au kuchanganya sarufi ya lugha ya Kiswahili.
Mfano:- sisi wote tunapenda nyama  badala ya kusema  Sisi sote tunapenda nyama.
4                    Machapisho na majarida mbalimbali ambayo kwa sehemu kubwa hutumia  lugha inayopotosha jamii, mfano:- pia vyombo mbalimbali vya habari kama Televisheni, Redio, Runinga. ambayo hutumia lugha hii visivyo na pengine hupotosha kabisa umma au jamii. mfano wa matumizi ya neno Chakachua ambapo mtu akakifanya vibaya wanasema amechakachua.
5                    Pia katika elimu kumekuwa na mkanganyiko mkubwa ambao unatoka na sera zisizo na msingi. Pia matatizo ya kimtaala ambayo huleta changamoto kubwa inayotokana na muhutasari wa elimu na mitihani inayotolewa. Katika muhutasari huonesha wanafunzi kujifunza kwa mlengo wa kimawasiliano unaopigia chapuo wanafunzi kupewa stadi za kuwasiliana zaidi huku ikilenga katika masuala mengine hususani upade wa sarufi.
6                    Pia kuna makosa ya kimsamiati ambapo watu huchanganya sana hususani wakati wa kuzungumza  hutumia msaniati usiolingana na maana iliyokusudiwa, pengine hutokana na kushindwa kutofautisha maneno hayo. Mfano: nenepa na nona, wasilisha na wakilisha, ajali na ajili, na mazingira na mazingara. Mfano:- Siku hizi Rachel amenona, badala ya Siku hizi Rachel amenenepa.
Haya ni baadhi ya makosa ya matumizi yasiyokuwa sahihi yanayofanywa na umma wa watanzania. Uzoefu unaonesha kuwa kati ya umma wa watanzania watu wa vyombo vya mawasiliano na habari vya umma huchukua nafasi kubwa ya kufanya makosa ya Kiswahili sanifu watu hao ni waandishi wa habari, wahariri wa magazeti na watangazaji wa redio runinga. kwa kubainisha vyombo hivi vichache  ni kama vifuatavyo: Magazeti Mtannzania, Mwananchi , uwazi, Nipashe, Uhuru Mzalendo Mwanahalisi na habari leo. Kwa upande wa Redia ni TBC Taifa, Radio one, Sauti ya Zanzibar, Redio uhuru nk Pia runinga ni TBC, ITV, Star TV, TVZ, ATA, EATV na DTV. Kinacho jitokeza hapa ni kuwa makosa yanayofanywa na watu hawa husambaa sana na kuchukua asilimia kubwa takribani pande zote za Tanzania na duniani kote tena kwa haraka zaidi. Matarajio ya wengi ni kuwa umma wa watanzania kuwa na uchungu wa lugha hii adhimu ya Kiswahili na kuwa mstari wa mbele katika kusimamia na kuthibiti uenezi wa Kiswahili sahihi na fasaha. lakini hali haiku hivyo, bali iko kinyume na matarajio
TAATHIRA ZA UMMA WA WATANZANIA KUTANYA MAKOSA KATIKA KISWAHILI SANIFU
Kuna taathira nyingi ambazo zinasababisha mawasiliano ya umma wa watanzania kuwa na matumizi yasiyosahihi kama yalivyoonekana hapo awali. Taathira za msingi hasa ni kama zifuatazo
TAATHIRAYA KUTOELEWA LUGHA YA KISWAHILI NA UTAMADUNI WAKE
Kiswahili ikiwa ni lugha kamili yaa mawasiliano ina kanuni zake za kisarufi na kiutamaduni. Kwa mfano kanuni za kisarufi katika kitenzi ambacho husimama kuwa sentensi basi lazima kiwe na kiambishi cha utendaji, kiambishi cha wakati na shina la kitendo chenyewe. Yaani kama kitenzi atakuja. Kwa upande wa utamaduni mbele ya wenyewe waswahili mtu hawezi kusema au kuandika kwa mfano:- Kama nilivyosema hapo mbeleni. kwani nene mbeleni ni matusi kwa mswahili mzawa.
Kinachoonekana kwa watanzania ni kutokuwa waledi na mahiri wa sarufi na utamaduni wa lugha ya Kiswahili. Kwa watu waliowageni wa lugha hii ya Kiswahili hususani katika sarufi ya Kiswahili wanafanya makosa makubwa na kuleta matatizo makubwa. Kwakuwa katika mawasiliano, kwao kufanya makosa sio tatizo ikiwa mazungumzo au maandishi yao yanaeleweka. Mhina anasema Kiswahili ni lugha ya watu wa unguja kwa hiyo tunapata Kiswahili safikutoka kwa watu wa jamii ya waunguja.
TAATHIRA YA KUKIDHARAU KISWAHILI KUWA HAKINA MWENYEWE
Taathira nyingine inayopelekea Kiswahili kuzungumzwana kuandikwa kimakosa na vyombo vya habari ambayo inasikitisha zaidi ni kuwa kila mmoja ana uhuru wa kuzungumza kukizungumza na kukiandika anavyoona au atakavyo. Hali hii ndiyo inayofanya wengine kusema kuwa Kiswahili hakina mwenyewe. hii ni dharau kubwa na kejeli ya hali ya juu kwa wazawa na wajuzi wa lugha hususani kwa wanazuoni.
Hii inadhihilisha ule usemi usemao anayekutukana hakuchagulii tusi, umechukua mkondo wake. Kwani haijapata kusikika wa haitarajiwi kusikika kuwa Kingereza, Kiarabu, Kifaransa, Kihaya, Kisukuma, Kibena na Kihehe kuwa lugha hizi hazina mwenyewe. Kwa hakika lugha kama haina mwenyewe basi haipo. Ikiwa lugha ya mazungumzo au maandishi lazima lugha hiyo iwe na wenyewe ambao ni binadamu tu. Wala si lugha ya wanyama, wala si lugha ya miti wala si lugha ya majabali na wala si lugha ya anga ombwe. Hivyo ni muhimu kuunga mkono mawazo ya  Mnyapala na Shiragddin wanaposema “… kiswahi kama zilivyo lugha nyingine hakina budi kukua na …”  mawazo haya ni ya kweli kwa yameandikwa na na wageni wa lugha nautamaduni wa Kiswahili ndio walioanza na matumizi ya yasiyo sahihi na yasiyofasaha. kinachobainika katika maandishi hayo ni kuwa wao ni wataalamu zaidi kuliko wale waswahili wenyewe katika kuandika vitabu vyao. ukweli usiopingika kuwa mawazo ya mazungumzo au maandishi yenye makosa yaliyotendeka na yanayoendelea kutendeka hayakubalikia na hayatakubalika kamwe na baadhi ya waswahili , kwani Kiswahili kina wenyewe. Amabao hawaoni kuwa lugha kama kifaransa au kiingereza ni bora au ni tajiri kuliko Kiswahili. Pia hawa hawaha wala hawatakuwa na dhana kuwa sarufi au lughawiya ya Kiswahili lazima ifuate lughawiya ya lughaya kiingereza au lugha nyingine. Msimamo huu pia unaoneshwa tena na Mnyapala na Shiraghdin  “kulazimisha lugha ya Kiswahili katika sarufi ya kiingereza ni kama kupika mchanyato wa ndizi mbivu… matokeo yake utakuwa si mchanyato bali ni bokoboko la ndizi. Kwa sababu sarufi ya kizungu ni kitu mbali na sarufi  ambayo isingefaa katika Kiswahili kwa namana nyingine.”
TAATHIRA YA WIGO NA KUTOJIAMINI KWA BAADHI YA WANAHABARI
Baadhi ya wanahabari hususani watangazaji wa redio runinga waandishi na wahariri wana mtindo wa kuiga kwa kutojiamini. hali hii hujitokeza pale wanahabari wanapowaiga ama wanahabari wenzao ambao nao wanafanya makosa katika kazi zao. Wanahabari hao huwaiga wanasiasa au viongozi wa nchi japokuwa kile kilichosemwa au kuandikwa ni makosa kabisa hapo ndipo utakapowasikia wakisema:- Chakachua  kusimikwa kwa watu kumi na watano, katoto kale kanaingia sasa. nk. Wanahabari hutumia maneno hayo kwa kuiga bila kujiani. ikitokea nafasi ya kuuliza mbona unatumia maneno hayo? utasikia jawabu atakalo kupa kuwa “mbona watu wengi wanalitumia neon hilo na limekwishaenea. Hoja ya msingi hapa si suala la neon kutumiwa na watu wengi au kuenea, bali ni kuwa neno hilo matumizi yasiyokuwa sahihi na halikubaki katika jamii ya wanazuoni wa Kiswahili.
TAATHIRA YA LUGHA ZA VIJANA KUKIINGILIA KISWAHILI SANIFU
Kiswahili mara nyingine hupata Taathira ya lugha za vijana na baadhi ya watu kuanza kuhusudu na kuyatumia maneno ambayo hayana asili ya Kiswahili na utamaduni wake. mfano Kama neno mambo? kwa maana ya uhali gain? na jawabu lake ni poa yaani sijambo au haliyangu ni njema. Pia kuna neno jingine linalouliza Vipi? na jawabu lake ni Fresho au hamna noma. lakini kuna maneno mengine kama vile Matingo, kughairisha, magharibi na kujiongeza. Kwa hakika lugha hizi si sahihi wala si fasaha kwa kutumiwa na watu wote katika shughuli zilizo rasmi. Lakini la kushangaza ni kuwa utawasikia baadhi ya viongozi wanahabari, wazee na walimu ambao tunawategemea wawemstari wa mbele kukilinda na kukienzi Kiswahili wanatumia lugha hizi zinazotumiwa na vijana. Lakini ilivyo lugha hizi kwa vijana zina sehemu zake maalumu kwa vijana wenyewe tu si kwa watu wenye kustahiwa kama hao waliotajwa hapo juu.
TAATHIRA YA KUCHANGANYA KISWAHILI NA KIINGEREZA (ATHARI ZA UMAGHARIBI, WINGI LUGHA)
Kuchanganya mazungumzo ya lugha ya Kiswahili na lugha ya kiingereza ni suala lililotawala mno katika mawasiliano ya umma na katika vyombo vya habari. Mara nyingi utawasikia watu wakichanganya Kiswahili na kiingereza. Hii ni kutaka kuhakikisha kuwa wanakifahamu kiingereza na kujitukuza mbele yaw engine. Mfano:-
            Ok ndugu wasikilizaji sasa tunaendelea na mchezo wa drama.
well nimekusikia ndugu mtazamaji kwa mchango wako lakini kwa upande mwingine perhaps watu wana mtazamo mwingine juu ya issue hiyo.
Uchanganyaji wa Kiswahili na kiingereza kama huo umewatawala watu wengi wakati wanapozungumza Kiswahili na kukichanganya na lugha hii ya kigeni. wakiti mwingine baadhi ya watu hufikia hatua ya kusema sijui nitumie neno gain hapa la Kiswahili ili ajihalalishie kuchanganya Kiswahili na kiingereza.
TAATHIRA YA KUTOLINGANA KWA TAALUMA YA FONOLOJIA NA OTHOGRAFIA
Mara nyingi wasomi wa lughawia za kiingereza wanatengua baadhi ya matamshi na maandishi ya Kiswahili kwa kuathiliwa na lugha ya iingereza ambacho nacho kimeathiliwa na taaluma ya kifaransa. hali hii husababisha matamshi ya sikuwa sahihi na yasiyokuwa fasaha katika Kiswahili ambacho kina utaratibu wa lugha za kiafrika kuandikwa kama kinavyotamkwa. mfano maneno kama;- themanini, tofauti, arobaini na dhoruba. Maneno kama haya hutamkwa vingine na kuandikwa vingine. ukihoji utajibiwa kuwa ndivyo yalivyokubalika kuandikwa kisanifu na pia baadhi ya maneno huandikwa kinyume na yanavyotamkwa yaani hapa ni kuiga kiingereza lakini hakuna  hoja kwani tukiyaandika kama yanavyotamkwa kama maneno mengine kuna ukakasi gain? Na wenyewe waswahili ndivyo wanavyotamka? Kwa hoja hizi ni wazi kuwa kuna matumizi yasiyosahihi ya matamshi ya maneno haya. La kusikitisha zaidi katika makosa hayo yamoo katika maandishi yote yaliyomo vitabuni, magazetini na katika majarida. Kwa ujumla sababu hizo kama zilivyofafanuliwa hapo katika matumizi yasiyo sahihi ya Kiswahili sanifu. Sababu hizi ni kama sababu zilizofafanuliwa na Pamela Ligami na wenzake wakisema “ kuna sababu mbalimbali zinazochangia matatizo katika lugha ya Kiswahili. Miongoni mwao na athari za lugha ya kwanza: makosa ya kimatamshi, mazingira, sarufi, matatizo ya kijamii na namna ya ufundishaji”
TAATHIRA YA KUDHARAULIWA KWA LUGHA YA KISWAHILI
Taathira nyingine ya msingi ni iayopelekea lughaya Kiswahili kudharauliwa na ama wageni au hata wale wenyeji hasa vijana ambao hawana uchungu wa asili wa lugha yao na utamaduni wao na vilivyo vyao. Hali hii huwasononesha wataalamu wengi hususani wenye uchungu na lugha hii na wakereketwa wa Kiswahili na ambao wanaithamini lugha yao na kujivunia katika Afrika mashariki. Wakereketwa au watu wenye uchungu na lugha yao wanapoona au kusikia matumizi yasiyokuwa sahihi ya lugha yao tukufu huwa na majonzi na masikitiko na ndipo baadhi yao huchukua hatua ya kukemea ama kwa kusema au kwa kuandika kama inavyokemea kimaandishi makala hii
MAKOSA MBALIMBALI YANAYOJITOKEZA KATIKA LUGHA
Kutokana na taadhira hizi kuna aina mbalibali za makosa yanayojitokeza kwa watumiaji wa lugha. Makosa hayo yamegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni makosa ya Kisarufi na makosa ya kimantiki. Katika kipengele hiki tutaangalia makosa hayo na namna ya kurekebisha.
MAKOSA YA KISARUFI
Kila lugha ina kanuni na taratibu ambazo hutawala katika matumizi ya lugha ili watu waweze kuelewana kanuni hizo zipo vunjwa au kukiukwa huweza kusababisha makosa kujitokeza na upotovu katika lugha. Makosa ya kisarufi yanaweza kugawanyika katika sehemu zifuatazo:- makosa ya kimsamiati, makosa ya kimuundo, makosa ya matamshi, kuongeza vitamkwa au viambishi, kuacha maneno, makosa ya tafsiri sisi.
MAKOSA YA KIMSAMIATI
Watumiaji wa lugha huchanganya masamiati wakati wa kuzungumza au kuandika. Watu hutumia msamiati usiolingana na msamiati usiolinga na maana iliyokusudia
Mfano:- Nona na nenepa
Wengi husema siku hizi umenona sana.
Badala ya kusema, Siku hizi umenenepa sana.
mazingira na mazingara
Watu husema Mazingara yameharibiwa sana siku hizi.
badala ya kusema Mazingira yameharibiwa sana siku hizi.
Ajali na ajili
Watu husema Amefariki wa ajili ya gari.
badala ya kusema Amefariki kwa ajali ya gari.
Wakilisha na wasilisha
Watu husema, Waziri wa fedha atawakilisha bajeti ya mwaka kesho.
Badala ya kusema Waziri wa fedha atawasilisha bajeti ya mwaka kesho.
MAKOSA YA KIMUUNDO
Kwa kawaida sentensi za kiswahili huanza na nomino ya mtenda au mtendwa.
Mfano:- mtoto mpole anacheza
Mzungumzaji asiye fuata kanuni husema Mpole mtoto anacheza.
Kalamu yangu imeibwa.
badala ya kusema kalamu yangu imeibiwa.
MAKOSA YA KIMATAMSHI
Watu wengi hushindwa kutamka baadhi ya sauti za kiswahili wakati mwingine huchanganya na kubadili sauti hizo Mfano Wakurya hutumia ’r’ badala ya ’l’
Nenda karare
badala ya kusema nenda kalale
Wandali hutumia ’s’ badala ya ’z’ na ’dh’ na ’th’
mfano selasini
badala ya thelathini
Sahabu
badala ya dhahabu
Samani
Badala ya zamani
Makosa haya mara nyingi yanatokana na athari ya lugha mama. Kwa kuwa lugha ya kiswahili ni lugha ya pili kwa wazungumzaji wengi. Hivyo lugha ya kwanza huwa na athari kubwa kwa mzungumzaji wa wa lugha ya pili.
KOSA LA KUONGEZA VITAMKWA
Baadhi ya wazungumzaji huongeza vitamkwa mahari pasipo hitajika na hivyo kuharibu lugha.
Mfano. Nendaga
badala ya nenda
Mashule
badala ya shule
Huwaga anapenda fujo
badala ya huwa anapenda fujo
KOSA LA KUACHA MANENO
Watumia lugha huweza kuacha maneno katika sentensi na bado wakafikiri wanatoa ujumbe uleule uliokusudiwa.
mfano, Watu husema Juma ameondoka kazini akiwa na maana kuwa Juma ameondoka kwenda kazini lakini sahihi ni kuwa Ametoka kazini.
Alfredi amerudi kazini akiwa na maana kuwa Afredi ametoka kazini.
Kwa mzungumzaji anatoa maana ambayo ni kinyume kabisa na ile maana aliyo kusudia kusema. Ambapo anakusudia kuuliza kama Alfredi amekwenda tena kazini.
MAKOSA YA TAFSIRI SISISI
Tafsiri sisisi ni tafsiri ya neno kwa neno. Tafsiri hii inapofanywa huleta matatizo ya kisarufi katika lugha
mfano. Kimbizwa hospitali She runed to hospital
badala ya kusema amepelekwa hospitali
At the end of the day
Mwisho wa siku.
Badala ya kusema hatimaye.
MAKOSA YA KIMANTIKI
Mantiki ni utaratibu mzuri wa kufikiri. Makosa ya kimantiki ni yale yanayoonesha kukosekana kwa utaratibu wa fikra. Nimakosa yanatokana na upotovu wa mawazo ya mzungumzaji
Mfano watu wengi husikika wakiema hivi: Usimwage kuku kwenye mchele mwingi
Badala ya usimwage mchele kwenye kuku wengi
Nyumba imeingia nyoka  Badala ya kusema Nyoka ameingia ndani ya nyumba
Chai imeingia nzi Badala ya kusema Nzi ameingia kwenye chai.
MSWAHILI
Kutokana na mtazamo hiyo na dhana na maendeleo ya lugha ya kiswahili, inaonekana wazi kuwa ni vigumu kumpata mswahili ambaye ni mmiliki wa lugha hii ya kiswahili. Inaonesha dhahili kuwa mswahili anaweza kutazamwa kwa namna tofauti kama zifuatazo;-
i).  Mswahili anaweza kuwa ni mtu mahuruti yaani ni mtu chotara ambaye ni lazima awe ametokana mwingiliano wa pande mbili ambao ni wabantu na watu wanaonasibishwa na Waarabu
ii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu wa mjini aliyeacha dini, utamaduni, mila na desturi zake za asili na kukimbilia dini, utamaduni, mila na desturi kutoka mataifa mengine kutoka uarabuni na nchi za kimagharibi
iii). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye anazungumza vizuri lugha ya kiswahili kwa kufuata taratibu zote za kiisimu na utamaduni wa lugha ya kiswahili
iv). Mswahili anaweza kuwa ni mkazi wa ya Afrika Mashariki hususani paeneo ya Pwani ya Afrika Mashariki.
v). Mswahili anaweza kuwa ni mtu anayeishi katika maeneo ya kawaida ya mjini (uswahilini)
vi). Mswahili anaweza kuwa ni mtu ambaye ni mwafrika asili, anayepatikana katika nchi za Kenya na Tanzania
v). Mswahili ni mtu mwenye maumbile na ya kiafrika, ikimaanisha kuwa ni mtu wa miraba minne.
HITIMISHO
Kabla ya uhuru kulikuwa na juhudi za makusudi za waasisi wa Taifa letu kukuza na kukiendeleza kiswahili. Miaka hamsini baada ya uhuru kiswahili kimekuaa na kuenea kwa sehemu kubwa dunia. Pamoja na hayo kiswahili kimekumbwa na changamoto mbalimbali ambazo zimeweza kupotosha lugha hii. Upotoshwaji huo hufanywa na wazawa au watumiaji wa kiswahili na kukifanya kiswahili kionekane kuwa hakina maana wala thamani kwa watu wengine. Watanzania ambao ni watumiaji wakuu wa lugha yakiswahili wanatakiwa kuchukua juhudi za makusudi katika kukifanya kiswahili kiwe katika hadhi yake. Kimatamshi, kimuundo, na kimsamiati. Pia Serikali ichukue juhudi za makusudi za kukikuza na kukiendeleza kiswahili kwa kuwaelimisha na kuwatunza wataalamu wa lugha hii adhimu ya Tanzania. Wataalamu wawe na msimamo mmoja katika taaluma hii maana wakati mwingine huwachanganya watu wanaojifunza lugha hii. Lugha hii ya kiswahili ibaki katika misingi ya sarufi yake ya lugha za kibantu ambazo kwazo zimeunda kiswahili.
VITABU VYA REJEA
  1. Chiraghdin S. na Mnyapala M. (1977) Historia ya Kiswahili, Oxford University Press Nairobi
  2. Nkwera, F.M.V, (1978), Sarufi na Fasihi Sekondari na Vyuo, THP, Dar es salaam.
  3. Massamba na wenzake (1999) Sarufi Miundo ya Kiswahili  Sanifu(SAMIKISA), TUKI, Dar es  Salaam
  4. Khamis, A.A, 2003 Uchambuzi Halisi wa Matumizi ya Kiswahili Asilia, Zanzibar. SUZA Press
  5. Msokile M (1992) Historia na Matumizi ya KiswahiliEPD Kibaha
    TUMI ( ) Kiswahili Sekondari,
  1. Broomfield (1930) Sarufi ya Kiswahili, London, The sheldon press
  2. Habwe J. na Karanja P. (2004), Misingi ya Sarufi ya Kiswahili, Nairobi phonex Publishers LTD
  3. Mwansoko HJM na Tumbo. (1996) Matumizi ya kiswahili Bungeni, TUKI, Dar es salaam
  4. BAKITA, (2004), Makala ya siku ya Kiswahili Kiswahili na Utandawazi, Dar es salaamu
  5. TUKI, (2004), Kamusi ya Kiswahili Sanifu, Toleo la pili, Oxford university press, Nairobi

Print this item