Mikakati ya utekelezaji wa sera ya Kiswahili kwa kufundishia
Dkt. Z.S.M Mochiwa
TANGU kuanzishwa kwa shule na mitalaa ya kigeni nchini mwetu matumizi ya lugha ya kufundishia yalikuwa yanalingana na makusudi ya elimu yenyewe. Kwa sababu kubwa makusudi ya elimu ya kikoloni na/au ya kimisheni yalikuwa kujenga stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu. Kwa msingi huo, shule zilitazamiwa zitoe watekelezaji wa mambo ambayo yanapangwa na watu wengine.
WAHITIMU wa shule hizo hawakutizamiwa kuwa chimbuko la fikra mpya. Wahitimu waliofuzu walikuwa na stadi hai za kukumbuka na kuiga.
Tanzania ilipopata uhuru, Nyerere (1967) alifanya tathmini ya kina ya elimu nchini. Dhima ya elimu, kwa mujibu wa Nyerere, ni kumuwezesha mpokeaji ajitambue na ajijengee stadi za akili na mwili za kumfanya ajitegemee, atanzue tata na awe na fikra angavu. Mhitimu wa elimu hii ni mweledi wa vipawa vyake na pia hujiamini. Elimu hii humpa ujasiri wa utangulizi badala ya kuwa mlunguzi. Msisitizo wa elimu hii umo katika kumpa changamoto mpokeaji kiakili na kimwili ili amudu kujisawiri na kuyasawiri mazingira yake.
Mtalaa unaokidhi malengo ya elimu ya namna hii ni ule unaoibukia ndani ya utamaduni wa mpokeaji na ambao unazingatia mahitaji yake katika viwango vyote.
Kasoro kubwa iliyojitokeza, na tukabaki nayo hadi leo, ni kwamba falsafa iliyomo katika elimu ya kujitegemea haikutoa msimamo kuhusu matumizi ya lugha madarasani.
Badiliko lililotokea baada ya kutangazwa kwa falsafa hiyo ni matumizi ya Kiswahili kwa kufundishia elimu ya msingi tu. Badiliko hilo lilileta athari maradufu. Mosi, limeifanya elimu ya msingi ‘kupungua thamani’ machoni mwa Watanzania. Elimu hiyo ilionekana kuwa ya kienyeji kwa kuwa inafundishwa kwa lugha ya ‘kienyeji’: Kiswahili. Ni elimu ya kila Mtanzania aliye, na asiye na akili. Kwa mtazamo huo, ilihisika kuwa elimu ya kweli kweli haifafanuki kwa lugha ya kienyeji. Aidha, moja ya sababu zilizoifanya Tanzania isibadili lugha ya kufundishia elimu ya sekondari na vyuo ni kuamini kuwa Kiswahili hakiwezi kufafanua mambo makubwa ya kisayansi.
Athari ya pili ya badiliko la lugha ya kufundishia elimu ya msingi tu ni kukatika kwa mfululizo wa usawiri wa mpokeaji. Kwa maneno mengine, matumizi ya lugha mbili za kufundishia: Kiswahili katika shule ya msingi na Kiingereza katika sekondari na vyuo vya juu, kunasababisha mgawanyiko wa mtalaa kiakili au kisaikolojia.
Mwanafunzi wa shule ya msingi anayebahatika kuliona darasa la kidato cha kwanza hujigundua kuwa mbumbumbu kutokana na kushindwa kuelewa Kiingereza. Dhana alizozizoea hazionekani kwa kuwa zimemezwa na lugha mpya ya kufundishia. Kwa msingi huo, kuingia kidato cha kwanza si kuendeleza uzoevu uliopatikana katika elimu ya msingi bali ni kuanza mtalaa mpya na kusahau wa zamani.
Katika umri wake wote, Jamhuri ya Tanzania iliendelea kufumbia macho kasoro hii kwa kukosa ujasiri wa kuikabili uso kwa macho. Badala yake, Jamhuri ikaendelea kuliundia tume suala hili na wakati mwingine kuviagiza vyombo vya ukuzaji wa lugha ‘kukiandaa’ Kiswahili ili kimudu majukumu mapya.
Katika hatua ya kushangaza zaidi, Jamhuri imepata kuwaalika wananchi wote katika mjadala wa kufaa/kutofaa kwa Kiswahili na/au kuweza/kutoweza kwake jukumu la kufundishia.
Mtaalam anayefuatilia mwenendo wa sera ya lugha nchini Tanzania atagundua dosari kadhaa. Dosari ya kwanza ni uelewa tofauti wa suala linaloikabili nchi. Ni kwa kiasi gani wale waliopata kulichangia wanajua nafsi ya suala lenyewe? Je wanajua kinachowalema wanafunzi ndani ya Kiingereza cha kufundishia? Wanaohoji uwezo wa Kiswahili wa kukidhia haja ya elimu ya juu wanajua lugha ni nini? Laiti wangejua wangethubutu kuuliza swali hili? Aidha, maelekezo ya kuandaa Kiswahili kwa majukumu mapya hayatokani na ujuzi wa dhati ya lugha. Ni kwa vipi lugha ya Kiswahili ikuzwe na kikundi cha watu nje ya matumizi? Aidha, maelekezo haya yanaifanya lugha katika jamii kuwa gwanda ambalo, mara baada ya kushonwa na fundi maalumu, linamtosha kila mwanajamii. Hii ni miongoni mwa fikra ambazo tumedumu nazo hadi sasa.
Makusudi ya makala hii ni kuonesha, hatua kwa hatua, utekelezaji wa sera ya kuleta maendeleo ya elimu nchini Tanzania. Katika azma hiyo, makala itatoa kwa muhtasari lugha zilizopo nchini na manufaa yake, baada ya kufafanua suala lililopo. Baada ya hapo, makala itafafanua uhusiano utakaokuwepo baina ya lugha zilizopo pindi sera itakapoanza kutekelezwa. Makala itajadili maandalizi muhimu yatakayoandamana na utekelezaji huo. Tuanze na suala lenyewe.
Suala la msingi
Mfumo wa elimu nchini Tanzania huanza na Kiswahili katika kufundishia shule za msingi. Wakati wanafunzi wanajiunga na shule hizo wanalazimishwa kuacha lugha za mama zao. Kutokana na lazima ya shule, wanafunzi hao hujifunza Kiswahili hadi ya kukimiliki (ang. Mochiwa 1999). Kwa kuwa lugha za mama zao zilizo nyingi ni za Kibantu, changamoto ya kubadili lugha hubebeka bila ya maumivu na bila ya uwezekano wa mwanafunzi kushindwa.
Anapoingia katika shule ya sekondari, mwanafunzi hulazimika tena kubadili lugha ya kufunziwa. Safari hii, lugha hiyo haina nasaba yoyote na lugha ya mama zao wala Kiswahili. Nasaba inayokusudiwa hapa ni ile inayoziunganisha lugha kisarufi na si nasaba ya kimsamiati. Kikwazo kilicho mbele ya mwanafunzi na ambacho kitaukilia mafanikio yake endapo atakishinda ni sarufi ya lugha ya Kiingereza.
Kwa muda wote huu wa mdahalo wachangiaji wanaounga mkono kuendelea kwa matumizi ya Kiingereza katika kufundishia, wameshikilia kidinindi kuwa Kiswahili hakina msamiati wa kutosheleza mahitaji ya elimu ya juu. Tatizo hili – na ni lazima sote tukiri kuwa liko – linaweza kupungua uzito endapo kihalisi cha nafsi ya lugha kitakuwa sehemu ya uzoevu wa Watanzania. Kihalisi chenyewe ni kwamba lugha ni sarufi. Wanaoshindwa kumiliki Kiingereza wanashindwa kumiliki sarufi yake. Kwa mantiki hiyo, badiliko la lugha ya kufundishia shule za sekondari na elimu ya juu linatokana na kukiri kuwa wanafunzi wanashindwa kuimudu sarufi ya Kiingereza. Aidha, tunapoliangalia tatizo hili kwa mwanga huo, itakuwa vyepesi kuona kuwa msamiati wa lugha yoyote huweza kuingizwa katika lugha yoyote. Kw msingi huo, kama ilivyokuwa katika Kiingereza, Kiswahili kitavuna msamiati ndani ya matumizi yake. Laiti nafsi ya lugha ingalikuwa ni msamiati wake, Kiingereza kisingepata sifa ya kuwa kubwa duniani kwa sababu asilimia ya msamiati wake asilia ni ndogo kuliko ile ya mkopo.
Kutokana na kutoelewa nafsi ya tatizo hili la elimu, baadhi ya wanaounga mkono kuendelea kwa Kiingereza kwa kufundishia, wanaelewa kuwa pendekezo la badiliko ni la kuking’oa Kiingereza hapa nchini. Watu hao wanafikiri kuwa Kiswahili kinapoingia sekondari, Kiingereza hakitakuwa na nafasi kabisa. Kutoelewa huko kumelifanya badiliko linalokusudiwa kuleta kitisho kwa kila mtu anayejua nafasi ya Kiingereza katika zama hizi. Kiswahili kina vitabu vya rejea? Kwa kuwa jibu la swali hili si “ndiyo”, ndipo wakapendekeza vitafsiriwe vitabu vya kiada na vya ziada. Kwa ufupi, wataalam wanapendekeza ijengwe maktaba ya Kiswahili kwanza kabla ya kuliingiza badiliko hilo la lugha ya kufundishia.
Mara inapochukuliwa kuwa kweli kwamba hatua muhimu za utekelezaji wa sera hii ni ujenzi wa maktaba ya Kiswahili, kila mtu huona kuwa badiliko hilo haliwezekani. Aidha, itaonekana dhahiri kuwa badiliko hilo litasababisha maafa makubwa kielimu na kiuchumi. Sasa tujipe fursa ya kuabiri lugha zilizopo kabla ya kuratili badiliko linalofikiriwa.
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) ni idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania. Taasisi hii ni miongoni mwa taasisi kongwe za lugha nchini Tanzania. Madhumuni yake yakiwa ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya lugha ya Kiswahili. Hadi mnamo mwaka 2009 taasisi hii ilijulikana zaidi kwa jina la TUKI au “Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili“
Historia yake
Ilianzishwa mnamo mwaka 1930 kama Inter-territorial Language (Swahili) committee ya Nchi za Afrika ya Mashariki, baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1964 kamati ilifanywa kuwa Sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaamu. Baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Lugha ya Kiswahili. Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuunda Taasisi kubwa zaidi inayoitwa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili – TATAKI
Majukumu
Mwanzoni, Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ni taasisi ya utafiti ilipewa jukumu la kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni, na kuchapisha matokeo ya utafiti huo. Hivyo pamoja na BAKITA (Baraza la Kiswahili Tanzania) TUKI ndiye mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili katika Shahada za Awali, Mahiri na Uzamivu.
Kazi yake
Kutafiti na kuchapisha matokeo ya utafiti katika nyanja mbalimbali za Lugha, Isimu na Fasihi ya Kiswahili, TATAKI inasimamia Tafsiri na Ukalimani. Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa Kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili. Kati ya kamusi hizi ni
TUKI imehariri toleo la Kiswahili la “Historia Kuu ya Afrika” iliyotungwa na kamati ya wataalamu ya UNESCO.
Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ( TATAKI) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni asasi kongwe inayojishughulisha na ufundishaji, utafiti na utoajiushauri wa kitaaluma katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili. TATAKI inadhamana ya kufundisha na kutafiti vipengele vyote vya lugha, kwa kuzigatia vipaumbele vya Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
HISTORIA YA TATAKI
TATAKI ni Taasisi yenye historia ndefu kuliko Taasisi zote zinazohusika na ukuzaji na uendelezaji wa lugha ya Kiswahili duniani. Historia ya TATAKI inaanzia mwaka 1930 ilipoanzishwa kamati ya lugha (ya Kiswahili) ya Afrika Mashariki. Mnamo mwaka 1961 Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilianzishwa kama Chuo Kikuu Kishiriki cha London.
Kuanzia mwaka 1962, viongozi wa kamati waliaza kufikiria kuhamisha shughuli za kamati kwenye Chuo Kikuu kimojawapo. Vyuo vilivyofikiriwa ni Makerere na Dar es Salaam. Mwaka 1963 shughuli za kamati zilihamishiwa katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam na hatimye kamati ilibadili jina na kuwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Majukumu ya Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili hayakutofautiana na yale ya kamati ya lugha.
Mwaka 1970 baada ya kuanzishwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ndipo Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ikaanzishwa chini ya ibara ya 22(3) ya sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika kipindi hiki ilianzishwa pia idara ya Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam iliyokuwa chini ya Kitivo cha Sanaa na Sayansi za Jamii. Miongoni mwa majukumu ya idara ilikuwa ni kufundisha lugha ya Kiswahili kwa wanafunzi kutoka ndani na nje ya Tanzania. Kuanzia mwanzoni mwa miaka 2000, Chuo Kikuu kilianza kupitia upya muundo wake ili kufanyakazi kwa ufanisi na weledi. Katika mchakato huo yalitolewa mapendekezo mbalimbali ilikiwa ni pamoja na kuunganisha vitengo ambavyo majukumu yake yalionekana kufanana. Kwa kuwa malengo ya idara ya Kiswahili na TUKI yalilenga kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili, mnamo mwaka 2009 iliyokuwa idara ya Kiswahili ikaungana na TUKI na kuunda Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI). Majukumu ya TATAKI sasa yamejikita katika utafiti wa Nyanja mbalimbali zihusuzo lugha na fasihi ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali.
TATAKI inaidara mbili ambazo ni idara ya lugha ya Kiswahili na isimu na idara ya fasihi, mawasiliano na uchapaji. Idara hizi kwa pamoja zinashirikiana katika ufundishaji wa programu mbalimbali taasisini kama inavyoainishwa hapa chini:
PROGRAMU ZINAZOFUNDISHWA NA TATAKI
1. B.A. Kiswahili
Ni shahada ya awali ambayo hutolewa katika muda wa miaka mitatu. Katika shahada hii, kozi mbalimbali za Isimu na Fasihi hutolewa. Masharti ya jumla ya udahili ya Chuo Kikuu huzingatiwa. Hata hivyo ili mwombaji adahiliwe katika programu ya B.A (kiswahili) anapaswa, pamoja na masomo mengine, awe amesoma somo la Kiswahili kidato cha tano na sita na kufaulu kwa wastani wa angalau alama D au awe na sifa zinazofanana na hizo.
2. M.A. Kiswahili
Hii ni shahada ua umahiri ambayo hutolewa kwa Tamrini na Tasnifu katika Isimu na Fasihi kwa muda wa miezi 18 (Tamrini na Tasnifu); na miezi 24 (kwa Tasnifu pekee). Ili kujiunga na programu hii mbali na sifa za jumla za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, mwombaji anapaswa kuwa amefaulu masomo ya Kiswahili katika shahada za awali kwa WAKIA (GPA) isiyopungua 3.0 kwa kozi za Kiswahili.
3.PhD. Kiswahili
Masomo katika programu hii hutolewa kwa namna mbili. PhD kwa Tamrini na Tasnifu.PhD kwa Tamrini hutolewa kwa muda wa miaka minne na PhD kwa Tasnifu hutolewa kwa muda wa miaka mitatu. Ilikudahiliwa katika programu hizi mwombaji anapaswa kuwa amesoma Kiswahili au masomo yanayoendana na umahiri. Lugha inayotumika kufundishia na kuandika ripoti ya utafiti kwa programu zote ni Kiswahili.
VITUO VYA TATAKI
Mbali na idara za ufundishaji, TATAKI pia hufanya kazi za kiutafiti kupitia vituo vya utafiti na ushauri.
KITUO CHA FASIHI YA KISWAHILI NA MAPOKEO YA SIMULIZI YA KIAFRIKA
Miongoni mwa majukumu ya kituo hiki ni kuratibu na kusimamia shughuli zote za utafiti katika nyanja mbalimbali; kuandaa na kuchapisha Makala na vitabu vyo kufundishia kozi za fasihi, mawasiliano na uchapishaji kwa Kiswahili; kutafiti kuhusu kazi za wanafasihi mbalimbali wa zamani na sasa; kukusanya na kuhifadhi data, nyaraka na taarifu muhimuza kifasihi.
KITUO CHA ISTILAHI, TAFSIRI, UKALIMANI NA TEKNOLOJIA YA LUGHA
Jukumu kuu la kituo hiki ni kutoa huduma zinazohusu masuala ya istilahi, tafsiri, ukalimani na teknolojia ya lugha. Kwa kiasi kikubwa kituo hiki hujihusisha na shughuli za tafsiri ya nyaraka mbalimbali kutoka katika asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali.
KITUO CHA KISWAHILI KWA WAGENI
Kituo hiki kinahusika na kuratibu shughuli zote za ufundishaji wa Kiswahili kwa wageni. Wageni hufundishwa kwa vikundi au mtu mojamoja. Kituo pia kina mpango wa kujiimarisha na kuwa kituo cha weledi wa Kiswahili Ulimwenguni.
KITUO CHA KAMUSI NA SARUFI YA KISWAHILI
Hujishughuliasha na kufanya utafiti wa msamiati mpya unaotumika katika jamii na kuukusanya kwa ajili ya kuboresha kamusi na vitabu vingine vya sarufi ya Kiswahili. Hivi sasa kituo kimeshatoa kamusi ya Kiingereza-Kiswahili na Kiswahili-Kiingereza kwa njia ya nakala ngumu na kwa njia ya simu ya kiganjani. Aidha kituo kwa kushirikiana na shirika la uchapishaji la OXFORD tawi la Nairobi wametoa matoleo kadhaa ya Kamusi ya Kiswahili Sanifu.
UDAHILI WA WANAFUNZI
Wanafunzi wenye lengo la kusoma programu zinazotolewa na TATAKI hudahiliwa kwa kuzingatia taratibu zote za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
TAARIFA NYINGINE
TATAKI pamoja na kujishughulisha na ufundishaji, utafiti na utoaji ushauri, hujishughulisha pia na shughuli za uchpaji na uchapishaji. Uchapishaji hulenga kazi zilizoandikwa kwa lugha ya Kiswahili na uchapaji hufanywa kwa kazi zote bila kujali zimeandikwa kwa lugha gani ilimradi kazi hizo zizingatiye maadili ya uchapaji wa kitaaluma kama ilivyoinishwa katika Sera ya Uchapaji na Uchapishaji wa TATAKI.
Aidha, TATAKI hutoa huduma ya ushauri wa kitaalamu kwa watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi wa shule za sekondari na vyuo vya ualimu wanaokuja kufanyakazi mradi kwa lengo la kikamilisha matakwa ya kitaaluma katika masomo yao.
IKIWA idara ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.
Japo Kiswahili kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika Mashariki na Kati.
TUKI, kwa sasa TATAKI, ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language (Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.
Mnamo 1964, kamati ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.
Majukumu ya taasisi hii awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.
Hivyo pamoja na Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.
Inafundisha Kiswahili kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.
BAKITA
Ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BAKITA imekuwa na mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake.
Miongoni mwa majukumu ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.
Huhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.
TAKILUKI
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.
Inajishughulisha na kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.
TAKILUKI inatoa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.
CHAUKIDU
Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani.
Madhumuni yake ni kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari, uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.
Husambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.
Vilevile inashauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.
CHAWAKAMA
Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza kujiunga nacho.
Mara kwa mara, CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili, kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na
nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.
CHAKAMA
Chama cha Kiswahili Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini Bayreuth, Ujerumani. Kwa pamoja na Chama cha Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.
Aidha, huhifadhi kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.
Chama huandaa makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo mbalimbali katika nchi husika.
Katika makongamano hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.
Huko Mombasa, viongozi wa wenyeji – Waswahili – walishiriki katika uendeshaji wa siasa wa mji huo. Familia ya Mazrui toka Oman iliendelea kuwa huru kutoka kwa watawala wa Kioman wa Zanzibar kwa sababu ya ushirikiano wao wa karibu na masheikh wenyeji wa Kiswahili ambao walichangia nao utawala. Hata kwa kipindi fulani, baada ya utawala wa Wamazrui kupinduliwa, viongozi wa Kiswahili waliendelea kuwa mashuhuri katika uendeshaji wa mji.
Watawala wa kienyeji wa Zanzibar walianza kupoteza mamlaka yao kisiasa kadiri Waomani walivyozidi kuimarika katika funguvisiwa hili. Wakati huohuo, wenyeji wa Zanzibar walipokonywa ardhi na walowezi wa Kiomani ambao waliyanyemelea hasa maeneo yenye rutuba kaskazini na mashariki mwa kisiwa.
Pamoja na kuwepo kikosi cha kulinda ngome cha Waomani kwenye kisiwa cha Kilwa, Sultani mwenyeji alibakishiwa cheochake na sehemu ya moja ya tano ya ushuru, na alikuwa na mamlaka yake kiutawala kwenye pwani ng’ambo ya Kilwa Kisiwani. Upotevu wa mamlaka yake haukusababishwa tu na kuwepo kwa Waomani, bali pia kudhoofika kiuchumi kwa Kilwa Kisiwani yenyewe, kulikosababishwa na kuinuka kwa mji pinzani wa Kilwa Kivinje huko bara, ambao ulifanikiwa kuelekeza biashara ya watumwa na meno ya ndovu kutoka kisiwani kwenda depo ya bara.
Ilipofika mwaka 1800, Malindi, mji mwingine miongoni mwa miji ya pwani, ulikuwa umefifia sana kutokana na familia yake ya kiutawala kuhamia Mombasa kwenye karne ya 16.
Kaskazini mwa Malindi vilikuwepo visiwa vya Lamu na Pate. Ilipofikia 1800, Pate ilikuwa imeshaporomoka kutoka kwenye nafasi ya umashuhuri wa kibiashara iliyokuwa nayo katika karne ya 17 na ya 18 kutokana na migogoro ya urithi na mapambano na kisiwa jirani cha Lamu. Ushindani kati ya visiwa hivyo viwili baadaye ulirahisisha kuingiliwa na kutawaliwa kwao na Zanzibar.
Barani, mkabala na visiwa vya Lamu na Pate, waliishi Wabajuni ambao walienea pia kwenye mlolongo wa visiwa vidogovidogo vya pwani ya Somalia.
Utengano wa ndani ya nchi yake ulimwezesha Seyyid Said kupanua uchumi wake pasi na vikwazo. Aliona kuwepo kwa mifarakano na udhaifu kwenye pwani ya Afrika Mashariki kuwa fursa nzuri kwa upanuzi wa kiuchumi na wa kisiasa. Aidha aliona haja ya kupambana na tamaa ya nchi za Ulaya kwa kukita mikakati yake mwenyewe.
Alianza kufanya mawasiliano na wenyeji na watawala kwa kushauriana na kufanya mikataba nao, na kujihusisha kwenye ushindani wa wao kwa wao.
Ulipokifia mwaka 1823, alikuwa amekwisha kufaulu kuwa na mashiko katika visiwa vya Pate na Lamu, na jumuiya chache za jirani. Wapinzani wake wakuu walikuwa ni Wamazrui – nasaba ya kifalme iliyotawala Mombasa, pia wakiwa na chimbuko la Oman – ambao waliishawishi Uingereza kuweka Mombasa chini ya ulinzi wao mwaka 1824.
Hatua hii iliharibu kwa kiasi fulani mahusiano kati ya Sultan Said na Uingereza. Hata hivyo ulinzi huo wa Waingereza haukudumu muda mrefu kwa sababu Waingereza walionyesha kumpendelea Said, na Wamazrui hawakuwa na raghba tena juu ya ulindwaji huo kwa vile uliwalazimisha kugawana ushuru wao na Waingereza ambao walikuwa wameshindwa kuwasaidia (Wamazrui) kurejesha maeneo yao yaliyotekwa.
Uhusiano wa kibiashara wa Pwani/Bara
Muda mfupi baada ya Said kupata udhibiti wa Mombasa aliamua kuhamisha makao makuu ya usultani wake kwenda Zanzibar, mji ambao ulikuwa ukikua kwa haraka kama kituo cha kibiashara chenye shughuli nyingi. Said alivutiwa sio tu na suhula za kimeli za Zanzibar, bali pia na rutuba ya kisiwa na uwezekano wake wa kuzalisha mazao ya kilimo. Aliamua kuhodhi biashara yote ya kisiwa na akaendelea kukifanya kuwa kituo kikuu cha uchumi katika pwani ya Afrika Mashariki.
Nafasi ya Zanzibar iliimarika pia kutokana na kutambulika kwake kupitia mikataba ya kibiashara na mataifa ya nje kama vile Marekani, Uingereza na Ufaransa.
Meno ya ndovu na watumwa ndizo bidhaa zilizokuwa na faida kubwa zaidi kwa usultani wa Oman kwa sababu ya mahitajiyake makubwa ndani na nje ya nchi. Wayao, kikundi cha bara, walikuwa na mtandao wa biashara ya masafa marefuwaliotumia kuleta pwani meno ya ndovu na watumwa. Shughuli zao zilienea kuzunguka ziwa Nyasa, na bidhaa zao zilifika pwani ya Zanzibar kupitia Kilwa Kivinje. Kwa hakika kukua kwa umaarufu na ustawi wa Kilwa Kivinje kulitokana na kuongezeka kwa mashirikiano ya kibiashara kati ya watu wa pwani na bara katika karne ya 19.
Watumwa walipatikana kupitia mashambulizi na vita, ingawa si mapigano na mashambulizi yote yaliyotokea yalisababishwa na haja ya kuteka watumwa. Zaidi ya hayo, watu waliotiwa utumwani mara nyingi walitoka katika vikundi vya bara ambavyo vilikuwa vikifanya biashara ya watumwa kama vile Wayao, Wabisa, Wamakua na Wangindu.
Walikuwepo wafanyabiashara ya masafa marefu wengine kwenye eneo la kaskazini mwa ziwa Nyasa; waliokuwa mashuhuri zaidi ni Wanyamwezi, Wakamba na Wamijikenda. Hao walianzisha mahusiano na pwani kwa mara ya kwanza kunako takribani mwaka 1800, na baada ya muda mfupi wakaimarisha mitandao ya kibiashara kati ya eneo hilo la bara na pwani.
Kadiri bei za watumwa na meno ya ndovu zilivyozidi kupanda, baadhi ya wafanyabiashara wasio Waafrika walianza kuingia bara. Msafara wa kwanza ulioongozwa na wasio Waafrika kuelekea bara ulifika Unyamwezini mwaka 1824 na ilipofikia 1845, wafanyabiashara wengi wa pwani, hasa Waarabu, walikuwa wamekwisha penya ndani ya bara hadi kufikia Buganda.
Athari za kijamii na kiuchumi za biashara iliyokuwa inapanuka
Upanuzi wa biashara katika pwani na bara ya Afrika Mashariki ulikuwa na athari zake muhimu. Kwa mfano, upanuzi wa Wakamba nje ya makazi yao ya asili hadi kufikia kwenye maeneo ambayo hayakuwa na rutuba ya kutosha uliwafanya waanze uwindaji, ufugaji na biashara za kubadilishana mali kama njia ya kujikimu. Walifanya biashara na majirani zao kama vile Wakikuyu, Waembu na Wamasai, na hatimaye wakapanua mtandao wao wa biashara hadi pwani. Waliandaa misafara yao kwenda pwani na waliongoza katika biashara ya masafa marefu kwenye maeneo ya kaskazini ya bara ya Afrika Mashariki hadi miaka ya 1850, nafasi yao ilipochukuliwa na Waarabu na Waswahili.
Kutokana na mahusiano hayo ya kibiashara kati ya pwani na bara, mfumo wa kuishi katika makazi yenye ngome ya Wamiji kenda yaliyoitwa kaya ulianza kudhoofika. Watu walianza kuziacha kaya ili kwenda kufanya biashara. Mtawanyiko huu ulififisha umoja na mshikamano wa kaya, ukamomonyoa mamlaka ya wazee na kuua mfumo wa uongozi wa marika.
Athari nyingine ilikuwa desturi ya kuoa wake wa kigeni. Kuoana huku miongoni mwa vikundi tofautitofauti kulipelekea kuanzishwa kwa undugu miongoni mwa jamii zilizohusika. Maingiliano ya kiutamaduni kati ya Wabantu na Waarabu, na kati ya Wabantu na Waswahili yalitokana na kukua kwa matumizi ya watumwa wa nyumbani (wa kazi za ndani) kwenye mashamba na kuenea kwa usuria.
Katika usultani wa Oman desturi ya kuoa wake wa kigeni ilikuwa imeenea sana, hasa miongoni mwa tabaka la watawala. Maingiliano ya kiutamaduni kati ya Waarabu na wenyeji wao huko pwani yalikuwa makubwa kiasi kwamba kulikuwepo na tofauti bayana za kiutamaduni kati ya Waarabu wa Oman walioishi nyumbani (Uarabuni) na wenzao “walio-Afrikishwa” na kuishi katika miji ya Kiswahili.
Hali kadhalika kulikuwepo na mabadiliko kadhaa huko bara yaliyotokana na kushiriki kwa watu katika biashara ya pwani. Baadhi ya watawala wa bara walijenga upya miji yao mikubwa kwa mtindo wa pwani, wakipamba vitala vyao na bidhaa za pwani na hata kukuza hamu ya vyakula vya pwani.
Lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano mapana ya tabaka la wafanyabiashara pia ilienea sana huko bara. Mwanzo ilikuwa ikitumika kama lugha ya kibiashara, lakini muda ulivyozidi kusogea ndivyo na matumizi ya lugha yalivyoongezeka miongoni mwa wakazi wa bara.
Miongoni mwa matukio muhimu ya kijamii na kisiasa yaliyotokea miongoni mwa watu wa eneo la Maziwa Makubwa ni kuibuka kwa jumuiya kamili za kisiasa zenye utambulisho maalum kama ile ya Buganda. Buganda ilistawi kama dola unganifu yenye asasi sanifu za kisiasa. Lakini vikundi vya mashariki mwa ziwa Viktoria, isipokuwa ufalme wa Wawanga, havikuanzisha dola zozote unganifu.
Hata hivyo, si vikundi vyote vya bara viliathiriwa na utamaduni wa pwani. Wakikuyu, kwa mfano, hawakuonyesha raghba yoyote katika biashara ya pwani, hata wakati wa misafara ya Waarabu na Waswahili ilipoingia katika ardhi yao. Wamasaiwaliwazuia wafanyabiashara wa Kiarabu na Kiswahili kuingia katika ardhi yao.
Waasia hao walikuwa na busara nyingi katika kufanya biashara na walishika nafasi zilizo muhimu kabisa kama mawakala wa ushuru, walanguzi, mabepari na wakopeshaji fedha na wafanyabiashara ya jumla ya nchini Zanzibar. Ingawa kuwepo kwao na shughuli zao huko Zanzibar hazikuwapatia sauti yoyote katika siasa na uendeshaji wa shughuli za kiserikali, nafasi yao ya kiuchumi iliimarika sana. Baadhi yao walitajirika sana, kiasi kwamba hata baadhi ya Masultani wa Zanzibar waliwakopa fedha.
Kutokana na kuongezeka kwa umaarufu wa karafuu, Waarabu wa Kiomani kadhaa katika visiwa vya Zanzibar na Pembawalianza kulima karafuu katika mashamba makubwa. Jambo hili lilikuwa na matokeo mengi:
lilivunja ukiritimba wa Said katika biashara ya karafuu.
lilipelekea kwenye kufanya karafuu iwe tasnia ya kitaifa miongoni mwa Waarabu wa Oman.
liliongeza mahitaji ya nguvukazi ya watumwa, pia liliongeza biashara ya watumwa ya Afrika Mashariki.
lilifanya mazao mengine yapuuzwe kama vile nazi na mpunga.
ilileta matatizo ya ardhi kisiwani Zanzibar. Matatizo hayo ya ardhi hasa yaliharibu kwa kiasi fulani mahusiano kati ya Waarabu wa Oman na wakazi wa asili wa Zanzibar walioporwa ardhi yao na Waarabu.
Hata hivyo sera za kibiashara na za kiuchumi za Said sio tu ziliifanya Zanzibar kuwa kituo kikuu cha kibiashara kwenye pwani ya Afrika Mashariki, bali pia polepole ziliuingiza uchumi wa Afrika Mashariki kwenye mfumo wa kibepari wa (nchi za) Magharibi.
Taathira hasi ya hali hii ni kwamba wafanyabiashara kutoka Ulaya, Marekani na Asia walitajirika kwa kuwafukarisha wenyeji wa Afrika Mashariki, na hivyo kusababisha kudumaa kwa maendeleo yao. Rasilimali (watu na nyenzo) za Afrika Mashariki zilinyonywa kupitia ubadilishanaji usio na usawa uliokuwa ukifanywa kati ya wafanyabiashara wa kigeni na wenyeji.
Hitimisho
Kulikuwepo pia na ukuaji wa biashara ya masafa marefu ulioanzishwa na vikundi vya Waafrika huko bara. Baadaye, wafanyabiashara wa Kiarabu na wa Kiswahili walikwenda hadi bara kutafuta bidhaa zaidi. Biashara ya masafa marefu ilikuwa ikipanuka na kuwa na athari zake za kijamii, kiuchumi na kiutamaduni kwa vikundi vingi vya bara. Athari hizo zilijumuisha uenezi wa Uislamu na lugha ya Kiswahili.
Lakini baadhi ya matukio muhimu kama vile uvamizi wa Wanguni yalitokea bara pasi na kuhusiana na biashara ya masafa marefu.
Maendeleo ya ukuaji wa athari za kibiashara za Zanzibar yalipelekea kwenye ubadilishanaji (wa bidhaa) usio na usawa kati ya Afrika Mashariki na (nchi za) Magharibi. Aidha yaliuingiza uchumi wa Afrika Mashariki kwenye mfumo wa kipebari na hivyo kusababisha kudumaa kwa maendeleo ya eneo hili.
Marejeo
Bennett, N.R. (1981) A History of the Arab State of Zanzibar (London: Methuen)
Berger, I. (1981) Religion and Resistance in East African Kingdoms in the Precolonial Period (Tervuren: Musée royal de l’Afrique centrale)
Sutton, J. E. G. (1973). Early trade in Eastern Africa (Nairobi : East African Publishing House)
1. Kusaidia kuleta umoja wa bara zima.
2. Kudumisha utamaduni wa Kiafrika kuliko kufuata kasumba.
3. Kufanya Waafrika waamini zaidi mambo yao kuliko kutegemea tu ya kigeni.
4. Kurahisisha upatikanaji wa ajira kwa watumiaji wa lugha hiyo hata nje ya Afrika.
5. Kukuza sekta ya utalii.
Shughuli mbalimbali zinazowezesha Kukua na Kuenea kwa Kiswahili nchini
Baada ya uhuru kuna harakati mbalimbali zilizochukuliwa na serikali ya Tanzania katika kukiendeleza na kukikuza kiswahili. Harakati hizo ni pamoja na kupendekezwa kuwa lugha rasmi 1962. Mkwaka 1964 kiswahili kilipendekezwa kuwa lugha ya taifa na kuwa kitatumika katika shughuli zote za kiserikali na kitaifa mfano katika elimu hususani elimu ya msingi.
Kuundwa kwa Chombo cha usanifishaji ambacho kilikuwa na kazi ya kuhimiza maendeleo ya kiswahili, kutayarisha kamusi na vitabu mbalimbali vya sarufi na fasihi ya lugha ya kiswahili na kuandaa wataalamu watakaoshughulikia usanifishaji wa Kiswahili
Pia baada ya uhuru kulianzishwa Taasisi mbalimbali zitakazoshughulikia lugha ya kiswahili. Mfano:- BAKITA, TUKI, TUMI, UKUTA, UWAVITA, Idara ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaamu.
Baada ya uhuru nchini Tanzania kiswahili kilienea kwa kasi kubwa sana. Kuna sababu mbalimbali ambazo zilichangia kukua na kuenea kwa kiswahili hapa nchini. Baadhi ya sababu hizo ni pamoja na kuteuliwa kwa kiswahili kuwa lugha ya Taifa, Kiswahili kitumike katika Elimu, mfano kuwa lugha ya kufundishia katika shule za msingi. Kuundwa kwa vyombo mbalimbali vya kukuza na kuneza kiswahili, Kiswahili kuwa Lugha rasmi na lugha ya Taifa, shughuli mbalimbali za kidini, shughuli za kisiasa na kiutawala na shughuli za kiutamaduni na uchapishaji wa vitabu na majarida mbalimbali.
Kiswahili kuwa lugha ya taifa
Baada ya uhuru mwaka 1962 kamati iliundwa ili kuangalia uwezekano wa kutumia kiswahili katika shughuli zote rasmi, mfano bungeni na shughuli zote za kiofisi. Pia kiswahili kiliteuliwa kuwa lugha ya taifa 1964 ambapo katika shughuli zote za kitaifa zitaendeshwa kwa kutumia lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili kilihimizwa kutumika katika mawasiliano yote hasa katika shughuli za umma na Wizara zote, Serikali na Bunge, kiswahili kiliendelea kupanda hadhi zaidi wakati wa Azimio la Arusha la mwaka 1967 kwani azimio hilo lilitungwa na kuandikwa kwa lugha ya kiswahili.
Kuundwa kwa vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili
Tanzania baada ya uhuru ilifanya jitihada za kuunda vyombo mbalimbali vya kukuza na kueneza Kiswahili katika nyanja mbalimbali mfano wa vyombo hivyo ni UWAVITA BAKITA, TUKI, Taasisi ya Elimu,TAKILUKI na Chama cha Kiswahili Chuo Kikuu Dar es Salaam.
Kutumika katika elimu
Kiswahili licha ya kutumika katika shughuli mbalimbali za kiserikali, kilipendekezwa kutumika katika shule za Msingi na kufundishwa katika elimu ya sekondari kama somo na katika vyuo vikuu wanatoa shahada mbalimbali za lugha ya kiswahili. Pia katika Elimu ya watu wazima ambao hawakujua kusoma na kuandika. Watu hawa walijifunza masomo mbalimbali kwa lugha ya kiswahili na kuwafanya watu wengi kujua kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya kiswahili fasaha. Kampeni hii ilikuwa kwa nchi nzima ambapo walijifunza elimu ya Afya, Siasa, Kiswahili, Kilimo na ufundi kwa lugha ya Kiswahili na kuwafanya watu wengi kuzungumza kiswahili sanifu.
Vyombo vya habari
Tangu uhuru ulipopatikana kuna vyombo mbalimbali vya habari vilivyoanzishwa. Vyombo hivi hutumika kueneza kiswahili kwa kiasi kikubwa na hufikiwa na watu wengi licha ya kuwepo kwa changamoto za kiuchumi. Vyombo hivyo ni magazeti na majarida mbalimbali ambayo huandikwa kwa lugha ya kiswahili lakini kuna redio na runinga ambazo matangazo yake hutangazwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kukifanya kiswahili kuenea kote ndani na nje ya nchi.
Biashara
Shughuli za kibiashara nchini husaidia kuenea na kukua kwa kiswahili kutokana na kuwepo kwa makabila tofauti tofauti ambapo wafanyabiashara huweza kuunganishwa kwa lugha ya kiswahili. Hivyo kiswahili hudumishwa na kutumika katika biashara hizo.
Shughuli za siasa na utawala
Tangu wakati wa harakati za kupigania uhuru kiswahili kimetumika kama nyenzo muhimu kuwaunganisha wananchi. Shughuli za kisiasa zimetumia lugha hii katika kujiimarisha; mfano wakati wa chama kimoja, Azimio la Arusha na Mfumo wa vyama vingi Kiswahili kimetumika kama njia kuu ya mawasiliano. Pia katika utawala chama kinachotawala kimekuwa na harakati za kukiendeleza kiswahilli katika nyanja zote. Ambapo kiswahili kimekuwa kikitumika katika shughuli zote za kiutawala. Hivyo shughuli za kisiasa na kiutawala zimechangia kwa kiasi kikubwa katika kukuza, kukieneza na kukiendeleza kiswahili.
Uandishi na uchapishaji wa vitabu
Kuibuka kwa waandishi wa vitabu mbalimbali vya kiswahili vya sarufi na fasihi ambavyo vilichambua kwa kina mambo mabalimbali yahusuyo lugha ya kiswahili na utamaduni wake, mfano :- F Nkwera, Shabani Robart, Mathias Mnyapala na Shaffi Adam Shaffi. Waandishi wengine chipukizi walijitokeza na wanaendelea kujitokeza katika tasnia hii ya uandishi wa vitabu.
Shughuli za kiutamaduni
Shughuli za kiutamaduni zimechangia kueneza kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili. Shughuli hizo ni pamoja na harusi, misiba, matanga na sherehe mbalimbali za kijamii ambazo zimesaidia kukiendeleza Kiswahili kwa kuwa huwakutanisha watu tofautitofauti katika shughuli hizo, ambapo huwalazimu kutumia lugha ya kiswahili katika mawasiliano na kufanya kiswahili kuendelea. Pia katika Sherehe mbalimbali vikundi vya sanaa na muziki vinavyotumia lugha ya kiswahili kutumbuiza. Vikundi vingine huandaa nyimbo zao kwa ajili ya kukieneza Kiswahili.
Vyombo vya Ukuzaji na Uenezaji wa Lugha ya Kiswahili
Tangu Tanzania ipate uhuru hadi sasa kuna vyombo kadha wa kadha vilivyoanzishwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili baadhi ya vyombo hivyo ni hivi vifuatavyo:
BAKITA
Hii ni taasisi ya serikali iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza Kiswahili. Kutokana na sheria hii Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
BAKITA imekuwa na mchango mkubwa sana katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia majukumu yake. Majukumu ya Baraza kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni haya yfuatayo:
Kuratibu na kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini kote. Katika kufanya hivi Baraza lina jukumu la kuhakikisha Kiswahili kinaendelea na kuhakikisha kuwa matumizi ya Kiswahili yanakuwa sahihi.
Kushirikiana na vyombo vingine nchini vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili na kuratibu shughuli zao. Vyama vya Kiswahili kama vile CHAKAMA, CHAWAKAMA vina mchango mkubwa wa kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili kwa kushirikiana na BAKITA. Ushirikiano wa BAKITA na vyama hivi waweza kuwa ni wa kuto ushauri, au msaada wa kifedha, kwa mfano BAKITA imekuwa ikiwasaidia CHAWAKAMA pale wanapokuwa wanataka kufanya makongamano nap engine wanahitaji msaada wa kifedha, kwa hiyo BAKITA imekuwa ikiwasaidia kifedha.
Kuhimiza matumizi ya Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida. BAKITA imekuwa ikiandaa vipindi mbalimbli redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.
Kushirikiana na mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi. Katiaka uundaji wa istilahi, BAKITA imekuwa ikichapisha vitabu mbalimbali ikionesha istilahi sanifu zilizoingizwa katika lugha ya Kiswahili. kwa hiyo kupitia jukumu hili Kiswahili kimekuwa kinakua.
Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo yaserikali na asasi nyingine. Kupitia tafsiri zinazofanywa na BAKITA Kiswahili kimekuwa kikikuwa na kuenea.
Kuchapisha jarida au toleo linalohusu lugha na fasihi ya Kiswahili. Machapisho haya ya BAKITA yanaendelea kukifanya Kiswahili kukua kwa kuongeza msamiati mpya na hivyo watu wanaposoma machapisho hayo wanajifunza msamiati mpya na hivyo kufanya Kiswahili kukua.
Kushirikiana na mashirika ya kitaifa, asasi na watu binafsi, kufuatilia, kushauri na kusimamia shughuli zinazolenga kukuza Kiswahili nchini Tanzania.
Kutoa ushauri kwa waandishi na wachapishaji ili watumie Kiswahili fasaha. Kwa kufanya hivi matumizi bora ya Kiswahili yanakuwa yanaimarika.
Kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuthibitisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa. Hili pia ni jamabo linaloimarisha matumizi ya Kiswahili sanifu.
TAKILUKI
Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mwaka 1979 kwa lengo la kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar, ili kutimiza lengo hilo TAKILUKI inajishughulisha na kazi zifuatazo:
Kuratibu na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni, kuhariri miswada mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili katika Nyanja zake zote, hususani katika uwanja wa sarufi na fasihi.
Pia TAKILUKI wana kazi ya kuandaa istilahi za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za taaluma mbalimbali, kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mabalimbali kwa mashirika, idara, wizara, taasisi, kampuni na watu binafsi, kufundisha lugha za kigeni na kuandika vitabu mbalimbali vya Kiswahili.
Pia hujishughulisha na utoaji wa ushauri wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kama vile, mashirika, wizara, taasisi, vyuo na watu binafsi katika kuendesha shuguli za ukuzaji wa Kiswahili, mathalani kuandaa na kuendesha semina, warsha na kozi fupifupi za Kiswahili.
Vilevile hujishugulisha na usimamizi na ufuatiliaji wa matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo vya habari na katika shughuli mbalimbali za serikali na za kawaida.
TUKI/TATAKI
Majukumu ya TUKI ni pamoja na kuunda sera muafaka za kustawisha Kiswahili na pia kufanya utafiti katika lugha ya Kiswahili.
Majukumu mengine ya TUKI ni kuhariri, kuchapisha vitabu na kutawanya vitabu na majarida ya kitaaluma katika Kiswahili.
Kwa sasa TATAKI inatoa shahada ya awali na uzamili katika lugha ya Kiswahili, kwa njia hii inawaandaa wataalamu wa lugha ya Kiswahili ambao watatumika sehemu mbalimbali za ulimwengu kufundisha lugha ya Kiswahili.
CHAUKIDU
CHAUKIDU ni kifupi cha Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani, makao makuu ya chama hiki kwa sasa yapo chuo kikuu cha Wisconsin-Madison, Marekani
Madhumuni makuu ya CHAUKIDU ni: Kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea kasi ya malengo mahususi yafuatayo:
Kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo lugha hii inatumika au inaweza kutumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na utafiti wa maarifa ya aina zote, uandishi/utangazaji wa habari, uandishi wa vitabu, uchapishaji vitabu na majarida, utayarishaji wa safari za mafunzo katika Afrika ya Mashariki na Kati, n.k.
Kusambaza habari na matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao wa kompyuta juu ya vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana na Kiswahili.
Kuwajumuisha wanachama kwa ajili ya kubadilishana mawazo na tajiriba zao katika masuala mbalimbali yanayohusu Kiswahili (k.v. uboreshaji wa ufundishaji, utangazaji, utafiti, uandishi, nk.) kwa njia ya mkutano wa kila mwaka, warsha au semina au kongamano maalumu, na hata kwa njia ya mtandao.
Kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia, kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.
Kushauri ama kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera muafaka za kukiendeleza kadri ya uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni, kielimu, n.k.
CHAWAKAMA
CHAWAKAMA husimama badala ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki. Chama hiki kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale wanosoma Kiswahili na hata wale wenye mapenzi ya lugha ya Kiswahili pia wanaweza kujiunga na chama hiki.
Chama hiki kina utaratibu wa kuandaa makongamano ambapo wanachama wake kutoka nchi zote za Afrika Mashariki hupata fursa ya kukutana mara moja kila mwaka. Pamoja na utaratibu wa chama kuandaa makongamano pia uanzishwaji wake umeambatana na malengo kadhaa ambayo ndiyo dira inayoiongoza chama kwa mujibu wa katiba, malengo hayo ni haya yafuatayo:
Kuwapa wanachama nafasi ya kujadili, kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili.
Kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa lugha ya kiswahili.
Kueneza lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi.
Kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na kuimarisha lugha ya kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama.
Kuwaunganisha wanafunzi wa kiswahili Afrika Mashariki na kati katika kukikuza kiswahili.
Kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa kiswahili ndani na nje ya nchi kama vile BAKITA, TATAKI, TAKILUKI, UWAVITA, CHAKAMA, BAKIZA n.k.
Kuchapisha kijarida cha chama na machapisho mengine ili kusaidia kueneza taaluma ya kiswahili.
Kuweka kumbukumbu ya wataalamu wa kiswahili kwa nia ya kuwatumia katika kufanikisha malengo ya chama na wadau wa Kiswahili.
Kuratibu makongamano na mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma ya kiswahili.
Pamoja na malengo hayo, lengo kuu la chama hiki ni kueneza Kiswahili lakini sasa wanakienezaje? Wanachama wa chama hiki ambao ni nchi wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki wanakawaida ya kuandaa makongamano kwa ngazi ya kitaifa na ngazi ya kimataifa.
Kwa ngazi ya kitaifa kila nchi huandaa kongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote kutoka vyuo mbalimbali katika nchi husika. Katika kongamano hilo mada mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa juu ya maendeleo ya chama. Sasa katika mijadala kama hii inatoa nafasi ya Kiswahili kukua kwani makala mbalimbali huandikwa ambazo pia husomwa na watu mbalimbali. Makala hizi pia zimekuwa zikichapishwa katika majarida ya chuo husika na pia zimekua zikichapishwa mtandaoni ambapo hutoa fursa kubwa kwa watu wengi zaidi kuzifikia na kusoma, hivyo kwa njia hiyo Kiswahili kinakua kimeenea.
ZOEZI
Kiswahili kilienea kwa kasi sana katika kipindi gani?
A Kipindi cha Waarabu
B Kipindi cha Waingereza
C Wakati wa kupigania uhuru
D Baada ya uhuru
Mwaka ___ ni mwaka ambao Kiswahili kiliteuliwa kuwa Lugha ya Taifa.
A 1964
B 1960
C 1956
D 1962
Ni wakati gani ambapo Kiswahili kilitumika katika elimu?
A Wakati wa waarabu
B Wakati wa waingereza
C Kabla ya uhuru
D Baada ya uhuru
Vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili vilivyoundwa baada ya uhuru ni pamoja na hivi vifuatavyo isipokuwa___.
A UKUTA
B TUKI
C CHAUKIDU
D BAKITA
Kuenea kwa kasi kwa lugha ya Kiswahili baada ya uhuru kulichangiwa na lugha hii kuteuliwa kuwa___
A Lugha sanifu
B Lugha ya Afrika
C Lugha ya taifa
D Lugha ya kimataifa
Dhima ya kila Asasi inayokuza Kiswahili
Mafanikio na Changamoto Zinazovikabili Vyombo vya Ukuzaji wa Kiswahili
Mafanikio
Vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili vimejitahidi sana kukuza lugha ya Kiswahili, kwa hali ya Kiswahili ilivyo sasa ni matokeo ya juhudi za vyombo hivyo. Mafanikio ya vyombo hivyo ni pamoja na haya yafuatayo:
Machapisho ya lugha ya Kiswahili ni mengi sana nchini na nje ya nchi, kufanya mafunzo ya Kiswahili, kukua kwa matumizi ya Kiswahili na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa Kiswahili nchini.
Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika sehemu rasmi hasa katika ofisi za serikali na ofisi za watu binafsi inadhihirisha mafanikio ya jitihada za vyombo hivi kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili.
Kufundshwa kwa lugha ya Kiswahili kama taaluma kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na uzamivu. Hizi ni jitihada za TATAKI katika kuhakikisha kunapatikana wataalamu wa lugha ya Kiswahili, hivi sasa TATAKI wanafundisha lugha ya Kiswahili kwa ngazi ya shahada ya awali, uzamili na uzamivu.
Matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vyombo mabalimbali vya kimataifa, matumizi ya lugha ya Kiswahili katika vikao vya Umoja wa Afrika na pia ufundishwaji wa lugha ya Kiswahili katika vyo mabalimbali Duniani ni ishara tosha ya kuonesha mafanikio ya jitihada za vyombo vya ukuzaji na uenezaji wa Kiswahili.
Changamoto
Vyombo hivi vinakabiliwa na upungufu wa wataalam. Wataalamu wengi waliobobea katika taaluma za Kiswahili wanakimbilia nje ya nchi wakidhani huko ndiko kuna maslahi mazuri zaidi.
Upungufu wa fedha za kuendeshea shughuli za ukuzaji wa Kiswahili katika vyombo hivi pia limekuwa ni tatizo sugu. Kwa hiyo shughuli za ukuzaji wa Kiswahili zinakuwa zinakwenda taratibu.
Taasisi hizi pia zinashindwa kujitangaza vizuri kutokana na kwamba hazina vyombo vya habari binafsi ambavyo vingeweza kutumika kutangaza shughuli zao. Jambo hili limesababisha vyombo hivi kushindwa kutoa elimu ya Kiswahili kwa kutumia vyombo vya habari kutokana na kwamba gharama za kufanya hivyo ni kubwa.
Vyombo hivi baadhi havina ofisi za kudumu, na hivyo kuhamahama jambo ambalo linaathiri utendaji kazi wa vyombo hivyo.
ZOEZI
___ ni taasisi inayohusika na kukuza Kiswahili nje na ndani ya Zanzibar.
A TAKILUKI
B TUKI
C CHAUKIDU
D TAKIKUZA
Utafiti na sera ni moja ya majukumu chini ya uanzishwaji wa___.
A TUKI
B BAKITA
C TEHAMA
D TAUSE
Baada ya uhuru kuna asasi ziliundwa kwa ajili ya kukuza na kueneza Kiswahili ambazo ni___.
A CHAUMA, TATAKI
B CHAKIMA, TUKI
C BAKITA, TUKI, TAKILUKI, CHAWAKAMA
D CHAKAM, BAKITA, TUKI
Mojawapo ya Kazi za Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili Afrika Mashariki ni___.
A Kueneza Kiswahili
B Kufanya utafiti
C Kueneza Kiswahili Afrika Mashariki
D Kusanifisha Kiswahili
Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahli ilibadilisha jina na sasa inaitwa___.
Dhana ya lahaja ni changamani, hutokana na jinsi mtu aliyefasili dhana hiyo anatumia kigezo kipi. Mfano, kuna kigezo cha isimujamii, hiki ni kigezo cha kuwashirikisha wanajamii au wazungumzaji wa lahaja hiyo na ukapata msimamo wao kuhusu lahaja hiyo. Pia kuna kigezo cha kiisimu; hiki kigezo cha kutofautisha lugha na lahaja nyingine kwa kutumia vigezo vya msamiati wa msingi, fonolojia, pamoja na mofolojia.
Lahaja pia inaweza kufasiliwa kwa kuzingatia utengano wa kijiografia au kijamii. Hii ana maana kwamba unaweza kusikia kuwa lahaja fulani inazungumzwa mahala fulani au huzungumzwa na kundi la watu fulani. Mfano, lahaja ya kitumbatu huzungumzwa sehemu za kisiwa cha Tumbatu vivyo hivyo lahaja ya kipemba huzungumzwa na watu wa Pemba.
Hebu tuangalie uchangamani wa dhana ya lahaja kwa kuangalia fasili zifuatazo:
Msanjila (2009:124) anasema lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo inazungumzwa.
Massamba (2002) anasema kuwa lahaja ni lugha mbalimbali za pwani zilizokuwa na uhusianao wa karibu sana. Lugha hizo ni kama vile ci-mbalazi, ki-amu, ki-mvita, ki-jomvu, ki-mtang’ata, ki-makunduchi, ki-tumbatu, ki-mgao na ki-unguja. Wakati wengine wanaziita lahaja mfano, Polome (1967), Bryan (1959) pamoja na Temu (1980).
Kwa mujibu wa Wikipedia, Kamusi elezo huru lahaja ni vilugha vidogo vidogo vya lugha moja ambavyo hubainika kijamii au kijiografia.
Ukizitazama fasili hizi kwa makini utagundu kuwa kila mtu ana mtazano wake kuhusu lahaja, wengine wanasema ni vilugha, ni lugha inayojitegemea, wengine wanasema ni tofauti ndogondogo hasa za kimatamshi katika lugha moja. Lakini pia wengine wanaona lahaja ni tofauti za lugha kwa kigezo cha kijiografia na wengine wanaona ni tofauti za kijamii na kijiografia. Kwa hiyo mitazamo hii ndio hulete utata na uchangamani katika kufasili dhana ya lahaja.
Kimsingi fasili iliyotolewa na Msanjila (keshatajwa) inaweza kutusaidia kujua dhana ya lahaja kwani fasili hii ni ya kiutendaji.Kwa hiyo lahaja ni lugha mojawapo kati ya lugha ambazo kimsingi kuhesabiwa kuwa lugha moja isipokuwa zinatofautiana katika baadhi ya vipengele fulani fulani kama vile lafudhi, fonolojia, msamiati usiokuwa wa msingi au muundo kutokana na eneo lugha hiyo inamozungumzwa.
Mjadala kuhusu idadi ya lahaja za kiswahili na namna lahaja hizi vilivyoinukia:
Mjadala hu ulianza siku nyingi kidogo na hadi sasa hivi hakuna utafiti wa hivi karibuni unaoweza kutusaidia kuthibitisha idadi kamili za lahaji za Kiswahili. Hebu tuangalie wataalam jinsi wanavyojadili idadi ya lahaja za Kiswahili.
Chiraghdin na Mnyampala (1977) wametaja idadi ya lahaja ishirini, lahaja hizo ni kama vile; Kiunguja, Kimrima, Kimgao, Kimvita, Kihadimu, Kipemba, Kirumba, Kiamu, Kipate, Kisiu, Kitikuu, Kingazija, Kingozi, Kitumbatu, Kimtang’ata, Chichifundi, Chibalanzi, Kingwana, Kinyare, na Kijomvu.
Nurse na Spear (1985) wametaja idadi ya lahaja kumi na sita (16), na wamezigawa katika makundi mawili ambayo ni kundi la kaskazini na kundi la kusini. Mfano kundi la kaskazini lina lahaja saba (7) wakati kundi la kusini lina lahaja tisa (9). Baadhi ya lahaja hizo ni;- Kipate, Chimiini, Kibajuni, Kisiu, Kijomvu, Chifunzi, Kipate, Kiunguja, Kimtang’ata, Kimakunduchi na kuendelea.
Utata kuhusu idadi za lahaja za kiswahili unatokana na sababu zifuatazo;
Kigezo kilichotumika katika kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili. Unaweza kufanya utafiti wa lahaja za kiswahili kwa kutumia kigezo cha kijiografia, kijamii, pamoja na kiisimu. Vigezo hivyo vyote vinaweza kukupatia idadi tofauti za lahaja mfano, Massamba katika utafiti wake kwa kutumia kigezo cha kiisimu (1977) alifanya utafiti katika jamii za chi-ruri, chi-jita, na ki-kwaya akathibitisha kuwa hizi ni lahaja za lugha moja na si tofauti, pia kwa kutumia kigezo cha utengano wa kijiografia na kijamii mfano katika lugha ya Kiswahili kwa kiasi kikubwa uanishaji umefanywa kwa utengano wa kijiografia kama vile, kipate kinazungumzwa sehemu za Pate na lahaja ya kipemba huzungumzwa Pemba. Hivyo kutokana na sababu kama hizi husababisha watafiti wengi kutofautiana katika kupata idadi kamili za lahaja.
Kutokana na kukurubiana na kusigana kwa namna fulani kwa lahaja za Kiswahili, kukurubiana huko kwa lugha na mipaka ndiko kunakofanya wazungumzaji wake wajihisi wanazungumza lugha moja. Pia kusigana kwake kwa lahaja hizi husababisha hawa watu wajihisi wanazungumza lugha tofauti. Mfano, lakabu ya lugha ya Kiswahili tunaweza kuifananisha na lugha ya kichaga. Wachaga na lugha zao zote kuhesabiwa kuwa kichaga lakini lugha hizo pia zinatofautiana mfano, ki-machone, kinatofautiana na ki-rombo, ki-marangu, ki-kibosho na kusababisha wasemaji wa lugha hii ya kichagga kushindwa kuelewana kabisa ( Massamba 2002: 258) na hata Wazaramo,Wakwele,Waruguru hujihisi wanazungumza lugha zenye nasaba moja.
Kutokana na kutofautiana kwa majina ya lahaja kuna baadhi ya majina ya lahaja moja hutajwa tofautitofauti na wataalamu mbalimbali, mfano Chiraghdin na Mnyampala (1977) wanataja jina la lahaja ya kihadimu wakati Temu (1980), anasema lahaja ya kihadimu aliita kimakunduchi. Vivyo hivyo Nurse na Spear (1985) wanasema lahaja hiyo ni Kimakunduchi. Hivyo inaleta utata katika kujua kwamba hii ni lahaja moja au ni lahaja mbili tofauti. Pia Bryan (1959) anaitaja lahaja ya Kimbalazi na Polome (1967) ameiita kibrava, Whiteley (1969) ameiita Chimiini, Chiraghin na Mnyampala wanaiita Chibalazi.
Pia kutokana na maendeleo ya Kiswahili sanifu, mfano mpaka sasa kunabaadhi ya lahaja zimebakia kimaandishi lakini kiuhalisia hazipo na hazitumiki katika lugha ya Kiswahili, mfano, lahaja ya Kimgao iliyokuwa inapatikana sehemu za Kilwa imo kwenye maandishi ya wataalamu kama vile Chiraghdin na Mnyampala (1977), Nurse na Spear (1985), Temu (1980). Lakini watumiaji wake hivi sasa wanatumia Kiswahili sanifu, kwa hiyo inaleta utata katika kupata idadi kamili ya lahaja za Kiswahili.
Pia kuna baadhi ya lahaja zipo na zinatumika lakini baadhi ya wanazuoni hawajaziweka katika maandishi. Mfano, kiunguja kinachopatikana Unguja kipo lakini cha kushangaza baadhi ya wanazuoni kama vile Whiteley (1969), Temu (1980) pamoja na Nurse na Spear (1985) hawajaziweka katika maandishi.
Kwa ujumla hakuna idadi kamili ya lahaja. Unaweza kupata idadi ya lahaja kwa kuzingatia mtaalamu na kigezo alichotumia, suala la muda, na mahali unapoenda kufanyia utafiti wa hizo lahaja.
Kuinukia kwa lahaja
Kuna wataalam mbali mbali wanaeleza namna ambavyo lahaja mbalimbali za lugha ya Kiswahili zilivyoinukia. Wataalamu hawa wamegawanywa katika makundi mawili:
Kundi la kwanza; hili ni lile kundi la wanaoamini kuwa lahaja za lugha ya Kiswahili kwa ujumla zilianza sehemu fulani maalum.
Kundi la pili; Wanaoamini kuwa lahaja zilianzia sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja japo kwa kiwango tofauti.
Wafuasi wanaoamini kuwa lahaja kwa ujumla zilianza sehemu fulani maalumu au sehemu moja wanajikita katika hoja ya msingi kuwa lugha huanzia sehemu moja maalum na kusambaa sehemu nyingine na hii hutokana na kadri matumizi yanavyoongezeka na idadi ya watu inavyoongezeka ndivyo watu hawa hutawanyika kwenda sehemu tofautitofauti na kusababisha kutokea kwa lahaja tofautitofauti za kiswahili.
Kwa mujibu wa Nurse na Spear (1985) lugha huanzia mahali fulani pamoja katika kipindi fulani kadri wasemaji wanavyoongezeka na lugha huanza kubadilika na kuwa ya ana kwa ana. Hivyo kutokana na sababu ya kutawanyika kunapelekea kutokea kwa lahaja tofautitofauti. Mfano; hawa wanazuoni wanadai kuwa lahaja za kiswahili zilianzia kaskazini mwa Mombasa katika eneo la Lamu na kuendelea sehemu nyingine ya pwani ya Afrika Mashariki na hii ni kutokana na kwamba utafiti wa akiolojia unaonesha kuwa mbantu wa kwanza kabisa aliishi katika mji wa Lamu. Udhaifu wa mtazamo huu ni kwamba kama watu hao wametokea katika jamii moja yenye lugha moja, hivyo ni vipi wanaweza kutambulishwa kutumia lahaja zao yaani lahaja za kaskazini na lahaja za kusini.
Pia suala la muingiliano wa lugha kutokana na mabadiliko na maendeleo katika jamii halina nafasi katika maendeleo ya lugha. Kutokana na udhaifu huu kukapelea kutokea kwa kundi jingine.
Kundi la wale wanaoamini kuwa lahaja zilianzia sehemu mbalimbali kwa wakati mmoja ila kwa kiwango tofauti. Ugunduzi wa kiakiolojia wa hivi karibuni unaonesha maeneo mengine kama vile Unguja, Pemba na Kilwa. Mfano, Mji wa Kilwa kuwa maarufu kuliko mji wa Lamu. Ugunduzi huu unaonesha kuwa mbantu wa mwanzo aliishi Kilwa na sio Lamu kama inavyoelezwa na Nurse na Spear (1985). Kwa hiyo maelezo hayo yanatuonesha kuwa mji wa Kilwa ulikuwa maarufu zaidi kuliko Lamu.
Ni kutokana na ukinzani wa mji wa Kilwa na Lamu kiumaarufu ndipo wataalum wengine wakasema kuwa lahaja za Kiswahili ziliinukia sehemu mbalimbali kwa kipindi kimoja japo kwa kiwango tofauti.
Grenville (1959) katika makala yake ya “Medieval Evidence for Swahili” anasema wazo la kuinukia mapema kwa Kiswahili katika Kilwa na hakubaliani na fikra za kuwa lugha ilianzia Lamu kwani hata kumbukumbu za kihistoria kipindi cha kati zinadai kuwa mji wa Kilwa ulikua maarufu kuliko Lamu, hii ni kutokana na shughuli za kiuchumi zilizokuwa zinaendelea.
Pia Massamba (2007) anasema, hizi zinazoitwa lahaja za Kiswahili za sasa ziliinukia sawia sawia katika maeneo mbalimbali na kwa sababu ya kuingiliana kibiashara, kiuchumi na kijamii na huu ndio ukawa ndiyo mwanzo ya lahaja ya Kiswahili sanifu. Kwa mtazamo wake, Massamba anadai kuwa, lahaja za Kiswahili tunazozifahamu hivi sasa kama vile; kimakunduchi, kipate, kiamu, kimvita pamoja na kiunguja hapo zamani ziliitwa lugha zinazojitegemea. Lugha hizi ziliathiriana kutokana na ukaribu wake na zaidi kwa sababu zilitokana na mame bantu moja. Hivyo ukizichunguza kwa umakini utagundua kuwa zilizokaribu zinafanana sana kuliko zilizo mbali. Pia lugha zilizo malikuu moja hufanana lakini lugha zilizokaribu hufanana zaidi.
Hitimisho
Kwa ujumla lahaja za lugha ya kiswahili zilianzia sehemu tofauti tofauti na zikaendelea kukua sambamba na hii ni kutokana na muingiliano wa masuala ya kiuchumi, kijamii pamoja na kibiashara ndiko kulikopelekea kufanana kwa hizi lahaja za kiswahili. Ni dhahiri muingiliano wa watu katika jamii ni suala lisiloepukika kutokana na mabadiliko na maendeleo ya maisha.
MAREJEO
Chiraghdin, na M. Mnyampala (1977) Historia ya Kiswahili.Nairobi:Oxford University Press.
Massamba,D. P.B (2002). Historia ya Kiswahili: 50 BK hadi 1500 BK. Nairobi: Jomo Kenyatta
Foundation.
Msanjira, Y.P na wenzake (2009). Isimu Jamii: Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: Taasisi ya
Uchunguzi wa Kiswahili.
Nurse, D na T. Spear (1985). The Swahili. Reconstructing the History and Language of an
African Society. Philadelphia: University of Pennsylvania.