MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.
MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
#1
MBINU ZA UFUNDISHAJI KISWAHILI KWA WAGENI
  1. Malengo ya ufundishaji lugha kwa wageni
Lengo kubwa ni kwamba ili mwanafunzi aweze kujua lugha hiyo kwa stadi zote za lugha ile. Stadi za lugha ni 1. Kusikiliza 2.kuzungumza 3. Kusoma 4.kuandika 5. Sarufi 6. Utamaduni wa lugha ile
Malengo ya jumla ya kufundisha ili ni pamoja na:-
1)      Kumwezesha mwanafunzi ili aweze kumudu lugha.
2)      Kumwezesha mwanafunzi aweze kuwasiliana na wazawa wa lugha husika
LUGHA YA KWANZA
Stern (1983) anasema kwamba “lugha ya kwanza lugha ambayo mtoto hupata kutoka kwa mama yake mzazi angali mchanga.
LUGHA YA PILI
Stern (1983) anasema kwamba “ lugha ya pili si lugha ambayo mtoto/mtu aliipata alipoanza kukua na kupata lugha. Hii ni lugha ya kujifunza,kwa maana ya kwamba mtu huyu huwa tayari ana lugha nyingine.mfano. hapa Tanzania Kiswahili ni lugha ya pili kwa watu wengi
LUGHA YA KIGENI
Ni ile lugha ambayo unajifunza na kuitumia lakini wazungumzaji wake wako nje ya nchi au mbali na jamii anapokaa mwanafunzi huyo. Mfn lugha ya kiingereza ni lugha ya kigeni hapa Tanzania
MALENGO YA JUMLA YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI WA LUGHA YA KIGENI
Mara nyingi hii hutegemea taaasisi yenyewe lakini kuna malengo ambayo ni ya jumla:
1)      Kutaka kuwasiliana na wenyeji wa sehemu /nchi husika
2)      Kujiandaa kusafiri kwenda nchi nyingine kwa shughuli mbalimbali
3)      Kwa ajili ya kufanya biashara
4)      Kukidhi vigezo vya masomo
5)      Kufanya utafiti katika taaluma husika
6)      Ili kupata ajira nchi za ng’ambo
KITU GANI KIANZE KUFUNDISHWA SASA?
Onyo: usijaribu kumfundisha mwanafunzi sarufi za lugha hiyo kwanza, utamfundisha ikibidi lakini isiwe kipaumbele chako
W      Anza na salamu za kawaida, salamu katika utamaduni wa mwafrika ni kitu cha muhimu sana, hivyo fundisha salamu,maana lengo ni kwamba huyo mtu aweze kuwasiliana.
MALENGO YA UJUMLA YA UFUNDISHAJI LUGHA YA KISWAHILI KWA WAGENI
a)      Ili mwanafunzi wa Kiswahili ajue mambo yafuatayo:
i.            Aweze kumudu lugha ya Kiswahili
ii.            Aweze kuwasiliana na watumiaji wa lugha ya Kiswahili
iii.            Ili wanafunzi waweze kung’amua mambo yafuatayo:- Namna ya kusema jambo gani? Mfano anataka kwenda chooni Asemee wapi? Kwa nini aseme? Kwa nani aseme? Mazingira gani aseme?
iv.            Ili kuwapa wanafunzi mbinu mbalimbali za kujifunza lugha ya Kiswahili. Wanafunzi wafanye kwa vitendo ili waweze kujichukulia misamiati ya kutosha
v.            Wanafunzi wang’amue umuhimu wa lugha wanayojifunza
b)     ili wanafunzi waweze kutimiza malengo haya, mwalimu ni lazima wape wanafunzi:
kuchunguza®kugundua®kutalii kuhusu lugha ya Kiswahili
c)      wape uwezo wa kukuza lugha ya Kiswahili kila siku aweze kuongeza msamiati kwa kusoma vitabu mbalimbali vya hadithi
d)     wape nafasi kutumia mbinu mbalimbali lugha ili kukuza uelewa wao
e)      wape uwezo wa kukuza fikra zao na kudadisi
f)       wasaidie kufanya utumbuizi wa vipengele vya mfumo na utamaduni wa lugha ya Kiswahili
NADHARIA KUU ZA UJIFUNZAJI LUGHA
Kuna mambo mawili ambayo waalimu tarajili wanapaswa kujua
1)      mbinu za kujifunza lugha ya pili ni nyingi kama ilivyo waalimu wengi
2)      manzingira halishi wakati wa ujifunzaji. Rogers (2001) anasema kwamba “ wakati wa ufundishaji wa lugha ya kigeni hutumia mbinu mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wafikie malengo yao”
kuna nadharia kuu nne (4)za ujifunzaji lugha:
1)      NADHARIA YA UHULKA
ü  Mwasisi wake ni Noamy Chomsky (1957)
ü  Wazo kuu lake ni kwamba: binadamu huzaliwa akiwa na uwezo lugha. Yaani kwenye ubongo wake ana mfumo ambao huzaliwa nao kwa ajili ya kujifunza lugha. Ana kifaa kinachoitwa LAD (Kifaa cha upataji lugha)
ü  Naye Brown (2000) aliunga mkono mawazo haya. Mwingine aliyeunga mkono ni Ellis (1997) walikuwa na hoja kwamba kuna kipindi mtu akifikia umri Fulani hawezi kupata lugha sawasawa na wazawa wa lugha husika. Umri huo ni kuanzia 0-miezi 18. Kwa mujibu wa wataalamu hawa mazingira hayana msaada wowote katika ujifunzaji lugha.
2)      NADHARIA YA UTABIA
ü  Kwa mara ya kwanza ilidokezwa na E.Thonilke(1935). Kwa mujibu wa wanatabia ujifunzaji wa lugha ni mwigo
ü  Aliyetafiti zaidi katika nadharia ya ujifunzaji ni B.F SKINNER , Huyu alikubali ni mwigo lakini akaongeza kuwa ni uimarikaji wa tabia, hivyo mtoto mdogo hazaliwi na lugha bali huichota kutoka kwa wazazi wake
  • Nadharia hii inayapa mazingira nafasi kubwa katika ujifunzaji lugha
  • Je mtu akitengwa na jamii anaweza kuwa na lugha? Jibu unalo wewe mwenyewe!
3)      NADHARIA YA UTAMBUZI
ü  Nadharia hii iliasisiwa na Jean Hajet (1954)
ü  Alidai kuwa binadamu anapozaliwa kuna kipindi maalum cha kupata lugha
ü  Alidai kuwa kujifunza lugha ni sehemu ya makuzi ya binadamu, kwa kadiri unavyokua ndivyo unavyozidi kupata lugha
ü  Alidai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa.
ü  Arth(2003) anadai kuwa mtoto hupata lugha kabla ya kuzaliwa,kuanzia 0-miezi 18
ü  Nadharia hii haipingani na umuhimu wa mazingira katika ujifunzaji lugha
4)      NADHARIA YA UUMBAJI/ MAUMBILE
ü  Iliasisiwa na Jerome Brunner
ü  Wazo kuu la nadharia hii inasisitiza nafasi ya mama katika upataji lugha ya kwanza
ü  Mtoto hutengeneza lugha kutegemeana na mawasiliano ambayo mama yake anayatumia
ü  Alidai, ili mtoto aweze kupata lugha ni lazima mambo yafuatayo yatimizwe
  • Muktadha
  • Tajiriba (experience)
  • Upangilifu (organization)
  • Kujenga mazingira ya upekuzi (udadisi_
ü  Hukaza zaidi kuhusu mazingira katika ujifunzaji lugha
NJIA ZA UJIFUNZAJI LUGHA YA KISWAHILI
Njia za ufundishaji Kiswahili ni nyingi kama na waalimu nao walivyo wengi, lakini njia hizi itatengemea hali ya wanafunzi, hata hivyo njia zifutazo zinapendekezwa zitumike.
  1. Njia ya majadiliano-njia hii haifai kwa mwanafunzi ambaye ndio kwa mara ya kwanza anasikia Kiswahili. Lakini ni njia nzuri kwa mwanafunzi ambaye amewahi kusikia habari za Kiswahili
  2. Njia ya mahojiano. Mfano mwalimu aandae maswali, awaambie wanafunzi wajipe vyeo mfano mmoja anakuwa daktari mwingine anakuwa mgonjwa n.k
  3. Mchezo wa maswali. Kwa mfano. Kama wewe ungekuwa rais wa marekani ungefanyaje kuhakikisha unakomesha ugaidi duniani? Watajibu na kujipatia msamiati kibao
  4. Njia ya uigizaji-mwli awape wanafunzi mwongozo wa maigizo
  5. Njia ya maswali ya papo kwa papo (ana kwa ana) mfano: mimi ni Seni, wewe ni nani?
  6. Njia ya uwandani. Mfno ukitaka kuwafundisha misamiati ya sokoi wapeleke sokoni.
  7. Njia ya kutumia mazingira mbalimbali. Mfano kama mwalimu anataka kuwafundisha michezo wapeleke uwanja wa mpira
  8. Njia ya usomaji. Mfano kusoma pande nne za dunia,kuwapa matini mbalimbali wanafunzi
  9. Njia ya majadiliano funge. Yaani wanafunzi wanajadili vitu ambavyo vimewekewa mipaka
Angalizo:uteuzi wa njia ipi itumike itategemea aina ya wanafunzi na kazi zao!
HULKA/TABIA YA UANAFUNZI KUJIFUNZA LUGHA
Wanafunzi hutofautiana kulingana na hulka zao, mwalimu anahitaji kuangalia mielekeo ya wanafunzi wake. Baadhi ya tabia zao ni kama vile: ucheshi, hasira, aibu, hasira za kutojua, hapendi kusahihishwa, mkimya nk
ATHARI ZA KIJAMII KUHUSU LUGHA/WANALUGHA
Kila jamii ina mtazamo wake kuhusu ujifunzaji lugha, mtazamo hasi ndio ambao huathiri ujifunzaji lugha na kupelekea kutopata motisha wa kujifunza lugha. Baadhi ya mambo yanayoathiri ni kama vile
i.            Nia au lengo la kujifunza lugha hiyo
ii.            Jinsia
iii.            Umri
iv.            Mazingira
v.            Umilisi wa lugha kama akiwa na umilisi mdogo
Malengo ya mwalimu ni kuhakikisha anafanya mambo yafuatayo:
i.            Kuwatia motisha wa kujifunza lugha
ii.            Kumsaidia kuondokana na hasira
iii.            Kuondoa dhana potofu ya ujifunzaji lugha. Mf. Kuna wanaoamini kwamba Kiswahili ni lugha ya kiislamu
iv.            Kuondoa utata katika vipengele vya kisarufi
v.            Kuwaelezea aina mbalimbail za lugha na mahali zinapotumika
Kuhusu matumizi ya lugha ya ishara ni muhimu sana kujua ishara zinazotumika katika jamii. Hivyo mwalimu anapaswa awaeleze mambo yafuatayo
i.            Baadhi ya utamaduni huangalia usoni, tabasamu na kujiamini
ii.            Matumizi ya mkono wa kushoto au wa kulia
iii.            Kuonyesha vidole-jamii zingine haziruhusu kabisa
iv.            Namna ya kusimama na kuelezea jambo
Ili kutimiza hayo yote mwaimu lazima awe na sifa zifuatazo:
i.            Awe muwasilishaji mzuri
ii.            Awe na mpangilio mzuri
iii.            Awe mstahimilivu
iv.            Awe na ujuzi wa kufundisha
v.            Awe na uhusiano mzuri na wanafunzi
vi.            Awe na maarifa ya somo
SIFA ZA MJIFUNZAJI LUGHA
a)      Awe na utayari wa kujifunza lugha ya Kiswahili bila kulazimishwa
b)     Afanye mazoezi ya kuitumia lugha hiyo
c)      Atumie akili kupambanua dhana mbalimbali ili kugundua mambo ambayo jamii Fulani inayafanya
d)     Awe na uhuru wa kuzungumza lugha hiyo
e)      Awe na ratiba ya kujifuza
f)       Aweze kulinganua na kulinganisha lugha anayojifunza
g)      Awe na ukarimu ili aweze kuwa na uhusiano na jamii husika
h)     Awe mtendaji
i)        Azingatie ubora ili aweze kujifunza zaidi
MOTISHA
Ni tabia au msukumo katika kutimiza malengo Fulani. TUKI (2004) wanadai kuwa motisha ni kitu kama fedha inayotolewa ili kumtia mtu hamasa kujifunza jambo.
Hata hivyo, si lazima umpe kitu bali unamtia moyo mwanafunzi na kumsaidia. Mwalimu anapaswa kutumia motisha chanya sio hasi. Mfn hutakiwi kuchapa fimbo
Brown (1994) anasema kuwa motisha:
a)      Ni kiwango cha uchaguzi ambacho unafanya kuhusu lengo unalotaka kufikia
b)      Jitihada atumiazo mtu kufikia malengo hayo
SKINNER &WATTSON-hawa wanaangalia zawadi na uhimizaji kwa wanafunzi pamoja na adhabu ili kufifisha na kujenga hali Fulani
AINA ZA MOTISHA
  1. Mwamko wa mjifunzaji mwanyewe
  2. Mazingira mazuri ya kufundishia Kiswahili mfano, darasa, nje n.k
  3. Jamii inayomzunguka ni motisha pia
  4. Mwalimu anaweza kuwa motisha kwa mwanafunzi
  5. Zana/vifaa vya kujifunzia pia ni motisha
  6. Motisha wa ndani-
MOTISHA IPO KATIKA MAKUNDI MIWILI
ü  Haitegemei vitu vya nje ya yenyewe
ü  Hiki ni kile kinachoonekana kwa mjifunzaji lugha mwenyewe
ü  Hii haibadiliki kulingana na muktadha wowote ule
  1. Motisha wa nje
ü  Ni aina ya motisha ambayo mwanafunzi hutegema kupewa, kupata, kusikia au kuona
ü  Hivi vitamsaidia katika kujifunza lugha
Mwalimu wasaidie wanafunzi kutumia lugha kulingana na muktadha. Hapa kuna mambo ya kuzingatia:-
a)      Akili ya mwanafunzi: lazima utambue tofauti zao katika akili zao ili kujifunza lugha
b)     Kipaji chao-kuna wengine wana vipaji vya kujifunza lugha
c)      Umri-watu wazima huchelewa kujifunza lugha
d)     Jinsia-inasemekana wanawake wanaweza kupata lugha haraka kuliko wanaume
UFUNDISHAJI LUGHA KIMAWASILIANO
ü  Ni muhimu kuhakikisha kwamba katika kujifunza lugha ufundishaji uwe wa mawasiliano
ü  Ni mbinu ya kufundisha lugha ngeni na lugha ya pili
ü  Husisitiza mwingiliano maathiriano kama mbinu ya kujifunza lugha
KAZI ZA LUGHA
ü  Van (1975) anasema kuwa kazi ya lugha ni:
a)      Kutoa habari
  • Kusimulia
  • Kuuliza
  • Kutoa taarifa
b)      Kutafuta taarifa za kitaaluma
c)      Kuelezea mihemuko na misisimko. Mfno mapenzi, misisimko
d)     Kuelezea masuala ya uadilifu.mfn kuomba msamaha, ibada etc
e)      Kwenye mambo ya ushirikiano. Mfn kuamkia watu, kujitambulisha nk
Angalizo: hata kama mwanafunzi ana malengo mengine ya kujifunza lugha hiyo ni lazima umfundishe umuhimu wa lugha hiyo kulingana na muktadha
MASHARTI YA KUZINGATIA
a)      Azingatie majukumu ya kijamii mfn ataanzaje kuzungumza na mtu asiyemjua? Watu wengine ni wenye mamlaka Fulani, hivyo kuna namna ya kuzungumza nao
b)      Majukumu ya kisaikolojia-mfano asipendelee upande wowote mfn CHADEMA CUF na CCM
c)      Mazingira ya lugha ilipo. Je ni lugha ya taifa? Watu wanaokuzunguka wanatumiaje?
Angalizo: lugha sio sarufi tu au fonolojia bali ni chombo cha mawasiliano, hivyo inahitaji kufundishwa kimawasiliano zaidi
MUKTADHA WA UFUNDISHAJI LUGHA
ü  Haya ni mazingira halisi ambapo tukio la ufundishaji lugha hufanyika kwa kuzingatia wadau wakuu watatu
a)      Mwanafunzi
b)      Mwalimu
c)      Jamii
ü  Pamoja na motisha ufundishaji uzingatie sana mambo yafuatayo:
  • Utoaji wa kazi na mazoezi mengi
  • Tumia lugha katika mazingira halisi na yanayostahili ukilenga kwenye stadi nne za lugha
  • Matumizi ya lugha kwa kuzingatia muktadha
  • Utumizi wa mazingira halisi ya darasa.mfn picha, katuni. Nk
  • Himiza ushirikiano miongoni mwa wanafunzi baina yao na baina yako mwalimu
  • Tumia mbinu zaidi ya moja. Mfn vikundi, majibizano nk (rejea mbinu)
  • Fafanua kwa uangalifu masuala ya kisarufi
  • Ajue maono ya mwanafunzi. Mfn huzuni, ucheshi nk
  • Kuunda mazingira ya utani darasani
UFUNDISHAJI WA DARASA MSETO
ü  TUKI (2013) Mseto ni hali ya kuwa na mchanganyiko wa makabila mbalimbali kutengeneza kitu fulani
ü  Hapa ni mchanganyiko wa darasa lenye wanafunzi wanaotoka sehemu mbalimbali na wenye umri tofauti, malengo tofauti nk
ü  Hivyo mwalimu inakubidi utofautishe sana katika ufundishaji wako na uwe makini ili usije ukawakwaza wanafunzi wengine
NAMNA YA UFUNDISHAJI DARASA MSETO
a)      Lazima mwalimu uwe na maarifa ya wanajamii mfn utamaduni wao. Kama ni wazungu, wachina nk jua utamaduni wao
b)     Uwe na usisitizaji wa lugha lengwa. Kama ni Kiswahili basi pendelea kutumia Kiswahili ili usiwakwaze sana. Hata hivyo lazima wawe na lugha ambayo wewe unaijua
c)      Tumia vitendo halisi, ishara nk
d)     Arika wageni mbalimbali waje waeleze kuhusu lugha na mazingira
e)      Puuza(ignore) malengo ya wanafunzi
f)       Ufundishaji wa masuala ya utamaduni lazima ufungamane na muktadha husika
SIFA ZA MPATAJI LUGHA
Mpataji lugha ni lazima awe na sifa kuu mbili tu:
  1. Umilisi wa kiisimu
ü  Ni uwezo alio nao mjifunzaji lugha ambao unamwezesha kutofautisha viambo, miundo tofauti ya lugha na msamiati wa lugha
ü  pia kuweza kutamka lugha ile.
  1. Umilisi wa kiisimujamii
ü  Ni umilisi ambao mtumiaji wa lugha hupata lugha inayomwezesha kujifunza lugha na kuzingatia muktadha
NADHARIA /MBINU /MIKABALA ZA KUJIFUNZA LUGHA YA KIGENI
ü  Nadharia ni mkondo wa mawazo unaotumika kuelezea jambo
ü  Mtesigwa(2009) anasema “ nadharia ni kiunzi cha mitazamo, mawazo au vitendo vinavyohusisha uchunguzi, mpangilio na uchanganuzi wa matukio katika kukabili suala fulani kisayansi
®kuna mambo mawili ambayo lazima tujikumbushe:
a)      Njia za ufundishaji lugha ya kigeni ni nyingi kama waalimu walivyo wengi
b)      Kumbuka hali ya darasa. Tumia njia mbinu zaidi ya moja darasani, usitumie njia moja tu.
ü  Rogers&Richards (2001)wanasema kuwa tunapojiandaa kwenda kufundisha tunahitaji kujiuliza maswali yafuatayo:-
a)      Malengo ya ufundishaji lugha lengwa(LL) ni yapi? Mfano labda lengo lao linaweza kuwa wanataka kuzungumza tu.
b)      Upi ni msingi asili wa lugha lengwa na unaathiri vipi njia za kufundisha. Mfn kaida za lugha ya Kiswahili ni zipi?
c)      Ni misingi ipi inatumika kuchagua mambo katika ufundishaji lugha?
d)     Ni misingi ipi ya upangiliaji wa mada. Mfano kwa kuzingatia suala la utamaduni, mfano salamu nk
e)      Je lugha mama ya mwanafunzi ina jukumu gani katika kujifunza lugha? Mfano miundo ya lugha mama inafanana na lugha lengwa?
f)       Je wanafunzi binafsi watumie mbinu zipi katika kujifunza lugha hiyo?
g)      Je ni mbinu na vitendo vipi hufanikisha vizuri ujifunzaji lugha ya pili (kigeni)?
NADHARIA ZA KUJIFUNZA
  1. Mbinu ya tafsiri sauti
  2. Mbinu ya moja kwa moja(direct method
  3. Mbinu ya usomaji(reading approach method)
  4. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
  5. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
  6. Mbinu ya ukimya (silence method)
  7. Mbinu ya mawasiliano (communicative language approach)
  8. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
  9. Mbinu ya utambuzi (communitive code method)
  10. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
  1. Mbinu ya tafsiri sarufi
ü  wakati mwingine hujulikana kama mbinu ya kimapokeo. Huu ni mkabala ambao ufundishaji wa lugha ya kigeni umejiegemeza katika sarufi ya lugha ya Kiratini. Iliasisiwa/anzishwa na Meidinger (1783) na Ploetz (1849) wakati ule iliaminika kwamba lugha ya kiratini ndiyo lugha pekee.
ü  Nafasi ya lugha mama ilipuuzwa kwa kiasi kikubwa na ilijikita katika sarufi ya Kiratini, na hivyo mwalimu alipaswa kujikita katika kufundisha sarufi ya Kiratini na vipengele vingine vilipuuzwa
ü  Huu ulikuwa ni mkabala elekezi-yaani unawaelekeza watu namna ya kutumia lugha na sivyo wanajamii wanavyotumia lugha hiyo
  1. Mbinu ya moja kwa moja(direct method)
ü  Iliasisiwa na Gouin(1880)
ü  Nadharia hii inazingatia uzungumzaji wa lugha husika
ü  Mbinu zilizopaswa kufundishia ni zile zilizohamasisha wanafunzi kuzungumza. Mfn mbinu ya majadiliano,uigizaji,maswali katika vikundi
ü  Masomo yalianza kwa hadithi fupi halafu wanafunzi wanauliza maswali kuhusu hadithi waliyosimuliwa na mwalimu aliwaambia watoe maoni yao kuhusu hadithi hiyo.
ü  Matumizi ya vielelezo vilitumika zaidi. Mfano picha, ramani, katuni n.k
ü  Kipengele vya sarufi kilifungushwa kwa kufuata muktadha halisi ambamo lugha inatumika
ü  Kipengele cha utamaduni kilifundishwa kwa uchache sana
  1. Mbinu ya usomaji (reading approach method)
ü  Mbinu hii inatumika kufundishia kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ya kigeni ambao hawatarajiwi kutoka nje ya nchi ambapo lugha hiyo inatumika
ü  Malengo yake huwa kuendeleza uwezo wao wa kusoma ile lugha
ü  Vipengele vinavyofundishwa ni vile vinavyohusu usomaji, hivyo vipengele vingine havihusiki. Mkazo wake ni kwamba anayejifunza lugha aweze kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja.
ü  Mbinu hii haimpi mjifunzaji lugha uwezo wa kuzungumza lugha husika bali ni kuisoma tu.
  1. Kusikia na kusimulia (audiolingual method)
ü  Nadharia hii ilitokana na haja ya ukarimani nchini marekani miaka 1940.
ü  Iliasisiwa na Bloomfield (1942) na Fries (1945)
ü  Msingi mkubwa wa nadharia hii ni kile kinachosemwa
ü  Maandishi hayakupewa fursa kubwa bali kile kilichosemwa ndicho kilikuwa cha muhimu sana. Bloomfield alisema kuwa lugha si katika maandishi bali ni kile ambacho kinasemwa.
ü  Inahusisha kusimulia mada mbalimbali na kupima uwezo wa kusikia
ü  Walipenda sana kutumia miziki, nyimbo, usimulizi na ughanaji
ü  Walisisitiza stadi ya kusikiliza, kuzungumza, kusoma na kuandika
ü  Waliongeza kitu kingine chakuona
  1. Kushirikisha jamii (community langaage learning method)
ü  Iliasisiwa na curran (1976)
ü  Dai la nadharia hii ni lugha ni watu, kwa maana ya kwamba huwezi kutenga jamii na lugha
ü  Walidai kwamba ili uweze kumfundisha mwanafunzi mgeni basi nenda kwenye jamii husika
ü  Walidai pia kwamba kama utaamua kufundishia darasani bali darasa lako lifanye angalau lifanane fanane na jamii ya lugha husika
ü  Ili uweze kufundisha watu ni lazima ushirikishe watu wanaotumia lugha hiyo.
ü  Mwanafunzi atapata vichocheo vya aina nyingi katika jamii na kubaini ni mambo gani yanafaa na mambo gani hayafai
ü  Nadharia hii inaipa kipaumbele jamii kama chombo muhimu katika kujifunza lugha
  1. Mbinu ya ukimya (silence method)
ü  Nadharia hii inaamini kwamba kila lugha ina mfumo wake tofauti na lugha nyingine, hivyo ufundishaji wa lugha ya pili ulenge kumfanya mjifunzaji wa lugha kuwa mmilisi au kukaribia kuwa mmilisi wa lugha anayojifunza
ü  Nadharia hii inadai kwamba ujifunzaji wa aina yoyote ile unahusisha vitu viwili.
Kichocheo®     Mwitikio®       mgeuko
(Mwalimu)     (mwanafunzi)-(anabadilika)
ü  Ili kuweza kutimiza hili, mwalimu anahitaji kujenga mazingira ya utani katika darasa jambo ambalo litaleta matokeo mazuri ya umilisi wa lugha husika
ü  Nadharia hii inamhitaji mwalimu kufanya tathimini kwa wanafunzi wake ili kubaini kama kuna badiliko
  1. MBINU YA UTAMBUZI (COMMUNITIVE CODE METHOD)
ü  Nadharia hii inatokana na ukosoaji/udhaifu wa nadharia ya mbinu ya sarufi na ile ya moja kwa moja
ü  Ilianzishwa mwaka 1970
ü  Wanadai kwamba mwanafunzi apewe vipengele vyote vya lugha kwa ujumla mwanafunzi kumpa maarifa mapana kuhusu lugha, kumpakanuni za msingi kuhusu lugha, halafu yeye mwenyewe kulingana na utambuzi wake aweze kuielewa lugha.
ü  Uwafundishe kanunu za msingi. Kwa mfano katika lugha ya Kiswahili ni lazima ujue ngeli za majina-hii itakusaidia kutumia nomino katika mazingira tofauti tofauti, vitenzi-waeleze namna ambavyo vinaweza kukaa peke yake kama sentensi
  1. Mbinu ya mwitiko jumuishi(total physical response)
ü  Nadharia hii pia hujulikana kama mkabala asilia.
ü  Iliasisiwa na James na Asher
ü  Inatilia mkazo mfumo na muundo wa lugha.
ü  Kama ilivyo nadharia ya usikizi nadharia hii pia inasisitiza umuhimu wa kumudu mazungumzo kama sehemu ya umilisi wa lugha
ü  Ufundishaji uhusishe mazoezi ya kurudia rudia ambayo angalau unamfanya mwanafunzi kumudu anachojifunza
ü  Nadharia hii inasisitiza matumizi ya vitendo na ishara mbalimbali kama nyenzo mojawapo katika kujifunza lugha.
  1. Mbinu ya upendekezi (suggestopidia method)
ü  Ilianzishwa na Lonzano georgi (1979)
ü  Nadharia hii inayapa mazingira bora ya ujifunzaji lugha kama nyenzo muhimu mojawapo katika kujifunza lugha. Hii inamaanisha kwamba mazingira yanayotumika kujifunzia lugha ni lazima yamkumbushe mwanafunzi kile alichojifunza jana yake
ü  Wanaelezea namna ya mkao wakati wa kufundisha wanafunzi wageni. Mkao katika darasa uwe ni wa kutazamana, maana yake vikae kwa duara.
ü  Wanasisitiza matumizi ya mziki laini na mziki nyororo
  1.                 MBINU YA MAWASILIANO (COMMUNICATIVE LANGUAGE APPROACH)
ü  Inasisitiza maingiliano na maathiriano katika ya mwalimu, mwanafunzi na jamii
ü  Wanakaza kwamba kujifunza lugha ni kujifunza kuwasiliana.
ü  Kujua lugha kwa hakika sio kujua kanuni za lugha ile bali ni kujua namna ya kuwasiliana na watu wa jamii ile kwa kuzingatia mikitadha mbalimbali ambamo lugha hiyo inatumika
ü  Ni nadharia ambayo imeshaididiwa na wataalam wengi akiwamo Noamy Chomsky
ü  Hii ndiyo nadharia ambayo inafaa kutumia kwa ajili ya kujifunza lugha
VIWANGO VYA WANAFUNZI
  • Hapa inamaanisha uwezo alio nao mtu wa kutumia lugha Fulani.
  • Viwango hivi viliwekwa na shirika/taasisi moja isiyokuwa ya kibiashara wala kiserikali liitwalo Interagence Language Round Table (ILRT)
  • Kulingana na shirika hili wajifunzaji lugha wako katika viwango vitatu
a)      Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
b)      Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)       Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
a)                  Wanafunzi wa daraja la msingi (Kisw.DAMSA) Beginners Level
Daraja limegawanyika katika viwango hivi
  • Kiwango cha 0-®mwanafunzi hawezi kabisa kuzungumza lugha
  • Kiwango cha +0-®mwanafunzi amekaririshwa tu mahitaji muhimu akibadilishiwa tu basi Amepotea
  • Kiwango cha 1-®mwanafunzi anaweza kusitahimili mazungumzo ya ana kwa ana ila hawezi kuanzisha mazungumzo
  • Kiwango cha +1-®huyu anaweza kuanzisha mazungumzo yeye mwenyewe, hata hivyo ni kwa ajili ya kukidhi matarajio yake
INTERMIDIATE
  • Daraja la 2-lugha si kamilifu lakini anaeleweka kwa urahisi
  • Kiwango cha 3-anaweza kuzungumza lugha kwa muundo sahihi, ana msamiati wa mazingira fulani fulani tu ili kukidhi mahitaji ya kitaaluma
  • Anaweza kukithi mahitaji ya kitaaluma
b)            Wanafunzi wa daraja la kati (DAKATI)Intermediate Level
c)            Wanafunzi wa daraja la juu (DAJUU) Advanced Level
Mwl Maeda
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)