Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 98 online users. » 0 Member(s) | 97 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
RIWAYA NA HADITHI FUPI |
Posted by: MwlMaeda - 09-17-2021, 07:51 AM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
DARASA LA RIWAYA YA KISWAHILI
Kozi hii itajumuisha saa 3 za kujifunza kwa juma, ambapo saa 2 ni za mhadhara na saa 1 ya semina. Majuma 15 ya ufundishaji pamoja na majuma 2 ya mitihani ya chuo yatatumika kukamilisha ujifunzaji na ufundishaji wa kozi hii.
Maelezo ya msingi juu ya kozi hii
Kozi hii inalenga kutoa taaluma kunt‘u juu ya riwaya ya kiswahili kwa kuangazia chanzo na maendeleo ya riwaya sambamba na ufafanuzi wa vipera vyake. Vilevile inajadili athari zitokanazo na kuwepo kwa riwaya ndani ya jamii, mwisho, inaangazia vijenzi muhimu katika masimulizi ya kubuni.
Malengo ya kozi
Kozi hii itawawezesha wanafunzi kuuchunguza na kuutathmini muundo wa nje na wa ndani wa taaluma nzima ya riwaya ya kiswahili na riwaya zenyewe za kiswahili.
MUHTASARI WA KOZI
1. Nadharia ya riwaya:
· Dhana ya riwaya
· Historia ya chimbuko la riwaya
o Riwaya na matapo ya fasihi
o Dhana ya ubunilizi katika riwaya
o Muundo wa riwaya
o Mikondo (aina) kuu za riwaya
2. Riwaya ya kiswahili
· Maana ya riwaya ya Kiswahili
· Historia ya riwaya ya Kiswahilio Kabla ya uhuruo Baada ya uhuru
o Kipindi cha kuanzia miaka ya 1980
o Baada ya kutamalaki kwa zama za sayansi ya teknolojia
· Maendeleo ya riwaya ya Kiswahili (Sababu za kuibuka, kukua na keenea ama kudumaa kwa riwaya ya Kiswahili).
· Wanariwaya maarufu wa riwaya ya Kiswahili
3. Mbinu za kifani zinazotumika katika ujenzi wa riwaya za Kiswahili
o Naratolojia (Usimulizi, mwendo)
o Msuko wa vitushi na motifu zake
o Uhusika na wahusika
o Mtagusano wa kifasihi
o Matumizi ya lugha
o Mianzo na miisho ya kifomula
4. Mitazamo na mielekeo inayojichomoza katika riwaya za Kiswahili
o Dhana ya usomaji wa riwaya za Kiswahili (maana, hadhi matatizo)o Uhai au ufu wa riwaya za Kiswahilio Mawazo yaliyotamalaki katika riwaya ya Kiswahili katika mapito yakeo Masuala mtambuka katika riwaya za Kiswahilio Tathmini ya mchango wa riwaya ya Kiswahili kwa ustawi wa waswahili
5. Uhakiki wa riwaya Teule za Kiswahili
o Dhana ya uhakiki na nadharia za kuhakikia kazi za fasihi
o Kuchambua riwaya teule za Kiswahili
o Ulinganuzi na ulinganishi wa vipengele muhimu vya kiuhakiki vijitokezavyo katika riwaya za Kiswahili
Riwaya Teule zitakazoshughulikiwa:
o Nagona
o Kusadikika
o Kasiri ya Mwinyi Fuad
o Mfadhili
o Barua Ndefu kama hiio Mirathi ya Hatari
o Bwana Myombekele na Bibi Bugonoka
o Hofuo Pesa zako zinanuka
o Mzimu wa watu wakale
Namna ya Ufundishaji:
Mihadhara na Mijadala.
Saa za Ufundishaji:
Jumla ya saa 45, saa 30 za Mihadhara na 15 za Mijadala.
Upimaji:
Alama za Tamrini 40% na Mitihani ya mwisho 60%.
MATINI ILIYOTUMIKA
Nadharia ya Riwaya
Kumekuwa na misuguano kadhaa kutoka kwa wanazuoni waliothubutu kutoa fasili ya riwaya. Imeonekana wazi kuwa kunakukubaliana kwa baadhi ya masuala na kutofautiana pia katika kutoa fasili hii. Miongoni mwa masuala yaliyopelekea misuguano katika utoaji wa fasili hii ni pamoja na:o Dhima / maudhui ya riwayao Mipaka ya riwaya pindi inapohusishwa na hadithi fupi au novelao Ukubwa / urefu wa riwayao Aina za riwaya
Kuna wengine huchanganya utanzu wa riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari (yaani, vile vitumiavyo lugha ya mjazo) kama vile Hadithi fupi, Novela, Tawasifu na Wasifu.
Hadithi fupi
Tofauti yake na riwaya hujikita katika upeo na uchangamani. Hii inamaana kuwa hadithi fupi huwa sahili sana ilihali riwaya huwa imetanza zaidi.
Novela
Hii huwa ni changamani zaidi kuliko hadithi fupi. Huweza kuwa na visa vingi kiasi kulinganisha na hadithi fupi.
Tawasifu
Ni utungo utumiao lugha ya mjazo ukisimulia habari za mtunzi mwenyewe.
Wasifu
Ni utungo utumiao lugha ya mjazo ambapo mtunzi husimulia habari za mtu mwingine.
Ukichunguza kwa makini vijitanzu hivyo utaona kuwa vinatofautiana na riwaya katika vigezo vya: urefu, uchangamani, idadi ya wahusika, lugha, vitushi, U―Kina, dhamira n.k.
Hivyo, mtu anayetaka kuifasili dhana ya riwaya hupaswa kumakinika katika vipengele hivyo.
Maswali ya msingi
1. Wanazuoni mbalimbali wametoa fasili ya riwaya. Eleza fasili hizo.
2. Kwa nini fasili zao zimetofautiana?
3. Je, wewe unadhani riwaya ni nini?
4. Eleza tofauti ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari.
5. Unadhani tofauti hizo kati ya riwaya na vijitanzu vingine vya kinathari zinasababishwa na nini?
Sifa bainifu za riwaya
Ilinganishwapo na tanzu nyingine, riwaya huwa nasifa bainifu zifuatazo:
o Kutokufungwa na sheria nyingi (kinyume na makumbo mengine ya tamthiliya na ushairi).
o Matumizi ya lugha ya kinathari.
o Kuwa na mawanda mapana katika urefu na kina.o Ni zao halisi la kibepari.
o Kuwa na uhalisi kwa kiasi kikubwa.
o Mahitaji ya kusoma na kuandika.
o Kuwepo kwa maisha na makazi yenye utulivu.
o Kuwa na uwezo wa kugusia hadi vitu vionekanavyo kama vidogo (kwa maelezo zaidi, tazama. Madumulla, 2009).
Miega ya Riwaya
Mwega ni nguzo au kiunzi kitumikacho kushikilia jambo / kitu. Kama ilivyo kwa kila kazi ya fasihi, riwaya yoyote lazima ijiegemeze katika miega au nguzo tatu muhimu za muktadha, fani na maudhui. Miega hiyo huishikilia vema riwaya katika uundwaji pamoja na utumiwaji (usomaji na uhakiki) wake. Miega yenyewe ni hii ifuatayo:
Muktadha
Muktadha ni kitu cha lazima katika kila riwaya kwasababu ndiyo huipa uhai riwaya yoyote. Riwaya yoyote hutokana na muktadha fulani au mseto wa miktadha kadhaa. Aghalabu, miega mingi ya fani na maudhui hujengwa kutoka katika nguzo hii. Hivyo, ni lazima riwaya iiakisi miktadha hiyo. Aghalabu, ni nadra sana kukuta riwaya imejikita katika muktadha wa namna moja pekee. Kwa hiyo, riwaya nyingi ni zao la mseto wa miktadha ambayo mtunzi huipitia.
Tanbihi: dhana hii ya muktadha ni vema ikachukuliwa kwa upana wake. Wengi huifinya kwa kuinasibisha na mazingira ya kijiografia (mandhari) pekee! Miktadha yaweza kuwa ya:o Taarifa za msingi zinazomuhusu mtunzi (kuzaliwa, kazi, elimu n.k)o Jografia (mandhari) ya maisha na mapitoo Historia ya mapito yake / jamii yake (matukio muhimu yaliyomgusa yeye au jamii yake)o Utamadunio Uchumi n.k.
MAUDHUI
Nayo ni nguzo muhimu sana. Bila maudhui, hakuna riwaya. Hivyo, kila riwaya iliyosanwa vema lazima iwe na mwega huu. Ndani ya maudhui kuna mambo muhimu matatu ambayo ni: ujumbe, dhamira na vipopo vya fikra.
Dhamira
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa dhamira muhimu zipo 4: nazo ni: kuburudisha, kuhifadhi amali na historia, kuelimisha na kupambana na maovu / madhila yaikumbayo au yatakayoikumba jamii.
Vipopo vya Fikra
Vipopo vya fikra au vitumba vya mawazo ni mawazo yajengekayo katika akili ya msomaji au mhakiki kutokana na vitushi vya riwaya, aghalabu, hutokana na utambuzi wake binafsi kuhusu mambo mbalimbali au tajiriba. Wengine huviita dhamira ndogo ndogo. Mara nyingine, vipopo vya fikra siyo lazima vijioneshe moja kwa moja riwayani. Bali, msomaji au mhakiki huweza kujiwa navyo tu kadri asomavyo riwaya huku akihusisha na utambuzi wake binafsi au tajiriba.
Ujumbe
Haya ni mavuno ayapatayo msomaji kutokana na dhamira au vipopo vya fikra. Pia, si lazima ujumbe aupatao msomaji au mhakiki ulandane na kile alichokikusudia msanii. Hii ni kwasababu, msomaji au mhakiki huweza kujenga maana ya akisomacho kutokana na kuhusisha na mazoea na utambuzi wake binafsi.
FANI
Huhusisha vipengele vitengenezavyo umbo na sura ya riwaya (mjengeko na ladha ya riwaya). Vipengele hivyo viko katika makundi mawili ya: Muundo na Ubunilizi.
Dhana ya Muundo katika Riwaya
Hii hurejelea mjengo wa kazi yenyewe. Hujumuisha vipengele mbalimbali ambavyo huiweka kazi katika umbo na muundo husika. Muundo wa kazi ya mwandishi wategemea zaidi kanuni asilia za kazi husika pamoja na jamii aiandikiayo. Ili kupata mjengeko autakao katika kazi yake, msanii hutumia mbinu mbalimbali. Mbinu hizo huhusisha vipengele kama vile:
i. Mtindo
ii. Lugha
iii. Vitushi
vi. Migogoro
v. Udhamira
vi. Muwalai
vi. Wahusika
vii Mandhariv.
Ushikamani
Mitindo mbalimbali ya utunzi na uandishi hutokana na athari malimbali za jamii ambayo mtunzi amekulia au vionjo binafsi vya mtunzi.Kipengele kingine katika suala la mtindo ni matumizi ya nafsi. Dhana hii ya matumizi ya nafsi hurejelea matumizi ya midomo ya wahusika katika kufikisha mwazo yake. Waandishi wengi hupendelea nafsi I na ya III. Nafsi II haitumiki kwa sababu humrejelea msomaji. Hivyo, waandishi huepuka kumchoma na kumchusha msomaji. Nafsi I na III zina uhuru wa kuzitumia kwa sababu hujiweka mbali na athari zozote zimwelekeazo msomaji. Suala la nafsi ni muhimu sana katika uandishi. Kwa jumla, mbinu za kimuundo ni kipengele cha lazima cha mwega huu wa fani. Kamwe, hakiwezi kukosekana katika kazi husika na kazi hiyo ikabaki kuwa katika utanzu husika. Kipengele hiki ni tofauti na kipengele cha mbinu za kibunilizi.
Dhana ya Ubunilizi katika RiwayaRiwaya, pamoja na kazi za tanzu nyingine kama vile nudhumu na tamthiliya ni kazi za kibunilizi. Neno Ubunilizi au Ubunifu linatokana na kitenzi buni. Kubuni ni kuunda jambo. Aghalabu, jambo hilo huwa katika hali ya kidhahania kabla halijaonekana au halijadhihirika kwa hadhira kupitia ogani za fahamu. Hivyo, kwa jumla, twaweza kusema kuwa ubunilizi ni uwazaji na uundaji wa wazo katika hali inayohalisika. Dhana ya ubunilizi hutusaidia kutofautisha fasihi na matukio halisi maishani. Fasihi si maisha halisi bali ni tokeo la ubunifu wa mtunzi yaani, mtunzi ana uwezo wa kubuni visa na wahusika wake kwa njia ambayo haikanganyi hali halisi ya maisha. Mambo muhimu yamwezeshayo mtu kutunga kazi bunilizi ni:
o Silika / karama / kipawa
o Uwezo wa kiutafiti
o Uzoefu
o Mawazo au fikra (taaluma)
o Nia, lengo au azma
Misingi hii yatudokezea na kutusaidia kujibu swali la msingi tupaswalo kujiuliza tuifikiriapo kazi fulani ya kibunilizi na kuichukulia kuwa bora/nzuri ni: je, kazi hiyo ni tokeo/zao la msingi ya kitaaluma? Au silika (kipawa/karama)? Au tajiriba (uzoefu wa kimaisha)? Au ni tokeo la mseto wa vipengele hivyo vyote? Au ni tokeo la mseto wa baadhi ya vipengele hivyo?
Ubunifu wa riwaya na bunilizi za tanzu nyingine lazima uongozwe na kaida mbalimbali za hali halisi ya maisha. Mtunzi anapaswa kuufanya ulimwengu wake wa kubuni kuwa picha halisi ya maisha katika ukamilifu na ukweli wake. Uhalisia ni ukweli wa jambo kama lilivyo au linavyofahamika. Kuna ukweli wa aina 2 ambazo ni:
o Ukweli katika hali halisi (uhalisi na uasilia wa jambo/kitu).
o Ukweli wa kisanaa (husawiri mambo yaliyobuniwa na mtunzi).Hivyo, ubunilizi ni utengenezaji wa ukweli wa jambo kadri afikiriavyo na akusudiavyo msanii. Kwa jumla, msanii hufanya ubunilizi kwa kuzingatia vigezo muhimu vinne. Hivi ni:
o Kaida za jamii (yake au anayoiandikia)
o Uwezekano wa utokeaji wa jambo husika
o Azma au lengo (hisia? ufunuo? kujibu?)
o Hadhira
Yafaa ubunilizi usipitilize, kwani ni rahisi kwenda mbali na jamii halisi inayoandikiwa. Hata hivyo, ifahamike kuwa kumtaka mtunzi afuate kaida fulani si kumnyima uhuru wa ubunifu. Kama mtunzi atakanganya hali halisi ya maisha kama mbinu yake ya kutunga, basi na tumpe uhuru huo ilimradi kazi yake twaielewa kwa mtizamo huo. Kazi yoyote ya kisanaa lazima iwe na vipengele muhimu vya aina/makundi mawili. Haya ni: vipengele vya kimuundo na vipengele vya kibunilizi.
Vipengele vya kimuundoHivi ni vile vinavyoifanya kazi husika iwe katika utanzu au kumbo husika. Kila utanzu una aina na namna zake za vipengele vya kimuundo. Vipengele hivyo ndivyo huwa nguzo―msingi zishikiliazo tanzu husika. Kazi fulani hujulikana kuwa ni aina ama shairi, utenzi, utendi, hadithi, fupi, riwaya au tamthiliya kutokana na vipengele hivi. Vipengele vya kimuundo hutegemeana na utanzu husika. Hata hivyo, aghalabu, huhusisha vipengele kama vile: vitushi, uhusika na wahusika, ushikamani, lugha, muwala na mandhari.
Vipengele vya kibuniliziNi jumla ya mambo ambayo mtunzi huyabuni na kuyaingiza au kuyatumia katika kazi zake ili ilete mvuto na mnato kwa hadhira. Mbinu hizi huakisi kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi na kumtofautisha na watunzi wengine. Hii ni kwa sababu, kupitia mbinu hizo, kazi hubeba vionjo tofauti (hata kama kazi hizo tofauti zinazungumzia jambo au mada inayofanana, lazima zitatofautiana kutokana na matumizi ya mbinu tofauti za kibunilizi). Vipengele vya kibunilizi vitumiwavyo sana na watunzi wa riwaya za Kiswahili ni:
i. Taharuki
ii. Kisengerenyuma
iii. Utomeleaji
vi.Ufumbaji
v. Ritifaa
vi.Usawiri wa wahusikai
vii. Dayolojia
viii. Utanzia
xi. Ujadi
x. Ufutuhi
Taharuki Ni hali ya kuwa na dukuduku la kutaka kujua juu ya nini kitafuatia katika usimulizi wa kazi ya fasihi. Mtunzi huijengea hamu hadhira yake ya kutaka kujua zaidi. Mbinu hii hutumiwa sana/hujitokeza sana katika kazi za fasihi pendwa. Hujitokeza pia katika fasihi nenwa. Taharuki, katika kazi za fasihi simulizi hujengwa kwa kutumia:
o Mabadiliko ya lugha―uso/sura
o Vipashio vya fonolojia arudhi
o MatendoNa, katika fasihi andishi, taharuki hujengwa kwa kutumia:
o Mbinu nyingine za kibunilizi k.v. kisengerenyuma
o Utumizi wa wahusika wa ajabu―ajabu
o Mandhari ya ajabuajabu
Kisengerenyuma Ni namna ya kupangilia vitushi au kusimulia kwa kuanza na tukio―tokeo kisha kufuatia tukio―chanzi. Watunzi huitumia kwa namna tofautitofauti. Mbinu hii pia husaidia sana kuboresha hamu ya hadhira kutaka kujua muundo wa vitushi vya kazi husika.
UtomeleajiHujulikana pia kama mwingiliano wa tanzu. Ni kitendo cha kuchopeka/kuingiza vipande vya utanzu mwingine (ulio tofauti na utanzu ushughulikiwao) na katika utanzu mkuu ambao mtunzi anautunga. Kwa mfano, mtunzi wa hadithi fupi huweza kuchopeka mashairi/tenzi au barua katika kazi yake kuu. Utanzu wa nathari huongoza kwa uhuru wa kufanya utomelezi ulinganishwapo na tanzu nyingine. Mbinu hii huwa na tija zifuatazo:
o Kuonesha umbuji wa tanzu hizo
o Kuimarisha maudhui
o Kuondoa uchovu kwa wasomaji
o Kuweka msisitizo
o Kujikaribisha na uhalisi (senkoro, 2011:70―71).
UfumbajiNi utumiaji wa kauli zenye maana fiche. Kauli hizo huwa na maana iliyo kinyume au tofauti na umbo la nje la kazi au matini husika. Ufumbaji huweza kujitokeza katika: Anuani/mada/kichwa cha habari, majina ya wahusika, Aya, Sura ya kazi, kazi nzima n.k. tija zake ni:
o Kuonesha umbuji wa kisanaao Kuishirikisha hadhira kwa karibu
o Kujitanibu na ghasia za kufuatwa―fuatwa na mkono wa dola.
UjadiHuu ni utumiaji wa kauli, matendo au mazingira ya asili yanayofungamana sana na jamii inayoandikiwa. Aghalabu, ujadi hujumuisha:o Kauli kama vile methali, nahau, vipengele mbalimbali vya kimazungumzo ambavyo hutumiwa sana na jamii husika.o Matambikoo Vyakula asiliao Watunzi hufanya hivyo ili kujiweka karibu na hadhira yao.o Yaani, hadhira hujiona iko karibu sana na kazi husika waonapo baadhi ya vipengele vya usimulizi na kiutendaji vya kijadi wavitumiavyo kila siku vimetumiwa katika kazi fulani ya fasihi.
o Pengine, husaidia kuongeza au kupanua hadhira.
DayalojiaHii ni mbinu ambayo mtunzi hutumia kauli za majibizano katika kuwasilisha mawazo yake. Hutumia vinywa vya wahusika wake kudokeza maudhui ayalengayo. Katika baadhi ya tanzu, dayalojia huwa ni kipengele cha kimuundo (kwa mfano, tamthiliya dayalojia ndiyo kijenzi cha msingi cha utanzu huu husika). Na kwa tanzu nyingine hujitokeza kama kipengele cha kibunilizi. Tija zake ni:
o Huondoa uchovu kwa wasomaji
o Huonesha ufundi wa mtunzi katika matendo, maneno na hadhi ya wahusika.
o Husaidia kuwasilisha mawazo kwa hali ya uasili (mtunzi huwa mbali na uwasilishaji, hadhira hupata ladha ya maudhui kutoka kinywa asilia).
Usawiri wa wahusikaNi kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajenga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana au unaowiana na uhusika wao. Wahusika hutumia mbinu nyingi sana katika kuwasawiri wahusika katika kazi zao. Mbinu hizo ni:
o Majazi: utoaji wa majina kulingana na sifa, tabia au dhima. Kwa mfano, Rosa Mistika (katika Rosa Mistika) na Sulubu (katika Nyota ya Rehema).
o Uzungumzaji nafsi
o Kuzungumza na hadhirao Kuwatumia wahusika wengine (Mhusika 1 kumfafanua mwingine).
o Ulinganifu wa usambamba
o Maelezo (mtunzi kumwelezea mhusika)
RitifaaNi hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye (umbali huo huweza kuwa wa kijiografia au kufariki). Aghalabu, mawazo yasawiriwayo kupitia mbinu ya ritifaa huwa na vionjo vya kihisia sana. (kila mmoja kwa wakati wake achunguze ujitokeaji wa ritifaa katika riwaya zilizoteuliwa kama zilivyoainishwa kweye muktasari wa kozi hii).
UfutuhiNi mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali vizuavyo ucheshi, raha, kicheko au furaha kwa hadhira yake. Vipengele hivyo huweza kujengwa na kejeli, utani, dhihaka, ubeuzi na mizaha. Miongozi mwa tija zake ni:o Kufurahisha hadhirao Kuwaondolea uchovuo Kujikwepesha na nguvu za dolao Kulainisha uwasilishaji wa maudhui yanayochoma au yenye hisia kali (utasifida).
UtanziaMbinu hii ni kinyume cha ufutuhi. Ni mbinu ambayo mtunzi hutumia vipengele mbalimbali vizuavyo huzuni, masikitiko, jitimai na mateso kwa hadhira yake. Vipengele hivyo huweza kujengwa na: mateso, ugumu wa maisha, vifungo, mabaa kama vile njaa, gharika, kimbunga, magonjwa na ulemavu (wa viungo au michakato ya mwili kama vile ugumba na utasa).
HISTORIA YA RIWAYA
Riwaya na Matapo ya Fasihi
Matapo ni vipindi mbalimbali vya kihistoria ambavyo fasihi au sanaa kwa jumla imevipitia. Matapo pia huweza kutafsiriwa kuwa ni mkondo au makundi makuu ya kinadharia ambayo yametawala katika fasihi/sanaa katika nyakati maalumu. sanaa/fasihi imepitia katika mikondo mingi sana. Bali ile mikuu ni minne. Nayo ni:
o Tapo la Urasimi Mkongwe (850 ― 325 K. Y. M)
o Tapo la Urasimi Mpya (1680 ― 1780 B. Y. M)
o Tapo la Ulimbwende (1790 ― 1870 B. Y. M)
o Tapo la Uhalisia (Baada ya utawala wa Malkia Viktoria na Mapinduzi ya viwanda hadi sasa).
Matapo haya yaliingiliana na kukamilisha kwa kiwango kikubwa katika muda wa kuwapo kwake. Hivyo, yawezekana kuwa matapo mawili au zaidi yakatamalaki kwa wakati mmoja.
TAPO LA URASIMI MKONGWE
Dhana ya Urasimi humaanisha mkusanyo wa mikondo ya kifikra au kimtazamo ambayo chanzo chake ni sanaa na utamaduni wa Wayunani na Warumi. Dhana hii ilijiegemeza sana katika usimikwaji wa sheria na taratibu mbalimbali za kuongoza utendekaji wa sanaa/fasihi. Sehemu kubwa ya mawazo yao katika sanaa ilimezwa na nadharia ya MWIGO. waasisi/wadau wakuu wa Urasimi mkongwe ni: Plato na Aristotle
Muhtasari wa Mawazo ya Plato Kuhusu Sanaa
o Uhusiano baina ya uwezo wa mshairi na nguvu za Mungu. Anaamini kuwa msanii ni kiumbe kitakatifu ambach
o hupokea mawazo maalumu/ufunuo kutoka kwa Mungu ili afikishe ujumbe kwa hadhira.
o Uwezo wa msanii hautokani na hekima zake, bali jazba na mpagao utokao kwa Mungu.
o Muigo si chochote, kwani msanii huigiza uhalisia wa maisha ambao hata yeye mwenyewe haujui.
o Alitoa sheria muhimu zilizopaswa kuimiliki sanaa ya utungaji mashairi (wasanii wote walipaswa kuzifuata). Sheria hizo ni:
o Kazi yoyote ya ushairi lazima ipitiwe na kamati maalumu ya watu wenye umri wa zaidi ya miaka 50.
o Watunga mashairi wote lazima watimize miaka 50.
o Ushairi lazima ueleze mazuri tu (kama vile juu ya mashujaa na watawala wa nchi).
o Washairi wasitunge chochote kilicho kinyume cha sheria za Jamhuri. (Rejea kitabu chake, The Laws)
Muhtasari wa Mawazo ya Aristotle juu ya Sanaa
o Kuhusu Ushairi na Tamthiliya (sanaa): Mwigo/uwakilishi ni nadharia bora. Kulingana na Aristotle, mwigo ni kiwakilishi cha maisha (uhalisi), maisha yenyewe halisi. Mwigo hupunguza au kuondoa madhara yatokanayo na woga au hasira.
o Kuhusu Hadhira: Sanaa iwe na hadhira mbili ambazo ni: Hadhira ya watu wa nasaba bora (Tanzia) na Hadhira ya watu wa nasaba duni (Futui). Tanzia: kwa mujibu wa Aristotle, ni masuala tata yenye kusikitisha na kufikirisha. Futuhi: ni masuala mepesi na yanayochekesha. Watu duni wapewe haya kwa vile akili yao haiwezi kuchambua mambo.
o Kuhusu Muundo mahususi: Sehemu za kazi ya sanaa sharti zioane/ziwiane. Kazi ya sanaa iwe na sehemu 3 ambazo ni kichwa, kiwiliwili na miguu. Miundo hii itofautiane kulingana na aina ya kazi (kama ni tanzia au futuhi). Alisisitiza kuwapo kwa nguzo muhimu katika sanaa (tamthiliya).
Nazo ni:
ü Muundo/msuko
ü Wahusika
ü Nyimbo
ü Wazo kuu (maudhui)
ü Hadhira
ü Lugha bora kulingana na hadhira
oKuhusu Historian na ukweli katika sanaa: Sanaa ni mwigo au kiwakilisho cha ukweli na uhalisia wa maisha ya jamii. Hivyo, mwanasanaa huelezea historia kupitia sanaa. Huweza kuweka mipaka ya historia iliyopita na iliyopo. Pia huweza kuvuka mawanda ya uhalisia uliopita na uliopo. Hivyo akasema Sanaa ni halisi kuliko uhalisi wenyewe. Na ina ukweli zaidi kuliko ukweli wenyewe.
Vigezo vya Jumla vya Tapo la Urasimi
o Kuwapo kwa fani mahsusi
o Kuoana kwa fani na lengo/maudhui ya kazi ya sanaa (ulinganifu)
o Kueleweka kwa kazi ya sanaa (urahisi)
o Kutiliwa maanani kwa muundo na mpango mahususi
o Mtindo mahsusio Kuheshimu jadi
o Kutotawaliwa na jazba (msanii aitawale jazba).
TAPO LA URASIMI MPYABaadhi ya wadau wake ni: Donne, Market, Herrick, Hrbvert, Cowley, Vongham, Crasha na wengine wengi.
Mambo ya Msingi Kuhusu Tapo hili ni:
o Lilizingatia kigezo cha Mantiki na Mjadala katika kazi za sanaa (mashairi)
o Kazi za sanaa lazima ziwe na fumbo litakalomfikirisha msomaji (hadhira)
o Sanaa lazima iwe kwa ajili ya watu.
Wadau wa tapo hili walimchukulia binadamu kuwa ni kiumbe mwenye kasoro asotimia; ambaye alitakiwa arekebishwe na kazi za fasihi/sanaa. Hivyo, kufaulu au kushindwa kwa kazi ya fasihi/sanaa kupimwe kulingana na kufaulu au kushindwa kwake kumzingatia/kumtumikia mtu. Yaani, sanaa lazima imfurahishe, imsahihishe na imwelimishe mtu katika maisha yake.
o Kuwapo kwa Mpango mahsusi katika kazi ya sanaa.
o Kuzingatiwa kwa sheria za utungaji kulingana na aina ya utanzu.
Athari za Tapo la Urasimi Mpya katika Sanaa ya sasa
o Uteuzi mahsusi wa maneno na tungo/mishororoo Umuhimu wa taswira katika ushairio Matumizi ya akili kuliko jazba (hasa wakati wa utungaji wa kazi za fasihi)
TAPO LA ULIMBWENDELilishamiri barani Ulaya mnamo karne ya 18 hadi 19. Lilitokana na msisimko wa kifasihi, kifalsafa, kidini, kisiasa na kisanaa kutokana na Urasimi mpya. Wadau maarufu wa Tapo hili ni:
o Uingereza, walikuwa: William Wordsmith na George Grabbe
o Ujerumani, walikuwa: Goethe, Holderline na Schiller
o Ufaransa: Victor Hugo
o Italia: Novalis
Mambo ya Msingi kuhusu Tapo hili:
o Sifa yake kuu ni uhuru wa msanii. Msanii alipata uhuru wa kuchagua mada, hadhira na lugha kwa matakwa yake. Mambo ya kufikirika kama vile mambo ya ndoto/ruya yalianza kuandikwa.
o Pia wahusika wa ajabuajabu walianza kutumika kwa mfano, shetani na jangili.o Lilizingatia hisia za ndani pamoja na mazingira ya mzungukayo mtu huyo.
o Tapo hili lilielezea maisha jinsi wao (watunzi) walivyotaka yawe.Kuzuka kwa tapo hili kulichangizwa na kuwapo kwa mambo kadhaa ambayo yalisababisha msisimko na athari za maisha ya wakati huo. Mambo hayo ni:
o Safari za kuvumbua ulimwengu
o Harakati za USA kudai uhuru wakati huo
o Kuzuka kwa miji na viwanda kwa haraka
o Ulinganishi wa nguvu za kisilaha na kisiasa baina ya mataifa mbalimbali
o Mivutano na harakati za kitabaka.
Vigezo vya Jumla vya wana―Ulimbwende ni:
o Kutilia mkazo mazingira na asili
o Kuandika/kusana kazi mbalimbali zilizowazungumzia wahusika kuanzia utoto waoo Matumizi ya wahusika wa ajabuajabu kama vile shetani, jangili, wavunja sheria, Malaya n.k.
o Kuruhusu matumizi ya ndoto zilizovuka mipaka ya uhalisi wa maisha. Hii iliruhusiwa ili kurekebisha matumizi ya fani na maudhui katika utunzi.
o Kupinga sheria zilizowekwa na Wanaurasimi: kama vile: Kutenga hadhira, kutenga mitindo ya lugha kulingana na matabaka ya hadhira na kutenga baadhi ya wahusika kulingana na nasaba.
TAPO LA UHALISIA
Uhalisia ni sawa kabisa na udodosi―mambo ambapo huwa na uzingatiaji mkubwa wa uhalisi katika kuwasilisha uhalisi huo katika fasihi. Lilielezea maisha kwa jinsi yalivyo, yaani jambo lilielezwa kwa undani na kweli. Miongoni mwa waasisi wake ni Hegel. Mazingira na wahusika walisawiri kikwelikweli kuyaakisi maisha ya kila siku (kwa kuzingatia furaha, huzuni, matumaini, matazamio na matatizo)Lilishamiri katika karne ya 20. Tapo hili lilijihusisha sana na riwaya.
Mambo yaliyochochea kuzuka kwa Tapo hili
o Maendeleo ya sayansi na teknolojia
o Kuwepo kwa silaha kali na mapigano
o Mivutano au migogoro kati ya matajiri na maskini duniani kote
o Vuguvugu la nchi nyingine kudai uhuru
Vigezo vya Tapo la Uhalisia
o Demokrasia katika uumbaji wa fani na maudhui ya kazi ya fasihi
o Usawiri mwanana wa mambo yanayotokea kila siku katika maisha ya watu.
o Kuijua kwa kina dhana ya MWIGO. Mwanauhalisia lazima ajue jinsi ya kuiga na akijue akiigacho. Kwa kufanya hivyo, itasaidia nafasi kati ya kiingwacho na mwigo kutokuwa kubwa.
o Kutofungwa na ulazima wa kuwa na mpangilio wala muundo maalum katika kazi za sanaa. Hii ni kwa sababu maisha hayana muundo wala mpangilio maalum.
o Msanii azingatie athari za kazi yake katika hadhira yake.
o Athari hizo zaweza kuletwa na mambo kama vile urahisi (au usahili katika usanaji), umoja kwa moja katika kufafanua maudhui na usahihi wa mambo.
o Kazi yoyote ya fasihi lazima iwe na jukumu la kuadilisha na kufunza.
Aina za uhalisia
1. Uhalisia wa Kibwanyenye
2. Uhalisia wa Kihakiki
3. Uhalisia wa Kijamaa
4. Uhalisia Ajabu
Uhalisia wa Kibwanyenye
Waandishi wake huandika na kusawiri uozo wakati wa ubwanyenye. Hata hivyo, hawatoi masuluhisho ya kisayansi kuhusu migogoro iliyomo katika jamii.
Uhalisia wa Kihakiki
Mawanda yake hayaivuki jamii husika. Huihakiki jamii hiyo husika tu. Huchambua mambo ya jamii kwa namna moja, kwandani tu au kwa nje tu.
Uhalisia wa Kijamaa
Huchambua mambo ya jamii kutoka ndani na nje ya jamii. Humchambua mhusika kwa kumhusisha na nguvu mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa.
Uhalisia Ajabu
Wengine huuita uhalisia mazingaombwe. Huchanganya uhalisia na mambo ya ajabuajabu. Uajabu―ajabu hapa unarejelea matumizi ya wahusika, mandhari na hata vitushi vilivyo nje ya hali ya kawaida. Mfano mmojawapo wa kazi iliyo katika kijitapo hiki ni Baba alipofufuka, utata wa 9/12, Nagona n.k.
|
|
|
SHAIRI: MAMA WA NYUMBANI |
Posted by: MwlMaeda - 09-16-2021, 07:40 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
MAMA WA NYUMBANI
Cheo hiki sikitaki,
Kuwa mama wa nyumbani,
Tena nasema sitaki,
Kaumu sikilizeni,
Eti chini sijiweki,
Kutwa nipo sumbukoni,
Sitaki!
Cheo kisicho heshima,
Wenzangu wananihizi,
Ndio Mana nalalama,
Nafasi hii kuhozi,
Na Sasa kazi naigoma,
Kufanya tena siwezi,
Sitaki!
Kazi isiyo malipo,
Hainipi afueni,
Ningeokota makopo,
Nondoke umasikini,
Hivi Sasa niponipo,
Mafaufu magauni,
Sitaki!
Nipike nioshe vyombo,
Kisha nguo nizifue,
Wala siishiwi mambo,
Eti sema nipumue,
Kazi napiga kikumbo,
Nyingine nijifanyie,
Sitaki!
Wakirudi makazini,
Hawana adabu katu,
Hujiona wathamani,
Nami wanione fyatu,
Wasemavyo Nina nini,
Jamani huo ndo utu?
Sitaki!
Maisha yangu ni duni,
Zangu shida haziishi,
Mie nakosa sabuni,
Mavazi pia marashi,
Kucha kutwa sumbukoni,
Hivi kazi hazinishi,
Sitaki!
Shairi ninalifunga,
Mie mama wa nyumbani,
Safari ninaipanga,
Kubadilisha sidhani,
Mechoka kutangatanga,
Hizi kazi za nyumbani,
Sitaki!
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: ZAMU YETU BADO |
Posted by: MwlMaeda - 09-16-2021, 04:24 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
ZAMU YETU BADO
Nasibu sio awamu, ilivyokuwa ghafla,
Sasa tunangoja zamu, kuushika utawala,
Na hapo ndipo patamu, kushindwa semeni wala,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Miaka imesalia, michache muimaizi,
Umoja wetu sawia, tuujenge tusihizi,
Kiti kuking'ang'ania, wasemaje hatuwezi?
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Samia tunamtaka, imbeni tena imbeni,
Naye hatuna mashaka, wacha abaki kitini,
Hatuwezi kubanduka, wanawake simameni,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Limelia la mgambo, vita hivi tupigeni,
Walitupiga vikumbo, tukabaki Kama nyani,
Duniani Kuna mambo, nafasi hiyo shikeni,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Tunataka kampeni, vijiji na vitongoji,
mwendo mmoja nchini, wa mijini na majiji,
Tunarejea kitini, na walidhani hatuji,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Asitokee mmoja, kusema yeye hawezi,
Na pasiwe ngojangoja, tumepata mtetezi,
Sasa tumpe pambaja, aliye wetu mlezi,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Wakati ukiwadia, wakutafuta Raisi,
Sisi tunaye Samia, kutushinda si rahisi,
Kura tutawakombea, tusiwe na wasiwasi,
Ni imara Wana wanawake, twendeni kushika dola.
Tunaomba CCM, Samia huyo tupeni,
Hili ni jambo muhimu, nasema mrudisheni,
Sasa tutimize zamu, Wana'ke kuwa kitini,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Tuondoa tofauti, chama na zetu imani,
Tuipange mikakati, siye kutinga ngomeni,
Ni mipango madhubuti, mafarakano acheni,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Tuunganeni wa bara, pamwe huko visiwani,
Sisi ni jeshi imara, wingi wetu hamuoni?
Tukijaza zetu kura, atushinde mtu gani?
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Beti kadha nimegonga, nasihi tuunganeni,
Yetu mambo kuyapanga, Ni jambo lenye thamani,
Wetu umoja kuchunga, awamu kuishikeni,
Ni imara wanawake, twendeni kushika dola.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
SHAIRI: SAFARI YA KILELENI |
Posted by: MwlMaeda - 09-15-2021, 11:07 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
SAFARI YA KILELENI
Ukitaka kwenda juu, ufikie kileleni,
Kwanza shika vichuguu, mawe yaweke pembeni,
Usiheme juu juu, kujichokea mwanzoni,
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Inaweza kuwa ndefu, safari ya kileleni,
Hasa ukiwa dhaifu, utaishia njiani,
Hupaswi kuwa na hofu, yafaa kujiamini,
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Yataka maandalizi, safari si lelemama,
Ule ushibe mchuzi, wali au hata sima,
Tena uwe na pumzi, si kidogo wachutama
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Ngazi ikiwa imara, kuteleza ni muhali,
Siyo ngazi ya kuchora, bali ngazi kwelikweli,
Kama huna ngazi bora, kaa utulie tuli,
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Kamata mawe vizuri, kulia pia kushoto,
Yaegemee vizuri, ili upate fukuto,
Kwa jua la adhuhuri, yatakutunzia joto,
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Mapango yenye vijito, pia yapo safarini,
Maji matamu ya mto, waweza tia kinywani,
Si kwa pesa au vito, yalambe ukitamani,
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Utapata burudani, ukifika kileleni,
Milima yote nchini, ina uzuri wa shani,
Utaona kote chini, kutokea kileleni
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Ili upate pongezi, za mpandaji mzuri,
Katu usilete pozi, uonyeshe uhodari
Hutopata vizuizi, njia ukiikariri
Kufika juu ni kazi, yataka imara ngazi.
Shaaban Mwinyikayoka
(Mwanaupwa)
Iringa
|
|
|
UENEAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI |
Posted by: MwlMaeda - 09-14-2021, 06:32 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
UENEAJI WA KAZI ZA FASIHI SIMULIZI
Ueneaji: hii ni dhana inayotumiwa kueleza mojawapo ya nadharia za Fasihi simulizi. Hutumiwa kuelezea uhusiano unaokuwepo kati ya hadithi za jamii mbalimbali. Dhamira ya kimsingi ya nadharia hii ni kuonesha kuwa inawezekana kuwa jamii zinazohusika ziliingiliana kihistoria au kutokana na ukaribu wao wa kijiografia kuingiliana huku kunaweza kuwa msingi wa kuwepo kwa hadithi zinazosimuliwa ambazo zinafanana.
Hii ni nadharia ambayo inaelekea kupinga uwezekano wa hadithi hizo kuwa na vyanzo tofauti kwa mujibu wa wafuasi wa mtazamo huu. Inawezekana tu kuwa jamii moja iliathiri nyingine ambayo inaichukua hadithi ya jamii hiyo na kuingiza kwenye utamaduni wake. Kwa njia hiyo ikaishia kuwa na sifa za utamaduni wa jamii mpya. Kuna visakale viwili tunavyoweza kuvitaja kueleza uhalisi huu.
Mfano wa kwanza ni mugani wa Fumo Liyongo. Mugani huu unapatikana katika jamii kadhaa za pwani ya Kenya kama Waswahili, Wapokomo, Wabajuni, n.k. inawezekana kuwa kupatikana huku ni matokeo ya ueneaji, hasa kwa kuwa hizi ni jamii zinazokaribiana kijiografia na zilizohusiana kihistoria. Mfano wa pili unahusu shujaa wa jamii ya Wahaya anayeitwa Magasha. Kisakale chake kinapatikana katika jamii kadhaa zilizoko karibu na ziwa Victoria.
Sababu za kuenea kwa Fasihi simulizi - Kuanzishwa kwa vikundi vya sanaa na muziki
Vikundi mbalimbali vya sanaa na muziki vilianzishwa, kazi yake ikiwa ni kuendeleza tanzu mbalimbali za Fasihi simulizi hapa nchini. Vikundi vya sanaa za maonesho, vikundi vya taarabu na muziki vinafanya kazi kubwa ya kueneza Fasihi simulizi hapa nchini. - Mwingiliano na Fasihi andishi
Kuenea kwa kazi ya Fasihi simulizi kwa asili ni kwa mdomo na masikio, yaani usimulizi. Hata hivyo, maendeleo ya watu yamefanya baadhi ya kazi za Fasihi simulizi zienee kwa maandishi. Maandishi ni jitihada ya kuhifadhi kazi ya Fasihi simulizi na kuifikisha mahali ili ikatambwe, iimbwe au isimuliwe. Hadithi mbalimbali kama vile Hekaya za Abunuwas na Hadithi Nyingine (1915), Hadithi za Essopo (1890), Fasihi ya Mtanzania: Hadithi (1977) (TUKI)n.k. zimehifadhiwa na kuenezwa kwa maandishi. Vilevile Fasihi andishi inatumia vipengele mbalimbali vya Fasihi simulizi katika uandishi wao na hivyo kuviendeleza. Vipengele hivyo ni matumizi ya semi mbalimbali, matumizi ya nyimbo, matumizi ya hadithi ndani ya hadithi, matumizi ya mianzo na miishilizo ya hadithi za Fasihi simulizi, matumizi matumizi ya majigambo, utani, n.k. Kwa sasa, methali, vitendawili, nahau vimewekwa katika maandishi kwa ajili ya kumbukumbu za baadaye, na vipengele hivi vinaenezwa kwa njia ya maandishi. - Ufundishaji shuleni na vyuoni
Mfumo wa elimu nchini nao kwa kiasi kikubwa unasaidia kueneza Fasihi simulizi hapa nchini. Kwa sasa, Fasihi simulizi ni somo linalofundishwa kuanzia darasa la kwanza hadi ngazi ya chuo kikuu. Vilevile kuna shule na vyo mbalimbali hapa nchini vinavyofundisha baadhi ya tanzu mbalimbali za Fasihi simulizi kama vile sanaa za maonesho na muziki (chuo cha sanaa Bagamoyo, Butimba, Nyegezi na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam). - Mabadiliko ya kiteknolojia
Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, kwa sasa Fasihi simulizi inaenezwa na vyombo vya habari kama vile redio, televisheni na mitandao. Kwa mfano TBC kupitia vipindi vya “mama na mwana”, “watoto wetu” na “cheichei shangazi” vinasaidia sana kueneza Fasihi simulizi hapa nchini. Katika vipindi hivi, watoto husimuliana hadithi mbalimbali walizopata kusimuliwa, hutegeana vitendawili, humalizia methali na kuimba nyimbo. Televisheni nazo zinasaidia sana kueneza Fasihi simulizi hapa nchini, huonesha michezo mbalimbali ya kuigiza.
Kwa hiyo, mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia hayawezi kuiua Fasihi simulizi, bali Fasihi hii inaendelea kuzihudumia jamii zetu kulingana na mahitaji ya maendeleo ya wakati uliopo na ujao. Maendeleo ya kiteknolojia yanasaidia Fasihi simulizi kuenea na kufika mbali katika muda mfupi zaidi. Kanda za kunasia sauti, redio, televisheni, video na filamu ni vyombo vya kisasa ambavyo vinasaidia kuieneza Fasihi simulizi haraka zaidi kuliko njia ya masimulizi yam domo. - Mwingiliano na mataifa mengine
Hali hii imesaidia kuenea na kupanuka kwa fani za Fasihi simulizi, hasa kipengele cha muziki. Kutokana na mwingiliano huu tumepata muziki wa kizazi kipya (muziki wa kemo) pamoja na Rege. Vijana wa kizazi kipya wamechota miundo na mitindo ya muziki kutoka nje na kuendeleza muziki wao, ingawa maudhui bado wanajadili yaleyale yaliyojadiliwa na wanamuziki wa zamani.
Kwa ufupi, matumizi ya Fasihi simulizi katika sayansi na teknolojia yamesaidia sana kuenea kwa Fasihi simulizi; kwani Fasihi simulizi inapata hadhira kubwa kwa wakati mmoja, lakini hadhira hiyo haionani ana kwa ana na fanani wao kwa kutumia vyombo hivyo vya sayansi na teknolojia.
|
|
|
Mgawanyo wa Kazi Kutokana na Jinsi |
Posted by: MwlMaeda - 09-14-2021, 05:10 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
Maelezo ya Jumla
Katika sehemu hii tunajumuisha maandishi yenye kuonyesha misimamo mbalimbali juu ya swala la wanawake katika nchi nyingine za Afrika, Dunia ya Tatu, na mashirika ya kimataifa yanayosaidia hasa “nchi zinazoendelea”, Tanzania ikiwa mojawapo. Ilibidi tuchague maandishi machache tu kwa vile bibliografia hii inasisitiza zaidi Tanzania. Maswala makuu yanayojadiliwa katika maandishi haya ni mabadiliko ya mgawanyo wa kazi za uzalishaji na uendelezaji wa jamii kutokana na jinsi; hali na nafasi ya wanawake kama wakulima na wafanyakazi, mgawanyo wa kazi duniani na maswala yanayohusu mbinu za utafiti.
Mgawanyo wa Kazi Kutokana na Jinsi
Kihistoria wanawake wa Afrika wamefanya kazi nyingi za uzalishaji wa kilimo pamoja na kazi za kutunza familia au jamii nzima. Uchunguzi uliofanywa na Jeanne Henn (kitomeo 7) unadhihirisha kwamba sehemu mbalimbali za Afrika kabla ya ukoloni zilitofautiana katika mgawanyo wa kazi za kilimo kutokana na jinsi. Tofauti hizo zilitokana na sababu mbalimbali. Baadhi yake ni, aina ya mahusiano ya uzalishaji mali yaliyokuwepo kabla ya ubepari (kwa mfano: mahusiano ya kiumeni yenye msingi wa ukoo, mahusiano ya kikabaila au ya utumwa); mazingira ya ekolojia na mahusiano ya kisiasa na kiitikadi pamoja na mahusiano ya kiuchumi. Kwa hiyo mtu hawezi kutoa tamko sahihi la jumla linalohusu “wanawake katika Afrika”, hasa anapojadili kame zile za kabla ya ukoloni, wakati ambapo jamii za Afrika zilikuwa zinabadilika sana (tz. kitomeo 9).
Uchambuzi wa mgawanyo wa kazi kutokana najinsi unaonyesha kwamba wanawake wa Afrika ni kikundi cha wafanyakazi wanaoajiriwa au wanaofanya kazi kwa mapato madogo sana. Isitoshe, kazi zinazofanywa na wanawake shambani na nyumbani zinawapatia mshahara mdogo na bei ndogo ya mazao. Mshahara wa mfanyakazi haujumuishi hela zote zinazotumiwa kutunza familia. Hali kadhalika bei za mazao (tz. vitomeo 7, 8, 15, 18 vinavyotoa msimamo mbalimbali juu ya tatizo hili).
Wanawake Katika Kazi za Kuajiriwa na Uzalishaji wa Wakulima
Kwa jumla wanawake wanaofanya kazi viwandani wanapewa kazi zile zenye mshahara mdogo, yaani kazi zisizohitaji ufundi wowote, kazi zile “chafu”. Katika wafanyakari wanaoajiriwa kwa muda tu, wanawake ni wengi, na hawapati marupurupu ya wafanyakazi wengine na sheria za haki ya kufanya kazi’ haziwahusu (tz. vitomeo 5, 8, 9 na vingine katika sura zinazofuata). Katika uzalishaji wa kilimo wa kibepari, wanawake wanapewa kari zenye mshahara mdogo zisizohitaji ufundi. Wanawake wakulima wanafanya kazi za kulima mazao ya biashara bila kulipwa. Kwa kawaida wanatakwimu na wanauchumi “hawahesabu” kari hizi au wanaeleza kwamba ni “kazi zinazofanywa na familia, kazi zisizolipwa” (tz. vitomeo 3, 10, 13).
Mgawanyo wa Kazi Duniani
Kazi na mtaji unazidi kutawaliwa na soko la kimataifa na mahitaji yake. Ukweli huu unatusaidia kueleza kwa nini viwanda vingi vya makampuni ya kimataifa vya kutengeneza bidhaa za kuuza nje vimezuka katika nchi za Dunia ya Tatu. Viwanda vinavyoajiri wafanyakazi wengi badala ya kutumia mashine, kwa mfano viwanda vya nguo, ngozi na vyombo vya umeme, vinahamia pale palipo na wafanyakazi wanaoajiriwa kwa mshahara mdogo. Wafanyakazi hawa mara nyingi ni wanawake waliohamia kutafuta kazi (tz. kitomeo 5). Kwa kiasi fulani, sera ya Benki ya Dunia kuhusu Tanzania inatokana na haja ya mabepari wafanya biashara ya kilimo kupata soko kwa kuuza mbolea, dawa za kuua vidudu waharibifu, mbegu na chakula katika nchi za Dunia ya Tatu (tz. kitomeo 20), kama ilivyoelezwa kwa mfano katika Ripoti ya Maendeleo Duniani 1980 (Benki ya Dunia 1980). Msingi mmoja wa ripoti hii ni dhana ya “nafiiu linganishr (comparative advantage). Nchi zinazoendelea zitakuwa na nafuu zaidi zikijenga viwanda vinavyotengeneza bidhaa au vyakula vya kuuza nje badala ya kujenga viwanda vya msingi na kuuza nje bidhaa/vyakula vilivyotayarishwa viwandani kwa mauzo. Dhana hii ya nafuu linganishi inakubaliana moja kwa moja na muundo wa uchumi wa dunia na mgawanyo wa kazi duniani. Inatumiwa kutetea sera zinazojaribu kurekebisha uchumi wa nchi zinazoendelea ili upatane vizuri na muundo wa uchumi wa dunia.
Lakini ukweli ni kwamba sera inayosisitiza biashara na uzalishaji wa biashara za kuuza nje inazifanya nchi zinazoendelea kutegemea zaidi soko la dunia. Pia uchumi unazidi kutawaliwa na matakwa ya mtaji wa kihodhi. Nchi zinazoendelea haziwezi kushindana na soko la dunia la kibepari. Na haziwezi kujenga uchumi unaojitegemea zikiwa bado chini ya uchumi wa soko la dunia. Sera zinazokuzwa na Benki ya Dunia zinapingana na faida ya nchi zinazoendelea na hasa faida ya wakulima na wafanyakazi. kwa mfano, kutokana na hali ilivyo sasa, sera ya kulima mazao ya kuuza nje ni sawasawa na kujiua. Nchi inayouza vyakula vingi duniani ni Marekani. Serikali ya Marekani inatumia chakula kama silaha. Kwa mfano mwaka 1981 serikali ile ilikataa kutoa chakula kwa serikali ya Msumbiji na El Salvador kwa sababu ya sera ya kimapinduzi ya nchi hizo mbili. Hii ingeweza kutokea hapa Tanzania vilevile. Vilevile serikali ikilegeza sheria zinazohusu kusafirisha na kuingiza bidhaa, na ikaachia huru nchi za kigeni kuleta kitega uchumi hapa, uchumi wa nchi ungetawaliwa kabisa na mtaji ulioko nje. Serikali ikipunguza matumizi yake kwenye shule na huduma za afya, huduma hizo zitakufa kabisa, kwa sababu sasa hivi zinapewa hela kidogo sana za matumizi. Isitoshe, sera kama hizo zingeongeza umaskihi wa wananchi kwa jumla; zingekiuka msingi wa serikali za kimapinduzi kama Tanzania, na zingeleta fujo sana ya kisiasa. Kwa hiyo ingawa Benki ya Dunia ina sura ya kuwa shirika la kifedha, ukweli ni kwamba madhumuni yake ni kuimarisha faida ya mtaji wa kihodhi, na hasa wa Marekani.
“Msimamo nafuu” wa Benki ya Dunia unasisitiza haja ya kupunguza umaskini na kukuza maendeleo ya binadamu, yaani afya, lishe, elimu na uzazi. Vipengele hivi vyote havijaendelea sana. Ripoti ya Benki Kuu ya Dunia haikuzingatia kabisa uhusiano uliopo kati ya uenezaji wa ubepari na kuongezeka kwa umaskini, yaani mambo kama ukosefu mkubwa wa chakula bora, vifo vya watoto wengi na uhafifu wa elimu ya shule. Badala-ya kutambua kwamba msingi wa umaskini huo ni ubepari, Benki “inalaumu” ujinga wa maskini na kupendekeza utatuzi wa kiteknolojia, kwa mfano matumizi zaidi ya dawa za kuua mbu, kupunguza malaria (dawa ambazo ni dhahiri zitanunuliwa kutoka kwenye makampuni ya kimataifa). Ripoti inaonyesha wasiwasi mno juu ya jinsi idadi ya watu inavyoongezeka katika nchi zinazoendelea. Kuongezeka kwa idadi ya watu kunahusiana na umaskini na uwezekano wa kuzuka kwa mapinduzi au fujo ya kisiasa. Kwa hiyo Ripoti inasisitiza sana umuhimu wa kuchukua hatua za kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa. Hapohapo, haizingatii mambo muhimu yanayohusiana na swala la idadi ya watoto wanaozaliwa, yaani tatizo la vifo vya watoto wengi wachanga na jinsi wakulima wengi wadogo wanavyowategemea watoto kuongeza uzalishaji wa mazao. Ripoti inataja wanawake katika uzalishaji wa wakulima wadogo, hasa nafasi yao katika kuzalisha vyakula na katika maswala kama elimu, afya, lishe na uwezo wa kuzaa. Aya moja inataja kwamba wanawake, watoto na wakongwe ni “maskini wasiojitegemea?” Maneno haya hayana ukweli na yanatupotosha katika kuelewa nafasi ya wanawake kama wakulima wazalishaji au wafanyakazi katika nchi zinazoendelea.
Takwimu zinazoorodheshwa katika nyongeza ya ripoti ni pamoja na takwimu muhimu juu ya Tanzania, k.m idadi ya watoto wachanga wanaokufa, elimu ya wasichana na wavulana, kiwango cha lishe, cha uzazi, cha uajiri (wanawake kwa wanaume) n.k. Benki ya Dunia ni kituo kikubwa sana cha uchunguzi duniani. Ina uwezo wa kupata data nyingi za siri na inawaajiri wachunguzi wengi. Ingawa wapinzani wa Benki ya Dunia wanapinga mbinu za uchunguzi na sera ya Benki, wanategemea data yake kwa sababu mara nyingi ni data iliyokusanywa hivi karibuni hata kuliko data inayopatikana kwenye nchi zinazoendelea zenyewe.
Sisi tunajadili sana ripoti hii ya Benki ya Dunia kwa sababu hivi sasa Benki hii ina uwezo mkubwa sana wa kuongoza sera za kiuchumi na kisiasa duniani na hasa katika nchi zinazoendelea. Benki inatilia mkazo kwenye nchi “maskini kabisa”, Tanzania ikiwa mojawapo. Katika nchi hizo, inatilia mkazo tabaka maskini kabisa, yaani wakulima maskini, wafanyakazi na watu wa mijini wasio na kazi. Tanzania imekuwa uwanja wao wa majaribio katika mapambano kati ya mtaji wa kihodhi unaotetewa na Benki ya Dunia, na serikali zilizo mstari wa mbele. Sera ya Benki ya Dunia hazitanufaisha wanawake wakulima na wafanyakazi wa Tanzania. Kwa hiyo ni muhimu sana kwa wanawake kutafuta taarifa zaidi juu ya Benki ya Dunia na hasa miradi na mipango yake hapa Tanzania na sera ambazo inazikuza hapa.
Matatizo yanayokabili wanawake wakulima na wafanyakazi yana uhusiano na mgawanyo wa kazi duniani. Jambo hili ni la kimsingi katika majadiliano ya kukataa au kukubali Mpango Mpya wa Uchumi Duniani yanayofanywa huko kwenye Umoja wa Mataifa na penginepo (tz. vitomeo 8, 15, 18). Mkutano wa Dunia juu ya Miaka Kumi ya Wanawake umefanikiwa kuingiza swala la wanawake katika miradi na mbinu za maendeleo. Mapambano haya yamezusha uchunguzi mwingi juu ya wanawake na kazi. Ilionekana kwamba theluthi moja ya wakuu wa familia duniani pote ni wanawake. Jambo hili linadhihirisha mabadiliko makubwa yanayotokea katika mfumo wa familia na uendelezaji wa jamii. Kutokana na uchambuzi huu, wito umetolewa wa kutafuta teknolojia inayopunguza kazi za kilimo, hifadhi na uchukuzi wa mazao na hata utayarishaji wa vyakula pamoja na kuleta maji safi na kutafuta nishati ya aina nyingine (vitomeo 10, na 19). Ukweli kwamba wanawake ndio wazalishaji wakubwa wa chakula na utendaji yanayohusu uhaba wa chakula duniani (tz. kitomeo 19). Mara nyingi tatizo kubwa ni kuwepo kwa dhana ya kwamba kazi za wanawake katika uzalishaji na uendelezaji wajamii hazionekani wazi (tz. vitomeo 11 na 20). Kama kweli hili ndilo tatizo kubwa, kuna haja ya kufanya uchunguzi na kuwaelimisha viongozi juu ya mchango mkubwa wa wanawake katika uzalishaji.
Lakini msimamo huu wa kusisitiza kazi zinazoonekana au zisizoonekana umepotoka. Unaficha hali halisi ya unyonyaji na uonevu wa wanawake wanaofanya kazi ya aina yoyote. Kwa mfano, katika Tanzania kila mtu anajua kwamba wanawake wanapika, wanatunza watoto, wanalima na kukamua ng’ombe na/au wanafanya kazi za kuajiriwa. Lakini watu hawaelewi jinsi kazi hizo zinavyosaidia kushusha thamani ya kifedha ya kazi, ziwe kazi za kilimo au za kuajiriwa; yaani kazi hizo zinashusha mshahara, bei ya mazao na thamani ya njia nyingine za kujipatia maslahi. Tukitaka kuchunguza swala hilo zaidi, lazima tuchunguze mahusiano ya uzalishaji jinsi yanavyotawaliwa na mahusiano ya kibepari. Tumeshataja kwamba makampuni ya kimataifa yanahamia nchi za Afrika kutafuta wafanyakazi wa mshahara mdogo. Wanawake ndio wanaoajiriwa kwa mshahara mdogo kabisa; si hapa Afrika tu, bali ni duniani pote. Jambo kubwa linalozuia wanawake wasifanye kazi za kuajiriwa na wasilime mazao ya biashara ni mahusiano ya kiumeni na mgawanyo wa kazi kutokana na jinsi. Mabepari wanataka kuondoa vikwazo hivi au angalau mabepari wanataka vipengele vingine vya vikwazo hivi ili wazalishe bidhaa zaidi. Vilevile ubepari utanufaika kama mfumo wa kilimo cha kijungumeko, kilimo kinachotegemea sana kazi ya wanawake wakulima, utabatilishwa. Hii ni kwa sababu kadiri wakulima wanavyozidi kulazimishwa kununua mahitaji yao, ndivyo watakavyolazimishwa kuzalisha bidhaa zaidi ili wapatae hela, au watalazimishwa kutafuta kazi ya kuajiriwa. Kwa hiyo ubadilishaji wa kilimo cha kijungumeko unasaidia kujenga uchumi wa bidhaa katika jamii za wakulima. Vilevile unasaidia kuongeza idadi ya watu wasio na kazi na ambao wanaweza kuajiriwa kwa urahisi katika viwanda vya kibepari.
Ni dhahiri kwamba wanawake watanufaika kama mahusiano ya kiumeni yatabadilishwa. Lakini kuna haja ya kuchunguza kwanza mabadiliko yanayotokea sasa katika jamii za Afrika na kuandaa mbinu nzuri za utatuzi. Kama hatufanyi hivyo, “tutakomboa” wanawake wasionewe na mahusiano ya kiumeni lakini waendelee kuonewa na wale wakubwa wenye mashamba makubwa na viwanda; yaani mabepari au serikali yenyewe. Zaidi ya hapo, mtaji hautaki kubadilisha mambo mengine ya mahusiano ya kiumeni, hasa mbinu za kudhibiti wanawake, vijana na watoto.
Mbinu za Utafiti
Makala haya yanasisitiza mbinu za utafiti juu ya wanawake (vitomeo 3, 5, 7, 9, 12, 13, 14). Maswala ya utafiti hayahusu mbinu tu bali yanahusu jinsi tatizo la wanawake linavyoelezwa, hasa kwa kuzingatia hali ya mabadiliko katika jamii. Kwa mfano Ulrike von Buchwald na Ingrid Palmer (kitomeo 3) wanasisitiza umuhimu wa kuchambua jinsi aina ya uzalishaji na uundaji na ukuaji wa tabaka vinavyowaathiri wanawake. Maandishi mengine yanasisitiza mgawanyo wa kazi duniani kama msingi mmoja wa unyonyaji wa wanawake na wafanyakazi (vitomeo 5, 14 na sura zinazofuata). Swala la mgawanyo wa kazi duniani ni swala ambalo linaleta mapambano kati ya wachunguzi (vitomeo 5 na 14). Kutokea kwa maswala haya kunaonyesha haja ya kutunga nadharia inayoweza kuelezea unyonyaji na uonevu wa wanawake. Utafiti unaotoa maelezo ya jinsi hali ilivyo tu hauwezi kufanya hivyo. Vitomeo vingine vinasisitiza haja ya kufanya uchunguzi katika eneo dogo pamoja na uchambuzi badala ya nchi au mkoa mzima. Imeonekana pia vipo vipengele ambavyo ni muhimu sana kwa utafiti wa wanawake (tazama kitomeo 3). Jeanne Henn anajadili umuhimu wa uchunguzi wa kupima muda unaotumiwa kufanya kazi mbalimbali na kuchunguza ulaji kayani. Kwa kutumia takwimu, uchunguzi kama huo unadhihmsha kwamba unyonyaji wa wanawake wakulima upo (kitomeo 7). Kwa mfano, uchunguzi kama huo uliofanywa huko Cameroon (Henn, 1978). Makala nyingine zinapendekeza mada za uchunguzi (vitomeo 3, 5, 9, na 12). Takwimu zilizokusanywa na serikali ya Kenya juu ya elimu ni mfano mzuri wa aina ya uchambuzi wa takwimu unaojitajika katika ufafanuzi wa nafasi tofauti za wanawake na wanaume za kupata huduma mbalimbali kama elimu, afya na ustawi wa jamii.
Ripoti ya Mkutano juu ya Ukandamizaji wa Wanawake ulioandaliwa na IDS (Sussex) unaulizia swala la usambazaji wa matokeo ya taarifa za uchunguzi. Swala hili vilevile linahusu lugha, mawasiliano na mbinu za kupata maoni ya wanawake (na wanaume) wanaoathiriwa na uchunguzi huu. Pendekezo mojawapo ni kutayarisha vijitabu vidogo na maandishi mengine yaliyoandikwa kwa lugha rahisi ili wakulima na wafanyakazi waweze kuvisoma. Uchunguzi wa kushiriki unakuza ushirikiano kamilifu wa wakulima na wafanyakazi katika kufanya utafiti. Ipo mifano mbalimbali ya uchunguzi wa kushiriki katika sura zinazofuata. Uchunguzi huo umechambuliwa na kuhakikiwa katika mapendekezo ya Warsha ya Kanda juu ya Mbinu za Utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Mitaala na Maendeleo. Uchunguzi huo unatumia mtazamo wa uyakinifu wa kihistoria. Mtazamo huo unasisitiza hali halisi ya nchi na kuzingatia hali ilivyo duniani. Watafiti wanaanza kuunga mkono umuhimu wa kuzalisha na kusambaza ujuzi. Uchunguzi na maandishi hayana haja ya kulenga soko la kimataifa na kujibu au kujadili mambo ambayo mashirika ya kimataifa yanafikiri kuwa ni muhimu. Uchunguzi uwahusuo wenyeji na kujishughulisha na siasa ya vijiji, hauna lengo la kushindania “viwango vya kimataifa” vya utaalam. Lakini mtafiti akitilia mkazo anaweza kupata matatizo mengine ya binafsi. Swala linalojadiliwa katika vitomeo 13 na 14 la nani anafanya uchunguzi linaleta hoja kuwa je, uchunguzi unamnufaisha nani? Hakika jibu la swali hili litaonekana katika vitendo vya mchunguzi mwenyewe.
Marejeo
Benki ya Dunia 1980 World Development Report (Ripoti ya Maendeleo Duniani), Washington, D.C.
Jeanne Koopmen Henn 1978 Peasants, Workers and Capital: The Political Economy of Labour and incomes in Cameroons, Harvard University, tasnifu ya Ph.D. isiyochapishwa.
Warsha ya Kanda juu ya Mbinu za Utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Mitaala ya Maendeleo 1981 “Mapendekezo” katika Ripoti ya Warsha iliyotajwa hapo juu na iliyofanyika Usa River, Mkoa wa Arusha, tarehe 30 Machi mpaka tarehe 11 Aprili, 1981. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Mitaala ya Maendeleo.
Bibliografia
1. AAWORD (Association of African Women for Research and Development) (Jumuiya ya Wanawake Waafrika ya Uchunguzi na Maendeleo) bila tarehe, AAWORD, Dakar (B.P. 3186, IDEP, Dakar, Senegal) uk. 28.
Kijitabu hiki kinaeleza sababu za kuanzisha jumuiya ya wanawake Waafrika wachunguzi. Sababu hizo ni pamoja na lengo la maendeleo na ukombozi wa Waafrika na ubatilizaji wa ubaguzi wa jinsi au jamii yoyote. Madhumuni mengine ya AAWORD ni kuimarisha mfumo wa mawasiliano baina ya wanawake wachunguzi wanaojishughulisha oa swala la maendeleo ya Afnka, kukuza uchunguzi unaolenga kuleta mabadiliko kwa vitendo, kuhakiki mbinu za uchunguzi na kukuza uchapidiaji. Mwanamke Mwafrika yeyote anayeunga mkono maleago hayo anaweza kuwa mwanachama wa jumuiya hiyo. Shughuli za AAWORD zinasimamiwa na Baraza Ja Watu Watatu, Kamati ya Uhariri, na Mkutano Mkuu unaofanyika kila baada ya miaka miwili. AAWORD inakuza uchambuzi wa kihistoria na hali halisi ya Afrika na inapinga mwelekeo wa kusisitiza umuhimu wa kuchunguza swala la wanawake. Pia AAWORD inasisitiza umuhimu wa kuchunguza utamaduni na fikra zinazohusu hali ya wanawake, si nyanja za kiuchumi kama ukoloni mamboleo tu. Kutokana na mwelekeo huo, AAWORD inatilia mkazo maswala ya kisheria yanayohusu familia, ndoa, uashiki, elimu na uajiri.
2. BAUMANN, HERMAN 1972 “The Division of Work According to Sex in African Hoe Culture” Africa 1 (3): 289 – 319. (Mgawanyo wa kazi kutokana na Jinsi katika Jamii za Afrika zinazolima kwa Jembe). Makala inatoa hoja kwamba kilimo cha jembe kimegunduliwa kwanza na wanawake ili wawe na makazi ya kudumu. Polepole mwanaume alianza kutegemea uchumi wa mwanamke na hali yake ilishuka kisheria na kijaoui. Hah hii ilijenga msingi wa jamii za kiukeni. Lakini walipoanza kutumia plau, au kulima mazao ya biashara, wanawake walipoteza uwezo wao wa kusimamia matumizi ya shamba. Badala yake walipewa bustani zilizo karibu na nyumbani tu. Ni dhahiri kwamba mabadiliko hayo yanahusiana na kuzuka kwa jamii za kiumeni.
3. BUSHWALD, ULRIKE VON na INGRID PALMER 1978 Monitoring Changes in the Conditions of Women – A Critical Review of Possible Approaches, Geneva, UNRISD, paper for restricted circulation No. 94. (“Ukaguzi wa Mabadiliko katika Hali ya Wanawake – Uhakiki wa Mitazamo Mbalimbali”).
Makala haya yanaeleza mbinu zinazotumiwa kuanzisha ukaguzi wa kitaifa wa mabadiliko katika hali ya wanawake. Maandishi haya yanayohusu maswala kama athari za mabadiliko ya kilimo yaliyotokana na ukoloni na kutojitegemea kiuchumi; mifumo ya ukuzaji wa viwanda na miji, na nafasi ya wanawake katika jamii na mfumo wa uzalishaji mali. Makala inafafanua hitilafu za data aazotumiwa kuchambua mabadiliko katika hali ya wanawake, na kusisitiza takwimu juu ya shughuli za kiuchumi, elimu na mfunzOy afya iia chakula bora. Inajadili mitazamo na mbinu pamoja na kutaja haja ya kuangalia takwimu za kijumla pamoja na takwimu zmazotokana na uchunguzi wa mada maalum. Hatimaye wanapendckeza mfumo wa ukaguzi unaokusanya data mara kwa mara na kutathmmi data muhimu zinazohusu wanawake. Sasa UNRISD inaandaa mpango wa uchunguzi wa awali kuhusu ukaguzi wa mabadDiko katika hali ya wanawake kama hatua moja ya kutekekza pendekezo hilo. Lazuna tuache kuelezea tu snra ya hali ya wanawake kwa juujuu. Lazima tuchambue sababu halisi za hali hii na athari za mabadiliko. Kwa hiyo kuna haja ya uchunguzi wa kimsingi na uchunguzi unaochungaza eneo au mada ndogo tu. Mifano ya maswah ambayo yangeweza kuwa msingi wa ukaguzi ni kama ifuatayo:
Quote:1. Je, ni katika aina gani za uzalishaji mali ambapo wanawake wanajitokeza baada ya athari za dhamaji na uhaba wa kazi wakati ambapo kuna mapinduzi ya kiteknolojia katika kilimo na huko sehemu za vijiji uzalishaji mali unabadilika kuwa wa kisasa upesi upesi?
2. Je, mabadiliko ya kiuchumi na kikazi yanasababisha tofauti kubwa za tabaka? Je, yanapunguza usawa wa wanawake uliokuwepo katika uchumiwajadi?
3. Je, mgawanyo wa kazi na mamlaka ya kutoa uamuzi katika familia iliyokuwepo kimila yanabadilikaje kutokana na mabadiliko ya nafasi za wanawake na wanaume katika uchumi?
4. Ni mambo gani ya utamaduni wa jadi yanayoshusha hadhi ya wanawake katika sekta za jamii zinazoleta maendeleo?
5. Kuna uhusiano wa aina gani kati ya habari zilizopatikana (kwa mfano kuhusu elimu, kazi, uwezo wa kushika mimba) tukiangalia habari hizo kwa kuzingatia tabaka?”
Makala hii ni muhimu sana kwa watekelezaji wanaoanza kutambua hitilafu za takwknu na habari nyingine zinazohusu wanawake. Vilevile inafaa wale wanaofanya utafiti juu va wanawake na jinsi ya kuwasadia wanawake.
4. GODY, J. na JOAN BUCKLEY 1973 “Inheritance and Women’s Labour ni Africa” Africa 43 (2): 108 – 121. (“Urithi na Kazi ya Wanawake katika Afrika”)
Katika Afrika wanawake ndio wanaofanya kazi nyingi za kilimo, hasa katika jamii zmazotumia jembe. Nafasi hii muhimu ya wazi hasa huko Congo na kadka Afrika ya Mashanki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini. Lakini ingawa wanawake wanafanya sehemu kubwa ya kazi za kilimo, kwa kawaida mashamba humilikiwa na wanaume. Hali hii inaathiri sana mfumo wa uchumi, urithi na ukoo. Inaonekana kwamba nafasi muhimu ya wanawake katika kilimo ina uhusiano na aina mbili za urithi: Kwanza urithi wa kiukem na pili aina ya urithi ambao kwao mali ya wanaume inagawiwa kwa watoto kufuatana na mama zao. Aina hii ya pili ya urithi ni aina ya “urithi kutoka juu” ambayo Gluckman anaiita “mfumo wa nyumba-mali”. Mfumo huo unaonekana kwenye jamii za kiumeni na mara nyingine kwenye jamii zinazotoa urithi kutokana na pande zote mbili, upande wa mama na wa baba.
5. IDS BULLETIN 1979 Special Issue on the Continuing Subordination of Women in the Development Process Vol. 10 (3), Brighton, Institute of Development Studies, University of Sussex, uk. 67. (“Toleo Maalum Kuhusu Ukandamizaji Unaoendelea wa Wanawake katika Jitihada za Maendeleo”).
Ripoti inatoa pendekezo la Mkutano kuhusu mwanamke mmoja ambaye ni mfungwa wa kisiasa. Yeye ni Mzalendo wa Puerto Riko aliyefungwa jela na serikali ya Marekani. Vilevile ripoti inatoa mapendekezo na mwongozo wa uchunguzi. Inapendekeza kwamba msingi wa uchunguzi uwe uchambuzi wa kinadharia kuhusu maendeleo na mifumo inayojenga na kuendeleza utawala wa kitabaka na hitilafu katika hali za wanawake na wanaume. Inasisitiza haja ya kuwa na mawasiliano mazuri ya kupashana habari kwa wale wanaochunguza ukandamizajtwa wanawake, na vilevile kwa wachunguzi na vyama vya wanawake, vikundi vya uchunguzi wa wanawake na jumuiya ya wafanyakazi. Pia kuna haja ya uchunguzi wa pamoja, yaani uchunguzi unaofanywa na wataalam wa fani mbalimbali na uchunguzi unaolinganisha vipengele mbalimbali vya jamii. Makadirio ya miradi yote yawe na kitengo cha fedha kwa ajili ya kutafsiri ripoti ya mwisho ya uchunguzi kwa lugha ya wale waliochunguzwa. Ripoti hn iliandikwa kwa lugha ambayo inaeleweka kwa urahisi na ripoti ipatikane kwa urahisi na wale wanaohusika. Matokeo ya uchunguzi yawasilishwe mapema kwa wanaohusika kwa kutumia vifaa vya elimu kama sinema, picha, na kada za kunasia sauti. Matokeo yajadiliwe mara kwa mara na wale waliotoa habari.
6. KENYA, Central Bureau of Statistics, Ministry of Economic Planning and Community Affairs 1977 “Educational Trends 1973 – 1977” uk. 85 na Jedwali 65 (“Mielekeo ya Elimu 1973 – 1977”).
Kijitabu hiki kinachambua elimu ya msingi na ya sekondari kwa kipindi cha mwaka 1973 hadi 1977. Kina jedwali za takwimu za idadi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika kila wilaya, kama ni wasichana au wavulana, aina ya shule, na matokeo ya mitihani ya darasa la saba na ya sekondari. Serikali ilipofuta ada za shule ya msingi mwaka 1973, idadi ya wanafunzi iliongezeka, lakini bado uwiano wa wasichana na wavulana haujawa sawasawa. Inaonekana kwamba kwa wastani wavulana wote wa mijini na vijijini wanafaulu vizuri zaidi katika mitihani ya darasa la saba, yaani mitihani ya Kiingereza, Hesabu, na Maarifa, isipokuwa sehemu za mijini hakuna tofauti kati ya wasichana na wavulana katika mtihani wa Kiingereza. Takwimu za elimu vijijini zinaonyesha kwamba wanafunzi wa kike wanalingana zaidi na wenzao wa kike katika maksi zao na wavulana wanalingana zaidi na wavulana wenzao, hata kama ni wasichana/wavulana wa kikundi kimoja.
Vilevile zipo tofauti kati ya wanafunzi wasichana na wavulana katika shule za sekondari. Asilimia kubwa zaidi ya wasichana.wanahudhuria shule zile ambazo hazipewi ruzuku. Wanafunzi wa shule hizo hawafaulu vizuri. Idadi kubwa ya wasichana wanahudhuria shule hizo. Hii inaonyesha kwamba wazazi wana moyo wa kuwasomesha wasichana wao na kukabili tatizo la nafasi haba za wasichana katika shule zinazopewa ruzuku. Shule zinazopewa ruzuku zina nafasi chache za wasichana, na hasa katika sayansi nafasi chache mno. (Sisi tunafikiri kwamba tunahitaji kuangalia kwa makini hali hii ambapo 2/3 ya wasichana wote wanaosoma sekondari wanasoma kwenye shule hafifu ambazo hazipewi ruzuku – yaani asilimia 67 ya wanafunzi katika shule hizo hafifu ni wasichana. Idadi ya wanafunzi wasichana katika shule hizo inazidi kuongezeka, na hali hii inaonyesha kwamba shule hizo ni kama mahali pa kutupa wanafunzi wa kike ili kupunguza haja ya kutenga nafasi nyingi za wasichana katika shule zinazopewa ruzuku. Kwa hiyo wasichana wengi wanapata elimu ya daraja la chini).
Kwa kuangalia idadi ya wanafunzi waliopata daraja la kwanza na la pili katika mitihani ya Kidato cha 4 mwaka 1976, wasichana walifaulu vizuri kuliko wavulana. Zaidi ya hapo, wasichana wachache kuliko wavulana walishindwa (asilimia 28 wasichana na asilimia 41 wavulana). Ingawa sababu moja ya kufaulu kwao ni kwamba wasichana wanachujwa zaidi kabla ya kuingia shule ya sekondari, lazima tukumbuke vilevile kwamba wasichana wengi waaasoma kwenye shule zisizopata ruzuku na ambapo kwa wastani wanafunzi hawafaulu vizuri.
7. HENN, JEANNE 1981 “Who Benefits from Peasant Women’s Work? Insights from a Mode of Production Analysis” Economic Reflections 1 (1): 34 – 48. (Nani Anafaidi Kutokana na Kazi ya Wanawake Wakulima? Mawazo Yanayotokana na Uchunguzi wa Mfumo wa Uzalishaji Mali).
Makala haya yanachambua mahusiano ya uzalishaji mali wa kiumeni katika kiwango cha kaya, uzalishaji wa bidhaa ndogondogo ulioenea kwa wakulima wadogo, na uzalishaji wa kibepari. Mahusiano hayo yanathibitishwa katika uchunguzi uliofanyika kuhusu muda unaotumiwa kufanya kazi mbalimbali za uzalishaji mali na uendelezaji wa uzalishaji mali huko kayani na kutofautisha uzalishaji kwa ajili ya kaya na kwa ajili ya kuuza. Uchunguzi wa muda wa aina ya kazi unafafanua ni nani anayepata faida kutokana na kazi zinazofanywa nyumbani. Unaonyesha ni nani anayefaidi kwenye kaya, kijiji, taifa na hata kimataifa. Uchunguzi wa aina ya kazi pamoja na tofauti katika ulaji au matumizi unabainisha wazi mchango mkubwa wa wanawake wakulima katika kilimo na katika kutunza na kuendeleza familia za wakulima.
8. LUCILLE M. MAIR 1981 “New International Economic Order: What Does Development Really Mean to Women” IFDA Dossier 21 (Jan. – Feb.), uk. 56 – 68. (“Mpango Mpya wa Uchumi wa Dunia: Maendeleo yana maana gani kwa Wanawake”).
Makala haya yanatoa hoja ya kwamba wanawake wanafanya theluthi moja ya kazi zile zinazohesabiwa, pamoja na kazi za nyumbani zisizohesabiwa wala kulipiwa. Zaidi ya hapo theluthi moja ya wakuu wa familia duniani ni wanawake. Ukweli huo unapingana na fikra inayotolewa katika vitabu vya shule kwamba katika Afrika na kwingineko, wakuu wa kaya ni wanaume tu. Ingawa wanawake wanafanya theluthi moja ya kazi duniani, wanapata chini ya 1/10 ya mapato ya duniani na wanamiliki chini ya 1/100 ya mali ya dunia.
Hali ya wanawake inahusishwa na hali ya tabaka la chini, ambaioni tabaka la wanawake walio wengi. Asilimia 70 ya dunia inapata asilimia 30 ya mapato ya dunia. Mgogoro uliopo duniani unazidi kuwa mkali kwa sababu ya hali ya uchumi, matatizo ya nishati na madeni makubwa ya nchi zinazoendelea. Ingawa huu ndio ukweli unaoathinmaisha ya kazi ya wanawake wa “kusini”, (nchi-zinazoendelea), wanawake wa “kaskazini” (nchi zilizoendelea za kibepari) wanajitenga na harakati za kusini kwa jumla. Akijadili Mkutano wa Copenhagen wa Kimataifa wa Kipindi cha Miaka 5 ya Miaka kumi ya Wanawake, Mair anataja ubaguzi wa vyombo vya habari ambavyo vinasisitiza tofauti za siasa badala ya kujadili maswala ya wanawake. Anataja kwamba aya 284 kati ya aya 287 za mapendekezo ya utekelezaji zilipitishwa bila kupingwa. Wanawake wa dunia ya tatu, wanajua kwamba haitoshi kuanzisha taasisi zinazoshughulikia wanawake. Tukitaka kuleta ukombozi wa wanawake, kuna haja ya kukabili maswala ya uchumi na historia ya harakati za jamii. Wanawake hawakubali kulazimishwa kujadili aina yoyote ya maswala haya.
9. MBILINYI, MARJORIE J. 1971 “The Participation of Women in African Economies” Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Makala ya ERB Na. 71.12, uk. 34. (“Ushirikiano wa Wanawake katika Uchumi wa Kiafrika”). Pia Addis Ababa, UNECA.
Kwajumla makala haya yanachambua wanawake katika uchumi wa Afrika, lakini kwa kiasi fulani, msingi wa uchambuzi huo unahusu hali iliyopo Tanzania. Makala yanasisitiza kwamba haiwezekani kutoa matamko kuhusu “nafasi ya wanawake wa Kiafrika”, kwa jumla kwa sababu ya hali mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Imeandikwa kwa lugha inayoeleweka kwa urahisi na inachambua jinsi na kwa kiasi gani wanawake walishiriki katika sekta mbalimbali za uchumi kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni. Kwa kila kipindi makala inachambuamaswala ya umilikaji na udhibiti wa njia kuu za uchumi, uthibiti wa wafanyakazi na kazi zao, na ugawaji wa faida zinazotokana na kazi. Mambo yanayozuia uajiri wa wanawake ni ukosefu wa elimu – pamoja na elimu ya ufundi – na fikra na maadili ya kiumeni. Kuanzisha mbinu za kisasa za kilimo kunaleta kazi zaidi kwa wanawake. Pamoja na hayo, wanapoteza uwezo wa kufanya uamuzi kuhusu kazi zao. Uchambuzi uliofanyika juu ya elimu na elimu ya ufundi unadhihirisha ubaguzi wa wanawake katika uchaguzi wa masomo na nafasi za elimu ya juu. Makala inaeleza hatua na mazingira yanayotakiwa kuwapatia wanawake nafasi ya kufanya kazi, kulea familia na kutoa mchango wao kwa jamii. Hatua hizo ni pamoja na vituo vya watoto wadogo vijijini na mijini ambavyo vitatunza watoto siku nzima, chakula rahisi kilichotengenezwa tayari; huduma za afya na marupurupu mengine kwa ajili ya wanawake walioolewa na wasioolewa huko wanapofanya kazi; mshahara sawasawa kwa wanawake na wanaume wanaofanya kazi ya aina moja; uwezo wa kuamua kuhusu matumizi ya hela za mshahara au mapato mengine, na kusaidia wanawake wanaojitegemea oa wasioolewa kujiunga na vijiji vya ujamaa kama wanavijyi wengine. Makala yanachambua vilevile nafasi ya serikali, mashirika ya kimataifa na mashirika mengine. Mwongozo wa maswala ya uchunguzi unaambatanishwa.
10. MCDOWELL, JIM 1976 Village Technology in Eastern Africa. Ripoti ya Semina ya UNICEF kuhusu “Simple Technology for theRural Family” iliyoifanyika Nairobi, Juni, 1976, Nairobi, UNICEF Eastern Africa Regional Office, uk. 63 pamoja na vielelezo. (Teknolojia Vijijini Katika Afrika Mashariki).
Makala haya yanajadili faida ya kuleta teknolojia inayowafaa akina mama na watoto vijijini. Inasisitiza umuhimu wa kuleta vitu vmavyotengenezwa kwa urahisi na ambavyo vitapunguza kazi za wanawake. Vilevile inaonyesha umuhimu wa kuzalisha chakula bora na kingi zaidi kwa kutumia mbinu za kisasa za kilimo na uhifadhi na utayarishaji wa chakula. Inasisitiza vilevile umuhimu wa kuleta maji safi vijijini. Kwa jumla, makala yanatoa maelezo na kutoa mwongozo kuhusu aina nyingi za teknolojia ambazo zingefaa vijijini na jinsi ya kuwapasha habari na kuwaelimisha wanavijiji kuhusu teknolojia hii.
11. O’BARR, JEAN 1975 “Making the Invisible Visible: African Women in Politics” African Studies Review, 18 (3) uk. 19 – 27.(Kufanya Yule Asiyeonekana Aonekane: Wanawake wa Kiafrika katika Siasa).
Makala haya yanaangalia mawazo na fikra juu ya nafasi ya wanawake wa Kiafrika katika siasa na kupinga maoni yasiyo na msingi yanayotolewa na wataalam wa siasa na viongozi. Kwa sababu ya maoni potofu, uchambuzi mwingi uliofanyika kuhusu shughuli za siasa haukutaja wanawake. Makala yanatoa hoja kwamba “shughuli za kisiasa za wanawake ni muhimu sana katika kuelewa siasa ya jamii zinazoendelea”. Katika jamii za Kiafrika ambapo shughuli za nyumbani na shughuli za umma hazikutenganishwa sana, “wanawake wanashiriki kikamilifu katika siasa kwa kutoa hoja, kuendeleza hoja hizo na hatimaye kukubali au kukataa matokeo yake. Inataja makala mengine kuonyesha jinsi uwezo wa kiuchumi unavyojenga uwezo wa kisiasa na umuhimu wa nafasi ya pili ya wanawake. Mifano kutoka Tanzania inatolewa kutoka makala ya M.J. Mbilinyi (“Mwanamke ‘Mpya’ na Maadili ya Jadi Tanzania”) na utafiti uliofanywa na mwandishi mwenyewe huko Upare.
12. PALA, ACHOLA 1974 The Role of African Women in Rural Development, Research Priorities (Nafasi ya Wanawake wa Kiafrika Katika Maendeleo Vijijini Mada au la Uchunguzi) Nairobi, Institute of Development Studies Discussion Paper No. 203 uk. 31.
Makala haya yanachambua makala mengine kuonyesha kwamba katika uchumi wa Afrika kabla ya ukoloni, wanawake walikuwa na nafasi kubwa katika uchumi wa jamii wa wakulima na wafugaji. Hata hivyo, jambo hili halijazingatiwa katika kutunga mbinu za maendeleo vijijini, ingawa wanawake wanatarajiwa a kutoa mchango katika kujenga taifa. Hitilafu hii, kati ya nadharia na hali halisi inasababishwa na mambo mawili. Watawala walioandaa mipango ya kikoloni ya kilimo cha biashara waliwapendelea wanaume kuliko wanawake. Kwa hiyo “walikuza zaidi uzalishaji mali wa mfanyakazi mwanaume” na kumpunja mwanamke. Mtindo huu uliendelea hata baada ya Uhuru. Uchunguzi uliofanyika Tanzania na Kenya, unaonyesha kwamba huduma za kilimo na taarifa za matokeo ya uchunguzi zinapatikana kwa urahisi zaidi kwa wale wakulima “walioendelea”. Hawa kwa kawaida ni wakulima wa kiume wenye mashamba makubwa. Sekta ya kilimo ya kilimo cha kijungumeko wanaachia wanawake na kwa kawaida sekta hiyo haishughulikiwi. Sababu ya pili ni kwamba uchunguzi mwingi kuhusu wanawake wa Kiafrika umefanywa na wageni ambao hawaelewi vizuri mazingira ya uzalishaji mali wa Afrika na maendeleo yake au umefanywa na Waafrika ambao hawataki kutazama matatizo ya maendeleo vijijini kwa kuzingatia mawazo ya wakulima.
Makala yanasisitiza kwamba maendeleo vijijini hayana budi kuzingatia nafasi ya wanawake katika kuleta maendeleo ya wanaume. Kuna haja ya kuchambua mfumo wa jamii za vijijini na hali ya wanawake kiuchumi na kijamii jinsi inavyobadilika. Mwandishi anataja mada za uchunguzi zitakazosaidia mipango bora ya mabadiliko vijijini.
13. PALA, ACHOLA OKEYO 1981 “Reflections on Development Myths” (“Maoni juu ya Hadithi za Maendeleo”) African Report 26 (2) March – April: 7 – 10.
Makala haya yanatoa hoja ya kwamba pote duniani watu wanatambua kwamba hali ya wanawake ni ya chini na inazidi kushuka, na kwamba hali hii inaathiri vibaya maendeleo. Hivi sasa, wataalam wanaanza kutafuta mbinu za uchunguzi na ukusanyaji wa data ambazo zitafafanua vizuri zaidi kutokuwepo kwa usawa kati ya wanawake na wanaume. Kwa mfano mwandishi anasisitiza umuhimu wa kuacha mbinu ya kutotofautisha shughuli za uzalishaji wa chakula cha kuuza na cha matumizi ya nyumbani. Wakati huohuo lazima wanawake wote watafute mbinu za kutatua matatizo. Matatizo ya wanawake Waafrika yamefasiriwa “kwa nje”, yaani kwa kuzingatia mgawanyo wa kazi wa kimataifa na kusisitiza itikadi ya hali ya kiuchumi – jamii.
Mwandishi anapinga uchambuzi unaosisitiza utamaduni, kwa sababu uchambuzi huo unatenga utamaduni na siasa na uchumi na una fikra potevu kwamba mabadiliko ya utamaduni hauathiriwi na mambo mengine yaliyo nje ya utamaduni. Pia inapotosha kwa kutenga uchambuzi wa wanawake na uchambuzi wa hali ya kiuchumi-jamii na wa uchumi wa kimataifa. Msimamo wa wanawake wa nchi za magharibi ni kwamba mwanaume ni adui. Msimamo huo unatokana na hali halisi huko ambayo mwanamke hana maana. Hapa Afrika hali ni tofauti kwa sababu tangu zamani wanawake walizalisha mali. Kwa hiyo wanawake wa Kiafrika hawafikiri kwamba mwanaume ni tatizo. Isitoshe, wanawake wanapojaribu kuleta maendeleo, wanafanya hivi si kwa manufaa yao peke yao, bali kwa ajili ya familia zao. Hii haina maana ya kwamba wanaume hawapo katika maisha yao. Kwa hiyo ni kosa kusema kwamba “mipango ya wanawake inaweza kuleta mgogoro kati ya wanawake na wanaume”.
14. SCANDANAVIAN INSTITUTE OF AFRICAN STUDIES 1978 Women in Africa and Development Assistance (Wanawake katika Afrika na Msaada wa Maendeleo). Ripoti ya Semina iliyoandaliwa na Scandanavian Institute of African Studies, Uppsala, 20 – 21 Agosti, 1978 uk. 55.
Semina hii ilisisitiza maswala yafuatayo:
Misaada ya nje inaathirije wanawake? Wanawake wanahitaji msaada gani kujiendeleza? Ni Mbinu gani ambazo zingeweza kutumiwa ili misaada inayotolewa iwasaidie zaidi wanawake? Semina ilisisitiza haja ya kufanya uchunguzi unaoendelea kuhusu hali ya wanawake, ambao vilevile utalenga utekelezaji. Uchunguzi uliofanyika katika mazingira ya ukoloni mamboleo na mgawanyo wa kazi kimataifa unaonyesha kuwa wanawake wanafanya kazi kwa mshahara mdogo mno. Wanasemina vilevile walijadili dhana ya mgawanyo wa kazi za uchunguzi ambapo wachunguzi wagem na wachunguzi Waafrika wangetenganishwa. Wengine walitetea dhana hii na baadhi waliona kwamba “uchunguzi na matokeo yake ni muhimu zaidi kuliko swala la nani anaufanya”.
Uchunguzi na mipango ya msaada inayosisitiza zaidi “sera ya kuku” na kusaidia mahitaji ya kimsingi tu yanayombagua mwanamke mkulima na kumkandamiza kiuchumi. Wanawake wanahitaji mafunzo na kushirikishwa katika sekta zile za uchumi zilizoendelea sana.
15. IRENE TINKER 1981 “Policy Strategies for Women in the 1980’s” (“Mbinu za Sera ya Wanawake kwa Kipindi cha Miaka 10, 1980 – 1990”) African Report 2 (2) Machi – Aprili, uk. 11 – 16.
Makala hii inatoa maelezo ya historia ya dhana ya wanawake katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Ingawa inatoa uhakiki muhimu wa msimamo wa “Wanawake katika Maendeleo” haikuchambua kiini cha matatizo ya maendeleo yanayosababisha uonevu wa wanawake. Mwandishi anatoa hoja kwamba vyombo vingine vya Umoja wa Mataifa vimepitisha maazimio yanayolazunisha kila mradi kujumuisha wanawake kama watendaji na wapokeaji wa msaada. Mwandishi anataja kwamba mambo hayo hayakubadilisha hali halisi. Labda jambo la maana lililofanywa kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita ni ukusanyaji wa data na ukuzaji wa miradi midogo ya wanawake. Uchunguzi unadhihirisha kwamba wanawake wanafanya kazi kwa bidii, na kila inapowezekana wanafanya kazi kupata hela. Uchunguzi wa matumizi ya hela na muda wa kazi una data juu ya nani anatawala hela za matumizi nyumbani na takwimu nyingine za mapato. Kwa mfano, katika USA imeonekana kwamba wanawake wanalipwa senti 59 kwa kila dola anayolipwa mwanaume. Hii ni kwa sababu ya ubaguzi wa wanawake kazini. Wanawake wanapewa kazi za mshahara mdogo wa kima cha chini kama vile, wanawake Watanzania wanaofanya kazi viwandani.
Katika nchi zinazoendelea, ujima (kwa mfano baina ya majirani) umefifia. Hivi sasa familia, kwa mfano, mama na watoto pamoja na vibarua, wanafanya kazi hizi. Kazi hizi hazihesabiwi katika uchambuzi wa wafanyakazi. Kazi hizi ni pamoja na kutayarisha chakula, kuchota maji, kufuma mikeka. Kazi hizi hazihesabiwa kama shughuli za kiuchumi ingawa zinasaidia kuendeleza familia na mara nyingme huleta mapato. Mashine zinazoweza kufanya kazi hizi ni kama masbine ya kusagisha au jiko la mafuta ya taa. Mashine hizi ni ghali mno na wengi hawawezi kuzinunua. Kwa hiyo, wanawake wanarudishwa nyuma kwa kupewa kazi nyingi za kila siku, kazi ambazo zinaweza kuitwa “kazi bila ya mapato”. Mwelekeo wa kupanga miradi ya wanawake umetenga jitihada za wanawake na mipango ya maendeleo. Ni kama wanawake wanapewa msaada wa ustawi wa jamii tu. Isitoshe, kwa kawaida miradi hiyo ni midogo mno na kiuchumi haiwezi kufanikiwa. Kwa hiyo kwa kipindi cha miaka 10 cha 1980 – 1990, tuwe na msimamo wa kuandaa miradi inayolenga mambo ambayo ni muhimu kwa wanawake na mahitaji yao, na kuwashirikisha katika kupanga na utekelezaji. Vilevile, miradi izingatie mpango wa maendeleo ya kijiji au taifa zima. Miradi ya vyama vya wanawake bado ina umuhimu katika kujenga tabia ya kujiamini na ya uongozi, na kufanya majaribio ya mradi unaofikiriwa. Mwandishi anataja vilevile kwamba ‘vyama’ vya wanawake havijitangazi vya kutosha, pia vinashmdwa kuleta umoja utakaoathiri sera. Bado wanawake wanalazimishwa kupeleka maswala yao kwenye “dunia ya wanaume” kama wanataka kusikilizwa.
16. UMOJA WA MATAIFA 1979 Convention on the Elimination of all Forms of Discrimination Against Women (Mkutano wa Kufuta Ubaguzi wote wa Wanawake) New York, uk. 15. Inapatikana bure kutoka Ofisi ya UNDPDar es Salaam na Arusha, pamoja na makala mengine za Umoja wa Mataifa.
Mnamo Desemba 1979, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulikubali kuitisha Mkutano wa Kufuta Ubaguzi wa Wanawake. Ripoti hii inaeleza kisheria mwongozo uliokubalika kimataifa na hatua za kuleta haki za usawa kwa wanawake. Zipo ibara 30 zinazopendekeza sheria za kimataifa za kupiga marufuku ubaguzi wa aina zote. Kwa mfano, ubaguzi uliopo katika siasa, uchumi, jamii, utamaduni na serikali. Vilevile inapendekeza hatua za muda za kubadilisha mifumo ya kijamii au kiutamaduni inayoendeleza ubaguzi. Hatua maalumu ni pamoja na nafasi sawa za elimu na kufuta ubaguzi katika mihtasari ya masomo. Kwa mfano wasichana wanasoma sayansi kimu na wavulana wanasoma ufundi. Hatua nyingine ni kufuta ubaguzi katika uajiri kuhusiana na mshahara na usalama wa kazi; mwanamke akiolewa au akipata mimba. Ripoti inasisitiza vilevile kwamba wanaume na wanawake wana wajibu sawasawa wa kutunza familia na kufanya kazi za nyumbani. Kuna haja ya huduma za jamii kama vituo vya watoto, kuhakikisha kwamba wazazi wote wanaweza kutekeleza wajibu wa kazi, kutunza familia, na kushiriki katika siasa.
Sasa vyombo vya kimataifa vinatayarishwa ili kukagua mapendekezo hayo yaliyokubaliwa na mataifa. Lakini ni wajibu wa kila nchi kuhakikisha kwamba hatua zinachukuliwa dhidi ya ubaguzi wa wanawake, na ni wajibu kupigania sheria zinazohitajiwa ili zipitishwe Bungeni. Data zilizopo katika bibliografia hii zinaonyesha kwamba upo ubaguzi wa wanawake hapa Tanzania, na kuna mambo mengi ya kufanya ili kuufutilia mbali. Ubaguzi huu utafutwa ikiwa wanawake na wanaume watachunguza matatizo yanayozuia ushirikiano baina yao, hasa yale malatizo yanayosababisha wanawake kunyimwa haki zao.
17. UNECA, African Training and Research Centre for Women 1976 “The Education and Training of Rural Women for National Development” (“Elimu na Mafunzo ya Wanawake wa Vijijini kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa”). Makala iliyowasilishwa kwenye “International Workshop on Education for Rural Women” iliyofanyika Lushoto, Tanzania (PMO/UNICEF) uk. 14.
Makala haya yanaeleza hali ya wanawake vijijiini. Yanaeleza kwa nim hawapati elimu au mafunzo, hata mafunzo ya kilimo na kwa hiyo wanakuwa raia wa daraja la pili. Kwa hiyo lazima mafunzo yatolewe kwa wanawake wakulima na wanawake maofisa kilimo, na kuongeza shule za sekondari hasa zile zinazotoa masomo ya kilimo. Hapa Tanzania kuna shule 36 za sekondari zinazotoa masomo ya kilimo. Kati ya hizo 3 tu ni za wasichana. Wanawake wanahitaji mafunzo ya mifugo, biashara, viwanda vidogo na sanaa za mikono (ufinyanzi, ususi). Mafunzo yatasisitiza udhibiti wa ubora wa bidhaa, uongozi, mbinu ya kutengeneza bidhaa za aina mbalimbali badala ya aina moja, matumizi ya vifaa, namna ya kutayarisha na kuhifadhi vyakula, kuongeza kiasi cha ubora wa vyakula. Vilevile mafunzo yatasaidia kuelimisha upya wakunga wa vijijini, kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa vituo vya watoto wadogo na kliniki za kina mama na watoto wadogo na kuongeza huduma za kisomo cha manufaa.
18. UNECA 1977 The New International Economic Order, What Roles for Women? (Mfumo Mpya wa Uchuni wa Dunia una Nafasi Gani kwa Wanawake?) Addis Ababa, E/CN. 14/ATRCW/77/Wd3 uk. 54
Kitabu hiki kinachambua jinsi mapendekezo yalivyozingatia nafasi ya wanawake katika miradi hii. Vilevile kinapendekeza njia mbalimbali za kuangalia mchango wa wanawake na uwezo wao wa kupata nyenzo za kimsingi za maendeleo. Mapendekezo hayo ni pamoja na matumizi ya data iliyopo tayari na haja ya ukaguzi zaidi kupata data inayohitajika. Kinajadili matumizi ya jedwali za aina mbalimbali za data: uajiri (asilimia ya wafanyakazi wanawake, jinsi mishahara inavyolingana, saa za kazi za wanawake katika kazi zisizo na mkataba rasmi) elimu na mafunzo: (asilimia ya wanawake katika shule za msingi, sekondari na vyuo na masomo yao; ushirikiano wa wanawake katika mafunzo yasiyo ya shule kwa mfano, kilimo, mifugo, na kadhalika); afya na uzazi: (ushirikiano wa wanawake katika k.m. kuleta maji safi, zahanati); sheria (kumiliki ardhi, mikopo); teknolojia vijijini nafasi yao katika kutoa uamuzi.
19. UNITED NATIONS PROTEIN ADVISORY GROUP 1979 Women ni Food Production, Food Handling and Nutrition, with Special Emphasis on Africa. (Wanawake katika Uzalishaji wa Chakula, Utayarishaji wa Chakula na Lishe hasa katika Afrika). Ripoti ya Protein – Calorie Advisory Group (PAG) ya Umoja wa Mataifa, Roma, FAO, uk. 223.
Ripoti hii inasisitiza hali ya wanawake katika sehemu mbalimbali za Afrika, pamoja na Tanzania, kwa sababu wanawake ndio msingi wa uzalishaji mali katika Afrika. Inatumia utaalam wa masomo mbalimbali k.m. historia, chakula bora, sosiolojia, anthropolojia ya kijamii na vilevile makala za uchunguzi na za Umoja wa Mataifa. Ripoti matumia data hizo kutathmini: (1) nafasi ya wanawake katika uzalishaji mali, utayarishaji mali na utayarishaji wa chakula na lishe katika Afrika, na (2) kadiri mazingira ya kazi na maisha ya wanawake yanavyoathiri upatikanaji wa chakula na ubora wa chakula cha familia najamii zao. Ripoti iliona kwamba kuongeza chakula bora na uhaba wa vyakula vingine; lazima tuwe na ugawaji mzuri zaidi wa vyakula. Pia kama familia inaanza kupata hela zaidi, haina maana kwamba ubora wa chakula chao utaongezeka. Chakula kitakuwa bora zaidi ikiwa mama ndiye anayeamua kuhusu matumizi ya fedha hizo.
20. WORLD BANK (BENKI YA DUNIA) 1979 “Recognizing the ‘Invisible’ Woman in Development: The World Baok’s Experience” (“Kumtambua Mwanamke ‘Asiyeonekana’ katika Maendeleo: Uzoefu wa Benki ya Dunia”) Washington, d.C. uk. 31.
Utangulizi wa makala haya uliandikwa na Robert S. McNamara ambaye alikuwa Rais wa Benki ya Dunia kwa wakati ule. Kutokana na utangulizi huu, Benki ya dunia imeanza kutambua haja ya kuzingatia kwa makini athari za miradi yake kwa wanawake. Kwa hiyo mwaka 1977, Benki hii ilitenga nafasi moja ya kazi kwa Mshauri wa Wanawake katika Maendeleo, ambaye kazi yake ni “kukagua na kutoa ushauri juu ya athari za miradi na athari zinazoweza kutokana na miradi kwa hali ya wanawake”. Kwa mujibu wa McNamara, “kukiuka mipaka ya nafasi za jadi za wanawake wakiwa wazazi na wafanyakazi wa nyumbani na kuongeza nafasi zao za kiuchumi, kisiasa na kijamii, kutawawezesha kujishughulisha na kutumiwa uwezo wao katika uwanja mpana zaidi”.
Makala yenyewe inaanza na maelezo juu ya mambo yanayozingatiwa na Mshauri wa Wanawake katika Maendeleo anapokagua miradi: Miradi itasaidaje mahitaji ya wanawake na kukuza uwezo wao? Je, zipo njia gani za wanawake kufaidi miradi hiyo? Nafasi ya kiuchumi-jamii ya wanawake ikoje huko mradi unapotekelezwa? Je, mradi utaathiri vibaya wanawake? Tunawezaje kutambua athari hizi na kizizuia? Ingawa ripoti inauliza maswali muhimu na kutoa muhtasari mzuri wa matokeo ya uchunguzi, inatumia dhana ya kibepari ya maendeleo. Dhana hii inatenga wanawake na matnuiano ya kijamii na mifumo ya mabadiliko yanayotokea katika mazingira yao.
21. MARCIA WRIGHT 1975 “Women in Peril: A Commentary on the Life Stories of Captives in Nineteenth Century East-Central Africa” (“Wanawake Hatarini: Maoni juu ya Masimulizi ya Maisha ya Mateka wa Afrika ya Kati na ya Mashariki katika Karne ya 19”) African Social Research 20 (Desemba, uk. 800 – 819).
Makala hii inatokana na uchunguzi wa tawasifu zilizoandikwa na wanawake watatu na mwanaume mmoja waliokuwa watumwa. Hawa waliishi katika karne ya 19, wakati wa mabadiliko ya uchumi na jamii. Masimulizi ya kila mmoja yanachambuliwa ili kupata picha ya mabadiliko yaliyotokea katika hali ya wanawake kwa jumla.
Watu walibadilishana wanawake kwa kutumia njia mbalimbali. Njia mojawapo ilikuwa ni mahari au malipo ya kazi ya mwanamke. Wanawake vilevile walitumiwa kam’a malipo ya faini au fidia. Walitekwa katika vita na waliuzwa kwenye soko la biashara ya utumwa. Watoto wa watumwa walikuwa hawana hadhi – hawakuhesabiwa katika ukoo, hata kama wazazi (mzazi) walipewa hadhi katika ukoo kutokana na ndoa. Mifano inaonyesha kuwa nafasi mbalimbali za kazi za kuajiriwa na nyinginezo zilipatikana katika misheni au miji. Kazi hizo ziliwawezesha wanawake kutoroka maisha ya utumwa ili wajitegemee wakiwa wakuu wa kaya. Hata hivyo, katika hali zote wanawake walilazimishwa kuwa chini ya wanaume wenye hadhi iliyotambuliwa na sheria na jamii. Zaidi ya hapo, wanawake ndio waliotekwa na kufanywa watumwa kwa urahisi. Wanawake walikuwa na thamani kubwa sana kwa sababu ya nafasi zao kama “wazazi, wafanyakazi na bidhaa inayoweza kuuzwa au kurithishwa”.
|
|
|
MFANO WA MBAZI |
Posted by: MwlMaeda - 09-14-2021, 05:04 PM - Forum: Hadithi
- No Replies
|
|
Siku moja Panya akiwa darini alichungulia chini na kumuona mkulima na mkewe wakiaanda mtego utakaotumika kumnasa, Kwa majonzi alisikitika na kujiona anasiku chache za kuishi duniani.
Siku hiyo panya alizunguka huku na kule kuomba msaada wa mawazo kwa wanyama wenzake ili aweze kunusurika na mtego alioandaliwa, lakini wanyama wenzake hawakuweza kumsaidia huku wakisema matatizo yako hayatuhusu.
Awali panya alitoka ndani na kwenda kuonana na mbuzi, akamwambia mbuzi, mkulima na mkewe wananiwinda, wameandaa mtego wa kuniangamiza, tafadhali naomba nisaidie, naomba nisaidie mwenzako niepukane na kifo nilichoandaliwa, Mbuzi akamjibu ” Samahani Mimi sihusiki na mambo ya huko ndani na hayo matatizo yako hayanihusu, tafadhali acha kunisumbua, mimi siwezi kukusaidia nakuomba uondoke hapa haraka sana, mkulima akikuona hapa utanisababishia matatizo. Panya akaondoka kwa huzuni wakati huo akapata wazo la kuonana na ng’ombe akiamini ng’ombe si mbuzi japo wote ni wanyama kama yeye.
Basi Panya alienda kuonana na Ng’ombe, alianza kwa kusema ” Samahani ng’ombe, najua wewe ni mnyama kama wanyama wengine, tunachotofautiana Mimi na wewe ni ukubwa wa umbo ila ukiangalia mambo mengine hakika tunaendana, wewe una mkia na Mimi pia nina mkia, unakula mahindi na mimi pia ninakula mahindi. Tafadhali bwana naomba nisaidie mwenzako ninawindwa na mwenye nyumba kwani jana usiku nimemuona akitoa mtego unaoweza ukaniangamiza ndani ya dakika chache, najua wewe unaweza kuukanyaga ule mtego na kuuvunja vunja kabisa, nitakachofanya mimi ni kukujulisha mara tu atakapotoka, ukiuvunja nitakuwa huru kula nitakavyo, ng’ombe naye alitoa majibu kama ya mbuzi basi panya akawa amekosa kwa kukimbilia, zaidi zaidi alijiwazia mwenyewe kuwa itabidi awe makini kwa kila hatua atakayo iendea.
Usiku ule panya akiwa amelala alisikia mtego umefyatuka, mke wa mkulima na mumewe wakafurahi wakiamini kuwa ni panya amenaswa, haraka sana waliufuata mtego ulipo na kukuta mtego umenasa nyoka badala ya panya. mke wa mkulima alipojaribu kumtoa ghafla aling’atwa na hali yake ikaanza kuwa mbaya, ikabidi yule mkulima amkimbize mkewe hospitalini, hali ya mke wa mkulima aliendelea kuwa mbaya kutokana na sumu ya nyoka, watu wakawa wanakuja kutoa pole kwa mke wa mkulima, chakula kikapungua, mkulima aliamua kumchinja mbuzi, Panya aliyaona haya alisikitika huku akiwa anayakumbuka majibu ya mbuzi na kujiuliza mwenyewe kuwa mbuzi angesaidia kuuharibu ule mtego wala asingechinjwa, baadaye mke wa mkulima alifariki, watu wengi walikuja kwenye msiba, yule mkulima aliamua kumchinja ng’ombe wake ili watu wapate kitoweo siku ya msiba.
Ndivyo ilivyo katika maisha tunayoishi. Watu wengi wanakuwa na uwezo wa kutatua shida za watu wasio na uwezo, lakini kwa sababu haziwahusu hata wakiombwa msaada wanaishia kutoa maneno ya dharau na matusi huku wakisema shida zako hazinihusu wasijue msaada wanaoweza kuutoa unaweza ukawasaidia au kuwaepusha na jambo baya lililopo mbele yao.
Mbuzi na ng’ombe wangeamua kumsaidia panya kuuharibu ule mtego hata wasingeangamia, lakini kwa jeuri zao na kuona matatizo ya panya siyo yao wala hayawahusu mwishowe walijikuta wao ndio wanaangamia.
|
|
|
SHAABAN ROBERT KAMA MWANANATHARI |
Posted by: MwlMaeda - 09-14-2021, 04:55 PM - Forum: Watunzi wa Kiswahili
- No Replies
|
|
SHAABAN ROBERT KAMA MWANANATHARI
1.0.HISTORIA FUPI YA MWANDISHI
1.1 UZAWA NA MAISHA YAKE
1.1.1 UPANDE WA BABA YAKE
Asili ya wazazi wa Shaaban Robert ni Tunduru-Ruvuma kwa upande wa baba yake na Tanga kwa upande wa Mama yake.
Babu yake Shaaban Robert kwa upande wa baba aliitwa Kanduru. Alikuwa mzaliwa wa Wilaya ta Tunduru, mkoani Ruvuma. Katika suala la imani ya Kidini, Kanduru alikuwa anaamini Miungu ya Ki-mizimu ambayo wakati huo iliaminika kuwa ndiyo chanzo cha yote yaliyojiri katika maisha ya binadamu. Kanduru alipofika Mzizima kwa mara ya pili ili aje kufanya kazi, alimpata mke kutoka kabila la Wazaramo. Mke huyu alikuwa Muislamu kwa sababu eneo lote la Pwani lilikuwa tayari linakaliwa na wakazi wengi waliokuwa Waislamu. Kutokana na kumhitaji binti huyu, ilimlazimu Kanduru asilimu kwanza ndipo aozwe. Hivyo, Kanduru alisilimishwa na kuwa Mwislamu, akaitwa Jumaa, ndipo akaozwa.
Baada ya muda, walipata mtoto waliyempa jina la Ufukwe, jina alilopewa na watani kwa kuwa alizaliwa ufukweni mwa bahari ya Hindi wakati mama yake alipokwenda huko kutandaza Uduvi. Pia aliitwa Selemani, jina ambalo lilikuwa rasmi kwa muktadha wa dini ya Kiislamu. Tajiri wa Jumaa ambaye alikuwa mzungu, aliamua kumpa mtoto huyu jina la Roberto kutokana na mapenzi na furaha aliyokuwa nayo. Hivyo jina hili halihusiani na dhana ya dini. Baabaye, kutokana na athari za matamshi ya lugha ya Kiingereza, jina hili la Roberto lilibadilishwa na kutamkwa Roberts. Roberto au Roberts, ambaye majina yake ya Ufukwe na Selemani yalififia, alimuoa Mwanamwema binti Mwindau na kuishi naye huko Vibambani, Tanga. Mnamo tare 01 Januari 1909, wakamzaa mtoto waliyemuita Shaaban.( Ponera 2010:26).
1.1.2 UPANDE WA MAMA YAKE
Bibi Mwanamwema binti Mwidau alikuwa ni wa ukoo wa kina Kihere (yaani Kihere Mwalimu Kihere na Mwalimu Mwalimu Kihere), ambao wanatajwa sana katika barua nyingi za Shaaban Robert (kama zilivyo limbikizwa na kuhaririwa na M. M. Mlokozi). Alikuwa ni wakabila la Kimwamwande, na alizaliwa Msengenyeni, Tanga, mwaka wa kuzaliwa haujulikani. Alifariki mwaka 1967.
Bibi Mwanamwema aliolewa mara tatu na alijaliwa kupata jumla ya watoto 14. Mume wake wa kwanza alikuwa Bwana Kibwana. Huyu alizaa naye watoto 3, wa kiume wawili na mmoja wa kike. Watoto hao ni:
(i) Jafari Kibwana
(ii) Mwanagani Kibwana (mwanamke)
(iii) Khatib Kibwana
Kipindi cha kabla ya Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia (1914-1918). Bwana Kibwana alisafiri kwenda Uganda na hakurudi. Hivyo Bibie Mwanamwema akajikuta hana mume, na ndipo alipoolewa na Bwana Selemani au Ufukwe bin Jumaa, au jina jingine Robert. Huyu alikuwa ni Myao Upande wa baba, na Mzaramo upande wa mama, na alipewa jina la “Robert” kwa heshima ya mkulima wa Kizungu ambaye baba yake, yaani Mzee Jumaa, alikuwa akifanyia kazi.
Mwanamwema alizaa na Bwana Ufukwe mtoto mmoja tu, yaani Shaaban Robert. Baadaye wakaachana. Hata hivyo, Bwana Robert alikuwa na watoto wengine kwa wake wengine, ambao ni:
(i) Jumaa bin Robert wa Ngamiani, Tanga
(ii) Abdallah bin Robert wa Mnyanjani, Tanga
(iii) Mwansaumu binti Robert wa Mnyanjani
Mume wa tatu wa Bibie Mwanamwema alikuwa ni Bwana Mwinyiulenge Mworogo. Huyu alizaa naye watoto 10-wasichana watano na wavulana watano-wafuatao:
(i) Mwishehe Ulenge (Mvulana)
(ii) Mwanaidi Ulenge (msichana)
(iii) Mwanang’andu Ulenge (msichana)
(iv) Yusufu Ulenge (Mvulana)
(v) Mwanahadia Ulenge (Msichana)
(vi) Asha Ulenge (msichana)
(vii) Mwidau Ulenge (msichana)
(viii) Issa Ulenge (mvulana)
(ix) Ali Ulenge (mvulana)
(x) Maimuna Ulenge (msichana) (mulokozi: 2002:3)
1.1.3 SHAABAN ROBERT
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 01 Januari 1909, (Wakati wa ujana wake Shaaban aliacha kuliandika jina la Roberts, akaanza kujiita Shaaban Robert), alipelekwa madrasa, shule itoayo mafunzo ya dini ya Uislamu na mama yake akiwa na umri wa miaka tisa. Huko alijifunza mambo mengi yahusuyo dini ya Uislamu kama vile Hadithi za Mtume Mohammad (ambaye ni Kiongozi wa Waislam). Alianza masomo ya elimu ya msingi mwaka 1922 katika shule ya msingi ya Kichwele (sasa inaitwa Uhuru mchanganyiko) iliyopo mjini Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka 13. Wakati huo, tayari alikuwa amekwishapata elimu ya dini kwa kiwango kikubwa. Aliendelea kusoma elimu hiyo ya dini hata alipokuwa anaendelea na masomo haya ya shule ya msingi. Alihitimu masomo hayo mwaka 1926 na kufaulu vizuri kwa kushika nafasi ya pili kati ya wanafunzi kumi na mmoja. Baada ya hapo, aliajiriwa na serikali ya kikoloni na kufanikiwa kushika nyadhifa mbalimbali. (Ponera 2010: 27).
1.2 KAZI ALIZOZIFANYA - Alianza na kazi ya Ukarani wa serikali Forodhani Pangani mwaka 1926-1944.
- Idara ya hifadhi ya Wanyamapori (Mpwapwa) mwaka 1944-1946.
- Alifanya kazi katika Afisi ya Mkuu wa Jimbo Tanga mwaka 1946-1952.
- Afisa wa kupima nchi Tanga (Idara ya ardhi) mwaka 1952-1960.
- Pia kabla hajastaafu mwaka 1960, aliwahi pia kuhamishiwa Old Moshi.
Alipokuwa kazini aliheshimika katika sehemu zote alizofanya kazi kutokana na adabu, bidii na uadilifu wake.
1.3 KIFO CHAKE
Shaaban Robert alifariki tarehe 20/06/1962 katika hospitali ya Mkwakwani Tanga, Bombo na kuzikwa tarehe 22/06/1962 katika makaburi ya ukoo wa mama yake yaliyopo hapo hapo Vibambani Tanga. Alifariki akiwa na miaka Hamsini na tatu (53).
Chanzo cha kifo chake kinatajwa kuwa ni kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika. Pia wengine wanataja kuwa ni kwa sababu ya homa ya Kifua Kikuu. Alilazwa katik hospitali hiyo kwa muda mrefu akianzia katika wodi ya Kawaida kisha alihamishiwa katika wodi ya wagonjwa mahututi. (Ponera 2010:29).
1.4 MAISHA YA NDOA
Mke wa kwanza wa Shaaban Robert alikuwa ni Amina. Alimuoa mwaka 1930/1931. Aliishi naye kwa miaka kumi tu ambapo walizaa watoto wengi lakini wengi walifariki wakiwa bado wachanga.
Amina anakadiriwa kufariki mwaka 1942 (Kutokana na shairi la Amina, kutungwa Juni 1942) na kumwachia watoto wawili, ambao ni Selemani na Mwanjaa ambao walipona dhidi ya mauti ya mapema. Kutokana na ubovu wa barabara na hali mbaya ya hewa, alishindwa kusafirisha mwili wa Amina hadi Vibambani hivyo alimzika huko huko Pangani.
Baada ya kufariki Amina shaaban alitunga tenzi za Adili na Hatia kwa ajili ya Wanawe, Mwanjaa na Selemani ili zisimame pahala pa marehemu mama yao kimalezi.
Shaaban Robert alikaa takriban miaka mitatu bila ya mke hadi tarehe 14/09/1945 alipomwoa Bi Sharifa binti Hussein wa Chumbageni Tanga, ambapo pia walizaa watoto wengi ambao pia walifariki wakiwa wachanga ambapo watoto wanne tu walipona ambao ni Akili, Hussein, Mwema na Ikibali.
Baadaye Ugane ulimvaa tena Shaaban Robert, ambapo mke huyu wa pili alifariki mwaka 1955. Baada ya kifo cha mke wake wa pili alioa mke wa tatu ambaye ni Bi. Mwanambazi binti Ali. Huyu hakuzaa naye na ndiye aliyemkalia eda mara tu baada ya kifo chake tarehe 20/06/1962.
1.5 MWONEKANO WAKE KWA JUMLA
Shaaban Robert alikuwa ni Mcha Mungu ambapo alikuwa Mwislamu aliyeyazingatia maamrisho na miongozo ya dini hiyo kama vile kusali sala tano na mengineyo.
Pia Shaaban Robert alipenda kufurahi nakushirikiana na watu katika kazi na shughuli mbalimbali za kijamii. Aliutumia muda wake mwingi kufanya kazi alizopanga na baada ya kazi alijikita katika kuandika.
2.0 KAZI ZA KIFASIHI ZA SHAABAN ROBERT
Shaaban Robert ni miongoni mwa waandishi maarufu na wakongwe wa fasihi ya Kiswahili ambao wamejizolea umaarufu mkubwa kutokana na kuandika kazi mbalimbali za kifasihi zenye kutumia ufundi na unadhifu mkubwa wa lugha ya Kiswahili. Miongoni mwa waandishi hao ni kama vile Amri Abeid Kaluta, Mathias Mnyampala, Ibrahim Hussein, Mohammed Said Abdulla, Penina Mhando na wengine wengi.
Shaaban Robert amejipatia sifa kubwa ikilinganishwa na waandishi wengine kwani ana sifa za kipekee/ upekee mkubwa unajitokeza katika vigezo vifuatavyo;
- Idadi ya kazi zake za kifasihi ni nyingi ikilinganishwa na waandishi wengine.
- Udhati, uendelevu na uhalisi wa maudhui ya kazi zake.
- Umaridadi wa ufundi wa uandishi wake.
Shaaban Robert ndiye mwandishi pekee aliyeandika na kuchapisha kazi nyingi zaidi za kifasihi ya Kiswahili kwa lugha ya Kiswahili (kazi zilizokwisha kuchapishwa mpaka sasa ni ishirini na nne 24).
Aliandika kazi zilizo katika makundi mawili ambayo ni Nudhumu na Nathari.
Kazi yake ya mwanzo kabisa kuchapishwa ni makala ya “Hirizi ya shilingi mia” ambayo ilitoka katika gazeti la Mambo Leo mwaka 1932. Baada ya hapo aliendelea kuandika kazi nyingi za ushairi na nathari katika Magazeti.
Kisha alitunga tawasifu yake “Maisha Yangu” (ambayo baadaye aliipanua na kuiita “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”).
Mwaka 1939 ilianza Vita vya Pili vya Dunia na kwisha 1945 wakati wote huo alitunga “Utenzi wa Vita vya Uhuru” wenye beti 3000. Baada ya utenzi huo alianza kutunga nathari kama vile Kufikirika, Kusadikika, Adili na Nduguze na kadhalika.
Hakuwahi kuandika kazi yoyote ya Tamthiliya (Ponera 2010).
1 KAZI ZAKE ZA NUDHUMU NI;
- Masomo Yenye Adili, (1959), Art & Lit, Nairobi.
- Utenzi wa Vita vya Uhuru (1961), Oxford, Nairobi.
- Kielezo cha Fasili, (1962), Nelson, Nairobi.
- Pambo la Lugha, (1966), Oxford, Nairobi.
- Insha na Mashairi, (1967), Nelson, Nairobi.
- Ashiki Kitabu Hiki, (1968), Nelson, Nairobi.
- Mapenzi Bora (1969) Nelson, Nairobi.
- Mwafrika Aimba, (1969), Nelson, Nairobi.
- Koja la Lugha, (1969), Oxford, Nairobi.
- Maisha ya Shaaban Robert, (1971), Nelson, Nairobi.
- Sanaa ya Ushairi, (1972), Nelson, Nairobi.
- Almasi za Afrika, (1972), Nelson, Nairobi.
- Tenzi za Maadili Mema na Omar Khayyam (1973), T PH, Dar es Salaam.
- 14.2.2 KAZI ZAKE ZA NATHARI
Kazi za nathari za Shaaban Robet zinajumuisha kazi za makundi yafuatayo;
(i) Barua.
(ii) Insha.
(iii) Hadithi Fupi.
(iv) Riwaya za Kiwasifu.
(v) Riwaya za Kitawasifu.
Sifa zilizotumika katika kutofautisha makundi haya (hususani hadithi fupi na Riwaya ni;
(i) Urefu (idadi ya maneno).
(ii) Uchangamano wa vitushi (sahili na tata).
(iii) Lugha iliyotumika katika nathari husika.
(iv) Wahusika (idadi).
(v) Dhamira (idadi na uzito).
(vi) Mandhari (ukubwa na upana-Jiografia, historia, wakati).
Nathari za Shaaban ni kama hizi zifuatazo;
- Adili na Nduguze, (1952), Mcmillan, Londoni.
- Kusadikika, (1951), Nelson, Nairobi.
- Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini, (1949), Nelson, Nairobi.
- Kielezo cha Insha, (1954), Witwatersand, Nairobi.
- Methali na Mifano ya Kiswahili, (1997), TUKI, Dar es salaam.
- Kufikirika, (1968), Oxford, Nairobi.
- Utubora Mkulima, (1968), Nelson, Nairobi.
- Siku ya Watenzi Wote, (1967), Nelson, Nairobi.
- Wasifu wa Siti binti Saad, (1967), Nelson, Nairobi.
- Barua za Shaaban Robert, (2002), TUKI, Dar es salaam.
2.3 UHALISI NA UBUNILIZI KATIKA KAZI ZA SHAABAN ROBERT.
Uhalisi ni ukweli wa jambo kama lilivyo, kuna ukweli wa aina mbili ambao ni;
(a) Ukweli katika hali halisi.
(b) Ukweli wa kisanaa (ambao husawiri mambo yaliyobuniwa na mtunzi).
Ubunilizi, ni utengenezaji wa ukweli wa jambo kadri afikiriavyo msanii kwa kuzingatia uwezekano na azma yake. Hivyo basi yafaa ubunilizi usipitilize kwani ni rahisi kwenda mbali na jamii halisi.
Vipengele ambavyo ubunilizi hufanywa ni kama vile;
(a) Mandhari. Kwa mfano katika kusadikika mandhari iliyotumika ni ya kubuni ambapo tunaona nchi ya kusadikika iko hewani inaelea, inamipaka sita ambayo ni Ardhini, Mbinguni, Mashariki, Magharibi, Kusini na Kaskazini.
(b) Wahusika. Ambapo wahusika katika kazi za Shaaban Robert wanauwezo na sifa maalumu. Kwa mfano wanasifa za aina moja tu, kama ni mwema tu au waovu tu. Kama ilivyo kwa Waziri Majivuno, Karama na kadhalika katika kusadikika. Pia wahusika hawa huundwa kwa sifa ya kutokukata tama kwa mfano karama katika Kusadikika. Vilevile wahusika wengine siyo binadamu ni majini kama wanavyojitokeza katika Riwaya yake ya Adili na Nduguze, kuna wahusika kama vile Mrefu.
© Lugha. Katika kipengele hiki cha lugha kuna matumizi ya Taswira na tamathali za semi ambapo kwa mwandishi huyu Shaaban Robert ameonesha umahiri wa hali ya juu katika kipengele hiki, kuitumia lugha ya Kiswahili.
(d) Ushikamani, katika kipengele hiki huweza kufanywa kwa kutumia mbinu kama vile;
(i) Ubadala mfano katika Adili na Nduguze hakumtaja sana jina la Mfalme Rai bali alimtambulisha kwa vibadala (majina mengine ya ziada).
(ii) Urejeshi/ Kisengere nyuma. Ni ile hali ya mwandishi kuelezea hadithi Fulani kwa kuanza mbele na kurejea au kulielezea tukio la nyuma (urejeshi). Kwa mfano msuko wa matukio katika nathari ya kusadikika.
(ii) Udondoshaji, katika Adili na Nduguze mwandishi ameidondosha habari ya mama yao Hasidi, Mwivu na Adili.
(iv) Uunganishaji/ ujumuishaji. Mfano katika kusadikika kuna vitushi vya Salii na Sapa, safari za Ndege Mangere na kadhalika (kitushi ndani ya kitushi).
Hivyo basi kazi za Shaaban Robert zina mseto wa uhalisi na ubunilizi ambapo kazi zake za mwanzo zina kiasi kikubwa cha ubunilizi. Mfano Kufikirika, Kusadikika na Adili na Nduguze. Ambapo ubunilizi huo unajidhihirisha katika kipengele cha Lugha, Mandhari, Wahusika na namna ya kushikamanisha vitushi vyake ambapo Shaaban Robert ametumia mbinu mbalimbali kama vile Utomelezi, Taharuki, Ujadi na kadhalika.
Kazi zake za uzeeni zina ukweli kwa kiasi kikubwa sana. Kwa mfano Utubora Mkulima na Siku ya Watenzi Wote.
MBINU ZA KIBUNILIZI KATIKA KAZI ZA SHAABAN ROBERT NI;
(i) Ujadi.
(ii) Ufutuhi.
(iii) Utomelezi.
(iv) Taharuki.
(I) MBINU YA UJADI
Ni utumizi wa kauli za Kiutamaduni, kauli zilizozoeleka sana na jamii katika matumizi yao ya kila siku.
Vipengele vya Ujadi ni kama vile, methali, misemo, tamathali za semi. Vilevile mtunzi huweza kuiga kaida maalumu za uzungumzaji ambazo hutumiwa na wazungumzaji wa jamii yake. Mbinu hii ya ujadi husaidia kumweka mtunzi karibu zaidi na hadhira yake.
(II) MBINU YA UFUTUHI
Ufutuhi ni hali ijengwayo na maneno, matukio au mazingira yoyote yenye mvuto au yasiyo ya kawaida yenye kuwafanya watu watabasamu au wacheke. (Ponera 2010:6).
Hii ni mbinu ambayo mtunzi hutumia maneno au hali nyingine inayoweza kusababisha hadhira yake kupata kicheko/ Ucheshi.
Mfano: Ufutuhi wa majazi katika “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”.
Mume ni mume ingawa gumegume ana sifa ya mtume;
Na mke ni mke ingawa kikwekwe ana manufaa yake. (uk 101).
Tukio hili linazungumzia umuhimu wa maisha ya ndoa kwa mwanadamu. Majina ya “Gumegume” na “Kikwekwe” yanamaanisha sifa za kutokusikiliza na hali ya kukosa utulivu wa kiakili na kimaadili ya ndoa (Ponera 2010).
(III) UTOMELEAJI
Ni kitendo cha kuchukua vipande vya kazi za utanzu mwingine na kuuingiza katika hadithi. Kwa mfano nathari ya Shaaban Robert ya “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”, utomeleaji umejitokeza kwa kiwango cha juu katika ukurasa wa 4-5 katika shairi la Amina, ukurasa wa 6-20 katika Utenzi wa HATI, ukurasa wa 21-35 Utenzi wa ADILI. Mbinu hii hutumika ili ku’nogesha kazi yake pia kutia msisitizo juu ya jambo Fulani.
(IV) TAHARUKI
Ni hali ya kuwa na dukuduku la kutaka kujua nini kitafuata katika usimulijia wa hadithi au riwaya. Mbinu hii mtunzi huitumia ili kuamsha hamu ya msomaji kufatilia kisa kinachosimuliwa katika riwaya au tamthiliya fulani. Mbinu hii Shaaban Robert ameitumia kama kijenzi kimojawapo katika utunzi wake. Imejitokeza kwa kiasi kikubwa katika kazi zake nyingi kama vile “Kufikirika”, ambapo tunaona namna alivyounda matukio yake kwa namna ya kutia hamasa kuendelea kufuatilia kisa kwa ukaribu zaidi. Katika Kufikirika tunaona alivyokijenge kisa cha Mfalme na Malkia kuwa matasa, nathari hii ina muundo ufuatao; Mwanzo, Mfalme, Waganga, Matokeo ya Utabili, Mtoto wa Mfalme, Kafara, Baraza na Gereza.
- MAWAZO AU MTAZAMO WA SHAABAN ROBERT KATIKA MAISHA
Mtazamo ni jinsi ya kuyatazama au kuyaona mambo na mwelekeo wake. Katika kazi za Shaaban Robert zinaonesha kuwa mwandishi aliandika kwa kugusia karibu kila Nyanja ya maisha ya mwanadamu. Baadhi ya mambo hayo ni ukombozi na maendeleo ya nchi, udugu na familia, mapenzi, dini, umuhimu wa elimu, utu, ujumi wa kiafrika na kadhalika.
3.1. UTU
Maisha ya binadamu pasipo utu, hukosa thamani. Baadhi ya maswali yanayoonekana kumshughulisha Shaaban Robert katika maandiko yake ni kama vile Utu ni nini? Utu hujengwa wakati gani? na utu hupatikanaje? Utu wa mtu hujengwa na matendo yake mwenyewe kila siku. Shaaban Robert alilijua vema suala hili na alilichukulia kwa hadhari kubwa kama asemavyo katika nathari yake;
Hapa Shaaban anasema; “Wakati mmoja nilifikiri kuwa yote yaliyo azizi au bora kwa mtu ni matendo yake aliyotenda zamani; na kwa kuwa mimi sikupata kutenda tendo lo lote la maana nilijiona sawa kabisa na maskini. Wazo hili lilibatilishwa na fikira kuwa pengine ubora wa mtu huwezekana kuwa katika wakati ujao”. (Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini: uk 1)
3.2 SHAABAN NA DINI
Shaaban Robert alikuwa Muislamu hivyo aliakikisha pia wote wanaomzunguka pia wanaelekea katika njia ya kidini, Shaaban aliamini kuwa dini ndio msingi wa amani duniani, mkwa mfano aliwahusia wanawe kushika dini katika Tenzi zake za HATI na ADILI.
Kwa mfano katika Utenzi wa HATI anamwambia Mwanjaa na Walimwengu wote kwamba;
27 Shikamana na ibada,
Kutimiza kila muda,
Na kesho ina faida,
Ikisha hii dunia.
28 Dini mali ya roho,
Mwilini kama joho,
Unapoteza uroho,
Na anasa za dunia. (Maisha Yangu na Baada Ya Miaka Hamsini, uk 10).
Pia katika kitabu hichohicho ukurasa wa 22 anamuhusia mtoto wake wa kiume Selamani juu ya umuhimu wa dini katika maisha yake.
Vilevile alisisitiza uhuru wa kuabudu (Siku ya Watenzi Wote, ukurasa 111), Dhima za dini (Siku ya Watenzi Wote, ukurasa 16 na 63), Unafiki katika dini (Siku ya Watenzi Wote, ukurasa 10, 36 na 102). Hivyo basi suala hili kwa Shaaban Robert aliliona ni la msingi na lenye umuhimu mkubwa katika maisha ya Mwanadamu akiwa hai hapa duniani.
Pia alitoa maonyo na maelekezo mengi kwa mdogo wake Yusufu Ulenge juu ya suala hili la dini. Katika barua yake ya tarehe 24/07/1931 aliyomwandikia Yusufu Ulenge anadhihirisha hilo. Barua hii ipo katika Barua za Shaaban Robert 1931-1958, barua namba 5 ukurasa wa 32.
3.3 SIASA NA UKOMBOZI
Dhamira halisi ya Shaaban Robert kupitia maandiko yake haikuupenda ukoloni wala wakoloni wenyewe. Wahakiki wengi wanamtazama Shaaban Robert kuwa na mawazo ya hali mbili, uchanya na uhasi kuhusu Ukoloni. Wapo wanomwona kama mpinga ukoloni. Wengine wanamwona kama alikuwa msaliti/ mwoga juu ya ukoloni.
Katika kazi yake ya “Utenzi wa Vita vya Uhuru”, tunaona Mawazo ya Shaaban Robert juu ya Ukoloni. Utenzi huu umezungumzia tukio zima la vita hivyo. Yeye alijiegemeza katika upande wa Waingereza kama asemavyo bayana katika “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini” ukurasa wa 64-65. Hapa Shaaban Robert anasema;
“…. Mimi si raia wa Jerumani, ni raia wa Uingereza…”.
Hili ni mojawapo ya mambo yaliyozua mjadala kwa wahakiki kuhusu Utanganyika wake, wanadai Shaaban Robert aliwatukuza wakoloni. Maudhui ya utenzi huu huenda yaliathiriwa na lengo lake la kumtabarukia Mudir wa Elimu wa kikoloni kipindi hicho Bwana S. N. Eliufoo.
Mbali na utenzi wa Vita vya Uhuru, Shaaban Robert amezungumzia ukoloni na siasa katika kazi zake za “Kusadikika” na “Kufikirika”. Shaaban amefafanua mengi kuhusu adha za Ukoloni na Wakoloni, kwa mfano katika Tawasifu yake ya “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini” ukurasa wa 50-51, anaeleza naman alivyobaguliwa yeye na watoto wake pale aliposhushwa kutoka katika Lori la Abiria cheo cha pili ili kuwapisha Wahindi waliokuwapo ambao walikosa sehemu ya kukaa kutokana na nafasi katika Lori hilo kujaa.
SHAABAN ROBERT NA SUALA LA JINSI NA JINSIA
JINSI, ni tofauti ya kimaumbile inayojidhihirisha katika via vya uzazi na hivyo kuwatofautisha watu katika makundi ya wanawake na wanamume.
JINSIA, ni dhana ya Kisosholojia. Hii inahusu mgawanyiko wa Majukumu baina ya Mwanamke na Mwanamume. - Shaaban Robert amelizungumzia sana jambo hili katika kazi zake zote. Katika Barua za Shaaban Robert, kuna waraka namba 11.9 katika ukurasa wa 196. Shaaban aliandika Waraka huu kwa Bwana mtengenezaji katika gazeti la Mambo Leo, aliupa jina la“UKIJUA KUOA NA KUACHA UJUE”’.
- Vilevile suala hili amelijadili sana kwenye kitabu chake cha “Wasifu wa Siti Binti Saad”. Siti ameonekana kuwa mfano mwema wa wake watakiwao Afrika ya Mashariki na Afrika kwa ujumla.
- Katika nathari yake ya “Kusadikika”, anasema; “…..hapana haja ya kudharau mwanamke. Wanawake ni Malaika, makao yao sawa na yale ya pepo…”
- Pia katika “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”, tunamuona jinsi alivyomsifu Amina ukurasa wa 3. Vilevile anaendelea kumchora kwa kumtetea mwanamke katika ushairi wake. Kwa mfano katika Utenzi wa HATI katika “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”, pia na katika “Pambo la Lugha” katika shairi lisemalo “Mwanamke si Kiatu” (uk 19). Hivyo basi kwa ujumla maoni na kilio cha Shaaban Robert katika suala hili tunapata katika kuchunguza kazi zake zote ambapo anawatetea na kuwalalamikia wanaume kuwa ni watesi na wanyanyasaji wa wanawake. Pia katika maandiko ya Shaaban Robert hakuna andiko hata moja linalomzungumzia mwanamke vibaya.
3.5 LUGHA
Shaaban Robert katika kipengele cha lugha anabainika kama Mwalimu na mtetezi wa lugha, hii ni kutokana na maudhui yanayopatika kutoka katika kazi zake mbalimbali alizozifanya. Kwa mfano katika kitabu chake cha “Insha na Mashairi”, kuna Insha mojawapo ya “Lugha ya Tifa” (uk 25). Katika “Siku ya Watenzi Wote” (uk 41) anasisitiza umuhimu wa mtagusano wa lugha hususani katika kufanya tafsiri.
Pia katika ‘Diwana ya Almasi za Afrika”, kuna shairi la “Kiswahili 1” na “Kiswahili 2’ (uk 59-60), pia shairi la “Kitakoma Kiswahili” (uk 65). Vilevile katika barua zake anajitokeza mara kadhaa kumkosoa Yusufu kuhusu tahajia ya Kiswahili. Katika kazi hizo Shaaban Robert anajitokeza waziwazi kufundisha, kukemea na kurekebisha unapotokea upotoshaji wa matumizi ya Kiswahili.
3.6 UJUMI NA KITAMBULISHO CHA MWAFRIKA
Ujumi ni hali/ taaluma ya masuala ya kutambua uzuri na au ufahamu wa kitu.
Shaaban Robert alikuwa Mwafrika, aliupenda Uafrika wake na mambo yote yaliyoambatana na hali hiyo. Ithibati za kuuthamini Uafrika wake inajitokeza katika kazi zake mbalimbali kama vile;
“Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini” uk 98-100, kupitia utenzi wa ADILI kajitambulisha kuwa yeye ni Mwafrika. Pia katika uk 50 anasema “…Abiria Waafrika tulikua mimi na watoto wangu…”
Pia katika “Wasifu wa Siti Binti Saad” anabainisha utamaduni na Falsafa ya mwafrika wa Kiafrika.
Majina ya Diwani zake “Almasi za Afrika” na “Mwafrika Aimba”, licha ya majina humo pia kuna mashairi yasemayo juu ya suala hili. Kama vile “Istaklahi ya Tanganyika” na ‘Fahari ya nchi yangu”. Hivyo Shaaban Robert ni Mzalendo wa dhati kwani katika kazi zake anaonesha hilo kwa kutete nchi yake na bara lake, rangi yake, utamaduni wake (Kiswahili alichokipenda ni sehemu ya utamaduni), Mila na Desturi zake, Vyakula vya Kiafrika pamoja na Wanawake wa Kiafrika.
3.7 SHAABAN ROBERT NA MAPENZI
Shaaban Robert amejadili kwa kina mapenzi katika vipengele vya maana halisi ya Mpenzi, aina za mapenzi, wapi kwa kuyapata mapenzi, mtazamo wake kuhuzu watu wanavyo ya chukulia mapenzi, faida na hasara za mapenzi.
Mapenzi anayoyajadili Shaaban Robert ni Pamoja na yale ya Kiumbe kwa Muumba wake, mzazi kwa mtoto au mtoto kwa mzazi, ndugu kwa ndugu, Ya ndoa, Jamii na Wananchi kwa nchi yao, Mapenzi ya dhati na ya chati. Katika diwani yake ya “Mapenzi Bora” suala hili la Mapenzi limejadiliwa kwa undani sana.
Mapenzi ya ndugu kwa ndugu tunayaona katika nathari ya “Adili na Nduguze”, ambapo Adili alikuwa akiwapenda sana ndugu zake Mwivu na Hasidi kiasi cha kuwagawia mali zake nusu kwa nusu pale walipofilisika.
4.0 ITIKADI YA SHAABAN ROBERT
Itikadi ya Shaaban Robert ni Usoshalisti uliopea, ijapokuwa si katika hali ya kuufikia Ukomunisti. Itikadi hiyo inasawiri hatua ya juu ya Usoshalisti unaoelekea kwenye Ukomunisti (Chuachua 2010: 180)
5.0 FALSAFA YA SHAABAN ROBERT.
Shaaban Robert anaamini kuwa wema hushinda dhidi ya ubaya. Hii inajidhihirisha katika kazi zake nyingi ambazo mwisho wake huonesha watendewao ubaya huwashinda waovu na kupata haki. Mfano kama inavyojidhihirisha katika Kusadikika, Kufikirika, Adili na Nduguze na kadhalika.
- MCHANGO WA SHAABAN ROBERT KATIKA FASIHI YA KISWAHILI.
Shaaban ni kiungo dhabiti baina ya fasihi ya kale na ya sasa. Shaaban Robert ni miongoni mwa waandishi wa mwanzo katika fasihi ya Kiswahili na waliotumia nguvu kubwa katika uandishi ilikuitoa fasihi ya Kiswahili sana sana utanzu wa nathari kutoka katika hali ya kihekaya na kuuingiza utanzu huu ili usawiri maisha halisi ndani ya jamii ya waswahili.
Shaaban Robert ni mmoja kati ya waasisi wa uandishi wa nathari za kitawasifu katika fasihi ya Kiswahili kupitia tawasifu yake ya “Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini”. Tawasifu hii yenye sehemu kuu mbili yaani “MAISHA YANGU” na ‘BAADA YA MIAKA HAMSINI”, inajumla ya kurasa 124. Katika sehemu ya kwanza ya Tawasifu hii (MAISHA YANGU), imebeba sehemu kumi na tatu (13) ambazo ni Umri, Maisha ya nyumbani, Utenzi wa Hati, Utenzi wa Adili, Mke wa pili, Idara ya forodha, Uhamisho, Mapumziko, Abiria cheo cha pili, Idara ya utunzaji wa Wanyama, Naondoka Mpwapwa, Idara ya Utawala na Nilikuwa mshairi. Sehemu ya pili (BAADA YA MIAKA HAMSINI), inasehemu zifuatazo Bima, Siasa, Mwandishi, Ukinzani, Kustaafu, Msuso, Upigishaji chapa na Matukio.
Shaaban Robert, pia ni mmoja kati ya waandishi waliochangia sana katika maendeleo ya nathari ya Kiswahili. Baadhi ya nathari bunilizi zake ni; Adili na Nduguze, (1952), Kusadikika, (1951), Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini, (1949), Kielezo cha Insha, (1954), Methali na Mifano ya Kiswahili, (1997), Kufikirika, (1968), Utubora Mkulima, (1968), Nelson, Nairobi. Siku ya Watenzi Wote, (1967), Nelson, Nairobi. Wasifu wa Siti binti Saad, (1967).
Alikuwa na mchango mkubwa, katika fasihi ya Kiswahili. “Wasifu wa Siti Binti Saad”. Ni moja kati ya nathari za kwanza kabisa za kiwasifu. Nathari hiyo inaeleza Maisha ya mwanamuziki mashuhuri wa Taarab Afrika ya Mashariki “Siti Binti Saad”.
Ndiye aliyeizindua hadhira ya kazi za fasihi ya Kiswahili kuhusu matumizi ya vionjo vya fasihi simulizi katika fasihi andishi.
Ni miongoni mwa waandishi wa wakati wake walioandika na kuchapisha kazi nyingi zaidi za fasihi ya Kiswahili.
HITIMISHO
Shaaban Robetr ni miongoni mwa wanafasihi waliyoiletea heshima kubwa tasnia ya fasihi ya Kiswahili. Kazi zao zimekuwa Lulu na mwongozo kwa wanafasihi wanaochipukia katika uga wa fasihi ya Kiswahili. Msimamo wake wakuwa mwanamapokeo ulikuwa ni msimamo wa wastani kwani sio wakati wote alizitumia kanuni za kimapokeo, alizitumia kanuni hizi pale ilipobidi na pale alipotaka kuziacha aliziacha.Vilevile Shaaban Robert kupitia kazi zake amewasaidia wanazuoni wengi kufikia malengo ya kielimu, waandishi wakongwe kama E. Kezilahabi ametumia nathari za Shaaban Robert katika tasnifu yake ya Shahada ya Uzamili.
MAREJELEO
Robert, S, (1949), Maisha Yangu na Baada ya Miaka HamsiniNelson, Nairobi.
(1951), Kusadikika, Nelson, Nairobi.
(1952), Adili na Nduguze, Mcmillan, Londoni.
(1954), Kielezo cha Insha, Witwatersand, Nairobi.
(1967), Siku ya Watenzi Wote, Nelson, Nairobi.
(1967), Wasifu wa Siti binti Saad, Nelson, Nairobi.
(1968), Kufikirika, Oxford, Nairobi.
(1968), Utubora Mkulima, Nelson, Nairobi.
(1997), Methali na Mifano ya Kiswahili, TUKI, Dar es Salaam.
(2002), Barua za Shaaban Robert, TUKI, Dar es salaam.
|
|
|
|