MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 101 online users.
» 0 Member(s) | 100 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  SHAIRI: HADITHI
Posted by: John John - 09-14-2021, 02:31 PM - Forum: Ushairi - Replies (2)

HADITHI

1. Mbiu ninawapigia, wa mbali mkaribie,
    Nia kuisimulia, hadithi muisikie,
    Yale yalotukia, na ninyi myatambue,
    Hadithi nahadithia, yale nilojionea.

2. Alikuwepo aazi, baba asiye na inda,
    Mwenye kupenda uwazi, si mambo yaliyopinda,
    Aliyeboresha makazi, familia ikampenda,
    Hadithi nahadithia, yale nilojionea.

3. Ilikuwa ni adhama, familiye kuongoza,
    Maana alijituma, hewani kuipepeza,
    Imara ikasimama, wema wakampongeza,
    Hadithi nahadithia, yale nilojionea.

4. Alivipenda vya ndani, kuliko ughaibuni,
    Vikaipata thamani, vilivyoonwa ni duni,
    Wageni wakatamani, wawenavyo dalihini,
    Hadithi nahadithia, yale nilojionea.
           
              ITAENDELEA....

Mtunzi: John L. John
          Mwanafunzi wa shahada ya kwanza ya elimu                katika lugha na utwala chuo kikuu Mzumbe.

Simu;  0788514751/0747225775.
Email: johnlucasjohn074@gmail.com

Print this item

  SHAIRI: SAFARI YANGU
Posted by: MwlMaeda - 09-13-2021, 11:12 AM - Forum: Ushairi - Replies (1)

SAFARI YANGU

1. Anongozile Mtume,
Na Masihi Mfalme,
Nitunge tenzi niseme,
Waisome nchi hizi. 

2. Ninakuomba Wadudi,
Masihi na Muhamadi,
Mnitieni juhudi,
Beti nitunge mashazi.

3. Beti mashazi mashazi,
Nizinene waziwazi,
Zenee habari hizi,
Wazaliwa na Wazazi.

4. Wazaliwa na Wazazi,
Wazisome wasihizi,
Kumbe tele kuzihozi,
Zenye raha na machozi.

5. Nataka niwambe waja,
Ingawa kwao si hoja,
Basi mie Mara moja,
Wakanipe masikizi.

6. Moyoni linanipwita,
  Nabaki kutwetatweta,
Kooni likinipita,
Moyo wangu tabarizi.

7. Katika maisha yangu,
Yalinifika machungu,
Nami niliwaza tangu,
Kueleza waziwazi.

8. Nitapata afueni,
Hadhira waelezeni,
Likibakia moyoni,
Laniletea maradhi.

9. Leo nimedhamiria,
Ili nibaki sawia,
Ya sadiri tawambia,
Kwa kina bahari zi.

10. Zi ndo kina bahari,
Nizitunge beti nzuri,
Na watunzi mashuhuri,
Wazisifu beti hizi.

11.

Print this item

  TAMATHALI ZA SEMI KATIKA FASIHI
Posted by: MwlMaeda - 09-13-2021, 09:48 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Tamathali za semi ni maneno, nahau au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii ili kutia nguvu katika maana, mitindo na hata sauti katika maandishi ama kusema. Wakati mwingine hutumiwa kama njia ya kuipamba kazi ya fasihi na kuongeza utamu wa lugha (Senkoro, 1984:13). Hii ina maana kwamba ili msomaji wa kazi yoyote ya fasihi apate ujumbe hana budi kufikiri kwa kina.
Pia tamathali za semi ni fungu la maneno lililogeuzwa maana yake kamili ili kiuwakilisha maana nyingine (Msokile, 1992:210). Akiwa na maana kuwa katika tamathali zipo maana na matumizi mengine ya kisanii ambayo msanii anapaswa kuyatumia ili aweze kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira.
Tamathali za semi ni viwakilisho au vifananisho vya dhana fulani kwa dhana nyingine tofauti zinazo fanana. Huu ni usemi unaobadilisha maana dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana maalumu ya fasihi iliyokususudiwa na msanii. (Mwamanda, 2008:42).
Kwa ujumla tamathali za semi ni maneno au sentensi ambazo hutumiwa na wasanii au waandishi wa kazi za fasihi ili kutia nguvu katika maana, mtindo na hata katika sauti za kusema au maandishi. Hutumika katika fasihi kwa lengo la kuipamba kazi ya fasihi na kuongeza utamu katika lugha iliyotumika katika kazi husika. Tamathali hizi huweza kugawanyika katika vipengele tofautitofauti kama vile tamathali za mlinganisho, tamathali za mafumbo, tamathali za msisitizo pamoja na tamathali nyingine za semi.
Vipengele vya tamathali za semi ni muhimu sana katika kuunda au kutoa msisitizo wa maana pamoja na kuunda maana mpya katika kazi za fasihi, vipengele hivyo huweza kufafanuliwa na kuweza kutumika katika kazi za kifasihi kwa namna tofautitofauti kama ifuatavyo:
Tashibiha au Mshabaha ni aina mojawapo ya tamathali za semi inayofanya kazi ya kulinganisha vitu viwili visivyo na hadhi sawa kwa kutumia viunganishi kama; mithili ya, mfano wa, sawa na kama vile. Mara nyingi aina hii ya tamathali za semi huweza kufanya kazi endapo tu pana vitu viwili vinavyolinganishwa, wakati kimoja hutumiwa katika kukirejelea na kuelezea kingine na aghalabu kimoja kati ya vitu hivyo huwa kinaeleweka na hivyo hutumiwa ili kuangazia hicho kingine. Mfano katika tamthilia ya    “Ngoma ya Ng’wana malundi” (Mbogo, 2008) anasema:
                              “Vizuu wanakula kwa kupokezana kama nguruwe au vichaa” (Uk. 18).
                              “Uso uliparama kama jiwe la kiama”  (Uk. 8).
Pia katika riwaya ya “Janga sugu la wazawa” ( Ruhumbika, 2001:88) anasema:
                                    “Basi siku hiyo hiyo Bugonoka alitambua hali hiyo mpya ya mama
                                      yake nayo pia ni sehemu ya janga lake na watu wake hapa
                                     duniani, sawa kabisa na kifo cha baba yake…………”
Kwa kutumia tamathali hii ya semi wasanii  wameshushughulikia mambo makuu matatu ambayo ni Kizungumzwa, Kifananishi na Kiungo. Kizungumzwa ni kitu halisi ambacho huzungumzwa na kitu kinachofananishwa kwa fumbo, kifananishi kipo katika mawazo na huzingatia maana dhahania na kiungo ni sifa zipatikanazo katika kitu kinachozungumzwa. Kazi yake kuu ni kuhusisha vitu vyote viwili katika kuunda maana kama inavyoonekana katika mifano hapo juu.
Takriri ni aina nyingine ya tamathali za semi ambayo yenyewe huhusika na urudiajirudiaji wa maneno, silabi  au sauti zinazolingana katika kazi ya sanaa. Mwandishi huamua kwa makusudi kurudirudia maneno au vipengele hivyo kwa lengo maalumu kwa kusisitiza jambo ama kuleta mkazo wa jambo linaloelezwa (Msokile, 1992:61). Kwa mfano, katika riwaya ya “RosaMistika ” (Kezilahabi, 1971:67) takriri inaonekana kama ifuatavyo:
                                                                “Rosa, Rosa, Rosa, mtoto wangu, mimi ninakufa.
                                                                 Njoo karibu nikuguse, njoo nikupe baraka yangu
                                                                 ya mwisho.”
Pia katika tamthilia ya “Nguzo Mama” (Muhando, 2007:13), takriri inajitokeza  kwa kutumia walevi waliosema,
              “Tia lijae
                Hilo kimbo
                Tia lijae
                Sio nusu
                Tia lijae.”
Na katika tamthilia ya “Chuano” (Paukwa Theatre Group, 1995:8) wanasema,
                “Paukwa
                  Pakawa
                  Paukwa
                  Pakawa
                  Paukwa
                  Pakawa.”
Katika mfano wa kwanza na wa tatu msanii ametumia takriri ili kumwandaa msikilizaji awe makini kusikiliza jambo linalotaka kuzungumzwa ili hali mfano wa pili umetumiwa kusisitiza juu ya utendaji wa jambo fulani.
Matumizi ya tafsida ambayo ni miongoni mwa tamathali za semi hupunguza makali ya maneno au matusi katika usemi. Pia, hutumika hasa katika makundi ya watu wenye umri tofauti lengo likiwa ni kulinda haiba ya watu fulani (Ntalangi:2004). Katika riwaya ya “Mzingile”(Kezilahabi, 1991:132), msanii ametumia tafsida ifuatayo:
              “Hata baada ya kumwingilia mkewe bado tu ilibidi aendelee kuwaza
                hao wasichana dogodogo zake wa nje, la sivyo mkia wake
                unaanguka!”
Pia katika tamthilia ya “Orodha” (Reynolds, 2006:1), tafsida mojawapo ni;
                “Akipiga hatua mbele kwa huzuni, Ningependa kusema maneno
                 machache kuhusu furaha, binti yangu aliyetutoka.”
Katika mfano wa kwanza msanii amewasilisha dhana ya uboo kwa kutumia neno mkia. Vile vile neno aliyetutoka katika mfano wa pili limetumiwa kujenga dhana ya kifo.
Mdokezo ni tamathali ambayo hudokeza kitu fulani na kukiacha bila kukikamilisha kwa maana ya kwamba kinaweza kukamilishwa na mtu mwingine kisanaa (JPO Compony, 2008:45). Katika tamthilia ya “Orodha” (Reynolds, 2006:9) mdokekezo umejitokeza katika sehemu mbalimbali kama vile;
                 “Ndiyo……….ndiyo…………mwanangu……….endelea…….
                   Bwana huyaona yote……….lengama.”
Pia katika riwaya ya “Rosa Mistika” (Kezilahabi, 1971:57) mdokezo imedhihirika kama ifuatavyo;
                 “Wanawake wafupi………….wanawake warefu………………
                   Jinsi ya k………….namna ya kumfahamu mvulana …………
                   Namna ya kuweza kuzaa mtoto wa kiume au kike…………
                   Stahili zifutazo……………
Mara nyingi msanii wa kazi za fasihi atumiapo mdokezo katika kazi yake anakuwa na lengo la kumfikirisha msemaji  au hadhira juu ya jambo analolizungumza. Hivyo ni jukumu la hadhira kufikiri na kukamilisha wazo la msanii katika kazi yake ya kifasihi.
Tamathali za semi ambazo ni tashihisi huitwa fasili ya binadamu kwani katika tamathali hii vitu visivyo na sifa na uwezo wa kutenda kama binadamu hupewa sifa na uwezo wa kutenda kama anavyoweza binadamu. Katika riwaya ya “Vuta N’ Kuvute”(Shafi) tashihisi zinazojitokeza ni kama;
                  “Nuru ya jua iliingia kwa hamaki” (Uk. 49)
                  “Upepo ulikuwa unabishana nao”  (Uk. 225).
Pia katika riwaya ya “Almasi za Bandia” (Chachage, 1991:30) tashihisi zilizotumiwa na msanii huyu ni kama vile;
                   “Alimtazama Yakini kwa yanayocheka” ( Uk. 30).
Vile vile katika riwaya ya “Mfadhili” (Tuwa), tashihisi mojawapo iliyotumiwa na msanii huyu ni:
                  “Midomo yake ilikuwa inamtembea polepole” (Uk. 14).
Mara nyingi msanii anatumia tashihisi kuvutia msomaji na kukwepa kuweka wazi maana au wazo kiurahisi kwani si kila kazi ya fasihi inatakiwa kueleweka kiurahisi nyingine zinahijaji fikra za msomaji au mtizamaji kuweza kubaini baadhi ya mambo baada ya kufikiri na kuchambua kwa kina juu ya kazi hizo za kifasihi. Pia, msanii hutumia tashihisi ili kukwepa wimbi la udhibiti katika kazi yake.
Sitiari ni tamathali ya semi ambayo iko sawa na tashibiha lakini hulinganisha vitu ama watu lakini bila kutumia viunganishi linganishi vya mithili ya, sawa na, kama na kama vile. Hivyo katika tamathali hii vitu au watu hulinganishwa na vitu au watu wengine kana kwamba vitu na watu ni sawa kabisa. Waandishi mbalimbali wa kazi za fasihi wametumia sitiari kama ifuatavyo:
Katika Tamthilia ya “Chuano” (Paukwa Theatre Group) wanafasihi hawa wameweza kutumia sitiari kama ifuatavyo:
                “Tofauti kati yangu na maua ilikuwa haipo” (Uk. 48).
Aidha katika tamthilia ya “Nguzo Mama” (Mhando,2007:39), ametumia sitiari mbalimbali ambazo zimefanya kazi ya kusisitiza maana aliyokusudia. Kwa mfano:
                “Mbwa mume wako anayefuata wanawake ovyo.”
Wakati katika tamthilia ya “Chuano” (Paukwa Theatre Group) sitiari ambazo zimejitokeza ni pamoja na:
                 “Dunia ni kimbunga hung’oa nyumba zenye misingi nya mwamba”
                 “Dunia ni jinamizi hutia hofu unapostarehe usingizini”( Uk. 43).
Hivyo lengo kuu la wasanii wa kazi za kifasihi kutumia sitiari katika kazi zao ni kuonesha uhusiano au ulinganisho wa vitu na watu tofautitofauti katika kujenga uzito wa maana.
Katika tamathali mjalizo kunakuwa na mfuatano wa maneno katika sentensi yasiyo na viungo vyovyote (Senkoro 1984:19). Hivyo mjalizo ni maneno ambayo huweza kutajwa kwa mfululizo ambayo huunganishwa kwa alama ya mkato. Wasanii mbalimbali wametumia mjalizo katika kazi zao kama ifuatavyo;
Hussein katika tamthilia yake ya “Mashetani” ametumia mjalizo katika kazi yake kama vile:
          “Mimi shetani, ninajenga, ninabomoa, ninatukuza” (Uk. 1).
Hivyo mjalizo hutumiwa kwa lengo la kuifanya kazi ya sanaa ivutie na kuwa na uzuri wa kipekee na wa kisanaa ambapo msanii hutumia na kuifanya kazi yake kuwa ya kushawishi. Kwa kutumia maneno yanayofuatanafuatana kwa mfululizo bila kutumia viunganishi.
Nidaa ni msemo ambao huonesha kushangazwa kwa jambo fulani. Misemo hii huambatana na matumizi ya alama za  mshangao katika kukubali jambo, kuchukia au kuonesha heshima maalum (Msokile, 1992:63). Katika tamthilia ya “Nguzo mama”  Muhando (2007:12), nidaa imejitokeza sehemu mbalimbali kwa mfano pale Tololo alipokuwa anacheka:
            “Lo! hata na wewe Bi pili siku hizi unapika pombe, lo!
Pia katika tamthilia ya “Kaptula la Marx”(Kezilahabi,1999:2) nidaa mojawapo iliyojitokeza ni:
            “Aaa! Tayari! Nimetoboa tobo! ( Uk. 2).
Waandishi wa kazi za kifasihi hutumia nidaa kwa lengo la kuonesha kushangazwa au kushangaa juu ya mambo mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya wahusika. Mshangao huo ndio unaosisitiza maana husika.
Ritifaa ni tamathali ya semi ambayo mtu huzungumza na kitu au mtu asiyekuwepo ambapo mtu huyo husikiliza maongezi hayo katika fikra tu. Kwa mfano mtu anapoongea na mtu aliyekufa katika tamthilia ya “Janga Sugu la Wazawa” (Luhumbika, 2001:110) anasema:
         “Bugonoka, badala ya kulala na kujipumzisha kidogo alijikuta
           akiongea na ndugu zake wa ahera: Mama na baba mmeniona leo!
           Kazi yangu nimemaliza. Niko tayari sasa, siku yoyote kuja kujiunga
           nanyi. Nimemaliza kazi mliyoniachia. Mjukuu wenu nimemfikisha
           kwenye maisha tuliyokuja kumtafutia……………….”
Wasanii hutumia ritifaa ili kufikisha ujumbe kwa hadhira ambapo huonesha maisha halisi ya binadamu katika dunia akilinganisha na maisha ya ahera.
Taniaba ni tamathali nyingine ya semi ambayo jina la mtu binafsi hutumiwa kwa watu wengine wenye tabia, mwenendo, hali au kazi sawa na ya mtu huyo. Kwa mfano jina la Osama humaanisha mtu gaidi. Hali kadharika katika kazi za fasihi waandishi wametumia taniaba katika kazi zao kwa mfano katika riwaya ya “Almasi za Bandia” (Chachage, 1991:3) anasema:
            “Daktari David Livingstone, yule mmishenari aliyejitanguliza Afrika
             karne iliyopita kama Yohana mbatizaji.”
Tabaini ni usemi unaosisitiza jambo kwa kutumia maneno ya ukinzani mfano, Amekuwa mrefi si mrefu, mfupi si mfupi wa kadri. Katika tamthilia ya “Pambo” (Muhando, 1982:2), taniaba imejitokeza kama ifuatavyo:
           “Hivyo ninajua huna hela lakini leo ninakuambia tutakwenda
             upende usipende.”
Katika mfano huu tabaini imetumika kusisitiza utendaji katika tamthilia, ukilenga zaidi mtu asipuuzie jambo au kile anachoelezwa katika kukitenda au kukifanyia maamuzi kulingana na maelekezo yanayotolewa.
Taashira nacho ni kipengele cha tamathali za semi ambapo jina la sehemu ya kitu kimoja au la kitu kidogo kinachohusiana na kingine kikubwa hutumiwa kuwakilisha kitu kamili
(Senkoro, 1982). Kwa kutumia tamathali hii msanii huunda maana mpya kabisa, kwa mfano jembe hutumika kuwakilisha mkulima, Ikulu huwakilisha rais na kiti huwakilisha kiongozi. Katika diwani ya “Mloka” (Mloka, 2002:10) shairi la “Ardhi ujitizame”, msanii anasema:
                                 “Jembe bado nainama, sijatulia kulima,
                                  Ardhi ukae vema, ni japo sina huruma,
                                  Unainuuma intima, uliponiaja nyuma,
                                  Kila nilipo kufuma, meniacha nayoyoma,
                                  Umenitupia homa, augue hata mama,
                                  Jembe nitakaporejea, ardhi ujitazame.”
Hata katika jamii ya leo watu hutumia taashira katika mazingira mbalimbali kwa mfano hutumia neno pete kuwakilisha ndoa.
Tamathali nyingine ni ile ya mwigo ambayo hujikita zaidi katika kuiga sauti au milio mbalimbali katika kazi za fasihi. Mwanafasihi huwa na juhudi ya kujaribu kuiga kitu kama kinavyosikika katika mazingira ya kawaida. Aidha mwigo hujenga uhalisia wa kile wanachozungumzia (Msokile,1992). Tamathali hii imetumiwa na wanafasihi mbalimbali katika kazi zao kama vile katika riwaya ya “Usiku Utakapokwisha” iliyoandikwa na Msokile, anasema:
           “ Kree………………..kiti kikavutwa ( Uk. 14)
           “ Mya!mya!mya! sauti kali ya paka ilisikika juu ya paa” (Uk. 2)
           “ Akapiga ko……ko………ko……………(Uk. 16).
Katika tamthilia ya “ Kivuli kinaishi” iliyoandikwa na Mohamed tanakali sauti kadhaa zimetumika ikiwa ni pamoja na;
          “ Ha…….ha…….haaaaaaaa! (Uk. 59)
          “ Ha…….ha,ha…….ha,ha,ha,ha! ( Uk. 74)
           “ Bi Pili aliingia na vigelegele lululululululu! (Uk. 13)
           “ Bi moja aliingia na vigelegele Ai ai ai ai ai ai ( Uk. 2).
Msanii hutumia maneno yanayoiga sauti ya kitu fulani akiwa na lengo la kuburudisha au kuipa dhamira uzito fulani wa dhana na kuvuta usikivu.
Mubaalagha ni tamathali ya semi ambayo hutia chumvi katika maelezo yanayofanywa katika kazi ya sanaa hususani hadithi fupi ( Msokile 1992:56). Kimsingi tamathali hii husisitiza maana ya jambo linalozungumzwa. Wanafasihi hawako nyuma katika kuitumia kama inavyoonekana katika kitabu cha “ Misingi ya Hadithi fupi” ( Msokile, 1992:56) msanii anasema:
           “ Uso wake ulikuwa na mito ya machozi ya uchungu baada ya mume
              wake kushikwa na askari wa usalama wa taifa”
           “ Mwangalie alivyo na mlima wa matiti! Amebeba mzigo wa matiti.”
Vilevile mubaalagha umejitokeza katika tamthilia ya “Kaptula la Marx” (Kezilahabi, 1999:21) anasema:
          “Waziri wa mambo ya ndaniSadAkimvua Rais viatu vya matairi)
                                                          Siwezi kukutupa chama kimo katika
                                                          damu yangu.”
Pia, katika tamthilia ya “Ngoma ya Ngw’anamalundi” (Mbogo, 2008:35), kuna mubalaagha uliojitokeza kama vile:
            “CHIBUPA: Seche nikiziona nguo hizi moyo wangu unatirirka sumu
                                 ya mapenzi na utengano.”
Lengo la tamathali hii ni kufurahisha, kuchochea, kuchekesha au kusisitiza hoja. Hoja hizi mara nyingi zinaweza kuibua hisia za kuchoma moyo, kuchochea furaha na huzuni kama ilivyoonekana kwenye mifano ya kazi za fasihi hapo juu.
Tashititi ni mkazo wa maneno yasemwayo ama kuandikwa. Msanii hutumia mbinu za kuuliza maswali kwa jambo ambalo anafahamu jibu lake. Lengo ni kusisitiza jambo, kuleta mshangao (Msokile 1992:62). Katika tamthilia ya “ Nagona” (Kezilahabi, 1990), kuna tashititi ambazo zimejitokeza ikiwa ni pamoja na:
              Baba akimwangalia padri usoni aliuliza “Tumejuliana hali?”
              Padri alikaa kimya, wazee wote walimtazama “Je ulitaraji
              sisi sote hapa tukusalimu wewe kwanza?”
Aidha katika “Diwani ya Mloka” (Mloka, 2002:65) anasema:
                          “ Kweli amekufa kweli?
                            Watu walizua swali
                            Na huku wakijadili
                            Ajali ilivyokuwa”
Katika maswali yote yaliyoulizwa katika mifano hapo juu ni wazi kuwa majibu yake yanafahamika vyema kwa yule anayeuliza maswali hayo. Jambo la msingi linalooneshwa na  msanii ni msisitizo utakaotokana na kujibiwa kwa maswali hayo.
Kwa ujumla tamathali za semi zinamchango mkubwa katika kukamilisha kazi za kifasihi kwani hutumika kuunda au kusisitiza maana au kuunda maana mpya huku ikiwafanya wasomaji au watazamaji wahamasike kusoma au kusikiliza kazi husika.
MAREJELEO
Chachage, C.S.L (1991), Almasi za Bandia, Dar es Salaam University Press, Dar es Salaam.
Hussein, E. (2004), Kwenye Ukingo wa Thim, Oxford University Press, Nairobi.
Kezilahabi, E. (1990), Nagona, Dar es Salaam University Press, Dar es Salaam.
Kezilahabi, E. (1991), Mzingile, Dar es Salaam Unoversity Press, Dar es Salaam.
Kezilahabi, E. (1999), Kaptula la Marx, DUP Ltd, Dar es Salaam.
Mbogo, E (2008), Ngoma ya Ng’wana Malundi, Nyambari Nyanwine Publishers, Dar es Salaam.
Mloka, C. (2002), Diwani ya Mloka, Mkuki wa Nyota Publisher, Dar es Salaam.
Muhando, P. (1982), Pambo, Swala Publication, Dar es Salaam.
Muhando, P. (2007), Nguzo Mama, Macmillan Aidan Ltd, Dar es Salaam.
Msokile, M. (1992), Misingi ya  Hadithi Fupi, Dar es Salaam University Press, Dar es Salaam.
Mwamanda, J. (2008), Nadharia ya Fasihi Uchambuzi na Uhakiki, JPD Company & General Supplies Ltd, Da es Salaam.
Reynolds, S (2006), Orodha, Macmillan Aidan Ltd, Dar es Salaam.
Ruhumbika, G. (2001), Janga Sugu la Wazawa, E & D Limited, Dar es Salaam.
Senkoro, F.E.M.K, (1982), Fasihi, Press and Publicity Center, Dar es Salaam,

Print this item

  SHAIRI: KISWAHILI KINAFAA, KUJENGA JAMII PANA
Posted by: MwlMaeda - 09-11-2021, 10:34 PM - Forum: Ushairi - Replies (1)

KISWAHILI KINAFAA, KUJENGA JAMII PANA
*****************************************************
1.
N'napofanza utunzi, Mola unigee mwanga.
shukurani Mwenyienzi, nudhumu hini kutunga.
Lugha hino naienzi, ni ulimi unaunga,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
2.
Kiswahili lugha hii, ni gundi yaunga nyufa,
za kitaifa jamii, hata za kimataifa.
Inaunga dini hii, makabila na taifa,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
3.
Dini zawasiliana, kupitia Kiswahili,
makabila hukutana, yakiwamba Kiswahili.
Wanasiasa hunena, kutumia Kiswahili,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
4.
Na inavuka mipaka, lugha hini laazizi.
hadi ndani Afurika, 'mekita yake mizizi.
Duniani kadhalika, ina wengi watambuzi,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
5.
Mathalani Ujapani, Uchina na Marekani,
Uingereza Irani, aidha Ujerumani,
wana vipindi makini, vya Swahili redioni,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
6.
Ni ulimi watumika, jamii kusitawisha,
biashara 'kifanyika, watu kuwaendelesha.
Rahisi kueleweka, ujumbe kuwasilisha,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
7.
Ni ulimi muafaka, kuitafuta amani,
aidha unatumika, kuileta burudani,
nyimbo ze zinapendeka, hadi mbali Marekani,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
8.
Kula mpenda umoja, m'endeleo na amani,
Kiswahili ana haja, kwa sana kukithamini.
Tangia huko Ngadzija, Unguja na Mwambaoni,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
9.
Hata bara twaafiki, waamba ulimi huu,
Afurika Mashariki, kote Maziwa Makuu.
Lugha hii nahakiki, ndiyo ulimi mkuu,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
10.
Nitumie hu' wakati, kuwaenzi washairi,
Shabani bin Robeti, aliyekuwa mahiri.
Nawakumbuka kwa dhati, washairi walopita,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
11.
Napaswa nimuhongere, aliyetazama mbali,
Hayati baba Nyerere, alikuza Kiswahili.
Mchango wake si bure, wasifu asitahili,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.
12.
Nawatakia baraka, na wa Mola ufadhili,
Washairi watukuka, kwendeleza Kiswahili.
Kalamu chini naweka, hatima ya tungo hili,
Kiswahili kinafaa, kujenga jamii pana.

*******************
Rwaka rwa Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda)
JImbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,RWANDA.

Print this item

  SHAIRI: NAJUA HUJUI
Posted by: MwlMaeda - 09-11-2021, 09:00 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NAJUA HUJUI

Ewe wangu buibui, mtanda wa roho yangu,
Najua hautambui, ijapo jambo la tangu,
Uvaapo baibui, huwa na furaha chungu,
Najua kuwa ujui, ukongavyo moyo wangu.

Usione ni ajabu, leo kuweka bayana,
Haki hunitoka tabu, na moyo huwa mwanana,
Unapovaa nikabu, mie hufurahi sana,
Najua kuwa ujui, ukongavyo moyo wangu.

kijana mie labibu, nitake nini zaidi,
Ikiwa wewe sababu, ya moyo kuwa baridi,
Unapovaa hijabu, furaha inanizidi,
Najua kuwa hujui, ukongavyo moyo wangu.

Tamati hapa mwenzio, tambua unaniweza,
Zidisha mazingatio, stara sijeteleza,
Ayi! Yako mitandio, furaha huiongeza,
Najua kuwa hujui, ukongavyo moyo wangu.

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi @gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.

Print this item

  FASIHI YA KISWAHILI NA FASIHI KWA KISWAHILI IPI NDO IPI?
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2021, 06:22 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

FASIHI YA KISWAHILI NA FASIHI KWA KISWAHILI IPI NDO IPI?
Upo mdahalo ambao umezuka baina ya wahakiki wa fasihi ya Kiswahili kuwa kuna fasihi ya Kiswahili na fasihi kwa Kiswahili.
Washikilizi wa mtazamo huu aghalabu ni wahakiki na waandishi wa fasihi walio na usuli wao uswahilini. Wanadai kuwa fasihi ya Kiswahili  ni kazi zilizoandikwa na waswahili.Waswahili;kwa maana ya wazawa wa tumbo la waswahili au zinazozungumzia utamaduni wa mswahili na lugha ya Kiswahili,wanalosisitiza ni kuwa fasihi ya Kiswahili ni zao la mswahili na wala si Mswahili na kutokana na mtazamo huu wamezuumu kuwa fasihi ya Kiswahili inahusisha riwaya kama vile riwaya ya Kurwa na Doto, Mashairi ya Mwanakupona binti mshamu, kazi ya Mohammed Mwengo (takhmisa ya Liyongo) mashairi ya Said al Nasir (Utenzi wa Al Inkishafi) Utenzi wa Fatuma, mashairi ya Muyaka bin Haji, mashairi ya Mwanalemba, mashairi ya Hasan Maalim Mbega, tungo za Ahmed Sheikh Nabhany  miongoni mwa mengine.
Kwa upande mwingine fasihi kwa Kiswahili ni kazi zote zinazosimuliwa kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Mradi kazi imeandikwa kwa Kiswahili ni fasihi ya Kiswahili hata  ingawa haizungumzii tajriba za mswahili.
Mdahalo huu unanifanya niichokonoe tafakuri yangu na kuuhusisha na matukio yaliyojiri katika kongamano la chakama afrika mashairi kule Kigali aliposimama mhadhiri mmoja kutoka unguja na kuwaasa maulamaa wasio na unasaba uswahilini kuwa, kabla ya kuuamua au kutafutia lolote kuhusu Kiswahli wawaulize waswahili mwanzo.
Swali tunaloweza kuibua hapa ni je, mswahili ni nani? na nani mwenye Kiswahili? Je, kijelezi mwafaka cha dhana mswahili, mswahilina, na Kiswahili ni kipi?
Kamusi na wanaisimu wa Kiswahili hawajaweza kutoa tafsili toshelezi inayoeleza dhana hizi na kuzibainisha kinagaubaga. Tafsiri zilizotolewa zinaonesha ukuruba wa karibu mno ulioko katika dhana hizi.
Aidha nadharia na nadharia tete zinazojaribu kubainisha unasaba wa Kiswahili na mswahili zimekuwa na upungufu makubwa. Kwa hiyo wanaisimu wa lugha hii wameishia kuzuumu kuwa Kiswahili sawa na lugha zenza za kiafra ni zao la mamelugha Bantu. Hii ni kutokana na ithibati za kiisismu zilizodhihirishwa na Prof. Malcom Guthrie.
Kutokana na misingi hii hatuwezi kubainisha fasihi ya Kiswahili na fasihi kwa Kiswahili kwa sababu mwanzo dhana ya mswahili na Kiswahili haijatolewa tafsiri maalum wala usuli wa kubainishwa kikamilifu.
Jamii hubadilika kutokana na mitagusano na maingiliano na jamii zenza, kwa hiyo waswahili sawia na jamii yoyote ya kiafrika wameweza kuingiliana na jamii zenza kama vile kimijikenda, kipokombo, kitaita, kiarabu na kadhalika hivyo basi kuufumbata utamaduni badalia kwa sasa hivi tunapozungumzia mswahili, tunamzungumzia mwafrika mkengeushi katika karne ya ishirini na moja. Je, kazi zinazozungumzia maudhui ya mabadiliko ya mwafrika katika karne hii  tutazipuuza na kudai kuwa ni fasihi kwa Kiswahili kwa misingi kuwa hazizungumzii utamaduni wa mswahili? Je, mswahili bado hajabadilika? Na lugha ya Kiswahili, je imebadilika? zipo kazi za riwaya kama vile Safari ya Lamu na Prof. John Habwe inayozungumzia utamaduni wa mswahili katika mazingira ya Kiswahili. Riwaya hii imesawiri pia matumizi ya lahaja za uswahilini katika miktadha au maeneo mbalimbali kwa mfano mhusika anapokuwa Mombasa, Lahaja inayotamalaki ni kimvita lakini anapofika lamu kiamu kinashika usukani. Je, tutaipuuza kazi hii na kudai kuwa si fasihi ya Kiswahili kwa sababu Prof. Habwe ana usuli wake bara licha kwamba kazi hii inaakisi utamaduni wa mswahili katika mazingira ya uswahili.
Prof. Keni Walibora vilevile na siku njema anawatumia wahusika kama vile Zainabu Makame, Kongowea Mswahili, Vumilia binti Abdalla, Seleman Mapunda, Rashid Mpenda Raha ambao majina, uhusika na utamaduni wao ni wa uswahilini mandhari ambayo inatamalaki  katika riwaya hii ni Tanga Tanzania ambapo watu wanazungumza kwa lahaja ya kimtang’ata na Mombasa ambapo kimvita kimeshitadi. Hivyo basi je ni sahihi kusema kuwa hii si fasihi ya Kiswahili kwa kuwa mwandishi ni mzawa wa bara na wala hana mizizi uswahilini?.
Isitoshe mifano waliyotoa hapo juu ya riwaya ya Kurwa na Doto ya M.S. Farsay, Utenzi wa Mwana kupona, Utenzi wa Al-inkishafi imejiegemeza mno uarabuni na kujengwa kwa kaida za uislamu kwa hiyo haiakisi mia fil mia utamaduni wa mswahili ambao ni utamaduni wa mwafrika.
Aidha waandishi wengi na wahadhiri wanaoendeleza fasihi ya Kiswahili k.m Keni Walobora, E. Kezilahabi, Shabaan Bin Robert, Faraji Katalambula, K.W.Wamitila, Kethaka Wa Mberia, Prof. Senkoro, Mugyabuso Mulinzi Mulokozi, Kimani Njogu, Rocha Chimera, Chacha Nyaigoti Chacha, Joram Kiango na wengi wanausuli wao bara. Je, kazi zao si fasihi ya Kiswahili kutokana na unasaba wao?
Kwa mtazamo wangu ninaweza kusema kuwa wahakiki wa mtazamo huu ni wale waliozua nadharia tete kuwa Kiswahili kilitokana na kiarabu kwa kutaka kujinasibisha na uarabu na kuukwepa uafrika. Hivi ndivyo inavyodhihirika katika uteuzi wao wa kazi wanazoziita Fasihi ya Kiswahili zile zilizokitwa kwa misingi ya dini ya kiislamu na utamaduni wa uarabuni zimependelewa zaidi.
Swala hili la watu kutaka kusawiriwa waswahili zaidi ya  wengine au kukimiliki Kiswahili na kuwaponza watumizi wenza wa Kiswahili si geni katika jarida la taifa leo, yupo mshairi  mmoja maarufu aliyedai kuwa “Kiswahili ni cha wa pwani, wa bara mwakinyapia tu”
Kwa mujibu wa mada hii matumizi ya “ya” na “kwa” ni ujanja wa kisarufi unaonuia kuzua ubaidi na kuendeleza ukiritimba katika fasihi ya kiswhili na wala si fasihi kwa Kiswahili.
Kwa mujibu wa makala haya dhana  ya utambulisho itafaa mno katika kumtambua mswahili hususan katika karne hii ya ishirini na moja ambapo Kiswahili kimejitanua na kujizagaza kimawanda kwa hiyo kuizua jamii na jamiilugha mpya..misingi miwili mikuu ya kinadharia ambayo ni nadharia ya ujumuishi ya Giles (1979) na nadharia ya makutano na maachano (1982) itatupa dira na mhimili katika mdahalo..aidha nadharia ya ujumi mweusi wa kiafrika pia inaweza kusherehesha mdahalo huu wa utambulisho wa mswahili kwa kujikita katika ujumi mweusi wa kiafrika unaomfumbata.
Katika Biblia takatifu, yesu anadai kuwa ndugu na dada zao, yaani walio na unasaba naye ni wale wanaomsikiliza na kufuata kaida zake. Vivyo hivyo, Kiswahili nacho kinadai kuwa mswahili ni yule anayesikiliza, kufuata kaida zake, kukitetea na kukipa uhai. Anayefanya hivyo basi yumo ndani ya Kiswahili na Kiswahili kimo ndani yake kwa hiyo kazi atakayoiandika pasi na shaka ni fasihi ya Kiswahili.

Print this item

  UTAFITI WA FASIHI SIMULIZI
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2021, 06:06 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

UTAFITI WA FASIHI SIMULIZI

M.M. MULOKOZI
LENGO LA MUHADHARA
Kueleza:
  1. UMUHIMU WA UTAFITI WA FASIHI SIMULIZI
  2. PANDE TATU KTK UTAFITI – Mtafiti, Mtafitiwa,
  3. MBINU NA VIFAA VYA UTAFITI
  4. UCHAMBUZI WA MATOKEO NA UWASILISHAJI
UMUHIMU
  1. Kupata taarifa muhimu kuhusu suala linalotafitiwa
  2. Kuongeza hazina ya maarifa katika uwanja unaohusika
  3. Kipima-joto cha hali, fikra, mitazamo, matajario na maudhiko ya jamii ya watafitiwa
  4. Kuchangia katika kujenga na kuendeleza fani za fasihi simulizi na fani nyinginezo.
 MDHAMINI
  1. Huainisha nyanja za kufanyia utafiti na aula za utafiti
  2. Huainisha watafiti
  3. Hutoa fedha na nyenzo za utafiti
  4. Hupokea matokeo ya utafiti.
MTAFITI
  1. Ndiye mtafuta taarifa
  2. Huamua madhumuni na kuweka malengo ya utafiti
  3. Huchagua eneo na watu wa kutafitiwa
  4. Huchagua wasaidizi wa utafiti
  5. Hujenga uhusiano na watafitiwa
  6. Hupokea, kuchambua na kuchakata data za uwandani
  7. Hutayarisha ripoti na mapendekezo yatokanayo na utafiti wake.
Swali: Je, mtafiti ni jasusi?
MTAFITIWA
  1. Ndiye mtoa taarifa
  2. Hujenga uhusiano na Mtafiti
  3. Huchagua taarifa za kumpa Mtafiti
MCHAKATO WA UTAFITI
  1. Utafiti wa maktabani/makavazini/mtandaoni
Utafiti wowote ule sharti uanzie hapo. SOMA kazi za watangulizi kuhusu somo/mada yako.
1.1 Nyaraka za asili (k.m. barua)
1.2 Nyaraka rasmi (k.m. Ripoti za serikali)
1.3 Nyaraka zisizokuwa asilia – k.m. vitabu
  1. Pendekezo la Utafiti
2.1 Ainisha mada ya utafiti – baada ya kusoma kazi kadha za watangulizi
      katika uwanja huo
2.2. Fafanua tatizo la utafiti – baada ya kusoma kazi kadha za kinadharia
       katika uwanja huo
2.3 Eeleza madhumuni na malengo ya utafiti
2.4 Eeleza nadharia tete zitakazoongoza utafiti wako
2.5 Jadili machapisho yaliyoshughulikia suala hilo na onesha dosari na
      mapengo yake.
2.6 Onesha namna utafiti wako utakavyorekebisha dosari na kuziba
       mapengo hayo, na matarajio yako
2.7 Eleza mbinu na njia za utafiti zitakazotumika, pamoja na usampulishaji
      wa watafitiwa au wa data iwapo utahitajika
2.8 Eleza nadharia ya/za kiuchambuzi utakazotumia kuchambulia data zako 2.9. Onesha ratiba ya utafiti
2.10.Onesha makisio ya bajeti ya utafiti; bajeti iwiane na shughuli
        zitakazofanyika
2.11 Weka orodha ya marejeo
2.12 Ambatisha maswali, vidadisi, na zana nyingine za utafiti
       utakazozitumia.
  1. Ukusanyaji wa Data
3.1. Vifaa vya msingi
 – Kalamu na karatasi, shajara
– kinasa sauti
– kamera ya picha tuli
– kamera ya video
– vingine (k.m. kionambali) kama vitahitajika.
3.2. Njia
– Mahojiano
– Faida na hasara zake
– Kushuhudia
-Faida na hasara zake
– Kushiriki
– Faida na hasara zake
 – Kutumia vidadisi/majedwali, n.k.
– Faida na hasara zake
3.3 Kurekodi taarifa
Mbali na matumizi ya vifaa kama tepurekoda, tumia pia shajara na daftari kuandika yale yaliyo muhimu. Ripoti ya tukio iwe na yafuatayo:
– tarehe
– mahali
– muda
– majina ya wahusika (mtafiti, mtafitiwa/watafitiwa)
– Umri na jinsi ya mtafitiwa
 – malezo ya yaliyotendeka kwenye tukio hilo, malengo yake, na matokeo yake
– hali na hisia za wahusika
3.3 Muhimu
– Haja ya kuwa mnyenyekevu
– Usidokeze jibu kwa muulizwaji
– Usihubiri, sikiliza
– Usikemee au kuudhi muhojiwa
– Usivunje mila na kanuni za utamaduni wa wahusika
– Jitahidi ukubalike kwa jamii ya watafitiwa
– Usiridhike na taarifa au ushuhuda wa mtu mmoja; pata taarifa nyingi za watu mbalimbali kuhusu jambo lilo hilo ili uweze kuzilinganisha
– Chagua wakati unaofaa kulingana na utaratibu wa maisha wa wahusika (k.m. usiwe wakati wa kuandaa mashamba, au wakati usioendana na tukio unalotaka kulitafiti)
– Chagua msaidizi/mkalimani wa kufaa iwapo kuna haja
– Kuwa na shukrani kwa wanaokusaidia.
  1. Uchambuzi wa Data
4.1 Nukuu taarifa zote
4.2 Tafsiri taarifa unazohitaji (iwapo ziko katika lugha tofauti)
4.3 Tathmini data zote kwa makini (k.m. kwa kulinganisha na nyanja au vyanzo vingine, kama vile akiolojia, historia, sayansi, n.k.
4.4 Fanya uchambuzi wako kwa kutumia mbinu na nadharia ulizozichagua. Tumia pia fasili za watafitiwa au wanajamii inayohusika kama zipo.
4.5 Andika Ripoti na mahitimisho
4.6 Tayarisha Ripoti ya Fedha
4.7 Kabidhi Ripoti zote kwa Mdhamini/Msimamizi au yeyote anayehusika.
UTAFITI: UKUSANYAJI WA DATA MBINU ZA UTAFITI UKUSANYAJI WA DATA
  1. UKUSANYAJI WA DATA HUTAWALIWA NA MAMBO
4: a) Uwanja wa taaluma unaohusika
  1. b) Lengo/madhumuni ya utafiti
  2. c) Uwezo na nyenzo alizo nazo mtafiti
  3. d) Muda alio nao mtafiti
  4. VIFAA VYA UTAFITI (WA FASIHI NA LUGHA)
2.1 Vifaa vya Utafiti Hutegemea aina ya utafiti, lakini aghalabu baadhi ya vifaa hivi, kama si vyote, hutumika:
  1. a)     Shajara ya uwandani
  2. b)    Kalamu na karatasi za kuandikia kumbukumbu
  3. c)     Tepurekoda na vifaa vyake
  4. d)    Video/kamrekoda na vifaa vyake
  5. e)     Kamera na vifaa vyake
  6. f)      Kompyuta na vikorokoro (accessories) vyake
  7. g)     Vidadisi (hojaji) na dodoso
  8. h)    Vifaa vya kupimia/kuhesabia
  9. i)     Darubini, vionambali, n.k.
  10. NJIA KUU ZA UTAFITI
  11. a) Utafiti wa maktabani/ wa nyaraka
  12. b) Utafiti wa uwandani
  13. c) Utafiti wa maabarani/studioni
  14. UTAFITI WA MAKTABANI/NYARAKA
4.1 Nyaraka asilia (primary documents)
  1. a) Nyaraka rasmi/za kiserikali
  2. b) Nyaraka binafsi (barua, shajara, majalada, kumbukumbu, vyeti, n.k.)
4.2 Nyaraka fuatizi (secondary documents)
  1. a) Nyaraka rasmi/za kiserikali
  2. b) Nyaraka binafsi (vitabu, kumbukumbu, ripoti, magazeti,  n.k.)
  3. UTAFITI WA UWANDANI
Mbinu za utafiti:
  1. a) Kushuhudia (observation)
  2. b) Kushiriki (paticipation)
  3. c) Mahojiano (interviewing)
  4. d) Mijadala ya vikundi lengani
  5. e) Kutumia vidadisi na majedwali
5.1 Mbinu ya kushuhudia (observation)
Kushuhudia ni mbinu ya kuangalia tukio linapotendeka na kukusanya taarifa zake.
5.1.1 Namna za ushuhudiaji
  1. a) Uchunguzi na upimaji (k.m. katika jiografia, muziki) – Mtafiti awe na vifaa vinavyohitajika kwa kazi hiyo (k.m. rula, mizani, vipima-sauti)
  2. b) Ushuhudiaji fungemno (highly structured observation) – kwa kutumia mandhari yaliyodhibitiwa – kwa kutumia majedwali yaliyosanifiwa
  3. c) Ushuhudiaji funge (structured observation) – unatoa uhuru zaidi – huchanganya majedwali na mahojiano – mtafiti si mshiriki, lakini huangalia na kukusanya taarifa waziwazi – taarifa za ushuhudiaji husaidiana na taarifa za mahojiano na vidadisi
  4. d) Ushuhudiaji lengani (focused observation) – mtafiti huangalia tukio/tendo katika mazingira yake asilia bila majedwali. Taarifa hupatikana kutokana na kuzoeana na kuwa na mawasiliano ya muda mrefu na watafitiwa.
  5. e) Ushuhudiaji huru/ usiofunge (unstructured observation) – hufanywa kwa siri na mtafiti bila mtafitiwa kufahamu na bila mpangilio wa wazi.
5.1.2 Ukusanyaji wa taarifa za ushuhudiaji
  1. a) Majedwali: hujazwa na mtafiti au msaidizi wake
  2. b) Uandishi wa taarifa
Taarifa huandikwa wakati wa ushuhudiaji usio wa kificho. Taarifa hizo inabidi ziwe na mambo yafuatayo:
– tarehe
– mahali
– wakati
– mtu/watu wanaohusika
– vifaa
– maelezo ya lengo la shughuli
– maelezo ya mandhari
– mfuatano wa matukio
– ufafanuzi wa shughuli zilizofanyika
– hisia na ukereketwa wa wahusika
  1. c) Kupata taarifa za nyongeza
Taarifa za nyongeza zipatikane kutokana na:
– mazungumzo
– mahojiano
– nyaraka
– rekodi za kanda/video
– pichatuli
– chati, michoro na ramani
5.1.3 Tafsili ya taarifa (interpretation of data)
Tafsili ya taarifa za uwandani isitokane na hisia au mawazo ya mtafiti mwenyewe tu, bali itokane na kushirikisha watafitiwa wenye ufahamu wa mambo hayo.
5.1.4 Faida na mipaka ya utafiti wa kushuhudia
  1. a) Faida Humwezesha mtafiti:
– kukusanya taarifa kwa mpangilio mzuri
– kutaamali matendo na matukio ya kijamii moja kwa moja yanapotokea
– kuchunguza duru za shughuli au tabia katika mazingira yake asilia ya kijamii
– kuchunguza namna watu wanavyoishi na kufanya kazi bila kuingilia shughuli zao – kukusanya taarifa ambazo haziwezi kupatikana kwa njia ya mahojiano au mazungumzo
– ni njia inyomwezesha mtafiti kupata taarifa nyingi kwa gharama ndogo
  1. b) Mipaka/upungufu
– baadhi ya shughuli au matukio yanayochunguzwa hayawezi kufikiwa au kuonekana na mtafiti
– wakati mwingine, kuwapo kwa mshuhudiaji huweza kupotosha au kuathiri shughuli inayohusika
– njia hii hufaa zaidi kwa matukio ya wakati uliopo; haifai kutumika kuchunguza matukio yaliyopita/ya zamani
– njia hii haifai kwa kukusanya taarifa kuhusu mikabala, maoni, nia, maana, n.k.
– njia hii haifai kwa kuchunguza makundi makubwa ya watu
– huweza kuchukua muda sana, na haifai kwa kuchunguza mwenendo au mchakato kwa muda mrefu sana
5.1.5. Matatizo ya uhusiano kati ya mshuhudiaji na mshuhudiwaji
  1. a) Unawezaje kushuhudia bila kushuhudiwa?
  2. b) Utawezaje kuepuka “athari ya kuangaliwa”
– inayomfanya mtafitiwa kutotenda mambo kikawaida kutokana na kuwapo kwa mtafiti?
Baadhi ya njia za utatuzi
  1. a) Kama inawezekana, jifanye mshuhudiaji-mshiriki
  2. b) Pata imani ya wale unaowatafiti kwanza (hili huchukua muda)
  3. c) Chunguza bila kuonekana (utafiti wa siri)
–  hili nalo lina matatizo ya kiitikeli!
  1. d) Jaribu kuwapo bila kuvutia nadhari ya washiriki
  2. e)  Wakati wa kutafsili data yako, zingatia athari ya kuwapo kwako wakati wa kuikusanya
5.2 Utafiti kwa kushiriki Utafiti huu unahusu kwenda kuishi na kushiriki katika shughuli za wale unaowatafiti/ unazozitafiti
5.2.1 Manufaa ya njia hii
  1. a) Hukuwezesha kuwafahamu vizuri watu na shughuli unazotaka kuzitafiti, na pengine kukubaliwa na hao unaowatafiti
  2. b) Kutokana na tajiriba unayoipata kwa kuangalia na kushiriki, unapata ufahamu wa undani wa yale unayoyatafiti
5.2.2 Mipaka
  1. a) Utafiti wa kushiriki huweza kuhitaji muda mrefu zaidi kuliko ule alio nao mtafiti b) Si mara zote unaweza kushiriki katika shughuli unayoitafiti:
Mifano
– shughuli ya siri au mwiko
– shughuli haramu/ya kuvunja sheria
– shughuli isiyokubalika kijamii
– shughuli ya hatari
– shughuli inyodai sifa za kipekee kutoka kwa mtafiti (ambazo hana)
– mtafiti
-mshiriki huweza kuona ugumu kukaa kando na kuichunguza shughuli inayohusika kwa uhuru bila kuelemea upande fulani
  1. MAHOJIANO
6.1 Mahojiano ni nini?
Ni majibizano ya ana kwa ana (au ya simu, kidijitali/barua pepe), kati ya watu wawili au zaidi kwa lengo la kukusanya taarifa au maoni kuhusu suala fulani la kiutafiti lililoainishwa
6.2 Mambo ya kuzingatia wakati wa mahojiano
  1. a) Uchangamfu – usioneshe uhasama au chuki
  2. b) Kutoelemea upande fulani
  3. c) Jieleze kikamilifu ueleweke wewe ni nani na una nia gani – onesha vitambulisho na vibali iwapo kuna haja
  4. d) Kujenga muamana
– mhakikishie mhojiwa kuwa mahojiano ni siri baina yenu wawili
– anza na maswali ya jumla kabla ya kuingilia maswali mahsusi
– maswali nyeti yaulizwe baadaye kabisa mkishazoeana
– mwishoni muulize mhusika kama ana swali au ombi
  1. e) Muktadha wa kijamii: mila, utamaduni na maadili ya mahali panapohusika
– kuhoji mtu wa jinsi, umri, cheo tofauti
– miiko (k.m. kuhesabu watu, watoto)
– kanuni za maingiliano (jinsi, tabaka, ngazi za madaraka)
– uvaaji
  1. f) Muktadha wa tukio
– ulinge wa mahojiano (wa ndani, wazi kwa kila mtu)
– madhanio ya mhojiwa kuhusu madhumuni ya mtafiti
– madhanio yako kuhusu mhojiwa
– tabia, mwenendo na heba za wahusika
6.3 Mambo ya kuepuka
– kukusanya habari usiyoihitaji
– kutafuta taarifa ili kuhalalisha msimamo au imani yako
– ushabiki
– kudokeza majibu yanayotarajiwa
– tamaa ya kujua kila kitu mpaka kuvuka malengo yaliyokusudiwa
– kuonesha “ubosi”
– kuwa rasmi mno, kutosikiliza vizuri maelezo, kukatisha maelezo bila kujali hisia za mzungumzaji, n.k.
6.4 Mambo yanayoathiri wahojiwa
  1. a) Athari hasi
– kazi nyingi
– aibu ya kuonekana kuwa mjinga
– kutovutiwa na maudhui ya mahojiano
– kutovutiwa na mwenye kuhoji
– hofu (ya matokeo)
– ukosefu wa motisha (kifedha?)
– mahusiano binafsi na mhojiwa
  1. b) Athari chanya
– kuvutiwa na mwenye kuhoji
– kuvutiwa na maudhui
– ufahari (kuonekana unahusiana na asasi au mtu anayefanya utafiti)
– wajibu (kuonekana kuwa raia mwajibikaji)
– upweke
– matarajio ya tunzo (fedha au zawadi)
– mahusiano binafsi na mhojiwa
6.5 Matatizo ya kiutekelezaji
  1. a) fedha
  2. b) usafiri
  3. c) hali ya hewa/tabianchi (muda wa utafiti uzingatie mambo haya)
  4. d) usampulishi (sampling): nani wahojiwe, kwa nini na lini?
– sampuli kutegemea fursa (opportunity sample)
– wale ambao ni rahisi kuwahoji
– sampuli nasibu (random sample)
– sampuli nasibu tabakishi (stratified random sample)
– hukuwezesha kupata aina ya watu unaowahitaji
– sampuli
-kusudio (purposeful sample)
– sampuli-mgawo (quota sample)
– sampuli
-tajwa (snowball sample), n.k.
6.6 Aina za mahojiano
  1. a) Mahojiano funge (structured interviews)
– hujikita katika jedwali/ hojaji zilizotayarishwa kabla
– hufaa kama maswali mengi yasiyohitaji mjadala mkubwa yataulizwa
  1. b) Mahojiano nusu-funge (semi-structured)
– jedwali hutumika, lakini huacha mwanya kwa maswali mengine
  1. c) Mahojiano huru (unstructured)
Haya ni mahojiano ya kina zaidi, na huhitaji ujuzi na umakinifu katika kumwongoza mhojiwa kutoa taarifa zinazohitajika
– mahojiano huweza kuwa sanifu au huru
– njia itakayoteuliwa kutumika itategemea lengo
 6.7 “Mahojiano” dhidi ya “Hojaji” Uamuzi wa kutumia njia ya usaili au hojaji hutegemea mambo yafuatayo:
  1. a) Aina ya suala linalotafitiwa
  2. b) Aina ya utafiti
  3. c) Malengo ya utafiti
  4. d) Aina za maswali yanayoulizwa
  5. e) Walengwa (k.m. wasiojua kusoma na kuandika, wasomi, n.k.)
6.8 Faida za mahojiano
  1. a) Hukuruhusu kuuliza maswali ya papo kwa papo na kufahamiana na mhojiwa
  2. b) Hukuruhusu kuuliza mhojiwa maswali ya binafsi na ya ikirari (factual)
– yeye ni nani
– anafikiria nini, ana maoni gani
– anahisi nini, n.k.
  1. c) Hukusanya tabasuri na tafsili za wahusika kuhusu matukio yanayotafitiwa
  2. d) Huwaruhusu wahojiwa kuelezea misukumo na sababu za mienendo yao
  3. e) Hukuwezesha kuuliza maswali tokezi au ya nyongeza
6.9 Hasara/mipaka ya mbinu ya mahojiano
  1. a) Taarifa inayopatikana kwa kawaida huelemea upande mmoja
  2. b) Wahojiwa wengine hushindwa kujieleza kutokana na haya au sababu nyinginezo
  3. c) Njia hii hutegemea uhusiano unaojengeka kati ya mtafiti na mhojiwa; muulizaji mbaya huibua muulizwa mbaya
  4. d) Njia hii hutawaliwa na muktadha mahsusi
  5. HOJAJI
8.1 Hojaji ni nini?
Orodha (kwa maandishi) ya maswali au mambo yanayohitaji kujibiwa au kuelezewa na wahojiwa kwa lengo la kukusanya taarifa. Hivyo hojaji ni zana ya kukusanya na kurekodi taarifa.
8.2 Manufaa ya Hojaji
  1. a) Ina gharama ndogo na ni rahisi kutumia
  2. b) Huweza kupelekwa kwa wahojiwa wengi
  3. c) Ni rahisi kuchanganua (iwapo imebuniwa kwa makini na ustadi)
  4. d) Huweza kuibua taarifa nyingi katika muda mfupi
  5. e) Huhifadhi usiri (hasa kama haitaji majina)
8.3 Upungufu/hasara ya kutumia Hojaji
  1. a) Hutegemea uaminifu wa wahojiwa (kwa vile hakuna fursa ya mahojiano ya ana kwa ana)
  2. b) Mwitiko wakati mwingine huwa mdogo
  3. c) Huweza kukabiliwa na matatizo ya kiutekelezaji (k.m. huduma hafifu za posta au intaneti)
  4. d) Haziwezi kujazwa na watu wasiojua kusoma na kuandika
  5. e) Hakuna fursa kwa mtafiti kuweza kufafanua maswali yake kwa mhojiwa
  6. f) Hakuna fursa kwa mhojiwa kufafanua majibu yake
8.4 Namna ya kuandaa Hojaji
  1. a) Uwe na hakika kuhusu lengo lako: ni nini hasa unataka kukifahamu na kwa nini?
  2. b) Maswali yawe mafupi (usiingize maswali yasiyohitajika, k.m. ya kiwasifu).
  3. c) Hojaji isizidi kurasa 10, na ikiwezekana isichukue zaidi ya dakika 15 kujaza
  4. d) Uliza swali sahihi kwa mhojiwa sahihi
  5. e) Epuka maswali ya kibinafsi au yanayodhalilisha au kuudhi (k.m. yahusuyo siri za binafsi)
  6. f) Epuka lugha ya jaziba
  7. g) Tumia lugha sahili
  8. h) Epuka lugha ya kitaalamu, ila kama unawahoji wataalamu wa uwanja unaohusika
  9. i) Swali lilenge jambo moja, lisiulize mambo mengi
  10. j) Usimweke mhojiwa katika hali ngumu akashindwa kukujibu (k.m. swali kama “je, sasa umeacha wizi?”)
  11. k) Usichanganye matakwa ya ikirari (factual) na yale ya tathmini katika swali lilelile
  12. l) Changanya mitindo ili usimchoshe mhojiwa
  13. m) Mpangilio
 – anza na taarifa za lazima kisha nenda kwenye taarifa zisizo za lazima
– anza na maswali yasiyoelemea upande mmoja
  1. n) Maelekezo kuhusu namna ya kujaza Hojaji yawe bayana
  2. o) Epuka maswali yanayodokeza jibu
  3. p) Zingatia mahitaji ya kiuchanganuzi; k.m. iwapo utatumia kompyuta kuchanganua data, ni vizuri Hojaji ikawa na mfumo unaokubalika kikompyuta, k.m. matumizi ya misimbo
  4. q) Mwishoni mwa Hojaji andika neno la Shukrani
  5. r) Kumbuka kuandika vizuri anwani yako (ya posta na anwani-pepe), na hata namba ya simu, kwenye Hojaji au barua utakayoambatisha
  6. s) Toa ahadi ya kutunza siri
  7. t) Toa ahadi ya kumpelekea mhojiwa “Muhtasari wa Matokeo ya Utafiti” iwapo atauhitaji
  8. u) Onesha tarehe na siku ya kutuma Hojaji na tarehe na siku ya mwisho ya kurejeshwa kwa Hojaji
  9. v) Onesha tarehe halisi ya kurejeshwa kwa Hojaji (k.m. Jumatano, 10/2/2010)
  10. w) Hakikisha kwamba Hojaji ni safi na inavutia
8.5 Namna ya kutunga maswali ya Hojaji
  1. a) Ikibidi maswali-funge yajaliziwe na maswali ya kujadili
  2. b) Wakati mwingine kauli funge (structured statements) ni bora kuliko maswali
  3. c) Maswali yanayodai maelezo, japo magumu, huweza kuibua taarifa nyingi zaidi
  4. d) Orodha: Huweza kutumika kwa kumtaka mhojiwa ateuwe mambo fulani kutoka katika orodha
  5. e) Maswali ya uteuzi wa jibu (multiple choice) sahihi huweza pia kutumika
  6. f) Kupanga kingazi (rating): k.m. kitarakimu (1-9)
  7. g) Udarajishaji (rankings): chagua njia inayofaa
  8. h) Skeli- Liketi (Likert Scales): zitumike kupimia mikabala, hisia, n.k.
Majibu huweza kupewa thamani za kitarakimu: kwa mfano: nakubali, sijaamua, sikubali, nakataa kabisa
8.6 Usambazaji wa Hojaji
  1. a) Kutumia posta
  2. b) Kupeleka kwa mkono (kama sampuli ni ndogo)
  3. c) Kutumia mawakala/wasaidizi
  4. d) Kama mwitiko ni hafifu, waandikie wahojiwa, wapigie simu au watembelee kama wapo karibu
  5. e) Hojaji zinazorejeshwa zirekodiwe vizuri na kuhifadhiwa
  6. f) Hojaji ziharibiwe iwapo hazihitajiki tena
MAREJELEO
Adam, J na Kamuzora, F (2008) Research Methods for Business and Social Studies.  Morogoro: Mzumbe Book Project.
Bowern, C (2008) Linguistic Fieldwork: A Practical Guide. New York: Palgrave- Macmillan.
Kothari, C.R (2004) Research Methodology: Methods and Techniques. New Delhi: New    Age International.
Msokile, M (1993) Misingi ya Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: EAEP.
Mulokozi, M.M. (1983) “Utafiti wa Fasihi Simulizi” katika TUKI Makala ya Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili III: Fasihi. Dar es Salaam: TUKI.: kur. 1-25.
Ogechi, N.O, N.L  Shitemi, na K. I. Simala (wah) (2008) Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika. Eldoret: Moi University Press. Pons, Valdo (Mh) (1992) Introduction to Social Research. Dar es Salaam: DUP.
Sewangi, S.S. and Madumulla J.S. (eds) (2007) Makala ya Kongamano la Jubilei ya TUKI (Vol. I and II) Dar es Salaam: TUKI.
Simala, K.I. (mh) (2002) Utafiti wa Kiswahili. Eldoret: Moi University Press.
MASWALI YA MTIHANI
  1. Eleza na kujadili faida na mipaka ya mbinu ya kushuhudia ya utafiti wa uwandani.
  2. Eleza na kujadili faida na mipaka ya utafiti-shiriki kama njia ya kukusanya taarifa uwandani.
  3. Fafanua dhana ya usampulishi na aina zake. Eleza namna unavyoweza kutumia mbinu ya usampulishi katika utafiti wa lugha AU fasihi.
  4. Fafanua dhana ya hojaji. Taja na kujadili angalao mambo kumi yanayofaa kuzingatiwa wakati wa kuandaa hojaji ya utafiti wa lugha AU fasihi

Print this item

  DHANA YA FASIHI KWA UJUMLA
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2021, 05:51 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

.pdf   FASIHI KWA UJUMLA.pdf (Size: 312.07 KB / Downloads: 4)

Print this item

  Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2021, 05:30 PM - Forum: Semi - No Replies

.pdf   Matumizi ya Lugha Katika Vitendawili.pdf (Size: 80.52 KB / Downloads: 3)

Print this item

  Michezo ya Watoto/Chekechea
Posted by: MwlMaeda - 09-10-2021, 05:22 PM - Forum: Sanaa za maonesho - No Replies

Michezo ya Watoto/Chekechea
  • Michezo inayoigizwa na watoto katika shughuli zao.
Aina
  1. Mchezo wa baba na mama
  2. Kuruka kamba
  3. Kujificha na kutafutana
  4. Kukimbiza kibaramwezi dhidi ya upepo ili kizunguke
  5. Mchezo wa baba na mama
Sifa
  1. Waigizaji ni watoto.
  2. Huhusu shughuli za kiuchumi na kitamaduni k.v. arusi, siasa, ukulima.
  3. Huandamana na nyimbo za watoto.
  4. Huwa na miondoko mingi k.v. kujificha, kuruka.
  5. Huwa na matumizi mengi ya takriri.
  6. Huchezwa popote.
  7. Huwa na kanuni fulani.
  8. Hukoma watoto wakichoka au wakikiuka kanuni
Umuhimu
  1. Kufunza watoto majukumu yao ya utu uzima.
  2. Kuwatanguliza watoto katika sanaa ya uigizaji.
  3. Kukuza ubunifu wa watoto kadiri wanapoendelea kuigiza.
  4. Kudumisha utamaduni wa jamii.
  5. Kuburudisha watoto.
  6. Kukuza stadi ya uigizaji miongoni mwa watoto.
  7. Kukuza utangamano miongoni mwa watoto kwa kuwajumuisha pamoja.
  8. Kukashifu matendo hasi ya watu wazima kwa watoto.
  9. Kuwapa watoto ukakamavu na kujiamini wakiwa wachanga.

Print this item