LUGHA/LAHAJA ZA KIARABU
Waarabu wana lugha za kijamii zipatazo 30 ambazo 'International Organisation for Standardization wanaziona ni lugha zenye kujitegemea wakati 'Library of Congress' wanaziona ni lahaja za Lugha ya Kiarabu.
Kuna lahaja inayowaunganisha Waarabu wote (Wana uwezo wa kuifahamu) inaitwa 'Lahaja ya Umoja /Allahjatul Muwahhidat - اللهجة الموحدة) na hii ndiyo lahaja ya Kiarabu cha Qur'aan Tukufu na sasa huitwa Kiarabu Fasaha/ Al-Arabiyyatul Fusw-haa العربية الفصحى).
Lahaja nyingine za Kiarabu zinakaribiana na kuachana hapa na pale.
Kwa mfano, tuliangalie neno Kayfa كيف Vipi (Kiswahili), How (Kiingereza) katika lahaja mbalimbali za Kiarabu:
1. Kiarabu Fasaha: KAYFA كيف.
2. Saudia: KAYFA/SH-LOON كيف/ شلون.
3. Libya: KAYFA كيف
4. Morocco: KIIFASH كيفاش
5. Algeria: KIIFASH كيفاش
6. Misri: IZAAY إزاي
7. Jordan: KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
8. Shaam (Syria): KAYFA/SH-LOON كيف/شلون
9. Iraq: SH-LOON شلون
10. Sudan: KAYFA كيف
11. Yemen: KAYFA كيف
12. Kuwait: KAYFA/SH-LOON كيف
13. Imaraat (Falme za Kiarabu - UAE): SHAQAA/SHAQAAIL شقى/شقايل
14. Bahrain: SH-LOON/CHIIFAT شلون/جيفة
15. Oman: KAYFA كيف.
TANBIHI: Neno KAYFA baadhi ya Waarabu hulitamka KEEF.
Shairi ama utenzi, Mimi naona ni wimbo,
Lisoimbwa sijiponzi, hilo kulitia nembo,
Nikaanza kukienzi, kitu kichokosa umbo,
Ni shariti kuimbika, hapo taita shairi.
Shaaban Robert 1958:
Tena sanaa ya vina, tenzi nyimbo na shairi,
Maneno si mengi sana, fasaha yasiyo shari,
Shairi wimbo mpana, Wimbo ni dogo shairi,
Lililopea shairi, hilo twaita utenzi.
Naendelea Shabani, kueleza waziwazi,
Mwasema vina nini? Kufasili hamuwezi,
Sauti zilolingani, mfano silabi zi,
ziwe sare utungoni, hapo twaviita vina.
Mathias Mnyampala 1965:
Ni maneno ya hekima, tangu kale tungo hizi,
Cha thamani na heshima, Mfano wake feruzi,
Mwanadamu huyafuma, ya dunia maongozi,
Kwa maneno ya mkato, huyanena ya moyoni.
Jumanne Mayoka
1986:
Wa kisanaa utungo, mpangowe maalumu,
Wenye vina kwenye kingo, na mizani ilo timu,
Shairi haliwi chongo, zote pande ni muhimu,
Za fani na maudhui, manenoye kwa mkato.
Euphrase Kezilahabi 1973:
Ukale napiga teke, fikira zenu hafifu,
Kuzitaja sifa zake, Mimi naona dhaifu,
Sheria ni kitu teke, kinaleta usumbufu,
Sasa naleta usasa, nazivunja desturi.
Ni tukio ushairi, pia hali au wazo,
Lenye mpango mzuri, na mizani mzomzo,
Ufasaha sio shari, lugha iliyoliwazo,
Na ueleze ukweli, maisha ya binadamu.
Mulokozi na Kahigi 1973:
Ni mpango maalumu, wa fasaha na muwala,
Lenye mafunzo muhimu, liso funzo hilo wala,
lihusulo binadamu, yale ya lila na fila,
hisia ziguse moyo, yawe mahadhi ya wimbo.
Mtunzi:
Ulikuwa ubishani, ni kitu gani shairi,
Japo kidogo zamani, naona zake athari,
Husema vina vya nini? Wengine huleta shari.
Posted by: MwlMaeda - 10-11-2021, 06:23 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
BINADAMU NA WANYAMA.
______________________
1.
Binadamu na wanyama, tabia zinafanana,
hili ninalolisema, nalihakikisha sana.
Wa mapori kama kima, simba na kakakuona,
swala na wengine 'nyama, wanafanana na watu.
2.
Wa nyumbani ka'kondoo, mbwa,punda pia mbuzi,
chunguza yao mienendo, utapata utambuzi.
Wana ya watu matendo, nalifanya uchambuzi,
tabia zinafanana, binadamu na wanyama.
3.
Ntu kali mwenye nguvu, ni simba si masihara,
mpole na mtulivu, huyu kondoo si chura.
Twamwita mtu mwerevu, kuwa mjanja sungura,
binadamu na wanyama, tabia zinafanana.
4.
Ipo siri ya ajabu, ya tabia kufanana,
tena vina ukaribu, viumbe'vi hufaana.
Kwa ushindani na ta'bu, vyaishi kwa kukulana,
watu kwa watu na 'nyama, na wanyama kwa wanyama.
5.
Kwa tabia kufanana, haya jama malimwengu,
huku kutegemeana, siri kuu yake Mungu.
Wandugu wapendwa sana, haya ni maoni yangu,
binadamu na wanyama, tabia'zo kufanana.
************************************************
Rwaka rwa Kagarama,
Mshairi Mnyarwanda,
Jimbo la Mashariki,
Wilaya ya Nyagatare,
Jamhuri ya RWANDA.
WIVU
Sisemi kutaradadi, penzi lataka ujenzi
Moyo utatabaradi, linapostawi penzi
Wivu huwa ushahidi, humulika ja kurunzi Wivu zao la mapenzi, ela chunga usizidi.
Abuu ~ Abii Pandani Wete - Pemba.
WIVU CHUMVI YA HUBA
Chochote kinachozidi, na kiwango kikavuka,
Sema bila taradudi, hicho kimekengeuka,
Kususwa hakina budi, kiache japo wataka, Wivu 'kizidi mashaka, japo ni chumvi ya huba.
Khamis S.M. Mataka (PhD) Dar es Salaam, Tanzania.
Ulilonena Sayyid, mwalimu ulotukuka,
Hiyo yako tashdidi, ubetini uloweka,
Hata sukari 'kizidi, chakula hakitalika, Wivu ni Sunna hakika, tuchunge wake muradi.
Abuu ~ Abii Pandani Wete - Pemba.
MSI WIVU GENDAEKA!
Kweli ni Sunna hakika, Sunna ya Tumwa Rasuli,
Msi wivu gendaeka, hamo kundi la Rijali,
Mke wake akitoka, kona yeyeĺ hatojali, Ni duyuthi bilkuli, msi wivu pulikeni.
Posted by: MwlMaeda - 10-10-2021, 11:38 AM - Forum: Je, wajua ?
- No Replies
JANDONI KUNA MENGI YA KUJADILI
Dada mmoja alinipigia simu, kabla hata sijamuuliza sababu alianza kunielezea matatizo ya mume wake.
Alinielezea mambo mengi mabaya ambayo mume wake alikua akimfanyia.
Nilimsikiliza sana lakini kwa namna alivyokua anaongea nilihisi kuna kitu.
Niliamua kumsikiliza mpaka mwisho ambapo aliniambia “Kaka mimi nimeamua kuondoka huyu si mwanaume wa kuishi naye!.”
Baada ya kumaliza kuongea nilimuambia sasa hembu niambie mazuri ya mume wako.
Alikaa kimya kwa muda kisha akaniambia “Mimi sikukupigia ili kumzungumzia yeye nilitaka tu unipe ushauri kuwa niondokeje maana nimechoka.”
Niliendelea kumsisitiza aniambie angalau zuri moja la mume wake.
Aliniambia zuri nikwakua tu labda anamsomesha mdogo wake sekondari lakini hakuna kingine.
Nilimuambia wala sihitaji mengi, hilo moja tu linatosha, nilimuuliza unasema mume wako hakujali, hajawahi kukununulia nguo hata siku moja au kukutoa out kama wanawake wengine?
Akanijibu ndiyo, nikamuuliza mshahaara wake ni Shilingi ngapi, akaniambia ni kama laki saba kwa mwezi.
Nikamuuliza chakula anatoa akaniambia ndiyo, nikamuuliza kodi ya nyumba kwa mwezi mnalipa Shilingi ngapi akaniambia laki moja na nusu, kwa mwaka ni Shilingi ngapi?
Akanijibu milioni moja na laki nane.
Nikamuuliza umeme na maji analipa nani?
Akanijibu mlipaji ni mume wake.
Nikamuuliza kwa mwezi vinaweza fika shilingi ngapi?
Akasema kama elfu ishirini.
Nikamuuliza kwa mwaka ni shilingi ngapi? Akajibu ni kama laki mbili na arubaini, ukichanganya na kodi ni kama milioni mbili.
Nikamuuliza ada ya mdogo wako Shilingi ngapi?
Akaniambia kwakuwa anasoma shuke binafsi ni kama milioni tatu na laki tano kwa mwaka.
Nikamwambia ukichanganya na zile milioni mbili unapata ngapi?
Tukapiga hesabu ikaja kama milioni tano na laki tano.
Nikamuuliza kwa siku chakula anakuachia Shilingi ngapi?
Akaniambia elfu kumi.
Kwa mwezi ni kama ngapi? Akasema ni laki tatu kwa mwaka ni kama milioni tatu na laki sita.
Nikamwambia ukijumlisha na zile tano inakuja kama ngapi?
Tukakuta inakuja kama milioni tisa na laki moja.
Nikamwambia haya sasa tuangalie mshahaara wa mume wako ni Shilingi laki saba kwa mwezi, ambayo kwa mwaka ni Shilingi ngapi?
Tukakuta ni milioni nane na laki nne, nikamwambia kama mnatumia milioni tisa na zaidi tena hapo hamjaumwa, sijajumlisha na ndugu zake, sijajumlisha nauli, sijajumlisha na michango ya harusi na bado unalalamika hakutoi out, wakati matumizi yenu tu ni ziadi ya mshahara wake unataka nini, unataka awe anakupa na damu yake.
Alibaki kimya na kukata simu. Baada ya siku mbili alinipigia simu na kuniambia “Kaka nimeelewa sitaki kuondoka tena kwani nimeona nilikua namchanganya tu mume wangu.
Sikua na shukurani na sikuona mazuri yake kwakua akili yangu niliielekezea katika mabaya tu.”
SOMO
Watu wengi tunawachukia wenza wetu kwakua akili zetu tumezipeleka katika mabaya yao tu na si mazuri hivyo tunajikuta tunawachukia na kudhani kua hawatupendi.
Hebu leo amua kuangalia angalau zuri moja tu la mwenza wako...