SHAIRI: WIVU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: WIVU (/showthread.php?tid=1308) |
SHAIRI: WIVU - MwlMaeda - 10-10-2021 WIVU Sisemi kutaradadi, penzi lataka ujenzi Moyo utatabaradi, linapostawi penzi Wivu huwa ushahidi, humulika ja kurunzi Wivu zao la mapenzi, ela chunga usizidi. Abuu ~ Abii Pandani Wete - Pemba. WIVU CHUMVI YA HUBA Chochote kinachozidi, na kiwango kikavuka, Sema bila taradudi, hicho kimekengeuka, Kususwa hakina budi, kiache japo wataka, Wivu 'kizidi mashaka, japo ni chumvi ya huba. Khamis S.M. Mataka (PhD) Dar es Salaam, Tanzania. Ulilonena Sayyid, mwalimu ulotukuka, Hiyo yako tashdidi, ubetini uloweka, Hata sukari 'kizidi, chakula hakitalika, Wivu ni Sunna hakika, tuchunge wake muradi. Abuu ~ Abii Pandani Wete - Pemba. MSI WIVU GENDAEKA! Kweli ni Sunna hakika, Sunna ya Tumwa Rasuli, Msi wivu gendaeka, hamo kundi la Rijali, Mke wake akitoka, kona yeyeĺ hatojali, Ni duyuthi bilkuli, msi wivu pulikeni. Khamis S.M. Mataka Dar es Salaam, Tanzania |