SHAIRI: BINADAMU NA WANYAMA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: BINADAMU NA WANYAMA (/showthread.php?tid=1310) |
SHAIRI: BINADAMU NA WANYAMA - MwlMaeda - 10-11-2021 BINADAMU NA WANYAMA. ______________________ 1. Binadamu na wanyama, tabia zinafanana, hili ninalolisema, nalihakikisha sana. Wa mapori kama kima, simba na kakakuona, swala na wengine 'nyama, wanafanana na watu. 2. Wa nyumbani ka'kondoo, mbwa,punda pia mbuzi, chunguza yao mienendo, utapata utambuzi. Wana ya watu matendo, nalifanya uchambuzi, tabia zinafanana, binadamu na wanyama. 3. Ntu kali mwenye nguvu, ni simba si masihara, mpole na mtulivu, huyu kondoo si chura. Twamwita mtu mwerevu, kuwa mjanja sungura, binadamu na wanyama, tabia zinafanana. 4. Ipo siri ya ajabu, ya tabia kufanana, tena vina ukaribu, viumbe'vi hufaana. Kwa ushindani na ta'bu, vyaishi kwa kukulana, watu kwa watu na 'nyama, na wanyama kwa wanyama. 5. Kwa tabia kufanana, haya jama malimwengu, huku kutegemeana, siri kuu yake Mungu. Wandugu wapendwa sana, haya ni maoni yangu, binadamu na wanyama, tabia'zo kufanana. ************************************************ Rwaka rwa Kagarama, Mshairi Mnyarwanda, Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare, Jamhuri ya RWANDA. |