LAHAJA ZA KIARABU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Maendeleo ya Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=11) +--- Thread: LAHAJA ZA KIARABU (/showthread.php?tid=1315) |
LAHAJA ZA KIARABU - MwlMaeda - 10-14-2021 LUGHA/LAHAJA ZA KIARABU Waarabu wana lugha za kijamii zipatazo 30 ambazo 'International Organisation for Standardization wanaziona ni lugha zenye kujitegemea wakati 'Library of Congress' wanaziona ni lahaja za Lugha ya Kiarabu. Kuna lahaja inayowaunganisha Waarabu wote (Wana uwezo wa kuifahamu) inaitwa 'Lahaja ya Umoja /Allahjatul Muwahhidat - اللهجة الموحدة) na hii ndiyo lahaja ya Kiarabu cha Qur'aan Tukufu na sasa huitwa Kiarabu Fasaha/ Al-Arabiyyatul Fusw-haa العربية الفصحى). Lahaja nyingine za Kiarabu zinakaribiana na kuachana hapa na pale. Kwa mfano, tuliangalie neno Kayfa كيف Vipi (Kiswahili), How (Kiingereza) katika lahaja mbalimbali za Kiarabu: 1. Kiarabu Fasaha: KAYFA كيف. 2. Saudia: KAYFA/SH-LOON كيف/ شلون. 3. Libya: KAYFA كيف 4. Morocco: KIIFASH كيفاش 5. Algeria: KIIFASH كيفاش 6. Misri: IZAAY إزاي 7. Jordan: KAYFA/SH-LOON كيف/شلون 8. Shaam (Syria): KAYFA/SH-LOON كيف/شلون 9. Iraq: SH-LOON شلون 10. Sudan: KAYFA كيف 11. Yemen: KAYFA كيف 12. Kuwait: KAYFA/SH-LOON كيف 13. Imaraat (Falme za Kiarabu - UAE): SHAQAA/SHAQAAIL شقى/شقايل 14. Bahrain: SH-LOON/CHIIFAT شلون/جيفة 15. Oman: KAYFA كيف. TANBIHI: Neno KAYFA baadhi ya Waarabu hulitamka KEEF. Na: Khamis Mataka +255 713 603 050 |