MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 73 online users.
» 0 Member(s) | 71 Guest(s)
Applebot, Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  WARAKA WA UNESCO KUHUSU SIKU YA KISWAHILI KIMATAIFA
Posted by: MwlMaeda - 11-25-2021, 01:57 PM - Forum: Nyaraka muhimu kuhusu lugha - No Replies

.pdf   unesco kiswahili DR 2.pdf (Size: 160.41 KB / Downloads: 6)

Print this item

  NYIMBO ZA KUFUNDISHIA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 11-25-2021, 09:37 AM - Forum: Ushairi - No Replies

Mwalimu/Mzazi msikose uhondo wa Kiswahili kwa watoto. Bofya linki hizi na umpe mwanafunzi/mtoto wako kifaa cha kidijitali ili atazame nyimbo mbali mbali ajifunze Kiswahili huku akiburudika na chaneli ya Babusa TV. Usisahau kubofya SUBSCRIBE. 

Linki ya Babusa TV https://www.youtube.com/channel/UCf3lKKH...nQDvEB-pMg

WIMBO WA ALFABETI NA SAUTI ZA KISWAHILI https://youtu.be/rUhvxVIA59A

WIMBO WA TARAKIMU WA PILI https://youtu.be/1RRxyjMxaYo

NASIKIA SAUTI YA MAMA https://youtu.be/NjyyzElR16E

NAMNA YA KUUNDA MTOTO BANDIA KIDOLI KWA KUTUMIA VIFAA VYA NYUMBANI https://youtu.be/M7qorx6ABtg

Namna ya Kutengeneza MPIRA kwa kutumia karatasi na Kamba https://youtu.be/R4rh7dtPKHI

Wimbo wa Vokali: https://youtu.be/GDywZJc8bTk 

Wimbo wa Rangi: https://youtu.be/4JOQ8DLKCUA 

Wimbo wa Vifaa vya Darasani: https://youtu.be/dqjpWy_cgjo 

Wimbo Wa Tarakimu:  https://youtu.be/C4Z4SM_q25Q 

Wimbo wa Vichura: https://youtu.be/NAPxHMMOM5k 

Wimbo wa Korona: https://youtu.be/DZzyN9Yn5Q8 

Namna ya kuunda gari la kuchezea: https://youtu.be/Jn-qiOvU-mw 

Mwalimu Dominic akifundisha Vokali: https://youtu.be/fbgYU-yv2kw

Mwalimu Dominic na Abu wakicheza Vichura: https://youtu.be/k6NGFi8f3OQ

BABUSA TV, TUNAELIMISHA NA KUBURUDISHA!
KINDLY WATCH! SUBSCRIBE! AND SHARE WIDELY!
#nyimbozawatoto
#BabusaTv
#kiswahilichildrensongs

Print this item

  Sindimba Ngoma ya Makonde
Posted by: MwlMaeda - 11-25-2021, 07:35 AM - Forum: Historia ya makabila ya kibantu - No Replies

Print this item

  SHAIRI: ASILI YA MWAFRIKA
Posted by: MwlMaeda - 11-24-2021, 06:32 AM - Forum: Ushairi - No Replies

1.  Naanza na shukrani
Kumshukuru manani
Kutuleta duniani
Kama alivyojaliya.

2. Tunamshukuru Mungu
Kwa kutupanga mafungu
Kutuweka chungu chungu
Duniani kueneya

3. Hakufanya ubaguzi
Sababu si yake kazi
Kila kitu kiko wazi
Na sote twajioneya.

4.Mataifa kayaweka
Kama tulivyogawika
Kwengine ulikutaka
Ni kama kwenda tembeya.

5.      Kila mtu ana pao
Atembeapo kwa mwao
Palipo asili yao
Awezapo jivuniya.

6.      Waweza kuleta hoja
Ni ubora kuyataja
Mataifa moja moja
Kule yanako tokeya.

7.      Hapa petu afrika
Ndipo Mungu katuweka
Hatuwezi kuondoka
ila iwe kutemnbeya.

8.      Kuna ndugu wa Asia
Wana kwao nao pia.
Jingine huwezi tia
Utakuwa wa kuoseya.

9.      Wengine ni waarabu
Hawa kwao ni karibu
Ukiwataka si tabu
Unapo wahitajiya.

10.  Wazungu kwao Ulaya
Ndiko hasa asiliya
Makabila sitotiya
Nashindwa kupangiliya.

11.  Kila mtu amepewa
Pale alipojaaliwa
Akakaa akatuwa
Maisha yakamwendeya.

12.  Hiyo jadi ya azali
Tulikuwa hatujali
Hata kikiwa cha mali
Twaweza kuzawadiya.

13.  Tulikuwa makarimu
Bora maneno matamu
Twaweza kupewa sumu
Na huku twachekeleya.

KUJA KWA WAGENI

14.  Nazianza simulizi
Kuwasema wachokozi
Walivyoifanya kazi
Hata humu kueneya.

15.  Ujuzi nilionao
Siwashindi wajuao
Ni wale niwapatao
Wanaonidokoleya.

16.  Sababu ya walowezi
Kupanda zao jahazi
Wakenea nchi hizi
Kidogo taelezeya.
17.  Walisafiri wakaja
Mtu mmoja mmoja
Sababu hawakutaja
Hapo walipabaniya.

18.  Wakajita wavumbuzi
Kuuficha ubazazi
Ni kama waota njozi
Wanayo jiropokeya.

19.  Sababu kubwa ni njaa
Ndipo wakatapakaa
Afrika kuzagaa
Kila pembe kueneya.

20.  Walioshindwa kusubiri
Wakazianza safari
Haidhuru za hatari
Lakini hakuna njiya.

21.  Waliingiya vyomboni
Kusafiri baharini
Kwenda wasiko tamani
Japokuwa kupoteya.

22.  Hawakuwa majasiri
Hapo waliposafiri
Kwani pepo za bahari
Hakika zikitishiya.

23.  Dhiki ilipowabana
Wakaiona namna
Ndipo wakaandamana
Kila pembe kuelekeya.

24.  Walifika Afrika
Wakapokewa haraka
Kwa furaha na kucheka
Wakila na kuvimwaya.

25.  Jumla tulisimama
Kuwapokeya kwa wema
Hakuna aliyesema
Tuwatendee ubaya.

26.  Mambo haya kwa hakika
Ambayo nayatamka
Bara zima afrika
Kila walipofikiya.

27.  Walipokewa vizuri
Wasifanyiwe jeuri
Kila walipoabiri
Tabu haikutokeya.

28.  Yote waliyofanyiwa
Kuwekwa na kupokewa
Na hadhi kukirimiwa
Thamani hawakutiya.

29.  Waliona ni lazima
Wao kupewa heshima
Kwani walizinga nyuma
Kutufanyia ubaya.

30.  Sababu waligeuka
Wakaanza kutushika
Utumwa kutupeleka
Bila ya kukumbukiya.

31.  Wema hawakukumbuka
Macho yaliwakauka
Ni vile walivyotaka
Na walivyofikiriya.

32.  Walifanya watakavyo
Majambo yao ya ovyo
Wakiona hivyo ndivyo
Mabaya kutufanyiya.

33.  Hakika kwa siku hizo
Hatukuwa na uwezo
Tuliugeza mzozo
Bali walituzidiya.

34.  Kwani hatukukubali
Kugeuzwa yetu hali
Tena na watu wa mbali
Wale tulowapokeya.

35.  Tuliona ni wageni
Tukawamba karibuni
Hapa ni penu nyumbani
Na kula kuwapatiya.

36.  Kabisa hatuna chuki
Tunapenda marafiki
Twamtendea ya haki
Kila anaetujiya.

37.  Kumbe yote ni ya bure
Wakiitika kwa shere
Nyoyoni wapiga hure
Huku wanafurahiya.

38.  Sababu fikira zao
Ni kutawala wenzao
Na kupeleka makwao
Mapato na watu piya.

39.  Hisani walofanyiwa
Na walivyochukuliwa
Kamwe hawakutambuwa
Wala kujifikiriya.

40.  Haja yao watawale
Tena wakae milele
Wanyonye wende wakale
Wapate jifaidiya.

41.  Tulikuwa tumekaa
Kila mtu kwa wasaa
Ndipo wakaleta baa
Tusiyoitazamiya.

42.  Tukayaanza matata
Tukasimamisha vita
Rungu, mishare na nyuta
 Ndivyo tulivyotumiya.

43.  Tuuhifadhi uhuru
Tukaebila uhuru
Pasiwe wa kuamuru
Amri kututoleya.

44.  Tulivijaribu sana
Vita hivyo kupigana
Njia ikawa hapana
Mambo yakatutatuliya.

45.  Ndipo kukaa mezani
Wakazichora ramani
Wakagawana kwa kani
Bara letu nakwambiya.

46.  Waligawa kama nyama
Kila mtu atazama
Hatukuweza kusema
Ila kuwaangaliya.

47.  Yule kiga yule ini
Na wengine ni kichwani
Walobaki miguuni
Kila mtu atapiya.

48.  Bara wakaligawanya
Ili wapate linyonya
Na mali kuyakusanya
Vyomboni kuyapakiya.

49.  Wakatiya na mipaka
Kila walipopataka
Wakaanza kumushika
Na kuzitiya shariya.
50.  Bara zima Afrika
Majina wakabandika
Kila waliyoyataka
Nayetu yakapoteya.

51.  Yetu yasiwe na enzi
Yakafanywa ya kishenzi
Tusiwe nayo mapenzi
Tusije kukumbukiya.

52.  Hapo tukakosa haki
Hatuna pa kushtaki
Ndipo hapo tukabaki
Kuzifuata shariya.

53.  Wakatupora uhuru
Tukabaki kushukuru
Wakaanza kuamuru
Myaka ikateketeya.

54.  Makodi wakatutoza
Na huku wakatubeza
Ni mambo ya kuchukiza
Siwezi kuhadithiya.

55.  Amri hizi na hizi
Kuzikataa huwezi
Hata kama upuuzi
Ni lazima kutimiya.

56.  Na kama mkikataa
Mtaiona balaa
Mtafute pa kukaa
Na roho kutotuliya.

57.  Muone mashaka gani
Yaloingiya nchini
Ayaletayo mgeni
Msiemtazamiya.

58.  Kukubali ni lazima
Amri walizosema
Wala hawarudi nyuma
Ila kuzishikiliya.

UKOMBOZI

59.  Watu walikaa chini
Kufikiri kwa makini
Mambo haya hadi lini
Yatakapotokomeya.

60.  Hatuwezi kungojeya
Aula kuwaachiya
Lazima kuyazuwiya
Tumekwisha kuchokeya.

61.  Zamani tulijaribu
Kuziangusha dharubu
Wakatushinda kwa tabu
Ndipo walipoingiya.

62.  Sasa na tuanze tena
Kwa njia kila namna
Hata kama kubinyana
Ili wapate kimbiya.

63.  Maana tulifikiri
Watu hawa ni jeuri
Vipi waje washamiri
Na sisi tumetuliya.

64.  Fikra ikaeneya
Toka walio Ulaya
Na huku walobakiya
Wote wakafikiriya.

65.  Ulaya walikutana
Viongozi wa maana
Na maneno yakafana
Waliyozungumziya.

66.  Majina sitoyataja
Mtu mmoja mmoja
Bali kiasi cha haja
Ninayoyakumbukiya.

67.  Ni huko Manchesta
Ndugu Kwame na Kenyatta
Waliyazusha kuita
Dunia ikasikiya.

68.  Hawakuwa peke yao
Walikuwa na wenzao
Sijuwi majina yao
Ningeweza kuyatiya.

69.  Kama mnavyofahamu
Ulikuwa ni muhimu
Viongozi mahashumu
Ndio walohudhuriya.

70.  Huku kwetu Afrika
Sauti ilisikika
Hatukuwa na mashaka
Sote tuliipokeya.

71.  Muamko ukaanza
Kila pembe kujifunza
Zile hatuwa za kwanza
Ambazo za kuanziya.

72.  Jambo la kwanza umoja
Wala pasiwe na hoja (6)
Siku moja itakuja
Sote kuwa ni huriya.

73.  Hapana kurudi nyuma (29)
Wala mtu kusimama
Mababa na kina mama
Kusiwe wa kulegeya.

74.  Tumng’owe mkoloni
Arudi kwao nyumbani (35)
Kamwe tusikubalini
Bara letu ukaliya.

75.  Kakaliya bara letu
Anawatawala watu
Tusipokaza viatu
Hawezi kutuachiya

76.  Ukaanza ukombozi
Bara zima waziwazi
Tena bila ya ajizi
Sababu tulipaniya.

77.  Tukavianzisha vyama
Kwa jumla bara zima
Na tena vikasimama
Watu wakajitoleya.

78.  Wakajitoleya kwa mali
Na wengine kwa kitali
Tena bila ya kujali
Nini kitachotokeya.

79.  Ikawa bega kwa bega
Mkoloni kumswaga
Na damu tukaimwaga
Hapana kufikiriya.

80.  Ukombozi ukashika
Pembe zote afrika
Uhuru ukalipuka
Hakuna asosikiya.

81.  Wakoloni kwa hakika
Walikuwa wakicheka
Wasema mnayotaka
Vigumu kuyafikiya.

82.  Bure mwajihangaisha
Mnayatupa maisha
Sisi hapa kuwapisha
Hilo halijatuliya.

83.  Tena mwajipa mashaka
Msitake mkitaka
Kwani sisi kuondoka
Hamwezi kutwambiya.

84.  Hadi ufike mwishowe
Au tutake wenyewe
Na hapo ndipo mpewe
Siku tutayoridhiya.

85.  Na sisi tukatamka
Lazima mtaondoka
Bara letu twalitaka
Wenyewe kuangaliya.

86.  Tukendelea vitani
Mijini na vijijini
Na wengine misituni
Hakuna alotuliya.

87.  Mijini kuna siasa
Vijijini kuna visa
Sote twasema ni sasa
Wakati umewadiya.

88.  Vita vikaendeleya
Damu yetu tukamwaya
Na wao wakapoteya
Mawazo yakawajiya.

89.  Na mijini tumekaza
Siasa kuzieneza
Tukazidi kuikuza
Na wengi wakaingiya.

90.  Wazungu wakaogopa
Ndipo kuanza kutupa
Huko na kule na hapa
Nchi tukazipokeya.

91.  Uhuru wakautowa
Na wangine kunyakuwa
Bara na wenye visiwa
Ukaanza kueneya.

92.  Nchi nyingi zimepata
Zaendeshwa bila tata
Myaka mingi imepita
Nazo zinaendeleya.

93.  Walisema hatuwezi
Kuifanya hiyo kazi
Hakika ni upuuzi (55)
Maneno yaso na njiya.

94.  Huko ni kubabaika
Maneno ya kuropoka
Mtu hawezi tamka
Ambaye ametimiya.

95.  Ila alo mpungufu
Akilize za mkufu
Au harufu ya afu
Mara imeshapoteya.

96.  Nchi zilizobakiya
Ni kidogo nakwambiya
Majina nitayatiya
Na hivi nawatajiya.

97.  Kwanza hapo Rodesia
Hao hawajasikia
Wenyewe kutuachia
Bado wameshikiliya.

98.  Na Spanishi Sahara
Siku moja watahara
Watakuja pigwa ngwara
Wapate kutokomeya.

99.  Twende huko Namibiya
Pamoja na Azaniya
Kaburu wamezuwiya
Wala hataki sikiya.

100.                      Ameshika ubaguzi
Anaiona ni kazi
Duniya haisikizi
Kila wanavyomwambiya.

101.                      Na sehemu ya Somali
Faransa hakubali
Ameifunga kufuli
Ufunguo kufungiya.

102.                      Na visiwa vya Comoro
Kuna wake mgogoro
Wamekulaza kiporo
Hatuja watambuliya.

103.                      Ndugu zetu Msumbiji
Huko sasa twataraji
Tumepata mahitaji
Tuliyoyahitajiya.

104.                      Na Angola nako pia
Tumekwisha kusikia
Tunachokitarajia
Karibu kitatokeya.

105.                      Na sehemu nyinginezo
Ambazo zina mizozo
Tutavivunja vikwazo
Tusafishe kote piya.

MASHUJAA

106.                      Tukumbuke viongozi
Walioifanya kazi
Hadithi zao ziwazi
Siwezi kuzizuwiya.

107.                      Mashujaa wenye sifa
Ambao waliokufa
Ni jumla ya maafa
Yalokwisha tupitiya

108.                      Majina yao kutaja
Wote mmoja mmoja
Kichwani hayatakuja
Labda kutokozeya.

109.                      Najaribu kutamka
Majina kuyaandika
Yale nitayokumbuka
Ambayo yatanijiya.

110.                      Kwanza ndugu Nkuruma
Ambae alisimama
Wala hakurudi nyuma (29)
Uhuru kupiganiya.

111.                      Kuna ndugu Gabral
Huyo nae ni wa pili
Waloigeuza hali
Ikatambuwa duniya.

112.                      Tuje kwa ndugu Lumumba
Shujaa ambae kwamba
Alieivunja myamba
Ya ukoloni mbaya.

113.                      Sasa ndugu Mandlane
Nae pia tumnene
Jumla ni watu wane
Na bado naendeleya.

114.                      Abubakari Tafawa
Ambae alijitowa
Nchie kuikombowa
Wapate kuwahuriya.
115.                      Na ndugu yetu Karume
Alosimama kiume
Kutawaliwa kukome
Nchi ipate tuliya.

116.                      Na wangine wako ndani
Kuwekwa vizuwizini
Hivi wamo adhabuni
Nasi tunawaliliya.

117.                      Wakoloni wawaweka
Wapate sahaulika
Bure wanahangaika
Bado twawategemeya.

118.                      Majina yao ni haya
Najaribu kutatiya
Yale yanayonijiya
Wala sitoyaachiya.

119.                      Viongozi walo hai
Ambao twawatumai
Hatutoacha kudai
Hadi nnje kutokeya.

120.                      Kwanza ni ndugu Mandela
Anavyopata madhila
Kamwe hutoweza kula
Utapomfikiriya.

121.                      Amewekwa kisiwani
Nduguze hatumuoni
Na yeye atutamani
Kaburu amezuwiya.

122.                      Pili ni ndugu Nkomo
Hageuzi msimamo
Ameshika muandamo
Zimbabwe iwe huriya.

123.                      Smith amemuweka
Asipate kutamka
Lakini hajageuka
Siku anaingojeya.

124.                      Na ndugu wa Nabiya
Kaburu kawazuwiya
Nyayani amewatiya
Ili wapate tuliya.

125.                      Yote hayo kazi bure
Ni mruko wa papare
Siku ya kupinga hure
Mbona itatufikiya.

126.                      Bara zima afrika
Siku moja itafika
Sote tutafurahika
Kwa uhuru kutimiya.

UTAMADUNI

127.                      Wala hatukukubali
Kuyaacha ya asili
Tokeya hapo azali
Hadi sasa twatumiya.

128.                      Wageni walidharau
Tukaonwa mabahau
Upate kauka kau
Na uzidi kupoteya.

129.                      Mataifa Duniani
Yanayo utamaduni
La ajabu jambo gani
Kuwa nao nasi piya.

130.                      Utamaduni na mila
Kati ya zetu kabila
Zikiwa kila mahala
Bara zima kueneya.

131.                      Namna zilivyokuwa
Karibu zote ni sawa
Ufikapo wapokewa (28)
Utakapokufikiya.

132.                      Na sasa ndivyo zilivyo
Zitakwenda vivyo hivyo
Aone ni za ovyo
Anaweza jipakiya.

133.                      Akenda anakotaka
Arudi alikotoka
Na sisi hatuna shaka
Bara letu kutwachiya.

134.                      Mambo kushirikiana
Kwa kazi kila namna
Pamwe na kutazamana
Kwa shida zikitokeya.

135.                      Hapakuwa ubaguzi
Inapotokeya kazi
Kwa vijana na wazazi
Huwa pamoja sawiya.

136.                      Tunapokwenda mashamba
Aula kujenga nyumba
Sote huwa ni sambamba
Hako anaebakiya.

137.                      Labda awe mgonjwa
Au jambo lisovunjwa
Huyo pia hatopunjwa
Japo hakuhudhuriya.

138.                      Tukizifanya pamoja
Kazi zote bila hoja (6)
Mazao yanapokuja
Twayagawa yote piya.

139.                      Hatukuwa ni wavivu
Tulikuwa washupavu
Vigumu kuwa mwerevu
Kazi inapowadiya.

140.                      Hatukujuwa tabaka
Za watu kugawanyika
Wanyonge na watu kuka
Hilo haliutokeya.

141.                      Tafauti kubwa sana
Ambayo ungeiona
Ni wazee na vijana
Popote ukitembeya.

142.                      Ama misiba na ndowa
Namna ilivyokuwa
Kila watu wanajuwa
Njia wanazopitiya.

143.                      Upate wa ngoma zetu
Siwezi kusema kitu
Kwasababu kila mtu
Mwenyewe ajioneya.

144.                      Tukisemeya elimu
Tulikuwa nayo hamu
Tukijifunza humu
Pamwe na zetu tabiya.

145.                      Mambo tukijifundisha
Ya kupeleka maisha
Tena tukikamilisha
Zetu mila na tabiya.

146.                      Vijana na wasichana
Pamoja na wavulana
Elimu wakifunzana
Halafu kuitumiya.

147.                      Tukijifunza kuwinda
Kwa kila anaependa
Mchana kutwa hushinda
Misituni kuviziya.

148.                      Na vijana ufugaji
Halafu ni uchungaji
Pamoja na ulimaji
Hatuwezi uachiya.

149.                      Upande wa wanawake
Sio kwamba wakapike
Bali mikeka wasuke
Na maji kujitekeya.

150.                      Kwa hakika mambo mengi
Ambayo yana misingi
Tukiyafanya kwa wingi
Bila ya kuwategeya.

151.                      Kwa jumla mambo yetu
Tokeya wazee wetu
Hawakuyaacha katu
Nasi twayashikiliya.

152.                      Na sasa ndio Zaidi
Twaongeza jitihadi
 Kuyahifadhi ya jadi
Yasipate kupoteya.

153.                      Lugha kwa upande wake
Kila mtu ana yake
Wakati akiwa kwake
Anayoisumuliya.

154.                      Na nyingine zafanana
Maneno yanaungana
Sababu wakionana
Wanaweza kuongeya.

155.                      Na tungo tukizitunga
Za maneno ya mwanga
Na pia tukiyapanga
Sababu tukijuliya.

156.                      Kwa muwala na urari
Mpango ulo mzuri
Ukiona utakiri
Kazi iliyotimiya.

157.                      Na pia wakitutibu
Kina nyanya na mababu
Kwa dawa za mjarabu
Maradhi yakikimbiya.

158.                      Kitumiya miti shamba
Walokuwa wakichimba
Ya kupaka na kwamba
Zote tukizitumiya.

159.                      Na vitu tuligunduwa
Halafu vikatumiwa
Kama hori na mashuwa
Vingine naongezeya.

160.                      Juwa kali likiwaka
Visiwa vikikauka
Shuruti kuteremka
Ndipo atayafikiya.

161.                      Buyu likatobolewa
Vilo ndani vikagewa
Na Kamba likasukiwa
Ili maji kutekeya.

162.                      Hapo tukapata ndoo
Kwa wote si kwa ukoo
Watu wasema hoo
Tumekwisha tambuliya.

163.                      Baada ya kuipata
Tukawa maji twachota
Yeyote anaepita
Anaweza kutumiya.
164.                      Mchanga tukiuchoma
Kwa kutengenezeya  chuma
Kwa majembe ya kulima
Na mashoka kuchanjiya.

165.                      Vyembe pamwe na mikuki
Ni silaha hazitoki
Kukitokea halaki
Hutwaa kupiganiya.

166.                      Na moto tukipekecha
Popote kunapokucha
Wala huwezi uficha
Mwenzio wamgawiya

167.                      Kama utafanya choyo
Kwa kitu au kandeyo
Watakuacha pekeyo
Watu hawatakujiya

168.                      Jambo hilo ni aibu
Kama mtu lamswibu
Kutengwa na akrabu
Wapi atakimbiliya.

169.                      Na samaki tukivuwa
Kwa malema na mabuwa
Pia kwenda kuchokowa
Chaza pamwe na chapiya.

170.                      Wanyama tukiwatega
Ulimbo tukiumwaga
Wanase bila kupiga
Kitoweo cha kuliya.

171.                      Michezo tukiicheza
Tena yenye kupendeza
Wala hatukupuuza
Kuyaacha mambo haya.

172.                      Mchezo kama wa nage
Holi kifura msege
Hamkai lege lege
Na jungwe kuongezeya.

173.                      Na watu wakiitana
Wakati wa kupambana
Kwa wingi hukusanyana
Huku wakishangiriya.

174.                      Hakika michezo hiyo
Na Zaidi mingineyo
Ni mambo tuliyonayo
Toka zama asiliya.

175.                      Kwevu na kuendeana
Pamwe na kueleana
Na pia kualikana
Majambo yakiwadiya.

176.                      Haya ni mambo ya kweli
Kwenye bara letu hili
Wala hatuja badili
Mila zetu kupoteya.

UCHUMI

177.  Uchumi tukiufanya
Na mali tukikusanya
Wala sio kwa sinya
Udhalimu kutumiya.

178.  Tukitowa letu jasho
Tena sio kwa vitisho
Au kwa maamrisho
Ya mtu kutuwekeya.

179.Tukibadili mazao
Kwa wake watu wajao
Wakija na vitu vyao
Wakifika vyabakiya.

180. Vitabaki palepale
Wala hakuna kelele
Kama wanao mchele
Kunde watajitwaliya.

181.Kwa upande wa wanyama
Mbuzi wawili kwa ndama
Maneno watayasema
Na mwisho yatafikiya.

182. Tulikuwa na mazizi
Ng’ombe, kondoo na mbuzi
Yevu ni mali azizi
Jingine kutosikiya.

183.  Hatusikii maneno
Yawaza wala nong’ono
Japo ni mbuzi watano
Akiba twajiwekeya.

184.  Tukifanya biashara
Ya faida na hasara
Wala huwezi kugura
Kwa mali kukupoteya.

185. Pembe tukiuziana
Mali kibadilishana
Na kile ambacho huna
Mwinziyo takipatiya.

186. Watu wingiya nyikani
Mizigo yao nyikani
Wanalala machakani
Hawajali kuumiya.

187. Wauzaji wa urembo
Au vyombo vya mapambo
Wanashika zao fimbo
Wapita wakiteteya.

188.  Na mali ya asiliyo
Dhahabu uijuwayo
Wala siyampashiyo
Ni safi ya kutumiya.

189.   Tunayo na almasi
Na miti ya sandarusi
Nyinginezo hazikosi
Japo zimejifukiya.

190. Pangine hatujulii
Thamani yake ni hii
Zimefifiya fifii
Twabaki kuangaliya.

191. Kuna wanyama porini
Simba, twiga na manyani
Ni mali kubwa kamani
Watalii huwajiya.

192.                      Mungu bara kuliumba
Na tena akalipamba
Ni kututiya kasumba
Kwa kutudharauliya.

193.                      Lina mito na mabonde
Kwa kulima zetu konde
Maharage au kunde
Akiba kujiwekeya.

194.                      Majabali na milima
Yenye kujaa wanyama
Na miti iliyomema
Mwapendeza kutembeya.

195.                      Kuna ndege na wadudu
Na mauwa ya waridu
Mtu aweza husudu
Harufu akisikiya.

196.                      Na vitu vya kupendeza
Mungu alivyovijaza
Barani kavieneza
Kiasi katujaliya.

DUA

197.                      Sasa namuomba Mungu
Alo wa tangu na tangu
Naanza maneno yangu
Kuzidi kuombeleya.

198.                      Viumbe vyako dhalili
Twakuomba ya jalali
Utubadilishe hali
Maovu kutondoleya.

199.                      Bara letu litukuke
Duniani lisikike
Tukae tupumzike
Tupate kuendeleya.

200.                      Tupendane sisi sote
Mapenzi yalo na kite
Mfitina tuwakate
Wasipate pa kungiya.

201.                      Bara zima afrika
Ulishushie baraka
Mambo yapate swafika
Kila nchi kutuliya.

202.                      Zimwendee shukrani
Ndugu Yakub Gowon
Kutukaribu nchini
Tutokao Tanzaniya.

Utenzi huu uliingiya katika mashindano ya maonesho ya Afrika huko Lagos, Nigeria mwaka 1974.
Nilishinda nikawa mtu wa pili katika Tanzania.Niliuanza kuuandika tarehe 6, October, 1974 na kumaliza 29, October, 1974

SALIM ALI KIBAO
S.L.P 75339
DAR ES SALAAM

Print this item

  AINA MBALIMBALI ZA LUGHA YA MAZUNGUMZO
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:47 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Quote:
Quote:
Quote:
Quote:UTANGULIZI:
Quote:
Quote:
Quote:Lugha ya mazugumzo ni maongezi ya watu wawili au zaidi bila kutumia maandishi. Lugha ya mazungumzo ambayo ndiyo lugha kongwe zaidi ya lugha ya maandishi ina dhima kubwa ya kufanikisha mawasiliano miongoni mwa watu au kikundi fulani. Lugha hii ya mazungumzo ilianza punde tu binadamu alipoanza kukabiliana na mazingira yake, hivyo kimsingi lugha ya mazungumzo ndiyo nguzo kuu ya kufanikisha shughuli zote za kibinadamu kutokana na nafasi yake kimatumizi.
Quote:
Quote:
Quote:Lengo la kuandaa makala haya ni kuonesha aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia mazingira rasmi na yale yasiyo rasmi, utambulisho wa kijamii kama vile: matabaka, hadhi yake, mshikamano na mwachano. Pia tutatalii jinsi gani utambulisho wa kimuktadha unavyoweza kuzalisha aina tofauti tofauti za lugha ya mazungumzo kwa mfano; lugha ya siri na yenye mipaka, michezo ya vitendo, kucheza na maneno, uganga kama miviga na utani kama miviga.
Quote:
Quote:
Quote:Hebu sasa tujipe wasaa kwa kutalii kipengele kimoja baada ya kimoja kama vilivyoorodheshwa katika utangulizi wetu.
Quote:
Quote:
Quote:Aina ya lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia mazingira rasmi na yasiyo rasmi:
Quote:
Quote:
Quote:Mazingira rasmi: kwa mujibu Kihore (2004) haya ni yale mazingira yanayoendana na kaida za kijamii, kisheria na kiutamaduni ambazo huhusisha matumizi ya lugha iliyosanifu. Huu ni muktadha unaohusisha ushirika wa upande mmoja, kama vile msamiati wa kiufundi na adabu maalum. Mfano wa mazingira rasmi ni kama vile ofisini, mahakamani, bungeni, kanisani, msikitini na katika elimu. Katika mazingira rasmi tunapata aina mbili za lugha ya mazungumzo ambazo ni jagoni na rejesta.
Quote:
Quote:
Quote:Jagoni: ni aina mojawapo ya lugha inayotumika katika taaluma fulani mahususi kama vile fasihi, isimu, sheria, sayansi, uhandisi, biashara nakadhalika. Hii ina maana kwamba, lugha hii itafahamika na wale tu walioko katika taaluma husika au wenye maarifa ya taaluma hiyo. Kwa mfano wanaisimu hutumia maneno kama vimadende, vitambaza, vipasuo kwamizi nk. wakirejelea jinsi ya utamkaji wa aina fulani za sauti katika lugha. 
Quote:
Quote:
Quote:Rejesta: Halliday (1989), anafasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi au shughuli. Vilevile fasili hii inaendana na fasili ya Habwe na Karanja (2007).
Quote:
Quote:
Quote:Kwa ujumla tunaweza kufasili rejesta kama mtindo wa lugha kutegemeana na kazi fulani, muktadha wa matumizi, lengo na uhusiano wa wanaowasiliana. Katika muktadha rasmi rejesta hurejelea upande mmoja kama vile, msamiati wa kiufundi, adabu maalum na matumizi ya lugha fasaha, mfano katika elimu, mahakamani nakadhalika. 
Quote:
Quote:
Quote:Mazingira yasiyo rasmi: haya ni mazingira ambayo hayafungwi na kaida, sheria na tamaduni za kijamii. Mazingira haya hutumia msamiati ambao si rasmi yaani lugha isiyokuwa sanifu. Katika mazingira haya tunapata aina zifuatazo za lugha ya mazungumzo: misimu, agoti, rejesta na lahaja. 
Quote:
Quote:
Quote:Misimu: Msanjila na wenzake (2009:19) wanafasili dhana ya misimu kuwa ni aina ya misemo katika lugha ambayo huzuka na kutoweka. Sifa kuu ya misimu ni kwamba haidumu muda mrefu na sio lugha sanifu, na watumiaji wa misimu huwa ni kikundi cha wazungumzaji wa lugha katika jamii ambao kimsingi huishi katika eneo moja.
Quote:
Quote:
Quote:Ngure (2003:147) anaonekana kukubaliana na Msanjila kwa kiasi kikubwa isipokuwa yeye anaweka mkazo zaidi hasa pale anapodai kwamba, uzukaji wa misimu ni wa ghafla na wakati fulani hufuatana na mambo au matukio maalum ya wakati au msimu huo. Anaendelea kufafanua kuwa misimu huzuka/huibuka na kutokeweka kufuatana na hali mbalimbali za kimazingira. Hata hivyo baadhi ya misimu hudumu na kuwa sehemu ya lugha. Kwa mfano neno matatu (Kenya) au daladala (Tanzania) ni neno lililotumika kurejelea nauli iliyolipwa miaka ya sitini. Hivi leo limekuwa neno linalomaanisha aina fulani ya magari ya usafiri. Katika muktadha wa mazungumzo misimu inachukuliwa kama ni aina mojawapo ya lugha ya mazungumzo itumiayo maneno yanayozuka kutokana na matukio mbalimbali ya kijamii, ambayo hiibuliwa na makundi mbalimbali katika jamii, hivyo misimu hutofautiana baina ya kundi moja na jinguine. Kwa mfano, misimu wanayotumia vijana ni tofauti na wanayotumia wazee au yanayotumia wanaume ni tofauti na wanayotumia wanawake.
Quote:
Quote:
Quote:Vilevile hata mazingira inamotumika misimu si mazingira rasmi kutokana na maneno yake kuzuka na kutoweka na hayatumiwi katika mazingira rasmi.
Quote:
Quote:
Quote:Agoti: ni lugha itumiwayo na kundi fulani la wahalifu au watu ambao wanaficha uovu wao usifahamike katika jamii wanamoishi. Mara nyingi lugha hii hutumiwa katika mazingira yasorasmi na kikundi kidogo cha watu kama vile, madereva wa magari, watumiaji wa madawa ya kulevya (mateja), majambazi, vibaka na wahuni wa mtaani. Mfano wa agoti inayotumiwa na watumiaji wa madawa ya kulevya ni kama vile, ndumu – bangi, sherehe ilikuwa na waalikwa wengi – soko la madawa ya kulevya lilikuwa na wateja wengi. Rejesta: Katika mazingira yasiyo rasmi, rejesta hutumia msamiati usio rasmi, matumizi ya misimu na ukatizaji wa maneno pamoja na udondoshaji wa baadhi ya vipashio katika maneno. Mfano, rejesta inayotumika katika mazingira yasiyorasmi kama vile mgahawani au hotelini ni kama vile nani wali ng’ombe? Ikiwa na maana kwamba nani aliyeagiza wali na nyama ya ng’ombe.
Quote:
Quote:
Quote:Utambulisho wa kijamii, Katika kipengele cha utambulisho wa kijamii tunaangalia namna aina ya lugha ya mazungumzo inavyoweza kujidhihirisha miongoni mwa watumiaji wake au kuwatambulisha na kuwatofautisha wanajamii husika. Lugha ya mazungumzo huweza kutambulika kutokana na aina zake, kwani katika jamii kila mtindo wa lugha ya mazungumzo una utambulisho wake katika jamii, kwa mfano agoti katika utambulisho wa kijamii unajulikana kama ni lugha ya wahalifu, jagoni ni lugha ya wanataaluma nakadhalika. Pia katika utambaulisho wa kijamii tunaangalia vile ambavyo mtu hutambulika katika jamii kulingana na namna anavyoongea kulingana na hadhi, tabaka, na jinsi ambavyo mtu huyo anavyoweza kusababisha mshikamano au mwachano katika mazungumzo. Kwa mfano jamii itamtambua mwanajamii kuwa ni msomi kulingana na mtindo wa lugha ya mazungumzo anaoutumia.
Quote:
Quote:
Quote:Nafasi yake: Katika kipengele hiki tunaangalia nafasi ya aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo katika jamii husika. Je aina hizi za lugha ya mazungumzo kama vile agoti, rejesta, jagoni, lahaja na misimu zina nafasi gani katika nyanja mbalimbali za maisha ya mwanadamu? Kwa mfano, kiuchumi, kisiasa, kielimu na kiutamaduni. Tukianza na kiuchumi, kwa mfano rejesta, ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kiuchumi kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Hii ni kutokana na kwamba, kwa mujibu wa King’ei (2010:94) madhumuni makuu ya mawasiliano katika biashara ni kuwavutia wateja na kuwafanya kuamini kuwa bidhaa ama huduma wanazouziwa ni za kiwango cha juu na ni thamani bora kwa pesa zao. Hivyo lugha ya biashara (rejesta), kwa kawaida ni lugha ya kutangaza uzuri wa bidhaa au huduma, huwa na sentensi au vifungu vifupi, mfano “Okoa mapesa chungu mbovu” pia huwa na lugha ya kupumbaza na kuaminisha, mfano “Kunywa XYZ kufumba na kufumbua afya yako itakurudia”.
Quote:
Quote:
Quote:Pia inasaidia sana kurahisisha mawasiliano miongoni mwa wazungumzaji katika masuala mbalimbali ya kibiashara na hata katika huduma mbalimbali za kijamii. Mfano hospitalini “mbili mara tatu”, hotelini “kuku wali tafadhali”, sokoni “kata nusu” na maeneo mengine. Baadhi ya rejesta na misimu hutumika kupunguza idadi ya maneno hivyo kufanya mazungumzo yawe mafupi na yanayoeleweka kwa urahisi mfano msimu “Daladala” kwa Dar es salaam linaweza kueleweka kwa urahisi zaidi kuliko kusema magari madogo yanayotumika kuchukua abiria chini ya 50 kutokea eneo moja hadi jingine kwa nauli ya shilingi 300. 
Quote:
Quote:
Quote:Pia rejesta za hotelini kama vile:- Muuzaji: wapi ng’ombe? Mteja: hapa Muuzaji: wapi chai chapati? Mteja: hapa. Si katika uchumi tu bali hata katika elimu rejesta ina nafasi muhimu sana, kwani zipo rejesta ambazo zinatumika katika maeneo rasmi kama vile shuleni katika kutolea elimudunia. Hapa rejesta inayotumika huwa rasmi na yenye kudhihirisha nidhamu. Mfano hutumika katika kuwanukuu watu wanaohusika katika maandishi ya kitaaluma, kama vile “kwa mujibu wa Pamphily, A. J. (2012) anafafanua kwamba…” 
Quote:
Quote:
Quote:Pia katika kutolea elimu ya dini kanisani na msikitini rejesta ina nafasi kubwa katika kujenga maadili. Vilevile rejesta na misimu ina nafasi ya kupamba mazungumzo, wazungumzaji wengi wanapozungumza hapa na pale hupenda kutumia maneno tofautitofauti kama vile misimu ili kufanya mazungumzo yawe ya kuvutia. Pia baadhi ya watu wanaona kuwa matumizi ya mitindo ya lugha ndio ujuzi wa lugha, hivyo hupenda sana kutumia mitindo hii ya lugha ili kuweza kurahisisha mawasiliano. Hivyo ina pendezesha lugha wakati wa mazungumzo. Mfano mazungumzo miongoni mwa vijana: 
Quote:
Quote:
Quote:Kijana 1: Jo? vipi tena mbona zii? Kijana 2: Poa Jo. Kama kawa… mambo mwaaa! Si rejesta na misimu tu, hata jagoni ina nafasi kubwa sana katika maendeleo ya kitaaluma, kwani wanataaluma mbalimbali hufanikisha malengo ya taaluma zao kupitia aina hii ya lugha ya mazungumzo. Mfano wahadisi, wahasibu, wanasayansi na washeria kila mmoja ana jagoni yake ambayo humsaidia kurahisisha mawasiliano miongoni mwao. Nafasi ya rejesta haiishii katika elimu au taaluma tu, bali hupea hata kuvuka mipaka ya kielimu na kutamalaki katika uwanja wa kisiasa. Hapa wanasiasa kama vile wanasayansi na wanasheria nao wana namna yao ya kutumia lugha. Mfano hupenda kuteua msamiati wenye kuleta mvuto na ushawishi katika jamii. Mfano maneno ya nasaha, kauli za kifalsafa mfano; “tumethubutu, tumeweza na tunasonga mbele” na uradidi wa vifungu mbalimbali vya maneno, hii yote inalenga katika kumfikirisha au kumpumbaza mtu kisiasa. Mbali na nafasi yake katika siasa, lugha ya mazungumzo kama ilivyo misimu, jagoni na rejesta agoti nayo ina nafasi yake miongoni mwa watumiaji katika jamii. Mfano wa nafasi ya agoti katika jamii ni kama vile: hutumika katika kujihami, kuficha na kuhifadhi siri za kikundi. Pia tusisahau kwamba mitindo mbalimbali ya lugha kama vile misimu inayo nafasi kubwa sana katika kukuza lugha hasa kwa kuongeza msamiati wa lugha husika, hasa misimu. Kwa mfano misimu iliyosanifishwa na kuingizwa katika lugha sanifu ni kama ifuatayo:- Daladala Basi la mtu binafsi linalotumika kusafirisha abiria mjini, linatumika zaidi Tanzania, jina lililotokana na nauli yake hapo mwanzo kuwa sawa na thamani ya shilingi tano ambayo ilikuwa ikijulikana kama dala kama msimu ilioibuka kipindi hicho. Kasheshe Hali ya kutoelewana inayotokana na watu kutokubaliana na jambo fulani.
Quote:
Quote:
Quote:Kwa kifupi tunaweza kusema kwamba aina zote hizo za lugha ya mazungumzo zilizojadiliwa hapo juu zina nafasi kubwa sana katika kikundi husika kinachotumia mtindo huo na katika jamii nzima kwa ujumla. Mfano wa nafasi yake katika matumizi ni kama vile kujihami, kujitetea, kukosoa, kurekebisha mienendo isiyokubalika, kukejeli, kutoelea maarifa, kurahisisha mawasiliano, kuficha au kuhifadhi siri za kikundi fulani, kupamba lugha na kutambulisha jamii husika au kikundi husika. Mfano wa rejesta zenye uficho ni kama vile:- Maneno ya mitaani maana katika lugha sanifu Demu msichana Kanyoosha goti kafariki. Kula kona ondoka. Mfano wa agoti zenye uficho:
Quote:
Quote:
Quote:Maneno ya madereva wa daladala maana katika lugha sanifu. Maiti Askari au mwanajeshi. (abiria asiyelipa nauli) Mchawi Gari linalokuja nyuma. Bibi Titi Askari mwanamke.
Quote:
Quote:
Quote:Matabaka, kwa mujibu wa kamusi ya Oxford (2004) ni kundi la watu wenye hali moja linalotokana na jamii yenye mfumo wa kiuchumi ambao hugawa watu.
Quote:
Quote:
Quote:Katika kipengele hiki cha matabaka, tutaangalia lugha kama kitambulisho cha jamii huwa na mitindo mbalimbali ya uzungumzaji ambayo huweza kuitwa aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo. Aina hizi yaani rejesta, lahaja, jagoni, misimu na agoti ndizo zitakazo tudhihirishia uwepo wa matabaka mbalimbali miongoni mwa wanajamii. Njia mojawapo ambayo huweza kutumika katika kuonesha matabaka au tofauti za kijamii ni lugha azungumzayo mtu. Hii huweza kumtambaulisha kwamba yeye ni wa tabaka la juu au la chini, tabaka la wasomi au la wasiosoma, tabaka tawala au tawaliwa, tabaka la wenye nacho au la makabwela (wasio na kitu/masikini). Hivyo basi tujipe fursa ya kutalii matabaka haya huku tukihusianisha na aina ya lugha ya mazungumzo.
Quote:
Quote:
Quote:Tabaka la juu, yaani hili ni tabaka la watu ambao wana hadhi fulani katika jamii kama vile mamlaka au cheo. Tabaka hili katika uzungumzaji wao hutumia lugha rasmi, fasaha na yenye staha, uteuzi mzuri wa msamiati na miundo sahihi ya tungo, kwa lengo la kulinda hadhi na mamlaka yao na kujitofautisha na tabaka la chini. Mfano wa lugha inayotumiwa na kundi hili ni rejesta rasmi. Tabaka la chini, yaani watu wasio na hadhi au mamlaka yoyote katika jamii. Matumizi ya lugha katika tabaka hili si fasaha kutokana na muktadha waliomo. Kwani shughuli zao kwa kiasi kikubwa huzifanya baina ya wao kwa wao pasipo kuchangamana na tabaka la juu. 
Quote:
Quote:
Quote:Hivyo aina ya lugha ya mazungumzo itakayopatikana katika tabaka hili ni rejesta isiyo rasmi pamoja na lahaja. Tabaka la wasomi, hili ni tabaka la watu wenye taaluma fulani, mfano wadaktari, waalimu, wahasibu, wahandisi na wengineo. Aina ya lugha itayotumiwa na tabaka hili kulingana na taaluma zao ni lugha rasmi kama vile jagoni na rejesta rasmi. Tabaka la wasiosoma, hili ni tabaka pana sana ambamo ndani mwake mna makundi mbalimbali ya wazungumzaji kama vile makuli, wamachinga, wapiga debe, vijana wa vijiweni, mfano mateja, vibaka na majambazi. Kundi hili ni kundi ambalo lipo katika mazingira yasiyo rasmi kutokana na shughuli wazifanyazo. Hivyo ni wazi kwamba hata lugha wazungumzayo si rasmi. Mfano wa lugha ipatikanayo katika tabaka hili ni agoti pamoja na misimu.
Quote:
Quote:
Quote:Ieleweke kwamba, mgawanyo wa matabaka haya haimaanishi kuwa mzungumzaji wa tabaka fulani hataweza kuzungumza aina ya lugha au mtindo wa lugha wa tabaka jingine lahasha! Mzungumzaji wa tabaka lolote anaouwezo wa kuzungumza mtindo wowote wa lugha isipokuwa jagoni, kwani hapa mzungumzaji asiye wa taaluma hiyo hataweza kuzungumza mpaka awe na ujuzi wa taaluma husika. Hivyo mzungumzaji mmoja ataweza kuzungumza aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia vigezo vifuatavyo; umri, mada ya mazungumzo, mahusiano baina ya wazungumzaji, muktadha na hadhira. Pia katika mazingira mengine mzungumzaji anaweza kujinasibisha na aina fulani ya lugha ya mazungumzo inayopewa hadhi ya juu kama vile rejesta rasmi, misimu au jagoni kwa lengo la kutaka aonekane kana kwamba naye ni watabaka la juu au la wasomi.
Quote:
Quote:
Quote:Hadhi; Msanjila na wenzake (wameshatajwa) wanaeleza kuwa lugha yenye hadhi ni lugha iliyosanifishwa na kutumika katika mawasiliano yote rasmi, kwa mfano shuleni, kanisani au shughuli za kiserikali, katika kipengele cha hadhi hapa lugha ya mazungumzo inazingatia nafasi aliyonayo mtu katika jamii yake. Kwa hiyo hadhi ya lugha huendana na hadhi ya wazungumzaji wa lugha husika, kwa mfano mwalimu, askofu, ustadhi au kiongozi wa serikali katika mazungumzo yake hutumia lugha yenye hadhi ambayo ni lugha rasmi ambayo imesanifiwa na kukubalika kutumika katika mawasiliano yaliyo rasmi. Hadhi ya lugha huweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha ambayo ni kama vile rejesta na jagoni. Kwa mfano rejesta za shuleni hutumia msamiati wa lugha yenye hadhi ambayo ina msamiati ulio rasmi, kwa mfano msamiati utakaozungumzwa na mwalimu ni msamiti rasmi kulingana na hadhi yake na hadhi ya lugha inayotumika katika mazingira yote ya shuleni. Vile vile msamiati utakaozungumzwa na Askofu, padre au mchungaji atazingatia hadhi yake na hadhi ya lugha anayoitumia katika mazingira ya kanisani. Msamiati utakaotumika ni msamiati wa lugha yenye hadhi. Vilevile katika mtindo wa jagoni tunaweza kupata msamiati ulio rasmi na unaotumika na watu wenye hadhi fulani katika jamii. Kwa mfano:-
Quote:
Quote:
Quote:Jagoni za kikemia. Msamiati wa kawaida wa kiswahili. H2O Maji O2 Oksijeni Co Hewa ya ukaa. Jagoni hizo huzungumzwa na watu wenye ujuzi wa kemia.
Quote:
Quote:
Quote:Jagoni za wanaisimu msamiati wa kawaida wa Kiswahili. Uwandani Mafunzo kwa vitendo Ndaki Vyuo vikuu. Ndiva Bwawa kubwa la kuhifadhi maji. Jagoni hizi huzungumzwa na wasomi. Kwa hiyo hadhi ya wazungumzaji wa lugha hufungamana sana na hadhi ya lugha waitumiayo katika mazungumzo. Kulingana na utofauti wa kihadhi walionao wazungumzaji katika jamii ni wazi kuwa utofauti huu utapelekea kutokea kwa mambo kadhaa, kama vile: • Upekee katika mtindo wa mawasiliano, mfano hotuba, mahubiri, mawaidha nakadhalika. • Adabu katika mazungumzo. • Upekee katika uteuzi wa msamiati kulingana na hadhi. Hivyo aina ya lugha itakayopatikana kulingana na hadhi ya mzungumzaji itakuwa ni rejesta rasmi. Hii ni kutokana na kwamba mazingira ya mchungaji, ustadhi, ofisa na viongozi wa serikali ni mazingira rasmi na ndio maana hata rejesta inayotumika ni rasmi. 
Quote:
Quote:
Quote:Msikamano na mwachano: katika utambaulisho wa kijamii dhana ya mshikamano katika aina mbalimbali za lugha ya mazungumzo, Crastal anfafanua dhana ya mshikamano kuwa inamaanisha mfanano wa uzungumzaji uliopo katika watu, familia, jinsi, tabaka moja, watu wenye hadhi sawa au shughuli sawa au makabila sawa. Kwa hiyo watu hawa watakuwa na mshikamano (mfanano) katika namna ya utamkaji wa vipashio mbalimbali katika maneno na pia watakuwa na mshikamano katika msamiati. Mfano, walimu, madaktari, machinga, wahandisi na kadhalika.
Quote:
Quote:
Quote:Dhana ya mwachano: katika lugha ya mazungumzo dhana ya mwachano inamaana kwamba ni ile hali ambapo wazungumzaji wa lugha moja hutofautiana katika baadhi ya vitamkwa katika maneno na pia hutofautiana katika baadhi ya msamiati. Mfano, Mhandisi na Daktari huweza kuwa na mwachano katika baadhi ya msamiati, kwa mfano, daktari anaweza kutumia msamiati kama vile “bomba” akimaanisha kifaa kinachotumika kwa ajili ya kudungia sindano wakati huohuo mhandisi atatumia neno hilohilo akimaanisha kifaa kinachotumika kusafirishia maji kutoka chanzo chake hadi kwa watumiaji, hivyo hali kama hii huweza kusababisha mwachano. Mwachano huu uliopo baina ya wazungumzaji huweza kusababishwa na mambo yafuatayo:
Quote:
Quote:
Quote: • Elimu; Yule (1985) anasema kwamba hata wazungumzaji wasomi walio na usuli sawa wa elimu, mfano waliomaliza shule miaka ya hivi karibuni watakuwa na mwachano na wale wanaoendelea kusoma.
Quote:
Quote:
Quote:• Shughuli/kazi; Yule (ameshatajwa) anasema kwamba shughuli au kazi wanazozifanya watu katika jamii watakuwa na kiasi fulani cha athari kwa kila mzungumzaji, hii ni kwa sababu kila kazi ina kiasi fulani cha jagoni ambacho hakihusiani na shughuli nyingine, hivyo itapelekea kutokea kwa mwachano.
Quote:
Quote:
Quote:• Matabaka ya kijamii; Labov (1972) katika utafiti wake alioufanya katika jiji la New York aligundua kwamba kunamwachano mkubwa kati ya tabaka la chini na la juu, anasema kwamba sauti /˄/ kama katika neno sun /s˄n/ inatumiwa na tabaka la juu wakati tabaka la chini wanatumia sauti /ʊ/ katika neno hilo hilo, vilevile kiambishi tamati –ing katika neno kama vile coming kinatamkwa na tabaka la juu wakati tabaka la chini wanatamka kwa kuishia na kiambishi –in katika neno hilo hilo.
Quote:
Quote:
Quote:• Umri; Yule anasema mwachano au mshikamano unaweza kusababishwa na umri wa wazungumzaji. Anasema kuwa hata katika tabaka fulani katika jamii, mwachano huweza kudhihirika kutokana na kigezo cha umri wa wazungumzaji, kwa mfano vijana waishio katika eneo fulani watatofautiana na wazazi wao katika namna yao ya kuzungumza.
Quote:
Quote:
Quote:• Jinsi; hii pia hupelekea mwachano katika uzungumzaji, Yule anasema wasichana wanapenda kutumia miundo ya lugha ambayo inahadhi ya juu katika jamii, tofauti na wanaume ambao wote wana usuli sawa wa kijamii. Miundo kama I done it na he ain’t hutumiwa sana na jinsi ya kiume katika mazungumzo yao na miundo kama I did it na he isn’t hupatikana sana katika mazungumzo ya jinsi ya kike. Pia tofauti hujitokeza katika namna ya kutamka neno, matamshi hutofautiana namna wanavyotamka jinsi ya kike na jinsi ya kiume. 
Quote:
Quote:
Quote:• Tukio; mwachano mwingine hutokea katika hali ya mzungumzaji kulingana na tukio lililoko mbele yake. Mfano, mzungumzaji anayekwenda kufanya usaili wa kazi atazungumza na katibu mhutasi: “samahani, meneja yumo ofisini? Nina miadi naye”. Mzungumzaji huyo huyo anapomuuliza rafiki yake juu ya rafiki yake mwingine atasema: oya, huyo mjinga bado amelala? Nataka kuonana naye juu ya jambo fulani. Kwa hiyo kutokana na tofauti hizi wazungumzaji wengi wana uamuzi wa kuchagua mwachano upi au mshikamano upi wafuate, mfano anapokuwa na mchumba wake, mpenzi wake, watoto, bosi, daktari, mchungaji, padri, au sheikh.
Quote:
Quote:
Quote: Kwa ufupi David Crystal anasema kwamba, mwachano na mshikamano huonekana kwa urahisi pale ambapo meneja wa biashara fulani anapotumia lugha rasmi anapokuwa ofisini na kuhamia lugha isiyo rasmi anapokuwa nyumbani. Pia mhadhiri anapotoa mhadhara atatumia lugha rasmi na fasaha lakini anapokuwa na wahadhiri wenzake atajadili hoja hizo hizo katika lugha isiyo rasmi. Kimsingi dhana hizi mbili yaani mwachano na mshikamano ndizo hupelekea kutokea kwa aina za lugha kama lahaja, jagoni, rejesta, agoti na misimu.
Quote:
Quote:
Quote:Utambulisho wa kimuktadha. Katika kujadili kipengele hiki tutaangalia aina za lugha zinazojitokeza katika lugha ya siri na yenye mipaka, michezo ya matendo, kucheza na maneno, uganga kama miviga na utani kama miviga.
Quote:
Quote:
Quote:Lugha ya siri na yenye mipaka, ni lugha inayotumiwa na watu wawili au zaidi kwa kuzungumza lugha ambayo hubagua baadhi ya hadhira iliyopo. Lugha itumikayo haitoweza kueleweka kwa wale wasiolewa msamiti unaotumika, madhumuni ya kutumia lugha ya uficho ni kutaka mazungumzo hayo yawe siri baina ya wazungumzaji peke yao. Mara nyingi watu wanapotumia lugha ya uficho aghalabu misimu huzuka.
Quote:
Quote:
Quote:Mfano katika jamii ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna baadhi ya maneno yanatumika chuoni peke yake, iwapo maneno hayo yatatumika nje ya mazingira hayo ya chuo hayataeleweka kwa wanajamii wa nje ya chuo. 
Quote:
Quote:
Quote:Hivyo basi suala la mipaka ya kijiografia huingia katika suala hili. Mipaka ya kijiografia hutumika kuangalia jinsi msamiati kadhaa unavyotumika katika jamii bila kuvuka mipaka, kwa maana hiyo tunaweza kusema kuwa katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna msamiati ambayo huwa na mipaka, haiwezi kutumika nje ya chuo.Mfano wa masamiati kama vile madesa, neno hili lina maana ya kitini, kitini hiki huweza kuwa na ukubwa wowote. Kwa mwanafunzi yeyote wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam msamiati huo wa madesa ni msamiati ulio vichwani mwao na kueleweka. Lakini iwapo msamiati huu utatumika nje ya chuo (nje ya mipaka ya chuo) utakuwa ni msamiati mgumu kueleweka kwa walio nje ya chuo mfano msamiati huu ukizungumzwa maeneo ya Tabata, Mbagala au Tanga wananchi wa maeneo hayo hawataelewa. 
Quote:
Quote:
Quote:Pia katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuna msamiati mwingine unaotumika ambao ni “darasa la saba” wanachuo waonapo askari huwaita darasa la saba neno hili linaweza kuwa na maana sawa na msimu. Katika mipaka ya ndani ya chuo neno hili lina maana ya askari. Iwapo wanafunzi wawili kutoka chuoni wakiwa katika mazungumzo katika mazingira ya nje ya mipaka ya chuo huku wakiwa katika mazungumzo yao wakiwaona askari basi watasema, “…unawaona darasa la saba?….” wakimaanisha askari. Hivyo kama kuna wanajamii walioko pembeni yao hawatoweza kuelewa chochote kwani hii ni lugha yenye uficho na yenye uwezo wa kuwa na dhima ya misimu. Ruti, neno hili linamaanisha maandamano katika chuo cha Dar es salaam. Neno hili linaweza kuwa sawa na hadhi ya misimu iwapo litatumika nje ya mipaka ya chuo halitaweza kufahamika kwa hadhira hiyo. Wanafunzi wakitoka nje ya mipaka ya chuo na kusema “ …kesho tunapiga ruti…” Watu hawataelewa neno hilo litakuwa gumu kuelewa kwa wanajamii na litakuwa na uficho kwa wanaomzunguka yule anayeongea. Vilevile kikundi cha wahalifu kama vile wavuta bangi, hawa pia wana lugha siri na mipaka ijulikanayo kama agoti. Kundi hili huitumia lugha ya siri na yenye mipaka pale wanapokuwa katika vitendo vyao vya kihalifu. 
Quote:
Quote:
Quote:Lengo la kutumia lugha hii ni kuficha uhalifu wao kwa watu walionje ya kundi hilo. Kwa mfano wanapomuona askari utasikia wakisema “…soo mwana…” yaani wakimaanisha hali ya hatari. Hivyo basi kwa ujumla tunaweza kuona jinsi gani lugha ya siri na yenye mipaka inavyoweza kuzalisha lugha ya mazungumzo.
Quote:
Quote:
Quote:Michezo ya matendo: ni michezo ambayo aghalabu huendana na vitendo kutendeka kuendana na mazungumzo yanayozungumziwa. Mtu azungumzapo maneno fulani, basi hufanya vitendo vinavyolandana na maneno anayotamka. Katika jamii yoyote ile hapakosekani michezo, michezo hiyo inaweza kuchezwa na watu wa rika fulani, mfano watoto wadogo hawa wana michezo yao, pia katika umri wa vijana wanaobalehe au kuvunja ungo. Kwa mfano, katika mchezo wa watoto wa kujificha unaoitwa kombolela, katika mchezo huo watoto wengi hutakiwa kujificha sehemu mbalimbali na kumuacha mototo mmoja kulinda kopo moja lisigongwe na watoto wengine waliojificha na kuwakomboa wenzake. Neno “kombolela” limetokana na neno komboa, pindi mtoto mmoja anapojitokeza na kupiga kopo lile husema “kombolela” yaani nimewakomboa wenzangu.
Quote:
Quote:
Quote:Hivyo katika mchezo huu tutaweza kupata rejesta kama vile kombolela na pia katika mchezo huu mtoto mmoja akionekana na mlinda kopo basi mlinzi huyo hutamka neno moja (jina) la mtoto aliyemuona mfano Juma, Aziza, Salome au Ndege hapa akimaanisha nimemuona Juma, Aziza, Salome au Ndege. Hivyo atamkapo jina moja inamaanisha kuonwa kwa mtoto. Hii ni mojawapo ya lugha ya mazungumzo katika mchezo huu.
Quote:
Quote:
Quote:Pia katika mchezo mwingine wa vitendo ni mchezo wa karata, mchezo huu huchezwa na watu wenye umri tofauti tofauti, hutumia kadi ndogo ndogo zipatazo 54. Katika mchezo huu aghalabu tunapata lugha ya mazungumzo ambayo ni tofauti na lugha itumikayo katika michezo mingine kama mchezo wa mpira wa miguu, pete au ule wa watoto wa kombolela, hapa tunaweza kupata maneno tofauti tofauti kama vile:- “Lamba” neno hili linamaanisha ongeza karata au muda mwingine wachezaji husema “inama” wakimaanisha chukua karata au kadi ya ziada. “Lasti kadi” mchezaji iwapo amebakiwa na karata ya mwisho basi husema lasti kadi kumaanisha amebakiwa na kadi ya mwisho inayoweza kumaliza mchezo na kuibuka mshindi. 
Quote:
Quote:
Quote:Pia kuna maneno kama vile cheza mavi, kopa au kisu mchezaji mwingine, ataelewa lugha hiyo wakati wa kucheza mchezo. Neno jingine ni “geuza mchezo” mchezaji mmoja akitamka neno hilo basi humaanisha mwelekeo wa mchezo kama ulikuwa uelekee kushoto basi mchezo sasa utaelekea kulia, pia kuna neno stop, mchezaji akimaanisha mtu fulani aliye karibu yake katika mchezo anapaswa kusubiri, yaani asicheze kwanza. 
Quote:
Quote:
Quote:Kwa ujumla mchezo wa vitendo kama huu huwa na lugha yake ya mazungumzo ambayo kwayo tunapata dhana ya misimu na rejesta. Kucheza na maneno, ni mbinu ya kifasihi ambayo kwayo, maneno yanayotumiwa yanakuwa na hoja kuu ya kazi. Kimsingi hutumiwa kwa ajili ya kuleta athari iliyokusudiwa au kuburudisha. Mara nyingi mchezo wa maneno huusisha sifa zifuatazo, kutoa tabia za majina, maneno na maana zake zisizoeleweka kwa urahisi, usemaji wenye ujanja wa kuficha maana ya moja kwa moja na sentensi ambazo zinakiuka miundo ya kawaida ya sentensi. Mifano ya michezo ya maneno inayotoa tabia za majina ni kama ifuatayo:- Dar es Salaam = Lala salama Afrika nzima = Wazimana Tanga = Wanatanga tanga Wakenya = Wanakenyana Tanzania = Wanazamia Naiorobi = Wanaibiana Arusha =Wanarushana rushana Wasukuma = Wanasukumana Uganda = Wanagandana Mfano miundo ya sentensi zisizo na mpangilio maalumu kwa lengo la kuficha maana ya moja kwa moja. Kuzungumza kwa kupindua maneno na kuwa kinyume:- “naku zimwi ndapamea nyekwe riga”. Maana yake ni, kuna mwizi amepanda kwenye gari. Mfano mwingine wa kucheza na maneno, “katibu kata wa kata ya makata alikataza katakata kukata miti iliyo katikati ya kata ya makata”.
Quote:
Quote:
Quote:Vilevile katika lugha ya kiingereza mchezo wa maneno huweza kujidhihirisha kama ifuatavyo: “Katai is a maasai, Katai can tie and utie a tie, if Katai can tie and untie a tie why can’t I tie and untie a tie like Katai?”
Quote:
Quote:
Quote:Utani kama miviga, utani kama miviga ni kipengele cha lugha ya mazungumzo kinachoweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha. Oxford, (2004) wanaeleza kuwa utani ni taratibu za kimila ambazo zinawafanya watu kuambiana au kutendeana jambo lolote bila ya chuki, maneno ya kutania, dhihaka na masihara. 
Quote:
Quote:
Quote:Ipara, na Waituru, (2006) Utani ni kufanyiana mzaha au masihara baina ya watu na makundi mbalimbali katika. jamii. Maana ya miviga. Ngure, A. (kashatajwa) nafafanua kwamba miviga, ni sherehe za kijadi ambazo zinajihusisha na kumpa mtoto jina, harusi, mazishi, matambiko, kutawazwa kwa viongozi, unyago, jando na kadhalika. Utani kama miviga una umuhimu wake katika jamii, umuhimu huo ni kama vile kukumbusha mambo muhimu katika jamii, hapa mambo muhimu ni yale ya kihistoria ya jamii husika, pia hufundisha na kuadilisha, mila na desturi, maadili na tamaduni mbalimali katika jamii. Pia utani kama miviga huwa na dhima ya kuburudisha jamii. 
Quote:
Quote:
Quote:Vilevile utani kama miviga husaidia kuonyesha uhusiano iliopo baina ya wanajamii, kujenga na kudumisha mahusiano bora katika jamii, pia hutumika kutoa onyo, kutahadharisha jamii kwa njia ya ucheshi. Utani pia hujumusiha vitendo maalumu kama vile kuimba, kurukaruka na kucheza ngoma. Hivyo basi, kipengele hiki cha lugha ya mazungumzo huweza kuibua mitindo mbalimbali ya lugha isiyo rasmi ambayo ni kama vile rejesta na misimu.
Quote:
Quote:
Quote:Uganga kama miviga: Oxford wanafasili uganga kuwa ni kazi ya kuponya wagonjwa, utabibu, dawa. Mkwera, (hakuna mwaka) anadadafua dhana ya uganga kwa kuhusianisha na waganga. Anaeleza kwamba kuna waganga wa aina sita, katika makundi mawili. kundi la kwanza ni la matabibu wa kweli, waganga waponyao magonjwa. Hawa ndio waganga wa mitishamba wa dawa ndogo ndogo (waganga wa kienyeji), madaktari na wauguzi (hawa ni watu waliosomea elimu ya magonjwa mbalimbali, aidha teknolojia na njia mbalimbali zilizo safi na halali za uponyaji), waombezi (hawa ni waliokirimiwa na Mwenyezi Mungu karama (uwezo) ya kuponya. Kundi hili halina ushiriki na kusalia miungu. Kundi la pili ni wale naofanya uganga kwa kujishughulisha na kujihusisha sana na majini mizimu, kama vile waganga wa kitamaduni wa maradhi, wajuzi wa mazingira, wataalamu wa kienyeji na kadhalika. Katika kundi hili la pili wamo: wapiga ramli, walozi na wachawi.
Quote:
Quote:
Quote:Hivyo basi katika kipengele hiki tutaangali kwa jicho pevu uganga kama miviga unaofanywa na waganga walio katika kundi la pili. Uganga kama miviga ni sherehe maalum zinazofanywa kwa lengo la kuponya maradhi, kuagua, kutuliza miungu na mizimu, kuondoa mikosi na kutakasa wanajamii. Mara nyingi uganga kama miviga huambatana na matendo mbalimbali yafanywayo na mganga pamoja na washiriki wake. Matendo hayo ni kama vile kurukaruka, kuimba na kucheza na kububujika vifungu vya maneno visivyo na mantiki wala kueleweka. Kwa mfano, Mganga anamwita mhemba wake, “Msondo”
Quote:
Quote:
Quote:“Labekha Bwana”, aliitika Msondo.
Quote:
Quote:
Quote:“Lete lile pembe langu la tunguli, ubani, na kisu cha kuchinjia”
Quote:
Quote:
Quote:“Ewala Bwana”.
Quote:
Quote:
Quote:Anaendelea kububujika maneno yeye peke yake;
Quote:
Quote:
Quote:“Ndiyo, ndiyo, Nieleze Ruhani, yalikuwaje?”… “Kwa nini hunipi mfupa wa taarifa yote; ni wapi yalitokea yote haya?”… “Nani alimtuma? Kwa kisa gani? Ni nini akitakacho?”… “Ahaa! bibi yake alikwenda Bubuye kwa mganga na kuliomba hilo kombe?”… Mfano wa wimbo wakati wa shughuli za uganga, “Ee changu, changu njoo! Ee changu, changu njoo! Ee changu, change njoo!
Quote:
Quote:
Quote:Mlete babu mwamba, mlete yeye ajue’ Mlete yeye aone, mlete yeye tumchinje, Mlete yeye tumkamate; mlete, mlete, mlete!
Quote:
Quote:
Quote:Mlete, mlete, mlete! Mlete, mlete, mlete! Eee ee hoo; ee ee hoo; ee ee hoo!
Quote:
Quote:
Quote:Cheza, soma, toroka, itika, imba! Eee ee hoo; ee ee hoo; ee eehoo!”
Quote:
Quote:
Quote:Haya ni baadhi ya maneno ambayo pindi yatumikapo mara moja mtu hugundua ni mazingira ya nama gani yanazungumziwa hapa. Katika hali ya kawaida mtu asikiapo maneno kama hayo hawezi kuhusisha na mazingira ya kanisani, bali atahusisha na mazingira ya maeneo ya kiganga na nguvu za giza.
Quote:
Quote:
Quote:Kwa ujumla kipengele hiki cha uganga kama miviga, tunaona jinsi kinavyoibua mitindo ya lugha ya mazungumzo kama vile rejesta isiyo rasmi, lahaja, misimu ambayo huibuliwa na kutumika na makundi haya ya waganga. Pia agoti hujitokeza kwa lengo la kuficha siri ili mteja (mgonjwa) wake asigundue ujanja wake. Ifahamike kwamba mazingira haya si rasmi kama ilivyo kwa waganga wa kundi la kwanza, hivyo hata aina ya lugha ya mazungumzo itumikayo haitakuwa rasmi.
Quote:
Quote:
Quote:HITMISHO:
Quote:
Quote:
Quote:Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa katika kukamilisha dhana nzima ya matumizi ya lugha, tumeweza kuona uhusiano mkubwa uliopo kati ya mitindo mbali mbali ya lugha ya mazungumzo na utambulisho wa kijamii na kimuktadha na jinsi mitindo hiyo inavyoweza kutambulisha na kutofautisha makundi mbalimbali ya wazungumzaji katika jamii.

Print this item

  Lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi?
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:41 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha - No Replies

Lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi?. Huku ukijikita katika nduni za lugha ya mazungumzo, jadili kauli hii.

Katika kujadili swali hili, tutaanza kujadili nini maana ya lugha kwa mujibu wa wataalam mbalimbali, pia tutatoa maana ya lugha ya mazungumzo, maana ya muundo rasmi na hatimaye tutaingia katika kiini cha swali ambapo tutakubaliana na swali kwa kutumia uthibitisho wa nduni (sifa) za lugha ya mazungumzo jinsi zinavyofanya lugha ya mazungumzo isiwe na muundo rasmi. Yaani tutaangalia ni kwa vipi sifa za lugha ya mazungumzo zinavyopelekea lugha ya mazungumzo kukosa sifa ya kuwa na muundo rasmi. Na mwisho tutatoa hitimisho.
Massamba (2009) anaeleza kuwa, lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimekubaliwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano yao.
Mgullu (1999) kama alivyomnukuu Trudgil (1974) anafafanua kuwa, lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zinazotumiwa kwa mawasiliano miongoni mwa watu wa jamii fulani wenye utamaduni wake.
Kwa ujumla tunaweza kusema kwamba, lugha ni mfumo wa sauti nasibu ambazo zimebuniwa na jamii kwa madhumuni ya mawasiliano miongoni mwao.
Dhana yingine tuliyoiangalia kulingana na swali hili ni lugha ya mazungumzo. Kwa mujibu wa Wikipedia, wanasema lugha ya mazungumzo ni utaratibu wa kuongea baina ya pande mbili, kwa kawaida wahusika ni watu. Lugha ya mazungumzo huwa na mitindo mbalimbali kama vile rejesta, misimu, jagoni na agoti.
Kisha tukaangalia dhana ya muundo, kwa mujibu wa Concise Oxford Dictionary (2001) (toleo la 10) muundo ni mpangilio na uhusiano wa vitu katika kuunda kitu kizima;
Katika muktadha wa mazungumzo, muundo rasmi ni ule mpangilio unaohusisha kanuni na taratibu zilizowekwa katika uzungumzaji ambapo kila mzungumzaji hana budi kuzingatia wakati wa mazungumzo.
Vilevile tunapozungumzia muundo rasmi katika lugha huangalia mpangilio wa maneno na muundo wa sentensi na namna maneno na sentensi hizo zinavyopangiliwa na kuleta mtiririko wenye maana na uliokamilika na unaoweza kueleweka na watu wote.
Kutokana na fasili hii lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi, hii ni kwa sababu haizingatii vigezo hivyo wakati wa uzungumzaji na hivyo kuonekana kutokuwa na muundo rasmi na hii ndiyo sifa mojawapo kati ya sifa zinazojidhihirisha katika lugha ya mazungumzo.
Hivyo basi tunaweza kuthibitisha kauli hii kwamba, lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi kwa kujikita katika sifa au nduni za lugha ya mazungumzo kama ifuatavyo;
Kwa mujibu wa King’ei (2010), anaorodhesha sifa zinazojitokeza katika lugha ya mazungumzo ambazo ni kama ifuatavyo;
Ubadilikaji wa kila mara wa maudhui, na uteuzi usiotabirika wa maneno, kauli au usemi. Hivyo katika sifa hii tunaona kwamba hakuna muundo rasmi kutokana na kwamba mzungumzaji ana uteuzi wa maneno na kauli zisizotabirika, hivyo anaamua mwenyewe nini cha kusema bila kufuata muundo au kanuni zozote. Mfano anaweza kuanza na aina yoyote ya neno katika sentensi.
Utokezaji wa makosa wa aina tofauti katika mazungumzo, mfano kukosea matamshi, kusitasita, kusahau baadhi ya maneno, kuchanganya hoja, wazungumzaji kusema kwa pamoja na hivyo kupoteza uzi au mtiririko sahihi wa mazungumzo. Jambo hili hutokea kutokana na kukosekana kwa muundo rasmi unaowaongoza wazungumzaji. Kimsingi muundo rasmi hufuata kanuni madhubuti na utokeaji wa makosa haupo kwa sababu ya urasmi wake.
Pia kuwepo kwa uradidi / marudio na msisitizo kwa wingi katika mazungumzo na pia mazungumzo kukatishwa kwa vichekesho, miguno ama matumizi ya lugha ya ishara, hali hii hutokana na kutokuwepo na muundo maalum unaomwongoza mzungumzaji, ndiyo maana wazungumzaji hujikuta wakirudia rudia maneno wakati wa mazungumzo.
Masahihisho ya kila namna na pia ufafanuzi na maelezo hutolewa mara kwa mara pale utata unapotokea. Hii ni kwa sababu ya kutokuwepo kwa muundo maalum kama vile mpangilio wa mawazo, sentensi na mtiririko wa mawazo katika mada ndivyo vinapelekea kutokea kwa utata na kusababisha masahihisho ya mara kwa mara.
Matumizi ya sentensi fupi fupi, sentensi za neno moja moja au maneno yasiyokamilika hutokea kwa wingi katika mazungumzo pindi mzungumzaji anapozungumza kwa huweza kutumia sentensi fupi fupi, au kutumia maneno yasiyokamilika. Yote hii hutokana na kutokuwepo kwa muundo rasmi wa lugha ya mazungumzo. Katika hali ya muundo rasmi hauruhusu udondoshaji wa maneno au tungo au matumizi ya sentensi fupifupi ambazo hazijajitosheleza.
Msamiati mwepesi na unaofahamika kwa urahisi, pindi mzungumzaji wa lugha anapoongelea mada fulani mbele ya hadhira yake huangalia mandhari pamoja na uhusiano baina yake na wasikilizaji wake, hivyo anaweza kubadilika kulingana na hali halisi anayokutana nayo. Hii haijidhihirishi katika muundo rasmi kama vile lugha ya maandishi, mwandishi hazingatii muktadha au uhusiano baina yake na wasomaji wake, yeye huandika kazi yake bila kujua watakaosoma ni akina nani. Hivyo basi ubadilikaji huu wa msamiati kulingana na hadhira ya mzungumzaji unatuthibitishia kwamba lugha ya mazungumzo haina muundo rasmi.
Vilevile kuna uvunjaji wa kanuni za sarufi na matumizi sanifu kutegemeana na uhusiano wa wazungumzaji, katika lugha ya mazungumzo hakuna kanuni ambazo zinamfanya/kumbana mzungumzaji, hivyo basi kwa sababu ya kutokuwepo kwa kanuni hizo ni wazi kwamba lugha hii haitakuwa na muundo rasmi unaomuongoza mzungumzaji ndiyo maana mzungumzaji hujikuta akivunja kanuni. Mfano; mtu anaweka viambishi sehemu ambayo haihitajiki kiambishi kama vile neno nilikuwepo – nilikuwepogi, alimpaga au hakunaga. Pia wapare husema thatha ni thaa thaba kamili wakimaanisha kuwa sasa ni saa saba kamili. Vilevile Wahaya husema ngombe badala ya ng’ombe.
Pia katika lugha ya mazungumzo hakuna muda au nafasi ya kufikiria jambo lakuzungumza, hapa mzungumzaji hana muda wa andalio la anachotaka kusema, hutamka tu bila kufikiria jambo analotamka. Jambo hili la kutokuwa na muda wa kujiandaa ndilo hupelekea kutokea kwa miguno na makosa ya kimantiki. Lakini katika muundo rasmi mambo haya huwa hayajitokezi kwa sababu kuna maandalizi ya kutosha.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa, muundo wa lugha ya mazungumzo hauwezi kujidhihirisha moja kwa moja kwa watumia lugha isipokuwa huweza kuhusisha utaratibu fulani unaozingatia mada, muktadha na mahusiano ya wazungumzaji. Aidha hoja inasisitiza kuwa hakuna mada rasmi zilizozoeleka na zinazotumika na watu wote, vivyo hivyo kwa muktadha na mahusiano. Pia lugha hiyo haiwezi kuwa na mpangilio maalum wa kile kinachozungumzwa na maelezo yake kwa wazungumzaji baina yao.
MAREJEO:
Smith, T. (2001). Concise Oxford English Dictionary. (10th Edt). Oxford University Press. UK.
King’ei, K. (2010). Misingi ya Isimujamii. Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. Chuo Kikuu                                       cha Dar es salaam.
Massamba, D.P.B. (2009). Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha.TUKI, Dar es Salaam.
Mgullu, R.S. (1999). Mtalaa wa isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhornpublishers. Ltd. Nairobi

Print this item

  ZOEZI LA KUJIPIMA
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:35 AM - Forum: Mitihani - No Replies

SWALI: Onesha viunganishi katika sentensi zifuatazo na taja maneno na vipashio vinavyoungwa.

(a) Mama na mwanawe wameondoka
(b) Baba anachimba mashimo na mama anapanda mahindi
© Sitaongea naye hadi utakaporudi
(d) Mlipoondoka tu, mama yake alikuja kumtafuta
(e) Watoto waliofaulu wamechaguliwa kwenda sekondari
(f) Aliadhibiwa kwa sababu hana heshima.
Jaribu kujipima kwa kujibu maswali hayo na ukipata ugumu wasiliana nami kwa njia zilizopo.

Print this item

  MFANO WA SOGA
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:22 AM - Forum: Hadithi - No Replies

KIFENGE NA BARUA KWENDA KWA BWANA MUNGU
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Kifenge alikuwa maskini sana. Yeye na familia yake waliishi kwa kuombaomba chakula, mavazi na mahitaji mengine.
Siku moja wazo la kuomba msaada kutoka kwa Bwana Mungu lilimjia. Kifenge alienda dukani akanunua karatasi,bahasha na stempu akaamua kumwandikia Bwana Mungu barua.
Barua ilipofika posta wafanyakazi wa posta wakashangaa kuona  barua inatakiwa kutumwa kwa Bwana Mungu. Wakaifungua wakaisoma,wakamhurumia sana Bwana Kifenge. Wakaamua kuchanga fedha hadi zikafika laki tano,wakazituma katika anwani iliyokuwa kwenye barua.
Baada ya wiki moja fedha zikafika kwa Kifenge. Alifurahi sana na akamwambia mke wake, “Mke wangu sasa dhiki imeisha. Tununue mahitaji yote, tukae, tustarehe.”
Mke wake alifurahi sana akamuuliza mume wake, “Hivi siku zote tulikuwa wapi mume wangu? Kumbe ndiyo maana watu wanatajirika lakini hawasemi kama Bwana Mungu huwa anawatumia fedha?”
Wakanunua magunia ya mchele, sukari, unga, mafuta na nguo na mahitaji mengine mpaka fedha zote zikaisha.
Fedha zilipoisha na mahitaji yakaisha wakaandika barua ingine kwa Bwana Mungu kuomba msaada. Wafanyakazi wa posta walipoiona wakajua mwandishi ni yuleyule. Wakamjibu, fedha ulizopata kama hukuweka mtaji, hakuna fedha tena.
Bwana Kifenge alipoipata akazunguka kila mahali akitangaza kuwa atawashitaki wafanyakazi wa posta kwa sababu wameiba fedha zake alizotumiwa na Bwana Mungu. Hata hivyo wenye akili wakasema kweli wajinga ndio waliwao. “Hivi Kifenge hakujua kuwa ule ulikuwa ni msaada uliotoka kwa watu wema ambao alitakiwa kuutumia vizuri?”
Kelele za Kifenge hazikuzaa matunda, akarudia umaskini wake kama zamani.
Kutokana na hadithi ya Kifenge tunaona kuwa Soga ni hadithi fupi za kuchekesha au kukejeli. Mara nyingi wahusika wake ni watu wa kubuni, na huwa na kisa kimoja tu.

Print this item

  MFANO WA KISASILI
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:18 AM - Forum: Hadithi - No Replies

KISASILI
Kisasili ni hadithi fupi zinazoelezea asili ya jambo au maumbile fulani. Wahusika wake huwa ni wadudu, wanyama, binadamu, miungu na vitu visivyo na uhai, lakini huwa na hadhi ya kibinadamu. Mara nyingi kisasili huanza na “paukwa!”  mfano ni Kisa cha Nguruwe kukosa mkia. 
Paukwa! (Aliuliza bibi)
Pakawa! (Waliitikia wajukuu zake)
Hapo zamani za kale, palitokea ubishi kati ya nguruwe na ng’ombe. Kila mmoja akawa anatamba kuwa ana nguvu kuliko mwenzake. Bahati nzuri akatokea sungura akawauliza, “Kulikoni mbona mnabishana hivyo?” Nguruwe na ng’ombe wakamweleza chanzo cha ubishi wao.
Nguruwe akaanza kumkashifu mwenzake ng’ombe, “Huyu hanijui mimi! Ananisikia tu, nitamvunjavunja mbavu asahau hata njia ya kurudi kwao” Ng’ombe naye akadakia, “Wewe ni bwana mdogo tu, huo ufupi na unene wako hauwezi kunibabaisha.”
Sungura akasikiliza halafu akasema, “Hakuna sababu ya kubishana, mimi naona mshindane.” Wote wakakubali. Sungura akasema, “Nitawafunga mikia yenu pamoja. Nikihesabu moja, mbili, tatu muanze kuvutana. Yule ambaye mkia wake utakatika atakuwa ameshindwa.”
Basi wajukuu zangu, wote wakasema sawa. Nguruwe akamtahadharisha ng’ombe, “Mkia wako utakuwa halali yangu” Ng’ombe akaingiwa na woga, akatulia tuli kama maji mtungini, lakini akaamua kujikaza kisabuni.
Basi sungura baada ya kuwafunga mikia akahesabu moja, mbili, tatu wakaanza kuvutana. Wajukuu zangu mngekuwepo mngejionea kivumbi na jasho. Si mnajua wajukuu zangu, wapiganapo fahari wawili? Akauliza bibi. “Ziumiazo nyasi,” wakajibu wajukuu zake.
Punde si punde zilisikika kelele Guuuuu! Guuuuu! Guuuuu! na kishindo kikubwa puuu uu! Lahaula! Mkia wa nguruwe ulikatika, akaanguka chini puuuu na pua ikabonyea. Nguruwe akalia kwa uchungu, damu ikamtoka kwa wingi kama bomba la maji. Ng’ombe alikuwa mshindi.
Sungura kuona vile akakichukua kipande cha mkia; huyoooo! Akampelekea rafiki yake fisi. Nguruwe akajuta sana kwa nini alikubali ushindani.
Basi wajukuu zangu, hadi leo nguruwe na ukoo wake hawana mikia na pia pua zao zimebonyea. Wajukuu zake wakacheka na kusema, “Kumbe! Ndiyo maana nguruwe wana mikia mifupi”

Print this item

  ULAHAJIA NI NINI?
Posted by: MwlMaeda - 11-23-2021, 07:13 AM - Forum: Lahaja za Kiswahili - No Replies

Lugha ya Kiswahili ina Lahaja kadhaa kama vile Kiamu kinachozungumzwa Lamu, Kimvita(Mombasa), Kibajuni huzungumzwa sehemu za Kismayu, Somalia, Kipemba, Kitumbatu na Kimakunduchi huzungumzwa Zanzibar. Halima nyanza alitembelea visiwani Zanzibar, kujua zaidi juu ya Lahaja hizo zilivyoweza kuwa hai mpaka sasa, licha ya matumizi makubwa ya kiswahili sanifu.
Quote:
Ulahajia ni nini?
Dhana ya ulahajia inafaa vipi katika kuelezea utendaji wa lugha?
Quote:
Swali hili limegawanyika katika sehemu ‘a’ na sehemu ‘b’. Na katika kulijibu swali hili tukianza na kipengele ‘a’ tutajadili dhana ya ulahaji kutokana na wataalamu mbalimbali huku tukitoa fasili yetu kwa ujumla. Pia katika kipengele ‘b’ tutajadili kuhusu dhana ya utendi kwa mujibu wa wataalamu, pia tutajadili maana mazungumzo huku tukitoa fasili yetu. Na katika kujadili kiini chetu cha swali tutajadili dhana ya ulahajia jinsi inavyotumika katika kuelezea utendaji wa lugha na mwishoni tutatoa hitimisho la kazi yetu.
Dhana ya ulahajia imefasiliwa na wataalamu mbalimbali ambao wameifafanua dhana hii kama ifuatavyo:-
Crystal, D (2000) anafasili ulahajia kuwa ni taaluma inayohusu mfumo wa lahaja za kimkoa.
Wikipedia wanasema kuwa, ulahajia ni tawi la isimu linalojihusisha na taaluma ya lahaja.
Kwa hiyo dhana ya ulahajia hufafanuliwa kuwa ni taaluma inayojihusisha na uchunguzi wa lahaja za kimkoa.
Taaluma hii huchunguza utofauti wa lahaja kati ya mkoa mmoja na mkoa mwingine. Zamani taaluma hii ilijikita zaidi katika kufanya uchunguzi kwa wazee walioishi sehemu moja bila kuhama tangia kuzaliwa kwao, lakini kwa sasa taaluma hii uchunguzi wake umejikita zaidi katika maeneo ya mjini kutokana na kuchanganyika kwa makundi ya watu tofauti tofauti kutoka mikoa tofautitofauti.
Dhana ya utendi imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali ambao wamefasili dhana hii kama ifuatavyo:-
Wikipedia wanafasili utendi kuwa ni uzungumzaji wa lugha katika muktadha halisi, nini hasa mzungumzaji husema kwa kuzingatia makosa ya kisarufi.
Kwa hiyo utendi huweza kufasiliwa kuwa ni utumiaji wa lugha katika mazingira halisi. Lugha inayotumika lazima iendane na mazingira yaliyopo.
Vile vile mazungumzo yamefasiliwa na Oxford (2004) kuwa ni jambo linalojadiliwa na watu au kikundi cha watu kwa lengo fulani. Kwa mfano maongezi.
Halliday (1990) anasema mazungumzo huweza kuwa na makosa mbalimbali katika mpangilio wa sentensi au katika mtindo wa matamshi. Vile vile Halliday anasema lugha ya mazungumzo inasifa zake bainifu ambazo ni tofauti na zile sifa za lugha ya maandishi.
Kwa hiyo tunaweza kufasili mazungumzo kuwa ni jambo fulani linalojadiliwa na watu wawili au kundi la watu kwa lengo fulani.
Baada ya kujadili dhana hizo, sasa tunaweza kujadili ni kwa jinsi gani dhana ya ulahajia inavyoweza kuelezea utendaji wa lugha hususani katika lugha ya mazungumzo kwa kuzingatia lugha ya Kiswahili.
Utofauti wa matamshi. Ulahajia huchunguza matamshi ya wazungumzaji wa lugha kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano wazungumzaji kutoka mikoa ya kanda ya ziwa. Mfano wahaya kutoka mkoa wa Kagera katika matamshi yao hawana kitamkwa ng’ kwa hiyo wanapotamka maneno kama vile ng’ombe wao hutamka ngombe, neno ng’ang’ania hutamka ngangania, neno ung’amuzi wao hulitamka kama ungamuzi. Vile vile watu kutoka mkoa wa Mara ambao ni wakurya hutumia kitamkwa r badala ya l kwa mfano neno kula wao hulitamka kura, neno kulala hulitamka kurara, kulalamika wao hulitamka kuraramika. Pia wazungumzaji kutoka mikoa ya kusini mfano kutoka mkoa wa mtwara na lindi ambao ni Wamakonde wao hutumia kitamkwa n badala ya m kwa mfano mtoto hutamka kama ntoto, msichana hutamka kama nsichana, mchana hutamka nchana. Vile vile wazungumzaji kutoka mkoa wa mbeya ambao ni wanyakyusa wao hutamka f  badala ya v kwa mfano neno viatu vyangu hutamka kama fiatu fyangu, uvivu hutamka ufifu, viazi hutamka fiasi. Wazungumzaji wa kutoka mikoa ya kaskazini mfano wapare kutoka mkoa wa moshi hutumia kitakmwa th badala ya s kwa mfano badala ya kusema sisi sote ni wasichana wao hutamka thithi thote ni wathichana. Kwa hiyo tofauti hizo za kimatamshi zinatokana na athari za lahaja za mikoa waliyotoka.
Msamiati. Dhana ya ulahajia huweza kutumika katika kuchunguza msamiti mbalimbali wa wazungumzaji wa lugha moja kutoka mikoa tofauti tofauti. Kwa mfano watu kutoka Zanzibar wao hutumia msamiati tofauti na wazungumzaji wa mikoa ya bara, kwa mfano husema neno tungule kwa kumaanisha nyanya, neno malikiti humaanisha sokoni, mferejini humaanisha bombani, vile vile kabila la Wamakonde kutoka mkoa Mtwara hutumia neno kumaanika kwa kumaanisha kudharirika, kwa hiyo wazungumzaji hawa hutumia msamiati wa lahaja zao  kutokana na athari za lahaja hizo.
Muundo wa sentensi, vile vile dhana ya ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha kwa kuchunguza muundo wa sentensi wa wazungumzaji wa lugha moja, kwa kuchunguza muundo wa sentensi utaweza kubaini kuwa wazungumzaji wa lugha hii wanatokea mkoa gani, kwa mfano wazungumzaji wa mkoa wa Tabora hutumia wingi mahala pa nomino ya umoja wakiashiria heshima. Kwa mfano husema baba wanakuja badala ya kusema baba anakuja, mmefika salama? Badala ya kusema umefika salama?. Kwa hiyo mtu wa heshima kwao hutumia nomino ya wingi na hii yote ni kutokana na kuathiriwa na lahaja za mikoa watokayo.
Kiimbo. Ulahajia huweza kuchunguza kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti ya wazungumzaji wa lugha, kwa mfano kabila la Waluguru kutoka mkoa wa Morogoro wao huzungumza kwa kupandisha na kushusha mawimbi ya sauti.  Kwa mfano, “baba amekuja”. kwa hiyo athari hizo zimetokana na lahaja ya mkoa waliotokea.
Mkazo, mkazo ni kule kutumia nguvu zaidi katika kutamka maneno au sentensi. Yaani ni hali ya neno au silabi katika neno kusikika kuwa na nguvu zaidi kuliko silabi au maneno mengine. Kwa hiyo ulahajia huweza kuelezea utofauti wa mkazo uliopo katika baadhi ya wazungumzaji wa lugha moja. Kwa mfano kabila la Wasukuma kutoka mkoa wa Mwanza huweka msisitizo katika mazungumzo, kwa mfano “baba anakujaa”, pia wanaongeza vitamkwa ambavyo si vya msingi katika maneno yanayojitosheleaza. kwa mfano neno amekuja wao huongezea kitamkwa ga, = amekujaga, neno ameenda + ga, = ameendaga, hakuna + ga.=hakunaga.
Kwa hiyo mtu huweza kuwa na umilisi wa lugha fulani lakini asiwe mtendaji hususani katika lugha ya mazungumzo na hii ni kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuathiriwa na lahaja ya mkoa atokao, athari hizi hujidhihirisha zaidi katika lugha ya mazungumzo kama tulivyojadili hapo juu, lakini katika lugha ya maandishi athari hizi huweza kujidhihirisha kwa kiasi kidogo sana au zisitokee kabisa.
Kwa kuhitimisha tunaweza kusema kuwa dhana ya ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha husasani katika lugha ya mazungumzo kwani ndio rahisi sana kuchunguza tofauti za wazungumzaji wa lugha moja watokao sehemu tofauti tofauti, ambayo ni tofauti sana na kuelezea utendaji wa lugha katika lugha ya maandishi kwani ni vigumu sana kubainisha makosa ya kisarufi kama vile matamshi, kiimbo, mkazo, msamiati na hata muundo wa sentensi. Mara nyingi maandishi huandikwa kwa ufasaha zaidi ukilinganisha na mazungumzo na ndio maana ulahajia huweza kuelezea utendaji wa lugha hususani katika lugha ya mazungumzo.
Marejeo;
Crystal, D. (2002). The Cambridge of Encyclopedia of Language: Second edition. London. Cambridge University Press.
Halliday, M.A.K. (1990). Spoken and Written Language. London. Oxford  University Press.
Kamusi ya Kiswahili Sanifu, (2004). Nairobi. Oxford University Press.

Print this item