MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 79 online users.
» 0 Member(s) | 77 Guest(s)
Bing, Yandex

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  SHAIRI: KILA MTU NA MTUWE
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 07:44 PM - Forum: Ushairi - No Replies

*****KILA MTU NA MTUWE*****
Nilijua ndiye wangu , kumbe nae ana wake
Nikampa moyo wangu, Penzi langu alitunze
Kumbe siko peke yangu, Pengine Mtu wa nane
Nimepanda  penzi langu , kwenye mti wenye miba

Tena nilijimaliza , Mashoga kuwatambia
Mpenzi niliyepata, mfanowe sijaona 
Hana papara papara , macho ameyatuliza
Nimepanda penzi langu kwenye mti wenye miba

Mpenzi nilimpenda , Nikazama  hadi kichwa
Kila alichonambia ,  Binafsi sikumpinga
Niliona  nimepata , kumbe nimepatikana
Nimepanda penzi langu , kwenye mti wenye miba

Mpenzi  alitupanga, kila Mtu muda wake
Wote alitupeleka,Mpaka chumbani kwake 
Nguo tulimfulia , mpk  za siri zake 
Nimepanda  penzi  langu , Kwenye mti wenye miba

DINNA MINJA ( Mom JADEN)
K/ sec
8/8 /21

Ntaendeleaaaaaa.....

Print this item

  SHAIRI: LEO NADAI TALAKA
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 07:40 PM - Forum: Ushairi - No Replies

LEO NADAI TALAKA
Bwana nilimuamini, mfanowe sielezi,
Kuwa ni mwenye imani, amjuaye Mwenyezi,
Kumbe haikuwa dini, huyu bwana hajiwezi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Aliniambia hani, ni kufuru kwa Mwenyezi,
Ngoja tufike ndoani, tuianze yetu kazi,
Basi nami sawa hani, nikaacha uchokozi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Sasa tungali ndoani, imeshapita miezi,
Hakuna kitu chumbani, zaidi ya usingizi,
Jama huyu mume gani, asiyeipenda kazi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Jambo nimelibaini, haviachi visingizi,
Mara naumwa kichwani, na kubanwa kikohozi,
Ooh nimechoka hani, kama avyo sema juzi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Havui nguo mwilini, radhi alale na jezi,
Hukishusha kisirani, ati mie mpuuzi,
Niambieni jamani, waume wa siku hizi,
Kulala dada na kaka, leo nadai talaka.

Kumla ninatamani, kwa tamaa sijiwezi,
Mbuzi ina mana gani, kiwa haikuni nazi?
Najiuliza kichwani, mwazani huwa siwazi,
Kulala kaka na dada, leo nadai talaka.

Namkumbuka Mjuni, kijana toka Nyegezi,
Alivyoichanja kuni, kwa kazi hizi mjuzi,
Ni hatari kitandani, kama katoka Shirazi,
Kulala kaka na dada, leo nadai talaka.

Tuachane kwa amani, tusitoane machozi,
Nisemalo ukingoni, yangu mwisho maamuzi,
Twende basi ofisini, niwaambe viongozi,
Kuishi dada na kaka, leo nadai talaka.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo DSM
0753738704

Print this item

  SHAIRI: MOYO WA JIWE
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 07:31 PM - Forum: Ushairi - Replies (1)

MOYO WA JIWE

Sasa sinao uvivu, kiteko mie kuteka,
Sina tena maumivu, hata ninapoteseka,
Huwa nawa mtulivu, wala sina hekaheka,
Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

Ninao moyo wa jiwe, si tumbawe ni jabali,
lolote lile na liwe, kwangu halina ukali,
kipenzi achukuliwe, mwenzenu mie sijali,
kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

Kweli naweka bayana, kupenda kumenitenda,
Ayi! Nishaachwa sana, na wale nilowapenda,
Nilowaona wa mana, na kwa mama tukaenda,
Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

Wengine walinipata, nikawapa na mitaji,
Walivyotumia ata! Mie wala sikujaji,
Hatimaye katakata, tena hawanihitaji,
Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

wengine waniliweza, sikuwa nao mgando,
kabisa nikawekeza, nikawapa na vipando,
Ila wakaniumiza, moyo wakaupa n'gondo,
kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

Tama si kama zamani, kupenda ninao wigo,
Ayi! Kupenda jamani, tena hakunipi pigo,
Namshukuru Manani, sikuwatolea figo,
Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe.

Mshairi Machinga,
mfaumehamisi@gmail.com,
+255716541703/752795964,
Dar es salaam, Kkoo.

Print this item

  MTIHANI WA UTAMILIFU 2021 (MWANZA)
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 01:52 PM - Forum: Mitihani - No Replies

.pdf   MOCK MWANZA 2021.pdf (Size: 9.78 MB / Downloads: 108)

Print this item

  USIMULIZI
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 12:41 PM - Forum: Nukuu - No Replies

.pdf   USIMULIZI.pdf (Size: 113.8 KB / Downloads: 7)

Print this item

  Nitawapeleka Mtoni, Nitawalazimisha kunywa maji
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 08:51 AM - Forum: Je, wajua ? - No Replies

Nitawapeleka Mtoni, Nitawalazimisha kunywa maji
Siku moja baba alimuamsha kijana wake apeleke ng'ombe machungani.
Mtoto akatoka na kundi la ng'ombe hadi porini. Ilipofika majira ya alasiri akawapitisha mtoni kisha akawarejesha zizini.
Alipofika baba yake akamuuliza;
Baba: Ng'ombe wamekunywa maji?!
Kijana: Niliwapeleka mtoni.
Katika Elimu na mchakato wa kujifunza kuna mambo matatu muhimu:-
1. Kufundisha; Bila shaka mtakubaliana nami kwamba, kuna matendo ya kufundisha (teaching activities) ambayo mwalimu anatakiwa ayafanye.
2. Kujifunza; pia yapo matendo ya kujifunza (learning activities) ambayo mwanafunzi anatakiwa ayafanye.
3. Upimaji na Udhibiti; lengo lake kwa kiasi kikubwa ni kupima ufanisi wa 1 na 2 hapo juu. Anapimwa mwalimu kama amefundisha, na mwanafunzi kama amesoma.
Mwalimu ambaye ameandaa skimu, ameandaa nukuu za somo, amesaini mahudhurio ofisini, ameandaa lesoni plani, amesaini klasi juno, amefundisha, ametoa mazoezi na kazi mbali mbalimbali, anakuwa anatekeleza majukumu ya ufundishaji, sawa na kusema ng'ombe wamepelekwa mtoni.
Ikitokea wanafunzi hawajisomei, hawaadhibiwi, wanafeli mitihani, hawaukizi maswali kwa mwalimu; hii ni sawa na kusema ng'ombe wamefika mtoni hawataki kunywa maji
Baada ya matokeo kutoka;
Stakeholders: Mwalimu kwanini wanafunzi wamefeli. kwanini hawakunywa maji?!
Mwalimu: *_Niliwafundisha_* niliwapeleka mtoni.
Pamoja na ukweli kwamba kujifunza ni jukumu la mwanafunzi, lakini je, tunahakikisha wanafunzi wanafanya matendo ya kujifunza? Wanafunzi wanawajibishwa vipi ikiwa hawatekelezi jukumu lao au wanazembea?!
Siku moja nikiwa darasani, katika mazungumzo na wanafunzi;
Wanafunzi: Naipenda nchi yangu, sitakubali ihujumiwe...(salamu ya sasa kuhimiza uzalendo)
Mimi: Hujuma mwaifahamu!?
Tukapiga hesabu ya pesa ambazo serikali inalipa katika huu mpango wa elimu bure, kama ada na gharama nyingine.
Nikauliza kuna mwalimu wa somo lolote hayupo?!
Walimu wa kila somo wapo, na wanafundisha, walimu wanalipwa, chaki zinanunuliwa, vitabu vipo shuleni, madarasa yanajengwa na Ada hamlipi.
Nikawaambia 'hapo ukifeli basi umehujumu nchi yako ambayo unasema hutakubali ihujumiwe.'
Mimi ni mwalimu. Madarasa ninayofundisha pamoja na kutokosa kipindi changu hata kimoja na kuomba vya ziada, nimekuwa nikiwasisitiza waniletee maswali yanayowatatiza muda wowote. Kwa mwaka sasa hawazidi watatu wanaokuja lakini hasa ni mmoja..
Nakubali wapo baadhi yetu walimu wanaotia doa sehemu ya ufundishaji lakini kama mtaalamu katika nafasi yangu nasema kwa kinywa kipana kwamba upande wa mwanafunzi (kujifunza) kuna mapungufu makubwa.
Andiko hili si lawama kwa yoyote, bali ni kuhamasisha kila mdau atimize yanayomhusu.
Elimu yetu imeingiliwa na siasa, wataalamu wengi wa tasnia yetu wamekuwa wanafanya kazi kisiasa. Wakuu wa shule na maafisa elimu wanaelemea kwenye siasa kuliko utaalamu wao katika utendaji. Huenda miongoni mwa vigezo vya kuhudumu katika nafasi hizo ni kustawisha maslahi ya kisiasa ya mamlaka za uteuzi, badala taaluma na elimu.
Niwakumbushe wote waliopewa dhamana katika nafasi mbalimbali tuwe wazalendo kwa nchi na taifa letu, elimu yetu ni nyenzo muhimu katika ustawi wa taifa hili.
Uzalendo ni kupenda nchi yako kwa mapenzi na wivu mkubwa, na kuweka mbele masilahi ya taifa, na si kupenda serikali.
Tuelewane:
Uzalendo ni kupenda nchi, taifa.
Uzalendo si kupenda chama, serikali.
Ndio maana hata ukiwa mtumishi wa serikali kuna mambo inatakiwa ujifinze kuyakataa kwa maslahi ya taifa lako sababu uzalendo wako sio kwa serikali bali ni kwa taifa na nchi yako.
Ningeweza kugusia sehemu nyingi katika mfumo wetu wa elimu, lakini kwa vile kuna mchakato wa maboresho ya mitaala, tutatoa maoni yetu huko.
Lakini walau niseme kwa ufupi kuhusu somo la hesabu;
Somo hili liwe la lazima hadi kidato cha pili, kisha liwe hiari (optional) kuanzia kidato cha tatu.
Mada kama Statistics, Linear programming na Accounts ziitwe junior O-level mathematics, mahususi kwa kidato I na II ambazo zitakuwa ni lazima kwa wanafunzi wote.
Mada kama logarithms, exponent radical,  zipelekwe kidato cha tatu ili wasome wanaotaka (watakaochagua) kusoma Maths.
Siku moja katika wasaa wa kunasihi wanafunzi, (sisi walimu huwa tunatenga muda wa _kupiga stori_ na wanafunzi kuhusu mambo mbali mbali nje ya mada)..
We spare three to five minutes talking contemporary issues
...nikawasimulia hiki kisa cha mzazi aliyemtuma mwanawe porini kuchunga ng'ombe.
Mwisho nikawaambia professionally ilitakiwa niwapeleke mtoni lakini wakuu wangu wananitaka nihakikishe mnakunywa maji.
Buchu, Hamza O.
+255 715 345 789
10/07/2021
Mwanza

Print this item

  SHAIRI: YAMENIGANDA MAPENZI
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 08:36 AM - Forum: Ushairi - Replies (2)

YAMENIGANDA MAPENZI

Mapenzi anayejua, kwa hili simshangazi,
Haya yakisha kutua, kukung’uta hauwezi,
Vile hukung’ang’ania, kama chawa kwenye vazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Miaka imekimbia, tutengane na lazizi,
Fikirani hunijia, kumkataza siwezi,
Picha inanirudia, matukio ya miezi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Heri angekuwa Tanga, Shinyanga kwenda siwezi,
Uchumi unanizinga, huko mbali sikatizi,
Sasa nimebaki bunga, sioni lenye tatuzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Niliapo ni msiba, hayakatiki machozi,
Uso wangu nauzima, nizuie michirizi,
Haki nimekuwa zoba, mwenyewe ninajihizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Jambo linaniumiza, mtu huyo ni mzazi,
Ameoa naeleza, na watoto kwa majazi,
Ijapo najikataza, kufanya makumbukizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Akituma zake picha, mimi chali sijiwezi,
Nawaza kila kukicha, nimezidi siku hizi,
Roho yanambia ‘acha’, ila moyo mchokozi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Tatizo wake upole, kufoka huyu hawezi,
Nakumbuka siku zile, mweledi wa mapepezi,
Basi ilikuwa vile, bila yeye sijilazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Bwana huyu mtalamu, mithili kaenda kozi,
Yale mambo ni matamu, hadharani sielezi,
Ni kama mbuzi kwa ndimu, alikuwa mganguzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Yana ajabu mapenzi, yakianza hayasizi,
Marefu kama utenzi, wenye beti jozi jozi,
Na ukiwa mwanafunzi, hutaweza piga mbizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Nilidhani Mjaluo, kwa urefu mchokozi,
Weusi wenye vutio, afaa kwa matumizi,
Nikakiweka kituo, kwake sikupitilizi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Kijana wa kimanyema, kiliko chake kizazi,
Ni mkoani Kigoma, Tabora yake makazi,
Kwa sasa amesha hama, yupo Shinyanga kikazi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Kweli mahaba huua, kwa hili sibishilizi,
Nimekonda hadi pua, sijisifu siku hizi,
Heri zirudi hatua, hadi kwenye mwaka juzi,
Sipendi sasa naumwa, yameniganda mapenzi.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo DSM
0753738704

Print this item

  SHAIRI: USIKU
Posted by: MwlMaeda - 08-08-2021, 08:26 AM - Forum: Ushairi - No Replies

USIKU
Usiku unapofika, hapo jua hukimbia,
Macho hupewa mipaka, na mwanga ukafifia,
Basi ndani twajiweka, kitanda kukisumbua,
Usiku!

Mwengine huwa adhabu, usiku ukishafika,
Mawazo humpa tabu, aende mbali kufika,
Wengine za maajabu, zile ndoto huwafika,
Usiku!

Usiku kwa kikojozi, ni hasara na mashaka,
Ufikapo  usingizi, kibofu kumdhihaka,
Agutukapo ja mwizi, dimbwi limemzunguka,
Usiku!

Wengine kwao jubuni, usingizi kuwafika,
Hukoroma kama nyani, aitwaye gendayeka,
Husahau duniani, ahera hapo hufika,
Usiku!

Ukiwa unaye bwana, yule kwake ukadeka,
Na awe mjuzi sana, maji ya mto kuteka,
Usiku huwa Hossana, kuche nani anataka?
Usiku!

Usiku kwa mwenye njaa, macho katu kufunika,
Tumbole humkataa, asemalo kuitika,
Kucha anagaagaa, haoni pakujishika,
Usiku!

Usiku kwa mshairi, beti kwake hupangika,
Atumie umahiri, atunge bila kuchoka,
Hadhira ndipo hukiri, masifuni kumuweka,
Usiku!

Usiku ukishakwisha, kitandani twagutuka,
Hapo nyuso twaziosha, tuondoe takataka,
Hapo kiza hujishusha, jua huanza kuwaka,
Usiku!

Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item

Big Grin SHAIRI: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F
Posted by: jokafe - 08-08-2021, 12:00 AM - Forum: Ushairi - Replies (2)

NCHIYAKUDAI (Jovin. K. F)

1.Wananchi sikieni, naanza kuhutubia,
Masikio yategeni, hotuba kuwaingia,
Tulituli tulieni, vurugu sijeingia,
Mrejesho nawapeni, pema tuje kufikia,
Nchi hii yakudai, mwaikwamisha wadai.

2.Fanyakazi mnadai, wasokazi wanadai,
Hamfanyi kwa uhai, mwafanya ili mdai,
Nchi yashindwa kuwahi, yapambana na madai,
Mara posho hazifai, posho nono mnadai,
Nchi hii ya kudai, mwaikwamisha wadai.

3.Nchimbele haisongi, yapotezwa na miruzi,
Changamoto zawa nyingi, dawa ni kufanya kazi,
Posho mtapata nyingi, kama mkifanyakazi,
Muache kuwa waringi, hebu ifanyeni kazi,
Nchi hii ya kudai, mwaikwamisha wadai.

Mtunzi: Jovin Kamugisha Felician (jokafe)
Diwani: Tinga Tinga.
Simu: 0756882752
Barua pepe: jovinfelician1@gmail.com

Print this item

  SHAIRI: KUPENDA ASOPENDEKA
Posted by: MwlMaeda - 08-07-2021, 11:54 PM - Forum: Ushairi - No Replies

KUPENDA ASOPENDEKA
Paukwa ninatamka,nanyi semeni pakawa
Tungo iweze kufika,musikie sawasawa
Niwaeleze mashaka,moyo uweze kupowa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu

Apendwae ajuwapo,kubwa dhiki inakuwa
Takutesa mama popo,upotelewe afuwa
Utaishi kama hupo,huishi kusimbuliwa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu

Shemere ya mpendaji,kwa mpendwa ndiko huwa
Lau kama uwe jaji,sheria hupotelewa
Huwa mgonjwa wa uji,hali mzima ingawa
Kupenda asopendeka,juwa ni kubwa adhabu

Kutoka ktk Diwani ya FUTI KAFUTIKA FUTI
Abdul Ndembo

Print this item