Posted by: MwlMaeda - 08-07-2021, 12:10 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
NDOTO
Kufasiri mejaribu, kwa ndoto niiotavyo,
Hakika napata tabu, kwa ndoto inijiavyo,
Sasa nipeni jawabu, nitambue maanavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Azukapo afiriti, anitende atakavyo,
Nalikwepa varangati, vile juu nipaavyo,
Atahaha hanipati, vile mbali niendavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Ni nini kinanizinga, kwa ndoto niiotavyo?
Au ndoto yanikenga, nijione ndivyo sivyo?
Kukicha siwezi ringa, mbawa zinipotevyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Kigutuka ninawaza, ndotoni nipepeavyo,
Linazidi nitatiza, siku mbele ziendavyo,
Nimeona kueleza, mashaka yanijiavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Pengine nanusurika, vile anikimbizavyo,
Lizidivyo patashika, ndivyo juu niendavyo,
Nikimwepa namcheka, chini nimtazamavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Ndoto yanipa tatasi, na hivyo irudiavyo,
Yanijia wasiwasi, na ndivyo niandikavyo,
Nipeni majibu basi, ndoto niwaambiavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
Nane beti sio kenda, shairi niishiavyo,
Swali nalituma nenda, majibu nisubirivyo,
Ili nije pata wanda, niepuke nikondavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?
UMUGANURA
----------------
UMUGANURA ni siku,
maarufu Rwanda ino.
Maeneo yote huku,
ni sherehe ya mavuno.
-------
Ni Ijumaa ya kwanza,
ya kulla wa nane mwezi.
Sikukuu tunafanza,,
kimila tukiuenzi.
-------
UMUGANURA 'likuwa,
desturi asilia.
Wanajamii wakiwa,
pamwe wanafurahia.
---------
Nafaka pia maziwa,
wahenga walichangia.
Nazo nyama zililiwa,
togwa na kangara pia.
--------
Sikukuu ya mavuno,
kwetu ndo UMUGANURA.
Siku ya makongamano,
kukumbuka ya kikwetu.
--------
Twala mapishi ya jadi,
na vinywaji kutumia.
Tukipeana zawadi,
umoja kuzingatia.
-------
Mila za Waafurika,
sana zakaribiana.
Mshairi mshirika,
n'kusaili muungwana.
--------
Hini siku ya mavuno,
tunayoienzi sana,
jamii ya pande zino,
kwenu inapatikana?
-------
Utenzi natamatisha,
wasanii n'kiwaomba,
milazo kunijulisha,
awabariki MUUMBA.
=============
Rwaka rwa Kagarama
(Mshairi Mnyarwanda),
Jimbo la Mashariki,
Wilaya ya Nyagatare,
R W A N D A.
Posted by: MwlMaeda - 08-06-2021, 07:26 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Kuna wakati, Abunuwasi aliamua kuwa mfuga mbuzi. Alinunua mbuzi wa kufuga huku akiwa na lengo la kujiongezea kipato chake pindi mbuzi huyo atapoanza kuzaa, ili awafuge ndama wawe wengi na kumuwezesha kuwa tajiri kuliko wote waliokuwepo katika mji ule..
Siku moja Abunuwasi akipokuwa anampeleka mbuzi wake malishoni, alikuta kiatu kimoja kizuri sana katikati ya njia. Alisimama na kukiangalia. Kiatu kilipendeza machoni mwake ila akasema “kiatu hiki ni kizuri lakini mbona kipo kimoja tu?” Alitafuta kiatu cha pili pembezoni mwa njia ila hakukiona. Alipoona hawezi kuvaa kiatu kimoja, aliamua kukiacha palepale. .
Abunuasi akachukuwa mbuzi wake na mbele kidogo akaona kile kiatu cha mguu wa pili. Abunuwas alishangaa na akaona bora angelikichukua kile cha mwanzo kwa sababu cha pili kimepatikana.
Aliporudi pale mwanzo kukitafuta alichokiacha awali lakini hakukikuta tena, alijaribu kukitafuta lakini hakukiona. Basi akadhani kuna mtu amekiokota. Akarudi haraka alipomfunga mbuzi wake nako pia hakumkuta mbuzi wala kile kiatu kimoja. Mwisho akawa amemkosa mbuzi na viatu, Ndoto zote za Abunuwasi kupata utajiri zikaruka na akabaki na umasikini wake kwa sababu ya tamaa yake.
Posted by: MwlMaeda - 08-06-2021, 07:18 AM - Forum: Hadithi
- No Replies
Usiku Mmoja Kabla Muuza Duka Hajafunga Duka Lake Aliingia Mbwa Dukani Akiwa Na Kibegi Mdomoni Ndani Ya Kibegi Kulikuwa Na Pesa Kiasi Na Orodha Ya Vitu Vilivyotakiwa Kununuliwa.
Muuza Duka Alichukua Pesa Ile Kisha Akaweka Vitu Vilivyoorodheshwa Ktk Kibegi Hicho Mara Hii Mbwa Bila Kuchelewa Alichukua Kibegi Chake Na Kuanza Safari.
Muuza Duka Alishangazwa Sana Na Tukio Lile Na Akaamua Kumfuatilia Mbwa Yule Kwa Nyuma Ili Kujua Ni Nani Hasa Miliki Wake.
Baada Ya Kufika Kituo Cha Mabasi Mbwa Alisimama Kwa Dakika Chache Na Ndipo Lilipotokeza Bus Na Kusimama Mbwa Akaingia Ndani Ya Bus Na Safari Ikaanza
Akiwa Ndani Ya Bus Alimsogelea Kondakta Na Kuinua Kichwa Ili Kumuonesha Mkanda Wa Shingoni Ambao Ulikuwa Na Nauri Bila Kusahau Anuani Ya Mahali Alipotakiwa Kushuka.
Baada Ya Mwendo Kidogo Mbwa Alienda Mpaka Mbele Kwa Dereva Na Kuchezesha Mkia Wake Kuashiria Kuwa Alitakiwa Kutelemkia Eneo Lile, Hii Ni Kutokana Na Kondakta Kuto Kuwa Makini Na Maelekezo Ya Anuani.
Ndipo Dereva Aliposimamisha Bus Na Mbwa Akatelemka
Wakati Wote Huo Muuza Duka Alikuwa Akimfuatilia Yule Mbwa Kwa Ukaribu Sana.
Baada Ya Kutelemka Mbwa Alitembea Hatua Kadhaa Mpaka Alipolifikia Geti La Nyumba Moja Kubwa Na Kubonyeza Kitufe Kimoja Ktk Geti Hilo Kwa Kutumia Mguu Wake.
Sekunde Chache Baadae Geti Lilifunguliwa.
Bwana Mmoja Ambae Ni Mmiliki Wa Mbwa Huyo Akatoka Na Kipande Kirefu Kiasi Cha Waaya Na Kuanza Kumuadhibu Yule Mbwa Na Hapo Ndipo Muuza Duka Aliposhtuka Na Kuamua Kumuuliza Yule Bwana Ni Nini Hasa Sababu Ya Adhabu Ile!
Yule Bwana Mmiliki Wa Mbwa Akajibu “Amenivurugia Usingizi Wangu!! Alitakiwa Abonyeze Kitufe Cha Upande Wa Kushoto Na Geti Hili Lingefunguka.
***************************************
Huu Ndio Uhalisia Wa Maisha Yetu!! Binadamu Tumekuwa Wepesi Sana Kusahau Unaweza Kutenda Mema Mengi Sana Ya Kuwafurahisha Lakini Siku Utakapokosea Kidogo Tu Wanadamu Watakutuhumu Kwa Hilo Kosa Moja Dogo Na Wakati Mwingine Kukudharau Na Kukuona Hauna Maana Tena Kwao Wanasahau Mema Yote Uliyo Watendea.
Hata Hivyo Sikushauri Uache Kutenda Mema Bali Nakushauri Usitumie Nguvu Kumbwa Kuwafurahisha Wanadamu Wewe Tenda Yale Yampendezayo Mungu Wako Maana Yeye Pekee Ndiye Mwenye Kulipa Kwa Haki.