SHAIRI: MOYO WA JIWE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MOYO WA JIWE (/showthread.php?tid=803) |
SHAIRI: MOYO WA JIWE - MwlMaeda - 08-08-2021 MOYO WA JIWE Sasa sinao uvivu, kiteko mie kuteka, Sina tena maumivu, hata ninapoteseka, Huwa nawa mtulivu, wala sina hekaheka, Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. Ninao moyo wa jiwe, si tumbawe ni jabali, lolote lile na liwe, kwangu halina ukali, kipenzi achukuliwe, mwenzenu mie sijali, kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. Kweli naweka bayana, kupenda kumenitenda, Ayi! Nishaachwa sana, na wale nilowapenda, Nilowaona wa mana, na kwa mama tukaenda, Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. Wengine walinipata, nikawapa na mitaji, Walivyotumia ata! Mie wala sikujaji, Hatimaye katakata, tena hawanihitaji, Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. wengine waniliweza, sikuwa nao mgando, kabisa nikawekeza, nikawapa na vipando, Ila wakaniumiza, moyo wakaupa n'gondo, kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. Tama si kama zamani, kupenda ninao wigo, Ayi! Kupenda jamani, tena hakunipi pigo, Namshukuru Manani, sikuwatolea figo, Kupenda kumenifanya, niwe na moyo wa jiwe. Mshairi Machinga, mfaumehamisi@gmail.com, +255716541703/752795964, Dar es salaam, Kkoo. RE: SHAIRI: MOYO WA JIWE - jokafe - 08-08-2021 Tungo hii tamu sana, kuisoma hutochoka, Helo kwa mtunzi. |