MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F (/showthread.php?tid=797)

SHAIRI: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F - jokafe - 08-08-2021

NCHIYAKUDAI (Jovin. K. F)

1.Wananchi sikieni, naanza kuhutubia,
Masikio yategeni, hotuba kuwaingia,
Tulituli tulieni, vurugu sijeingia,
Mrejesho nawapeni, pema tuje kufikia,
Nchi hii yakudai, mwaikwamisha wadai.

2.Fanyakazi mnadai, wasokazi wanadai,
Hamfanyi kwa uhai, mwafanya ili mdai,
Nchi yashindwa kuwahi, yapambana na madai,
Mara posho hazifai, posho nono mnadai,
Nchi hii ya kudai, mwaikwamisha wadai.

3.Nchimbele haisongi, yapotezwa na miruzi,
Changamoto zawa nyingi, dawa ni kufanya kazi,
Posho mtapata nyingi, kama mkifanyakazi,
Muache kuwa waringi, hebu ifanyeni kazi,
Nchi hii ya kudai, mwaikwamisha wadai.

Mtunzi: Jovin Kamugisha Felician (jokafe)
Diwani: Tinga Tinga.
Simu: 0756882752
Barua pepe: jovinfelician1@gmail.com

RE: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F - MwlMaeda - 08-08-2021

Hongera sana kwa utunzi

RE: NCHI YA KUDAI na Jovin K. F - jokafe - 08-08-2021

(08-08-2021, 08:25 AM)MwlMaeda Wrote: Hongera sana kwa utunzi

Asante pia kwa jukwaa hili linaweza kusaidia sana kuibua vipaji vingi