SHAIRI: USIKU - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: USIKU (/showthread.php?tid=798) |
SHAIRI: USIKU - MwlMaeda - 08-08-2021 USIKU Usiku unapofika, hapo jua hukimbia, Macho hupewa mipaka, na mwanga ukafifia, Basi ndani twajiweka, kitanda kukisumbua, Usiku! Mwengine huwa adhabu, usiku ukishafika, Mawazo humpa tabu, aende mbali kufika, Wengine za maajabu, zile ndoto huwafika, Usiku! Usiku kwa kikojozi, ni hasara na mashaka, Ufikapo usingizi, kibofu kumdhihaka, Agutukapo ja mwizi, dimbwi limemzunguka, Usiku! Wengine kwao jubuni, usingizi kuwafika, Hukoroma kama nyani, aitwaye gendayeka, Husahau duniani, ahera hapo hufika, Usiku! Ukiwa unaye bwana, yule kwake ukadeka, Na awe mjuzi sana, maji ya mto kuteka, Usiku huwa Hossana, kuche nani anataka? Usiku! Usiku kwa mwenye njaa, macho katu kufunika, Tumbole humkataa, asemalo kuitika, Kucha anagaagaa, haoni pakujishika, Usiku! Usiku kwa mshairi, beti kwake hupangika, Atumie umahiri, atunge bila kuchoka, Hadhira ndipo hukiri, masifuni kumuweka, Usiku! Usiku ukishakwisha, kitandani twagutuka, Hapo nyuso twaziosha, tuondoe takataka, Hapo kiza hujishusha, jua huanza kuwaka, Usiku! Filieda Sanga Mama B Mabibo Dsm 0753738704 |