SHAIRI: KILA MTU NA MTUWE - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: KILA MTU NA MTUWE (/showthread.php?tid=805) |
SHAIRI: KILA MTU NA MTUWE - MwlMaeda - 08-08-2021 *****KILA MTU NA MTUWE***** Nilijua ndiye wangu , kumbe nae ana wake Nikampa moyo wangu, Penzi langu alitunze Kumbe siko peke yangu, Pengine Mtu wa nane Nimepanda penzi langu , kwenye mti wenye miba Tena nilijimaliza , Mashoga kuwatambia Mpenzi niliyepata, mfanowe sijaona Hana papara papara , macho ameyatuliza Nimepanda penzi langu kwenye mti wenye miba Mpenzi nilimpenda , Nikazama hadi kichwa Kila alichonambia , Binafsi sikumpinga Niliona nimepata , kumbe nimepatikana Nimepanda penzi langu , kwenye mti wenye miba Mpenzi alitupanga, kila Mtu muda wake Wote alitupeleka,Mpaka chumbani kwake Nguo tulimfulia , mpk za siri zake Nimepanda penzi langu , Kwenye mti wenye miba DINNA MINJA ( Mom JADEN) K/ sec 8/8 /21 Ntaendeleaaaaaa..... |