UTENDAJI SIMULIZI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi kwa ujumla (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=73) +--- Thread: UTENDAJI SIMULIZI (/showthread.php?tid=1380) |
UTENDAJI SIMULIZI - MwlMaeda - 10-25-2021 Usimulizi wa Hadithi katika Afrika
Okpewho anajadili usimulizi wa hadithi
katika Afrika. Anaeleza kuwa msimulizi wa kijadi ni tofauti na msimulizi anayepatikana katika maandishi. Usimulizi katika Afrika unafanyika wakati maalumu hasa wakati wa jioni au usiku watu wanapokuwa katika mapumziko baada ya vipindi maalumu vya kazi. Usimulizi wa hadithi katika Afrika hufuata
fomula maalumu. Usimulizi wa hadithi hizi huwa na mianzo na miisho ya kifomula ingawa mianzo na miisho hiyo hutofautiana toka jamii moja hadi nyingine. Kwa mfano matumizi ya paukwa pakawa, hadithi hadithi n k kutegemeana na utanzu husika. Pia usimulizi wa hadithi unaambatana
na ushiriki wa hadhira ambaye huonyesha kuwa anafuatilia simulizi hiyo. Kwa jumla, utambaji wa hadithi jukwaani huwa na
sifa kadhaa zinazoutambulisha. Sifa hizi huzitenga hadithi za mapokeo na zile tunazozisoma vitabuni. Utendaji huu unaandamana na sifa zifuatazo; 1.
Usemi halisi. msemaji anasema moja kwa moja 2.
Michepuko: msimuliaji hutoa kauli za pembeni au maoni yake. Anaiacha hadithi na kusema mambo ya pembeni au kando kabla ya kuendelea tena kuisimulia. Michepuko hii inaweza kuwa na jukumu la viliwazo hasa katika hadithi za kusikitisha au za kitanzia. 3. Urudiaji
4.
Matumizi ya wakati uliopo kihistoria/ au uliopita kisimulizi. Utambaji au usimulizi huwa katika wakati uliopita lakini huchanganya pia na sifa zinazohusishwa na wakati uliopo ili kuhakikisha kuwa umbali uliopo kati ya hadhira na hadithi yenyewe umepunguzwa. 5.
Kubadilisha
muundo wa hadithi: mtambaji anauwezo wa kuubadilisha muundo wa hadithi kwa
kuongeza vitushi fulani, kurudia visa fulani, kubadilisha msamiati, kurahisisha
kisa, kutia ucheshi n.k. Kwa hakika kila utambaji hadithi moja huwa ni tofauti
na utambaji wa hadithi hiyo wa mwanzoni yaani inafaraguliwa.
|