TANZU ZA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI (WATAALAMU MBALIMBALI) - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi kwa ujumla (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=73) +--- Thread: TANZU ZA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI (WATAALAMU MBALIMBALI) (/showthread.php?tid=1381) |
TANZU ZA FASIHI ANDISHI YA KISWAHILI (WATAALAMU MBALIMBALI) - MwlMaeda - 10-25-2021 Kama ilivyo kwenye tanzu za fasihi simulizi, haijawa rahisi kueleza tanzu za fasihi andishi kutokana na mikinzano inayoonekana
miongoni mwa wanazuoni.Wataalamu wengi wa awali wa fasihi ya Kiswahili walibainisha kuwa fasihi andishi ina tanzu tatu ambazo ni Ushairi, riwaya na tamthiliya.
MBUNDA MSOKILE 1992: Uhakiki wa fasihi
Yeye anasema tanzu za fasihi andishi zipo tatu; nazo
ni: –
Riwaya –
Ushairi –
Tamthiliya NKWERA 1976:
Sarufi na Fasihi, Sekondari na vyuo Anafanana na
Msokile, naye anatambua tanzu tatu ambazo ni: –
Riwaya –
Ushairi na –
Tamthiliya MULOKOZI 1996
Anaanza kuhoji
uhakiki wa tanzu tatu. Yeye anasema tanzu za fasihi andishi si tatu ni nne; nazo ni: –
Ushairi –
Riwaya –
Tamthiliya na –
Kisa M’NGARUTHI
2008 Yeye
anakubaliana na Mulokozi kuwa tanzu zipo nne lakini hakubaliana katika majina. Yeye anatambua: –
Ushairi –
Hadithi fupi –
Riwaya na –
Tamthiliya Kinachoitwa Kisa
na Mulokozi M’ngaruthi anakiita Hadithi fupi. Wataalamu wa Kenya wanakubaliana na M’ngaruthi, hivyo mfumo wa elimu ya Kenya unatambua tanzu alizoziainisha M’ngaruthi. Hata hivyo,
wataalamu wengine wameendelea kuhoji juu ya tanzu nne, kwa sababu novela nazo zinaingia wapi? Mfano:
WAMITILA, 2008 Yeye anataja:
–
Riwaya –
Tamthiliya –
Novela –
Insha –
Ushairi –
Hotuba –
Sira –
Masimulizi ya wasafiri Japokuwa Wamitila
hakiri moja kwa moja kuwa ni tanzu za fasihi andishi lakini anachambua vipengele hivi kama vinavyojitegemea kila kimoja. SABABU
YA MIKINZANO YA WANAZUONI JUU YA TANZU ZA FASIHI ANDISHI
1. Hawakubaliani
katika istilahi/majina ya tanzu mf. Mulokozi kuna utanzu anauita Kisa lakini M’ngaruthi anauita Hadithi fupi. 2. Hawakubaliani
katika idadi mf. Nkwera (1976) anasema kuna tanzu tatu wakati Mulokozi (1996) na M’ngaruthi (2008) wanasema zipo tanzu nne. 3. Kuna
utata katika mpangilio. Yaani ni utanzu
upi uanze, mf. Mulokozi (1996) anaanza na Ushairi, riwaya, Kisa na tamthiliya
wakati M’ngaruthi (2008) anaanza na riwaya, tamthiliya, mashairi andishi na
hadithi fupi.
|