MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 232 online users.
» 0 Member(s) | 230 Guest(s)
Facebook, Google

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 12-16-2021, 07:28 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

NADHARIA MBALIMBALI KUHUSU HISTORIA YA KISWAHILI

  Kiswahili Asili Yake ni Kongo
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni huko Kongo ambayo baadaye iliitwa Zaire na sasa inaitwa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo. Dai hili linaimarishwa na wazo lingine linalodai kwamba katika vipindi kongwe vilivyopata kuwako, sehemu za Pwani ya Afrika mashariki hazikuwa zimekaliwa na watu. Kutokana na hali ya vita, uchungaji na biashara, inadaiwa kuwa Wabantu walitoka sehemu za Kongo walisambaa na kuja pwani ya Afrika mashariki kupitia Kigoma. Baadhi ya wabantu hawa walipitia sehemu za Uganda. Wakati wa kusambaa kwao, walieneza pia lugha zao ikiwemo hii ya Kiswahili.

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba, madai ya kuwa asili ya Kiswahili ni Kongo hayana msingi kwani mpaka sasa wataalamu wanaodai hivi hawajaweza kueleza na kuthibitisha kisayansi ama Kihistoria juu ya lini hasa watu walianza kuishi pwani ya Afrika mashariki.

  Kiswahili ni Ki-Pijini au ni Ki-Krioli

(i)    Kiswahili ni Ki-Pijini
Baadhi ya wataalamu hudai kuwa Kiswahili ni Ki-Pijini. Wataalamu hawa hudai kwamba Ki-Pijini ni lugha ambayo huzaliwa kutokana na kukutanika  kwa makundi mawili (A) na (B) yanayotumia lugha mbili tofauti. Ili makundi haya yaweze kuwasiliana kunaundwa lugha ambayo kitabia ni tofauti  na zile zinazozungumzwa na makundi yanayohusika. Lugha hii inaweza kuwa na msamiati mwingi kutoka lugha kati ya zile mbili, au inaweza kuwa na msamiati wenye uzito sawa. Lugha hiyo ndiyo inayoitwa Ki-Pijini. Mazingira yanayosababisha kuwepo Ki-Pijini ni kama vile biashara, utumwa, ukoloni, nk.

Kwa mantiki ya nadharia hii, wataalamu hawa hukiona Kiswahili kuwa kilianza kama Ki-Pijini kwani ni tokeo la mwingiliano baina ya wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki na wageni wa kutoka Mashariki ya Kati, hususan Waarabu. Aidha, husisitiza kuwa lugha ya Kiswahili haikuwepo kabla ya hapo.

(ii)    Kiswahili ni Ki-Krioli
Wataalamu hawa wanadai kwamba watu wanaozungumza Ki- Pijini wanaweza kuishi pamoja kwa muda wa karne nyingi na kwa hiyo wakaweza kuzoeana na hata kufikia hatua ya kuoana. Wakioana watoto wao huikuta lugha ya ki-Pijini ama lugha yao ya kwanza. Inapofikia hatua ya aina hii kwa watoto wanaozungumza lugha hiyo, wao husemekana sasa  wanazungumza lugha ya Ki-Krioli, lugha ambayo ni hatua ya juu ya Ki-Pijini, yaani Ki-Pijini kilichokomaa.

Nadharia hii hutumia kigezo cha msamiati wa Kiswahili kuonesha uhusiano uliopo kati ya Kiswahili na Kiarabu. Wanadai kuwa, msamiati mwingi wa Kiswahili unatokana na Kiarabu. Hivyo huhitimisha kuwa hapana shaka Kiarabu kimehusika katika kuizalisha na kuikomaza lugha ya Kiswahili.

Udhaifu wa nadharia hii ni kwamba hutumia kigezo cha msamiati tu bila kuzingatia vipengele vingine vya lugha kama vile matamshi, maumbo ya maneno au muundo wa sentensi za Kiswahili. Aidha, wataalamu hawa hawakuhoji suala la kufanana kwa Kiswahili na lugha jirani katika hayo yaliyotajwa hapo juu na katika eneo la Kijografia ambamo Kiswahili na lugha hizo nyingine hujikuta zikizungumzwa. Vigezo hivi ni ushahidi tosha unaoonesha kuwa Kiswahili SI Ki-Pijini wala SI Ki-Krioli, bali ni lugha kama zilivyo hizo lugha jirani.

  Kiswahili ni Lugha ya Jamii ya Vizalia
Kundi la kwanza la wataalamu wa nadharia hii, Bishop Edward Steera, Bwana Taylor, Dkt. R. Reusch, (Katika Maganga, 1997)  hudai kwamba:

·        Waarabu na Waajemi waliohamia pwani ya Afrika ya Mashariki waliwaoa wanawake wa  ki-Afrika.

·        Watoto wao walijifunza maneno ya Kiarabu na ki-Ajemi kutoka kwa baba zao.

·        Aidha, watoto hao wakajifunza maneno ya ki-Bantu kutoka kwa mama zao.

·        Katika jitihada zao, watoto hao walijirekebisha kutokana na  tamaduni za wazazi wao ambazo ni tafauti: utamaduni wa Kiarabu na utamaduni wa ki-Bantu.

·        Vizalia hawa wakaanza kutumia lugha mpya ya mseto wa Kiarabu, Kiajemi na lahaja mbalimbali za ki-Bantu.

·        Kwa kiasi kikubwa, lugha mpya ya mseto ilikuwa ni upotoshaji wa lugha ya Kiarabu na Kiajemi.

·        Mwarabu au Mu-Ajemi alikuwa muumini wa dini ya Uislamu.

·        Umo humo, vizalia hawa wakayaingiza maneno ya Kiarabu, Kishirazi na Kihindi katika hii lugha mpya.

·        Pamoja na kuyaingiza maneno ya kigeni, lugha-mpya yao hii (Kiswahili), ilikithiri vionjo vingi vya lugha mbali mbali za ki-Bantu.

·        Ndipo baadaye, lughampya yao hii ikajulikana au kuitwa Kiswahili.

·        Kwa maoni ya wataalamu hawa, sehemu mbili kati ya tano (2/5) ya maneno yanayotumika katika lugha hii mpya ni ya ki-Bantu.

·        Sarufi ya lugha mpya hii ni mseto wa ki-Bantu (chenye utata na kisicho na mpangilio maalumu) pamoja na Kiarabu (chenye mantiki na kilichokomaa).
         
Kundi la pili la wataalamu wa nadharia hii, B. Krumm na F. Johnson lina mawazo yanayodai kwamba:
·        Kiswahili kilitokana na visiwa vya Lamu, Kilamu/Kiamu.

·        Wageni kutoka Ghuba ya Ushirazi/Uajemi na Arabia ya Kusini walikuja katika Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha tofauti.

·        Lakini kutokana na kuoana kwao na wenyeji, wageni hawa wakaichukua lugha ya hapo walipofikia, wakaikuza kwa maneno kadhaa na sentensi kadhaa kutoka lugha zao za asili, yaani Kiarabu, Kiajemi na Kihindi hususan katika masuala ya  biashara, ubaharia, vyombo vya kazi zao na nguo.

·        Aidha,  utumwa na tabia ya kuoa wake wengi ilisaidia kutoa kundi kubwa la masuria. Hali hii ikaondosha hisia za ugeni katika lugha zao; na maneno yote yakabatizwa kuwa ya ki-Bantu, na hata kupoteza kabisa sura ya ugeni.

  Kiswahili ni Kiarabu
Kuna hoja kuu tatu ambazo baadhi ya wananadharia hii huzitumia kutetea nadharia hii kuwa Kiswahili asili yake ni Kiarabu.
(i)          Inadaiwa kuwa maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama Pijini ya Kiarabu.

(ii)      Inahusu neno lenyewe Kiswahili ambalo asili yake ni Kiarabu. Neno Kiswahili linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani.

(iii)    Inadaiwa kwamba kwa kuwa Kiswahili kilianza pwani, kwa kuwa idadi kubwa sana ya wenyeji wa pwani ni waislamu, na kwa kuwa uisilamu uliletwa na Waarabu, basi Kiswahili nacho kililetwa na Waarabu.

  Kiswahili si Kiarabu
Madai kwamba Kiswahili si Kiarabu yanathibitishwa na hoja kinzani zifuatazo:

Tukianza na dai la kwanza ‘kwamba maneno yenye asili ya Kiarabu yaliyomo katika Kiswahili ni ishara tosha kwamba lugha hii ilianza kama pijini ya Kiarabu’ tunaona wazi kwamba madai haya hayana mashiko. Lugha ya Kiswahili imetokea kuwa na maneno ya mkopo yenye asili ya Kiarabu (na kwa hakika yapo yenye asili ya Kiajemi, Kireno, Kihindi, Kijerumani, Kiingereza nk.) kutokana na ukweli kwamba kulikuwa na mawasiliano ya karne na karne baina ya wenyeji wa pwani na wafanyabiashara wa Kiarabu. Wasemaji wa lugha mbili tofauti wanapokutana hawaachi kuathiriana kilugha. Kwa hiyo lugha kuwa na maneno mengi ya mkopo kutoka lugha nyingine, haifanyi lugha hiyo isemekane kuwa imetokana na hiyo lugha nyingine.

Pili wataalamu hawa wanadai kwamba neno lenyewe Kiswahili lina maana ya Kiarabu.

Kwani linatokana na neno “sahili” (umoja) na “swahil” (wingi) lina maana ya pwani. Hapa ingetupasa tuelewe kwamba kila mtu binafsi au jamii binafsi aghalabu hajiiti mwenyewe jina lake, yeye huitwa kwa hilo jina alilopewa na wengine: Jamii yake au wageni waliomtembelea kwake. Na hivi ndivyo ilivyojitokeza kwa upande wa jamii ya watu wa pwani ya Afrika mashariki, yaani Waswahili,  walipotembelewa na Waarabu na kuitwa As-Sahilyy au As-Sawahiliyy, na nchi yao kuitwa sahil (wingi wake Sawahil), yaani pwani (upwa), ufuo. Kwa mantiki hii, dai hili halina mashiko !

Kigezo cha dini nacho hakikubaliki lugha haiwi lugha kwa sababu ya imani. Hata hivyo lugha ya Kiarabu yenyewe ilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa dini ya Uislamu. Hali kadhalika, lugha nyingine za Kimagharibi zilikuwepo karne nyingi kabla ya kufunuliwa imani ya ukristo. Kama ilivyo kwamba Kiingereza au Kijerumani si ukristo, basi ndivyo vivi hivyo ilivyo kwamba Kiswahili hakiwezi kuwa dini ya uislamu, aslan! Wala Kiarabu nacho si uislamu. Tunachoweza kufanya ni kuitumia lugha kuifasili dini, lakini hatuwezi kuitumia dini kuifasili lugha.

  Kiswahili ni Kibantu
Vipengele vinavyotumika katika kuihalalisha nadharia inayodai kwamba Kiswahili ni Kibantu ni ushahidi wa ki-Isimu, ushahidi wa ki-Historia na kuichunguza lugha ya Kiswahili katika mfumo mzima wa historia ya mgawanyiko wa kusambaa kwa lugha za ki-Bantu. Wataalamu wa nadharia hii wanahitimisha kwa kudai kwamba Kiswahili ni mojawapo kati  ya lugha katika jamii kubwa ya lugha za ki-Bantu.

Baadhi ya wataalamu muhimu wanaoiunga mkono nadharia hii ni Prof. Malcon Guthrie, Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl na Prof. Clement Maganga.

Profesa Malcom Guthrie ni mtaalamu (mwanaisimu) mashuhuri kutoka Chuo Kikuu cha London, Uingereza. Alitumia miaka 20 kuchunguza uhusiano uliopo baina ya lugha za Kibantu zilizoko katika eneo lote ambalo hukaliwa na wabantu. Sehemu hii ni ile ambayo inajulikana kama Afrika, Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Alifanya uchunguzi wa mashina/mizizi (viini) ya maneno 22,000 kutoka lugha 200 za Kibantu. Katika uchunguzi wake alikuta mizizi (mashina) 2,300 imezagaa      katika lugha mbalimbali za Kibantu na Kiswahili kikiwemo. Mashina/mizizi 500          yalilingana katika lugha zote 200. Mashina haya yalipatikana katika lugha zote za Kibantu. Mashina haya yalikuwa ya asili moja. Baadhi ya lugha hizo 200 zilizofanyiwa uchunguzi Kiswahili kilionesha kuitikia ulinganifu sawa na Kikongo kwa asilimia arubaini na nne (44%).

Katika kuchunguza ni asilimia ngapi za mashina hayo 500 yaliyomo katika kila lugha, mgawo uliojitokeza ulikuwa kama ifuatavyo:

Kiwemba kizungumzwacho Zambia        -          54%
Kiluba kizungumzwacho Katanga            -          51%
**Kikongo kizungumzwacho Zaire          -          44%**
**Kiswahili kizungumzwacho Afrika Mashariki            44%**
Kisukuma kizungumzwacho Tanzania                41%
Kiyao kizungumzwacho Tanzania/Msumbiji -  35%
Sotho kizungumzwacho Botswana                        -          20%
*Kirundi kizungumzwacho Burundi        -          43%*
Kinyoro kizungumzwacho Uganda          -          37%
Kizulu kizungumzwacho Afrika Kusini  -          29%

Baada ya kupata matokeo haya, Profesa Malcom Guthrie anaiunga mkono nadharia hii ya kwamba Kiswahili ni ki-Bantu kwa kudai kwamba:
(i)    Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni;
(ii)    Anaonyesha kwamba Kiswahili kina uhusiano mkubwa na lugha za Kibantu;
(iii)  Mwisho anasema Kiswahili kilianzia Pwani ya Afrika Mashariki.
         
Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl: Wataalamu hawa wanaamini kwamba:
(i)                Wakati wa utawala wa Shirazi katika upwa wa mashariki ya Afrika kulikuwa na kabila la Waswahili;

(ii)            Kabila hili ni dhuria ya Wazaramo wa leo.

(iii)          Kwa kuwa hawa Wazaramo walikuwa wamezaliwa katika harakati za kibiashara, kwa hivyo wakafuata nyayo za wazazi wao.

(iv)          Lugha yao ilikuwa ya aina ya ki-Bantu.

(v)              Kwa kuwa Wabantu ni wengi zaidi kuliko jamii ya makabila mengine, lugha yao ya Kiswahili ikaanza kutumika na kuenea katika makabila mengine, hususan katika ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki.

(vi)          Baadaye, Waswahili hawa hawa wakafanya biashara na wageni waliokuja kuvinjari Afrika Mashariki, hususan Waarabu, Washirazi, Wamalaysia, Wahindi na Wareno ambao tayari walikuwa wamefurika katika pwani hii ya Afrika Mashariki miaka kadhaa kabla.
(vii)        Vifaa na majina ya vitu vya biashara vya wageni hao vikaselelea na kuingizwa katika mfumo wa lugha hiyo ya Waswahili ambayo ni ki-Bantu.

Madai ya nadharia hii yakichunguzwa, tunagundua kwamba inazingatia mitazamo miwili yaani, mtazamo wa ki-Isimu na mtazamo wa ki-Historia. Kwa mantiki hii, nadharia hii inaelekea kukubalika na wataalamu wengi kuwa ndiyo sahihi kuhusu asili au historia ya Kiswahili.

Profesa C. Maganga, na uthibitisho wake kwamba Kiswahili ni ki-Bantu. Kama tulivyoona, lugha ya Kiswahili ilifanyiwa utafiti na uchambuzi na wanataaluma kadhaa kwa madhumuni ya kuiainisha kama ilikuwa yenye misingi ya ki-Bantu au la. Prof. Maganga alifanya uchambuzi wa ki-Isimu na wa ki-Historia kuhusu lugha hii. Matokeo ya utafiti wake wa ki-Isimu kuhusu lugha ya Kiswhili (au lugha kwa ujumla) unadhihirisha mambo mengi, mojawapo ni asili ya lugha hiyo. Amethibitisha kwamba Kiswahili ni lugha ya Kibantu; na kwa hivyo, kuthibitisha kwa ushahidi thabiti hoja ya Dkt. C. Meinholf na Dkt. C. Rohl kama  tulivyoieleza hapo juu.

(i)        Ushahidi wa Kiisimu
(a)      Msamiati
Matokeo ya utafiti alioufanya kuhusu msamiati wa Kiswahili ulibaini kwamba 60% ya maneno yote yanayoweza kuandikwa na kutamkika katika lugha ya Kiswahili asili yake ni lugha za Kibantu, 30% ni lugha ya Kiarabu na 10% ni lugha nyingine za kigeni kama vile Kiingereza, Kireno, Kijerumani, Kihindi, Kiajemi, Kifaransa, nk. Kinyume chake ni kwamba msamiati wa Kiswahili na ule wa Kibantu hautofautiani.

Mfano:
            Kiswahili  Kindali  Kizigua  Kijita  Kikurya  Kindendeule         
            Mtu          Umundu    Mntu      Omun      Omontu      Mundu
            Maji        Amashi      Manzi    Amanji    Amanche    Maache
            Moto        Umulilo    Moto        Omulilo  Omoro        Mwoto

(b)      Tungo (Sentesi) za Kiswahili
Miundo ya tungo (sentesi) za maneno ya Kiswahili zinafanana sana na miundo ya tungo za maneno ya ki-Bantu. Sentesi za Kiswahili na za lugha za ki-Bantu zina kiima  na kiarifu.

Mfano:
Lugha za Kibantu              Kiima                        kiarifu
Kiswahili                              Juma                          anakula ugali.
Kizigua                                  Juma                          adya ugali.
Kisukuma                              Juma                          alelya bugali
Kindali                                  Juma                          akulya            ubbugali.
Kijita                                      Juma                          kalya  ubusima.
Kindendeule                        Juma                          ilye ughale.
©      Ngeli za Majina
Wanataalamu wanakubaliana kuhusu ngeli za majina kwa mujibu wa:
maumbo ya nomino (umoja na wingi wa majina) pamoja; na
upatanisho wa kisarufi katika sentesi.

Kigezo cha maumbo ya majina: Kigezo hiki hufuata maumbo ya umoja na uwingi katika kuyaainisha majina. Majina yaliyo mengi katika lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu hufuata mkondo wa umoja na uwingi. Majina ya lugha ya Kiswahili na lugha za ki-Bantu yaliyo mengi yana maumbo dhahiri ya umoja na uwingi.

Mfano:
Lugha za Kibantu              Umoja                        Wingi
Kiswahili                              mtu                -          watu
                                                mtoto              -          watoto
Kikurya                                  omanto          -          banto (abanto)
                                                omona                        -          bana    (abana)
Kizigua                                  mntu              -          bhantu
                                                mwana            -          bhana
Kindali                                  mundu            -          bhandu
                                                mwana            -          bhana
Kindendeule                        mundu            -          βhandu
                                                mwana            -          βhana

Kigezo cha upatanisho wa kisarufi katika sentesi: Katika kigezo hiki tunaangalia uhusiano uliopo kati ya kiima (jina na viambishi awali vya nafsi) na vivumishi katika vitenzi vya Kiswahili na ki-Bantu. Vivumishi, majina pamoja na viambishi hivyo vya vitenzi hubadilika kutokana na maumbo ya umoja na uwingi.

Mfano:
Lugha za Kibantu      Umoja                    -                      Wingi
Kiswahili                      Baba analima        -                      Baba wanalima
Kindali                          Utata akulima        -                      Abbatata bbakulima
Kikurya                        Tata ararema          -                      Batata(Tata)bararema
Kijita                            Tata kalima                        -                      Batata abalima
Kindendeule                Tate ilima              -                      Akatate βhilima

(d)      Vitenzi vya Kiswahili na Kibantu
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya vitenzi vya Kiswahili na vile vya lugha zingine za ki-Bantu. Vipengele vinavyothibitisha uhusiano huu ni: Viambishi, mnyumbuliko, pamoja na mwanzo au mwisho wa vitenzi, kama ifuatavyo:

Viambishi: vitenzi vya lugha ya Kiswahili na vya lugha zingine za ki-Bantu hujengwa na mzizi (kiini) pamoja na viambishi vyake vya awali na vya tamati.

Mfano:

Kiswahili      -          analima          =          a – na – lim -  a
Kiikuyu          -          arerema          =          a  –  re –  rem–a
Kindali          -          akulima          =            a  - ku  –  lim – a
                                                                          1  -  2  -  3  -  4
Sherehe:
1  -    Kiambishi awali kipatanishi cha nafsi.
2  -    Kiambishi awali cha njeo (wakati uliopo).
3  -    Mzizi/Kiini.
4  -    Kiambishi tamati.

Mnyambuliko wa vitenzi: Mnyumbuliko wa vitenzi vya Kiswahili hufanana na ule wa vitenzi vya lugha za ki-Bantu.

Mfano:       

Kiswahili      -          kucheka        -          kuchekesha  -          kuchekelea.
Kindali          -          kuseka            -          kusekasha      -          kusekelela.
Kibena          -          kuheka          -          kuhekesha    -          kuhekelea.
Kinyamwezi  -          kuseka            -          kusekasha      -          kusekelela.
Kikagulu        -          kuseka            -          kusekesha      -          kusekelela

Mwanzo wa vitenzi: Vitenzi  vyote vya Kiswahili na vile vya lugha za ki-Bantu huanza na viambishi ambavyo ni viwakilishi vya nafsi, kama ifuatavyo:

Mfano:

Kiswahili      -          Ni-nakwenda
Kihaya          -          Ni-ngenda
Kiyao            -          N-gwenda
Kindendeule -          Ni-yenda

Mwishilizo wa vitenzi: Vitenzi vya lugha za ki-Bantu na Kiswahili huishia na irabu –a.

Mfano:

Kiswahili      kukimbi-a      -          kuwind-a      -          kushuk-a
Kindali          kukind-a        -          kubhing-a      -          kukol-a
Kisukuma      kupil-a          -          kuhwim-a      -          Kutend-a
Kisunza          kwihuk-a      -          kuhig-a          -          kising-a
Kindendeule kuβhutuk-a    -          kuhwim-a      -          kuhuk-a

tafiti wa Prof. Maganga kuhusu ushahidi wa ki-Isimu wa kuthibitisha kama Kiswahili ni ki-Bantu au la ungeweza kuelezwa kimuhtasari kwa mifano mingine ifuatayo:

Mfano wa 1:

Lugha
Sentesi
Kiswahili
Kipare
Kindamba
Kichaga
Kihaya
Kikaguru
Kindendeule 
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
Jongo
anafuga
erisha
kafugha
nao he
n’afuga
kachima
ifuga
mbuzi
mbuji
mene
mburu
embuzi
m’ehe
mbuhi
kuku
nkuku
nguku
nguku
enkoko
ngu’ku
nguku
na
na
na
na
n’
na
na
ng’ombe
ng’ombe
senga.
umbe
ente
nn’ombe
ng’ombe

Katika mfano huu inaonekana kwamba mpangilio wa maneno katika sentesi una ufanano kwa sababu katika kila sentesi kuna kiima na kiarifu. Katika kiima kuna nomino, yaani jina la mtenda (Jongo) na katika kiarifu kuna kitendo kinachofanyika na nomino mtendwa. Pia nafasi ya viunganishi ni ile ile kwa lugha zote zilizoonyeshwa katika mfano huu.

Kuna mfano mwingine wa ufanano wa mpangilio huu.

Mfano wa 2:

Lugha
Sentesi
Kiswahili
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kizigua
Sitamkuta kesho
Timushangemu nyenkya
Natusanga intondo
Tumuhanga fadyu
Nesikemkiche yavo
Sirambila luvi

Katika sentensi hizo mpangilio wa maneno una ufanano kwa sababu kila sentensi ina kiima na kiarifu chenye kitenzi na kielezi. Pia kiambishi cha nafsi cha nomino ya mtenda kinajitokeza mwanzoni mwa neno la kwanza la kila sentesi.
Sitamkuta;    Timushangemu;        Natusanga;                                                                            Tumuhanga;            Nesikamkiche;                      Sitambila.

Viambishi hivyo vya nafsi ya mtenda pia vinaonyesha hali ya ukanushi katka kila sentesi na nafasi yake ni ile ile kwa kila sentesi.

Viambishi vya urejeshi navyo vinajitokeza katika kitenzi cha kila sentesi.

Viambishi {m}, {m}, {ti}, {tu} sitamkuta, timushangemu, natusanga, tumuhanga, nesikamkiche, na sitambwila ni vya urejeshi; vinawakilisha nomino mtendwa.

Kwa hivyo, hali hii inadhihirisha kwamba miundo ya sentensi hizi inafanana na vitenzi vyake vina tabia mbalimbali, kama vile:

(i)        kubeba viambishi vya nafsi, mtenda na mtendwa,

(ii)      kuonyeshga hali ya ukanushi njeo za wakati na kitendo kinachofanyika.

Mfano wa 3:

Lugha                 
Sentesi
Kiswahili
Kizigua
Kihaya
Kisukuma
Kinyaturu
Kipare
Kindendeule
Akija mwambie anifuate
Akeza umugambe anitimile.
Kalaija omugambile ampondele
Ulu nahali anikubije
Newaja mwele ang’onge.
Ekiza umti aniratere
Anda ahikite n’nongerera angobhekeraye

Katika sentesi hizo inaonekana kwamba sentesi zote zinafanana  kimpangilio. Pia maneno yake yanakubali uambishaji, kwa mfano:

(i)        Katika maneno ya mwanzo:
            akija, akeza. kalaija, akuja, newaja, ekiza, herufi zilizopigiwa vistari ni viambishi vya nafsi vinawakilisha dhana ya mtenda.

(ii)      Vivyo hivyo katika maneno:
anifuate, ampondele, anitimile, ang’nge, aniratere, angobhekeraye, viambishi vilivyoko katika viarifu vya sentesi hizo vinawakilisha nafsi za watenda.

(iii)    Pia vitenzi vya sentesi hizo vina tabia ya kubeba virejeshi vya nafsi kama ilivyo katika, mwambie, omugambile, nahali,mbwele na umti, vinaonyesha njeo na hali ya uyakinifu- hali inayoonyesha ufanano wa maumbo ya maneno.

(iv)      Licha ya kuwa na mpangilio unaofanana na wa lugha nyingine za kibantu, kwa mfano, katika mifano tuliyoiona hapo juu, baadhi ya maneno yanafanana: tazama maneno:
            kafugha (Kindamba); nafuga  (Kihaya);
            nifuga (Kindendeule); anafuga  (Kiswahili).

Pia maneno:

            nkuku  (Kipare);                  nguku (Kindamba);
            nguku  (Kichaga);              enkoko  (Kihaya);
            ng’uku  (Kikaguru);                        nguku(Kindendeule);
            nguku    (Kindendeule)

Katika mfano wa 3, maneno yafuatayo yana ufanano:

Akeza  (Kizigua);                kalaija  (Kihaya);    alize  (Kisukuma),
newaja  (Kinyaturu);          ekiza  (Kipare);      anda ahikite,... (Kindendeule);
akija,  (Kiswahili.)

Pia maneno;

umugambe  (Kizigua);        omugambile  (Kihaya);      unongeraye (Kindendeule);  na mwambie (Kiswahili).

Ufanano huu wa msamiati, maumbo ya maneno pamoja na wa mpangilio wa maneno katika sentesi, vyote vinathibistisha kwamba lugha ya Kiswahili ni ya kibantu kama zilivyo nyingi nyinginezo.

(ii)    Ushahidi wa Kihistoria Kwamba Kiswahili ni Kibantu
Baada ya kuangalia ushahidi wa kiisimu kuhusu asili ya Kiswahili, katika sehemu hii Maganga (1997) aliendelea kuchambua ushahidi wa Kihistoria unaothibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa katika upwa wa Afrika Mashariki hata kabla ya ujio wa wageni kama vile Waarabu na Wazungu. Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika hapa Afrika Mashariki. Wote wanathibitisha kuwa lugha ya Kiswahili ilizungumzwa hapa Afrika Mashariki kabla ya ujio wa wageni.

(a)    Ugunduzi wa Ali-Idris (1100-1166)
Ugunduzi huu yasemekana ulifanywa huko Sicily yapata mwaka 1100-1166. Kwenye mahakama ya mfalme Roger II. Licha ya kufahamika kuwa Kiswahili, kilipata kuandikwa kabla ya 10BK. Ali-Idris alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni Unguja. Katika maelezo yake anaandika pia majina kama vile kikombe, mkono wa tembo, muriani, na kisukari, ambayo ni ya ndizi mbalimbali zilizokuwa zikipatikana huko.

(b)    Ushahidi wa Marco Polo
Huyu ni mzungu ambaye alijishughulisha sana na masuala mbalimbali ya kijiografia na alisafiri sehemu nyingi duniani. Marco Polo aliandika hivi:

“Zanzibari ni kisiwa kizuri ambacho kina ukubwa wa mzunguko wa maili 200. Watu wote wanaabudu (Mungu), wana Mfalme na wanatumia lugha yao, na hawalipi kodi (ushuru) kwa mtu.” Safari za Marco Polo 1958:301

Marco Polo anasemekana aliandika pia kitabu cha jiografia ambacho hakikupata kuchapishwa lakini sehemu zake zimepata kufasiriwa kwa Kirusi na Kifaransa. Mfano mmojawapo ni huu unaofuata:

“Katika visiwa vya Sjawaga vilivyoshughulikiwa katika sura hii, ni kile kisiwa cha Andjaba ambacho mji wake mkuu unaitwa katika lugha ya kwao. Zanguabar/Ungudya, na wakazi wake, japokuwa ni mchanganyiko, kwa sasa wengi wao ni Waislam…chakula chao kikuu kikiwa ndizi. Kuna aina tano ambazo zinajulikana kama kundi, fili, ambazo uzito wake waweza kuwa wakia 12, Omani, Marijani, Sukari....”

Maelezo haya ya Marco Polo yanathibitisha mambo ya msingi kuhusu wakazi wa Pwani ya Afrika ya Mashariki na lugha yao; mintarafu ya dini, chakula na utamaduni wao kwa ujumla.

©    Ushahidi wa Al-Masudi (915 BK)
Katika moja ya maandiko yake, Al-Masudi anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la “wazanji”. Kwa dhana hii, neno Zanzibar linatokana na Zenzibar yaani “Pwani ya Zenji”. Katika maelezo yake Al-Masudi anaonyesha kwamba Wazenji walikuwa  “Watawala Wakilimi” ambao waliaminiwa kuwa walitawala kwa nguvu za Mungu. Kuna maelezo kuwa huenda neno “wakilimi” lina maana ya “wafalme”. Al-Masudi alisisitiza katika maelezo yake kuwa Wazenji walisema lugha kwa ufasaha na walikuwa na viongozi waliowahutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno “zenji” kuna uwezekano kuwa kabla ya majilio ya Waarabu, Kiswahili kiliitwa “Kiazania” au “Kizanji” na wageni waliofika pwani.

(d)    Ushahidi wa Ki- Historia wa Mji wa Kilwa
Kimsingi habari zinazoeleza historia ya mji wa Kilwa katika karne ya 10-16BK zinataja majina ya utani kama vile: mkoma watu, nguo nyingi, nk. ambayo walipewa Masultani wa kwanza wa Kilwa Ali Ibn Hussein na mwanae Mohamedi Ibn Ali. Kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili ilishaanza kusemwa mnamo karne ya 10 au ya 11 BK. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwa Talt Ibin Al Husaini ambaye alipewa jina la utani “Hasha Hazifiki”.
(e)      Utenzi wa Fumo Liyongo (13 BK) kama Ushahidi
Shairi la zamani kabisa lililopata kuandikwa la Kiswahili, linalojulikana ni lile la Utenzi wa Fumo Liyongo. Utenzi huu inasemekana uliandikwa karne ya 13BK. Kuweko kwa shairi hili kunadhihirisha kuwako kwa lugha ya Kiswahili kabla ya karne hiyo, na kwa hivyo, huenda Kiswahili kilianza kutumika kabla ya karne ya 10BK. Baadhi ya beti za utenzi wa Fumo Liyongo ni hizi zifuatazo:
Ubeti  6:        Liyongo Kitamkali,
                        Akabalighi vijali
                        Akawa mtu wa kweli
                        Na hiba huongeya.

Ubeti 7:          Kilimo kama mtukufu
                        Mpana sana mrefu
                        Majimboni yu maarufu
                        Watu huja kwangaliya.

Ubeti 10:        Sultani pate Bwana
                        Papo nae akanena
                        Wagala mumemwona
                        Liyongo kiwatokeya.

(Kutoka E.A. Swahili Committee 1973)

Lugha hii ndio mfano wa lugha iliyokuwa ikitumika kunako karne ya 13BK. Ni wazi kuwa lugha hiyo ilianza kusemwa mapema kabla ya muda huo. Hoja za kihistoria inaelezea historia ya lugha ya Kiswahili toka karne ya 10BK hadi karne ya 18BK. Kutokana na ushahidi huu ni dhahiri kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Wabantu wa Afrika ya Mashariki.

MAREJELEO

Maganga (1997), OSW 102: Historia ya Kiswahili. Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
Masebo, J. A. Nyengwine, N. (2002), Nadharia ya Lugha ya Kiswahili, Kidato cha 5 na 6.  Aroplus Industries Ltd: Dar es Salaam.
Nkwera, Fr. F. V. (2003), Sarufi, Fasihi na Uandishi wa Vitabu, Sekondari na Vyuo. Creative Prints Ltd: Dar es Salaam.

Soma zaidi>>>>>>http://petermwiza.blogspot.com/2014/03/nadharia-mbalimbali-kuhusu-historia-ya.html

Print this item

  NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 12-16-2021, 07:26 AM - Forum: Taasisi za kukuza lugha - No Replies

NAFASI YA VYAMA NA TAASISI MBALIMBALI KATIKA MAKUZI YA KISWAHILI 

Kwa Mukhtasari

IKIWA idara ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI), awali
ikiitwa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI) ni miongoni mwa taasisi kongwe
zaidi za lugha nchini Tanzania na Afrika Mashariki. Madhumuni yake ni kusimamia
usanifishaji na maendeleo ya Kiswahili.

Japo Kiswahili
kimeendelea kubaki nembo ya Afrika, mjadala usio na mwisho kuhusiana na ni ipi
lugha ya kufundishia katika shule na vyuo nchini Tanzania ni ithibati kwamba
Kiswahili hakijapokezwa hadhi inayostahiki katika mengi ya mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati.

TUKI, kwa sasa TATAKI,
ilianzishwa mnamo 1930 ikijulikana kama International-Territorial Language
(Swahili) Committee kwa nchi tatu za Afrika Mashariki na baadaye ikaitwa Kamati
ya Kiswahili ya Afrika Mashariki.

Mnamo 1964, kamati
ilifanywa kuwa sehemu ya UDSM na baadaye ikaitwa Chuo cha Uchunguzi wa
Kiswahili. Tangu 1970 kimepewa jina la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili
(TUKI). Mwaka 2009, TUKI iliungana na iliyokuwa Idara ya Kiswahili ya UDSM na
kuunda taasisi kubwa zaidi inayoitwa TATAKI.

Majukumu ya taasisi hii
awali yalikuwa ni kutafiti nyanja zote za lugha ya Kiswahili, fasihi na
utamaduni na kuchapisha matokeo ya utafiti huo.

Hivyo pamoja na Baraza
la Kiswahili Tanzania (BAKITA), TUKI ni mlinzi wa usanifu wa lugha ya Kiswahili
katika Tanzania. Baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili, sasa TATAKI
inafundisha Isimu, Fasihi na Historia ya Lugha ya Kiswahili.

Inafundisha Kiswahili
kama lugha ya pili hasa kwa wageni kutoka nje ya ulimwengu wa Waswahili na
kuendeleza utungaji wa kamusi mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili.

BAKITA

Ni taasisi ya serikali
iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na.27 ya mwaka 1967 kwa madhumuni ya kukuza
Kiswahili. Kutokana na sheria hii, Baraza ndilo mratibu wa kusimamia asasi zote
na mawakala wote wanaokuza Kiswahili katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

BAKITA imekuwa na
mchango mkubwa katika ukuzaji na uenezaji wa lugha ya Kiswahili kupitia
majukumu yake.

Miongoni mwa majukumu
ya Baraza hili kama yalivyofafanuliwa katika sheria hiyo ni kuratibu na
kusimamia maendeleo na matumizi ya Kiswahili nchini pamoja na kushirikiana na
vyombo vingine vinavyojihusisha na maendeleo ya Kiswahili.

Huhimiza matumizi ya
Kiswahili katika shughuli rasmi na za kawaida, huandaa vipindi mbalimbali
redioni ili kuhimiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili, hushirikiana na
mamlaka zinazohusika kuthibitisha tafsiri sanifu za istilahi, hutoa huduma za
tafsiri na ukalimani kwa serikali, mashirika ya serikali na yasiyo ya serikali
na asasi nyingine pamoja na kuidhinisha vitabu vya Kiswahili vitakavyotumika
shuleni na vyuoni kabla havijachapishwa.

TAKILUKI

Taasisi ya Kiswahili na
Lugha za Kigeni (TAKILUKI) ilianzishwa mnamo 1979 kwa lengo la kukuza na
kueneza Kiswahili ndani na nje ya Zanzibar.

Inajishughulisha na
kuratibu, kuendesha mafunzo ya Kiswahili visiwani Zanzibar, kuhariri miswada
mbalimbali ili kuthibitisha ufasaha wa Kiswahili na kufanya tafiti za Kiswahili
katika nyanja zake zote, hususan sarufi na fasihi.

TAKILUKI inatoa ushauri
wa kitaaluma kwa watunzi wa vitabu ili waweze kuandika kazi zenye ubora, na
kushirikiana na wadau wengine wa Kiswahili kuandaa na kuendesha semina, warsha
na kozi fupifupi za Kiswahili.

CHAUKIDU

Chama cha Ukuzaji wa
Kiswahili Duniani (CHAUKIDU) kina makao makuu katika Chuo Kikuu cha
Wisconsin-Madison, Marekani.

Madhumuni yake ni
kuwajumuisha pamoja wakuzaji wa Kiswahili duniani kote kwa lengo la kuchochea
kasi ya malengo mahususi kama vile kukuza Kiswahili katika nyanja zote ambamo
lugha hii inatumika na kuongeza ufanisi wa mawasiliano katika ufundishaji na
utafiti wa maarifa ya aina zote mathalan uandishi na utangazaji wa habari,
uandishi na uchapishaji wa vitabu na majarida pamoja na utayarishaji wa safari
za mafunzo katika Afrika Mashariki na Kati.

Husambaza habari na
matokeo ya utafiti kwa kutumia machapisho mbalimbali na teknolojia ya mtandao
wa kompyuta kuhusu vipengele mbalimbali vya Kiswahili na masuala yanayohusiana
na Kiswahili. CHAUKIDU inaelimisha umma juu ya umuhimu wa kujivunia,
kuendeleza, na kuheshimu Kiswahili.

Vilevile inashauri ama
kushinikiza serikali za nchi ambamo Kiswahili kinazungumzwa kutambua thamani
iliyobebwa na maliasili hii ili kuunda sera mwafaka za kukiendeleza kadri ya
uwezo wake kwa manufaa ya maendeleo ya serikali na watu wake kijamii, kisiasa,
kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

CHAWAKAMA

Chama cha Wanafunzi wa
Kiswahili katika vyuo vikuu vya Afrika Mashariki (CHAWAKAMA), kilianzishwa
mnamo 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika
Mashariki kupitia kwa wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni.

Wanachama wa chama hiki
ni wale wanaosomea taaluma za Kiswahili ila wapenzi wa Kiswahili pia wanaweza
kujiunga nacho.

Mara kwa mara,
CHAWAKAMA huandaa makongamano kwa lengo la kuwapa wanachama nafasi ya kujadili,
kuimarisha, kuendeleza na kukuza vipawa vyao vya lugha na fasihi ya Kiswahili,
kuamsha ari ya mapinduzi ya utamaduni wa Kiswahili, kueneza Kiswahili ndani na
nje ya nchi, kushirikiana na vyama vingine katika juhudi za kuendeleza na
kuimarisha Kiswahili ndani na nje ya nchi wanachama, kuwaunganisha wanafunzi wa
Kiswahili Afrika Mashariki na Kati katika kukikuza Kiswahili pamoja na
kushirikiana na asasi mbalimbali zinazojihusisha na ukuzaji na uenezaji wa
Kiswahili.

CHAKAMA

Chama cha Kiswahili
Afrika Mashariki (CHAKAMA) ndicho cha tatu kwa umaarufu zaidi miongoni mwa
wasomi, wataalamu na wahadhiri wa vyuo vikuu baada ya CHAUKIDU na Chama cha
Walimu wa Lugha za Kiafrika (ALTA) ambacho haundaa makongamano yake jijini
Bayreuth, Ujerumani.

Kwa pamoja na Chama cha
Kiswahili cha Taifa (CHAKITA), CHAKAMA huchapisha jarida la chama na machapisho
mengine ili kusaidia kueneza taaluma za Kiswahili.

Aidha, huhifadhi
kumbukumbu za wataalamu wa Kiswahili kwa nia ya kutumia katika kufanikisha
malengo ya chama na wadau wa Kiswahili pamoja na kuratibu makongamano na
mijadala mbalimbali inayohusiana na taaluma za Kiswahili.

Chama huandaa
makongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote katika vyuo
mbalimbali katika nchi husika.

Katika makongamano
hayo, mada mbalimbali zinazohusu Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa
lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa kuhusu maendeleo ya chama. Makala
mbalimbali huandikwa na kuchapishwa kwa minajili ya kusomwa na watu mbalimbali.

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'HEKIMA'
Posted by: MwlMaeda - 12-15-2021, 08:22 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' HEKIMA'

Neno *hekima* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Maarifa, uwezo wa akili alionao mtu unaomuwezesha kufikiri kwa kina na kutoa uamuzi unaokubalika; busara.

2. Uwezo wa akili katika kutoa maamuzi kutokana na tajiriba na uzoefu wa muda mrefu.

3.  Akili inayomuwezesha mtu kufikiri na kuweza kutoa uamuzi unaofaa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *hekima* ( soma: *hikmatun/hikmatan/hikmatin* *حكمة* ) lina maana zifuatazo:

1. Uamuzi, *masdar* *مصدر* *tendo-jina* kutokana na *kitenzi* cha Kiarabu *hakama* *حكم* (ameamua/ametoa uamuzi).

2. Maarifa ya kujua kilicho bora zaidi kwa kutumia njia bora za kielimu; falsafa.

3. Taaluma ya kujua uhalisia wa mambo.

4. Uwezo wa kudhibiti nafsi na mihemko wakati wa kupandwa na ghadhabu/hasira.

5. Haki, uadilifu.

6. Sababu ya kutokea jambo fulani.

7. Maneno machache yenye maana kubwa na pana.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *hikmatun* *حكمة*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *hekima* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika ingawa imejifunga katika uwezo wa akili wa kufikiri na kutoa uamuzi unaofaa.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA'
Posted by: MwlMaeda - 12-15-2021, 02:28 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA'.

Neno muktadha (wingi: miktadha) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Mazingira yanayobainisha mahali jambo lilipofanyika.

2. Mazingira ya neno (msamiati) katika tungo au sentensi yanayoonesha uhusiano wake na maneno mengine.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *muktadha* ( soma: *muqtadhwaa* *مقتضى* ) lina maana zifuatazo:

1. Kinachohitajika/kinacholazimu; jina la Mtendewa wa kitenzi cha Kiarabu iqtadhwaa اقتضى (-،mehitaji, -melazimu.)

2.  Mazingira ya jambo fulani.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *muqtadhwaa* *مقتضى*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *muktadha* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA'
Posted by: MwlMaeda - 12-15-2021, 07:42 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

*HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA'.*

Neno *Shajara* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Kitabu maalumu ambacho hutumika kuandika kumbukumbu ya matukio ya kila siku.

2. Mpango maalumu unaoonesha mfuatano wa kuzaliwa katika familia au ukoo; utaratibu wenye kuonesha uhusiano wa ukoo mzima kadiri walivyozaliwa kuumeni na kuukeni.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *shajara* ( soma: *shajaratun/shajaratan/shajaratin* *شجرة* ) lina maana zifuatazo:

1. Mmea ulio na mizizi, shina gumu na matawi yenye majani; mti.

2. Maelezo ya nasaba ya familia au ukoo. 

3. Mti wa uhai ( *shajaratul* *Hayaat* *شجرة* *الحياة* ) - mti wa kujua mema na maovu - ambao Nabii Adam na Bi. Hawa (Eva) walikatazwa kula matunda yake walipokuwa peponi.

4. Mti wa Krismas ( *shajaratul Miilaad* *شجرة* *الميلاد* ).

5. Mti uliolaaniwa *shajaratuz Zaqquum* , Mti wa Zaqqum *الشجرة* *الزقوم*  mti wowote wenye sumu inayoua (infernal tree with bitter fruit. - Special food that causes death to its eater - in hell)

6. Alama ndogo (doa) katika kidevu cha mtoto mchanga.

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *shajarat* *شجرة*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *shajara* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika ingawa imejifunga katika uwekaji wa kumbukumbu na mambo ya nasaba.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  MFAHAMU ABDILATIF ABDALLA
Posted by: MwlMaeda - 12-15-2021, 07:35 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO ' HIRIZI'
Posted by: MwlMaeda - 12-15-2021, 12:45 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' HIRIZI'.

Neno Hirizi katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Dawa inayojumuisha maandishi, pamoja na uganga mwengine unaofungwa ama kwenye kitambaa au kwenye karatasi, kwa imani kuwa inaweza kufanya kile kinacholengwa mfano kumpa mtumiaji kinga dhidi ya madhara. 

2. Kitu kilichofungwa kwenye ngozi au nguo au kijikaratasi chenye maandishi ya Kiarabu kinachoaminiwa kuwa ni dawa ya kujikinga na madhara ambacho huvaliwa mwilini. 

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *hirizi* ( soma: *hirzun/hirzan/hirzin* *حرز* ) lina maana zifuatazo:

1. Kifaa kilicho ngao ya kujilinda.

2. Eneo lenye ulinzi na amani ambalo watu hupata hifadhi ya maisha yao; ngome.

3. Kitu kinachotoa KINGA dhidi ya madhara.

4. Kanzi ya kuhifadhi vitu vya thamani.

5. Fungu analopata mrithi kutokana na mgawanyo wa mirathi.

6. Kitu kinachoandikwa kwa nia ya kumkinga atakayekibeba dhidi ya shari na maradhi (kama wanavyodai).

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *hirizi/hirz* *حرز*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *hirizi* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika ingawa imejifunga katika mambo ya uganga na kago.

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'BALAGHA'
Posted by: MwlMaeda - 12-14-2021, 07:01 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' BALAGHA'.

Neno Balagha katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Ufundi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi maelezo na kuuliza hadhira maswali yasiyo na majibu kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji.

2. Mtu ambaye ni stadi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji.

3. Swali linaloulizwa kwa udadisi na lisilohitaji majibu.

4. Ufundi wa matumizi ya lugha kwa nia ya kumfanya msikilizaji ashawishike au afurahike.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *balagha* ( soma: balaaghatun/balaaghatan/balaaghatin بلاغة) lina maana zifuatazo:

1. Namna bora ya kutoa maelezo na nguvu ya kushawishi na kuathiri.

2. (Kwa Wanazuoni wa Taaluma ya Balaagha-Elimu ya Ufasaha wa kusema/kuandika) ufasaha wenye kubeba maneno yanayosadifu muktadha.

3. Ufasaha wa kutamka na kunyoosha maneno.

4. Balaagha ya Kiarabu: Taaluma ya ufasaha wa kusema na kutia madoido inayojumuisha fani tatu, nazo ni: ALBAYAAN (Rhetoric), ALMAAN (Semantic) na ALBADII'I (The Art of Figures of Speech/The Art of Metaphors and Stylistics/Good Style)

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *balaagha *(tun)* *بلاغة*  ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *balagha* , maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - hazikubadilika bali imeongezeka maana ya mtu ambaye ni stadi wa kutumia lugha kwa kutia chumvi kwa lengo la kuvutia hisia za msikilizaji. Mtu mwenye sifa hizi kwa Kiarabu huitwa *baliigh* *بليغ* na sio *balagha* .

*Shukran sana.*

*Khamis S.M. Mataka.*

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA'
Posted by: MwlMaeda - 12-13-2021, 11:11 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA'

Neno Muamala  (wingi: miamala) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:

1. Tukio la kibiashara, kifedha na kiuchumi kama vile ununuaji, uuzaji, uchukuaji au uwekaji fedha benki.

2. Uhusiano wa kibiashara baina ya upande, mtu au nchi moja na nchi nyingine, unaowezesha uuzaji na ununuaji bidhaa baina ya pande husika.

3. Hali ya uwelewano baina ya watu.

4. Uendeshaji wa biashara, ununuaji na uuzaji wa bidhaa.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *muamala* ( soma: muaamalatun/muaamalatan/muaamalatin معاملة ) lina maana zifuatazo:

1. Kuamiliana/kutendeana/kufanyiana (Tendo-jina la kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita aamala عامل (tendeana)). Wingi wa neno muaamala(tun) معاملة ni muaamaalaatun معاملات

2. Kivumishi - enye uhusiano na biashara. Muaamalatun Tijaariyyah معاملة تجارية shughuli ya biashara baina ya pande mbili au zaidi.

3. Hukumu za kisheria zinazohusiana na mambo yasiyo ya kiibada muaamalaatun معاملات

Kinachodhihiri ni kuwa neno hili (muaamala (tun) معاملة) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *muamala*(wingi: *miamala* ) maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - hazikubadilika.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item

  SHAIRI: NILETEENI TAULO
Posted by: MwlMaeda - 12-12-2021, 05:15 PM - Forum: Ushairi - No Replies

NILETEENI TAULO
Inanikuta izara, dawatini nikiketi,
Duara inanichora, katika yangu sketi,
Hapo naificha sura, naaibika banati,
Nileteeni taulo!

Hunikosesha jubuni, wenzangu wananicheka,
Hapo nakosa amani, kando nao kujiweka,
Ninapokuwa hedhini, kweli ninaaibika,
Nileteeni taulo!

Haiachi kumwagika, nikisimama upesi,
Vile inatiririka, ni damu sio kamasi,
Kila mwezi ukifika, nahisi mwenye mkosi,
Nileteeni taulo!

Hunandama wavulana, na nyimbo kuniimbia,
Huruma nao hawana, hawawezi kutulia,
Kusoma jambo la mana, hedhi inanikosea,
Nileteeni taulo!

Nashindwa vema kusoma, yanifikavyo madhila,
Masomoni ninakwama, nenda bwenini kulala,
Kweli hedhi na kusoma, ni Kama lila na fila,
Nileteeni taulo!

Walimu huniadhibu, hudhania makusudi,
Hali inanipa tabu, mie siye mkaidi,
Hedhi inaniadhibu, masomo nyuma narudi,
Nileteeni taulo!

Enyi wafadhili wema, macho mnitupieni,
Ninachoka kuwa wima, inijapo darasani,
Nahofia kuchutama, sije toka hadharani,
Nileteeni taulo!

Serikali nanyi pia, hebu mnichinhuzeni,
Hedhi yanitia doa, hasa niwapo shuleni,
Kwenu leo ninalia, taulo nileteeni,
Nileteeni taulo!

Nimefika kaditama, ombi langu nalitua,
Nami nibaki salama, nisome bila udhia,
Mkinipa nitasoma, darasani tatulia,
Niliteeni taulo!

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

Print this item