ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA' (/showthread.php?tid=1737) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA' - MwlMaeda - 12-13-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MUAMALA' Neno Muamala (wingi: miamala) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Tukio la kibiashara, kifedha na kiuchumi kama vile ununuaji, uuzaji, uchukuaji au uwekaji fedha benki. 2. Uhusiano wa kibiashara baina ya upande, mtu au nchi moja na nchi nyingine, unaowezesha uuzaji na ununuaji bidhaa baina ya pande husika. 3. Hali ya uwelewano baina ya watu. 4. Uendeshaji wa biashara, ununuaji na uuzaji wa bidhaa. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *muamala* ( soma: muaamalatun/muaamalatan/muaamalatin معاملة ) lina maana zifuatazo: 1. Kuamiliana/kutendeana/kufanyiana (Tendo-jina la kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita aamala عامل (tendeana)). Wingi wa neno muaamala(tun) معاملة ni muaamaalaatun معاملات 2. Kivumishi - enye uhusiano na biashara. Muaamalatun Tijaariyyah معاملة تجارية shughuli ya biashara baina ya pande mbili au zaidi. 3. Hukumu za kisheria zinazohusiana na mambo yasiyo ya kiibada muaamalaatun معاملات Kinachodhihiri ni kuwa neno hili (muaamala (tun) معاملة) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *muamala*(wingi: *miamala* ) maana zake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - hazikubadilika. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |