ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA' (/showthread.php?tid=1744) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA' - MwlMaeda - 12-15-2021 *HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'SHAJARA'.* Neno *Shajara* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Kitabu maalumu ambacho hutumika kuandika kumbukumbu ya matukio ya kila siku. 2. Mpango maalumu unaoonesha mfuatano wa kuzaliwa katika familia au ukoo; utaratibu wenye kuonesha uhusiano wa ukoo mzima kadiri walivyozaliwa kuumeni na kuukeni. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *shajara* ( soma: *shajaratun/shajaratan/shajaratin* *شجرة* ) lina maana zifuatazo: 1. Mmea ulio na mizizi, shina gumu na matawi yenye majani; mti. 2. Maelezo ya nasaba ya familia au ukoo. 3. Mti wa uhai ( *shajaratul* *Hayaat* *شجرة* *الحياة* ) - mti wa kujua mema na maovu - ambao Nabii Adam na Bi. Hawa (Eva) walikatazwa kula matunda yake walipokuwa peponi. 4. Mti wa Krismas ( *shajaratul Miilaad* *شجرة* *الميلاد* ). 5. Mti uliolaaniwa *shajaratuz Zaqquum* , Mti wa Zaqqum *الشجرة* *الزقوم* mti wowote wenye sumu inayoua (infernal tree with bitter fruit. - Special food that causes death to its eater - in hell) 6. Alama ndogo (doa) katika kidevu cha mtoto mchanga. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *shajarat* *شجرة* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *shajara* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika ingawa imejifunga katika uwekaji wa kumbukumbu na mambo ya nasaba. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |