ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA' (/showthread.php?tid=1746) |
ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA' - MwlMaeda - 12-15-2021 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO ' MUKTADHA'. Neno muktadha (wingi: miktadha) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo: 1. Mazingira yanayobainisha mahali jambo lilipofanyika. 2. Mazingira ya neno (msamiati) katika tungo au sentensi yanayoonesha uhusiano wake na maneno mengine. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *muktadha* ( soma: *muqtadhwaa* *مقتضى* ) lina maana zifuatazo: 1. Kinachohitajika/kinacholazimu; jina la Mtendewa wa kitenzi cha Kiarabu iqtadhwaa اقتضى (-،mehitaji, -melazimu.) 2. Mazingira ya jambo fulani. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *muqtadhwaa* *مقتضى* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa likawa *muktadha* maana yake katika lugha yake ya asili - Kiarabu - haikubadilika. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |