MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 48 online users.
» 0 Member(s) | 47 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  SHAIRI : UTAMU WA NDOA
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 07:28 AM - Forum: Ushairi - No Replies

UTAMU WA NDOA
Kuna vilivyo vitamu, Ndoa ni zaidi yao
Tena ile ilodumu, Utamu kila uchao
Ndoa rahaye adhimu, Heshima ikiwa ngao
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Tunafaidi ndoani, Yangu hamu kuwajuza
Utamu uso kifani, Kwa dhati nawaeleza
Ndoa jambo la thamani, Kubwa sauti napaza
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Tunavila vya halali, Haramu twaikimbia
Vya karibu sio mbali, Bila ya kufakamia
Ikiwa nzuri kauli, Ndoa haitokimbia
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Ndoa ni jambo la enzi, Walioana wahenga
Tena jambo la mapenzi, Ni wajibu kuichunga
Ndoa hitaki ushenzi, Wala magomvi kujenga
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Utamu wanaujua, Wanandoa majumbani
Magonjwa wakiugua, Kudekea mapajani
Jamani tuombe dua, Ndoa ziwe na amani
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Wanandoa marafiki, Mahaba kiunganishi
Jitengeni wanafiki, Wacheni uchonganishi
Ndoa tamu hivunjiki, Toeni wenu uzushi
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Yapikwa mahanjumati, Ndoani papakuliwa
Halua na kalimati, Vitamu sana vyaliwa
Samaki wali chapati, Utamu wa kuchachawa
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Amwambie mume mke, Mume nakupenda sana
Mume kidogo acheke, Ndomana tumeoana
Basi uje unishike, Pingamizi kwako sina
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Njoo tuoge bafuni, Mume wangu “mai dia”
Kisha tulale chumbani, Usiku umewadia
Leo sijui kwanini, Hamu imenizidia
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Ndoa yazaa watoto, Faraja ya wanandoa
Pia huzidi kipato, Ridhiki MUNGU hutoa
Utamu ndoa si ndoto, Nawambia wasooa
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

Hatima nimeifika, Tamu ya ndoa kunena
Kwaherini naondoka, Ishala tutaonana
Ndoa sifa kuipaka, La kuongezea sina
Tamu kuliko asali, Ndoa jaala ya MOLA

(Kitogo wa Kitogo, Mwananchi wa Kawaida, Julai 31, 2018, Morogoro)

Print this item

  SHAIRI : TUCHAGUE KWA MAKINI VIONGOZI TANZANIA
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 07:22 AM - Forum: Ushairi - No Replies

  1. Hoja ninaieleza, uchaguzi Tanzania
    Ni yupi anyeweza, usukukani kuchukua?
    Pasi kutudidimiza, tupate kumchagua
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  2. Wengi wamejitokeza, nafasi kuziwania
    Sera wanatueleza, watakazozitumia
    Ahadi zinapendeza, wanazotutangazia
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  3. Wengi wamejitokeza, ikulu kugombania
    Mazuri wayatangaza, tupate kuwachagua
    Kama ukiwachunguza, ni vigumu kuamua
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  4. Ugumu ninaowaza, ni jinsi ya kuchagua
    Kila mtu atangaza, ndiye anayetufaa
    Kutuondolea giza, na kutuletea taa
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  5. Sera wanazoeleza, wakiwa kwenye jukwaa
    Kama wakitekeleza, tuendako kunang’aa
    Swali ninajiuliza, ni nani anotufaa
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  6. Nataka kupendekeza, jambo la kuzingatia
    Umakini natangaza, ndio wa kutegemea
    Lisijekutuumiza, maamuzi kujutia
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  7. Mola pekee anaweza, kutupatia “Kifaa”
    Maombi tukiongeza, Yeye atatusikia
    Kamwe hatutateleza, Mungu kumtegemea
    Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  8. Asiyejitanguliza, kwake kujipakulia
        Awezae kufukuza, wanaotuharibia
        Mwenye kuitekeleza, katiba ya Tanzania
       Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

    9. Yule asiyewabeza, fukara kuwabagua

         Aweza kuwatangaza, mali wanotuibia
        Vijana nao ajuza, aweze kuwatetea
       Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

   10. Awezae kuzitunza, mali zote zaraia
        Wageni wanowekeza, wazingatie sheria
       Aweze kuwahimiza, kodi zetu kulipia
       Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

   11. Ninarudia kukaza, jibu la Watanzania
        Maombi jambo la kwanza, Mola asikie dua
       Mmoja kumchomoza, hata wangekuwa mia
      Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  12. Tumuombeni Muweza, hekima kutujalia
       Tusipate makengeza, wakati wa kuchagua
       Kalamu isijecheza, na kisha tukakosea
       Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

  13. Naomba kuwahimiza, tuombee wagombea
        Mungu aweze watunza, afya usalama pia
       Kampeni kumaliza, bila baya kutokea
      Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

 14. Maadui wanaweza, Uchaguzi kutumia
       Mabaya kuyapenyeza. ili kutuchafulia
      Lakini Mungu aweza, mabaya kutukingia
      Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

15. Jingine linaloweza, majanga kutuletea
     “Media” zikitangaza, upande kuegemea
      Au zikitueleza, mambo yanayochochea
     Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

 16. Shairi nalikatiza, hapa sitaendelea
       Maneno niloeleza, nibudi kuzingatia
      Mungu uliye Muweza, ibariki Tanzania
     Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania

Print this item

  SHAIRI : RAIS ANAYEFAA KWA MUNGU ATATOKEA
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 07:12 AM - Forum: Ushairi - No Replies

  1. Kampeni zimeanza, uchaguzi wasogea
    Ilani wanatangaza, kuwanadi wagombea
    Swali la kujiuliza, nani anayetufaa?
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea.

  2. Wengi wamejitokeza, ikulu kugombania
    Mazuri wayatangaza, tupate kuwachagua
    Kama ukiwachunguza, ni vigumu kuamua
    Raisanayefaa, kwaMunguatatokea

  3. Chama gani kinaweza, kuivusha Tanzania?
    Kero zetu kumaliza, watu waache kulia?
    Rushwa kuitokomeza, ufisadi kufukia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  4. Sifa za anayeweza, kuwa Rais sawia
    Ni amchaye Muweza, Muumbaji wa dunia
    Mwenye kujinyenyekeza, watu kuwatumikia
    Rais anayefaa, kwa Munguatatokea

  5. Asiyekwenda kuuza, mali za Watanzania
    Wala kujipendekeza, kwa wanaotuibiaMwenye sifa ya kuweza, maovu kuyakemeaRais anayefaa, kwa Mungu atatokea
  6. Asiyejitanguliza, kwake kujipakulia
    Awezae kufukuza, wanaotuharibia
    Mwenye kuitekeleza, katiba ya Tanzania
    Raisanayefaa, kwa Mungu atatokea

  7. Yule asiyewabeza, fukara kuwabagua
    Aweza kuwatangaza, mali wanotuibia
    Vijana nao ajuza, aweze kuwatetea
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  8. Awezae kuzitunza, mali zote zaraia
    Wageni wanowekeza, wazingatie sheria
    Aweze kuwahimiza, kodi zetu kulipia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  9. Kilimo kiwe cha kwanza, njuga akikivalia
    Viwanda wamedumaza, yeye ajekufufua
    Ajira kuzitokeza, uchumi kuufufua
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  10. Utalii kuukuza, kipato kuongezea
    Ufanisi kuukaza, huduma za jumuia
    Ukali kuongeza, uzembe ujepotea
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  11. Kila ninakoangaza, simjui anofaa
    Mola peke anaweza, kutupatia Kifaa
    Maombi tukiongeza, Yeye atatusikia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  12. Yeye atakayeweza, usukani kuchukua
    Pasi kutudidimiza, ni vigumu kumjua
    Mungu kumtanguliza, ndio njia nawambia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  13. Wengi wamejitokeza, wakidai wanania
    Ya machungu kumaliza, ikulu wakiingia
    Kumbe myoyoni wawaza, faida kujipatia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  14. Wagombea nakataza, mziepuke ghasia
    Yaache yenye kukwaza, kote mtakotembea
    Sera zenu kueleza, pasi kuleta udhia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  15. Ninarudia kukaza, jibu la Watanzania
    Maombi jambo la kwanza, Mola asikie dua
    Mmoja kumchomoza, hata kama wajemia
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  16. Shairi nalikatiza, hapa sitaendelea
    Maneno niloeleza, nibudi kuzingatia
    Mungu uliye Muweza, ibariki Tanzania
    Rais anayefaa, kwa Mungu atatokea

  1. Rodgers Namwenje0764 222244

Print this item

  SHAIRI : AMANI
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 07:06 AM - Forum: Ushairi - No Replies

SHAIRI NAWALETEA, HAKIKA KUWAIMBIA,
SIKIO KUNIPATIA, MENGI MKAYASIKIA,
AMANI  YA TANZANIA, NA DUNIA NI SIKIA,
TUIDUMISHE  AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
HALI YA MTU YEYOTE, KUISHI BILA KUWASI,
HASA KWENYE MAMBO, YOTE AMANI INA NAFASI,
UCHUMI NA PANDE ZOTE, SIASA ISIYOASI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI GAO MUHIMU
 
AMANI KWENYE TAIFA, KATIKA NYANJA MUHIMU,
AMANI KWENYE TAIFA, KWAMBA MTU AHITIMU,
AMANI HAINA NYUFA, KUITUNZA SIO NGUMU,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI  NI NGAO MUHIMU.
 
AMANI HUVURUGIKA, YAKIWEPO MACHAFUKO,
DAMU NYINGI HUMWAGIKA, WATU WENGI HANGAIKO,
WANAWAKE HUDHURIKA, WAKUWA KAMA VIFUKO,
TUDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
UROHO WA MADARAKA, BINAFSI CHANZO NDIO,
RAIA WAFEDHEHEKA, VIONGOZI HAO SIO,
HAWATAKI KOSOLEWA, WANAKUWA NI TISHIO,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
MAKUNDI YA UGAIDI, DUNIANI KWA JUMLA,
YANAFANYA MAKUSUDI, MACHAFUKO KUTAWALA,
UCHUMI NYUMA WARUDI, WADUMAA KAMA SWALA,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
UCHOCHEZI NAO SHIDA, UNAZUA MIGOGORO,
TAIFA LAWA HUSUDA, HUCHIMBWA KAMA MTARO,
AMANI YAFANYWA ODA, YAWEKOSA KAMA PAJERO,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
UDINI NA NI NJIA, YA KUONDOA AMANI,
UMAARUFU SIKIA, UTAWALA KUTAMANI,
MAKUNDI KUSHIKILIA, MACHAFUKO DUNIANI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
YAFUATAYO TUMIA, ILI KULINDA AMANI,
UCHOCHEZI ACHILIA, UDINI KUTOTAMANI,
UGAIDI FUTILIA, TAIFA KULIDHAMINI,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU
 
MWISHONI NIMEFIKIA, MENGI NIMESHAYATOA,
MENGINE YAWE USIA, KAZI MPATE TENDEA,
VIJANA KUZINGATIA, SHERIA KUSHIKILIA,
TUIDUMISHE AMANI, KWANI NI NGAO MUHIMU.
 
Na: Verian T. Francis (HKL-2018)

Print this item

  SHAIRI : ENENDA KOFI ANNAN
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:48 AM - Forum: Ushairi - No Replies

[Image: 494f4456-eb30-477b-a982-7fb095dc5c5b.jpg]
SHAIRI : NAMBE
Methali nimeziona, kuna daka, pia suke,
Ila hii imenona, naitwisha Sifa zake,
Naiwekea na vina, kwenye uga isomeke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake.

Kipi kilicho na mwanzo, mwisho wake usifike,
Nani alipata tunzo, kila mwaka peke yake,
Ipi iliyo na nyenzo, siku isitetereke?
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake?

Nambe aliyezaliwa na kifo kisimdake,
Nani aliyejaliwa kuishi milele peke,
Ni sote tutafukiwa, tunataka tusitake,
Nambe kilicho na mwanzo,kikakosa mwisho wake.

Nani aliye na dini, salam zote ahusike,
Asubuhi na jioni, maombini asitoke,
Yu kutwa madhabahuni, na kula asikumbuke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake?

Tongoa alo na nywele, zilojaa kichwa chake,
Akae Nazo milele, vyovyote zisinyoleke,
Atembee kwa jefule, akifa budi zing’oke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake.

Yupi alo kiongozi, na umma achagulike,
Apendwe kama kinyozi, yaani aaminike,
Iko siku namaizi, watampiga mateke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake?

Longa aliye mbabe, amkose mwanzi wake,
Silaha nzito abebe, Tena asipepesuke,
Hayuko alo na ngebe, akaachwa apayuke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake.

Basi ndo hivyo wenzangu, waume na wanawake,
Tumrejeeni mungu, kesho tukathaminike,
Mambo ya ki ulimwengu, yasitupe sekeseke,
Nambe kilicho na mwanzo, kikakosa mwisho wake?

Enenda Kofi Anani, huko Salama ufike,
Ulofanya duniani, Rabi yamefika kwake,
Anajua kwa yakini, wapi wewe akuweke,
Bwana Kofi Anan, mno tutakukumbuka.

Na: Mwl R.R. Mfaume(Fundi)
Kivuli cha Mvumo open school
Morogoro

Print this item

  SHAIRI : KISWAHILI LUGHA YETU
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:46 AM - Forum: Ushairi - No Replies

1:Kiswhahili lugha yetu,Lazima tuitunuku
Shani tuipe mwakwetu,na maua tutunuku
Lugha yenye ladha kuntu,Tuipambe kwa vikuku
Tuipambe kwa vikuku,lugha yetu kiswahili

2:Lugha iliyosambaa ,Bara hata
visiwani
Lugha isiyo mawaa,tuipe yake thamani
Watu waiongelelea,lugha hii yenye shani
Tuipambe kwa vikuku,Lugha yetu kiswahili

3:Lugha iliyo thabiti,imeshika usukani
Ni tamu kama matiti,ya mwana yu kifuani
Lugha imejizatiti,Kutambaa duniani
Tuipambe kwa vikuku ,Lugha yetu kiswahili

4:Maneno imesheheni,mabini na mabanati
Mubashara na rosheni,sawia sasa ni kuntu
Asante ikongoleni,Kiswahili chetu kuntu
Tuiipambe kwa vikuku,Lugha yetu kiswahi

5:Beti tano zanitosha,Lugha yangu kuisifu
Lugha mejaa bashasha,wanagenzi nawasifu
Lugha yanifurahisha, siku zote naisifu
Tuipambe kwa vikuku ,Lugha yetu kiswahili.

mwl Mwenda Juhudi s.s

Print this item

  SHAIRI : MANENO YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:41 AM - Forum: Ushairi - No Replies

Kwanza kaa ufikiri, maneno haya yapime
Usimle kwa kikiri, kaa kwanza mtazame
Litaja kunguza kweli, kaa lenye moto shume
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kata mchongoma ule, ela situmie shoka
Kayaaza maji tele, na kata imekatika
Katibu wa kata ile, duniani katutoka
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kweli mepatiwa pasi, ya kusafiri nchini
Nguo ukapiga pasi, ili wende safarini
Mitihani ulopasi, hairidhishi lakini
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Bi haji kufuma kamba, mwenyewe keshazoea
Wala hana jingi vumba, kamba samaki muruwa
Jamaa yule kwa kamba, uongo amebobea
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Paa pia ukitua, juwa huwi kama njiwa
Ninaomba kumjua, paa aloliezua
Ukila utasinzia, paa mtamu sawia
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kwenye nyumba za kupanga, kuna vituko pomoni
Refa apiga kipenga, panga lipo kiunoni
Mipango uliyopanga, yote ya kihayawani
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Ua lakini ujue, hilo silo jambo jema
Ua wa bibi somoe, umeanguka mchana
Ua lipi niangue, nimpe aloegama
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Maneno haya tapenda, kwenye lugha kiyajua
Taa, pamba, nalo ganda na neno litwalo jua
Kwa kweli yalivyoundwa, ni utamu kitumia
Ayapinganye maneno, si mswahili wa ndani

@haki zote zimehifadhiwa
#mzee m. y

Print this item

  TENZI TATU ZA KALE
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:35 AM - Forum: Ushairi - No Replies

[Image: DSCF0436%5B1%5D.JPG]

Na Profesa Mbele
Leo napenda kukitambulisha kwako mdau kitabu muhimu cha ki-Swahili, Tenzi Tatu za Kale. Nilinunua nakala yangu miaka kadhaa iliyopita katika duka la vitabu la Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kitabu hiki ni mkusanyo wa tenzi tatu za kale maarufu: Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Kijumwa; Al Inkishafi, uliotungwa na Sayyid Abdalla bin Ali; na Mwanakupona, uliotungwa na Mwana Kupona binti Mshamu. Kitabu kimehaririwa na M.M. Mulokozi, profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kilichapishwa na Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili mwaka 1999.
Hizi ni kati ya tenzi maarufu kabisa katika ki-Swahili. Kwa msingi wa sanaa na maudhui, tenzi hizi zina hadhi kamili ya kuwemo katika orodha ambayo kwa ki-Ingereza huitwa “classics.”
Fumo Liyongo ni hadithi inayomhusu shujaa Fumo Liongo, ambaye mimi, kutokana na utafiti wangu wa miaka mingi, napendelea kumwita Liongo Fumo. Huyu ni shujaa wa kale, labda miaka elfu moja iliyopita, na ndiye anayesifika kuliko wote tangu zamani katika jamii ya wa-Swahili.
Alikuwa pandikizi la mtu, mwenye vipaji kadhaa: kuwashinda maadui, shabaha katika kutumia upinde na mshale, ufundi wa kutunga nyimbo na mashairi. Juu ya yote, alikuwa muungwana sana, mfano wa kuigwa. Lakini alifanyiwa visa na ndugu yake ambaye alikuwa mfalme, hadi hatimaye akauawa na kijana mdogo, ambaye alikuwa mpwa wake.
Al Inkishafi ni utenzi wa tafakuri na falsafa kuhusu maisha, ambao umejikita katika kuuliza maana ya maisha ni nini. Mtunzi alilishughulikia suali hili kwa kuzingatia jinsi ustawi na utukufu wa wa-Swahili, hasa wa mji wa Pate, ulivyoanguka. Pate ulikuwa mji maarufu, wenye hadhi na mali, lakini kutokana na masaibu mbali mbali, ullipoteza hadhi hiyo na kuishia kuwa magofu.
Hii dhamira imeshughulikiwa tangu zamani na waandishi wengi wa pande za Arabuni, Uajemi, Ulaya na sehemu zingine duniani. Wanafalsafa pia wamehoji maana ya maisha, hasa wanafalsafa wa mkondo wa “existentialism.”
Mwana Kupona ni utenzi uliotungwa na mama kumuusia binti yake kuhusu maisha ya ndoa, wajibu wake katika maisha hayo, na wajibu wake kwa watu kwa ujumla. Huu ni utenzi maarufu sana, ambao ni chimbuko la tungo za waandishi wengine, kama vile Shaaban Robert.
Mhariri amefanya kazi nzuri ya kuweka maelezo juu ya historia ya tenzi hizi, kuhusu watunzi, na kuhusu tafiti zilizofanywa juu ya tenzi hizi. Ametoa orodha ya maandishi ya wataalam mbali mbali, kumwezesha msomaji kufuatilia zaidi masuala hayo.
Kwa bahati nzuri, katika utafiti niliofanya kwa miaka mingi kuhusu tungo za kale za ki-Swahili, nimezitafiti tenzi hizi tatu, hasa Utenzi wa Fumo Liongo, ambao nimeutafiti kwa kina na kujipatia umaarufu kama mtafiti anayeongoza katika utafiti wa utenzi huu na masimulizi husika.
Watafiti bado wana majukumu makubwa ya kutafiti tenzi hizi na tenzi zingine. Kazi moja muhimu inayohitaji kufanyiwa bidii sana ni kuangalia miswada mbali mbali ya kila utenzi. Inahitajika juhudi na umakini kuangalia maneno yaliyotumika katika miswada hiyo, sentensi na lahaja, na kubaini tofauti zinazojitokeza.
Kuna tofauti za kila aina baina ya mswada na mswada, na ni juu ya watafiti kuzitambua na kuzitolea maelezo. Miswada ya tenzi zote za zamani za ki-Swahili inatofautiana katika vipengele mbali mbali.
Jukumu jingine ni kuzunguka katika maeneo ya wa-Swahili, kama vile mwambao wa Kenya, ambako nilifanya utafiti miaka ya 1989 hadi 1991. Huko nilikutana na mabingwa wa lugha na tungo za ki-Swahili, kama vile Mzee Ahmed Sheikh Nabhani wa Mombasa, na wazee wengine wa miji kama Witu na Lamu. Ni muhimu watafiti waende Pate, Siu, na kadhalika. Pia tunahitaji kufanya utafiti zaidi katika hifadhi za miswada ya ki-Swahili iliyopo katika maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha London, Berlin, na sehemu zingine.
Tenzi Tatu za Kale ni hazina kubwa kwa wasomaji wa kawaida, watafiti, na wanafunzi, hadi kiwango cha chuo kikuu. Kwa bahati nzuri kitabu hiki kinapatikana kirahisi Tanzania. Ninakipendekeza kwa yeyote anayetaka kujiongezea ufahamu wa lugha na fasihi ya ki-Swahili.

Print this item

  DHANA NA DHIMA YA UMAPOKEO KATIKA USHAIRI
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:32 AM - Forum: Nukuu - No Replies

Kwa Muhtasari
MKABALA wa kimapokeo ndio ulioanza katika kutoa fasili ya ushairi kutokana na ukweli kwamba watetezi wake waliupokea tu kutoka kwa wazee bila kuhoji ikiwa kweli mambo yalivyoelezwa ndivyo yalivyo au la.
Wao waliurithi tu. Dhana hii ya umapokeo ni tafsiri ya ile dhana ya Kiingereza “ Traditional approach.”
Gituma (2010) anafasili shairi kuwa ni mtungo wa kisanaa wenye mpangilio maalumu wa lugha ya mkato katika usemi, maandishi au wimbo unaoelezea wazi kuhusu mawazo, hisi au tukio kuhusu maisha na ambao hufuata utaratibu wa urari na muwala maalumu uliosheheni kanuni za utunzi wa mashairi.
Fasili hii inasisitiza kwamba “shairi ni wimbo, shairi huwa na urari (bila shaka wa vina na mizani), shairi huwa na kanuni mbalimbali.”
Maelezo haya bila shaka yametokana na athari za Abedi (1954:1) ambaye imani hiyo ilimfanya kuandika kitabu alichokiita ‘Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri’.
Jambo la dhahiri hapa ni kwamba utunzi wa mashairi una kanuni maalumu na kwamba kama shairi haliimbiki basi halina maana. Mtazamo huu kwamba shairi ni wimbo ndio unaotawala sana miongoni mwa wanamapokeo wengi.
Hili lina maana kwamba shairi linatungwa ili liimbwe na hadhira husika. Wazo hili linapewa nguvu na fasili ya Uvetie (1976) anaposema kwamba, “napenda kuwafafanulieni kwamba mashairi ni usemi usemwao kwa namna ya mafumbo na pia ni nyimbo.”
Zaidi ya kusisitiza ushairi kuwa ni wimbo, dhana nyingine kwamba shairi lazima liwe fumbo ni kusema kuwa kama shairi si fumbo basi si shairi.
Aidha, Mnyampala (1964:4) anabainisha kwamba mashairi ni nyimbo zenye maghani ya mvuto wa madoido na vingorimbo bora. Anachokisema hapa ni kwamba ushairi lazima utumie lugha tamu yenye madoido ya kuupamba. Dhana ya ushairi kama utamu wa lugha inaonekana pia kwa Uvetie (1976) ambaye anachagua kukiita kitabu chake cha mashairi ‘Utamu wa Lugha’.
Ingawa hivyo, fasili hizi zinaweza kuonekana kuwa sahihi zaidi katika fasihi simulizi ambapo utanzu wa ushairi (na hasa ushairi simulizi) unachukuliwa kuwa ni wimbo.
Kimsingi, tunapozungumzia utanzu wa ushairi katika fasihi simulizi tunazungumzia nyimbo za aina mbalimbali za makabila ya Kiafrika.
Ushairi kama wimbo ulionekana sana katika miaka ya awali ya maendeleo ya taaluma ya ushairi wa Kiswahili (kabla ya miaka ya 1960).
Baada ya hapo, dhana ya ushairi kama wimbo ilipingwa vikali. Hadi sasa inakubaliwa miongoni mwa wanazuoni na katika fasihi ya Kiswahili kwamba, shairi si lazima liimbike. Shairi linaweza kughaniwa, kutongolewa au hata kusemwa.
Kwa kusema kwamba shairi lazima liimbike, ina maana kwamba shairi lazima liwe na urari wa vina na mizani. Mashairi yanayopishana sana kivina na mizani ni vigumu kuyaimba.
Dhana hii ya urari wa vina na mizani kama sifa kuu ya shairi imepingwa vikali na hatimaye kubainika kwamba shairi linaweza kuwa na urari wa vina na mizani au lisiwe nao lakini bado likabaki kuwa shairi.
Jambo la kukumbuka ni kwamba shairi linapokosa urari wa vina na mizani kuna uwezekano mkubwa wa shairi husika kutoimbika.
Hivyo basi, dhana ya shairi kama wimbo si ya msingi japo hatuwezi kuipuuza kabisa kwani inajaribu kutupa upande mmoja wa sarafu ya shairi.
Zaidi ya msisitizo katika kanuni na uimbikaji, fasili nyingine za ushairi zimejikita zaidi katika dhima ya ushairi. Mnyampala (1975) anaufasili ushairi kwa kuzingatia nguvu ya shairi kuiasa, kuiongoza jamii kwa pamoja licha ya kusheheneza uzuri na utamu wa lugha.
Anauona ushairi kuwa ni utungo wenye maneno ya hekima na kwamba ndio utungo ulio bora sana katika maongozi ya dunia.
Anafafanua kwamba kuna aina tano za mashairi kwa kuzingatia maongozi na mafunzo yanayotoa. Aina hizo ni mashairi ya kawaida, mashairi ya furaha, mashairi ya huzuni, mashairi mazito na mashairi ya kuadibu.
Mashairi ya kawaida ni yale ambayo yana mawaidha ya dunia, visa na mikasa ya kawaida na mengine ya aina hiyo wakati mashairi ya furaha hushangilia tamasha iliyopo, kutakia heri na mafanikio, ombi la kudumisha furaha hiyo na waadhi kwa ajili ya tafrija hiyo.
Kwa upande wa yale yaliyomo katika mashairi ya huzuni, anayataja kuwa ni rambirambi, maombezi kwa Mungu kwa ajili ya marehemu, maombezi kwa wale waliobaki, historia ya marehemu na kumbukumbu itakiwayo.
Nayo mashairi mazito huwa ni mashairi ya kuzama (kufumba), mashairi ya tambo, pigo kuu la ushairi, furaha ya ushairi na taaluma zake na kuonyesha mbinu za lugha ya mshairi yule.
Aina nyingine ni mashairi ya kuadibu ambayo humwonya mtu kinagaubaga bila kutumia utusi, kumtanabahisha ya hatima, mashairi yanayohusu maandiko matakatifu na yale yahusuyo uungwana.
Wakati ambapo tunakubaliana na wazo kuwa shairi linaweza kumwongoza mwanadamu, tunaona kwamba ushairi unapaswa kufasiliwa kwa kuzingatia nduni bainifu na si nduni jumuishi kwani tanzu zote za fasihi huwa na jukumu hilo la kumwongoza mwanadamu.
Moja ya dhima kuu za fasihi ni kuelimisha, na huko ni kusema tanzu zote za fasihi huelimisha. Hata hivyo, izingatiwe kwamba si kila shairi hubeba mawazo ya hekima na linakusudia kutoa maongozi kwa jamii.
Yapo mashairi mengi ambayo yanapotosha jamii. Zaidi ya uwezo wake mkubwa wa kuielimisha jamii, fasihi inaweza pia kuipotosha jamii hiyo.

Print this item

  SHAIRI : NI NANI KAMA MWALIMU!?
Posted by: MwlMaeda - 01-03-2022, 11:24 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NI NANI KAMA MWALIMU!?
————————————

1.Naja nikiwakumbusha kuipitia nudhumu,
anayejenga maisha, laazizi maalimu,
yule alotufundisha, kwanza kushika kalamu,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

2. Nalola siku ya kwanza, nikipelekwa shuleni,
na wakati nilianza, kuingia darasani,
mwalimu alinifunza, ‘lufabeti kwa makini,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

3. Sana nilizikariri, herufi alonifunda,
tena nikiwa mahiri, wa nyimboze nilopenda,
hadi leo ninakiri, nafaidi ye matunda,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

4. Nakumbuka nikianza, kuandika mchangani,
kalamu yangu ya kwanza, ni kijiti wajameni,
Huyo aliyenifunza, mgee kheri Manani,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

5. Nakumbuka kuhesabu, tangu moja hadi kenda,
wakati ‘likuwa tabu, ikiwa inanishinda,
chonde chonde taratibu, mlezi akanifunda,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

6. Leo miye mhasibu, taasisi ya takwimu,
mdogo wangu tabibu, jijini Darisalamu,
si kwa bahati nasibu, ni matunda ya mwalimu,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

7. Wanoitwa wata’lamu, wa’zo maridhawa fani,
alowafunda mwalimu, leo wakuu nchini,
mlezi wangu mwalimu, sana ninakuthamini,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

8. Kumbukeni ni mwalimu, wa mataifa mlezi,
alowagea elimu, wa dunia welekezi,
kiongozi ufahamu, yoyote uliyo ngazi,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

9. Na wasifa wake jama, haumaliziki wala,
ndefu ja hadithi kama, alufu lela ulela,
namuombea salama, nipulike wangu Mola,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

10. Subukhana shukurani, beti kumi kutimia,
yaliyokuwa moyoni, hadhira nimepatia,
na baraka maishani, walezi n’kiwatakia,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?

*********
Rwaka Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda).
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,RWANDA.

[Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg][Image: 1f1f7-1f1fc.svg]

Print this item