SHAIRI : TUCHAGUE KWA MAKINI VIONGOZI TANZANIA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI : TUCHAGUE KWA MAKINI VIONGOZI TANZANIA (/showthread.php?tid=1982) |
SHAIRI : TUCHAGUE KWA MAKINI VIONGOZI TANZANIA - MwlMaeda - 01-04-2022
Mwenye kuitekeleza, katiba ya Tanzania Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 9. Yule asiyewabeza, fukara kuwabagua Aweza kuwatangaza, mali wanotuibia Vijana nao ajuza, aweze kuwatetea Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 10. Awezae kuzitunza, mali zote zaraia Wageni wanowekeza, wazingatie sheria Aweze kuwahimiza, kodi zetu kulipia Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 11. Ninarudia kukaza, jibu la Watanzania Maombi jambo la kwanza, Mola asikie dua Mmoja kumchomoza, hata wangekuwa mia Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 12. Tumuombeni Muweza, hekima kutujalia Tusipate makengeza, wakati wa kuchagua Kalamu isijecheza, na kisha tukakosea Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 13. Naomba kuwahimiza, tuombee wagombea Mungu aweze watunza, afya usalama pia Kampeni kumaliza, bila baya kutokea Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 14. Maadui wanaweza, Uchaguzi kutumia Mabaya kuyapenyeza. ili kutuchafulia Lakini Mungu aweza, mabaya kutukingia Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 15. Jingine linaloweza, majanga kutuletea “Media” zikitangaza, upande kuegemea Au zikitueleza, mambo yanayochochea Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania 16. Shairi nalikatiza, hapa sitaendelea Maneno niloeleza, nibudi kuzingatia Mungu uliye Muweza, ibariki Tanzania Tuchague kwa makini, viongozi Tanzania |