MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : MANENO YA KISWAHILI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI : MANENO YA KISWAHILI
#1
Kwanza kaa ufikiri, maneno haya yapime
Usimle kwa kikiri, kaa kwanza mtazame
Litaja kunguza kweli, kaa lenye moto shume
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kata mchongoma ule, ela situmie shoka
Kayaaza maji tele, na kata imekatika
Katibu wa kata ile, duniani katutoka
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kweli mepatiwa pasi, ya kusafiri nchini
Nguo ukapiga pasi, ili wende safarini
Mitihani ulopasi, hairidhishi lakini
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Bi haji kufuma kamba, mwenyewe keshazoea
Wala hana jingi vumba, kamba samaki muruwa
Jamaa yule kwa kamba, uongo amebobea
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Paa pia ukitua, juwa huwi kama njiwa
Ninaomba kumjua, paa aloliezua
Ukila utasinzia, paa mtamu sawia
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Kwenye nyumba za kupanga, kuna vituko pomoni
Refa apiga kipenga, panga lipo kiunoni
Mipango uliyopanga, yote ya kihayawani
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Ua lakini ujue, hilo silo jambo jema
Ua wa bibi somoe, umeanguka mchana
Ua lipi niangue, nimpe aloegama
Ayapingaye maneno, si mswahili wa ndani

Maneno haya tapenda, kwenye lugha kiyajua
Taa, pamba, nalo ganda na neno litwalo jua
Kwa kweli yalivyoundwa, ni utamu kitumia
Ayapinganye maneno, si mswahili wa ndani

@haki zote zimehifadhiwa
#mzee m. y

Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)