Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 40 online users. » 0 Member(s) | 39 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
VIPERA VYA USHAIRI SIMULIZI |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 09:14 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
VIPERA VYA USHAIRI SIMULIZI
(1) Nyimbo
Nyimbo ni tungo za kishairi zenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti, muwala maalumu na mapigo ya kimuziki na huwasilishwa kwa kuimbwa. Hutumia lugha yenye uwezo wa kuleta picha akilini. Msingi mkubwa wa nyimbo ni kuwako kwa sauti. Nyimbo huweza kuimbwa na mtu mmoja au kikundi cha watu. Nyimbo ndio asili ya ushairi. Kuna aina mbalimbali za nyimbo ambazo hutegemea mambo kadha: malengo, umri, jinsia, maudhui, wakati wa kuimba na mahali pa kuimba nyimbo hizo.
Sifa za nyimbo - Kuwapo kwa watu wanaoimbiwa au hadhira inayosikiliza uimbaji huo.
- Muktadha wa kuimbwa kwenyewe, yaani wimbo unawasilishwa wapi na katika muktadha gani. Kwa mfano harusi, ibada na kadhalika.
- Kuchezwa au miondoko ya kucheza ya mwili ya mwimbaji au hadhira yake.
- Maneno yanayoimbwa au matini yenyewe.
- Wimbo unaweza kumlenga mtu au hadhira iliyopo au isiyokuwepo.
- Sauti ya mwimbaji au waimbaji : mmoja huwaongoza wengine.
- Huandamana na matumizi ya ala za muziki kama ngoma, baragumu, siwa, zumari au chochote kile ambacho hutegemea jamii husika.
- Hugusa na kuibua hisia kwa njia mbalimbali.
- Waimbaji wanaweza kuwa na maleba ingawa si lazima.
- Nyimbo hutumia lugha nzito yenye kuibua taswira na hisia nzito za furaha, huzuni,mapenzi.
- Hutolewa kwa mahadhi ya kupanda na kushuka kwa sauti.
- Nyimbo hutumia lugha ya mkato yenye mpangilio maalum wa silabi, mishororo na beti zenye mapigo ya kimuziki.
- Huwa na takriri.
- Huweza kuwa na kiitikio kinachokaririwa.
Umuhimu wa nyimbo katika jamii - Huhifadhi matukio muhimu ya kihistoria.
- Hutumiwa kama burudani ya kutumbuiza waimbaji na hadhira.
- Hutumiwa kuliwaza na kufariji wenye majonzi.
- Hudumisha na kuwasilisha usanii wa tamaduni za jamii mbalimbali.
- Hutumiwa kuhamasisha watu kushiriki katika kutenda mambo fulani.
- Hutumiwa kama chombo cha kupitisha utamaduni wa jamii.
- Huelimisha, hukejeli na kuonya.
- Hutumiwa kuongoa watoto walale ama hata wapende kitu.
- Hurithisha sanaa yenyewe kwa vizazi kwa kupokeza kizazi hadi kingine.
- Hutumiwa katika vipera vingine kama vile ngano kuhusisha hadhira.
- Huchangia katika kukuza uzalendo, kwa mfano wimbo wa taifa na mengine ya kisiasa.
- Hukuza utangamano. Nyimbo za kazi (hodiya) zinapoimbwa hufanya watu kutangamana katika kundi moja.
- Hutia ujasiri. Wimbo kama vile nyiso na ule wa kivita huwapa wahusika ujasiri kukabiliana na yanayowaka bili au yatakayowakabili.
- Huweza kutumiwa kuwazindua watu walioko katika hali fulani (nyimbo za kisiasa)
- Hutumiwa kuonyesha ustadi wa msanii. Wimbo bora huonyesha ubora wa msanii husika.
- Ni mojawapo wa njia za kujipatia riziki.
Muundo wa nyimbo - Nyimbo hugawika katika mafungu (beti)
- Beti au mafungu huwa na mistari inayoitwa mishororo.
- Mishororo huwa na silabi zenye mdundo wa kimuziki.
- Huweza kuimbwa kwa kupokezana baina ya kiongozi na waimbaji ambao huimba kiitikio.
- Mafungu au mistari yanaweza kurudiwarudiwa kama kiitikio.
- Lugha huwa nzito na fiche.
- Hutumia lugha ya mkato.
- Waimbaji wanaweza kubuni maneno ya ziada na kuongezea kulingana na hafla.
- Baadhi ya nyimbo huwa na vina.
Sifa zinazofanya nyimbo ziwe mashairi - Huwasilisha ujumbe kwa kutumia lugha ya mkato.
- Kifungu kimoja au kadha huweza kukaririwa sawa na kibwagizo katika ushairi.
- Beti za mashairi hulinganishwa na stanza au vifungu vya nyimbo.
- Baadhi ya nyimbo huzingatia urari wa vina n ahata mizani katika mishororo na vifungu.
- Mishororo inayounda ubeti inalinganishwa na mistari inayounda vifungu katika vya nyimbo.
Umuhimu wa nyimbo katika masimulizi ya hadithi - Nyimbo hutumiwa kurefusha masimulizi ili kujenga hali ya taharuki
- Hujenga uhusiano wa karibu kati ya mtambaji na ha dhira yake.
- Nyimbo hutumiwa kuibua hisia kwa msimulizi kama vile hisia za furaha, huzuni na kadhalika.
- Nyimbo hutumiwa kuelezea jambo la siri kati ya wahusika, kwa mfano, mhusika aliye kwenye taabu fulani huweza kuomba msaada aokolewe kisirisiri kwa kutumia nyimbo.
- Husisimua hadhira na kuondolea ukinaifu wa masimulizi makavu.
- Huangazia maadili katika hadithi.
- Hutenganisha matukio yanayojumuisha hadithi.
- Ni kama kipumuo.
- Nyimbo huburudisha wakati wa utambaji hadithi.
Athari hasi za nyimbo - Kuna ukosefu wa maadili katika baadhi za nyimbo.
- Huweza kutumika kueneza propaganda kwa kutoa ujumbe au picha isiyo ya kweli kwa nia ya kufaidika kwa mwimbaji huku wakipotosha wasikilizaji.
- Huweza kuibua hisia za ukabila au utabaka na kwa hivyo kuchangia kuleta au kukoleza uadui au kutoelewana kwa wahusika.
- Nyimbo zinalevya; zinapumbaza.
- Baadhi ya nyimbo huwa na mawaidha mabovu,
hivyo, huwapotosha watu katika jamii. Kwa mfano, nyimbo zinazowapotosha vijana kuhusu kushiriki mihadarati.
Vibainishi vya nyimbo
(i) Vigelegele
Vigelegele ni mlio wa sauti ifanywayo kwa kutembeza ulimi mdomoni upesiupesi. Katika wimbo, vigelegele hutumika kuonyesha upeo wa juu wa furaha. Vigelegele huweza kupigwa pia kumpongeza mchezaji ambaye amecheza vizuri au mwimbaji kwa uimbaji wake muruwa.
(ii) Mkarara
Huu ni ule msitari au ubeti ambao hurudiwarudiwa mara nyingi na washiriki. Mkarara hasa ndio huwafanya wasikilizaji kushiriki.Husaidia kuondoa udhia wa kumsikiliza mshiriki mmoja.Aidha, huondoa usingizi na kumpa mwimbaji fursa ya kupumzika kidogo.
(iii) Mshindo
Ni mapigo ambayo hupigwa kwa mwendo ule ule katika nyimbo zetu, hususa zile za kucheza.Mapigo haya hufanywa kwa mguu mmoja au miwili. Katika baadhi ya jamii, miguu ya wachezaji hufungwa njuga, msewe au makopo.Njuga husababisha mlio ambao huleta uzuri au utamu wa aina yake.
(iv) Makofi
Makofi hutumika kumtia hamasa mchezaji aliye katikati yao na kadiri makofi yaongezekavyo ndivyo mchezaji huchangamka.
Aina za nyimbo
Nyimbo huainishwa kutegemea wahusika, sherehe au shughuli zinazohusishwa. Zipo aina nyingi sana za nyimbo za fasihi simulizi
Ifuatayo ni mifano ya aina hizo:
(a) Bembelezi/ bembea/ pembejezi
Ni nyimbo za kuwafariji au kuwabembeleza watoto walale au waache kulia.
Huimbwa taratibu kwa sauti ya kuongoa. Huwa fupi na zinazoonyesha kuliwaza. Kuna kurudiwarudiwa kwa maneno. Hutumiwa lugha shawishi na
wakati mwingine hutolewa ahadi za kununuliwa watoto zawadi.
(b) Mbolezi/ tahalili
Huimbwa wakati wa matanga au kifo.Hutegemea jamii inayohusika
na hata umri wa anayehusika. Huimbwa kwa nia ya kuwafariji waliofiwa. Huwatoa woga kwani hueleza kuwa kila mtu atafariki. Hukikashifu kifo na kukibeza kwa kuwachukuawapendwa. Aidha, mbolezi huweza kuimbwa katika hafla ya kuadhimisha makumbusho ya mtu.Mbolezi huimbwa kwa toni ya huzuni na pengine uchungu, hivyo kuibua hisia za ndani za mwombolezaji.
© Nyimbo za watoto / chekechea
Mtoto mchanga anapokua, akaweza kwenda, kukimbia na kusema, naye huanza kuimba pamoja na wenzake. Nyingi katika nyimbo hizi huimbwa katika michezo ya watoto; baadhi huimbwa kwa kujibizana.
(d) Sifo / tukuzo
Nyimbo za aina hii huweza kupatikana katika miktadha tofauti kama kwenye sherehe za kitamaduni, uwanja wa kisiasa, arusi na kwingineko. Hujaza maneno ya sifa na aghalabu matumizi ya chuku, istiari (kwa mfano, kuwalinganisha wanaosifiwa na wanyama wakali).
(e) Nyimbo za kisiasa
Huimbwa katika hadhara ya kisiasa au kwingineko. Ni nyimbo za kawaida sana katika jamii zetu. Nyimbo za kisiasa huwa na maudhui mapana kama vile kuzindua, kuhamasisha, propaganda, mapambano, kutia ari, kukejeli.
(f) Nyiso
Hizi ni nyimbo ambazo huimbwa jandoni. Hutumiwa kuwaandaa kihisia
Wanaotahiriwa kwa kuwapa ari ya kupitia kijembe cha ngariba. Nyiso huhimiza ujasiri na kukebehi woga. Huwaambia kuwa wameingia katika hatua nyingine ya maisha, yaani hatua ya utu uzima.
(g) Nyimbo za mapenzi / chombezi
Huimbiwa wapenzi. Hizi ni nyimbo ambazo huwa na maudhui ya kimapenzi. Huelezwa kwa maneno matamu yenye hisia nzito nzito. Huenda ukaimbwa na mtu kumsifu mpenziwe, kuomba msamaha au hata kuomba uchumba.
(h) Kimai
Ni nyimbo zinazoimbwa katika shughuli mbalimbali za baharini. Hizi hujumuisha nyimbo za mabaharia, wavuvi na wasafiri wa vyombo vyombo vya baharini. Nyimbo hizi hazina idadi kamili ya vina na mizani na pia swala la vina na mizani si lazima.
(i) Tumbuizo
Tumbuizo ni nyimbo ambazo huimbwa ili kuwafurahisha watu katika sherehe mbalimbali kama vile kwenye ngoma au kwenye harusi. Husifia wahusika wakuu katika sherehe husika. Huweza kuwa na sehemu zinazorudiwarudiwa.
(j) Nyimbo za migomo
Huimbwa na watu wanapoandamana na hukashifu serikali au shirika kwa
kutoshughulikia haki za wafanyikazi. Aidha, huwasifu viongozi wa wafanyikazi au kundi fulani. Nyimbo za migomo hunuiwa kuwashinikiza viongozi kuyatatua matatizo ya wagomaji.
(k) Nyimbo za vita
Hizi ni nyimbo zinazoimbwa au kuimbiwa watu wanaokwenda vitani kuwapa hamasa na moyo wa kuitetea hadhi na heshima ya taifa lao kwa matu mizi ya silaha.
(l) Hodiya / chapuzo
Hizi ni nyimbo ambazo huhusishwa na kazi kama vile kutwanga nafaka,
kufua nguo, kuvuna, kupalilia, kuinua gogo na kadhalika. Huimbwa wakati watu wanapofanya kazi. Huimbwa na kundi la wafanyikazi au mtu mmoja wakati anapofanya kazi.
(m) Nyimbo za harusi
Nyimbo hizi huimbwa katika sherehe za harusi, kuwatakia mema maharusi katika uhusiano wao wa kindoa zinazoimbwa kumsifu Mtume Muhammad zinazoimbwa katika Maulidi.
(n) Jadiiya
Hizi ni nyimbo za kitamaduni ambazo zinaimbwa na kupokezwa kwa mdomo kutoka kizazi kimoja hadi kingine. Nyimbo hizi husimulia mambo mengi hasa yaliyotukia katika historia ya jamii fulani kama vile majanga, ucheshi.
(o) Kijapuzi
Ni wimbo unaoambatana na hadithi.
(p) Kongozi
Nyimbo za kuaga mwaka mkongwe na kualika mwaka mpya hususa katika jamii ya Waswahili.
(q) Wimbo wa taifa
Ni wimbo unaotambulisha taifa fulani. Nyimbo hizi huimbwa na watu wa taifa moja kuonyesha mapenzi yao na uzalendo kwa nchi yao.
® Vave / wawe
Ni nyimbo zinzoimbwa na wakulima wakiwa katika shughuli za kilimo (kufyeka, kulima, kupalilia, kupanda mbegu, kukata magugu, kuteketeza moto na kadhalika) Baadhi ya wawe huwa na mtu anayewaongoza wengine katika uimbaji.
(s) Taarabu
Muziki wa mahadhi yenye asili ya mwambao wa Afrika Mashariki unaotumia ala za Mchanganyiko wa Kiarabu, Kihindi na Kizungu.
(t) Nyimbo za uwindaji
Huimbwa na wawindaji wakiwa katika usasi.
(u) Nyimbo za kidini
Nyimbo hizi huimbwa maabadini wakati wa ibada za sala / swala.
(v) Nyimbo za siku ya kuzaliwa
Nyimbo za aina hii huimbwa kuadhimisha ukumbusho wa siku ya kuzaliwa.
(w) Nyimbo za kishujaa
Huimbwa kusherehekea ushindi wa tukio fulani kama vita au kupata uhuru.
(2) Maghani
Maghani hutumiwa kuelezea ushairi ambao hutolewa kwa kalima, yaani kwa njia ya maneno badala ya kuimbwa au kughaniwa kama mengineyo. Sauti ya juu au ya chini katika neno hutilia uzito maana ya anayeghani. Kimsingi,huu ni ukariri wa nusu kusemwa na nusu kuimbwa. Kuna aina mbili kuu za maghani: - maghani ya kawaida
- maghani ya masimulizi (maghani simulizi)
(a) Maghani ya kawaida
Hutumiwa kuelezea aina ya tungo ambazo hupatikana katika fasihi simulizi na ambazo hugusia maswala mbalimbali kama mapenzi, siasa, harusi, dini, kazi na maombolezo. Mashairi yanayogusia maswala haya yanapoghaniwa (kukaririwa kwa kalima) basi huwa maghani ya kawaida. Maghani ya kawaida ni pamoja na kivugo /majigambo, tondozi na pembezi / pembejezi.
(b) Maghani simulizi
Haya ni maghani ambayo husimulia hadithi, tukio, kisa au historia. Usimulizi unaohusika hapa unaweza kuambatanishwa na muziki wa ala kama zeze, njuga, marimba au hata ngoma. Maghani ya aina hii hupatikana katika jamii nyingi Afrika na uhusishwa na wasimulizi ambao hujulikana kama yeli au manju. Mifano ya simulizi ni rara, tendi / utenzi, ngano.
Sifa za maghani - Maghani ni tungo za kishairi, kwa hivyo zina mapigo ya kimuziki au maneno mateule yenye muwala.
- Huwa katika umbo la shairi.
- Huzungumzia mashujaa na ushujaa.
- Muundo huwa na utaratibu fulani.
- Hueleza mambo ya kiutenzi.
- Tamathali za usemi hutumika kwa wingi kujenga taswira.
- Huweza kutolewa na mtu mmoja au kundi la watu.
- Hutungwa papo hapo na kutongolewa mbele ya watazamaji / hadhira.
- Hutumia tamathali za usemi kwa wingi.
Dhima ya maghani - Huwatukuza mashujaa
- Hutumiwa kukejeli au kukashifu sifa mbaya katika jamii.
- Kufurahia fanaka ya watu binafsi na jamii kwa jumla.
- Hutumiwa kueleza sifa maalumu za mashujaa.
- Hukuza uhusiano bora miongoni mwa wanaojigambia wenzao.
Kipera cha maghani kinaweza kuainishwa katika vijipera vifuatavyo:
(i) Kivugo/ majigambo
Haya ni mashairi yanayohusu majisifu ambayo hutungwa na mtu anayehusika. Hutungwa kwa namna ambavyo hujenga taswira ama picha ya anayehusika kwa hadhira yaje kwa kuonyesha ubingwa wake katika jambo fulani kama vile vita, masomoni, michezoni, ucheshi na kadhalika.
Majigambo huwa ni ya papo hapo na huelekezewa wale wanaomjua na kumtambua anayejisifuna hivyo huwa vigumu kwa wale wasiomjua kuelewa. Katika jigambo hilo anaweza kujieleza jina lake, ukoo wake na lakabu zake.
(ii) Tondozi
Haya ni maghani ambayo huwasifu watu, wanyama au vitu. Tondozi inaweza Kumsifu mtu kwa mambo kama umbo, kimo, tabia, sura, wema, na kadhalika. Pia mnyama wa mwitu anaweza kusifiwa kwa ukubwa wake, ujasiri, ukali kama ambavyo mti unaweza kusifiwa kwa umbo ama manufaa yake. Msingi hapa ni kuwa kinachosifiwa kinapewa sifa fulani. Lugha ya kuvutia na yenye kuvuta taswira hutumika katika tondozi.
(iii) Pembezi / pembejezi
Hizi ni tungo za kusifu kama zilivyo tondozi. Pembezi hutumiwa kuwasifu watu mashuhuri ambao wametenda matendo maarufu kama ya ushujaa, uongozi namaendeleo ya jamii husika.Watu hawa husifika pia kutokana na nafasi au nyadhifa walizonazo katika jamii.
(iv) Simango
Ni maghani ambayo dhima yake kuu ni kumsimanga mtu fulani juu ya mambo aliyoyafanya au anayoaminiwa kuyafanya na sifa alizonazo mtu au anazoaminika kuwa nazo. Kwa kawaida, anayosimangiwa mtu huwa ni mambo mabaya na hayakubaliki katika jamii ya binadamu.
(v) Tendi /utenzi
Tendi ni tungo ambazo hutumiwa kusimulia matukio ya kihistoria yanayohusishwa na watu maarufu katika jamii. Mara nyingi wahusika wa tendi huwa mashujaa au majagina wanaodhaniwa waliishi katika jamii na walifanya matendo ya kijasiri. Tungo hizo huyaeleza maisha ya mashujaa hao kuanzia kuzaliwa hadi kufa kwao. Wahusika wanaopatikana katika tendi huwa na sifa zinazokiuka uwezo wa binadamu wa kawaida. Huwa na sifa zinazofanana na mashujaa wa mighani.
(vi) Rara
Rara ni hadithi fupi na nyepesi za kishairi zinazosimulia tukio la kuvutia.Tukio hilolaweza kuwa la kweli kama sherehe za uhuru au liwe tukio la kubuni tu. Rara hutongolewa ukiandamanishwa na ala za muziki.
(vii) Rara nafsi
Huu ni ushairi wa kinafsi ambao hutungwa na mtu kuelezea hisia, matatizo na fikra zake mwenyewe kama vile kuhusu mapenzi, usaliti, talaka, kifo. Rara nafsi huwasilishwa kwa njia ya uimbaji unaoandamana na ala za muziki.
(viii) Ngano
Hizi ni tungo ambazo hutokea katika muktadha wa utambaji wa ngano lakini huwa pia zinaandamana na ala za muziki kama marimba, njuga na mengineyo.
(3) Ngonjera
Ngonjera ni tungo za kishairi ambazo huwa na muundo wa kitamthilia. Mazungumzo katika ngonjera ni kulumbiana au kujibizana. Mhusika mmoja husema au huuliza jambo na mhusika mwingine hujibu au kuendeleza mazungumzo. Mazungumzo yanaweza kuwa baina ya watu wawili au zaidi. Ngonjera huanza na fikra kinzano yakiwa na azma ya kutatua utata fulani kuhusu jambo fulani. Suluhisho la utata huo hupatikana hatimaye mwishoni mwa ngonjera.
|
|
|
SHAIRI : NANI KAMA MWALIMU ? |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 09:06 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
NI NANI KAMA MWALIMU
————————————
Naja nikiwakumbusha kuipitia nudhumu,
anayejenga maisha, laazizi maalimu,
yule alotufundisha, kwanza kushika kalamu,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Nalola siku ya kwanza, nikipelekwa shuleni,
na wakati nilianza, kuingia darasani,
mwalimu alinifunza, ‘lufabeti kwa makini,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Sana nilizikariri, herufi alonifunda,
tena nikiwa mahiri, wa nyimboze nilopenda,
hadi leo ninakiri, nafaidi ye matunda,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Nakumbuka nikianza, kuandika mchangani,
kalamu yangu ya kwanza, ni kijiti wajameni,
Huyo aliyenifunza, mgee kheri Manani,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Nakumbuka kuhesabu, tangu moja hadi kenda,
wakati ‘likuwa tabu, ikiwa inanishinda,
chonde chonde taratibu, mlezi akanifunda,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Leo miye mhasibu, taasisi ya takwimu,
mdogo wangu tabibu, jijini Darisalamu,
si kwa bahati nasibu, ni matunda ya mwalimu,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Wanoitwa wata’lamu, wa’zo maridhawa fani,
alowafunda mwalimu, leo wakuu nchini,
mlezi wangu mwalimu, sana ninakuthamini,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Kumbukeni ni mwalimu, wa mataifa mlezi,
alowagea elimu, wa dunia welekezi,
kiongozi ufahamu, yoyote uliyo ngazi,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Na wasifa wake jama, haumaliziki wala,
ndefu ja hadithi kama, alufu lela ulela,
namuombea salama, nipulike wangu Mola,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
Subukhana shukurani, beti kumi kutimia,
yaliyokuwa moyoni, hadhira nimepatia,
na baraka maishani, walezi n’kiwatakia,
NI NANI KAMA MWALIMU, HUSUSAN WA MSINGI?
***********************
Rwaka Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda).
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,RWANDA.
|
|
|
SHAIRI : KAMA MNATAKA MALI |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 09:00 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
1. Karudi baba mmoja,
toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja,
na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja,
ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafae maishani.
2. Akatamka mgonjwa,
ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa,
haitoki homa kali,
Roho naona yachinjwa,
kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini,
kiwafae maishani.
3. Yakawatoka kinywani,
maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani,
sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani,
mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali,
itufae maishani
4. Baba aliye kufani,
akajibu lile swali,
Ninakufa maskini,
baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni,
kama mnataka mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
5. Wakazidi kumchimba,
baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba,
hatujui fumbo hili,
akili zetu nyembamba,
hazijajua methali,
Kama tunataka mali,
tutapataje shambani?
6. Kwanza shirikianeni,
nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani,
mwisho mtapata mali,
haya sasa buriani,
kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
7. Alipokwisha kutaja,
fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja,
roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
8. Fumbo wakatafakari,
watoto wale wawili,
wakakata na shauri,
baada ya siku mbili,
wote wakawa tayari,
pori nene kukabili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
9. Wakazipanda shambani,
mbegu nyingi mbalimbali,
tangu zile za mibuni,
hadi zitupazo wali,
na mvua ikaja chini,
wakaona na dalili,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
10. Shamba wakapalilia,
bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia,
wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia,
wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
11. Wakanunua na ng’ombe,
majike kwa mafahali,
wakapata na vikombe,
mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe,
sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali,
mtayapata shambani.
12. Wakaongeza mazao,
na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao,
wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao,
wakaandika kauli…
“KAMA MNATAKA MALI
MTAIPATA SHAMBANI”.
Miaka hiyo tuliimba tu kama kujifurahisha wala hatukujua maana yake, leo twatambua nini maana yake, nasisitiza, kama mnataka mali mtaipata shambani
|
|
|
USHAIRI NI NINI? |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 08:51 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
USHAIRI NI NINI?
Hadi hapa tumekwishakuona kuwa ushairi wa Kiswahili si sanaa ya vina kama Shaaban Robert alivyotuambia; na wala vina na urari wa mizani siyo roho au uti wa mgongo wa ushairi wa Kiswahili kama Abdilatif, Mayoka na wanajadi wengine wanavyohubiri. Kwa hakika, mojawapo ya sababu ya wanajadi kuamini kuwa shairi lazima liwe na umbo maalum, na kuwa umbo hilo lazima litawaliwe na vina na urari wa mizani, ni kuwa dhana yao ya ushairi imetawaliwa na utaratibu wa kimaandishi. Hebu tulidadisi jambo hili zaidi.
Ni rahisi kuthibitisha kuwa umbo la shairi la vina na mizani ni la kimaandishi, kwani karibu watu wote hapa kwetu hulitambua shairi kama linavyoonekana kwenye ukurasa wa karatasi (uwe ukurasa wa Uhuru, au wa Mzalendo au wa diwani yoyote ya mashairi). Kwa mujibu wa mtazamo huu, insha ni insha kwa vile huonekana imeandikwa kwa njia ya mjazo; na shairi ni shairi kwa vile laonekana lina vina na urari wa mizani. Hebu tuangalie andiko hili hapa chini:
Pasipo na mwanamke dunia ingekuwaje?
Mwanamme peke yake sijui angeishije! Maisha yetu ya kwanza yangekosa msaada; ya kati yakawa giza kwa furaha kuwa shida; na ya mwisho yangekuwa ni ghali kwa pesa moja: ingekuwa si dunia kwa uchache wa faraja.
Andiko hili lililoandikwa kwa njia ya mjazo, bila shaka laonekana kuwa nathari. Lakini andiko hilo hilo tukigeuza umbo lake, “dhana” ya watu wengi juu ya hulka yake itageuka pia:
Pasipo na mwanamke dunia ingekuwaje?
Mwanamme peke yake sijui angeishije!
Maisha yetu ya kwanza yangekosa msaada;
Ya kati yakawa giza kwa furaha kuwa shida;
Na ya mwisho yangekuwa ni ghali kwa pesa moja:
Ingekuwa si dunia kwa uchache wa faraja.
Umbo hilo haliwakanganyi watu wengi: waliangaliapo mara moja hurukia kusema kuwa ni shairi, na wakiulizwa kwa nini hujibu kuwa andiko lina vina, urari wa mizani, n.k.
Tuchukue andiko jingine lifuatalo:
Wakadha namshukuru Mungu
Kwa ajili ya sahibu yangu
Mtunzi na kungwi wa mizungu
Mathias Mnyampala
Mfadhili na mwenye jamala
Mashuhuri kwa mashairi ya muwala
Na uandishi wa makala
Ambaye ameniomba niandike hii dibaji
Asaa iwafariji wasomaji
Ambao sanaa hii wanaitaraji
Niwabainishie yaliyo muhimu
Kuhusu Kiswahili na utungaji
Na kubatilisha riwaya za mafukala.
Katika andiko hili tunaona upatanifu wa aina fulani wa vina vya ‘ngu’, ‘la’, na ‘ji’, ni ‘mu’ tu ambayo haina kina chenziye. Na si ajabu wapo watu ambao wanaweza kuliita andiko hili ubeti wa shairi lenye dosari au guni, kwa sababu wameona upatanifu fulani katika umbo lake. Kumbe andiko lenyewe katika uasili wake lilikuwa katika umbo la mjazo kama ifuatavyo:
Wakadha namshukuru Mungu kwa ajili ya sahibu yangu, mtunzi na kungwi wa mizungu, Mathias Mnyampala, mfadhili na mwenye jamala, mashuhuri kwa mashairi ya muwala na uandishi wa makala, ambaye aliniomba niandike hii dibaji asaa iwafariji wasomaji ambao sanaa hii wanaitaraji, niwabainishie yaliyo muhimu kuhusu Kiswahili na utungaji, na kubatilisha riwaya za mafukala.
Kutokana na hayo yaliyokwishasemwa, tunaona kuwa “ana ya ushairi” ya wanajadi imefinywa kwenye “umbo maalum lenye utaratibu wa vina na urari wa mizani”, ambayo kwa kweli ni dhana ya kimaandishi. Na nathari kwao ni andiko lolote ambalo halina utaratibu huo. Wanayaangalia matumizi ya lugha katika tabaka mbili zisizoingiliana: matumizi ya kishairi na yale ya kinathari. Mtazamo huu kuhusu lugha umepotoka sana, na hapo baadaye tutaonyesha upotofu wake. Kwa sasa inafaa tulikabili suala la ushairi ni nini.
Iwapo “umbo” lionekanalo kwenye karatasi haliwezi kutiwa maanami katika ufafanuzi wowote thabiti wa ushairi, basi ushairi ni nini? J.A. Ramadhani, katika makala yake juu ya ushairi, ameeleza kwa urefu na kwa undani maana na sifa za ushairi. Mambo mengi muhimu ameyataja.
Anatuambia kwamba:
(1) Ushairi huanza na hisi au mchomo unaosababishwa na mazingira;
(2) Hisi hizo huwasilishwa kwa msomaji kwa njia ya lugha teule ya kitamathali;
(3) Hisi hizo lazima ziambatane na mawazo na mtazamo wa fikira;
(4) Hali ya kishairi inahusiana kidogo na hali ya kindoto au tabia ya kuona yasiyoonekana na kuwania yasiyowezekana;
(5) Ushairi umefungamana na ubuni, na kwa hiyo hauwezi kuwekewa sheria zisizobadilika, na kwamba kuogopa kubuni kunadumaza maendeleo ya ushairi wa Kiswahili;
(6) Uwezo wa kubuni wa mshairi umetoka kwa Mungu ambaye ndiye mfalme wa sanaa zote.
(7) Shairi ni muungano wa fani na yaliyomo (maudhui).
Kimsingi, ufafanuzi huo wa ushairi hautofautiani sana na ufafanuzi alioutoa Kezilahabi. Anatuambia kwamba:
Ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno fasaha yenye mizani kwa ufupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha.
Fafanuzi hizi mbili zinarekebisha ile fikira ya wanajadi kwamba ushairi lazima uwe na urari wa mizani na vina. Hata hivyo, fafanuzi hizi zina upungufu wake.
Upungufu wa maelezo ya Ramadhan umo hasa katika imani yake kuwa uwezo wa kishairi unatoka kwa Mungu.
Hapa sipo mahali pa kujadili imani ya kidini ya Ramadhan juu ya uwezo wa kishairi; suala hili ni kubwa na pengine linahitaji makala ya pekee. Inatosha tu tukisema kuwa ni kawaida ya falsafa za kidhanifu kumuweka Mungu kuwa chimbuko la mema aliyo nayo mtu; na kumuweka shetani kuwa chimbuko la mabaya yote. Upungufu wa kauli ya Kezilahabi hasa umo katika fungu la maneno “ukweli fulani wa maisha”. Je, ni kweli kuwa ushairi lazima ueleze ukweli fulani wa maisha, na siyo uongo? Hali halisi inatueleza kuwa wapo washairi wasemao ukweli fulani kuhusu maisha, na wapo wengine wasemao uwongo, na pia mshairi mmoja anaweza kusema ukweli katika shairi moja na uwongo katika shairi jingine. Fikra hii ni potofa kama ile isemayo kuwa mshairi ni chemchemu ya hekima.
Jambo ambalo halikutiwa maanani katika fafanuzi hizo linahusu dhima ya fasihi na ushairi kama vyombo vya kuburudisha na kustarehesha watu. Ushairi hauelezi mawazo tu kama kemia au fizikia. Ushairi lazima uguse hisi, lazima umsisimue yule anayeusema, kuusoma au kuuimba na yule ausikilizae. Shairi lisilogusa hisi ni kavu na butu, na hata kama limesarifiwa katika vina na urari wa mizani, shairi hilo litaishia katika kuhibiri tu. Na fasihi ikisha hubiri mahubiri makavumakavu kama kasisi mimbarini, bila mvuto wowote wa kifasihi, itakuwa imeshindwa kugusa pale ambapo inapaswa kugusa – hisi za watu. Kwa hiyo basi ufafanuzi thabiti wa ushairi lazima uzingatie uwezo wake wa kugusa hisi za watu.
Kutokana na hayo tuliyokwisha sema, tunaweza kutoa ufafanuzi wa ushairi ambao unazingatia yale yaliyokwisha semwa na hao hapo jua, pamoja na dhima ya ushairi ya kugusa moso au hisi. Nao ni huu: Ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalum wa maneno fasaha na yenye muwala, kwa lugha ya mkato, picha au sitiari au ishara, katika usemi, maandishi, au mahadhi ya wimbo, ili kueleza wazo au mawazo, kufunza au kueleza tukio au hisi fulani, kuhusu maisha au mazingira ya binadamu, kwa njia inayogusa moyo. Hapa lazima tuseme kuwa, ingawa ushairi wa aina yoyote unaweza kuimbwa, lakini siyo kila kiimbwacho kitaitwa ushairi.
Ushairi ni sanaa ya lugha, na usanaa wake uko katika “mpangilio maalum wa maneno fasaha yenye muwala, kwa lugha ya mkato… kwa njia ya kugusa moyo”, siyo katika uimbaji, unaweza kuuongezea (au hata kuupunguzia!) mguso.
Kwa mujibu wa maelezo haya, uimbaji wa hesabu au aya kutoka kwenye kitabu cha siasa si ushairi.
Ufafanuzi huo wa ushairi unazingatia halka ya ushairi usiofuata urari wa vina na mizani na ule unaofuata urari huo; ule ulio katika fasihi simulizi na ule ulio katika fasihi andishi.
Jambo moja linalojitokeza ni kuwa ushairi ni lugha katika hali ya matumizi maalum; na matumizi maalum haya ni matumizi ya kisanaa ya vipengele vya lugha. Hapa chini tutajadili kwa ufupi baadhi ya vipengele muhimu vinavyoupambanua ushairi.
VIPENGELE VYA USHAIRI
Washairi wa jadi wanadai kuwa “vina na mizani ndio uti wa mgongo wa ushairi.” Dai hili ni batili kifasihi, kwani linageuza kipengele kimoja kidogo cha kisanaa kuwa ndicho msingi wa sanaa yenyewe.
John Ramadhani amezieleza sifa za ushairi kwa urefu na vizuri zaidi. Yeye ametaja mambo yafuatayo yaliyo mahimu:
1) Katika ushairi vitu hupewa nafsi na utu;
2) Picha ni sifa muhimu ya ushairi;
3) Ushairi huweza kuwa na mpangilio wa maneno usio wa kawaida;
4) Ushairi una ridhimu, mlingano wa sauti na mapigo;
5) Shairi ni lazima lionyeshe sifa ya kiumbaji, lisiwe ni nakala ya shairi jingine.
Yote haya ni sawa, ila sisi tutajaribu kuyafafanua zaidi na kuongezea sifa zingine ambazo hazikutajwa. Suala hili tutalijadili kwa kufuata vichwa hivi:
1) Mpangilio wa maneno
2) Picha
3) Tamathali za usemi
4) Takriri na ridhimu
5) Hisia za kishairi
6) Fani na maudhui
Mpangilio wa maneno
Watu wengi wameichukulia kuwa kweli isiyopingika kuwa mpangilio wa maneno (mfuatano wa vipashio vya sentensi) katika ushairi ni tofauti na ule ulio katika nathari. Mpangilio wa maneno hufuata kanuni za miundo inayowezekana katika lugha fulani. Tukichukua Kiswahili, kwa mfano, sentensi iliyozoewa sana ni ile yenye muundo huu:
Kiima – Kitenzi – changizo…
Nomino – kimilikishi – kitenzi – kielezi…
Katika Kiswahili tunaweza kusema:
Baba hujua kulima
Mama hujua kusaga
Mimi sijui chochote
Baba yangu anajua kulima kwa plau
Hii ni miundo ya kawaida ambayo imezoewa sana na wasemaji wa Kiswahili. Lakini, mzungumzaji anaweza kuipangua miundo hiyo, na kutumia miundo isiyo ya kawaida sana, kwa madhumuni ya kuleta msisitizo wa jambo fulani:
Kulima baba hujua
Kusaga mama hujua
Chochote mimi sijui…
Jambo la kusisitiza hapa ni kuwa mtu yeyote, mradi awe ni mzungumzaji wa lugha fulani, anaweza kutunga muundo wa kawaida au usio wa kawaida sana (pengine bila yeye kujua).
Mzungumza lugha anao uhuru wa kutamba katika uwanja wa lugha yake ili aweze kueleza hisia na mawazo yake. Jinsi atakavyopanga maneno katika sentensi itategemea ujuzi na ustadi na uzoefu wake katika jambo hili. Je, mshairi anautumiaje uhuru huu wa kutunga miundo iliyo ya kawaida sana, na ile isiyo ya kawaida sana?
Jambo la kusisitiza hapa ni kuwa mshairi si mtu wa pekee katika ujuzi wa lugha aitumiayo kutungia mashairi yake.
Jambo tuwezalo kulisema pasipo wasiwasi wowote kuhusu tofauti baina ya mshairi na mtu wa kawaida ni hili: mshairi anao uzoefu katika kutunga mashairi, lakini mtu wa kawaida hana uzoefu huo. Uzoefu huu katika sanaa hii humwezesha mshairi kuitumia miundo ya lugha hiyo kutimilizia malengo yake ya kishairi. Uhuru wa mshairi wa kuchagua muundo fulani na kuacha muundo mwingine, kupanga vipengele fulani kwa njia fulani na kuacha kuvipanga kwa njia nyingine, ni uhuru unaotawaliwa na kanuni za sanaa yake, uwezo wake wa kuvipanga vipengele hivyo ili vilete athari iliyokusudiwa hutegemea uzoefu wake, ubingwa wake, na hali aliyo nayo wakati wa kutunga shairi lake.
Katika ushairi wa Kiswahili, mbinu ya upangaji wa vipengele vya sentensi kwa njia isiyo ya kawaida hutumika sana. Utakuta washairi wanasema: mzuri msichana, wangu mke, n.k. badala ya msichana mzuri, mke wangu. Miundo mingine ni kama ile tuliyoitoa mfano hapo juu (kulima baba ajua n.k.).
Ipo miundo mingine isiyotumika sana katika mazungumzo ya kawaida inayotumiwa na washairi. Mpangilio huu usio wa kawaida huvuta udadisi kuliko ligha ya kawaida, na hutumika katika kusisitiza vipengele fulani vya hisi au wazo la mshairi.
Lakini shairi siyo lazima liwe na mpangilio wa maneno usio wa kawaida ili lipendeze. Shairi linaweza kuwa na mpangilio wa kawaida tu, na athari ya mguso ikaletwa na vipengele vingine kama vile picha, takriri, n.k. Kwa hiyo, ingawa mpangilio tulioujadili unaweza kuwa alama mojawapo ya ushairi, lakini si lazima kila shairi lithibiti mpangilio huo.
Picha
Picha ni matumizi ya lugha yanayopambanuliwa na utenzi mzuri wa maneno, uangalifu na udhahiri wa maelezo wenye kuhusisha na kujumuisha dhana mbali mbali tofauti ndani ya dhana moja ili kuleta taswira na athari maalum katika mawazo ya msomaji (au msikilizaji). Kezilahabi ameeleza kuwa athari hiyo aipatayo msomaji au msikilizaji wa ushairi inaweza kuwa ni ya aina ya vionjo vyenye kuhusiana na milango ya fahamu ya kusikia, kuona, kunusa na kugusa. Kwa hiyo, kwa kutumia picha, mwandishi anaweza kumfanya msomaji wake asisimke, aogope, afurahike, avutike, akirihishwe, alie, anyamae au aghadhabike kwa kuathiriwa na picha zilizoteuliwa na kusanifiwa kwa ufundi. Ugumu wa kutunga mashairi ya mtiririko uko katika utenzi na upangaji wa picha na tamathali za usemi zenye kuoana na maudhui yaliyokusudiwa zisizotengua ridhimu ya shairi na zisizofanya lugha ya shairi ipoteze uasili wake. Wakati huo huo, shairi hili liwe na uwezo wa kindanindani wa kuvutia na kudumisha hamu ya msomaji au msikilizaji hadi mwisho. Katika ushairi wa fasihi-simulizi, hamu ya hadhira hudumishwa na uteuzi wa maneno, muziki (kama ala za muziki zinatumika), mazingira au sherehe inayoambatana na tungo hiyo, ushirikishaji wa hadhira kwa kutumia kibwagizo, makofi na vipengele vingine, na umuhimu wa kijamii au kihistoria wa yale yanayoelezwa.
Katika ushairi-andishi wenye vina na mizani, hamu ya msomaji zaidi hudumishwa na ulinganifu wake wa ridhimu na sauti unaotokana na vina na urari wa mizani. Mapigo ya shairi la aina hiyo hufuata mgawanyo wake katika vipande vyenye mizani sawa na shairi husomeka upesi upesi bila kuitumikisha sana akili ya msomaji. Kifani, vina na urari wa mizani katika ushairi-andishi hufanyakazi ya ala za muziki katika ushairi-simulizi.
Ushairi wa mtiririko ni wa kiwango cha juu zaidi kwa sababu unakataa kupata uhai wake kutokana na mbwembwe za kijuujuu, mambo ya nje ambayo ni nyongeza muhimu juu ya ushairi, lakini si lazima yawe sehemu ya ushairi: vina na urari wa mizani. Ushairi huo unapata uhai wake na utamu wake kutokana na mfumo wake wa ndani ambao ni fungamano la matumizi mahususi ya lugha nzito, hisia nzito na maudhui ya kishairi. Mashairi haya yanamlazimisha msomaji atumie akili zaidi, ajihusishe zaidi kijaziba katika hisia za mtunzi, na atafakari zaidi, badala ya kumkokota kikuku kwa utamu wa kijuujuu wa muziki wa vina na urari wa mizani. Mtiririko ni mashairi yaliyokusudiwa yasomwe na watu wazima, mengi hayafai kusomwa na watoto wa shule za msingi kwa sababu uwezo wao wa kuichambua fasihi bado ni mdogo. Hivyo hapana shaka kuwa kwa miaka mingi ijayo mashairi yenye vina na mizani yataendelea kupendwa zaidi na watoto wadogo, mradi lugha yake isiwe ngumu sana. Kwa ajili ya adhira hiyo, mashairi ya aina hiyo ni lazima na bora yaendelee kutungwa. Bali kwa ajili ya watu wazima waliofikia kiwango fulani cha ufahamu wa fasihi, mashairi ya aina hiyo si lazima, ingawa si mwiko kuyatunga. Kila mshairi apewe uhuru wa kutumia fani inayofungamana vizuri zaidi na maudhui yake, uwezo wake, na pia hadhira aliyokusudia.
Ingawa matumizi ya lugha huweza kuzindua hisi na maono fulani katika akili ya msomaji juu ya kile kinachozungumziwa, lakini ni muhimu kukumbuka kuwa uhusiano huo unaozinduliwa kati ya picha ya mawazoni na kitu halisi kinachozungumziwa (kinachochorwa) ni wa kinadharia, si wa kimaumbile au wa moja kwa moja. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya maana au umbile la kitu na uwakilishaji wa kitu hicho katika lugha – katika neno mofimu na fonimu. Kifasihi uhusiano tuupatao tunapotumia picha ni ule unaoumbwa na akili ya msomaji mwenyewe inapozinduliwa na ustadi wa mshairi wa matumizi ya lugha na kunga nyingine za ushairi. Usanifu wa mashairi humfanya msomaji wake awe msanifu vile vile; mshairi hudokeza, msomaji hukamilisha; mshairi huumba, msomaji humalizia na kuhusisha kile kilichoumbwa na hali halisi anayoijua. Kwa hiyo msomaji wa mashairi si mpokeaji tu wa sanaa hiyo bali ni mpokeaji msanii vile vile.
Hebu tuutazame mfano ufuatao unaotoka katika shairi la Shaaban Robert, “Mtu na Malaika”.
Mtu Na Malaika
Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho,
Wa huku hafiki huko, wala halina malisho.
Halishibishi huchosha, njiaye ina uchovu,
Na tabu isiyokwisha, wala hupati utuvu.
Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka,
Na milima akapanda, apendako akafika.
Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
Na mitoni akavuka, hata alikonuia.
Na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dirani,
Hupati kupanda bara, na hushuki baharini.
Tazama mashaka gani, njia ya dira si njia.
Katika dondoo hii tunapewa picha tatu mahsusi. Picha ya kwanza ni neno linalozunguka… Mshairi anatuambia kuwa neno ambalo halifuati njia iliyonyooka ‘neno lenye mzunguko” halifikii mwisho wake na halileti mradi uliokusudiwa “halina malisho”. Hapa neno limefanywa kuwa kitu chenye uwezo wa kutembea, kuzunguka. Athari ya neno hilo kwa anayehusika ni kwamba halileti shibe wala utulivu, linachosha: “Halishibishi huchosha”. Hapa tunapewa picha ya shibe, neno linapewa uwezo wa chakula – kitu yakini kinachoshikika na kinacholiwa. Bali mtu hatosheki na “chakula hicho” hatatui matatizo yake iwapo njia anayotumia ni ya mzunguko, ya kulegalega, ya ugeugeu na woga.
Picha ya pili tunayopewa ni ya mtu aendaye safari ngumu kwa ujasiri na moyo na dhati, akipanda milima na kushuka mabonde, akipenya misitu na kuvuka mito, hadi kufika kule anakokwenda. Huyu ni mtu asiyeogopa matatizo, anayeshikilia njia ngumu lakini nyoofu, alimradi anajua kuwa itamfikisha kwenye lengo lake. Ni mtu anayepambana na matatizo badala ya kuyakimbia. Mtu wa aina hii ndiye hupata mafanikio. “Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka”.
Picha ya tatu tunayopewa ni dira. Dira ni chombo kitumiwacho na mabaharia na wasafiri wengine kusahihisha majira yao ili wasipotee njia. Dira ni chombo cha mviringo na mshale wake aghalabu huzungukia pale pale ulipo, katu hautoki nje ya dira. Picha hii inasisitiza wazo la mwandishi kuwa njia yenye kuzunguka haiwezi kumfikisha mtu kwenye lengo lake. Mshale wa dira huzunguka daima lakini haufiki kokote.
Picha hizi tatu kwa pamoja zinafaulu kutupa ujumbe wa mwandishi kuhusu maisha na namna ya kuyakabili: tuyakabili kwa juhudi na ujasiri na nia. Tuamue jambo na tulifanye bila kutetereka. Tusiogope vikwazo wala matatizo.
Maisha ni mapambano.
Kwa kutumia picha hizi tatu, mwandishi kafaulu kufikisha kwetu ujumbe wake wa kishairi. Maudhui yake ni ya kishairi, yanapatikana kwa kuzichambua na kuzifafanua picha alizozitumia. (Shairi hili lingeweza vile vile kufasiriwa kidini kama alivyofanya J. Ramadhani katika makala yake “Ustadi wa Shaaban Robert Mshairi” Mulika No. 7, uk. 46-48)
Mpangilio wa lugha
Katika dondoo tulilolichunguza picha imejitokeza kwa njia ya sitiari (kitu kimoja kuwa badala ya kitu kingine kilicho tofauti: k.m. “msitu” badala ya “matatizo”, “dira” badala ya “tabia ya kukwepa matatizo” n.k.) na mpangilio wa lugha na mawazo. Dhana tatu zinazotofautiana – neno linalozunguka mtu anayesafiri kupitia msituni na baharini, n.k. na dira inayozungukia mahali pale pale ilipo zinaleta wazo moja mahsusi. Zote zimechangamana ili kujenga dhana moja.
Umoja wa wazo linalozungumziwa unaimarishwa pia na mfungamano wa ubeti mzima – pana mfululizo wa fikra na hisi tangu mstari wa kwanza hadi wa mwisho, kifungu kizima ni ubeti mmoja, hakuna mgawanyo wa beti za mistari miwili miwili au minne minne. Wazo linafululiza bila kusita au kukatishwa hadi mwisho kama vile ambavyo maudhui ya shairi lenyewe yanavyotuhimiza kufululiza katika njia moja bila kutetereka hadi mwisho. Muundo wa shairi umeoana na maudhui yake.
Mpangilio wa lugha – herufi, silabi, mofimu hadi maneno na sentensi ni sharti uoane na maudhui. Washairi hutumia kunga mbali mbali za kisauti na kimpangilio ili kuleta hisia fulani. Baadhi ya kunga hizo ni onomatopea, mizani, vina, asonansi (mlingano wa sauti za irabu), konsonansi (mlingano wa sauti za konsonanti) takriri-konsonanti (marudio ya konsonanti) takriri-vina, n.k. Vipengele vyote hivi, isipokuwa onomatopea, ni aina ya takriri na tutavijadili chini ya mada ya takriri.
Onomatopea
Onomatopea ni mwigo wa sauti. Hii ni kunga inayotumiwa na washairi ili kutoa picha au dhana ya kile kinachowakilishwa au kupambanuliwa na sauti hizo. Kwa mfano tukisema:
“Maji yalimwagika mwa” neno mwa ni onomatopea, linawakilisha sauti au kishindo cha maji yanayomwagika. Baadhi ya onomatopea ambazo zimekwisha kuwa sehemu ya msamiati wa kawaida wa Kiswahili ni: pikipiki, bombom, mbwa, yowe, ngurumo, bunduki, gumia, kata, n.k.
Katika shairi lake la “Cheka kwa Furaha” Shaaban Robert ametumia onomatopea ili kuleta ile dhana ya kucheka:
Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha! ha! ndiyo ada duniani.
Basi cheka kwa! kwa! kwa! kwa! usafike moyo wako
Pamoja na malaika, wema mbinguni waliko;
Maneno yaliyoandikwa kwa italiki ni onomatopea, yanatoa
picha ya kusikika ya sauti ya mtu anayecheka. Huu ni
mpangilio maalum wa sauti ili kutoa picha ya kusikika ya
dhana inayozungumziwa.
TAMATHALI
Tamathali za usemi ni vifananisho au viwakilisho vya dhana fulani kwa dhana nyingine tofauti au zinazofanana. Ni usemi wenye kupanua, kupuuza au kubadilisha maana za dhahiri au za kawaida za maneno ili kuleta maana maalumu ya kishairi iliyokusudiwa na mtunzi. Tamathali nzuri hupanua, huyakinisha na huipa uhai na uhalisi zaidi dhana inayoelezwa, huburudisha na kuzindua akili ya msomaji au msikilizaji wa shairi, na huacha athari ya kudumu katika hisi na mawazo yake.
Tamathali zinazotumika zaidi katika ushairi ni tashbiha, meonymy, uhaishaji (personification) (Tashihisi) synecdoche, baalagha, kejeli na sitiari.
Tashbiha
Hi ni tamathali ya ufananisho au mlinganisho wa vitu viwili au zaidi. Katika tashbiha, kama ilivyo katika sitiari, huwa kuna vitu vitatu vinavyofananishwa ambavyo wataalamu wameviita kizungumzwa, kifananishi na kiungo. Kifananishi ndiyo usemi wenye kuzingatia maana-dhahnia, ni chombo kinachobeba mlinganisho. Kizungumzwa ndicho kitu halisi ambacho kinazungumziwa na kifananishi kwa mafumbo. Kiungo ni zile sifa ambazo zinapatikana katika kizungumziwa na kifananishi na hivyo kuhusisha vitu hivyo viwili. Katika tash- biha, kizungumzwa na kifananishi huhusishwa bila mafumbo kwa uwazi, moja kwa moja, kwa kutumia maneno fulani ya ulinganisho, km. “kama” “fanana na”, “mithali ya” n.k.
Katika tashbiha hakuna maana dhahnia, bali kuna ulinganishaji wa vitu viwili vilivyo bayana. Angalia mfano ufutao:
Kweli ni sawa na radi inapotoa kauli…
Kweli kinywani ikiwa sawa na Mto wa Nili
Kweli kama msumeno hukereza sawa kweli.
Katika dondoo hilo maneno yaliyochapwa kwa italiki yanaunganisha vitu viwili vinavyotofautiana na kuvifananisha. Mstari wa kwanza “kweli” inalinganishwa na radi, mstari wa pili inalinganishwa na “Mto Nili” na mstari wa tatu inalinganishwa na “msumeno”.
Tashihisi (uhaishaji)
Washairi mara nyingine huweza kukipa kitu kisichokuwa na uhai sifa za kitu chenye uhai, hasa za binadamu. Matumizi ya lugha kwa njia hiyo ndiyo huitwa uhaishaji au tashihisi.
Kisanaa maelezo ya kitashihisi huwa na upekee unaomwingia msomaji akilini haraka, kwani si jambo la kawaida, mathalan, kuona mti “ukimpungia mtu mkono” au nyumba “ikimkodolea macho” mgeni. Tashihisi, basi, ni aina ya sitiari na kisanaa kazi yake ni kama ile ya sitiari, japo kwa kiwango cha kidhahnia zaidi.
Mfano wa matumizi ya tashihisi:
Kimya hakineni jambo, si kimya chawatazama…
Kimya chaja zua mambo, pasiwe mwenye kusema…
Kimya kipimeni sana, msione kutosema
Kimya hakichi kunena, kitakapo kusimama
Kimya chaja watukana kizuwe yaliyozama…
Katika dondoo hili, “kimya” (ambayo ni nomino-dhahnia) kimepewa sifa za binadamu, kinaweza kunena, kutazama, kuzua mambo, kusimama nakutukana.
Katika shairi lake la “Fedha”, Shaaban Robert anaipa fedha sifa za binadamu:
Fedha huita wazuri,
Wakaitika labeka,
Wakenda bila hiari,
Mahali wasikotaka.
Mfano mzuri wa matumizi ya tashihisi kishairi tunauona katika shairi la Bwana Rajabu M. Kianda (Selukindo) liitwalo “Jembe”.
Jembe wangu nifariji, nami nikupe uzima,
Jembe wewe ndiye jaji, twakuenzi zote dhima,
Jembe wewe ni mpaji, wa baba na kina mama,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Jembe wewe msifika, utuonee huruma,
Jembe shamba tukifyeka, njoo ufanye kulima,
Jembe njoo pasi shaka, ukija lete mtama,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Jembe kwetu ukifika, tunapata usalama,
Jembe kote umeshika, ukweli tunausema,
Jembe yakija masika, nawe fika nyuma nyuma,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Jembe jua likitoka, nawe usife mtima,
Jembe usije kuchoka, au kupatwa na homa,
Fanya bila kukongoka, fanya usirudi nyuma,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Mola akupe hakika, usende kamwe mrama,
Nenda upate kufika, kama tunavyokutuma,
Sote huko tukifika, tutaishi kwa neema,
Jembe ndiwe mtawala, tangu enzi za wahenga.
Katika shairi hili “Jembe” limepewa sifa za binadamu: ni mfariji, jaji, mpaji, mtawala, mkulima; linaweza kusafiri, kubeba mtama, kufa mtima, na kupatwa na homa. Ingawa tunajua wazi kuwa jembe ni kifaa tu kinachotengenezwa na kutumiwa na binadamu, kuwa halina hata mojawapo ya sifa hizo, lakini tunaposoma shairi tunaathirika na kushawishika kuwa yasemwayo ni kweli na sana maana. Tunalikubali kwa sababu tunaelewa kuwa tukisomacho ni kiwakilishi tu, ni ishara ya dhana nyingine nzito na muhimu: Umuhimu wa kilimo katika uchumi na uhai wetu, na katika historia wa binadamu. Mtunzi katumia uwezo wake wa kisanaa kuumba picha hii ya jembe, nasi wasomaji inatubidi tutumie uwezo wetu wa kuumba na kutafsiri ishara ili tulielewe na kulifurahia shairi hili. Matumizi ya tashihisi yanaliongezea shairi hili uzito wa kimaana, na yanatushirikisha sisi wasomaji katika ufumbuzi wa “kitendawili” chake. Hivyo shairi hili linatuathiri sana kwa kuwa linatushirikisha akili zetu katika kutafakari vipengele vyake na maana yake.
Karibu.
Jambo!
Habari yako?
Hujambo?
Sijambo!
Habari za safari?
Nimefurahi kukutana na wewe.
Jambo.
Hamjambo.
Hatujambo.
jambo.
karibu.
habari yako?
hujambo?
sijambo.
habari za safari?
nimefurahi kukutana na wewe.
habari?
|
|
|
SHAIRI : KIMZINYI LAHAJA YA WAPI ? |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 08:27 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
SHAIRI : KIMZINYI
Hodi hodi na salamu, wa ushairi Mamwinyi.
Nna wasaili kwa hamu, wenye jawabu ni nyinyi.
Miye msinilaumu, akina Gakurya Mwinyi.
Mengi sijayangamua, hebu nifundeni ninyi.
Hususan pwani huko, Kiswahili kulikoni.
Yaliko yake mashiko, na miziziye kwa ndani.
Lahaja nyingi ziliko, kama vile Kibajuni.
Jamani huko mliko, Kimzinyi lahaja gani?
Kiswahili lugha tamu, kinazo nyingi lahaja.
Mathalani kihadimu, Kingwana na kiunguja.
Ninakipata kiamu, Kimgao na Kingadzija.
Kimzinyi mwafahamu, ya wapi hii lahaja?
Chibalonzi na Kimvita, Chimiini na Kimwani.
Kingozi na Kimtangata, nazielewa makini.
Hino lahaja ni tata, jama nitatulieni.
Kimzinyi wapi ntapata, manaye hii lahaja?
Zipo zingine lahaja, ni nyingi za Kiswahili,
Miye yangu moja haja, nijuzeni jambo hili.
Wasanii tu wamoja, nipeni yenu kauli.
Kimzinyi ni lahaja, ya cha nani Kiswahili?
Subukhana shukurani, tamati menifikisha.
Ya ushairi makini, hoja umepeperusha.
Baraka wajalieni, pia kuwaneemesha.
Wote hapa Kisimani, wape maisha marefu.
*****************************
Rwaka rwa Kagarama, (Mshairi Mnyarwanda)
Jimbo la Mashariki, Wilaya ya Nyagatare,RWANDA.
rwakakagarama2020gmail.com
|
|
|
MFANO WA MAJIGAMBO |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 08:22 AM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
MFANO WA MAJIGAMBO
Mimi ni nani?
Mimi ni fulani bin fulani
Mimi ndiye niliyemkomesha yule mshenzi
Yule samba kasoro mkia!
Mimi ndiye yule ninayepigana kifua wazi
Ilinichukua muda mfupi tu kumkomesha!
Kumkomesha nduli aliyevamia kijijini
Mimi ndiye yule mwenye kifua cha chuma
Kifua kisichopitisha mkuki!
Kifua kisichopitisha risasi!
Mimi mpiganaji
Nilikusanya askari wa jicho moja
Wakamkomesha mshenzi
Mimi nisiyeweza kuhangaishwa na vidudu mwitu!
Tazama – nikisema, nanguruma!
Sauti yangu inatetemesha ardhi!
Na vipofu wakajionea
Viwete wakasimama wakiwa mashujaa!
Usiku ulipoingia
Sauti yangu husababisha sisimizi wakasimama kwa miguu mitatu
Maajabu ya mwana makumbi!
|
|
|
‘MGOGORO’ KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 08:10 AM - Forum: Nukuu
- No Replies
|
|
‘MGOGORO’ KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
Mgogoro” katika ushairi wa Kiswahili umekuwapo kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Una misingi yake katika utata wa mambo mawili:
(i) Maana ya jumla ya shairi
(ii) Maana ya shairi la Kiswahili.
Mvutano huu, sawa na uk tulioutaja katika nchi za Ufaransa, Uingereza na Marekani, una pande kuu mbili. Upande mmoja wapo wanamapokeo ambao wanasisitiza kuwa vina na urari wa mizani ni roho ya ushairi wa Kiswahili.2 Upande wa pili wako wanamabadiliko, washairi wa kisasa, ambao wanaeleza na kuthibitisha kuwa si lazima shairi liwe na vina na urari wa mizani ndipo liitwe la Kiswahili.
“Tatizo” lilianza rasmi katika miaka ya mwisho ya sitini na mwanzoni mwa miaka ya sabini walipotokea “watundu” watatu: Ebrahim Hussein, Euphrase Kezilahabi na Jared Angira. Hawa waliandika na kusoma mashairi kwa lugba ya Kiswahili bila kujali kanuni zilizo “uti wa mgongo” wa ushairi wa Kiswahili kwa wanamapokeo. Baadaye waliungwa mkono na washairi wengine kama akina M.M. Mulokozi, K.K. Kahigi, na hivi karibuni Henry Muhanika na Theobald Mvungi. Baadhi ya wanamabadiliko hawa hali kadhalika wameandika nadharia za ushairi za kuonyesha kuwa si lazima shairi la Kiswahili libanwe na kanuni na sheria hizo. Jambo ambalo wanamapokeo kama vile Jumanne Mayoka na Abdilatif Abdalla hawakuzingatia katika vita vya maneno baina yao na wanamabadiliko ni kwamba akina Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wenzao hawana vita na ushairi wa Kiswahili unaofuata hizo sheria. Kwa mfano, katika diwani ya Mulokozi na Kahigi ya Malenga wa Bara3 zaidi ya nusu ya mashairi yao ni ya kimapokeo yafuatayo “sheria” za vina na mizani! Jambo walilolisisitiza watundu hawa ni kuwa kila kitu na kila kiumbe duniani daima kiko katika mwendo wa mabadiliko; na kuwa fani ya ushairi wa Kiswahili pia isingesimama tisti tu katika mzingo wa “sheria” daima dumu. Walilotilia mkazo basi, ni kuwa uwanja wa ushairi wa Kiswahili uyakubali mabadiliko ya fani zilizotumiwa na washairi kueleza maudhui mapya.
Kwa kueleleza kiini cha mgogoro huu, tutatoa maana za ushairi zilivyoelezwa na wanamapokeo na zile za wanamabadiliko. Baada ya hapo tutazichuja zote na kutoa maana tuonayo kuwa inafaa zaidi.
Shaaban Robert, ambaye tunaweza kumchukua kuwa kielelezo cha waumini wa ushairi wa kimapokeo, alitoa maana ifuatayo ya ushairi:
Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi. Zaidi ya kuwa sanaa ya vina ushairi una ufasana wa maneno machache au muhutasari… Wimbo ni shairi dogo, sbairi ni wimbo mkubwa na utenzi ni upeo wa ushairi… kina ni mlingano wa sauti za herufi. Kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti, na ufasaha ni uzuri wa lugha. Mawazo, maono na fikira za ndani zinapoelezwa kwa muhtasari wa ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.4
Kabla ya kuichambua maana hii ya ushairi, tuangalie maana zingine zilizo na welekeo sawa na wa hiyo ya Shaaban Robert.
Mathias Mnyampala, ambaye aliishi enzi za Shaaban Robert pia, aliueleza ushairi hivi:
Ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kaie. Ndicho kitu kilicho bora sana katika maongozi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalumu kwa shairi.5
Nayte Abdilatif Abdalla kaueleza ushairi kuwa:
Utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja baada ya chenziye; wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizo pungufu wala zilizo zaidi; na vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalum na yenye lugha nyofu, tamu na laini, lugha ambayo ni tetelezi kwa ulimi kwa kuitamka, lugha ambayo ina uzito wa fikra, tamu kwa mdomo wa kuisema, tumbuizi kwa masikio ya kuisikia na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ulivyokusudiwa.*
Katika maana hizi za ushairi kuna mambo kadhaa yanayoibuka. Kwanza kabisa, kipengele cha lugha kinatiliwa mkazo na washairi wote hao waliojaribu kueleza maana ya ushairi japo kwa mitazamo tofauti tofauti. Shaaban Robert anasisitiza kuwa shairi zuri halina budi kuwa na ufasaha wa lugha. Naye Mathias Mnyampala anakieleza kipengele hiki kwa kusema kuwa ushairi lazima utumie “maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata.” Abdilatif hatofautiani na wenawe kwani naye pia kasisitiza kuhusu “maneno ya mkato maalum na yenye lugha nyofu, tamu na laini.”
Kwa jumla basi, wanamapokeo hawana ugomvi wowote na washairi wa kisasa kuhusu kipengele cha lugha. Wote wanakubaliana kuwa lugha ya ushairi haina budi iwe ya mkato na ya ufasaha.
Jambo hili tunaliona tujaribupo kuchunguza maana za ushairi kama zilivyotolewa na wanamabadiliko. Tutadondoa maana hizo kama zilivyotolewa na M.M. Mulokozi na E. Kezilahabi, ambao tunaweza kuwachukulia kama wawakilishi wa wanamabadiliko. Kezilahabi anasema:
Ushairi ni tukio, hali au wazo ambalo limeonyeshwa kwetu kutokana na upangaji mzuri wa maneno ya fasihi yenye mizani kwa kifupi ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha.7
Naye M.M. Mulokozi ametoa maana ya ushairi kuwa ni:
… mpangilio maalumu wa maneno fasaba yenye muwala, kwa lugha ya mkato, katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo, ili kueleza wazo au mawazo, kufunzaau kuelezajambo au hisi fulani kuhusu maisha ya binadamu kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo. 8
Mgogoro uko katika matumizi ya urari wa mizani na vina, kwam wanamapokeo wanashikilia kuwa vipengele hivi ni vya lazima; kuwa ni sheria za kutumiwa katika ushairi, hususan ule wa Kiswahili. Kwao vina na urari wa mizani ni uti wa ushairi wa Kiswahili. Haya yamepigiwa muhuri na mfuasi mkuu wa tapo hili Jumanne M. Mayoka, ambaye akiwa kajawa na jazba alisema haya kuhusu mashairi ya kitabu chake cha Mgogoro Wa Ushairi na Diwani ya Mayoka:
Katika kitabu hiki, tungo kama za Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wengineo watungao tungo tutumbi zisizokuwa na sanaa yoyote nimezitupa pembeni… Mwundo wa mashairi yote yaliyomo kitabuni humu ni wa asili ya Kibantu. Kila utungo wa shairi umefungika upande wa mistari: ni lazima kila ubeti wa shairi uwe na idadi maalumu ya mistari; umefungika upande wa vina: ni lazima mistari iwe na vina; umefungika upande wa mizani: ni lazima kila mstari uwe na idadi sawa ya mizani. Mashairi yote yaimbwa; yawcza pia kusomwa au kusemwa tu. Tungo zisizotimiza yote hayo si mashairi.9
Tumemdondoa Mayoka kwa kirefu kwa sababu matamko yake, na hasa lazima alizozisisitiza ni mfano mzuri wa sheria za kirasimi10 ambazo akina Kezilahabi, Kahigi, Mulokozi na wengineo wanaeleza kuwa si za lazima.
Labda kabla ya kuuingilia “mgogoro” huo, tuangalie vipengele vingine vijitokezavyo katika maana za ushairi tulizoziorodhesha.
Vina na urari wa mizani ni vipengele vya ushairi vilivyo na asili yake kama itakavyodhihirika baadaye. Ni udhaifu wa kianazuoni kusisitiza juu ya kipengcle kimoja au viwili vya fani ya kazi ya fasihi na kuviita ni uti wa kazi hiyo. Mathalani, ni wazi kuwa kuna mashairi na nyimbo mzo mzo katika fasihi andishi na simulizi ya Kiswahili ambazo hazifuati hivyo vipengele alivyoviwekea ulazima mtaalamu Mayoka, na ambazo hazina vina wala urari wa mizani, na bado – tupende au tusipende – ni kazi nzuri sana za sanaa.
Katika maana ya kwanza tuliyoiangalia, kwa kutaroka kuwa “wimbo ni shairi dogo” Shaaban Robert anaweza kumtatanisha mwalimu na mwanafunzi wa ushairi. Tujuavyo, si kila wimbo ni shairi. Sifa ya “udogo” ambayo kaitumia Shaaban Robert ina utata pia, le udogo huo ni wa kifani au kimaudhui?
Shaaban Robert aelezapo kuhusu “maono na fikra za ndani (ambazo) huvuta moyo kwa namna ya ajabu” anaungana na wengine kama Abdilatif anayeongelea juu ya nguvu ya ushairi katika kuathiri moyo uliokusudiwa, na hata Mulokozi ambaye amesisitiza kuwa ushairi unatoa maudhui yake “kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo.”
Nadharia hizi zina udhaifu wake kwani katika ushairi hakuna maajabu yoyote yale. Ijapokuwa huenda wataalamu hawa walikusudia tu kueleza juu ya umuhimu wa ushairi kujaribu kunasa hisia za watu, unasaji huo si lazima uwe kwa upande wa ushairi tu bali, kwa hakika, ni unasaji wa lazima kwa kazi zote za sanaa.
Ziko nadharia dhanifu zilizopandikizwa kuhusu uwezo wa mshairi. Nadharia hizi humweka mshairi juu ya watu wengine, juu ya jamii; nazo humgeuza kuwa Mungu-mtu mwenye visima vya hekima na zamzam za mawazo na maeneno mazito yanayovuta mioyo ya watu “kwa namna ya ajabu.”
Imani hii ambayo imeenea basa katika nchi za kibepari ambako mwanasanaa ni mtu maalumu asiye mmoja wa watu anaoandika juu yao, imepata nafasi kubwa sana katika kuipotosha nadharia yote ya ushairi wa Kiswahili. Kwa kufuatana na nadharia hii, baadhi ya washairi wa Kiswahili wameshikilia kutumia maoeno magumu magumu-hasa ya Kiarabu katika mashairi yao. Kwao hao mapambo ya sheria za vina na urari wa mizani ni ya lazima kafika ushairi. Wasioweza kuzitimiza sheria hizo kali basi wasijitie kuwa ni washairi! Kuhusu msisitizo huu wa matumizi ya “mapambo”, M.M. Mulokozi kasema:
… Uozo na ubaradhuli wa maisha ya kiumwinyi, hasa wakati mfumo huo unapoanza kutetereka kutokana na mabadiliko ya nguvu za jamii na uchumi, huwafanya mamwinyi, katika maisha yao ya kizembe na kifasiki, wapendelee sana mambo ya kuvutia macho na kuliwaza pua, kama vile mapambo aina aina, wanawake wazuri, nakshi na marembo ya rangi za kuvutia katika makazi na malazi yao… marashi na manukato, udi na ubani, (nakadhalika…)11
Ni wazi kuwa baadhi ya washairi wetu wa Kiswahili wanaosisitiza mno kuhusu mapambo katika maana ya ushairi wanasisitiza tu mtazamo wa kimwinyi waliorithi na kuuchukua vivi hivi tu bila kutambua asili yake.
Mtazamo huo pia – kwa vile unahusu tabaka hilo nyonyaji la kimwinyi – huwania kuweka sheria na kanuni mbalimbali za kuulinda utamaduni wake. Ni mtazamo unaoumba sanaa na wanasanaa wenye kujitenga na janui, wajionao wao kuwa ndio tu wamejawa na hekima katika bongo zao – hekima na uwezo ambao ni siri yao tu. Ili kusisitiza kuhusu upekee wa wanasanaa wenye mtazamo huo, wengi wao huanza kazi zao kwa kumwita Mungu na kuongea naye. Twaelezwa kuwa huyu, huwaongezea hekima na vipawa. Haishangazi kuona kuwa washairi wetu wengi waliopokeatu “ada” hii ya kinafiki ya kujiona kuwa na kipaji na hekima yenye asili ya uwezo wa Mungu, daima huanza mashairi yao kwa dua. Leo hii hili jambo la kuanza shairi au utenzi kwa kumwita Mungu ni dhahiri kuwa ni njia dhaifu mno ya kuanzia kazi yoyote ya fasihi; ni kujidanganya kuwa ni mkongojo wa mpingo kumbe ni “wa bua” tupu!
Kwa Mayoka, maana ya “shairi” imeishia tu katika idadi ya mistari, vina, urari wa mizani na kule kuimbika kwa utungo. Utungo usiofuata “sheria” hizo basi kwa mtaalamu huyu haufai kwani hauna “sanaa yoyote.” Lakini labda swali la kuuliza hapa ni je, sanaa ni nini? Sanaa ni uoanishaji mzuri wa fani na maudhui katika kazi ya mwigo aifanyayo mtu. Tanzu za sanaa hukua, hubadilika, na hata wakati mwingine hupigwa vikumbo na nguvu za kijamii ikabaki kuwa historia katika kumbukumbu za nyaraka za kale. Tanzu hizi basi, daima huwa katika mwendo wa mabadiliko, na ijaribupo kusimama tu bila kuguswa na mwendo huo hujikuta imechacha. Hii ina maana kuwa mtu aiwekeapo sanaa sheria na kuziita takatifu zisizoguswa na wakati na aina ya jamii, anadunisha na hata kuudharau uhai wa sanaa hiyo!
Katika maana aitoayo Kezilahabi utata unajitokeza katika sehemu mbili: kwanza anapotaja ulazima wa mizani katika shairi, halafu pia anapotamka kuwa kila shairi linaonyesha “ukweli fulani wa maisha.”
Kuhusu mizani, inabidi kuzingatia kuwa Kezilahabi anaongelea kipengele ambacho ni tofauti na kile cha urari wa mizani. Urari wa mizani ni kulingana kwa silabi za kila mstari wa ubeti katika shairi, kila silabi moja ikiwa ndio mizani moja. Urari wa mizani hupambanuliwa na mizani tu katika msisitizo wa idadi sawa za silabi. Mizani aisisitizayo Kezilahabi ni mapigo (rhythm) ambayo ni muhimu katika kila shairi ijapokuwa si lazima yaws ya kufanana kwa kila mstari. Mapigo haya hujulikana pia kama wizani. Ni mapigo yanayosaidia kuainisha mwendo wa shairi. Kwa mfano, iwapo shairi linahusu kifo, lazima mwcndo wake utakuwa wa polepole na mapigo yake yataonyesha huzuni na majonzi. Vile vile, iwapo shairi linahusu mapenzi ni wazi kuwa litakuwa na wizani laini na nyororo inayooana na maudhui ya kimapenzi. Wizani pia huainishwa na mambo kama vile urefu wa mstari au sentensi, ucbaguzi wa maneno na jinsi hayo maneno yanavyohusiana yenyewe kwa yenyewe katika kujenga mstari, ubeti au hata shairi zima.
Kufaulu ama kushindwa kwa shairi kutoa maudhui yanayoeleweka vizuri akilini mwa msomaji au msikilizaji hutokana na ufundi wa mshairi wa kuchagua mwendo na mapigo yanayolandana na maudhui anayoyashughulikia katika shairi lake.
Wizani inajitokeza katika hali mbalimbali, na wala siyo lazima ibebwe na mizani minane au kumi na sita kama ambavyo yaelekea wanamapokeo wanataka iwe. Hali kadhalika siyo lazima wizani iletwe na vina vya kati na vya mwisho, na hata siyo lazima kuwepo na vina katika shairi ili kuleta wizani. Wakati mwingine msisitizo uletwao na marudiorudio ya maneno fulani fulani katika shairi huleta mapigo mahsusi katika mtiririko wa hilo shairi. Yako mashairi mengi katika fasihi ya Kiswahili ambayo yanatumia mbinu hii ya matumizi ya maneno yenye kurudiwarudiwa.
Kwa kifupi basi, tunaweza kusema kuwa wizani ni mpangilio wa urudiaji wa mapigo au mwendo tunaosikia katika tungo. Hata hivyo haimaanishi kuwa lazima wizani ijitokeze tu katika ushairi. Sentensi ifuatayo imedondolewa kutoka katika nathari (Rosa Mistika ya Kezilahabi) na bado ina wizani utokanao na ufupi na usambamba ndani yake. “Jualikatua. Gizalikaingia. Mwezi ulitokea.”
Wizani husaidia sana wasomaji au wasikilizaji wa shairi kwani hufungamana oa yale maudhui akusudiayo kuyatoa mshairi. Mathalani, katika shairi la “Wimbo wa Kunguni” tulilolidondoa katika Kitangulizi, mshairi kaamua kuwa mstari wa 12 uwe na neno moja tu, tena wa mizani mbili tu: “sasa.” Inambidi msomaji ajiulize kwa nini mshairi kafanya hivyo. Ielekeavyo, hapa mshairi alitaka kuwekea mkazo neno hili, na kulipa nguvu ya msisitizo kuwa mambo yote hayo yahusuyo matatizo na migogoro ya ndoa yanatokana na usasa kwani hayakuwapo zamani. Ni wazi kuwa neno hili lingepoteza nguvu yake ya kusisitizwa kama lingewekwa na maneno mengine.
Kwa hiyo basi, sheria za kuifunga wizani katika mapigo ya aina hiyohiyo na ya idadi hiyohiyo ya silabi kwa kila mstari zinaweza kuifanya sanaa ivie, na shairi kama hilo la “Wimbo wa Kunguni”, lisingeleta athari hiyo ya kimaudhui kama lingefungwa na sheria hizo.
Tamko la Kezilahabi alitoalo katika maana yake ya shairi, kuwa katika kila shairi mna ukweli fulani wa maisha linatatanisha, kwani hata maana ya “ukweli” ina utata pia. Labda kwa vile baadhi ya wanafalsafa wamesema kuwa kila uongo ni ukweli fulani wa maisha; lakini tamko la Kezitahabi linaibusha swali moja muhimu: Je, huu “ukwell wa maisha” ni kwa macho ya nani? Kwa mtano, ni wazi kuwa shairi au kazi yoyote ya fasihi ya kipinga maendeleo – tuseme fasihi iliyoandikwa na kaburu anayeabudu ubaguzi wa rangi – itajaa wongo mtupu kuhusu hali za wanaobaguliwa; na itanuia kuuimarisha uongo huo ili kuendeleza unyama wa ubaguzi wa watu kufuatana na rang zao. Yako mashairi mengi sana yaliyojaa wongo mwingi ndani yake!!
Tamko la Kezilahabi halitotautiana na lile la Jumanne Mayoka ambaye, kati ya mengi aliyoyasema, kahitimisha juu ya ushairi kwa kusema: “kamwe ushairi hauwezi kuwa na uhusiano wowote na ujinga wa binadamu. Kazi ya ushairi ni kuuzindua na kuuelimisha umma wa binadamu.”13
Tatizo kubwa la Mayoka ni kuwa ametoa matamko ya jumla jumia mno kutokana na imani yake ya “utakatifu” wa usbairi. Kazi ya ushairi ya “kuuzindua na kuuelimisha umma wa binadamu” hutegemea masuala mbalimbali ya kijamii, hasa ya maslahi ya kitabaka. Katika jamii za mfumo wa kibepari, kazi ya ushairi mara nyingi ni ya kuwalaza na kuwapumbaza watu ili waendelee na ujinga wao kuhusu hali zao. Kazi za namna hii ni zile zinazoeleza uzuri wa maua na machweo ya jua; utamu wa nyimbo za ndege na za mawimbi ya bahari; pamoja na mambo mengine ya kindotondoto wakati ambapo mamilioni ya watu katika jamii hiyo hiyo wanaendelea kuteswa na kugandamizwa. Kazi za namna hii za ushairi katika jamii hizi husiflwa sana na vyombo vya habari, majarida na wahakiki; na zile zinazojaribu kuwazindua oa kuwaelimisha wanyonge zinapigwa vita vikali. Ijapokuwa kwa Mayoka shairi ni lile tu linalozindua na kuuelimisha umma, lakini tujuavyo yamejaa mashairi chungu ozima ya kupumbaza na kuuzubaisha umma.
Mayoka angeihusisha nadharia yake ya ushairi na mifumo mbalimbali ya kijamii, pamoja na nguvu za kitabaka katika mifumo hiyo, angelupatia nadharia sahihi zaidi.14
Sehemu ya mwisho ya maana aitoayo Mulokozi nayo ina matalizo kidogo. Siyo lazima kila shairi lieleze mambo yake “kwa njia inayoburudisha moyo,” kwani yako mashairi mengi mno yanayotoa maudhui vake kwa niia inayokasirisha na hata kukera moyo.
Abdilaut Abdalia naye atuelezapo juu ya “lugha nyofu, tamu na laini,” tena lugha “tetelezi kwa ulimi kuitamka” anatetereka kwani matumizi ya lugha hutegemea maudhui ya shairi. Lugha “nyoofu, tamu na laini” huweza kutumiwa kwenye maudbui kama yale ya mapenzi; wakati ambapo iwapo shairi linahusu vita au hasira lugha itakayotumika ni kali, chungu, na ya kukatakata.
Baada ya kuchunguza kwa kifupi kuhusu maana za ushairi kufuatana na mawazo ya wataalamu wa fasihi ya Kiswahili, sasa tunaweza kutoa maana tuonayo inasadifu kuueleza ushairi.
Ushairi ni utanzu wa fasihi utumiao mpangilio wa lugha ya mkato, ya kipicha na iliyopangwa kwa njia iletayo mapigo mahsusi kufuatana na maudhui yahusikayo.
USHAIRI WA KISWAHILI
Zamani sana lugha ya Kiswahili ilikuwa ya watu wa pwani ya Afrika ya Mashariki tu. Lakini leo hii hutumika Afrika ya Mashariki yote pamoja na nchi za jirani kama vile Zaire, Burundi, Somalia na Malawi. Kwa hiyo ni wazi kuwa wakati tukiongelea kuhusu ushairi wa Kiswahili mara nyingi tunamaanisha ule ushairi uliotungwa kwa lugha ya Kiswahili, na ambao unawahusu watu watumiao lugha ya Kiswahili maishani mwao.
Kwa sababu tunajua wazi kuwa historia ya ushairi wa Kiswahili haianzi na matumizi ya vina na mizani – kwam tuna ushairi mwingi wa Kiswahili kutoka katika fasihi simulizi ambao haufuati “sheria” za vina na mizani15 – sisi hatutachukulia vina na mizani kuwa ni uti wa ushairi wa Kiswahili. Pia tunajua wazi kuwa kuita vina na mizani kuwa ni roho ya ushairi wa Kiswahili ni kosa kwani ushairi wa Kiarabu na mataifa mbalimbali ya Ulaya pia una mizani na vina kama atuelezavyo mtaalamu Lyndon Harries:
…kwa mujibu wa arudhi ya Kiarabu ilishikiliwa kuwa, bila kujali urefu wa shairi, vina vya mwisho katika kila ubeti lazima vipatane tangu mwanzo hadi mwisho wa shairi. Kwa hiyo, hata katika tungo zenye vina vya kati, mtunzi akishaamua tu kutumia kina fulani katika kipande cha kwanza, ilibidi akitumie kina hicho hicho hadi mwisho… utaratibu wa namna hii bado unafuatwa katika mashairi mengi ya Kiswahili…16
Kumbe basi hicho wakntacho “roho” ya ushairi wa Kiswahili kipo katika ushairi wa Kiarabu na mataifa mengine. Je, ushairi wa Kiarabu ni ushairi wa Kiswahili kwa sababu kote ipo “roho” hiyo?
Si nia ya kitabu hiki kujaribu kupuuza sanaa ya urari wa vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili. Ni wazi kuwa sanaa hii ikitumiwa vizuri ni pambo zuri sana katika ushairi. Hata hivyo jambo linalosisitizwa hapa ni kuwa vina na mizani sio yipengele pekee katika sanaa ya ushairi wa Kiswahili; wala sio lazima vina na urari wa mizani utumiwe katika utungaji wa ushairi wa Kiswahili.
Usanii katika kazi ya fasihi huamuliwa na mambo yaliyomo katika kazi hiyo. Yaani kutumia au kutotumia mambo kama vile tamathali, vma, mizani, na kadhalika, hutegemea jambo linaloongelewa katika kazi ya fasihi. Kwa kifupi fani ya kazi ya fasihi huamuliwa na nwudhui ya kazi hiyo. Sasa basi, ushairi wa Kiswahili ni upi?
Mwanzoni tulitaja uhusiano wa fasihi na utamaduni wa jamji inayohusika. Uhusiano huu utatusaidia hapa katika kueleza ushairi wa Kiswahili. Tutaamua kuwa kazi fulani ni ya fasihi ya Kiswahili au la kutokana na jinsi ilivyojitambulisha na ilivyojihusisha na utamaduni wa Waswahili. Hapa neno Waswahili halimaanishi kabila la Waswahili kwani kabila la namna hiyo halipo leo. Waswahili hapa ni wananchi wa Afrika ya Mashariki na Kati kwa ujumla na wala si wale tu wanaoishi katika pwani ya nchi hizi.
Sasa basi, utamaduni huo wa Waswahili ni upi? Huu ni ule unaohusu mila na jadi za Waswahili; sanaa zao, siasa, sayansi na uchumi wao; pamoja na mambo mengineyo yanayokamilisha maisha ya watu hao. Kwa hiyo ushairi wa Kiswahili ni dhahiri kuwa utakuwa na wahusika, mawazo, maudhui, falsafa, historia, dhamira na mambo mengineyo yanayoambatana na maisha ya Waswahili. Kutokana na mambo yote haya, hata kama shairi lina vina na mizani, kama halitekelezi mambo hayo ya kiutamaduni, basi hatuwezi kuliita la Kiswahili!
Maelezo
- Wazo hili la kuwa chanzo cha ushairi ni uchawi limcelezwa kwa kirefu na mtaalamu George Thomson katika Studies in Ancient Greek Society: The pre-historic Aegean (Lawrence and Wishart, London, 1961). Katika Kiswahili wazo hili limeendelezwa na wahakiki kama vile K.K. Kahigi katika makala yake “Ushairi (Mtazamo wa Kisayansi)” katika Kiswahili, Tol. 411, (Machi 1975). Baadhi ya wataalamu wa ushairi wa Kiswahili wameligusia jambo hili – labda bila wao wenyewe kuwa na habari – kwa kuupa ushairi Sifa ya kuuathiri moyo kwa “namna ya ajabu,” ijapokuwahawakulipanua. Ila Jumanne Mayoka, katika kitabu chake cha Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, (Dar es Salaam, TPH, 1986), ameielewa vibaya nadharia hii akadhania kuwa akina George Thomson na Kahigi waongeleapo “uchawi” wana maana ya “tunguli za kichawi” na uramali. Nguvu za kishairi zinazoweza kumfanya mtu alie, ahuzunike, apate moyo wa ujasiri, na kadhalika, ndizo zilizokusudiwa hapa na wataalamu hawa; kwa hiyo “uchawi” ni neno ambalo limetumiwa kishairi zaidi kuliko kwa maana ya ulozi.
- Dai hili la kwamba vina na mizani ni uti wa ushairi wa Kiswahili linajitokeza katika matamko mengi ya wanamapokeo. Mathalani, katika kitabu cha Jumanne Mayoka, Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka, (uk. 28), mwandishi anadai hivi:
Vina na urari wa mizani ni uhai, roho na uti wa ushairi wa Kiswahili. Iwapo vitaepukwa au kubezwa hatutaweza kutambua kuwa hili ni shairi au la.
Dai kama hili linalochukua vipengele viwili au vitatu vya fani na kuviita kuwa ni robo na uhai wa kazi fulani ya saoaa linaua sanaa!!
Yakaenda na kwa kasi
Ni kukanda bila rasi
Na mikanda kuiasi
Hebu basi pigilia.
Utungo huu nimeutunga harakaharaka tu kwa kutumia maneno ya Kiswahili yaliyojipanga katika vina vya kati oa urari mzuri wa mizani. Lakini maneno yenyewe hayana maana wala mantiki, ijapokuwa hiyo roho na uhai audaio Mayoka upo. Huu ni ubeti kibudu, hauna ubai wowote! Uhai wa kazi yoyote ya sanaa hutokana na uwiano mzuri baina ya fani na maudhui, na kamwe hauwezi kutokana na vipengele viwili au vitatu tu vya fani!
- M.M. Mulokozi, na K.K. Kahigi: Malenga wa Bara, (Dar es Salaam/Kamnala/Nairobi: East African Literature Bureau, 1976).
- Shaaban Robert, “Hotuba Juu ya Ushairi,” Journal of The East African Swahili Committee, 28/1 (1958).
- Mathias Mnyampala, Diwani ya Mnyampala, (Dar es Salaam Kampala/Nairobi: East African Literature Bureau, 1970); “Dibaji.”
- A. Abdalia, “Tanzu za Ushairi na Maendeleo Yake.” Makala, (Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili, 1974).
- E. Kezilahabi, “Ushairi wa Mapokeo na Wakati Ujao,” katika kitabu cha J.P. Mbunda (Mhariri), Uandishi wa Tanzania: Insha, (Nairobi/Kampala/Dar es Salaam: East African Literature Bureau, 1975), uk. 23.
- M.M. Mulukozi, “Ushairi wa Kiswahili ni Nini?” Lugha Yetu, Na. 26 (1975), uk. 12
- J. Mayoka, Mgogoro wa Ushairi, uk. x
- Ili kuelewa zaidi kuhusu matapo ya fasihi za Ughaibuni na yale ya fasihi ya Kiswahili ya urasimi mkongwe, urasimi mpya, ulimbwende na uhalisia, soma sura za 1 na 2 za kitabu cha F.E.M.K. Senkoro, Fasihi na Jamii (Das es Salaam: Press and Publicity 1987).
- Mulokozi, “Ushairi na Kiswahili ni Nini?” uk. 12
- Yafuatayo ni baadhi ya marejeo kwa wenye nia ya kusoina zaidi KUHUSU wizani: C. Kugh Holman (Mhariri), A Handbook to Literature (Indianapolis: Odyssey, 1975), hasa kurasa za 4456-457; William R. Bascon na Melwile J. Herskovits (Wahariri), Continuity and Change in African Cultures (Chicago & London: The Univ, of Chicago Press, 1959); Ruth Finnegan, Oral Poetry (Cambridge: Cambridge Univ. Press, 1977); Desmond Graham, Introductin to Poetry (London: Oxford Univ. Press, 1968); na A.M. JONES, African Rhythm.” Africa 24 (1954)
- Kezilahabi, “Ushairi wa Mapokeo.” uk. 5
- Nimejaribu kuainisha fasihi katika mifumo tofauti ya jamii tangu jamii ya mwanzo hadi ya sasa katika Sura ya Kwanza (“Fasihi Katika Mifumo Tofauti ya Jamii”) ya Fasihi ya Jamii.
- Huu ulikuwa katika umbo la cyimbo za ngoma, za kazi, majigambo, na kadhalika. Kuhusu jambo hili, Mnyampala alisema haya: “… Mashairi ya Kiswahili, kabla ya watu hawajajua kuandika, yalikuwa yanatungwa na kuimbwa katika ngoma, majando, nyago, harusi na kadhalika; kwani mashairi si kitu kingine, ni nyimbo, na waliokuwa wakizitunga nyimbo hizo au kuziimbisha katika ngoma waliitwa ‘Manju’ au ‘Malenga’, nazo ziliendelea kuimbwa na kukumbukwa namna hiyo…” (Waadhi wa Ushairi, East African kuwa “mashairi si kitu kingine ni nyimbo” kwani si lazima kila shairi liimbike – na tujuavyo bila kuimbika maneno hayaitwe wimbo – hata hivyo Mnyampala anapoelezea kuhusu ushairi wa Kiswahili kabla ya maandishi anatudhihihshia wazo letu la awali kuhusu vina na nuzani. Kwani, si kila wimbo ulikuwa na vina na mizani kati ya hizo za majaodo, oyago, ngoma, na kadhalika.
- Lyndon Harries, Swahili Poetry, (London, 1966) uk. 186. Msisitizo wangu.
TANBIHI: Kutoka kitabu cha Ushairi – Nadharia na Tahakiki (Dar Es Salaam University Press, 1988, 168 p.) cha F.E.M. K. Senkoro
|
|
|
CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 08:03 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI WA KISWAHILI
Mazrui na Syambo (1992:43) wanadai kuwa utafiti katika fasihi ya Kiswahili unadhirisha ya kwamba ushairi umeanza na zile nyimbo za kale.…….. nyimbo hizi ni zile zilizokuwa zikiimbwa katika hafla mbalimbali: harusini, unyagoni, mavunoni, pungwani na kadhalika na inaonekana hazikuwa na utaratibu wa vina na mizani.
Sitaki kuchimba sana kuhusu chimbuko la ushairi wa Kiswahili kwani lengo ni kuchunguza na kubaini vina viliibukaje au vilitokea wapi mpaka kuwepo katika ushairi wa Kiswahili.
VINA NA MIZANI.
TUKI (2003:94) wanadai mizani ni jumla ya silabi zilizomo katika kila msitari wa ubeti. Wanaendelea kwa kusema, hizi ndizo zileatazo urari wa mapigo, kwani kila msitari watakiwa uwe na mizani sawa na mistari mingine (au wakati mwingine ule msitari uwe nusu ya mizani ya msitari mmoja).
Nao Mazrui na Syambo (1992:40) wanasema mizani ni hesabu au idadi ya silabi katika neno au katika kifungu cha maneno (kama mshororo wa ubeti).
Kabla ya kuchambua fasili hizo za mizani, ni vema tukaitizama pia dhana ya vina kisha tuvitazame kwa pamoja.
Mazrui na Syambo (1992:40) wanafasili vina kama sauti au silabi za aina moja zinazopatikana mwisho wa kipande au mwisho wa mshororo wa kila ubeti.
Aidha, kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili Sanifu ya TUKI (2004), kwa kuegemea katika nyanja ya fasihi, mizani ni idadi ya silabi katika msitari wa shairi na utenzi.
Kwa ujumla, vina ni ufanano wa silabi za sauti za mwisho wa kila msitari (mshororo) wa ubeti wa shairi au utenzi (utendi). Ufanano huu waweza kujitokeza katikati kwa maana katika kila kipande kwa shairi lenye vipande viwili au mwishoni au vyote kwa pamoja (yaani kati na mwisho).
Kwa mfano:
Kijana sina maisha, magenge yanishawishi,
Ukata taniuisha, tuibe ili kuishi,
Arobaini zikisha, kipigo mwisho kuishi,
Maisha haya ni kifo, kifo si kukata roho.
Katika ubeti huo, kina cha kati ni –sha na kina cha mwisho ni “-shi”; lakini kuna uwezekano shairi la vipande viwili likawa na vina mwishoni lakini lisiwe na vina katikati.
Mizani ni idadi ya silabi katika mshororo (msitari) wa shairi au utenzi. Idadi hiyo inaweza kuwa na ulinganifu au isiwe na ulinganifu kwa kila mshororo au ubeti kutegemeana na bahari husika.
Kwa mfano:
Alibino kauwawa,
Mwuwaji ana kiganja,
Maswali kaelemewa,
Adai kweli kachinja,
Uchunguzi wendelea.
Katika ubeti huo, kila mshororo (msitari) una mizani nane.
CHIMBUKO LA VINA NA MIZANI KATIKA USHAIRI
Mazrui na Syambo (1992:43), wakiitetea hoja yao kuwa ushairi umetokana na nyimbo, wanataja mambo makuu matatu yaliyopelekea kuibuka kwa mbinu ya vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili; nayo ni: mdundo katika nyimbo, methali za Kiswahili na athari za kigeni. Baada ya kuyachambua mawazo yao nimebaini kuwa, mambo wanayoyataja kama sababu za kuzuka kwa vina na mizani ni mitazamo mitatu tofauti katika kujadili na kuchunguza chimbuko la mbinu hizi za utunzi, kwa kuwa wao hawathibitishi moja kwa moja kuwa zote zilipelekea, tuzitazame hoja hizo.
- Hitaji la kuongeza ladha ya mdundo katika nyimbo
Mazrui na Syambo (1992:43) wanasema kuwa pole pole, manju wa Kiswahili, katika kujaribu kuongeza ladha katika nyimbo zao walianza kutumia mbinu za vina na baadaye mizani. Huo ukawa mwanzo wa elimu arudhi, (elimu ya kanuni na kawaida za ushairi zilianza kuwa na nguvu).
Nakubaliana na wataalamu hawa kwa kuwa ili wimbo usisimue ni sharti uwe na mdundo mzuri, kwa hivyo, katika uboreshaji wa mdundo, kuna uwezekano mkubwa kwamba manju walizidi kutia vionjo katika nyimbo kiasi cha kufikia kuweka vina na mizani, nyimbo zikanoga na msisimko ukashamiri na kwa hivyo ndio kikawa chanzo hasa cha vina na mizani katika ushairi wa Kiswahil.
- Athari ya methali za Kiswahili
Utanzu wa methali unaaminika kuwa ni mkongwe na yawezekana ndio ulioasisi matumizi ya mbinu za vina na mizani. Mazrui na Syambo (1992:43) wanatoa mifano mitatu ya methali ambazo zimezingatia mbinu hizi zote.
(1) Haraka haraka
Haina baraka.
(2) Haba na haba
Hujaza kibaba
Methali zote mbili zimezingatia mbinu ya vina kwa kuwa silabi za mwisho katika methali (1) zinafanana, zote ni “ka” na katika methali (2) kuna ufanano wa silabi “ba” inayojitokeza katika kila msitari.
Hali kadhalika, katika methali (1) kuna ulinganifu wa idadi ya silabi katika kila msitari (mizani) kama inavyodhihirika hapa chini.
(1) Ha-ra-ka ha-ra-ka (mizani sita)
Ha-i-na ba-ra-ka. (mizani sita).
Kutokana na uhalisia wa baadhi ya methali kutumia mbinu hizi, na kwa ukweli kwamba methali zimekuwepo siku nyingi; kuna uwezekano mkubwa kwamba washairi walioanza kutumia vina na mizani waliathiriwa na tabia ya baadhi ya methali kwa kuwa methali pia zina mchango mkubwa katika suala la maudhui na na kuchopekwa kama zilivyo katika mashairi mbalimbali.
- Athari za kigeni
Hii inaelezwa kuwa sababu nyingine iliyoleta vina na mizani katika ushairi wa Kiswahili. Wageni hawa hasa Waajemi na Waarabu walipokuja (kuhamia) mwambao wa Afrika ya Mashariki waliathiri utunzi wa ushairi wa Kiswahili kwa kuwa wao walianza kutunga mashairi yaliyokuwa na arudhi na miundo yao waliyokuja nayo. Mazrui na Syambo (1992) wao wanawataja baadhi ya watunzi waliotunga mashairi yaliyokuwa na vina na mizani hapo zamani. Nao ni Fumo Liyongo ambaye mashairi yake yaliimbwa katika ngoma za “gungu” na ‘kisarambe”. Kadhalika alitunga mashairinmengine mengi tu ya tumbuizo na ukawafi.
Mwingine ni Aidarusi, huyu alipata kuishi karne ya 17; Aidarus alitafsiri wasifu wa Mtume Muhammad uliokuwa umeandikwa kwa lugha ya Kiarabu (yeye aliutafsiri kwa mfumo wa ushairi). Inadaiwa kuwa tafsiri hii ilitumia Kiswahili cha kale sana, nayo iliitwa, Hamziya.
Mnamo karne ya 18, uliibuka utenzi au utendi, utenzi huu ulikuwa na vina na mizani; miongoni mwa tenzi (tendi) za kale ni Chuo cha Utendi au Utendi wa Tambuka, au Utendi wa Herekali uliotungwa na Bwana Mwengo wa Athumani; utenzi huu unasimulia vita vilivyotokea baina ya majeshi ya Mtume Muhammad na yale ya mfalme Herakliosi wa Wayunani.
Utenzi mwingine ni ule uliotungwa na mtoto na mrithi wa Bwana Mwengo wa Athumani, huyu aliitwa Bakari wa Mwengo, nazo ni Utenzi wa Katirifu na Utenzi wa Mwana Fatuma.
Utenzi wa Inkishafi wa Sayyid Abdalla ni utenzi mwingine uliopata kutungwa ukizingatia vina na mizani.
Washairi waliotajwa wote ni wakazi wa sehemu ya Pate na ushairi wao ulikuwa na vina na mizani.
Nako Lamu kulikuwa na watunzi kama Zahindi Mgumi, Muhammad al- Lami, Mwenye Shehe Ali na Mtunzi wa Kike Saada (kwa uchache). Hawa, utunzi wao ulichochewa na na vita baina ya Mombasa na Lamu na Oman hali iliyopelekea kutungwa kwa mashairi ya Kisiasa.
Inasemekana kuwa Lamu iliathiri maeneo mengine jirani ikiwemo Pemba, Unguja, Mombasa, Tanga na kusambaa zaidi katika maeneo mengine.
Watunzi wote wa wakati huo waliathiriwa na utunzi wa Kiarabu ulioenea hasa kupitia dini ya Uislamu na hivyo washairi wa ushairi wa Kiswahili wakaanza kutumia kawaida za wageni hawa ikiwemo vina na mizani.
Athari nyingine ni ile ya ujio wa wakoloni wa Kiingereza ambao waliathiri utamaduni wetu, miongoni mwa athari zake kuhama kwa hati ya maandishi kutoka hati ya Kiarabu kwenda hati ya Kilatini. “Cheche” za ukoloni ziliposhamiri, washairi wa Kiswahili kama Shaaban Robert na wengine kama Kaluta Amri Abeid, na Mathias Mnyampala (kwa uchache), walianza kutunga wakiutetea Uafrika huku wakiulaani ubaya wa ukoloni na mkoloni mwenyewe na wakati huu kulishakuwa na mwamko wa kujua kusoma na kuandika kwa mwafrika.
HITIMISHO
Kwa ushahidi wa wazi kabisa, chanzo cha ushairi ni mahitaji ya jamii kutumia lugha kwa ajili ya mawasiliano, kwa hivyo ni sahihi kuwa kwa vyovyote vile ushairi wa awali haukuwa na vina wala mizani bali maendeleo ndiyo yaliyoleta kaida hizi. Kwa hivyo, ushairi wa mwanzo haukuwa na vina na mizani bali kawaida hizo ziliibuka mbele ya safari ndefu ya ushairi wa Kiswahili kama ilivyoelezwa katika hoja za utetezi.
Bibliografia
Mazrui, A. M. na Syambo, B. K. (1992). Uchambuzi wa Fasihi. Nairobi: East African Educational Publishers.
Mulokozi, M. M. na Sengo, T. S. Y. (2005). History of Kiswahili Poetry: A.D. 1000 – 2000. Dar es Salaam: Institute of Kiswahili Research, University of Dar es Salaam.
TUKI. (2003). Makala za Semina ya Kimataifa ya Waandishi wa Kiswahili (III): Fasihi. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (2004). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Nairobi: Oxford University Press.
|
|
|
Aina za Lugha Katika Isimu Jamii |
Posted by: MwlMaeda - 01-04-2022, 07:42 AM - Forum: Sarufi na Utumizi wa lugha
- No Replies
|
|
Aina za Lugha Katika Isimu Jamii
- Lafudhi – Ni upekee wa mtu katika matamshi (accent) unaoathiriwa na lugha ya mama, mazingira yake ya kijiografia au kiwango ujuzi wake wa lugha.
- Lahaja – ni vijilugha vinavyoibuka kwa lugha moja kuu kutokana na tofauti za kijiografia baina ya wazungumzaji wa lugha hiyo. Kwa mfano lugha ya Kiswahili ina lahaja kadhaa kama vile Kimtang’ata, Kilamu, Kimvita, n.k. Tofauti baina ya lufudhi ni kama msamiati, muundo wa sentensi au matamshi.
- Lugha rasmi – ni lugha inayotumika katika shughuli za kiofisi ama ya wakati wa mawasiliano rasmi katika taifa fulani. Kwa mfano, lugha rasmi nchini Kenya ni Kiingereza.
- Lugha rasimi – ni mtindo wa lugha uliotumiwa na mtu/watu fulani mashuhuri (zamani) na ambao huonekana kuwa mtindo bora wa lugha unaofaa kuigwa na wengine. Kwa mfano lugha ya Shakespeare.
- Lugha ya taifa – ni lugha inayoteuliwa na taifa fulani kama chombo cha mawasiliano baina ya wananchi, kwa maana inazungumzwa na wananchi wengi katika taifa hilo. Lugha ya taifa, nchini Kenya ni Kiswahili; Uganda ni Kiganda.
- Lugha Sanifu – Ni lugha iliyokarabatiwa na sheria zake (k.v muundo wa sentensi, msamiati, sarufi, n.k) kubainishwa na kuandikwa, na kwa hivyo huzingatia sarufi maalum na upatanisho sahihi wa sentensi. Kwa mfano: Kiswahili sanifu – ni lugha isiyokuwa na makosa ya kisarufi.
- Lingua Franka – Ni lugha inayoteuliwa miongoni watu wenye asili tofauti wasiozungumza lugha moja ili iwe lugha ya kuwaunganisha katika shughuli rasmi au za kibiashara.
- Pijini – ni lugha inayozaliwa kutokana na mchanganyo wa lugha zaidi ya moja. Kwa mfano. Sheng’ (lugha ya vijana mitaani nchini ni lugha iliyoibuka kutoka kwa Kiswahili na Kiingereza.
- Krioli – Ni pijini iliyokomaa na kukubalika.
- Lugha mame – hii ni lugha isiyokua na ambayo hubaki kati umbo lake la awali. Kwa mfano lugha ya Kilatini haibadiliki na hivyo hutumika katika kubuni majina ya kisayansi, n.k.
- Lugha azali – ni lugha inayozaa lugha nyinginezo.
- Misimu – ni lugha yenye maneno ya kisiri ambayo hutumiwa na kikundi fulani cha watu katika jamii, inayoeleweka tu baina yao. Misimu huibuka na kutoweka baada ya muda.
|
|
|
|