MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 48 online users.
» 0 Member(s) | 47 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  SHAIRI: MWAKA HUU SISHIRIKI
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:38 AM - Forum: Ushairi - No Replies

MWAKA HUU SISHIRIKI

Mwaka huu sishiriki, nanioneke mjinga
Sitaki thama sitaki, mbali nanyi najitenga
Kumbe hamtendi haki, mshindi mshampanga
Na nioneke mjinga, mwaka huu sishiriki

Sitaki kujipa dhiki, Ni mjuvi wa uhenga
Wamewamwaga samaki, kwa nini niwape unga
Wallahi sitadiriki, uovu kuupa kinga
Na nioneke mjinga, mwaka huu sishiriki

Sijitii ushabiki, tuli nangoja kipenga
Hata nikipewa laki, uwanjani sitotinga
Siuwezi unafiki, ndiyo leo najifinga
Mwaka huu sishiriki, na nioneke mjinga

MBARUKU ALLY
MOTO WENU Jr
0717199835
11/05/2017
17:40
CHUO KIKUU DODOMA
TANZANIA

Print this item

  SHAIRI : NAWAENZI MAMA ZETU
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:28 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NAWAENZI MAMA ZETU
Situngi kwa desturi, ela pawapo na haja
Ulisanifu shairi, haraka pasi kungoja
Sineni kama tuyuri, kasuku jina likaja
Nawaenzi mama zetu, walo kote duniani

Wote walo duniani, niambwe sema mmoja
Alo na kubwa thamani, kwa wanyama pamwe waja
Litanitoka kinywani, Mama peke mwenye tija
Nawaenzi mama zetu, walo kote duniani

Beti tatu shairini, nisioneke kiroja
Kumuomba Rahmani, mbili ama tatu hoja
Walio ulimwenguni, awape mema korija
Na wale walo mavani, pepo wawe waingoja
Nawaenzi mama zetu, walo kote duniani

Wa Makame Mariamu, Mzazi aso harija
Malezi yake adhimu, ninayosijayafuja
Namtukuza dawamu, mi kuruti yeye meja
Nawaenzi mama zetu, walo kote duniani

Wakatabahu matini, kalamu yangu yavuja
Yamkini naamini, ujumbe umeshakuja
Ombi uishi vichwani, kwa sote na kwa umoja
Nawaenzi mama zetu, walo kote duniani

Print this item

  SHAIRI: HALI HALISI
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:23 AM - Forum: Ushairi - No Replies

HALI HALISI
Hali ya watunga hoja, ujinga kutokosowa
Hali ya jinsi moja, kuandamania ndowa
Hali hii ni kioja, kwa dini wanaojuwa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa

Hali ya walo na pesa, kuzidi kuongezewa
Hali ya waso na hisa, kuishi kama wakiwa
Hali yanitesa hasa, ni nani wakuondowa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa

Hali ya wale makada, ya tatizi kuyazuwa
Hali kwa wanuka shida, kushindwa kusaidiwa
Hali yaleta kaida, wabaya kusujudiwa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa

Hali ya wapenda hoji, na tufani kuzolewa
Hali ya unyanyasaji, ja samaki kuvuliwa
Hali hino sitaraji, kwa nchi nilozaliwa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa

Hali ya elimu bora, vyuoni walopatiwa
Hali hakuna ajira, na walishahaidiwa
Hali mbaya itagwira, chalinze walitongowa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa

Hali ya wenye ubavu, vya wanyonge kukwapuwa
Hali kwa wenye uvivu, kufikiri fikiriwa
Hali ya pembe za ndovu, weziwe tuzo kupewa
Hii ndo hali halisi, ya uwongo sijazuwa
Hali ya kila utungo, mzuri tamati huwa
Hali ni kwenye ukingo, mashuwa yangu yapwewa
Hali likamili lengo, kalamu chini natuwa
Iwapo siyo halisi, nasubiri kosolewa

Print this item

  SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:18 AM - Forum: Ushairi - No Replies

NA NIKIFA WASICHANGE

Ewe mwanangu taali, Njoo hapa kwenye mwanga
Njoo usiketi mbali, Kisha na mlango funga
Nataka kupa kauli, ishike kama usinga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Ndiye wewe wa awali, rika si mwana mchanga
Timamu zako akili, huna chembe ya ubunga
Ninakupa uwakili, usikubali matanga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Sinazo nguvu za mwili, kwa maradhi kunizonga
Mwanangu wajidhalili, mikono kwao kukinga
Hupati japo kalili, wote wakupiga chenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Leo ni dhoofu hali, ndiyo kisa wanitenga
Niliwalea azali, maisha yao kujenga
Sasa nipo muhimbili, Dawa za kuungaunga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Huu ni mwaka wa pili, toka nipate majanga
Moyo unatundu mbili, yangu moja imefunga
Dhati nateseka kweli, wafumba yao maninga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Daftari na bakuli, wakipitisha kuchanga
Piga teke vyende mbali, usishiriki ujinga
Nakuomba wakabili, usihofu zao ngenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Mauti yakiwasili, ombi nizikwe Mkinga
Moa kijiji aali, sitaki kuzikwa Vanga
Mwanangu wosia mali, wapuuzao hutanga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Hapa natia kufuli, na hotuba kuifunga
Wewe wangu abtali, tayari nishakuganga
hima fanya kulihali, yangu usijeyatenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

MBARUKU ALLY
MOTO WENU Jr
(FAHARI YA TANGA)

Print this item

  TENDI TATU ZA KALE
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 08:17 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

UCHAMBUZI WA TENDI TATU ZA KALE 

Ikisiri
Tangu Finnegan (1970:108) alipodai kwamba, katika fasihi simulizi ya Afrika Kusini mwa Sahara ni nadra sana kupata Tendi, dai hili limeibua mjadala mrefu wa kitaaluma miongoni mwa wataalam mbalimbali wakiwamo: John William, Thomas A. Hale na Stephen Belcher ambao ndio waliodondoa baadhi ya beti katika tendi za Kiafrika na kuziweka pamoja katika kitabu kinachojulikana kwa jina la Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent. Mbali na hao, mtaalam mwingine ni Mulokozi (1999) ambaye naye anathibitisha upo wa tendi katika Afrika Mashariki kwa kukusanya pamoja tenzi tatu za kale katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale. Pia kuna mtaalamu mwigine Belcher (1999) ambaye naye alizungumzia tendi za Kiafrika katika kitabu chake kinachojulikana kwa jina la Epic Tradition of Afrika. Hivyo basi, ni wazi kwamba uchapishaji wa vitabu hivi ni matokeo chanya ya tafiti zilizofanywa na wataalamu mbalimbali na kuamua kukusanya na kuziweka pamoja kama mifano ya uwakilishi wa utamaduni wa tendi Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa lengo la kufungua milango ya kutambulika zaidi.
1.0     Utangulizi
Makala hii itajishughulisha zaidi na mapitio-hakiki ya vitabu viwili ambavyo ni, Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent na Tenzi Tatu za Kale. Katika mapitio hayo vipengele mbalimbali vitajadiliwa kama vile: fasili ya tendi, mpangilio wa tendi katika vitabu hivyo, waandishi wa vitabu husika, uhakiki: usuli wa yeli/manju, usuli wa kijamii-kihistoria, utendaji-uwasilishwaji, udhaifu/mapungufu, ubora wa kazi, ulinganisho na tendi nyingine, hitimisho na marejeo. Kwa kuanza na fasili ya tendi;
[url=https://www.blogger.com/null][/url]
1.1  Fasili ya Tendi
Miongoni mwa wataalam waliofasili dhana ya utendi ni pamoja na Bowra (1930) yeye anatumia fomula kuelezea maana ya utendi kuwa ni E = M + Ms yaani, (Epic = Mars + Muse/music). Hii ina maana kamba utendi ni mungu, muziki na vita (U = M + V). Hivyo basi, maana ya maelezo ya Bowra ni kuwa utendi ni tukio la kimuziki linalozungumzia vita kwa njia ya ushairi ulioandikwa.
Mulokozi (1996) anasema, Tendi ni nyimbo ndefu za kimasimulizi au za mawaidha, nyimbo hizo zinahusu visa vya mashujaa.
Wamitila (2006) anasema, Tendi ni aina ya utenzi ambao unazungumzia maisha na matendo ya shujaa au mashujaa wa jamii fulani.
Kwa hiyo, kutokana na fasili hizi tunaweza kusema kuwa, utendi ni kama Saiklopidia au maktaba ya jadi ya historia ya jamii fulani ambayo kupitia tendi mbalimbali jamii inatambua historia yake katika vipindi mbalimbali, chimbuko lake, mashujaa wao pamoja na kujua mila na desturi zao pamoja na utamaduni.
2.0     Mpangilio wa tendi katika vitabu

Johnson na wenzake (1997) katika kitabu chao cha Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent wanajaribu kukigawa katika sehemu kuu tatu. Sehemu ya kwanza wameweka tendi mbalimbali za Afrika Magharibi, sehemu ya pili wameweka Tendi za Afrika ya Kaskazini na sehemu ya tatu wanamalizia kwa kuweka tendi za Afrika ya Kati. Je mpango huu ni wakinasibu au kuna uzingativu wa jambo fulani? Je tendi za Afrika Mashariki zinatambulika miongoni mwa tendi za Kiafrika? Kwa nini hazijitokezi katika kitabu hiki?
Wataalamu hawa wanadai kuwa, tendi hazipatikani kila mahali, kuna matokeo ya muunganiko wa jamii na mazingira ya kihistoria pamoja na utendaji wa namna mbalimbali. Tendi zilizokusanywa katika ukanda huu zina sifa zinazoingiliana/zinazohusiana miongoni mwazo ingawa si lazima ziwe na utamaduni pamoja na historia inayofanana.
Pia hata katika Tenzi Tatu za Kale mwandishi naye amekigawa katika makundi makuu matatu au sehemu kuu tatu ambazo ni: sehemu ya kwanza inahusu Utendi wa Fumo Liyongo, sehemu ya pili mwandishi amehakiki Utenzi wa Al-Inkishafi na sehemu ya tatu ni Utenzi wa Mwanakupona.
2.1     Waandishi wa vitabu husika
Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent ni kitabu kilichoandikwa na kuhaririwa na John William Johnson (Indiana University), Thomas A. Hale (The Pennsylvania State University) na Stephen Belcher (The Pennsylvania State University).
Pia Mulokozi (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) ameandika na kuhariri kitabu cha Tenzi Tatu za Kale. Wataalam hawa katika kukusanya na kuhariri tendi mbalimbali za Kiafrika walibaini nduni bainifu za tendi za Kiafrika na masuala majumui yanayopatikana katika tendi za Afrika na tendi za Ulaya kama tutakavyoona hapo baadaye.
Johnson na wenzake wanasema kuwa, koja/diwani hii yenye dondoo 25 za tendi za Kiafrika ni ya kwanza na ya aina yake kutokea duniani na ni toleo la tatu katika mkururo wa tendi za Kiafrika zilizozinduliwa na “Indiana University Press”. Hii ni hatua muhimu sana iliyofikiwa katika kubadili fikra za kimagharibi kuhusu tendi katika muktadha wa kiulimwengu.
Hegel (1963) akinukuliwa na Johnson na wenzake (kashatajwa) anadai kuwa, Waafrika hawanaLiterature, hivyo ni wazi kamba hata historia hawana. Dai hili halina mashiko, kwani leo hii tunaona kwa kupitia tendi uibukaji wa vyote viwili historia na Fasihi ya Kiafrika ambavyo vilifunikwa na ujinga wa wazungu kwa muda mrefu sana. Lakini pamoja na hayo, bado wanahoji juu ya fasili ya fasihi simulizi.
3.0     Usuli wa manju/yeli
Kwa ujumla tendi ni tungo ndefu ambazo huimbwa na mafundi fulani wanaojulikana kama mayeli na huwahusu mashujaa walioishi au wanaosadikiwa kuishi katika jamii fulani. Mfano mzuri ni utendi wa Sundiata/Sunjata wa jamii ya Wamande nchini Mali ambao uliimbwa na mayeli wa jamii hiyo kama vile Fa-Gigi Sisoko. Pia utendi wa Fa-Jigi ambao yeli wake ni Seydou Camara akisaidiana na mkewe ambaye alikuwa akipiga narinya-kifaa cha muziki, utendi wa Sonsan of Kaarta ulisimuliwa kwa kuimbwa na Mamary Kuyate’, huku wimbo ukiambatana na muziki, utendi wa Almami Samori Toure’ yeli alikuwa ni Sory Fina Kamara.

Pia wasimulizi au mayeli wa utendi wa Wagadu ni Diarra Sylla ambaye aliandika mistari 257 na Jiri Silla ambaye naye aliandika mistari 800. Kwa pamoja waliweza kupata simulizi moja linaloeleza mambo yaliyowatokea watu wa Wagadu.
Aidha utendaji katika tendi za Kiafrika huweza kutofautiana kutoka yeli mmoja kwenda mwingine. Sababu za utofauti huo huweza kuwa masuala ya mila na desturi za jamii husika, hivyo huweza kukuta yeli/manju husimulia hadithi yake ya kiutendi kwa kuzingatia taratibu za jamii hiyo. Licha ya hayo, vilevile yeli huyohuyo huweza kusimulia hadithi ileile ya kiutendi kwa namna tofauti tofauti kulingana na muktadha.

Katika tendi za Kiafrika mayeli walikuwa ni watu walioheshimika sana katika jamii husika, kwani wao ndio waliojua historia na tamaduni za jamii na ndio wanaopitisha historia ya jamii kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Mfano, Johnson na wenzake wanatuambia kuwa, katika jamii ya Wamande yeli (Sara) alikuwa mwanamke wa heshima sana na hata alipokufa mwaka 1989 ng’ombe 15 walitolewa sadaka wakati wa sherehe za maziko yake.
3.1     Usuli wa kijamii-kihistoria
Kama tulivyosema hapo awali utendi ni kama saiklopidia ya jamii fulani kwani umesheheni masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo historia pamoja na mila na desturi za jamii mbalimbali. Mfano, tendi zote za Kiafrika kama vile wa Bamana Segu, Sonsan of Kaarta, Almami Samori Tuure’, Musadu, Fa-Jigi na Son-Njara kwa kuzitaja chache, zote zinaelezea masuala ya kijamii-kihistoria kama vile: matukio ya kivita, kidini-hija, asili ya koo mbalimbali, mila na desturi za jamii ya Wamande kama vile: masuala ya matambiko, salamu nk. Ndio maana utendi kama waSundiata umesimuliwa katika nchi za Ghana, Sudan, Gambia, Ivory Coast, Mali na Mauritius nk. kama njia mojawapo ya kurithisha amali za jamii hiyo.
Vilevile utendi wa Wagadu ni simulizi maarifu sana katika historia ya Soninke’kuanzia wakiwa wamoja kabla ya kuanguka kwa ufalme na kusambaratika katika maeneo mbalimbali ya Sahel, Senegal na Ghana.
4.0     Utendaji-uwasilishwaji
Tendi nyingi za Kiafrika hutumia mbinu mbalimbali katika uwasilishaji wake. Mfano huweza kusimuliwa kwa njia ya kinadhari au kwa njia ya ushairi/nudhumu yaani kuimbwa kama vile utendi wa Hambodedio and Saigalare,  Fa-Jigi huwasilishwa kwa kuimbwa na manju pamoja na mkewe ambaye husaidia kupiga kifaa kiitwacho narinya (nanga), pia utendi wa Sara wa jamii ya Maninka uliimbwa na Sara pamoja na kaka yake Yamuru Jabate’. Katika utendi huu unajitokeza urudiaji rudiaji wa korasi, mfano;
5. Chorus:       Ah! Sara is sung for those of one voice.
Don’t you see it?
Sira Mori: Sara! Sara is sung for those with promises.
Don’t you see it?
Pia mwandishi anafafanua kuwa, tendi simulizi za Afrika mara nyingi katika uwasilishwaji wake huambatana na uigaji wa matendo ya watu pamoja na muziki kutoka kikundi cha waimbaji na hadhira.
Vilevile, mwandishi anaibua hoja juu ya mjadala ulioongozwa na Lucy Duran juu ya uwepo wa suala la ujinsia katika tendi. Japokuwa anakiri kwamba, mjadala haupo wazi sana kutokana na vyanzo visivyorasmi kushindwa kutofautisha kati ya sifa ziimbwazo na wote wanaume na wanawake na simulizi za kitamaduni katika utawala wa wanaume. Duran anadai kwamba, wanawake wataimba utendi mzima kama hakuna wanaume wa kuimba. Hata hivyo hakuna utendi wa mwanamke ulioonekana katika machapisho. Hoja hii inahitaji ushaidi wa kitafiti zaidi.
Aidha katika mapitio haya inajibainisha wazi kuwa, tendi simulizi za Kiafrika hazina mpaka halisi unaotenganisha tendi, visasili, ngano, visakale, maghani, nyimbo, n.k. Kwa mfano Utendi wa son-Jara, una kisakale cha Biblia; masimulizi ya uumbaji wa Mungu kwa Adamu na Eva. Lakini katika tendi za kimagharibi tunaona mpaka uliodhahiri.
Hivyo tunaona kwamba, tendi nyingi zinazohusu mashujaa huingiza sifa nyingi za visasili, visakale, maghani au hata ngano ndani yake. Kwa mfano, utendi wa Fumo Liyongo, Wagadu, Lihanja, Mwindo, nk. sifa hii huonesha kwamba, tendi huchota visa vya sanaa jadi nyingine kutoka tamaduni zenye tendi simulizi. Kwa mfano, Fumo Liyongo, Mwindo, Rukiza, Sundiata, n.k. ni miongoni mwa mashujaa wenye sifa sawa na mashujaa wengine wa kiutendi ulimwenguni kama vile, Gilgameshi na wengineo.

Tenzi Tatu za Kale ni kitabu cha fasihi chenye baadhi ya tungo mashuhuri za zamani, zilizokusanywa na kuhifadhiwa pamoja. Tungo hizo ni pamoja: Utendi wa Fumo Liyongo, uliotungwa na Muhamadi Abubakar Kijumwa mwaka 1913, Utenzi wa Al-Inkishafi uliotungwa na Sayyid Abdallah bin Ali bin Nasiri na Utenzi wa Mwanakupona uliotungwa na Mwanakupona Binti Mshamu kwa ajili ya binti yake aliyeitwa Mwana Hashima binti Mataka.
Mwandishi wa kitabu hiki amebainisha vipengele mbalimbali vya utendi vinavyojitokeza katika Utendi wa Fumo Liyongo. Anaeleza kwamba, Fumo Liyongo ni utendi unaohusu matukio muhimu ya kihistoria na kijamii, hueleza kuhusu ushujaa wa shujaa. Anamwona Fumo Liyongo kama shujaa anayependwa na watu. Sifa hii pia tunaiona hata katika tendi nyingine za Kiafrika. Kwa mfano: Utendi wa Sundiata unaakisi historia na utamaduni wa jamii, huelezea matukio ya kishujaa na mashujaa. Pia hata Utendi wa Lihanja nao anawakilisha chimbuko la taifa la Wamongo.
Aidha, mwandishi anadondoa baadhi ya sifa za tendi za Kiafrika kwa kuhusianisha na shujaa Liyongo. Anamwelezea shujaa huyu kuwa, ni mtu mwenye nguvu za kimwili. Mfano kitendo cha kubeba mizigo ya kujaza chumba kiliwashangaza Wagalla, kupuliza panda na kusua nk. Pia ni rijali. Mfano, Wagalla walimwomba sultani awaruhusu wapate mbegu yake. Licha ya nguvu za kimwili pia alikuwa na nguvu za kisirihi. Mfano, udhaifu wake ulikwa kitovuni, hivyo haikuwa rahisi kudhurika kwa namna yoyote ile isipokuwa kwa kuchumwa sindano kitovuni. Vilevile alikuwa na mshikamano na jamii yake ndio maana hata aliweza kusaidiwa na mama yake pamoja na kijakazi Saada pindi alipokuwa kifungoni. Hatimaye alifaulu kutoroka.
Sifa hizi alizonazo Liyongo pia zinajitokeza hata katika tendi nyingi za Kiafrika, kwa mfano Mwindo anasaidiwa na shangazi yake, mjomba pamoja na watu wengine kwenda kulipiza kisasi kwa baba yake. Pia mbali na sifa hizi, mashujaa wengi wa Kiafrika huzaliwa kwa njia isiyo ya kawaida. Kwa mfno, katika Utendi wa Jeki la Njambe’ Inono shujaa Njambe’ Inono kabla ya kuzaliwa anaongea tumboni akielekeza mahali atakapozaliwa. Baada ya kuzaliwa anarudi tena tumboni, halafu baadaye anataka kuzaliwa kwenye chupa. Mfano,
…So they began to go back with waves. It was then that a voice spoke from Ngrijo Epee Tungum’s womb: “Ina! Sit down in the water and give birth to me!”
Mulokozi (2002) katika utafiti wake kuhusu tendi za jamii ya Wayaha hasa Utendi wa Rukiza anaungana mkono na mawazo ya Johnson japokuwa anaongeza kuwa, shujaa wa Kiafrika sharti awe ni msaada kwa watu wake na hivyo: (USHUJAA: Ushakiri+Sihiri+Watu) Hivyo basi, tunaweza kusema kuwa, Utendi wa Fumo Liyongo una sifa fawafu kama ilivyo katika tendi nyingine za Kiafrika. Kwanza ni masimulizi ya kinadhari yenye uunganifu, pili nudhumu, yaani ni utungo wa kishairi, tatu ni simulizi linalohusu matukio muhimu ya kijamii-historia na mwisho huelezea kuhusu ushujaa.

Fauka ya hayo, mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale amejadili pia Utenzi wa Al-Inkishafi kuwa ni miongoni mwa tenzi mashuhuri sana katika lugha ya Kiswahili na ulichipuka kutokana na jadi ndefu ya tenzi za Kiswahili mjini Pate. Utenzi huu ulitungwa na Sayyid bin Ali bin Nasiri mwaka 1800-1820 unahusu matukio mbalimbali yaliyotokea katika jamii ya Waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki, kwa mfano, mgogoro hasa wa kuanguka kwa mji wa Waswahili kulikosababishwa na uvamizi wa Wareno.

Kihalisia ni kweli mambo hayo yametokea. Kwa hiyo utenzi huu una dhima ya kihistoria katika jamii ya watu wa Pwani ya Afrika Mashariki. Pia unawakilisha utamaduni wa jamii ya Waswahili wa Pwani ya Afrika Mashariki kutokana na lugha iliyotumika ambayo ni Kiswahili kilichochanganyika na Kiarabu kwa kiasi fulani, utamaduni wa watu hao, miji iliyotajwa ambayo ni Pate, Kilwa, Lamu na  Mombasa.

Vilevile katika Tenzi Tatu za Kale kuna Utenzi wa Mwanakupona ni utenzi wa kimawaidha uliotungwa na Mwanakupona Binti Mshamu kwa ajili ya binti yake aliyeitwa Mwanahashimu binti Mataka mwaka 1858. Utenzi huu unaonekana kuwakilisha vyema tungo za utamaduni na maonyo ya wakati huo. Lakini pia aligusia kwa vijana wengine wa kike wapate kuusoma utenzi huu ili nao wapate maonyo hayo (Ubeti wa 94 na 95). Utenzi huu unaonekana kuibadilisha jamii ya uswahilini baada ya kuona kuwa unafaa hasa kwa malezi ya kijadi kwa watoto wa kike kwa kuwafunda. Yawezekana Jambo hili ndilo linaloufanya utenzi huu uonekane kuwa msaada wa jamii hata leo hii.

Kihistoria, tunaelezwa kuwa huu ni utenzi wa kale uliokuwa unaendana na mazingira ya wakati huo. Mwandishi aliuandika kwa kuilenga jamii ya wakati ule hasa kwa kufuata mila na desturi za jadi za wakati huo kama vile: heshima ya ndoa, wanawake kuwekwa utawani, kutoonesha sura zao mbele ya watu, kumtukuza mume kama Mungu wao wa pili. Pia unaonekana kuwa ulikuwa ni utenzi wa tabaka tawala.

5.0     Udhaifu katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale na Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent.

Pamoja na kwamba, Utenzi wa Mwanakupona una baadhi ya sifa za utendi kama vile: unudhumu, uunganifu, unahusu masula ya kijamii mfano, mafundisho katika jamii, mianzo na miisho ya kifomula, nk. bado hatuwezi kuuingiza kwenye kumbo la tendi kwani unakosa baadhi ya sifa za msingi za kitendi kama vile: masuala ya kishujaa na mashujaa, matendo ya kivita nk. Vivyo hivyo hata katika Utenzi wa Al-Inkishafi pia unakosa sifa hizo za msingi.

Kimsingi Utenzi wa Inkishafi na Mwanakupona hazizungumzii suala la ushajaa wala shujaa zaidi ya kumwona mwandishi akitamalaki kwa kiasi kikubwa kama kwamba yeye ndiye shujaa. Swali la kujiuliza Mwandishi anawezaje kuwa shujaa? Kama ni shujaa ruwaza yake ni ipi? Anafuata kanuni za shujaa wa namna gani? Wa Kijadi/Kiafrika au Kimagharibi, au Kiarabu? Hoja hii haihusiani na kitabu cha Tenzi Tatu za Kale lakini inafaa kujiuliza maana wengine huweza kufikiri kwamba, mwandishi ni shujaa kutokana na tajiriba aliyonayo, mfano mtunzi wa Utendi wa Mwanakupona.

Pia katika Tenzi Tatu za Kale, mwandishi amechanganya pamoja Tendi na Tenzi na kuziita zote kwa pamoja TENZI TATU ZA KALE, yaani Utendi wa Fumo Liyongo na Utenzi wa Al-Inkishafi pamoja na Utenzi wa Mwanakupona. Je, kigezo gani kimetumika? Kama mwandishi alilenga kuzishughulikia kazi zote tatu ndani ya kitabu kimoja, basi angepaswa kukwepa neno hilo ili kuepuka kuchanganya dhana mbili zinazotofautiana, badala yake angeziita TUNGO TATU ZA KALE. Nadhani msamiati huu ungekuwa fawafu kabisa kwa kazi zote tatu.

Mkanganyiko mwingine tunaouona ni kwamba, mwandishi hakuweka bayana kuwa Utenzi wa Inkishafi ni utendi au ni utenzi, maana baadhi ya sehemu ndani ya kitabu ameita Utenzi na sehemu nyingine ameita Utendi. Mfano, ukurasa wa 73 anasema; “Utenzi wa Inkishafi unapata nguvu yake kutokana na lugha tukufu na taswira anazotumia mtunzi…” ilhali katika ukurasa wa 77, mwandishi anasema; “Inkishafi ni Utendi wa Kiafrika…” Hivyo tunaona kwamba, hapa mwandishi anawaweka wasomaji katika hali ya sintofahamu kipi ni kipi!

Pia suala jingine la kujiuliza kuhusu Tenzi Tatu za Kale ni kwamba, je huo ukale anaousema mwandishi unaanzia wapi na unaishia wapi? Je tunawezaje kubaini mipaka ya ukale na usasa? Kwani ukale unaanza lini na unaisha lini?

Aidha, mwandishi hajaonesha bayana mkabala au nadharia iliyomwongoza katika ubatizaji wa tungo hizi na kuziita TENZI TATU ZA KALE? Je ameangalia lugha iliyotumika au mambo yalisheheni katika tungo hizo?

Suala la udhaifu pia linajitokeza hata katika Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent. Inaonekana kuwa, mwandishi hakufanya utafiti wowote katika Afrika Mashariki ndio maana hakuna chochote kilichoelezwa kuhusu tendi za Afrika Mashariki. Hii inawapa picha wasomaji kwamba, Afrika Mashariki hakuna tendi ilhali tunajua kuwa, Afrika Mashariki kuna tendi na wapo watafiti wabobevu waliofanya tafiti za tendi sehemu mbalimbali za Afrika Mashariki kama vile: Mulokozi, Mbele, Kagame, nk.

Kosa kama hili tunaliona pia hata kwa Belcher (1999) katika Epic Traditions of Africa. Belcher amechunguza baadhi ya tendi za Afrika hasa tendi za Afrika Magharibi na Afrika ya Kati na kugundua kuwa zinamfanano katika baadhi ya vipengele. Hii inadhihirisha kwamba, katika ukanda wa Afrika Mashariki wataalamu wa tafiti katika uwanja huu ni wachache sana, hivyo kuna haja ya wataalamu chipukizi kumakinikia katika uwanja huu.
6.0     Ubora wa kazi hizi
Mbali na mapungufu ya hapa na pale, pia tutakuwa wachoyo wa fadhila kama hatutaona ubora uliosheheni katika kazi hizi. Kwa mfano, Johnson na wenzake katika kitabu chao cha Oral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent wamefanya kazi nzuri sana katika kuzitambulisha tendi mbalimbali za Kiafrika kwa ulimwengu mzima ili hata wale waliopotoshwa na Finnegan waweze kubadili mtizamo wao.

Pia wamesaidia kuonesha ufanano mkubwa uliopo katika tendi za Kiafrika hasa katika baadhi ya mambo kama vile manju au mayeli, japokuwa kuna utofauti za kimsamiati lakini dhima yake ni ileile. Kwa mfano wanajulikana kwa majina kama: gewel, gawlo, jali, jeli, mabo, gesere, jesere, nk.

Vilevile mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale amefaulu sana katika kutoa maana mbadala za maneno au msamiati mgumu uliotumika ili kuwarahisishia wasomaji kuelewa kwa urahisi ujumbe unaokusudiwa katika tungo zote tatu.
Licha ya hayo, utangulizi na maelezo ya mwandishi wa Tenzi Tatu za Kale yamenisaidia sana kama mwanafasihi chipukizi hasa kujua maudhui ya tungo hizi tatu na pia kujua namna bora ya kujenga hoja zenye mantiki na maelezo yenye mtiririko fawafu.
7.0        Hitimisho
Kwa ujumla tunaweza kuhitimisha makala haya kwa kusema kuwa, wataalamu hawa wamejitahidi kwa kiasi kikubwa kutuonesha namna tendi simulizi za Kiafrika zinavyoakisi historia ya jamii husika katika utamaduni, mila na desturi, mahusiano na mshikamano wa kijamii. Vilevile wote kwa pamoja wametuonesha kuwa, utendi pamoja na hadithi mbalimbali za mashujaa huwa na ruwaza inayofanana ambayo hutuwezesha kupata muundo wa msingi wa tendi ambao ni wa kimajumui.

Mulokozi (kashatajwa) ameainisha sifa za shujaa wa tendi za nanga kama ifuatavyo: Anatoka tabaka la juu au la kawaida, shujaa huwa ni jasiri, anatumia sihiria, anakuwa rijali, hutegemea nguvu za wahenga au mizimu na anahitaji msaada wa umma. Ukiangalia tendi nyingi katikaOral Epic from Africa: Vibrant Voices from a Vast Continent ruwaza za mashujaa wa Kiafrika kwa kiasi kikubwa zinalandana na ruwaza za mashujaa Gilgamesh na Enkidu katika utendi waGilgamesh. Mwandishi Sandars (1960), haoneshi kuzaliwa kwa Gilgamesh na Enkidu. Utendi huu unawaonesha mashujaa hawa wakiwa tayari watu wazima kama vile kwa Fumo Liyongo. Gilgamesh ameanza kuelezewa tayari akiwa kiongozi wa mji wa Uruk wakati Enkidu ameanza kuelezewa tayari akiwa anaishi porini na wanyama. Maelezo haya yanajidhihirisha katika kigae/kibao cha I & II na katika kitabu uk. 61.
                Kigae/kibao cha I na kitabu (uk. 61)
 I WILL proclaim to the world the deeds of Gilgamesh. This was a man to whom allthings were known; this was the king who knew the contries of the world. He was wise, he was misteries and knew secret things, he broughy us a tale of the days before the flood

Kibao/kigae cha II Then he, Enkidu, offspring of the mountains,
who eats grasses with the gazelles,
came to drink at the watering hole with the animals,
with the wild beasts he slaked his thirst with water.
 
8.0        MAREJEO
Belcher, S. (1999), Epic Traditions of Africa, Bloomington, Indiana University Press.
Finnegan, R. (1970), Oral Literature in Africa. Oxford. Clarendon Press.
Johnson, J. W. na wenzake, (1997), (Ed.), Oral Epics from Africa: Vibrant Voices from a VastContinent, Bloomington, Indianapolis University Press.
Mulokozi, M. M. (1996), Fasihi ya Kiswahili, Dar es Salaam: Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.
                              (1999), (Mha.), Tenzi Tatu za Kale, Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi                                 wa Kiswahili.
                           (2002), The African Epic Controversy:  historical, Philosophical and
                Aesthetic Perspectives on Epic Poetry and Performance. Dar es salaam,                 Mkuki na Nyota Publishers.
Wamitila (2006) Kamusi ya Ushairi, Nairobi: Vide-Muwa Publishers Ltd.
Sandars N. K (1960), The Epic of Gilgamesh. Cox & Wyman Ltd: Great Britain.

Print this item

  TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI: SHUJAA LIYONGO NA EMANUEL KATIKA BIBLIA
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:58 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi - No Replies

TASWIRA YA KIFO CHA SHUJAA KATIKA UTENDI:  SHUJAA LIYONGO NA EMANUEL (YESU) KATIKA BIBLIA

.pdf   SEHEMU YAKWANZA.pdf (Size: 144.72 KB / Downloads: 1)

Print this item

  Sifa za kifani za utendi andishi wa Kiswahili katika Utenzi wa Ras 'lGhuli
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:45 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla - No Replies

Sifa pambanuzi za kifani za utendi andishi wa Kiswahili zinavyojitokeza katika Utenzi wa Ras ‘lGhuli

Ikisiri
Utendi wa Ras I’Ghuli kama tunavyoelezwa na Leo Van Kessel (1973,dibaji) kuwa unatokana na kisa kimoja cha Kiarabu kiitwacho Futuhu ‘lYamani maana yake ni kushindwa au kutiishwa kwa Yemeni. Kisa hicho cha Kiarabu husimulia jinsi nchi ya Yemeni ilivyoshindwa na kutekwa na majeshi ya Waislamu. Mwanzoni kisa hiki kiliandikwa katika lugha ya kigeni (Kiarabu). Hivyo si Waswahili wengi walioweza kukielewa ndipo Mwalimu Mgeni bin Faqihi aliamua kukibadili kisa hicho kutoka katika usimulizi wa kawaida kuwa utenzi na  kukiandika kwa lugha ya Kiswahili lakini kwa kutumia hati za Kiarabu ili kiweze kusomwa na watu wengi zaidi. Kwa kuwa kisa hicho kwa asili kilikuwa kinawahusu Waarabu na Uislamu na kiliandikwa kwa lugha ya Kiarabu swali la kujiuliza je kutafsiriwa kwa kisa hicho kwa lugha ya Kiswahili lakini kikiandikwa kwa kutumia hati za Kiarabu na baadaye kuandikwa kwa haati za Kirumi, je tunaweza kuujumuisha utendi huo kuwa ni utendi wa Kiafrika au Kiswahili? Hivyo makala haya yanakusudia kuuhakiki utendi huo kama una sifa za kuitwa utendi wa Kiswahili au la. Hivyo basi kukamilisha lengo hilo kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu nne. Sehemu ya kwanza ni utangulizi katika sehemu hii tutatoa fasili ya utendi, muhtasari wa kitabu na usuli wa mwandishi na sehemu ya pili, kwa kuwa kulishawahi kutolewa mawazo kuwa hakuna utendi wa Kiafrika tutaongozwa na vigezo kama vilivyopendekezwa na Mulokozi (1999) kuuhakiki utendi huo kama unakidhi vigezo vya kuitwa utendi wa Kiafrika kabla hatujazama kuutazama utendi huu kama una sifa za kuitwa utendi wa Kiswahili. Sehemu ya tatu tutajikita kuangalia kama Utendi wa Rasi ‘lGhuli unakidhi vigezo vya kuitwa utendi wa Kiswahili tukimakinikia vigezo vya kifani na kimuundo. Na sehemu ya mwisho ni hitimisho.
1.0   Utangulizi
Dhanna ya utendi ni dhanna iliyowashughulisha wataalamu mbalimbali. Mathalani, Chaligha (20013:82) anatueleza kwamba, mtaalamu Bowra (1930) anatumia fomula kuelezea maana ya utendi kuwa ni U=M+V (Utendi =Muziki + Vita) akiwa na maana utendi ni tukio la kimuziki unaozungumzia vita na miungu kwa njia ya ushairi ulioandikwa. Kwa upande wake Mulokozi (2009), anasema, utendi ni utungo mrefu wa kishairi wenye kusimulia hadithi ya ushujaa na mashujaa, na utenzi ni utungo wowote mrefu wa kishairi, aghalabu wenye kutoa mawaidha ya kidini au ya kidunia au kusimulia habari fulani. Aidha, Belcher (1999: xiv) anasema kuwa, tendi ni masimulizi ya papo kwa papo yanayohusu masuala ya kihistoria ambayo hutolewa hadharani mbele ya hadhira na yeli maalumu. Anaendelea kufafanua kuwa, tendi nyingi huambatana na muziki. Aidha Wamitila (2003:333) anasema kuwa, utendi ni shairi refu la kisimulizi linalozungumzia kwa mapana na mtindo wa hali ya juu matendo ya mashujaa au shujaa mmoja.
Ama kwa hakika tukiwaangalia wataalamu wote hawa kimsingi hawatofautiani sana isipokuwa wengine wamejikita zaidi kutoa fasili zinazoegemea katika utendi simulizi na wengine wamejikita katika utendi andishi na wapo wengine ambao fasili zao zimejumuisha aina zote za utendi yaani utendi simulizi na utendi andishi. Mathalani Bowra anauona utendi kama kazi iliyoandikwa akijikita zaidi katika utendi andishi wakati Belcher, Molokozi na Wamitila wote wanakubaliana kuwa utendi ni shairi/nyimbo ndefu za kisimulizi wakijikita katika kigezo cha utendi simulizi.
Kutokana na maelezo ya wataalamu hao kuhusu tendi, tunaweza kujumuisha mawazo hayo kwa pamoja kwa kusema, utendi ni masimulizi marefu yenye umbo la kishairi yanayoelezea visa kuhusu mashujaa na matendo yao ya kishujaa, historia na ustawi wa jamii. Tendi inaweza kuwa katika umbo la usimulizi ama uandishi mara nyingi utendi ukiwa katika usimulizi uwasilishaji wake huambatana na muziki.
1.1    Muhtasari wa Utendi wa Rasi ‘lGhuli
Utendi wa Rasi ‘lGhuli unatokana na kisa cha Kiarabu kiitwacho Futuhu ‘lYamani ikiwa na maana kushindwa au kutiishwa kwa Yemeni. Kisa hicho cha Kiarabu husimulia jinsi nchi ya Yemeni ilivyoshindwa na kutekwa na majeshi ya Waislamu yakiiongozwa na Mtume Muhamadi[1] mwenyewe, Seyyidna Ali bin Abi Talibu[2](kuanzia sasa Seyyidna Ali) na Seyyidna Umar bin Khatab kunako karne 6. Tafsiri ya utendi huu umepewa jina la Rasi ‘lGhuli linalotokana na jina la kebehi la mtawala wa makafiri wa Yemeni ambaye jina lake halisi aliitwa Mukhariki bin Shahabu. Jina hili la kebehi Ras ‘lGhuli lina maana ya Kichwa cha Nyoka.
Kwa ujumla utendi huu una beti zipatazo 4584. Kuanzia ubeti wa 1-43 ni nyongeza ya mshairi ambapo anaanza kwa kumsifu Mungu na anaeleza sababu ya kutafsiri kisa hicho kutoka lugha ya Kiarabu hadi Kiswahili. Kisa chenyewe kinanzia aubeti 44- 4,565 na kuanzia ubeti 4,566 hadi 4,584 ni nyongeza ya mshairi ambapo anamalizia kwa kuomba dua.
Visa vya utendi huu vimepangwa katika sehemu viii (nane). Utendi unaanza Muhamadi akielezwa jinsi mtawala wa Yemeni Mukhairiqi bin Shahabu (Rasi ‘lGhuli) anavyo wadhulumu watu wake. Muhamadi anatokewa na malaika Jiburili na kumtaka kumtuma mtu kwenda kupeleleza nchi ya Rasi ‘lGhuli.
Malaika Jiburili anamweleza Muhamadi habari za kukamatwa kwa Zuberi, Sayyidna Umari anatumwa kuipeleleza nchi ya Rasi ‘lGhuli. Mtume anaamua kupeleka jeshi kupambana na Rasi ‘lGhuli. Rasi ‘lGhuli anaazimia kuishambulia Madina, mapigano makubwa yanaanza majeshi ya pande zote mbili yanapigana siku kucha Muhamadi anamuomba Mungu dua, Mungu anaitikia sala yake anawatuma malaika kusaidia jeshi la Waislamu kupambana na makafiri na anatuma na tufani ya mvua makafiri wanashindwa na kukimbia wengine wanasilimu. Majeshi ya Waislamu yanateka miji kadhaa. Rasi l’Ghuli anaomba msaada kwa majeshi mengine. Majeshi ya Waislamu yanazidiwa nguvu mpaka anapowasili Sayyidna Umar majeshi ya makafiri yanashindwa na kukimbia.
Vita vinaanza upya Rasi ‘lGhuli anawapa silaha askari wake. Muhamadi naye anaandaa vikosi viwili vya jeshi moja linaongozwa na Sayyidna Ali na lingine linaongozwa na Sayyidna Umari. Majeshi ya Rasi ‘lGhuli yanashambuliwa. Majeshi ya Rasi ‘lGhuli yanalivamia jeshi la Waislamu katakati ya mapambano Rasi ‘lGhuli anakimbia na kukimbilia mjini anaingia gerezani bila kutarajia anamkuta Sayyidna Ali.  Wanapigana hatimaye Sayyidna Ali anafanikiwa kumuua kwa kumkata kichwa na kuamuru kichwa chake kitundikwe katika lango la mji ili kila anayepita akione. Makafiri wanakimbizwa mpaka milango ya mji wanapoona kichwa cha Rasi ‘lGhuli wanafadhaika wengine wanasilimu wasiosilimu wanauwawa Mtume Muhamadi anaweka utawala mpya na kurudi na watu wake Madina baada ya ushindi. Kwa ufupi kisa cha utenzi huu kiliandikwa katika muktadha wa kuanzishwa na kuenezwa kwa dini ya Kiislamu huko Saudia Arabia na Yemen.
Tunataarifiwa kuwa, utendi huo hughanwa au kusomwa wakati wa sherehe kama vile matanga, harusi, n.k. na mghani maarufu wa utendi huo tunaambiwa kuwa alikuwa ni Mwalimu Sefu bin Hamidi wa Bagamoyo Leo Van Kessel (keshatajwa, dibaji).
1.2 Usuli  kuhusu mwandishi wa Utenzi wa Ras ‘lGhuli
Kwa mujibu wa Mhariri wa utenzi huu, Bwana Leo Van Kessel anatueleza kuwa, Mgeni bin Faqihi alikuwa ni Mtumbatu kutoka Unguja aliyehamia Bagamoyo.[3] Inasemekana kuwa alizaliwa mwanzoni mwa karne ya 19. Huko Bagamoyo alikuwa akifundisha dini ya Kiislamu katika vyuo vya Kiislamu. Alitumia muda wa miaka mitano kukamilisha utendi huu kwani inasemekana alianza kuandika utendi huu mwanzoni mwa miaka ya 1850 na kuukamilisha mwaka 1855. Ni miongoni mwa  washairi na watunzi wazuri wa kazi za fasihi kutoka Zanzibar waliopata kuwepo. ama kuhusu tarehe ya kufariki kwake bado mpaka sasa haijuikani.
Aidha kwa kuwa, kazi hiyo inaitwa Utenzi wa Ras ‘lGhuli na kwa kuwa unatokana na kisa cha kiarabu na unazungumzia habari za Waarabu na dini ya Kiislamu. Je huu ni utendi? Kumbuka si kila utenzi unaweza kuwa utendi. Hivyo ili kutegua kitendawili hiki itatulazimu kwanza kuondoa utata huo kwa kuangalia sifa za utendi wa Kiafrika ili kuuona utenzi huu kama unakidhi sifa hizo na tunaweza kuuweka katika kundi la tendi, ndipo sasa tuingie katika msingi wa hoja yetu, ya kuthibitisha kama utenzi huu una sifa za utendi wa Kiswahili ama la.
2.0 Sifa za utendi wa Kiafrika
Ama kuhusu sifa za utendi, wataalamu mbalimbali wameainisha vigezo au sifa za utendi wa kiafrika. Miongoni mwa wataalamu hao ni, Finnegan (1970) Okpewho (1979), Johnson (1986),  Mbele (1986), Belcher (1999), Mulokozi (1999), kwa kuwataja wachache. Aidha Utendi wa Rasi ‘lGhuli ni utendi unaonekana kuzingatia vigezo vya utendi kama vilivyopendekezwa na Mulokozi (1999:11) baada ya kufanya  majumuisho ya mawazo ya watafiti mbalimbali na kupata vigezo vipya vya utendi wa kiafrika ambavyo ni: (a) Utendi kuwa na sifa ya usimulizi yaani huwa na umbo la kihadithi, (b) Ni nudhumu yaani hutolewa kishairi na huwasilishwa kwa kughanwa hususani pamoja na ala ya muziki, © Huhusu matukio au masuala muhimu ya kihistoria na/au kijamii, (d) Huelezea habari za ushujaa na mashujaa, (e) Matini yake kwa kawaida hutungwa papo kwa papo na (f) Utendi hutawaliwa na muktadha wa utunzi na uwasilishaji wake kwa jamii.
Ama kwa hakika, ingawa vigezo hivi vinavyotajwa na Mulokozi (keshatajwa) kujikita zaidi katika utendi simulizi, na tukiuchunguza Utendi wa Ras ‘iGhuli tutaona kuwa unakidhi vigezo hivyo. Hebu tuanze kuangalia vigezo hivyo jinsi vinavyojitokeza katika utendi huo. Tukianza na:
Kigezo cha masimulizi yaani utendi kuwa katika umbo la kihadithi. Utendi wa Ras ‘lGhuli ni miongoni mwa tendi ambazo zinakidhi kigezo hiki cha usimulizi. Leo van Kessel (keshatajwa, viii) anatubainishia hili anapotuambia kuwa, mshairi ni msimulizi bingwa. Anatuhadithia wingi wa mambo ya kusisimua yaliyojiri wakati wa vita. Ukiisoma utendi huu utagundua kuwa ni masimulizi yaliyo katika umbo la kihadithi  yanaeleza habari za kuinukia kwa dini ya Kiislamu na mapambano ya vita yaliyoongozwa na Seyyidna Ali bin Abi Talib, Seyyidna Umar bin Khatab na Mtume Muhamadi kunako karne ya sita na ushindi walioupata katika vita hivyo kuwashinda makafiri na Mtume Muhamadi kusimika utawala mpya na kurejea Madina ambako walipokelewa kwa furaha. Rejea ubeti wa 4560-4563. Ama kwa hakika tukichunguza beti hizi utaona kuwa utendi huu umekaa kisimulizi msimulizi anatusimulia hadithi ya kuinukia kwa dini ya Kiislamu na vita vya mapambano kati ya majeshi ya Waislam na makafiri na ushindi wa majeshi ya Muhamadi na namna walivyorejea Madina na kupokelewa.
Sifa nyingine ambayo inajitokeza katika utendi huu ni kuwa na sifa ya nudhumu. Wamitila (keshatajwa, 171) anaeleza nudhumu ni tungo za kifasihi zenye matumizi ya lugha yanayozifanya tungo hizo kubaguliwa au kubainika kama zisizo za kinathari. Anaendelea kufafanua kuwa tungo hizo hutumia mapigo kwa utaratibu maalumu aghalabu neno hili hutumiwa kwa maana ya tungo za kishairi. Kwa maelezo haya yanatupa maana kuwa utendi unatakiwa kuandikwa au kutolewa kishairi na kuwasilishwa kwa kughanwa. Utendi huo una sifa ya kishairi na vipengele vifuatavyo ndivyo vinavyoufanya utendi huu kuwa na sifa ya kishairi:
(a)    Utendi umeundwa na beti, Wamitila (keshatajwa, 243) anasema ubeti ni kifungu cha mshororo mmoja mmoja au mishororo kadha katika shairi na ambacho kinajitosheleza. Utendi wa Rasi ‘iGhuli umeundwa na beti 4584 na kila ubeti umeundwa na vipende vinne vya mistari ambavyo vinajitosheleza na hivyo kubeba sifa ya ushairi.
(b)   Kila ubeti umeundwa na vina na mizani 8 kwa kila kipande cha mstari. Abedi (1953: 15) anasema tenzi nyingi zaidi huwa zenye mistari minne na mizani nane kama inavyojitokeza katika Utendi wa Rasi ‘iGhuli.(rejea beti za utenzi huo). Tukitazama beti hizo tunaona kuwa, kila kipande kimeundwa na mizani nane (8) na kuhusu vina kila ubeti umebeba vina vyake huku kukiwa na kina bahari cha ri kinachojitokeza katika beti zote. Sifa zote hizo zinaufanya utendi huo kuwa na sifa ya kishairi. Ikumbukwe kuwa tendi nyingi za Kiswahili huundwa na beti ambazo kila ubeti huundwa na mistari minne ingawa pia zipo tendi zenye kutumia mistari zaidi ya mine katika beti, mfano mzuri ni Utenzi wa Vita vya Kagera msimulizi amechanganya mistari zaidi ya minne. Tendi nyingine za Kiswahili zinazotumia mistari mine kwa kila beti ni kama vile Utendi wa Fumo Liyongo, Al-inkishafi, Mwanakupona kwa kutaja chache.
Aidha sifa nyingine kama ilivotajwa na Mulokozi ni utendi kuelezea matukio au masuala muhimu ya kihistoria au kijamii. Utendi wa Rasi ‘iGhuli una sifa hii kwani unahusu masuala ya kihistoria hususani historia ya kuanzishwa kwa Uislamu huko Saudi Arabia na Yemen katika karne ya saba.
Kigezo kingine kinachojitokeza katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli ni utendi kuelezea habari za ushujaa na mashujaa.[4] Mashujaa wanaozungumziwa katika utendi huu ni Mtume Muhammad na masahaba wake kama vile Seyyidna Ali bin Abdala Talib na Seyyidna Umar bin Khatab. Mathalani msimulizi anatueleza jinsi shujaa Ali alivyofanikiwa kumuua Rasi ‘iGhuli anatueleza kuwa Rasi ‘iGhuli baada ya kuona mapigano yamepamba moto anaamua kukimbilia mjini na kuingia na kumkuta Ali wanapigana hatimaye Ali anaibuka shujaa kwa kumkata kichwa Rasi ‘iGhuli na kichwa chake kutundikwa juu ya lango la mji. Rejea kuanzia ubeti wa 4528-4532.
Aidha utendi huu unakidhi hata vigezo vya utendi vilivyotolewa na Ruth Finnegan (1970:108-109) hususani kigezo cha urefu na uunganifu ambavyo havijitokezi katika vigezo vilivyoainishwa na Mulokozi. Mathalani kwa upande wa Urefu shairi hili linakidhi kigezo hiki. Leo van Kessel (keshatajwa, viii) anatueleza kuwaUtendi wa Rasi ‘lGhuli ndio utenzi mrefu kuliko zote zilizopata kuchapishwa katika lugha yoyote ile ya Kiafrika. Utendi huo una beti 4584.
3.0 Sifa pambanuzi za kifani za utendi andishi wa Kiswahili zinavyojitokeza katikaUtenzi wa    Rasi ‘lGhuli    
                    
Tunapozungumzia utendi wa Kiswahili tunatakiwa kuhusisha na dhana nzima ya fasihi ya Kiswahili. Tunaarifiwa kuwa mwanzo mwa miaka ya 1970 hadi 1990 dhana ya fasihi ya Kiswahili ilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wanataaluma wa fasihi. Wapo waliokuwa wanaona kuwa kuna fasihi ya Kiswahili na upo upande mwingine uliona kuwa hakuna fasihi ya Kiswahili. kwa kuwa si lengo la makala haya kujikita katika mjadala huo. Itoshe kusema kuwa, wataalamu hao walikubaliana kwamba, fasihi ya Kiswahili ni ile inayotumia lugha ya Kiswahili na hata iliyotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili, Sengo (1987), Mazigwa (1991). Aidha Synambo na Mazrui (1990) wanasema kuwa fasihi ya Kiswahili ni ile iliyoandikwa kwa Kiswahili tu na iwapo inazungumzia utamaduni wa Kiswahili au utamaduni mwingine. Hivyo basi, kwa mawazo hayo tunaweza kusema kuwa utendi wa Kiswahili ni utendi ulioandikwa au kusimuliwa kwa lugha ya Kiswahili na unaozingatia fani na maudhui (utamaduni) ya Waswahili wenyewe au jamii nyingine maadamu umeandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
Ama kwa hakika, utendi andishi wa Kiswahili una sifa zake pambanuzi za kifani ambazo huweza kutumika kuzitofautisha na tendi nyingine zisizo za Kiswahili. Wamitila (keshatajwa, 41) anaeleza fani kuwa ni dhana inayotumiwa kuelezea muundo au mpangilio wa kazi fulani ya kifasihi au hata sehemu zake. Anaendelea kufafanua kuwa fani huelezea mbinu na mtindo wa kuyawasilisha yaliyomo au maudhui. Njogu na Chimerah (2008:312) wanasema, fani ni usanifu wa kazi ya fasihi. Wanaendelea kufafanua kwamba, fani ni vipengele mbalimbali vya sanaa na jinsi kazi hiyo inavyojengwa ili kupata maana yake. Hivyo basi katika utendi tunapoangalia fani tunaangalia tunaangalia vipengele mbalimbali vya sanaa ya utendi wa Kiswahili ama mbinu au mtindo anaoutumia msimulizi kuwasilisha mawazo yake kwa hadhira.
Ama kwa hakika Utenzi wa Rasi ‘lGhuli unakidhi sifa za kuitwa utendi wa Kiswahili kutokana na kubeba sifa pambanuzi za kifani za utendi wa Kiswahili. Utendi wa Kiswahili una sifa pambanuzi zifuatazo za kifani ambazo kwa hakika zinajitokeza katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli:
Kwanza ni matumizi ya fomula. Wamitila (2003:49) anasema fomula ni istilahi inayotumiwa kuelezea kiunzi cha msuko au sifa fulani ambazo hutumiwa katika uundaji wa kazi za kifasihi. Anaendelea kufafanua kuwa usimulizi na utambaji wa hadithi katika fasihi simulizi hutangulizwa na kianzio cha fomula. Katika tendi za Kiswahili kuna mwanzo wa kifomula ambapo msimulizi huanza na kuomba dua na kumsifu Mungu na Mtume. Fomula hii inajitokeza katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli ambapo msimulizi anaanza kwa kuomba dua na kumsifu Mungu kama anavyoanza katika ubeti wa 1-8:
1.      Awali bisumi ‘llahi                         
 Jina la mola ‘llahi                                  
               Pweke asiye shabihi                             
               Ndiye wahidi qahari.           (unaweza angalia pia katika ubeti 2-8)
Tukiziangalia beti hizo zinatuonesha kuwa msimulizi anaanza kwa kuomba dua na kumsifu Mungu (Allah). Hii ni fomula inayojitokeza katika tendi za Kiswahili. kwa mfano katika utendi mwingine wa Kiswahili wa Utendi wa Fumo Liyongo tunaona sifa hii ya fomula ya kuanza na dua na kumsifu Mungu au Mtume ikijitokeza katika ubeti wa 1. Pia tukiangalia Utendi wa Al-Inkishafi tunaona fomula hii pia ikijitokeza, rejea ubeti wa kwanza wa utenzi huo.
Aidha utendi wa Kiswahili unakuwa katika mpangilio wa beti. Utendi wa Rasi ‘lGhuli nao ni utendi unaoundwa na beti, una beti 4,584 na kila ubeti umeundwa na vipande vinne vya mstari ambapo kila kipande kina mizani nane (8). Aidha beti hizo huwa na vina vinavyofanana katika vipande vya mwanzo na kina cha kipande cha mwisho ni kinabahari ambacho huishia na -ri kuanzia ubeti wa kwanza hadi wa mwisho. Hili tunaweza kuliona tukitaza beti zote kuanzia ule ubeti wa kwanza hadi wa mwisho. Beti hizo tatu tukiziangalia zinatuonesha kuwa kila ubeti una vipande vinne vya mstari na kila kipande kina mizani 8. Kina bahari kikiwa ni –ri. Abedi (keshatajwa, 16) anasema kila utenzi wa mizani nane huimbika vizuri.
Vilevile matumizi ya majigambo ni sifa nyingine inayoitambulisha utendi wa Kiswahili. tendi za Kiswahili huwa na matumizi ya majigambo. Wamitila (keshatajwa, 107) anaeleza majigambo kuwa ni aina ya maghani (au sifo) yanayohusu kujisifu au sifa. Anaendelea kufafanua kuwa majigambo hutongoa utungo wa kujisifu kuhusiana na kitendo fulani, ushujaa, urijali au matendo muhimu. Katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli tunaona kabla mashujaa hawajaanza kupambana huanza kujigamba kwanza na kuanza kuelezea sifa na uwezo wao mbele za adui zao. Mfano mzuri ni Sayyidna Ali anajigamba mbele ya adui wake Zuheri na Zuheri kwa upande wake anajigamba mbele ya adui yake huyo. Hebu tuangalie ukurasa wa 43 kuanzia ubeti wa 845-847.
    845. Jina langu takwambia                    847.   Ndimi samba maarufu
            Ndi mimi Shekhe Alia                               Ndimi mvunda sufufu
Ibunu amu Nabia                                      Wajapo kuwa elfu
            Muhamadi ‘lBashiri.                                  Siwajali sifikiri.
Kwa upande wake Zuheri naye anamjibu Sayyidna Ali akijigamba kuanzia ubeti wa 865-868 (Rejea beti hizo).
Pia unaweza angalia ubeti 867 na 869. Beti hizo zinatuonesha namna mashujaa hao walivyokuwa wakijagamba kila mmoja akijisifu mbele ya mwenzake na mara baada ya kumaliza majigambo hayo huanza kupambana kwa kupigana rejea ubeti 887-892 (uk. 45). Sifa hii ya majigambo tunaona pia ikijitokeza katika Utenzi wa Nyakiiru Kibi.  Majigambo hayo yanaoneshwa na    Kanyamaishwa na Nyakiiru Kibi. (rejea ubeti 383-389)
Sifa nyingine ya utendi wa Kiswahili inayojitokeza katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli ni sifa ya matumizi ya Kiswahili cha Lamu kwani ndiyo husemekana kuwa ni Kiswahili cha kishairi. Taylor akinukuliwa na Mbaabu (2007:15) kuhusu lahaja ya Lamu (Kiamu) kuhusishwa na ushairi anasema kuwa, ni ukweli unaotajwa na Waswahili wenyewe kwamba Kiamu kinasifika kwa utajiri wa lugha ya kishairi. Hivyo basi katika utendi huo sifa hii inajitokeza kwani kuna matumizi makubwa sana ya Kiswahili au msamiati kutoka lahaja ya Kiamu.maneno kama ndia likiwa na maana ya njia ubeti wa 447, nti likiwana maana ya nchi katika ubeti wa 524, matolikiwa na maana ya macho katika ubeti wa 437 na 462, mtana likiwa na maana ya mchana katika ubeti wa 565 kwa kutaja maneno machache.
Matumzi ya Kiswahili cha kale ni sifa pambanuzi nyingine ya utendi wa Kiswahili. Wamitila (2010:73) anasema utanzu wa ushairi unatumia msamitai wa kale ukilinganishwa na utanzu wa riwaya au wa tamthiliya. Sifa pia  inajitokeza  katika Utendi wa Rasi ‘lGhuli. Utendi umetumia msamiati wa kale baadhi ya msamiati wa kale unaojitokeza katika utendi huo ni, akima likiwa na maana ya akisimama katika ubeti wa 785 na 818,akita likiwa na maana ya akaita katika ubeti wa 789 na 884.
 Si hivyo tu, utendi wa Kiswahili una sifa ya kuchanganya wahusika wanadamu na wasio wanadamu. Msokile (1993:32 )  anaeleza kuwa wahusika ni watu , wanyama au vitu katika kazi ya kisanaa ya kifasihi. Kwa mfanoUtendi wa Rasi ‘lGhuli unachanganya wahusika binadamu ambao wanaongozwa na Mtume Muhamadi na masahaba na wafuasi wa Kiislamu, pia kwa upande mwingine kuna binadamu makafiri wanaongozwa na Rasi ‘lGhuli lakini pia msimulizi amechanganya na wahusika wengine wasio binadamu kama vile malaika, Mungu n.k. Mathalani katika ukurasa wa 13-19  ubeti wa  350-362  anasema;
354. Kiwasili Jiburili                             359.  Kanituma nikujie
                        Akamwambia Rasuli                              Na maneno nikwambie
         Akusalamu Jalali                                     Tuma mtu amwendee
         Salamu nyingi kathiri.                            Sultani wa kufari.
Tukiziangalia beti hizo tunaona kuwa kuna wahusika malaika wanajitokeza katika utendi huo. Ukirejea beti ya 354 na 359 tunamwona malaika Jibilii akimpa amri Mtume Muhamadi kwenda kwa Rasi ‘lGhuli. Aidha kuhusu wahusika Malaika rejea pia ukurasa wa 189 ubeti wa  3761 – 3770 ambapo tunawaona Malaika wakijitokeza kusaidia majeshi ya Muhamadi katika vita.  Aidha kuna mhusika Ibirisi anajitokeza katika utendi huu, tunamwona ibirisi akijibadilisha maumbo ya watu mbalimbali ili kuwahadaa Waislamu, kwa mfano kuna wakati anajibadilisha na kuingia katika sanamu ni kuwahadaa watu kuwa yeye ni Mungu kama msimulizi anavyotuambia katika ubeti wa 473-476. Tuangalie beti chache:
              473. Ibilisi maluuni                                      475. Sikuzaa sikuzawa
        Achondoka iyo hini                                      Naua na kufufua
        Akangia sanamuni                                        Naumba nikiumbua
        Sultani kumghuri.                                         Ndimi wahidi Qahari.
Vilevile, kuna wakati ibirisi anajigeuza  Kharid mmoja wa masahaba wa Mtume Muhamadi na kwenda kuwaambia kuwapa taarifa za uongo kuwa Muhamadi ameuwawa. Rejea ubeti wa 2397- 2399. Kwa ujumla wahusika kama Lata, Uza na Manata, miungu ya uongo wa kike, Ibirisi na shetani ambao si binadamu wanajitokeza katika kazi hii.
Kwa upande mwingine sifa ya matumizi ya sintaksia au sarufi ya kisimulizi kama sifa ya utendi simulizi pia inajitokeza katika Utenzi wa Rasi ‘lGhuli. Wamitila (keshatajwa, 84) anaeleza muundo wa sintaksia unaweza kuwa msingi muhimu wa kuakisi jinsi mawazo ya mhusika au wahusika wa kifasihi walivyo. Sintaksia katika usimulizi ina maana upatanisho wa kisarufi unaoibua usimulizi fulani katika ngano mara nyingi hujitokeza viambishi vya -ki-. Hebu tuangalie ubeti wa 99 (ukurasa 5) na ubeti wa 353 ukurasa wa 18: anaposema;
99.Wakikamata wanangu                          353. Akishuka mualimu
Wakiwafunga kwa pingu                                   Ametukua alamu
Wakiwakusa matungu                                       Akibalighi salamu
Na mwenyewe hubusuri.                                   Akitikia Bashiri.
Hitimisho
Katika makala haya tumefanya uhakiki kwa kuchambua Utenzi wa Rasi ‘lGhuli kama unastahili kuitwa utendi wa Kiafrika na vilevile kama unafaa kuwekwa katika kundi la tendi za Kiswahili. ili kujibu maswali hayo tulijikita zaidi kuangalia vigezo vya utendi wa Kiafrika lakini pia tukaangalia utendi huo kama unakidhi vigezo vya kuitwa utendi wa Kiswahili kwa kumakinikia zaidi katika sifa pambanuzi za kifani na kimuundo za utendi wa Kiswahili. Ama kwa hakika baada ya kupitia vigezo hivyo na utendi husika tunakubaliana kuwa Utenzi wa Rasi ‘lGhuli kama tulivyoona hapo juu ni utendi unaokidhi sifa za kuitwa utendi wa Kiafrika kutokana na kukidhi vigezo vya utendi wa Kiafrika kama vilivyotajwa na Mulokozi (keshatajwa, 11) lakini pia unakidhi vigezo vya kuwa utendi wa Kiswahili na hii si kwasababu tu umeandikwa kwa lugha ya Kiafrika au Kiswahili ni kwa sababu umekidhi vigezo vyote vya utendi wa Kiafrika na Kiswahili.
[1] Majina mengine ya Mtume Muhamadi kati utenzi huu ni kama vile, ‘lBashiri, Mursali, Rasua, Rasuli
[2] Majina yake mengine yanayojitokeza katika utenzi, Shekhe Ali, Aba ‘lHasani, Haidari (samba), Imamu, Jabali Abu Qubesi
[3] Ni wilaya inayopatikana Tanzania Bara katika Mkoa wa Pwani.
[4] Shujaa ni mtu mwenye moyo thabiti anayeweza mambo hata kama ni ya hatari TUKI (1981:258). Aidha Mlokozi (1999:11) anataja sifa za shujaa kuwa ni nguvu za kimwili na nguvu za kiume, kuwa na nguvu za uganga na sihiri, kuwa na mshikamano na kundi au jumuiaya fulani.

Print this item

  SHAIRI: JAMANI SINA BAHATI
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:38 AM - Forum: Ushairi - No Replies

MTUNZI: IBN MAJOR ABDUL OMARY
Jama nanena jamani, mja nisokuwa jumu,
Jua naweka jamvini, waja msinihujumu,
Msijifanye jinuni, mkakosea hukumu,
Najishutumu jamani, Sina bahati janjuzi.
Janjuzi sina bahati, tokea kwangu zaoni,
Mama hakwisha jamati, kubembeleza manani,
Apate moja gameti, toka mwake fumbatyoni,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Ikamfikia zama, niwe la kwake pakato,
Pumzi ikawa zahama, mfumbati kwa fumbato,
Kinywa wazi akihema, akatoa mgong’oto,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Mgong’oto alotoa, pakato li hadharani,
Tabasamu akatoa, tabasamu la mwishoni,
Neno tena hakutia, furungu kawa kooni,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Kwenye gao la mkunga, nikawa najililia,
Sauti kama kipenga, za dunga kama shazia,
Nikafungwa mitulinga, nisiweze jihemea,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Hatima kwangu ikawa, kunyonya uji mseto,
Domo likafanywa bwawa, nikajifia kingoto,
Ikanijaa shakawa, kama lo ndani ya puto,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Jamaa waso maono, tuhuma wakanitia,
Mtoto asomavuno, jina baya wanitia,
Kumweka mama kibano, ikawa yangu hatia,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Mungu aso athumani, nuru akanangazia,
Vidato kwangu gambani, mabuku nikabukua,
Badala ya kauleni, digri nikachukua,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Japo njia so laini, wengi walinieleka
Sasa nala kilaini, ila roho yasongeka,
Majonzi tele mbonini, vile mama akopeka,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Masikitiko kibao, leo naitwa Janjuzi,
Mengi mazuri mafao, nala peke kama jizi,
Sikumpa kizibao, mama yangu wa kipozi,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.

Ila namwomba rabuka, mola wa zote sayari,
Yalo mema kutunuka, mama yangu wa sahari,
Aishi bila upeka, adumu kwa ufahari,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.

Print this item

  SHAIRI : SINA BAHATI
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:33 AM - Forum: Ushairi - No Replies

Mtunzi:RamaB.
Hivi hawa matajiri, walifanya kazi gani?
Kuondoa ufakiri, wakawa mamilioni.
Nipeni yao siri, iniingie kichwani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.

Nikalikamata jembe, panga na shoka begani.
Nikautoa uzembe, mpunga panda kondeni.
Ukajaliwa na ng’ombe, nikabaki kichwa chini.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaitwaa mashua, nikaitweka baharini.
Samaki kwenda kuvua, mingisi si saladini.
Wimbi kubwa la bamvua, chombo kikenda mwambani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Carina nikanunua, teksi bubu kituoni.
Abiria nangojea, ilala na buguruni.
Trafiki kaniotea, shitaka mahakamani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikauza vitumbua, asubuhi na jioni .
Wateja walinijua, ni gwiji la mtaani.
Mgambo wakang’amua, nauza bila leseni.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaenda mgodini, kujichimbia madini.
Nikaona sa nawini, naunga umasikini.
Magufuli kabaini, ninauhujumu uchumi.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Bunduki yangu begani, nikaingia porini.
Kuwawinda hayawani, kwenda uuza sokoni.
Wakaja nisweka ndani, segerea gerezani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikalipiga kabumbu, golikipa namba wani.
Nikawa kama mzungu, Ronado haoni ndani.
Nikavunjika mguu, nipo hoi taabani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaicheza singeli, asiyejua nani?
Wote walikubali, si Tandika si Mtoni.
Nikazushiwa kejeli, navuta bange kizani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Bora nirudi nyumbani, ni Mafia kisiwani.
RamaB ni mashakani, sijui nifanye nini.
Zaharia na kinyemi, mwenzenu nisaidieni.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Rabana nipe sahali, mja wako Ramadhani.
Mikiki nilo himili, na bado ni masikini.
Beti hizo ni kamili, peni naweka chini.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.

Print this item

  ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI'
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:27 AM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili - No Replies

HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI'

Neno rijali katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:

1. Nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: marijali ] mwanamume mwenye nguvu nyingi za kiume.

2. Nomino: [Ngeli: a-/wa-] mwanamume shujaa katika jambo.

Mshairi mmoja alipata kutongoa:

Ufukara jambo zito, aliloumba Qahari,
Mkubwa huwa mtoto, na rijali huwa thori,
Asemalo huwa ndoto, hakubaliwi shauri.

Katika lugha ya Kiarabu, neno hili rijali(soma: rijaalun/rijaalan/rijaalin رجال ) ni nomino wingi wa neno rajuli (soma: rajulun/rajulan/rajulin رجل) lenye maana zifuatazo:

1. Mwanamume mwanadamu aliyebalehe.

2. Mtu anayeshughulika na jambo fulani, rajulu Al-Aamaal (soma: Rajulul Aamaal رجل الأعمال mfanyabiashara.

3. Hali ya kutembea kwa miguu, rijaalan رجالا.

4. Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima moto, rijaalun رجال.

5. Wakongwe, wakubwa wa ukoo au jambo.

Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili badala ya kuchukuwa neno rajuli رجل lililo katika umoja, walichukua neno rijaali رجال lililo katika wingi na wakalipa maana ya neno rajuli رجل lililo katika umoja.

Shukran sana.

Khamis S.M. Mataka.

Print this item