Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 49 online users. » 0 Member(s) | 48 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
HISTORIA YA USHAIRI WA KISWAHILI |
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:25 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
Imeandikwa na Kornelio G. Maanga 22/1/2015
A.G. GIBBE (1980) akimnukuu Shaaban Robert anasema kuwa; Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa nyimbo mashairi na tenzi zaidi ya kuwa ni sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.
Mulokozi na Kahigi (1982) wanasema ushairi ni sanaa inayopambanuliwa kwa mpangilio maalumu na fasaha na wenye muala, kwa lugha ya picha, sitiari au ishara katika usemi, maandishi au maundui ya wimbo ili kuleta wazo au mawazo, kufunza au kuelekeza tukio au hisia fuani kuhusu maisha au mazingira ya binadamu kwa njia inayogusa moyo.
Hivyo basi tunaweza kusema kuwa ushairi ni kazi ya sanaa yenye kuandikwa au kimbwa kwa kufuata kanuni za ushairi ikiwa na maana kuwa ushauri waweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa ilimradi ushairi huo uwe na ujumbe.
Ushairi wa Kiswahili ni ule ushairi unaotumia lugha ya Kiwahili, utamaduni wa waswahili, lugha ya picha na lugha ya sitiari na wenye mtiririko mzuri na mpangilio wa maneno fasaha ili kufikisha ujumbe kwa hadhira.
Ushairi wa Kiswahili una historia ndefu sana. Ushairi simulizi wa Waswahili unasemekana kwamba ulikuwapo tangu lugha ya Kiswahili ilipoanza kutumika. Samweli na wenzake, (2013) wana wanukuu Mulokozi na Sengo kwa kusema kwamba si rahisi kueleza ni lini hasa ushairi simulizi wa waswahili ulianza. Hali hii inatokana na sababu kuu moja kwamba Wataalamu mbalimbali wamekuwa na mitizamo tofauti juu ya jambo hilo. Kama Swamweli na wenzake (2013) walivyomnukuu Knappert (1979) kuwa anadai ushairi andishi wa mwanzo wa Kiswahili ni Hamziya ulioandikwa mnamo mwaka (1652). Pia wamemnukuu Harries (1995) akidai ushairi wa mwanzo wa Kiswahili ni Tambuka(Tabuka) ulioandikwa mwaka 1728. Hata hivyo utafiti wa Mulokozi na Sengo unabainisha kwamba huenda wote wawili (Knappert na Harries) wamekosea na kuwa ushiri andishi wa mwanzo wa Kiswahili umekuwapo tangu wa Fumo Liyongo ambaye anaaminika kuishi karne ya 13 huko Pate katika pwani ya Kenya. Aidha utafiti huo unabainisha ushairi andishi wa mwanzo wa kiswahiili ni “Swifa kwa mwana wa Manga” unaojulikana pia kama “Tumsifu yanga” ambao unahusishwa moja kwa moja na Fumo Liyongo.
Tangu kuibuka kwa ushairi wa mwanzo wa Kiswahili hadi sasa ushairi huo umepitia historia ndefu sana na vipindi tofauti tofauti vya kihistoria. Tunaweza kuvigawa vipindi hivyo katika makundi makuu mawili; Kipindi cha kabla ya ukoloni na wakati wakati wa ukoloni. Kipindi cha kabla ya ukoloni tunaweza kukigawa katika makundi tofauti madogo madogo, kundi la kwanza ni kipindi cha ujima, na kundi la pili ni kipindi cha Ustawi wa miji, Utamaduni na tawala za Waswahili.
Kipindi cha kwanza, cha Ujima kilidumu tungu binadamu alipopata Urazini na kutoka kwenye Uhayawani ikikadiriwa hadi mwaka 600. Inadaiwa kwamba binadamu anatokana na Sokwe na alipitia hatua mbalimbali hadi kufikia kuwa mtu kamili (Homo Sapiens). Kipindi cha ujima kilianza pale binadamu alipopata Urazini na kuanza kuishi kama mtu kamili baada ya kutoka katika hali hiyo ya usokwe. Katika hatua za awali za kipindi cha ujima, binadamu waliishi kwa uwindaji na ukusanyaji wa matunda. Taratibu binadamu alipiga hatua na kuanza kuyatawala mazingira yake na kuanza kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kazi ya kilimo katika kile kinachoitwa mapinduzi ya kilimo (Neolithic Revolution). Mpinduzi haya ya kilimo yalisababisha maendeleo makubwa katika maisha ya binadamu na binadamu sasa wakaanza kuishi pamoja.
Katika kipindi chote hiki cha ujima, mwanadamu alishaibua ushairi kama njia mojawapo ya kujiliwaza wakati wa kufanya kazi. Hakuna ushaidi kuwa katika kipindi hiki kulikuwa na kazi nyingine za fasihi bali ushaidi uliopo unaonesha kwamba hiki kilikuwa ni kipindi kilichotawaliwa na nyimbo za kazi. Hivyo ushairi wa kazi unachukuliwa kuwa ndiyo ushairi wa mwanzo kabisa. Mwanadamu aliimba nyimbo mbalimbali wakati wa shughuli mbalimbali alizozifanya.(E. Senkoro, 1988) anasema kuwa ushairi huu wa awali ambao ulijitokeza zaidi katika nyimbo za kazi. Uliathiri hisia za mwimbaji na kumsukuma kufanya kazi kwa dhati zaidi na kumsahaulisha ugumu wa kazi ile. Anaendelea kueleza kwamba jukumu hili la nyimbo la kufanya kazi ngumu na nzito ionekane. Kutokuwa na hatari yoyote ndilo linaloonesha nguvu ya ushairi na hata wataalamu wengine wameipa nguvu hii sifa ya UCHAWI na kusema kuwa ushairi umetokana na uchawi. Nyimbo za kazi ziliendelea kudumu kwa muda mrefu na hadi sasa ingawa kuna mabadiliko makubwa katika utanzu wa ushairi. Nyimbo za kazi (ushairi wa kazi) bado umeendelea kuwa sehemu muhimu ya ushauri wa Kiswahili.
Kipindi cha pili ni kipindi cha Ustawi wa miji, utamaduni na tawala za waswahili kilidumu takrbani miaka 600 hivi (kuanzia mwaka wa 900-1500BK (Baada ya Kristo). Kipindi hiki kilimalizwa na utawala wa Wareno.
Kipindi hiki kipindi cha ustawi wa miji, utamaduni na tawala za waswahili kilidumu kuanzia karne ya kumi na kumi na sita. Kama tulivyoeleza hapo awali, ushairi wa Kiswahili unatokana na ushairi simulizi wa Kibantu. Ushairi huu ulihusisha majigamo, tondozi, pembezaji, mbolezi, nyiso, chapuzo na nyimbo za kazi na kadhalika. Mulokozi na Sengo kama walivyonukuliwa na Swamweli na wenzake (2013) wanabainisha kwamba kipindi hiki kilitawaliwa na tungo zilizodaiwa kuwa za Fumo Liyongo. Kutokana na mapokeo tunaambiwa kwamba mshairi wa kale zaidi anayefahamika ni Fumo Liyongo, ambaye inasemekana kuwa aliishi maeneo ya Shaka Kipini na Pate huko pwani ya Kenya katika karne ya 13.
Ingawa inaaminika kuwa Lyongo aliishi kabla ya karne ya 16 lakini tungo zinazomhusu (zilizotungwa na wengine) ambazo tunazo ziliandikwa mwanzoni mwa karne ya 19. Tungo hizo ni Takhmisa ya Liyongo (Sayyid Abdallah bin Ali inyayokadiriwa iliandikwa 1800) na “Utenzi wa Fumo Liyongo” (Muhamadi Kijumwa 1913) hata hivyo, tungo hizi za baadaye zilitokana na fasihi simulizi inayomuhusu Liyongo na iliyotungwa zama za Liyongo mwenyewe. Hivyo kwa kiasi fulani kimaudhui na kihisia zinaakisi kipindi 900-1500BK (kabla ya Kristo) tunachokizungumzia. Kwa hivyo, utendi wa Fumo Liyongo ndio utenzi wa kale zaidi katika tenzi tatu za kale (tenzi nyingine mblili ni
Utenzi wa Mwanakupona na utenzi wa Ali Inkishafi) ingawa umewekwa katika maandishi karne ya 20 Tazama (Mulokozi, 1999) Katika kitabu cha Tenzi Tatu za Kale.
Tungo za Fumo Liyongo zinahusu ustawi wa miji ya pwani, miji hiyo ni pamoja na Kilwa, Mombasa na Pate. Miji hii ilistawi kutokana na biashara ya bahari ya Hindi (Indian Ocean SlaveTrade) iliyoshamiri sana. Utendi wa Fumo Liyongo kwa mfano, unaelezea kuhusu kustawi kwa mji wa Pate alipoishi Liyongo. Utenzi huu ulitungwa kutokana na hadithi za kimapokeo kuhusu Fumo Liyongo miongoni ya waswahili. Hata hivyo masimulizi ya maisha ya Liyongo kama yanavyotokea katika utendi huo si kamili bali ni simulizi mojawapo tu ya maisha yake. Masimulizi mengine kama yanavyotokea katika nyimbo zake.
Kwa kuhitimisha tunaona kuwa ni kweli kabisa kuwa kabla ya uhuru na hata kabla ya ujio wa wageni ushairi wa Kiswahili ulikuwepo na ulikuwa na maendeleo kadha wa kadha. Pmoja na hoja kadha zilidhotumika katika kujadili historia ya ushairi wa Kiswahili kabla ya uhuru tunaona kuwa ushairi wa Kiswahili ulikuwa na dhima mbalimbali ikiwemo mojawapo ya kuhimiza kazi ambayo ndiyo iliyokuwa dhima kuu katika ushairi wa Kiswahili kabla ya ukoloni. Ushairi w Kiswahili hasa nyimbo za kazi ziliimbwa wakati wa kazi ngumu na kumburudisha mwimbaji na msikilizaji. Pia Ikumbukwe Kuwa nyimbo za kazi ndiyo Ushairi wa awali kabisa wa Kiswahili, ushairi huu pia ulipunguza uchovu wa watu hasa katika kazi kama vile kilimo, ufugaji, uwindaji na kadhalika. (Gibbe, 1980)(Samweli, Kabiero, & Seleman, 2013)(Mulokozi & Kahigi, 1982)
Marejeo
Gibbe, A. (1980). Mitaala ya Lugha na Fasihi. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Mulokozi, M. (1999). Tenzi Tatu za Kale. Dar es Salaam: TUKI.
Mulokozi, M., & Kahigi, K. (1982). Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Samweli, M., Kabiero, A., & Seleman, A. (2013). Ushairi wa Kiswahili. Dar es Salaam: Meveli Publishers.
Senkoro, E. (1988). Ushairi Nadharia na Tahakiki. Dar es Salaam: Dar es Salaam University Press.
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (1) |
Posted by: MwlMaeda - 01-11-2022, 07:22 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
Kitangulizi
Ushairi
umeonekana kwa baadhi kubwa ya waalimu na wanafunzi kuwa ni somo gumu sana, na hata kuogopwa. Kitabu hiki kimetungwa kwa makusudi ya kuuondoa woga huu. Kimeandaliwa ili kiwasaidie waalimu, wanafunzi na wapenzi wa ushairi wa Kiswahili kulikabili somo hili vizuri zaidi katika mdharia na uchambuzi wake. Katika sura mbili za mwanzo nimejaribu kutoa vigezo vya nadharia ili kutoa changamoto ya mjadala wa maana ya ushairi. Kwa vile kitabu kimelengwa basa kwa wanafunzi wa vidato vya 3-4, cheti cha ualimu daraja A, diploma ya ualimu, na kiasi fulani kwa wale wa vidato vya 5 na 6, nadharia zilizotolewa katika sura hizi zimerahisishwa kukidhi haja za viwango hivyo.
Baada
ya hapo nimehakiki vitabu kumi vya ushairi, vingi vikiwa ni vile vitumikavyo
katika mihutasari ya viwango vilivyotajwa. Sura ya nne imeandikwa na E.
Kezilahabi, mwenyewe akiwa ni mshairi na mwanazuoni maarufu. Sikuona haja ya
kukihakiki upya kitabu cha Sheikh Kandoro baada ya kuyaona makala haya ya Dkt.
Kezilahabi ambayo kwa hakika yanasadifu sana kiwango cha wanafunzi wa vidato
vya 3 na 4.
UCHAMBUZI WA MASHAIRI: VIDOKEZO
Ushairi
ni aina ya fasihi inayotofautiana na hadithi na tamthilia hasa katika umbo na
matumizi yake ya lugha. Wakati ambapo fasihi ya kinathari inatumia lugha ya
mjazo na ya mtiririko, ushairi hutumia lugha ya mkato yenye kueleza maudhui
yake kimuhtasari, na aghalabu huyaficha maudhui hayo ndani ya taswira na
ishara.
Kwa
hiyo basi, inakuwa muhimu kwa msomaji wa shairi kuwa tayari kwanza kupata maana
ya juu juu ya shairi analolikabili. Kwa maana hii, kwa mfano,
“siku ya mawingu mengi” si kitu kingine bali ni siku iliyojaa utando
wa mawingu angani. Baada ya maana hiyo ya moja kwa moja, msomaji wa shairi
anatakiwa afasili kauli hiyo ya “siku ya mawingu
mengi” kwa maana ya ndani; maana ya kiishara na
kitaswira.
Kwa
kawaida siku iitwayo nzuri ni ile yenye mbingu angavu, yenye ndege warukao na
kuimba nyimbo nzuri. Siku ya namna hii katika ushairi huweza kutumiwa kuwa
ishara ya furaha na amani; wakati amoapo “siku ya mawmgu mengi”
kushara huweza kuwakilisha kununa kwa mtu ambaye hana raha bali kajawa na
karaha.
Hatua
hii ya mwanzo huweza kumsaidia msomaii wa shairi ambaye huwa analikabili shairi
hilo katika ngazi zake hadi kufikia maana kamili.
Katika
kazi ya fasihi, hususan ile ya ushairi, huwa hakuha jibu au tafsiri moja tu.
Inategemea jinsi mpokeaji wa shairi atakavyolikabili shairi hilo tangu mwanzo,
mradi tu aweze kuthibitisha hoja zake kwa mifano dhahiri. Tuchukue mfano mdogo
ufuatao wa shairi la E. Kezilahabi, “Wimbo wa Kunguni” (Kichomi, uk.
20):
Mwanadamu kama huiui
Ndoa ni mkono karibu na goli
Na firimbi imelia
Golini namna mtu
Lakini goli upana futi moja
Viatu vimechanika, na mpira ni tofari.
Uwanja kijiji ndani ya nyumba.
Washangiliaji na wazomeaji wengi sana.
Maswati mengi kama nayo
Manung’uniko mengi kama hayo
Matatizo mengi kama hayo sasa
Yaonekana ingawa zamani hayakuwako.
Shairi
hili linahusu ndoa, kwa hiyo dhamira yake tunaweza kusema kuwa ni
“mabadiliko katika ndoa.” Mstari wa pili ndio unaotupa kidokezo juu
ya dhamira hii. Mshairi anaifananisha ndoa na mchezo wa mpira, lakini mchezo
wenyewe si mpira wa kawaida tuujuao kwani golini hakuna mtu, upana wa goli ni
futi moja, na mpira si huu wa kawaida uliojazwa hewa bali ni tofari. Hiki ni
kinyume cha mambo, nasi tumetakiwa na mshairi tuzichukulie tamathali hizi
kitaswira kuwa zinawakilisha ugumu wa maisha ya ndoa. Ndoa siku hizi ni
matatizo matupu, na mshairi anaonyesha kama vile kwenye mchezo wa mpira, katika
ndoa pia mmejazana washabiki: washangiliaji na wazomeaji.
Mpaka
hapa shairi halijaleta utata. Lakini tuanzapo kujadili jina la shairi pamoja na
mstari wake wa mwisho, utata unaanza. Kwa nini “Wimbo wa Kunguni”?
Maana mojawapo tuwezayo kuitoa hapa ni kuwa kwa vile kunguni hupatikana katika
vitanda vya watu masikini, basi katika shairi hili wimbo huu ni wa mtu
masikini. Kunguni ndiye mwenye fursa ya kuyaona na kuyasikia yote yatokeayo
kati ya mume na mke kwani analala kitanda kimoja nao. Kwa hiyo malalamiko haya
kuhusu ndoa yanatokana na udhati wa kuyaishi maisha ya ndoa chungu ya
kimasikini.
Maana
nyingine tuwezayo kuitoa kuhusu taswira hii ya kunguni ni ile ya mtu anayemtegemea
mwenziwe katika maisha yao ya ndoa, naye amebaki kulalamikia hali yao duni
akiwa kang’ang’ania katika uvivu wake wa kusubiri aletewe kila kitu. Huyu,
kutokana na kutofanya kazi, anaishilia katika manung’uniko, malalamiko, na
kutokuridhika.
Mstari
wa mwisho unaweza pia kuwa na maana zaidi ya moja. Mathalani, kwa wengine
mstari huu huweza kuwa na maana kwamba ndoa za siku hizi, kinyume na za zamani,
zimejaa machungu mengi. Kwa baadhi ya wasomaji mstari huu unaweza kuchukuliwa
kuwa ni sehemu ya malalamiko ya mtu mmoja kwa mwenziwe kuhusu ndoa yao ambayo
mwanzoni ilikuwa nzuri lakini sasa imegeuka kuwa karaha tupu.
Kutokana
na haya, tumeona jinsi shairi moja liwezavyo kujadiliwa na kupewa maana zaidi
ya moja na bado maana zote zikakubalika kufuatana na hoja zilizotolewa na
uthibitisho ulioambatana na hoja hizo.
Ziko
njia kuu mbili ambazo huweza kutumiwa kuchambulia shairi. Njia ya kwaoza
hupitia vipengele mbalimbali vya shairi, kimoja hadi kingine. Kwa njia hii
mhakiki huangalia sehemu mbalimbali za fani na maudhui kama vile dhamira,
maana, ujumbe, falsafa, matumizi ya lugha, taswira na ishara, vina na mizani
(kama ipo), na kadhalika. Njia hii ndiyo ambayo nimeitumia sana katika tahakiki
zilizomo humu kitabuni.
Mbinu
ya pili ni ile ya kulichambua shairi hatua kwa hatua kutoka ubeti mmoja hadi
mwingine.
Mara
nyingi, uchambuzi wa mashairi huchukua njia zote mbili, ijapokuwa uamuzi wa
mhakiki kutumia njia hii ama ile hutegemea pia shairi linalohusika. Hata hivyo,
mara nyingi njia ya pili ina hatari kwani huweza kuishia katika kufasili tu na
kuyaeleza kinathari yale yanayojitokeza katika shairi.
Kwa
jumla, katika uchambuzi wa mashairi au hata wa washairi, maswali yafuatayo
huulizwa:
1. Je, mshairi
ninayemshughulikia ni wa aina gani? Historia ya maisha yake ni ipi? Ina mchango
gani wa moja kwa moja katika fani na maudhui ya ushairi wake?
2.
Ni dhamira gani kubwa na ndogo zinazojitokeza katika ushairi wake? Je, dhamira
hizo zina nafasi gani katika jamii ya leo? Na kama ni mshairi wa zamani,
dhamira hizo zilikuwa na nafasi gani katika jamii ya mshairi ya wakati huo?
3.
Kutokana na ushairi wake tunaweza kusema mshairi anao msimamo au mtazamo
maalumu unaojitokeza mara kwa mara, au mshairi huyo huwa anaandika tu kuhusu
mambo yanayomgusa na kumuathiri kwa wakati huo? Iwapo ana msimamo maalumu, ni
upi na unabeba falsafa aina gani?
4.
Fani iliyotumiwa katika shairi au mashairi yanayohusika ni ya aina gani? Kwa
mfano, mshairi katumia lugha ya aina gani? Taswira azitumiazo ni za aina gani?
Je, katumiaje viegezo vya vina na mizani (iwapo ni ushairi wenye vina na
mizani), mitindo, muundo, na mbinu nyinginezo za kisanaa?
5.
Iwapo zipo kazi nyingine za ushairi au hata washairi wengine wanaoshabihiana na
mshairi anayehusika, wanafanana ama kutofautianaje katika fani na maudhui ya
mashairi yao na ya mshairi huyu? Au ikiwa mshairi anayechunguzwa ni wa pekee,
ni sifa gani za kifani na kimaudhui zinazompa upekee huo?
Haya
ni baadhi tu ya maswali muhimu ambayo yafaa yatiliwe maanani na walimu na
wanafuna wa ushairi.
Ni
matumaini yangu kuwa iwapo vidokezo hivi pamoja na nadharia na tahakiki
mbalimbali humu hazikufaulu kuyajibu maswali ya wanafunzi na waalimu kuhusu
ushairi, walau zimeelekeza kwenye chanzo cha majibu ya maswali hayo.
Shukrani
Nawashukuru
Bibi Demere Kitunga-Chachage na Bwana Justin Mallya kwa kazi waliyoifanya
kuuhariri mswada wa kitabu hiki pamoja na mapendekezo yao mengi kuhusu maudhui
yaliyomo humu. Pia ninawashukuru E. Kezilahabi, M.M. Mulokozi, K.K. Kahigi,
M.L. Balisidya-Matteru, N.O. Mmbaga, E.N. Hussein, G. Ruhumbika, J. Madumulla,
na Nyalobi Mayunjanda Gibbe kwa maoni yao waliyoyatoa wakati wa mijadala ya
ushairi.
Tunawashukuru
waandishi na wachapishaji wa vitabu mbalimbali vilivyohakikiwa humu. Mwisho
shukurani na upendo mwingi kwa Chichi, Mbazi na Aisha walioithamini kazi
niliyokuwa naifanya, wakanipa moyo kuwa jasho la akili ya mtu humpatia na
kumsongea ugali.
F.E.M.K. Senkoro
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Juni, 1987.
|
|
|
SHAIRI: SINA NAFUU -2 |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 10:32 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
SINA NAFUU
Kula mie ninakula, bila kula sijilazi,
Langu tatizo kulala, japo ni mema malazi,
Najaribu Ila wala, siupati usingingizi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Daima ninamuwaza, mwendani wangu lazizi,
Vile ananipuuza, ninakonda siku hizi,
Hata nikimueleza, hunita mie mpuzi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Ashiki mwili mzima, kuhimili siiwezi,
Jamani nisijezima, inikatike pumzi,
Msione nalalama, hali yangu sijiwezi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Usiku wa katikati, ninakesha kama mwizi,
Nadhani sina bahati, au tatizo ujuzi,
Moyo wangu hatihati, yanimwagika machozi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Kiwa kuna matibabu, inifae hiyo dozi,
Niondokewe taabu, niwe kama mwaka juzi,
Leo yanayonisibu, kusimulia siwezi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Ninazidi kuteseka,vile sina muuguzi,
Wengine wananicheka, eti mie siyawezi,
Donda limenifumuka, maumivu hayapozi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Kitu niwaambiacho, kilianzia miezi,
Chaniweka wazi macho, ninakosa usingizi,
Nipatacho sicho ndicho, ananitesa lazizi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Anaitwa Raphael, Rukwa ndo yake makazi,
Ananifanya silali, ninakonda siku hizi,
Najiuliza maswali, ingawa hasikilizi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Au walivyo wafipa, wakipewa hii kazi,
Mapenzi anayonipa, hebu niyaweke wazi,
Si mnofi ni mfupa, wala hauna mchuzi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Hata nikipiga simu, kitufe hakibonyezi,
Swali langu la muhimu, au mie haniwazi?
Naona Bora kalamu, niishushie pumzi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Tungo ndefu zinachosha, Jueni kusoma kazi,
Beti sitateremsha, japo yote sielezi,
Mapenzi yananichosha, shikeni habari hizi,
Yananitesa mapenzi, mwenzenu sina nafuu.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU' |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 10:28 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
- No Replies
|
|
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU'
Neno *kuntu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:
1. *Kihisishi:* Neno linaloonyesha ukubalifu wa moja kwa moja katika moyo wa mtu; sawasawa, barabara, hasa. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili).
2. *Kielezi:* Sawasawa, bila ya shida yoyote. (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21).
3. *Kielezi:* Kwa ufupi, kweli, hakika; hasa; kabisa; ndivyo. (Chanzo: Kamusi Teule ya Kiswahili).
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kuntu *(soma: kun + tu كنت* ) ni kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita *fiilu maadhwi فعل ماض* kwa nafsi ya kwanza, chenye maana ya: nimekuwa/nilikuwa.
Kitenzi hiki kimenyumbulika kutokana na kitenzi cha Kiarabu *kaana كان* amekuwa/alikuwa.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *kuntu كنت* lilipoingia katika Kiswahili lilipewa kategori ya kihisishi/kielezi na kupewa maana mpya tofauti na maana yake ya awali katika lugha ya Kiarabu ya kuwa kitenzi chenye maana ya: nilikuwa/nimekuwa.
*Shukran sana.*
*Khamis S.M. Mataka.*
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (5) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 12:50 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
4. Saadani A. Kandoro: Mashairi ya Saadani
SURA YA NNE
Na E. Kezilahabi
Bwana Saadani Abdu
Kandoro alizaliwa Kasingirima Street, Ujiji, Mkoa wa Kigoma tarehe 8 Desemba,
1926. Baada ya masomo ya Shule ya Primary Ujiji aliendelea na masomo yake
Government School Iringa, Mwanahela School na Teachers Training School Bwiru.
Mwaka
1944, Bwana Kandoro aliingia katika Idara ya Kuweka Hazina Uyui Tabora. Katika
miaka iliyofuata alishughulika sana kuanzisha Vyama Vya Ushirika na Ustawi wa
Jamii ya Waafrika na hatimaye alikuwa Diwani wa kwanza katika Advisory Council
ya Mji wa Tabora. Katika mwaka 1952 alikuwa Provincial Secretary wa Tanganyika
African Association, Lake Province. Mwaka 1954, alikuwa miongoni mwa watu 17
walioanzisha Chama kitukufu cha TANU mjini Dar es Salaam.
Maneno
haya tunayosoma karibu na picha yake kwenye jalada la kitabu yanatosha
kuonyesha kuwa Bwana Kandoro ni mwanasiasa, na maandishi yake ambayo
tunayajadili katika makala haya hayako mbali naukwelihuu.
Katika
dibaji ya kitabu hiki Bwana Mnyampala anasema “ilikuwa vigumu kuweza
kupambanua baina ya tungo za Sheikh Amri na mpwae huyu Sheikh Kandoro.”
Hii si kweli, maana mengi ya maandishi ya Amri Abedi yaliambatana sana na
misingi ya dini wakati ya Kandoro yanamhusu hata mwanadamu katika jitihada ya
kushindana na mazingira yake.
Katika
muhtasari wetu wa Kiswahili imeandikwa kwamba baadhi ya mashairi yaliyomo
katika kitabu hiki tunayaona katika Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani
ya Amri na tofauti hizi si ndogo. Nafikiri Kandoro angeweza kutunza
majina yale yale na mahali ambapo ameongeza beti ingekuwa bora kama angeeleza
hizo beti zimetoka wapi. Jambo hili ni muhimu sana maana linaweza kumpa shaka
mhakiki. Kosa kama hili lilitendeka pia kwa baadhi ya maandishi ya Shaaban
Robert.
Udhaifu
mwingine wa Bwana Kandoro tunauona katika muundo wa mashairi yake. Huu si
udhaifu wa Kandoro peke yake, ni udhaifu wa washairi wengi wa siku hizi. Karibu
mashairi yote yaliyomo kitabuni ni ya mizani kumi na sita na mistari ni minne,
yaani tarbia. Mashairi ya aina ya tathlitha, takhmisa na ukawafi hatuyaoni
kabisa. Sifa hii anayo Shaaban Robert na inaonekana washairi wa siku hizi
wameshindwa kuvaa taji lake. Wale ambao wamejaribu kulivaa naona limcwapwaya.
Katika
dibaji hayati Mnyampala anatwambia: “Bwana Kandoro ni mshairi maarufu sana
nchini Tanzania.” Watunzi wenye fani ya Bwana Kandoro ni haba sana leo.
Wenye fani sawa na yake walikuwa akina marehemu Sheikh Shaaban Robert na
mjombae Sheikh Kaluta Amri Abedi n.k. Lakini mimi naona Kandoro bado anao
udhaifu mwingine. Ukisoma kwa uangalifu baadhi ya mashairi yake utaona kwamba
ameiga mno ushairi wa Muyaka. Kwa mfano shairi la “Usione Kwenda
Mbele” (uk.32) halina tofauti sana na shairi la Muyaka liitwalo
“Kurudi Nyuma si Kazi.” Katika shairi la Kandoro liitwalo “Baada
ya Dhiki Faraja” (uk.l29) tunasoma:
Baada ya dhiki faraja,
Muyaka alifumbua
Uendepo ngezi maji, kwa safari ya mashu wa
Hapo ukumbuke mbiji, ya kutweka na kutuwa
Muyaka alifumbuwa, baada ya dhiki faraji.
Ubeti
huu unatukumbusha mashairi mawili ya Muyaka “Baada ya Ohiki Faraji”
na “Simba wa Maji”. Vile vile shairi la Kandoro liitwalo “Kimya
Kina Mambo Mbele” (uk. 133) linafanana sana na shairi la Muyaka liitwaio
“Kimya” ingawa Kandoro kalitumia katika mazingira tofauti.
Baada
ya kujadili kwa kifupi udhaifu wa Kandoro mshairi, na ingawa si kawaida kuanza
na udhaifu, inafaa sasa tuone upande wake mzuri ambao nafikiri utachukua nafasi
kubwa zaidi.
Mashairi
yaliyomo kitabuni si ya mtu mmoja. Yamo pia mashairi ya Amri Abedi, Mathias
Mnyampala, Abubakari Mohamedi Mikdadi, Maria Rajabu, Salehe Tambwe, na
wengineo. Katika ufafanuzi wangu wa masbairi ya Kandoro nitatumia yale yaliyo
yake, na yale ya wengine nitakuwa nayataja tu inapohitajika – naona vigumu
kupima uwezo wa mtu kwa kutumia maandishi ya watu wengine.
Tabia
ya Bwana Kandoro imeelezwa vizuri sana na Sheikh K. Amri Abedi katika Utenzi
wa Saadani tuuonao mwanzoni mwa kitabu. Beti hizi tano zatukumbusha
machache tu kuhusu tabia yake.
Wema wake kwa yakini
Umemvutia shani
Ingawa kiduniani
Hupendezi wote pia.
Kwa kuwayu muhsani
Hufikiwa na wageni
Wajuu hata wa chini
Hupenda kufikia.
Hujitia mashakani
Ili kuridhi wageni
Hujingiw hatarini
Ili kuwatumikia.
Kijana mwenye makini
Ana nguvu ya maoni
Ana busara kichwani
Mengi hum wongokea.
Mwamuzi wa hisani
Watu wamtumaini
Uzukapo ukindani
Nduguze humuendea.
Shairi
lake la kwanza “Staharaki” (uk. 10) laeleza maana ya jina lake la
ushairi. Anaeleza kwamba hataharaki kwa tendo – hana haraka katika kutenda
jambo, haghadhabiki na hakasiriki upesi.
Ndiye mimi Saadani,
muendapole wa mwendo
Abdu si la utani, jina langu la upendo
Kandoro wangu ubini, baba simuweki kando
Sitaharaki kwa tendo, msonijua jueni.
Msonijua jueni, staharaki kwa tendo
Tendo nikilibaini, silifanyii vishindo
Vishindo ulimbukeni, limbuko si wangu mwendo
Staharaki kwa tendo, msonijua jueni.
Staharaki starani, staha wangu mtindo
Staharaki tatmi, kupigwa hata kwa nyundo
Staharaki kutamani, moyo huupigafundo
Staharaki kwa tendo, msonijua jueni.
Mshairi
ametumia mtindo mzuri wa kuandika maelezo kidogo ya mashairi yake. Jambo hili
karibu ni lazima katika ushairi wa Kiswahili. Mashairi mengi ya Kiswahili, hasa
yale ya tambo na malumbano, ni vigumu sana kueleweka kwa watu wasio’ua chanzo
au asili ya kuandikwa kwa mashairi hayo. Lakini Bwana Kandoro ameeleza kidogo
maana ya mashairi fulani fulani, asili ya kuandikwa, na pengine wakati au mwaka
shairi hilo lilipoandikwa. Maelezo haya tunayapata katika kila mwanzo wa
shairi. Maelezo yake si mengi sana kiasi cha kumtafunia msomaji. Yanatosha
kuwekamsirigi unaohitajika.
Tuchunguze
kidogo jinsi Kandoro anavyoanza mashairi yake. Mara fulani fulani Kandoro
anaanza mashairi yake kwa kishindo. Tazama kwa mfano, mwanzo wa
shairi liitwalo “Mnapowacha Madogo na Makubwa Mtawacha” (uk. 25):
Amkeni kumekucha,
wakubwa hata wadogo,
Wadogo sikuwaacha, kwa kuogopa kinyongo,
Kinyongo sikukificha, kukificha ni wongo,
Mnapowacha madogo, na makubwa mtawacha.
Tutazame
mfano mwingine kutoka shairi liitwalo “Kigeugeu” (uk.22):
Kigeugeu geuka,
kupinduka ni ulema
Ni uleme kupinduka, geuka ziso hekima
Kila mara kugeuka, ni kuharibu heshima
Kigeugeu si chema, kila mara kugeuka.
Katika
shairi lake jingine liitwalo “Shujaa Haogopi Kitu Kilicho Halali
Yake” (uk. 66) tunaona mwanzo huu.
Nisemayo muyashike, hii
nishmri letu
A kuitae mwitike, tuendeshe mambo yetu
Shujaa na kitu chake, hadhulumiwi na mtu
Shujaa hahofu kitu, kilicho halaliyake
Vilevile
tunapata mfano mwingine katika shairi la “Mkamia Kifo Nani?” (uk.
54).
Wasomaji kutaneni,
pimeni inavyosema
Yatieni akilini, kwa busara na hekima
Tumekaa duniani, mambo mengi tunasema
Kufa mtu ni lazima, mkamia kifo nani?
Mifano
hii inatosha kueleza jinsi Kandoro anavyoanza inashairi yake kwa kishindo.
Tunasikia sauti yenye nguvu, sauti ya mtu mzima akizungumza, sauti ya mtu
anayejua anachokizungumzia. Mwanzo kama huu husaidia kuamsha ari ya msomaji ya
kutaka kuendelea.
Dhamira Kuu
Sasa
tuone mawazo yake makuu yanayojitokeza katika kitabu uki. Mawazo haya
nitayajadili katika mafungu matano:
1. Mawaidha
yanayoambatana na misingi ya dini
2. Uvumilivu katika maisha
3. Uhusiano wake na Amri Abedi, na wenyeji wa Mafia
4. Ukoloni
5. Baada ya Uhuru
Misingi ya Dini
Katika Mashairi
ya Saadani tunaona mashairi fulani fulani ambayo yanaambatana sana na
misingi ya dini. Katika shairi liitwalo “Ihsani” (uk. 30) mshairi
mwenyewe anatupa kwanza maelezo haya: “Shairi hili linajieleza lenyewe
jinsi ya kuwafanyia ihsani viumbe na ubora wa kutenda ihsani, yaani wema.
Inaeleweka katika mafunzo ya dini mbalimbali kwamba ukiwa mtenda mema japo
uwatendeao wakulipe nuksani, yaani ubaya, mbele ya Mungu utalipwa wema
wako.”
Japo fakiri niwa,
usikini na fukara
Na ubaya kufanyiwa, na kunionya ishara
Na matendo kulipiwa, ya faida na hasara
Isani kitu bora, mtenda na mtendewa.
Wazo
hili kidogo sikubaiani nalo maana lina sehemu ndogo sana katika ulimwengu wa
leo, ulimwengu wa kuoneana kisiasa, kiuchumi na kadhalika. Nashangaa kuona
Bwana Abdu Kandoro akileta tena wazo la kupigwa shavu na kutega shavu la pili
kwa tegcmeo la kulipwa na Mungu baadaye. Wazo hili linarudiwa tena katika shairi
liitwalo “Binadamu Tenda Wema” (uk.18).
Katika
shairi liitwalo “Moyo Maovu Sifate” (uk. 31) tunamsikia rnshairi
akiuonya moyo wake:
Moyo wanambia kata, kitu
cha watu sikate
Moyo wanambia vuta, kitu cha watu sivute
Moyo wanambia ita, usomjua simwile
Maovu moyo sifate, utanitia matata.
Uvumilivu Katika Maisha
Uvumilivu
na kufanya kazi kwa bidii ni wazo mojawapo kubwa ambalo linaweza kujadiliwa
pekee. Kwa kifupi tunaweza kusema kwamba Mashairi ya Saadani ni kitabu
kinachoonyesha jitihada ya Bwana Abdu Kandoro katika kujiendeleza mwenyewe,
matatizo aliyoyapata, na hatimaye kufanikiwa kwake. Tunamwona yeye na rafikiye,
Tambwe, wakikazana wapate kujisukuma mbele katika maisha. Kwa upande wa Bwana
Kandoro, amefanikiwa sana katika maisha. Amepata kuwa · mkuu wa wilaya, na hakuna kufanikiwa
kuliko kutenda jambo ambalo umma unalitambua. Katika “Naisubiri
Subira” (uk. 61) tunamsikia akisema:
Mpaka kubahatisha, ndipo
upate bahati
Bahati yafurahisha, mbeleya watu umati
Aipatae hutisha, akawekwa katikati
Mtu hapati bahati, mpaka kubahatisha
Bahati kuimarisha, yataka umadhubuti
Mpaka umejichosha, kazi yako kudhibiti
Kazi yako imarisha, usiiwachie kati
Mtu hapati bahati, mpaka kubahatisha
Bwana
Kandoro anapoanza kuona matunda ya kufanikiwa kwake maishani anasema katika ‘Usiku
Ukikomaa Karibu Kupambazuka’ (uk.77):
Kipigo ukapigika, mfano
wa kulemaa
Ndipo juto hukuftka, wakati wa kuchumaa
Na kupona kutafika, usiondoe tamaa
Usiku ukikomaa, karibu kupambazuka.
Amri Abeid na Weayejt wa Mafia
Uhusiano
uliopo kati ya Kandoro na Amri Abedi umechukua pia sehemu kubwa kitabuni, nao
umezungumziwa si katika kitabu hiki tu bali pia katika baadhi ya mashairi
yaliyopo katika kitabu cha Amri Abedi cha Sheria za Kutunga Mashairi na
Diwani ya Amri. Hapa tunaweza tu kufupisha mazungumzo haya kwa kutumia
maneno ya Mathias Mnyampala yaliyomo katika Jarida la Kiswahili Toleo
35/1 Machi. 1965.
Mgogoro ule ulioanza
wakati wa kuoana kwao yeye na mkwewe, Shami ulizuka tena. Fitina hiyo siwezi
kuieleza hapa bali kila mmoja anaweza kuona na kusoma mashairi yaliyomo katika
kitabu cha Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Kisa
na mkasa vimeelezwa humo. Bwana Saadan Abdu Kandoro alijitahidi sana
kupatanisha ugomvi huo. Juhudi hiyo ilifaulu kidogo tu na mwaka 1951 Sheikh
Amri Abedi alimtaliki Bi Shami Binti Sudi baada ya mgogoro mkubwa sana.
Kati
ya mashairi yanayoweza kugusa sana msomaji ni lile la “Mola Muweke Peponi
Mjomba Wangu Kaluta” (uk.50), shairi juu ya kilio cha Bwana Kandoro kuhusu
kifo cha Amri Abedi.
Makiwa yamenipata,
imenishika huzuni
Meno ninajikeketa, nimeku wa msibani
Kandoro na ata-ata, la kushika silioni
Mola muweke peponi, mjomba wangu Kaluta.
Njiani ninapopita, mawazo tele moyoni
Msiba niliopata, kifo cha mwanachuoni
Kifo cha Sheikh Kaluta, kimemkaba yakini
Mola muweke peponi, mjombo wangu Kaluta
Jjapo tutamfata, kifo hakina fulani
Sikitiko ni kujuta, tulobaki mashakani
Maisha mwenye kufua, mwenye nguvu ni Manani
Mola muweke peponi, mjomba wangu Kaluta.
Ukoloni
Kuanzia
ukurasa wa 124 hadi 164, tunaona mashairi ya kisiasa. Mashairi ya kisiasa
yanachukua sehemu kubwa kitabuni kuliko mashairi ya aina nyingine. Bwana Abdu
Kandoro – kama tulivyosema hapo awali – ni mmoja katika watu kumi na saba
walioanzisha chama cha TANU mwaka 1954. Ni mmoja kati ya watu waliokazania sana
uhuru wa Tanganyika miaka ile ya ukoloni. Bwana Kandoro alipigania uhuru kwa
njia mbili: kimatendo na kimaandishi. Katika mashairi yake haya sehemu zote
mbili tunaziona. Tunamwona anasafiri kwenda Mwanza kwenye mkutano wa kisiasa. Kwa
upande wa maandishi Bwana Kandoro lazima apewe sifa kubwa sana kwa ujasiri
aliokuwa nao – ujasiri wa kuandika mashairi yaliyokashifu serikali ya mkoloni
wakati (mkoloni) akiwa bado nchini akitawala. Watu wachache sana walionyesha
ujasiri huu wa kumpinga mkoloni. Washairi waliotaka kujipendekeza kwa wazungu,
au walifanya hivyo kwa woga – wakiogopa utawala wa mkoloni! Lakini Bwana
Kandoro ni kinyume cha waandishi kama hao. Sikiliza kwa mfano, sauti yake ya
hasira katika shairi la “Kwetu Ni Kwao Kwa Nini? (uk. 139).
Mtu kuuliza nini, kitu
hiki cha nini?
Kitu hiki ni cha nani, na hiki kitu cha nini?
Nacho kinailwa nim, ni cha nani na kwa nmi?
Kwetu ni kwao kwa nini, na kwao kwetu kwa nini?
Na kwa nini cha nani, na chake kwa njia gani?
Jawybu liweyakini, lisiwe purukshani?
Kwa nini sababu gani, kwao ni kwetu kwa nini?
Kwetu ni kwao kwa nim, na kwao kwetu kwa nini?
Kwa nini kwao kwa nini, kuwe kwetu ni kwa nini?
Na kwetu pia kwa nini, kuitwa kwao kwa nini?
Kwa nini ina yakini, kwetu ni kwao kwa nini?
Kwetu ni kwao kwa nini, na kwao kwetu kwa nini?
Mtu kwao kuthamini, ijapokuwa jiweni,
Pia alale mtini, na baraza liwe chini
Nile matunda porini, kuitwa kwenu kwa nini?
Kwetu ni kwao kwa nini, na kwao kwetu kwa nini?
Wakati
Sheikh Amri Abedi alipokuwa kule Missionary College Rubwa, Pakistan, Bwana
Kandoro alimuandikia shairi la “Siafu Wamekazana” ili kumjulisha
maendeleo ya wananchi katika kupigania Uhuru. Ni shairi la kiwango cha juu
sana, lakini hapa nitadondoa beti mbili tu:
Nyoka amegutuka, ndani
ya shimo katuna
Tena amekasirika, hasira zenye kununa
Nyoka anababaika, shimoni kwa kujikuna
Siafu wamekazana, nyoka amekasirika.
Shimoni ataondoka, hilo nataja kwajina
Nyoka anajuwa fika, siafu wakiungana
Nguvu zinaongezeka, shimoni watagombana
Siafu wamekazana, nyoka amekasirika.
Baada ya Uhuru
Jambo
la mwisho ambalo nitagusia ni mashairi yake yaliyoandikw, baada ya uhuru.
Katika mashairi haya tunamwona Kandoro huko Mafia akiwa mkuu wa wilaya hiyo, na
jinsi anavyoshirikiana na watu na kuwahimiza wafanye kazi kwa bidii. Mhakiki wa
kitabu hiki anasema:
Washairi wengine nyoyo
zao huguswa zaidi na vitu kama uzuri wa umbile la dunia, mabonde, milima, ndege
n.k. Wengine huguswa zaidi na fikira za upeo mbali mbali kama vile mwenendo
mwema, imani kwa Mungu, ubaya na wema katika maisha n.k. Bwana Kandoro anaguswa
zaidi na watu wenzi wake, sahiba zake, na hata wapinzani wake.
Mashairi
aliyoandika baada ya uhuru yanatufikisha kwenye upeo wa maisha yake. Kwa
kumalizia tunaweza kusema kwamba Bwana Kandoro ameweka msingi mzuri sana kwa
washairi wa Tanzania – nchi ambayo inajali zaidi watu kuliko uzuri wa milima na
mabonde wanamoishi.
Maswali
1.
Ijadili dhamira ya uzalendo ijitokezavyo katika Mashairi ya Saadani.
2.
Tumia shairi la “Siafu Wamekazana” ujadili matumizi ya taswira katika
kujenga dhamira ya shairi hili.
3.
Chagua dhamira kuu tatu zijitokezazo katika Mashairi ya Saadani ujadili
kufanikiwa au kutofanikiwa kwa mwandishi katika kuziibua dhamirahizo.
4.
“Katika Mashain ya Saadani tunagundua mshairi ambaye yu mwanasiasa tangu
mwanzo hadi mwisho.” Jadili.
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (8) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 09:49 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
7. K.H.A. Akilimali Snow-White: Diwani ya Akilimali
SURA YA SABA
Utangulizi
Akilimali Snowhite ni miongoni mwa washairi wachache wa enzi wa akina Sbaaban Robert ambao tuna bahati ya kuwa nao leo hii. Wenzake wengine tunaowcza kuwataja ni akina Sheikh Saadani A. Kandoro, na Shaha wa Malenga Mwinyihatibu Amiri. Hawa na wengine kama akina Shaaban Robert, Mathias Mnyambala na K. Amri Abedi ndio walioendeleza jadi ya kimapokeo katika ushairi wa Kiswahili. Kwa mfano, katika ushairi wao kanuni za vina na mizani zilizingatiwa kuwa ni sheria, ijapokuwa hapa na pale baadhi yao (akiwemo Shaaban Robert) walikiuka “miiko” hiyo. Haya yote yanajitokeza kwa namna hii ama ile katika Diwani wa Akilimali.
DHAMIRA KUU
Katika “utangulizi” wa diwani hii, K. Amri Abedi ametoa muhtasari mzuri kuhusu maudui wa mashairi ya Diwani ya Akilimali kama ifuatavyo katika (uk.iii):
Quote:Mashairi haya mazuri yanaeleza kwa wingi mwendo wa siasa wa vijana, na maonyo na maagizo, pamoja na hekima ya mambo yenyewe kwa namna yanavyofasirika katika maoni ya mtungaji wetu stadi. Baadhi ya mashairi ni jawabu ya mashairi yaliyoandikwa na watungaji wengine… Baadhi ya mashairi haya ni mashangilio au masimango. Baadhi ni maombi au dua. Na merigine ni mashairi yanayohusu mapenzi, ndoa na talaka. Mashairi merigine yamo katika sura ya fumbo…
Kwa maneno haya, K. Amri Abedi amemrahisishia mwalimu na nwanafunzi kuyagawa mashairi haya kidhamira, japokuwa si lazima kufuata mpango huu.
Katika kuyajadili maudhui ya diwani hii, sura hii itachunguza jumla ya dhamira sita ambazo ndizo kuu bumu:
Quote:1. Mapenzi
2. Maadili na maana ya maisha
3. Ndoa na nafasi ya Mwanamke katika jamii
4. Umuhimu wa kazi
5. Siasa
6. Dini na Mungu.
Mapenzi
Karibu theluthi nzima ya mashairi ya Diwani ya Akilimali inashughulika na dhamira ya mapenzi au mahaba baina ya wanaume na wanawake. Kati ya mashairi havo yamo ya “Daima Nilikiwaza” (uk. 5), “Enenda Mwana Kunenda” (uk. 8), “Gud Bai Mai Diri” (uk. 11), “Kupenda Kimasikini” (uk. 27), “Kwako Nina Tadhalali” (uk. 30), “Laiti ukisubiri Utapoa Moyo Wako”, (uk. 30), “Mapenzi Niliyo Nayo” (uk. 31), “Nala Nikimetameta Moyo Wangu Umetua” (uk. 49), “Nini Dawa ya Mapenzi” (uk. 50), “Nisipomtunza Wangu Nikamtunze wa Nani?” (uk. 52), “Ni Tangu Huniulizi Nimekonda Taabani” (uk. 52), “Nimemshika Mnana” (uk. 53), “Nisalimiye Hidaya” (uk. 55), “Pendo” (uk. 57), “Penzi” (uk. 57), “Sipotaka Niwe Nawe” (Uk. 65), “Simbulizi” (uk. 65), “Tangu Tumefarakana” (uk, 66), “Ua la Moyoni Ua” (uk. 67), “Usiponipenda Wewe” (uk. 70), “Umenipunguwa Hiba” (uk. 70), na “Wazuri Wanao Semwa” (uk. 76).
Mashairi yote hayo yanatoa nyuso mbalimbali za mapenzi na mahaba. Kwa mfano, shairi la “Daima Nilikiwaza” linaonyesha dukuduku linalokuwapo baina ya wapendanao, hasa pale ambapo ulikuwapo ukimya wa kutokuandikiana kati yao.
Katika shairi la “Enenda Mwana Kunenda” tunauona uso wa pili wa sarafu ya mapenzi: kuwa mapenzi siyo mito ya asali na maziwa daima dumu. Katika mapenzi kuna kufarakana na kugombana, pamoja na kukwaruzana hadi hata kuamua kutengana:
Quote:Nimechoshwa na vituko, daima vina nikifu,
Moyo sinapumvko, bali mwingi usumbufu,
Enenda ondoka vyako, moyoni unanikifu,
Quote:Quote:Enenda mwana kunenda, wendako nisalimie.
Quote:………………………………………………………………………
Enenda nitapumua, na kubwa sumbuko hili,
Kama mapenzi yaua, kheri potelea mbali,
Na kama ni kuugua, nitapoa siku mbili,
Quote:Quote:Enenda mwana kunenda, wendako nisalimie.
Shairi lingine linaloonyesha kufarakana kwa wapenzi ni lile la “Sipotaka Niwe Nawe” ambalo linamtaka mmoja wa wapenzi arudishe vyote alivyopewa na mwenziwe.
Hata hivyo, kuagana kwa wawili wapendanao si lazima kuwe kwa shari bali kwaweza kuwa kwa heri, kama tuoneshwavyo katika shairi la “Gud Bai Mai Diri”, ambamo mmoja wa wapenzi anamuasa mwenziwe kuwa wakumbukane kwa barua.
Masuala ya mapenzi yameshikamana sana na yale ya hali ya mtu ilivyo, hasa kiuchumi. Hili tunaonyeshwa na mshairi katika shairi la “Kupenda Kimasikini” ambamo twaonyeshwa kuwa katika “kupenda kimasikini, apendwae hana raha.” Umasikini hauleti matatizo katika masuala ya mapenzi tu bali hata katika ndoa, kama ubeti wa mwisho wa shairi hili la “Kupenda Kimasikini” unavyosisitiza:
Quote:Mpe mema maikazi, nafusi ipate wanda,
Awe nao vijakazi, shamba asiwe wa kwenda,
Mke mfanye azizi, mapenzi si kumdunda,
Quote:Quote:Kupenda kimasikini, apendwae hana raha.
Kwa hiyo basi, sawa na vile ambavyo maisha ya kuiabudu fedha yametawala nyanja zingine za uhai wa jamii, vivyohivyo taasisi ya ndoa imekumbwa na nguvu hii pamoja na mahusiano ya kimapenzi. Mshairi ameirudia dhamira hii ya mapenzi ya pesa katika shairi la “Penzi” ambamo anaonyesha tena jinsi ambavyo pendo kwa mtu fakiri ni kujiumbua bure. Suala hili tutaliangalia vizuri zaidi wakati wa kuishughulikia dhamira ya ndoa na nafasi ya mwanamke katika jamii.
Baadhi ya mashairi ya mapenzi katika diwani hii hapohapo r.i ya kimaadili. Mathalani shairi la “Kwako Nina Tadhalali” linasisitiza umuhimu wa wapenzi kupatana hata kama wamegombana, wakati lile la “Laiti Ukisubiri Utapoa Moyo Wako” linaasa kwamba katika mapenzi kuna haja ya kuwa na subira kwani harakaharaka haina baraka. Katika shairi hilihili mshairi anayakosoa mapenzi ya nyakati zake kuwa yamegeuka kuwa utani mtupu:
Quote:Penzi la sasa utani, sionl wafaidio,
Umebakia utani, kufanya kisingiziio,
Asili hauwaoni, wapenzi wapendanao,
Quote:Quote:Laiti ukisubiri, utapoa moyo wako.
Mashairi mengi ya mapenzi katika Diwani ya Akilimali yanaonyesha dhahiri ujana mwirigi aliokuwa nao mshairi alipoyaandika. Haya ni yale tunayoweza kuyaita ya “mapenzi ya sili silali” ambayo maneno yake yametiwa chumvi ili kukoleza mapenzi yenyewe. Mathalani, katika shairi la “Mapenzi Niliyo Nayo,” mshairi anamweleza mpenziwe:
Quote:Mchana kutwa nalia, kwa fikirazo benati,
Moyo wanichechemea, kwa penzi sili siketi,
Quote:Quote:Mapenzi niliyo nayo, kwako hayana kiyasi.
Quote:Kwa wingi yamefurika, mapenzi nikupendayo,
Mwili damu nakauka, kwa kwikwi hata kiliyo,
Na kisha ninasumbuka, haunitulii moyo
Kauli za namna hii zinajitokeza pia katika shairi la “Tangu Tumefarakana,” hasa katika ubeti wa pili na wa tatu:
Quote:Kwa raha sili silali, si usiku si mchana,
Nimedhoofika hali, sili nisipokuona,
Mpenzi nambiye kweli, lini nitapokuona,
Quote:Quote:Tangu tumefarakana, nimekonda sina hali.
Quote:Nimekonda takiraba, hali nimebadilika,
Sili mwana nikashiba, tangu ulipoondoka,
Rejea nipate tiba, huenda nikatibika,
Quote:Quote:Tangu tumefarakana, nimekonda sina hali.
Ijapokuwa haya na mashairi mengine tuliyokwishayataja yanaonyesha nguvu za mapenzi, ni wazi kuwa mtu hawezi kuwa analia kila siku kwa siku nzima kwamba hali chakula na halali eti kwa sababu ya mapenzi. Akifanya hivyo hufa. Hata hivyo lugha hii ya “sili silali” ni ya kawaida kwa wapenzi, hasa miongoni mwa vijana ambao ndio kwanza wanauingia ulimwengu wa urafiki baina ya wasichana na wavulana.
Maadili na Maana ya Maisha
Mashairi mengi pia katika Diwani ya Akilimali yanashughulikia maadili na maoni kuhusu maisha kwa jumla. Shairi la kwanza, kwa mfano, linasisitiza juu ya umuhimu wa kufanya na kuheshimu kazi, jambo ambalo lina umuhimu sana katika maisha ya Watanzania hata leo hii. Pia shairi linakazia kuwa mtu hawezi kupata uzoefu wa mambo yote yahusuyo maisha kutoka kwa wazazi wake: lazima awe tayari kufunzwa na ulimwengu, yaani kujifunza kutoka kwa wengine zaidi ya baba na mama yake. Mshairi anasema:
Quote:Kazi nilizojifunza, babangu hakuzijua,
Hakujua Kingereza, kuuza na kununua,
Bali kujipendekeza, ndipo mwana nikajua,
Quote:Quote:Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.
Katika shairi la “Aso Sudi na Bahati” mshairi anaeleza jambo tata lihusulo dhana ya “bahati”: kuwa kila mwenye kupata jambo huwa analipata kwa “bahati”, na kwamba asiye na bahati habahatishi. Shairi hili ni zuri sana kwa majadiliano. Je, mwandishi si anajipinga mwcnyewe anaposisitiza katika baadhi ya mashairi yake kuwa mafanikio yanatokana na juhudi na uhodari katika kazi wakati ambapo hapohapo anadai kuwa ili kufanikiwa maishani mtu hana budi kuwa na bahati?
Shairi la “Ajionae Mbora” (uk.3) linashauri kuwa hakuna haja ya kujiona au kuwa na majivuno. Kwa vile hili ni shairi fupi sana tunaweza kulidondoa lote:
Quote:Ajionae mbora, mbora wa jadi yake,
Milele ana hasara, anavunja utu wake,
Apite kihangarara, watu wasimtunulce,
Quote:Quote:Ajionae mbora, daima ana hasara.
Hili limeungana na la “Akiba si Mbaya” (uk. 3) linaloonyesha umuhimu wa kuweka akiba. Tatizo la shairi la “Akiba si Mbaya” ni kwamba linajaribu kuwaeleza watu kuwa kupata au kukosa kwao hutokana na majaliwa ya Mungu (ubeti wa 5), jambo ambalo leo hii si rahisi kukubalika miongoni mwa wasomaji wengi.
Shairi la “Dunia Rangi Rangile” (uk. 6) ni mfano mzuri pia wa shairi la maadili. Humu mshairi anaeleza umuhimu wa kuheshimu na kujituma katika ufanyaji kazi. Ni shairi linalosisitiza juu ya kujitegcmea, kama asemavyo mshairi katika ubeti wa pili:
Quote:Dunia kwa mwanamume, yataka kujichumia,
Kila pembe ujitume, nawe kujisaidia,
Siyo ungoje wachume, ukaliye kutumia,
Quote:Quote:Dunia rangi rangile, yataka kujichumia.
Katika shairi la “Dunia si Uungwana” (uk. 7), mshairi kaunga mkono maadili anayoyatoa katika “Dunia Rangi Rarigile” ambamo anatuasa kuwa maisha yanataka taratibu, ustaarabu na kuishi vizuri na watu. Maadlii haya yameendelezwa katika shairi la “Dunia Ndiyo Ni Njema” (uk. 8) ambamo mshairi anatueleza kuwa kwa asili mtu si mwema. Shairi hili nalo linatoa kauli tata inayoweza kuonekana ni ya kujipinga yenyewe inaposema “Dunia ndiyo ni njema, wanaadamu si wema.” Je, inawezekana tuwe na “dunia njema” yenye “wanadamu wabaya”?
Hata hivyo, katika shairi hilihili Akilimali anasisitiza kuwa ni tabia ya kawaida kwa mwanadamu kuwa karibu nawe wakati wa raha na kukukimbia wakati wa janga:
Quote:Wanadamu si wema, zingatia nisadiki,
Sione kukuengama, moyo ukataharuki,
Mtapendana pa nema, pa dhiki hawaoneki,
Quote:Quote:Dunia ndiyo ni njema, wanaadamu si wema.
Kuwa na fahari kumepigwa vita katika shairi lingine la kimaadili la “Fahari Inafilisi” (uk 9). Shairi hili linasuta tabia ya mtu kujiona kwa mambo ambayo si ya kweli Ubeti wa 3, kwa mfano, unashauri:
Quote:Humpotei kundini upendae kusifiwa,
Ingawa awe ngomani, fahari ataitoa,
“Mimikwangu khamsini, nitayari kuzitou”,
Quote:Quote:Fahari inafilisi, hadharini na fahari.
Pamoja na kuepuka ufahari, mshairi anashauri pia kuwa kuna umuhimu wa kufanya mambo kwa uangalifu. Haya anayaeleza katika shairi lake la “Ghafula Inaumiza,” shairi ambalo linaungana na lile la “Hasira Ina Hasara” (uk. 11) linalosisitiza kuwa kama mtu asingeyakabili mambo kipupa na kwa hasira hata pale panapoudhi, angekuwa na maisha mazuri sana. Maadili, ya namna hii yanaibuka pia katika shairi la “Hujafa Hujaumbika” ambalo linaeleza umuhimu wa heshima kwa watu, na kusisitiza kuwa kuna haja ya kukwepa majitapo, ujeuri, ufahari na kiburi. Wakati huohuo shain hili ni kama linaeleza pia maana ya maisha: kuwa maisha ya mtu yamo katika mabadiliko mengi kiasi ambacho ni vigumu kwa mtu huyo kujidai kuwa amekamilika kabla hajafa.
Utenzi wa “Hisani” pia ni wa kimaadili unaosisitiza juu ya umuhimu kwa watu kuwa na hisani, fadhili na huruma. Hisani imepewa sifa nyingi katika utenzi huu. Mathalani, imeitwa “tamu kama zabibu,” “tamu kama sharubati,” nayo “yavuma kama zumari”, “husitawi kama shamba” na “hunukia kama tunda”.
Katika utenzi huu pia, sawa na tuonavyo katika shairi la “Jalisi Ukiandisi” (uk. 19), mwandishi anasisitiza umuhimu wa kuisbi na watu kiutaratibu, bila mabavu au ugomvi. Ametumia mifano wa Bwana Msosi katika mashairi yote mawili kulisisitiza jambo hili:
Quote:Watemi wamefilia, akina Bwana Msosi,
Nguvu walikitumia, wakinyang’anya kwa fosi,
Na wanao wandamia, wawangojea mkosi,
Quote:Quote:Jalisi ukiandisi, ichungue dunia
Quote:Quote:Quote:Quote:Quote:Quote:Quote:(“Jalisi Ukiandisi”)
Quote:Basi dunia sifosi,
Yataka mwendo wa ngisi,
Wawapi kina Msosi,
Nguvu walikitumia?
Quote:Quote:Quote:Quote:(“Hisani”)
Katika beti hizi mbili mshairi anagusia suala la uongozi bora kuwa hautakiwi uwe wa “fosi” na mabavu kama ahokuwa nao Mtemi Bwana Msosi. Utumiaji mabavu umepingwa pia katika shairi la “Kila Mtaka Uluwa” ambamo adili kubwa lipatikanalo ni lile Sa kuwaasa watu wasitumie nguvu bali wawe wavumilivu:
Quote:Kupata huwa si nguvu, si vishindo na ghasia,
Kwataka uvumilivu, uukosapo tulia,
Autakae kwa nguvu, jela inamngojea,
Quote:Quote:Kila mtaka uluwa, dunia aichukia.
Zaidi ya uvumilivu, mshairi pia anahubiri juu ya umubimu wa ujirani mwema na kusaidiana. Pia ahasuta tabia ya watu kutetane ar hata kuingiliana katika unyumba. Haya anayasema hasa katika shairi la “Jirani Yako Ni Ndugu” (uk. 20).
Maadili mengineyo ni yale yanayoeleza umuhimu wa kuwa na tahadhari na uhakika wa matendo yetu, na umuhimu wa kuwapa watoto malezi mema kwani mtoto umleavyo ndivyo akuavyo (“Kitendo Ni Majuto” uk. 24); tusiropoke maneno ovyo (“Kinywa Humponza Kichwa,” uk. 25); tukwepe upokeaji hongo na rushwa (“Kila Mpenda Rushuwa,” uk. 27); uzuri wa subira maishani (“Mume Asiye Subira,” uk. 32); na pia tunaaswa kuwa ijapokuwa tabia ya upole na ukimya kwa jumla ni nzuri, lakini sifa hizi ni lazima ziwe za wasiani kwani upole na ukimya unapozidi huweza kuwa na hasara kwetu (“Upole Wachusha,” uk. 69).
Kwa jumla, mashairi haya ya maadili ni mazuri kwani yanajaribu kujenga tabia nzuri na mahusiano mazuri pia miongoni mwa wanajamii, Tatizo moja kubwa la maadili ya namna hii ni kwamba yanatoleva kimahubiri mno bila hasa kuchambua chanzo cha matatizo yahusikayo. Kwa mfano, siyo vizuri kusema tu “usiibe” biia kuangalia ni mambo gani katika jamii yanayomfanya mtu aamue kuiba Inawezekana kabisa kwamba yako matatizo yanayotokana na jamii kugawanyika kati ya matajiri sana waisbio kwa jasho la wengine, na wengine kwa kutoa jasho la mchana kutwa kuwatumikia hao matajiri. Hawa watoa jasho haitakuwa jambo laajabu “waibapo” kutokakwa matajiri hao, na wala si sahihi kuwahubiria na kuwakemea kuwa wasiibe.
Kwa hiyo basi, japokuwa maadili mengi katika mashairi ya Diwani ya Akilimali yanasikilika vizuri sana masikioni, mengi ya hayo pia yamekosa misingi ya kijamii kwa hiyo yanapwaya
Ndoa na Nafasi ya Mwanamke Katika Jamii
Kwa vile suala la ndoa linashirikiana sana na lile la natasi ya mwanamke katika jamii, tutazichambua dhamira hizi kwa pamoja.
Katika shairi la “Mume Asiye Subira” (uk. 32) Akilimali anasema kuwa maisha ya ndoa yanahitaji subira na uvumilivu mwingi:
Quote:Subira kitu azizi, ni vyema kisiachiwe,
Subirs ni utoshezi, na mkubwa msadawe,
Wenye subira wapeno, wanaishi pasi yowe,
Quote:Quote:Mume asiye subira, maisha yumashakani.
Suala la ndoa lilizishughulisha sana kalamu za washairi wa enzi za Shaabn Robert akiwemo Akilimali Snow-White. Hili lilijadiliwa na kulumbaniwa hasa katika gazeti la Mambo Leo. Mashairi merigi yaliyolijadili jambo hili yalieleza ubaya wa ujane, na yalisisitiza kuwa naoa ni wajibu kwa watu wote. Hili tunaliona, kwa mfano, katika shairi la “Oa Mwana Kwetu Oa” (uk. 56).
Mashairi mbalimbali yanayozungumzia ndoa pamoja na uhusiano wa mume na mke, hapohapo yanagusia suala lililokuwa muhimu sana enzi za akina Shaaban Robert: suala la nafasi ya mwanamke katika jamii. Wakati ambapo Shaaban Robert aliwatetea wanawake bila kujipinga sana katika msimamo wake juu ya suala hili, Akilimali amejitahidi kumwinua mwanamke bila kujua kuwa aina ya utetezi aitoayo hapohapo inamdhalilisha sana mwanamke. Tuangalie mifano michache ya jambo hili. Katika shairi la “Mume Asiye Subira” beti za 5 na 7 zasema hivi:
Quote:Kazi ya mume kwa mke, ni kumfuza mkewe,
Muradi mlimike, mkeo aongokewe,
Sio kucha kekereke, mkeo umsumbuwe,
Quote:Quote:Mume asiye subira, maisha yumashakani.
Quote:Mke sikumwacha fuvi, sabiliaachiliwe,
Japo mke mjuvi, mfunde pasipo yowe,
Kisha maneno si chumvi, siku moja ayajuwe,
Quote:Quote:Mume asiye subira maisha yumashakani.
Taswira tuipatayo ya mwanamke napa ni sawa na ya mtoto mdogo mjin’ga ambaye mwalimu wake daima ni mwanamume. Taswira hii imerudiwa katika shairi la “Mke Ni Fingo la Nyumba” (uk. 35), hasa katika beti za 7, 8 na 9:
Quote:Muwekee matumizi, sanaa zisiwe haba,
Jitume ufanye kazi, mke apate kushiba,
Na ikifikia mwezi, apate cha kujipamba,
Quote:Quote:Mke ni fingo la nyumba, hadhari kumchezea.
Quote:Umpe mema malezi, atuwe katika nyumba,
Awe nao vijakazi, na vitwana kumpamba,
Msabiliye ghawazi, atumiye kujiramba,
Quote:Quote:Mke ni fingo la nyuma, hadhari kumchezea.
Quote:Kumchezea maizi, mtunze mfano shamba,
Mpambe kwa vidarizi, vya dhahabu kumpamba,
Na kama hivyo huwezi, mpambe japo vya shaba,
Quote:Quote:Mke ni fingo la nyumba, hadhari kumchezea.
Katika beti hizi tatu, licha ya mwanamke kuonekana kuwa yu kiumbe duni cha kutunzwa na kulelewa, pia iko taswira imdunishayo, ya kumwona kuwa ni pambo la kuyafurahisha macho ya mwanamume. Mwanamke tumwonaye hapa hatofautiani na yule tumkutaye katika Utenv wa Mwanakupona, kwani, aghalabu vijakazi na vitwana hawa waliotajwa huwa wa kike. Hawa tunakutana nao pia katika utenzi wa Sayyid Abdallah A. Nassir wa Al Inkishafi, (Oxford, 1939) wakiwapepea, kuwakanda na kuwaimbia nyimbo za kuwabembeleza wafalme wa mji wa Pate.
Utii, unyenyekevu, na unyorige huo wa mwanamke umesisitizwa pia katika utenzi wa “Mke na Mume” (uk. 42-49). Haya yamejitokeza hasa katika beti za 19-23, za 30-38, na za 44 na 49. Katika beti hizi mwanamke hatakiwi awaze, anahitajiwa angoje “cha kuwaziwa”:
Quote:19. Mwanamke hapasiki,
Kutaka hiki na hiki,
Mwanamke ana haki,
Quote:Quote:Kungoja cha kuwaziwa.
Quote:23. Mume ni yako hirizi,
Yakupasa kumuenzi,
Mtii kwa kila kav,
Quote:Quote:Asemalo nyenyekea.
Quote:24. Linalompasa mke,
Ndiyo nyumba uishike,
Nyumba ni mume na mke,
Quote:Quote:Nyumba si mume pekee.
Hapa mwanamke anatakiwa anyenyekee lolote lisemwalo na mumews; atii kama mtoto mdogo tu.
Beti za 24-29 zinasisitiza kuwa nafasi ya mwanamke ni nyumbani, naye hana budi kuisafisha nyumba vizuri. Amalizapo kufanya hivyo ametakiwa asiranderande ovyo bali atulie nyumbani na ajipambe:
Quote:31. Unapopata wasaa,
Kupumzika kukaa,
Uwache kugaagaa,
Quote:Quote:Jikoshe ukipumua.
Quote:32. Ebu jitiye utuli,
Unawiri wako mwili,
Uwe mke kulihali,
Quote:Quote:Jasho baya kuondoa.
Japokuwa kijuujuu mawaidha baya ya kujipamba na kujifanya msafi huweza kusifiwa kwaai hulandana na kaida za afya bora. tuyachunguzapo kwa undani tunagundua kuwa yanamdhalilisha mwanamke kwani anatakiwa ayafanye hayo yote ili kumridhisha mwanamume. Haya yametiliwa mkazo katika ubeti wa 44:
Quote:44. Nenda mwendo maridhia,
Mume ukimsikia
Alitakalo sikia,
Quote:Quote:Mume ukimridhia.
Katika shairi, la “Nala Nikimetameta, Moyo Wangu Umetua” jambo hilo limerudiwa. Mshairi anafurahi kuwa ana mke anayefuata lolote asemalo:
Quote:Moyo wangu umetua, nala nikimetameta,
Mke nilio muoa, mpole hana matata,
Mpole hana udhia, nimwambialo hufata,
Quote:Quote:Nala nikimetameta, moyo wangu umetua.
Quote:Kicheko nakiangua, kwa mke niliopata,
Ndio wangu maridhawa, dumu nikimlafuta,
Mke wangu ni mtawa, nje hapendi kupita,
Quote:Quote:Nala nikimetameta, moyo wangu umetua.
Taswira sawa na ya beti hizi mbili inajitokeza pia katika shairi la “Nisipomtunza Wangu Nikamtunze wa Nani?” (uk. 52), hasa katika ubeti wa 3.
Kwa Akilimali, ni ushindi mkubwa sana kuwa amepata mke anayefua kwa adabu na upole lolote analomwambia; mke anayetawa ndani ya nyumba Huu ni utamaduni wa kipwani wenye asili ya Uarabu na Uislamu. Leo hii utawa huu pamoja na upole anaoufurahia Snovv-White utaonekana na unyonge wa mwanamke, vitu ambavyo vafaa vipigwe vita. Ukombozi wa mwanamke ambao ni mada muhimu katika mikutano na makongamano mbalimbali duniani unapinga sana adili. Hata tamathali azitumiazo mshairi kumhusu mwanamke leo hii zinaweza zionekane kwa baadhi ya watu kuwa ni za kumdhalilisha zaidi mwanamke badala ya kuwa sifa za kimaendeleo. Mathalani, kumfananisha mwanamke na ua zuri au ndege mzuri (angani ubeti wa 2 wa “Nimcmshika Mnana”, uk. 53) kunamgeuza mwanamke na kumfanya pambo tu la kuyafurahisha macho ya mwanamume, kwa hivyo kutaonekana kuwa kunapingana na ukombozi wa mwanamke kutoka katika unyonge wake.
Hata hivyo, kuna mashairi machache ambayo tunaweza kuyaita ya kimaendeleo kuhusu suala la nafasi ya mwanamke katika familia na jamii. Shairi la “Wapenzi Shangilieni Uzazi” (uk. 75), zaidi ya kuonyesha jinsi ambavyo furaha ya ndoa ni kupata watoto, linaungana na lile la “Mke Mzazi Nyumbani” (uk. 41) kuonyesha umuhimu wa mwanamke hasa katika jukumu lake la umama la kuendeleza uhai; jukumu ambalo linataka aheshimiwe na pia apate haki zote, hata za urithi. Umuhimu wa jukumu hili la umama limesisitizwa katika beti za 40-47 za utenzi wa “Radhi” ambamo mshairi anaeleza kuhusu uchungu na maumivu ya uzazi, mzigo ambao kina mama huuvumilia ilimradi waendeleze maisha na uhai wa jamaa na jamii.
Shairi lingine ambalo limeendeleza utetezi huo ni la “Wapeni Vyeo Mabibi” (uk. 74). Ijapokuwa huenda kwa baadhi ya wasomaji utetezi huu leo hautaonekana kuwa na uzito kwani kwa sasa hivi wako viongozi wa kikc serikalini na pia katika mashirika na makampuni, tuzirigatiapo wakari alipoandika bwana Snow White itadhihirika kuwa huu uiikuwa utetezi thabiti ambao pia ni hatua muhimu ya mwanzo katika ukombozi wa mwanamke.
Umuhimu wa Kazi
Hapa na pale katika mashairi ya Diwani ya Akilimali upo msisitizo kuhusu umuhimu wa kufanya na kuheshimu kazi.
Katika shairi la kwanza kabisa la “Asofuzwa na “Wazazi Hufunzwa na UIimwengu” anasema haya kuhusu kazi:
Quote:Kiasi nilijifunza, si haba kwa kubabia
Nitokapo napendeza, kazi njema natumia
Ni vigumu kuibeza, jinsi inanielea
………………………………………………….
Haifai kupuuza, kwa kitu usichojua,
Jaribu kupeleleza, na kisha ukichungua
Nia unapoikaza, hushindwi kitu kujua
Quote:Quote:Asofunzawa na wazazi, hufunzwa na walimwengu
Quote:Kazi nilizojifunza, babangu hakuzijua
Hakujua Kingereza, kuuza na kununua
Bali kujipendekeza, ndipo mwana nikajua.
Mawaidha haya yamesisitizwa katika shairi la “Dunia Rangi Rarigile” ambalo lote linatilia mkazo tabia ya kujituma na kuwajibika katika ufanyaji kazi. Shairi hili linasisitiza juu ya umuhimu wa mtu kujitegemea kwa kutolea jasho kila kitu badala ya kusubiri kusaidiwa. Mshairi anasema:
Quote:3. Jitume huku na huku, upate kujichumia
Si wajibu kila siku, mwanadamu kungojea
Na usingoje usiku, kakayo kumlilia
Dunia rangi rangile, yataka kujichumia.
8. Kiwacho cha jasho lako, ni chema kwa kutumia
Kulikoni cha mwenzako, kitu cha kusimangia
Akunyimapo mwenzako, lipi litakufalia
Duniarangirangile, yataka kujichumia.
Japokuwa katika shairi la “Unapokosa Shukuru” (uk. 71) kuna mawazo yanayoweza kupingwa na baadhi ya wasomaji kutokana na udhaifu wake wa kuhusisha “kupata” au “kukosa” na mipango ya Mwenyezi Mungu, lakini baadhi ya beti zake (hasa ule wa mwisho) zinapinga uvivu na kusisitiza kuwa mtu hana budi kufanya kazi:
Quote:Kazi zote njema sana, sioni wake ubovu
Hata hiyo ya kushona, bali usiwe mvivu
Kazi yeyote kijana, yataka shime na nguvu
Mashairi haya yote, japokuwa ni machache katika diwani hii, yanamfanya Akilimali Snow-White awe na nafasi muhimu katika jamii ya Tanzania ya leo ambamo kazi inathaminiwa kuwa ni kipimo cha utu.
Siasa
Japokuwa dhamira ya siasa tumeitenga hapa, kwa hakika si sahihi kuitenganisha na ile ya umuhimu wa kazi, kwani siasa ni mfumo wa kiitikadi unaofuatwa na jamii, kikundi au tabaka fulani katikajamii, na ufanyaji kazi pamoja na ugawanyaji wa mali ni sehemu ya itikadi. Hata hivyo neno “siasa” hapa tunalihusisha hasa na hali ilivyokuwa nchini katika enzi za ukoloni, wakati Snow-White alipoandika baadhi kubwa ya mashairi yake. Je, mshairi aliisawiri vipi hali hiyo?
Labda tuanze na shairi la “Hongera Kuini Wetu” (uk. 11). Shairi hili lina utata kidogo, kwani tujuavyo, kuini huyo alikuwa mkuu wa Dola ya Uingereza, naye ndiye hasa kiongozi wa ukoloni ulioinyonya na kuigandamiza Tanganyika. Iweje basi mshairi wa Kitanganyika amsifu adui huyu?
Hata hivyo, kwa upande mwingine, inawezekana kabisa kuwa Akilimali alipoandika shairi hili alilitumia kikejeli na labda kuwataka wasomaji wake walisome kila neno katika kinyume chake. Msomaji afanyapo hivyo atagundua ujumbe wa kumlaani kabisa “kuini” huyo.
Shairi la “Kila Ndege na Tundule” (uk. 22) ambalo ni tambo, huweza kuwa la kisiasa pia. Hili linajikita katika uzalendo wa kila mtu kupenda nchi na utamaduni wake (“tundu”), na hili tunaling’amua hasa katika ubeti wa mwisho:
Quote:Rabi naomba kabuli, tujalie heri njema
Tuzidishe ikibali, tujifunze taaluma
Tuishi na Kiswahili, lugha ngeni kuzitema
Quote:Quote:Kila ndege na tundule, tundujingine karaha.
Maudhui ya “Kila Ndege na Tundule” yamesisitizwa pia katika shairi la “Kila Mdharau Chake” (uk. 24) ambalo hali kadhalika tunaweza kulihusisha na uzalendo wa mshairi; na pia katika lile la “Mcheza Kwao” ambamo mshairi anaasa kuwa mtu hana budi kujenga na kuimarisha nchi yake.
Mashairi ya “Nafingwa Ningali Hai” (uk.51), “Rabi Humlipizia Mnyonge Mkosa Haki” (uk.58) na “Walimwengu Tutendeje” (uk.75) ni ya kisiasa yanayotetea haki za wanyongc. Wakati ambapo inaelekea lile la “Walimwengu Tutendeje” limetumiwa kuwafumbia wakoloni kwani “shida” itajwayo yaweza kuwa ukoloni na madhila yake, wakati ambapo “nguruwe” wanaojitokeza kula miche ya mahindi ipandwayo na wananchi huweza kuwawakilisha wakoloni na unyonyaji wao; katika mashairi ya “Nafingwa” na “Rabi Humlipizia” mshairi ‘amepinga dhuluma moja kuwa moja. Anasema katika shairi la “Nafingwa”:
Quote:Napigwa pigo la goti, miguu nimelemewa
Kilicho changu sipati, naomba bila kupewa
Nafingwa kama kijili, nanyimwa kwa kuonewa
Quote:Quote:Nafingwa ningali hai, kinywa nazibwa kunena.
Zaidi ya kupinga uonevu wa kutoruhusiwa hata kulalamikia maovu yaiiyopo nchini wakati wa ukoloni, mshairi ananung’unikia pia ubaguzi wa rangi uliokuwa umezagaa wakati huo katika shairi hili:
Quote:Japo navuta sauti, kauli kutaka toa
Natishwa Snowaiti, kwa rangi niliopewa
Kwa kunifunga kijiti, bila sababu kujua
Quote:Quote:Nafingwa ningali hai, kinywa nazibwa kunena.
Kwa jumla, mashairi ya aina hii si mengi katika diwani hii, lakini haya machache yanatoa maudhui mazito mno ambayo yanafifisha udhaifu wa mashairi ya aina va lile la “Hongera Kuini Wetu.”
Dini na Mungu
Katika uchambuzi wa dhamira mbalimbali tuliokwishafanya tuligusia hapa na pale kuhusu mawazo ya mwandishi huyu juu ya nafasi ya dini au Mungu katika maisha ya jamii. Hapa tutaendeleza tu mjadala huo kwa kuuhusisha na mashairi yanayoshughulikia dhamira hii ama moja kwa moja, au kwa kuitaja tu.
Karibu mashairi yote ya kimaadili yanagusia suala la dini na Mungu. Mwandishi inaelekea yu muumini mkubwa wa dini, naye anaamini kabisa kuwa jambo lolote linalotokea duniani ni kwa amri ya Mungu.
Shairi la “Ikuze Dini ya Kiislamu” (uk. 16) moja kwa moja ni la kuitangaza dini hiyo ambayo mshairi anaamini ndiyo sahihi yenye “nuru” ya kuwaangaza watu wakati zingine zote ni za kikafiri. Anasema haya katika ubeti wa mwisho wa shairi hili:
Quote:Yarabi tusheheneze, Isilamu twasongeka
Farijiko tueneze, dhiki hizi kututoka
Ukafiri ukimbize, ukome na kutoweka
Quote:Quote:Ikuze na inyanyuze, dini ya Kiislamu.
Bwana Shaaban Robert, mshairi mwenzake Akilimali, ubeti kama huo anaupinga kwani alikwishavuka mipaka ya kanisa na msikiti na kusema, hasa katika kitabu chake cha Siku ya Watenzi Wote, kwamba watu wote, bila kujali dini, rangi au taifa, hawana budi kuungana katika juhudi za kuleta maendeleo ya jamii.
Katika shairi la “Nisipomtunza Wangu Nikamtunze wa Nani?” ubeti wa mwisho unasema:
Quote:Tamati hapa ni basi, daima nashukurani
Naujutia ukwasi. Mungu alio nihini
Mke wangu angepasi, kwa kila la tamaduni.
Hapa mshairi anaeleza kuwa mtu kuwa tajiri au masikini ni matakwa ya Mungu. Ujumbe huu anaurudia katika shairi la “Unapokosa Shukuru” (uk. 71) anapodai:
Quote:Shukuru unachopata, japo ukipata mbovu
Mungu mwenyewe tafeta, nzima pasipo ya nguvu
Bure pesa hutapata, pasipo uelekevu
Unapokosa shukuru, kupata kuna Rabuka.
Mashairi ya namna hii yanaweza kurudisha nyuma maendeleo ya baiakati za watu za ujenzi wa jamii zao hasa watakapohitimisha kuwa matatizo yao na hali zao zote ni mipango ya Mungu.
Katika utenzi wa “Radhi” mshairi kaanza na mtindo wa kimapokeo unaomwita Mungu na kumwomba ampe msaada na baraka katika utunzi wake. Iliaminika miongoni mwa washairi wa kimapokeo kuwa mtunzi wa tenzi hupata kipaji kutoka kwa Mungu, jambo ambalo linazidi kupoteza waumini wengi kila uchao, hasa kwa washairi wa kizazi kipya cha leo. Hawa wanaamini kuwa kila jambo hutokana na mtu mwenyewe, kwa juhudi pamoja na maarifa yake.
Dhamira Zinginezo
Tulizoziangalia si dhamira pekee zijitokezazo katika diwani hii. Ziko zingine ambazo zinajitokeza katika shairi moja moja au mawili hivi. Nyingi ya hizi ni zile zinazojitokeza katika mashairi ya tambo. Mathalani umuhimu wa kujali na kutunza kile alicho nacho mtu (“Bora Shaba Sibadili na Dhahabu,” uk. 4); kuheshimu ndoa (“Jozi,” uk. 18); hasara za kudodosa mambo, hasa yamhusuyo mtu wa karibu nawe (“Kuku Ukimchungua,” uk. 27); na umuhimu wa kutunza siri (“Panapo Wingi wa Ndege,” uk. 56).
Shairi la “Kiswahili” (uk. 29) linaungana na yale ya kizalendo kwani linausifu na kuutukuza utamaduni wa Mtanganyika. Mshairi kasema kwamba Kiswahili ni kama “zamaradi”, na kuendelea kwamba:
Quote:Katika yangu fuadi, Kiswahili ndiyo memo
Nakipenda sina budi, kwafasaha na upimo
Lugha nyingine fisadi, yanivuruga msemo
Quote:Quote:Ingawa najitahidi, kusema sipati kimo.
Shairi la “Manahodha Kuwa Wengi, Ni Kuzamisha Mashuwa” linaibusha dhamira muhimu hata katika Afrika ya leo. Dhamira hii inahusu uongozi bora, nayo inaeleza kuwa mabavu hayafai katika majukumu ya uongozi.
Japokuwa suala la elimu ni dhamira ndogo kitabuni humu ilinganishwapo na zingine kama za “mapenzi” na “maadili”; linayo nafasi muhimu pia katika diwani hii.
Katika shairi la “Asofunzwa na Wazazi Hufunzwa na Ulimwengu” mshairi amegusia dhamira hii kwa kutuonyesha kuwa elimu si ya darasani tu bali pia hupatikana katika malezi ya wazazi na ya dunia.
FANI KATIKA DIWANI YA AKILIMALI
Wakati wa kujadili maudhui ya diwani hii hapohapo tulikuwa tunagusia kuhusu vipengele mbalimbali vya fani vilivyotumiwa na mshairi kuyaibushia maudhiu hayo. Mathalani, tulieleza juu ya kipengele cha picha au taswira ya mwanamke tuipatayo ambayo inapingana na ukombozi wa mwanamke alioukusudia Akilimali. Haya yote yametokana na ukweli kuwa maudhui na fani ya kazi ya fasihi ni vitu viwili visivyotenganika; kwa hiyo, mara tu mhakiki aanzapo kujadilj kipengele kimoja hujikuta akikihusisha na cha pili, apende asipende.
Katika sehemu hii basi, tutajaribu kugusia vipengele ambavyo hatukuvitaja vinavyochangia sana kwenye uundaji wa fani katika diwani hii.
Kwa jumla mshairi ametumia mtindo wa kimapokeo katika mashairi na tenzi zake zote. Kanuni za vina na mizani zimefuatwa kimapokeo, na mashairi mengi ni unne yenye vina vya kati na vya mwisho vilivyo sawa katika mistari mitatu ya kwanza kwa kila ubeti, lakini vyenye kubadilika katika mistari ya mwisho mwa beti.
Mwandishi amejitahidi kutumia tamathali za mlinganisho, kama hasa zile za sitiari na tashbiha. Hizi ni tamathali za mlinganisho, kama vile alivyouita ustaarabu kuwa ni dhahabu (ubeti wa 7 wa “Dunia Si Uungwana,” uk.7). Pia amatumia sifa mbalimbali kuhusu hisani kwa kuiita “zabibu”, “sharubati”. “zumari”, “juba” na kadhalika (“Hisani,” uk. 14); mfano mwingine ni ule wa kumwita mke ni fingo la nyumba.Tamathali hizi na zinginezo ambazo msomaji atazigundua katika mashairi mengine, zaidi ya kuipamba lugha zimeongezea pia uzito katika kutupa picha ya kikamilifu zaidi ya jambo lihusikalo.
Zaidi ya tamathali, mshairi ametumia pia methali katika baadhi ya mashairi yake, hasa katika vichwa vya mashairi hayo. Mfano ni mashairi ya “Asofunzwa na Wazazi, Hufunzwa na Ulimwengu,” “Hasira Hasara,” “Hujafa Hujaumbika,” “Haliwezi Mwanadamu Lishindalo Fisi,” “Kila Ndege na Tundule,” na mengi ya aina hii ambayo matumizi yake ya methali yamesaidia katika kuleta ujumbe uliokusudiwa.
Kuna baadhi ya mashairi ambayo matumizi yake ya vina ni tofauti kidogo. Mathalani, tunaweza kusema kuwa shairi la “Oa Mwanakwetu Oa” lina vina vitatu katika kila mstari kwa sababu neno “oa” linarudiwa katika sehemu zile zile kwenye kila mstari. Marudio haya yanafanya kuwe na kina cha a mwanzoni mwa kila mstari na pia katikati ya kila mstari, na kina kingine mwishoni mwa mstari. Hapa basi, tunapata mpangilio wa vina kama ifuatavyo:
Quote:Oa mwana kwetu oa, oa mrembo jamali
Oa mwana mlelewa, mwenye utu mwenye hali
Marudio haya ya neno “oa” hapohapo vanasisitiza umuhimu wa ndoa.
Mshairi anao mtindo wa kutumia maneno ya Kiingereza kwa kuyatohoa. Wakati mwingine haya yameleta ucheshi wa habari anazozieleza. Kwa mfano katika shairi la “Akiba Si Mbaya” katumia neno “poni” kwa maana ya lile la Kiingereza la “pawn”, na katika shairi lingine ambalo kichwa chake kinachekesha katumia “Gud Bai Mai Diri” kwa maana ya “Goodbye My Dear” Haya pamoja na maneno “Twenti eiti” – kwa maana ya “Twenty eight” katika shairi la “Ndugu-Arusi'” (uk. 55) huenda kwa wengine yakaonekana kuwa ni kasumba badala ya ucheshi.
Hata hivyo, japokuwa tumevitaja viungo vyote hivyo vya fani, kwa hakika mashairi mengi katika diwani hii yanasomeka moja kwa moja tu bila kuwaha ile lugha ya mvutc ya “kishairi'” tuikutayo katika mashairi mengine ya kimapokeo kama vila ya akina Shaaban Robert au Mathias Mnyampala. Huenda tutakuwa tunamwonea Akilimali Snow-White, hata hivyo, kwa kumtaka awe na kiwango sawa na cha hao mashaha wa malenga kwani hata kiumri alikuwa mdogo sana kwao, na kuizoefu pia hizi zilikuwa juhudi zake za mwanzo. Ndiyo sababu tunamwona Akilimali wakati mwingine akikosa msamiati na kurudiarudia maneno hayohayo si kati -a shairi tu, bali hata ndani ya ubeti huohuo; marudio yanaonekana dhahiri kuwa si kwa ajili ya msisitizo, bali ni matokeo ya uchanga wa Akilimali Snow-White katika bahari ya ushairi wakati alipoandika mashairi ya diwani hii. Mathalani, katika ubeti wa mwisho wa “Dunia Rangi Rangile” neo “mwenzako” isingefaa lirudiwe; na neno “balia” isingefaa kutumiwa mara mbili katika beti zilizofuatana za 17 na 18 za utenzi wa “Mke na Mume.”
Bila kujali udhaifu huo tulioutaja, ni dhahiri kuwa Akilimali Snow-White katika Diwani ya Akilimali ameshughulikia dhamira mbalimbali zilizo muhimu na ambazo huwavutia wasomaji wengi vijana.
Maswali
1. Chagua dhamira mbili kati ya zifuatazo ujadili zilivyoibushwa katika Diwani ya Akilimali:
Quote:1. Maadili na maana ya maisha
2. Ndoa
3. Siasa
4. Ukombozi wa mwanamke.
2. “Kutokana na kutapakaa kwa dhamira ya mapenzi katika diwani hii, tunaweza kusema kuwa Akilimali kawaandikia vijana zaidi kuliko wazee”. Jadili.
3. Linganisha jinsi Akilimali na mshairi mmoja kati ya wafuatao walivyoishughulikia dhamira ya siasa.
Quote:1. Theobald Mvungi (Raha Karaha)
2. Saadani Kandoro (Diwani ya Saadani)
3. Francis Semghanga (Teuzi za Nafsi).
4. Je, ni nani kati ya Saadani Kandoro (Mashairi ya Saadani), Francis Semghanga (Teuzi za Nafsi), na Akilimali Snow-White (Diwani ya Akilimali), ambaye amefaulu zaidi katika kuoanisha fani na maudhui ya ushairi wake? Toa sababu na uthibitisho wa hoja zako.
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (9) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 09:44 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
8. Shaaban Robert: Ashiki Kitabu Hiki
SURA YA NANE
Kabla ya kuanza kuyachambua masuala mbalimbali yanayojitokeza katika mashairi ya diwani hii ya Ashiki Kitabu Hiki, tuichunguze kwanza kwa kifupi historia ya Shaaban Robert.
Shaaban Robert alizaliwa tarehe 1 Januari 1909 huko Vibambani, Tanga. Alisoma katika shule mbalimbali Dar es Salaam tangu 1922 hadi 1926, na baada ya hapo alifanya kazi huko Pangani, Longido, na baadaye Tanga. Alifariki tarehe 20 Juni, 1962.
Zaidi ya kuandika riwaya na insha, Shaaban Robert aliandika vitabu vingi sana vya mashairi; na kwa kweli ushairi ndio hasa uliompa umaarufu mwandishi huyu. Kati ya vitabu au tuseme diwani za ushairi za mwandishi buyu zipo za Pambo ta Lugha (1948), Marudi Mema (1952), Uhuru (1967), Ashiki Kitabu Hiki (1968), Mashairi ya Shaaban Rohert(1968), Mwafrika Aimba (1969) na Sanaa ya Ushairi (1972).
Ili kuweza kupata undani wa mashairi ya diwani yoyote ya Shaaban Robert ni vizuri kusoma baadhi kubwa ya diwani hizo zilizotajwa, au hata zote, kwani dhamira mbalimbali alizozishughulikia mshairi huyu katika maisha yake ya uandishi zimejitokeza karibu katika kila diwani.
DHAMIRA KUU
Jambo moja linalojitokeza sana katika mashairi mengi ya diwani hii ni lile la malumbano. Malumbano ni majibizano kati ya washairi kuhusu mambo mbalimbali, na aghalabu malumbano hayo huwa na kujisifu kwirigi kunakotolewa kiushairi. Kujisifu huku kulikuwa kwa kawaida sana kati ya washairi ambao waliandika kuringia na kujigambia ushaha wao katika uwanja wa ushairi.
Katika diwani hii mashairi yafuatayo tunaweza kuyaweka katika kundi hfli la malumbano: “Utangulizi” (uk. xi-xii), “Sichi” (uk. 1), “Wapinzi” (uk. 3), “Ngozi ya Simba” (uk. 3-5), “Bahati” (uk. 10), “Ni Wapuzi” (uk. 27-28), “Tosa Haitatukuka” (uk. 35-36). “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” (uk. 37-39), “Mwezi Hauwi Jua” (uk. 39-40), na “Si Kweli” (uk. 40-41).
Ni wazi kuwa mashairi haya ya malumbano hayaishilii katika kiwango cha kujitapa tu kwani zaidi ya kuringia usanii, hapohapo iliwabidi wanaolumbana kuonyesha ujuzi wao wa mambo waliyokuwa wanayajadili. Kwa mfano katika mashairi ya “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” na “Mwezi Hauwi Jua” suala la umuhimu wa ndoa na ubaya wa ujane linajadiliwa kimalumbano. Mojawapo ya mbinu kubwa zinazotumiwa na washairi wakati wa malumbano ni ile ya kufumba kwa kutumia lugha ya kilinge na sanaa ya hali ya juu. Kwa hiyo katika mashairi haya tunakuta matumizi ya tamathali za usemi, nahau, methali, na mifano mingi ya lugha nzito inayozidisha hali ya shairi kuwa tambo. Nia wakati mwingine ni ya kuwadunisha “maadui” hadi wajione kuwa wao ni chawa wadogo tu ambao hawastahili kuuawa kwa shoka wakati ukucha unatosha.
Katika diwani hii. Shaaban Robert anazungumzia hasa mambo yafuatayo
Quote:1. Suala la Wanawake
2. Athari za Pesa katika jamii
3. Falsafa kuhusu maisha
4. Hakidhidiyauovu.
Suala la Wanawake
Shaaban Robert ni mmoja wa washairi wa Kiswahili ambao kalamu zao zimelishughulikia sana suala la mwanamke na nafasi yake.katika jamii. Tunaugundua utetezi wake wa mwanamke si katika ushairi tu bali pia katika kazi zake zingine, kwa mfano katika Wasifu wa Siti Binti Saad (1955) na Siku ya Watenzi Wote (1968). Katika kazi hizi anajaribu kuonyesha kuwa haifai mwanamke anyanyaswe au kunyonywa na kugandamizwa na mwanamume. Yafaa – na kwa kweli ni lazima – apate haki na nafasi sawa na ya mwanamume katika nyanja zote za maisha kisiasa, kiutamaduni, na kiuchumi katika jamii. Hata katika Utenzi wa Hati Shaaban Robert anasisitiza kuhusu umuhimu wa kujitegemca na kujiendeleza kwa mwanamke ili asibaki jikoni na kitandani tu.
Katika diwani hii ya Ashiki Kitabu Hiki mashairi yaliyomshughulikia mwanamke ni kama vile “Sijui” (uk. 5), “Nani Atakutendea” (uk. 13). “Kuoa” (uk. 18-22), “Maango” (uk. 22-24) na “Mwanamke” (uk. 32-33).
Katika shairi la “Milango” (uk. 22-24) mshairi anamtetea mwanamke kwa kuonyesha vile ambavyo taasisi ya ndoa inampa nafasi duni. Anasema katika ubeti wa 3.
Quote:Ndoa mlango wa tatu,
Mume humiliki vitu,
Ila mke hawi mtu,
Huwa baa kwa kupoa
Taasisi hii katika jamii yenye maisha ya kimwinyi na kibepari humgeuza mwanamke knwa kitu kimojawapo kinachomilikiwa na mwanamume. Na haya yote hutokca ijapokuwa ni kweli kwamba mwanamke ndiye hasa chanzo kikuu cha uhai wa jamii kwani ndiye abebaye mimba na kuzaa – ndiye aliye na jukumu kubwa la kutimiliza jambo la kwanza kati ya matatu muhimu yaelezwayo na mshairi katika shairi la “Matatu Muhimu” (uk.42).
Katika jamii ambayo imezingwa na utamaduni wa kibepari unaoabudu pesa, kila kitu kinachowezckana kugeuzwa kuwa bidhaa ya kuuzika hufanywa hivyo. Mwanamke hali kadhalika huuzwa ama hulazimika kujiuza kama bidhaa zinginezo. Ndiyo sababu katika shairi la “Sijui” mwandishi anauliza:
Quote:Bilashi msijivune
Quote:Quote:Nanyi ni makurumbesa
Quote:Hamna jambo jingine
Quote:Quote:Ila kudai mapesa!
Quote:Sijui mwauza nini
Quote:Quote:Hata mkataka pesa?
Quote:Na kuwapasha madeni
Quote:Quote:Waume makubwa hasa?
Dhamira hii inajitokeza pia katika shairi “Mwanamke” hasa beti za 2 na 5:
Quote:Mwanamume kinyozi,
Dada mimi simwezi,
Heri nipande ngazi,
Quote:Quote:Nende japo kwa Goa.
Quote:Sinifanyie kelele,
Maneno mapesa mbele
Nikanunue mchele,
Quote:Quote:Huko nitakofikia.
Kwa hiyo mashairi mengi yamhusuyo mwanamke katika diwani hii si ya kumtetea hasa bali yanamwonyesha vile ambavyo katumbukia katika maisha ya kibepari yanayoifanya pesa kuwa kiungo pekee kati ya mtu na mtu. Kwa sababu dhamira hii ya fedha ina uzito wake, tuipe nafasi yake mahsusi katika mjadala wetu.
Athari za Pesa Katika Jamii
Mashairi yote katika diwani hii ambayo yameongelea kuhusu pesa yanatupa taswira ya maisha ya kibepari ya kuabudu fedha na kuzifanya kuwa Mungu pekee wa jamii.
Mashairi tuliyokwishayataja ya “Sijui” pamoja na ya “Nyumba za Ngoma” (uk. 12-13), na “Nani Atakutendea?” (uk. 13-14) yanaonyesha jinsi ambavyo imani hii juu ya pesa imeunda soko la kuuzia kila kitu. Ili kuonyesha kuwa si kwa wanawake tu bali pia kwa wanaume, mshairi kaweka beti mbili za mashairi mawili ambazo zina ushabihiano. Ubeti wa mwisho wa “Nyumba za Ngoma” unasema:
Quote:Wana wake magunge,
Wamezidi pangapunge,
Heri tusiwahonge,
Wataka kutuibia.
Na ubeti wa mwisho wa shairi la “Nani Atakutendea?” nao unasema:
Quote:Na wanaume magunge
Wamezidi pangapunge,
Kina dada tujitenge
Hasara itatujia.
Uhusiano huu wa kibiashara kati ya wanaume na wanawake ndio unaomfanya Shaaban Robert awaite “magunge” na “pangapunge.”
Shairi la “Fedha” (uk. 8 – 9) ni kielelezo dhahiri cha vile ambavyo fedha imeyatawala maisha ya jamii. Ubeti wa 4 unatoa muhtasari wa milki hiyo ya fedha:
Quote:Fedha imevunja nguu,
Milima ikatambaa,
Fedha ni kitu kikuu,
Aliye nayo shujaa,
Hutiiwa na wajuu,
Wa chini wakaridhia.
Halafu mshairi anaendelea kutueleza jinsi ambavyo fedha zimeua utu wa watu, na kuwafanya watu wabaya walio nazo waheshimiwe:
Quote:Mtu aliye nafedha,
Japo duni ni kubeli,
Asemafo lina ladha,
Neno lake ikibali,
Hazukiwi na bughudha,
Uongowe huwa kweli.
Hata hivyo baadaye mshairi anatueleza katika ubeti wa 8 kuwa athari za fedha zina ncha mbili: ncha moja huwafikisha watu jehanam, na ya pili huwapeleka peponi.
Shairi la “Simwezi” (uk. 24-25) hali kadhalika linashughulikia suala la athari za fedha na vile ambavyo huumba watu wenye tamaa nyingi, tamaa ishindayo hata ile ya fisi (ubeti wa 5).
Ndoa
Suala la ndoa nalo lilimshughulisha sana Shaaban Robert katika maisha yake ya uandishi. Katika riwaya za Utubora Mkulima na Siku ya Watenzi Wote, na pia katika mashairi yake mengi, Shaaban Robert ameiona ndoa kuwa ni wajibu kwa watu, mradi tu wanaooana wawe watu kufu. Ndiyo sababu hata katika ubeti wa 6 wa shairi la “Kuoa” (uk. 20) mshairi anatuambia:
Quote:Kuoa mke si kufu,
Quote:Quote:Atakuliza machozi,
Quote:Kwa mambo yake dhaifu,
Quote:Quote:Ukonde ubaki ngozi,
Quote:Huwezi kumsarifu.
Quote:Quote:Cheo chako hakiwazi,
Quote:Kwake kama upuuzi,
Quote:Quote:Yafahamu yasemwayo.
Hata hivyo tunagundua kwamba mawazo na falsafa ya mshairi huyu kuhusu ndoa si yale yale daima – uko wakati yanapingana. Kwa mfano, wakati anapopinga ujane na kusisitiza kuhusu umuhimu wa ndoa (tazama mashairi ya “Halali Kitu Akram,” “Situmii Shoka Ukucha Unapofaa” na “Mwezi Hauwi Jua”) bapohapo yapo mashairi ambayo yanaonyesha kuwa ndoa haina maana sana kwani furaha yake ni adimu sana kupatikana. Shairi la “Kuoa” (uk. 18-22) linaonyesha vile ambavyo ni vigumu kupata mke anayefaa ndoani; shairi la “Simwezi” na la “Milango” yanasisitiza jinsi ambavyo ni vigumu kuwa na ndoa yenye furaha. Kwa hiyo tunaelezwa katika ubeti wa kwanza wa “Milango” kwa mfano, kuwa ndoa ina matata na giza. Kwa ujumla mashairi haya yanasisitizajinsi ambavyo taasisi ya ndoa imeharibika. Ila mshairi haingii ndani zaidi kuchambua hasa chanzo na mzizi wa kuharibika huko.
Falsafa Kuhusu Maisha
Mashairi kadhaa katika diwani hii yanajishughulisha na suala la maana ya maisha. Shairi la “Nyuso Mbili” (uk. 1), kwa mfano, linasisitiza wazo kuwa maisha yana nyuso mbili na kwamba maisha lazima yana mwisho kwani “Maisha ni matembezi ya kukoma tasihili.” Kwa hiyo, katika shairi la “Kubadilishana Zamu” (uk. 30) umuhimu wa mabadiliko katika maisha umesisitizwa; na shairi hili linatuasa kuwa hakuna refu lisilo na ncha.
Shairi la “Maswali na Majibu” (uk. 14-18), linatukumbusha shairi lingine maarufu la mshairi huyu huyu liitwalo “Gharika” (linapatikana katika kitabu cha Masomo Yenye Adili).Nalo linaonyesha wasiwasi na machafuko yaliyoenea katika dunia. Katika ubeti wa 3 wa shairi la “Maswali na Majibu” kwa mfano, mshairi anasema:
Quote:Dunia imetubana,
Quote:Quote:Imetuvika masombo.
Quote:Tulikwenda kwa mapana,
Quote:Quote:Tukapiga watu fimbo,
Quote:Ngoma ikivuma sana,
Quote:Quote:Ni kupasuka kiwambo,
Quote:Roho vmejaa mambo,
Quote:Quote:Radha ziko wapi tena?
Malalamiko haya yanarudiwa kwa namna nyingine katika shairi la “Hai” ambamo mshairi anaomboleza kifo cha mwanae, ingawa hapa mshairi anaonyesha pia tumaini jema la faraja ya maisha baada ya kifo. Anasema kuwa japokuwa uhai ni kitu kidogo sana, lakini faraja ipo katika uhai uliopo “huko Ng’ambo hiyo.” Mawazo haya ni sawa na yale ayatoayo mwandishi huyuhuyu katika riwaya yake ya Siku ya Watenzi Wote – faraja yake yote iko juu ya siku ya ufufuo wakati watenzi wote watakapopangwa mbele ya Mola wao kupewa thawabu za matendo yao bora. Kwa Shaaban Robert tofauti baina ya masikini na matajiri zitaondolewa tu na Mwenyezi Murigu siku hiyo ya ufufuo. Utatuzi huu wa “kiutopia” ndio msingi mkubwa wa falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha.
Hata hivyo, hii haimaanishi kuwa Shaaban Robert kakata tamaa kabisa kuhusu maisha ya hapa duniani. Bado yapo mashairi machache ambayo yanaonyesha kuwa maisha hapa duniani yana uzuri wake. Kwa mfano, shairi la “Dunia Njema” (uk. 28) linaeleza kuhusu uzuri wa maisha. Beti za 2 na 3 zinasisitiza jambo hilo:
Quote:Dunia nzuri na mambo yake,
Yana fahari ya peke yake,
Juu sayari ni taa zake,
Quote:Quote:Chinijohari ardhi yake.
Quote:Zulia lake nyasi kijani,
Na majiyake mvua mbinguni,
Kushuka kwake milele shani,
Sifa ni zake Mola Manani.
Kutetea Haki na Kupinga Uovu
Shaaban Robert alijishughulisha pia na masuala ya kisiasa ya kutetea haki na kupinga unyonyaji, unyanyasaji, na uovu mwingine wote. Katika kitabu chake cha Maisha Yangi na Baada ya Miaka Hamsini tunaona jinsi alivyokuwa anapinga ubaguzi wa rangi uliomfanya Mwafrika kudunishwa, kudharauliwa na kunyanyaswa kutokana na rangi yake. Hate riwaya zake za Kusadikika (1951) na Kufikirika (1951) kimsingi zinatetea haki na kupinga ukoloni.
Katika diwani hii pia yapo mashairi ambayo yanapinga dhuluma na uayonyaji, japokuwa si mengi. Shairi la “Nani Atakutendea” (uk. 13), japokuwa linaeleza mambo mengi mengineyo, hapohapo linapinga unyonyaji wa mtu kufanyishwa kazi bila kupewa malipo:
Quote:Kazi bila manufaa,
Nani atakutendea
Sinifanyie hadaa,
Kungwi hakuniusia.
Sinifanye hamaki,
Shetani wangu hataki,
Sharti unipe haki,
Ndipo ataputulia.
Hata hivyo ni shairi la mwisho katika diwani hii, shairi la “Shukrani,” ndilo linaloiongelea dhamira ya vita baina ya uovu na wema kwa kirefu raidi ya mengine. Shairi hili ni la chereko chereko na lelemama za kupatikana kwa uhuru wa Tanganyika. Katika kuupokea uhuru huo mshairi anaturudisha ayuma na kutueleza madhambi ya ukoloni mkongwe. Anatueleza jinsi ambavyo wakulima wanatoka jasho kwa faida ya watu wengine. Anasema katika ubeti wa 2 na wa 3:
Quote:Kulima na kuchimbua halivunji mapatano,
Hasa tukikumbukia mapito mazito mno:
Na kulima kwa beluwa hali si yetu mavuno,
Wala halikuwa neno kwa wenye kututumia.
Kwa wenye kututumia hatukuwa na maneno,
Mchana kutwa wa jua katika ngwe ya mbono;
Kwa jazila ilikuwa ujira senti tano!
Hapakuwa na miguno yote yalivuniliwa.
Shairi hili pia linaonyesha jiasi ambavyo hali hiyo iliathiri hata mahusiano baina ya mke na mume (ubeti wa 4) kukawa na kutoelewana na kutotoshelezana kati yao. Twaelezwa vilevile kwamba, wananchi walizidi kukondeana kwa kutumikishwa katika mashamba ya mbono, ngano, katani, miwa, na kadhalika; mazao ambayo yote yalisafirishwa na kuyanufaisha mataifa ya nje.
Shaaban Robert, basi, anashangilia kupatikana kwa huo uhuru ambao anasema umefutilia mbali unyonyaji na unyanyaswaji huo. Kwa hiyo anamshukuru Mungu kwa huo uhuru; na baada ya napo anaishukuru Uingereza kwa kuikirimia Tanzania. Wakati ambapo ni rahisi kuelewa kwa nini Shaaban Robert anamshukuru Mungu hasa tukijua kuhusu maisha na malezi ya kidini aliyoyapata mshairi huyu, inakuwa vigumu kuzikubali shukrani azitoazo kwa Waingereza katika ubeti wa mwisho. Waingereza hawakukaribishwa na Watanganyika waje kututawala. Walitawala kwa nguvu; ndio wao waliowalimisha na kuwanyanyasa wananchi. Badala ya kuwashukuru dhalimu hawa ingefaa walaumiwe kwa ukoloni wao! Hapa basi, msimamo wa mshairi kuhusu suala la uhusiano baina ya mkoloni na mtawaliwa kuwanyenyekea wakoloni unatetereka.
Dhamira Zinginezo
Zaidi ya dhamira kuu tulizokwishachunguza, diwani hu imeshughulikia dhamira nyinginc ndogondogo kama furaha (“Kama Mfaime,” uk. 10), bahati (“Bahati,” uk. 10), kweli (“Nyuso Mbili,” uk. 1), mahaba na mapenzi (“Nasadiki,” uk. 6, “Siwezi,” uk. 24; “Nyakati,” uk. 26); umalaya (“Nyumba za Ngoma,” uk. 12), na mcagineyo.
MATUMIZI YA VIPENGELE VYA FANI
Katika diwani hii, kama ilivyo katika diwani zinginezo za Shaaban Robert, mshairi ameonyesha ustadi wakc wa kutumia mitindo mbalimbali ya ushairi.
Wakati ambapo waumini wa ushairi wa kimapokco wameviita vigezo vya mizani kumi na sita na vina kuwa ndivyo roho ya ushairi wa Kiswahili, Shaaban Robert amepevuka zaidi kwani katuonyesha kuwa si vizuri mshairi atawaliwe na muundo ule ule mmoja daima.
Katika diwani hii mshairi kaandika mashairi ya mizani minne hadi ishirini. Shairi la “Ni Wapuzi”‘ (uk. 27), kwa nafano, ni la mizani minne tu, na la “Nani Atakutendea” (uk. 13-14) ni la mizani 8, wakati ambapo yako ya mizani 12, 16 na kadhalika.
Kuhusu vina, mashairi mengi humu yamefuatia muundo wa vina wa ab/ab/ab/ab, Muundo huu unamaanisha kuwa vina vya kati vya kila mstari vinafanana katika kiia ubeti, na vya mwisho hali kadhalika. Muundo huu wa vina pamoja na ule wa ab/ba/ab/ba mara nyingi huonekana katika mashairi ya tarbia (au ya unne). Hapo hapa upo muundo wa kufuata jozi za vina ambapo mistari miwili ya kwanza ina vina vyake tofauti na vile vya mistari miwili ya mwisho ya ubeti. Hapa tunapata muundo wa ab/ab/cd/cd.
Pamoja na wingi wa miundo ya vina pia upo ule wa jumla ya mistari ya kila ubeti wa mashairi mbalimbali. Hapa pia ni rahisi kwa msomaji kuainisha mashairi tangu ya uwili hadi yale ya mistari ishirini kwa kila ubeti. Ila yatubidi tu tuelewe kuwa wingi au uchache wa naistari iundayo beti hutegemea jambo linaloongelewa. Wazo dogo tu hupewa mistari michache itakayolifanya liweze kunasa akilini mwa msomaji haraka. Jambo linalohitaji maelezo marefu hupewa mistari mingi, tena mirefu, na aghalabu huwa na beti nyingi zaidi ya zile za mawazo madogo madogo.
Matumizi ya taswira na ya misemo mbalimbali iliyoundwa ndani ya methali na nahau yamesaidia sana katika kuleta uzito wa mawazo yatolewayo. Shairi la “Mnyomele” (uk. 5) ni mfano wa fumbo lililofichika vizuri sana kutokana na matumizi yake ya taswira iniayowakilisha kitu kingine kabisa maishani.
Mshairi pia katumia taswira za maumbile kutoa maudhui ya mashairi yake. Kwa mfano tukiangalia shairi la “Dunia Njema” (uk. 28) tunaona vile ambavyo maumbile yamepewa jina la zulia. Twaiona dunia kuwa kama jengo zuri linalowahifadhi watu.
Katika shairi la “Nyakati” (uk. 26) mshairi katumia taswira ihusuyo fuajira na vile ambavyo lazima yanabadilika, halafu akatumia ustadi wa kulinganisha na kulinganua kwa kutumia tabaini kwa kila jambo. L’fundi huu umefaulu kumdanganya msomaji hadi sehemu ya mwisho ya ubeti wa mwisho ambapo ndipo ukweli kuwa shairi linaongelea mapenzi hujitokeza.
Mashairi mengi ya malumbano ama hutumia taswira nzito nzito au lugha ya kimafumbomafumbo ya kimethali. Mfano ni shairi la “Nazi” (uk. 7′) linavyodai kuwa kamwe nazi haiwezi kuvunja jiwe; au lile la “Silumii Shoka Ukucha Unapofaa” (uk. 37-39) ambalo moja kwa moja linafaulu kuwanyamazisha wapinzani kwa kuwafanya wajisikie wadogo wasiofaa mbele ya mshairi huyu. Katika fungu hili tunaweza kuyaweka pia mashairi ya “Wapinzi” (uk. 3), “Ngozi ya Simba” (uk. 3-5), Mwezi Hauwi Jua” (uk. 39-40), na kadhalika.
Shairi la “Halali Kuca” twaweza kulichukua kuwa mfano mzuri wa matumizi ya lugha ya kinahau. Ndoa imeitwa kuwa ni “Nyama ya mafuta.” Ilivyo, nyama ya mafuta ni nono inayotamaniwa na watu wengi. Mfano huu unaifanya ndoa ionekane kitu bora sana ikilinganishwa na ujane.
Matumizi ya aina hii ya lugha, ishara na taswira, pamoja na upana ws miundo ya vina na mizani katika ushairi wa Shaaban Robert, ndivyo vigezo vilivyosaidia sana kuvafanya maudhui ya mashairi yake yaeleweke vizuri, na kuyafanya mashairi yake kwa jumla yapendwe sana na yampe sifa ya shaha wa malenga.
Maswali
1. Zijadili dhamira muhimu ambazo zimeibuka katika Ashiki Kitabu Hiki. Je, mwandishi kafaulu au kashindwa vipi kuzichambua dhamira hizo?
2. Jadili msimamo wa Shaaban Robert kuhusu wanawake kama ujitokezavyo katika Ashiki Kitabu Hiki.
3. Taswira ya athari za maisha ya kibepari inajitokezaje katika Ashiki Kitabu Hiki?
4. Zijadili falsafa za mwandishi kuhusu ndoa na maisha kama zijitokezavyo katika Ashiki Kitabu Hiki.
5. Yajadili matumizi ya vipengee vifuatavyovya fani kama yalivyojitokeza katika Ashiki Kitabu Hiki:
Quote:a) vina na mizani
b) mistari
c) matumizi ya picha (taswira)
d) lughakwajumla
e) ishara.
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (12) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 09:36 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
11. Shaaban Robert: Kielelezo cha Fasili
SURA YA KUMI NA MOJA
Katika Kielezo cha Fasili, Shaaban Robert kwanza kabisa katutolea nadharia yake ihusuyo fasili na ufafanuzi wa mashairi. Ufasili, katwambia, waweza kufanywa kwa njia kuu mbili: sabilia na sisisi. Twaelezwa kuwa wakati sabilia huhusu fasili kwa ujumla, sisisi hushughulilda vipengele mbalimbali vya kazi inayofasiliwa.
Katika kitabu hiki basi, mwandishi kafasili mashairi yake mwenyewe, akayapa maana alizozikusudia alipoyaandika. Jambo hili limembana msomaji au mhakiki wa mashairi haya kwa kutoachiwa uhuru wa kutoa maana natafsiri imjiayo mawazoni mwake. Hata hivyo, kwa wale ambao ndio kwanza wanauingia ulimwengu wa ufafanuzi wa mashairi, huenda kazi aliyoifanya Sbaaban Robert ikawa ya manufaa kwa kuanzia.
Kwa kifupi, maelezo ya Shaaban Robert yanamwelekeza msomaji wa mashairi kujiuliza na kujaribu kuyajibu maswali kadhaa muhimu baada ya kusoma shairi. Kati ya hayo, mengi yanahusu kiini cha shairi, yaaai mfuatano wa fikra za mshairi hadi kufikia hitimisho fulani. Kwa hiyo basi, kadri msomaji anavyoendelea kusoma shairi hujiuliza kama mshairi anataka kusema nini, na hicho atakacho kukisema anakisemaje.
Baada ya kujiuliza haya, msomaji sasa yuko tayari kulichambua shairi. Katika ukurasa wa (xix) wa Kielelezo Cha Fasili, Shaaban Robert katoa maonyo kadhaa kuhusu namna ya kufasili, yaani jinsi ya kusema habari iliyokwishasemwa na mtu mwingine kwa namna ambayo si ya kukariri au ukuasuku wa habari asilia. Japokuwa rnaonyo ayatoayo Shaaban Robert ni nauhimu sana kwa msomaji na mhakiki wa mashairi, ni wazi kuwa kwa leo hii nadharia yake ya uchambuzi baitoshelezi japo ilikuwa kianzio kizuri. Hapa tutatilia maanani mawazo yake pamoja na yale tuliyotoa katika Utangulizi wa kitabu hiki kuyachambua mashairi ya Kielezo Cha Fasili.
DHAMIRA KUU
Katika diwani hii, Shaaban Robert ameshughulikia dhamira mbalimbali ambazo aghalabu hujitokeza katika kazi zake zinginc za ushairi, riwaya na hata insha na wasifu. Baadhi ya hizo zinahusu mambo yafuatayo:
Quote:1. Maana ya maisha
2. Maadili (kuadibu)
3. Siasa
4. Mambo mengineyo kwa jumla
Maana ya Maisha
Kuhusu maana ya maisha, Shaaban Robcrt anao msimamo uyaonayo kuwa ni ya utupu, hayana furaha wala amani. Katika shairi la “Sikia Yanena” (uk. 2) twaelezwa vile ambavyo maisha hayawapi watu chochote kingine isipokuwa hofu na wasiwasi.
Shairi la “Mtu na Malaika” (uk. 11-12) ni kielelezo kizuri sana cha falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha. Shairi lote ni ndoto imkutanishayo mtu na malaika; na katika ndoto hii mtu anapata “ufunuo” ambao unamweleza kuhusu maana ya maisha. Shairi zima linalinganisha maisha na safari, tena safari yenyewe ni ya mzunguko usio na mwanzO wala mwisho. Twaelezwa:
Quote:Neno lenye mzunguko, halipatikani mwisho
Wa huku hafiki huko, wala halina malisho
Hapa, shairi linaongelea dira, na dira hii inaonyesha kuwa maisha ni utaratibu maalumu usiobadilika japokuwa ingekuwa vema sana kama watu wangeweza kwenda katika njia iliyonyooka itakayowapeleka na kuwafikisha watakako. Mshairi anaendelea kusema:
Quote:Heri ya mtu ni kwenda, njia iliyonyooka,
Na milima akapanda, apendako akafika,
Mabondeni akashuka, mwituni akatumbua,
Na mitoni akavuka, hata alikonuia.
Sehemu hii ya shairi inaeleza umuhimu wa kufanya juhudi ya kuendesha maisha hata kama maisha yenyewe yaelekea kuwa “njia” ya dira” ambayo kwa hakika si njia, kwani twaelezwa, “na mzunguko wa dira, mwisho wake ni dirani.”
Kwa hiyo basi, japokuwa taswira ya dira ni ya kukatisha ‘tamaa kwani yatoa kauli kuwa maisha ni mzunguko usio na mwisho, na mzunguko huu umejazana taabu, mashaka na wasiwasi mwingi; shairi hili pia lina upande wake wa pili uibushao moyo wa matumaini mema kuhusu maisha.
Ncha hiyo ya pili ya shairi la “Mtu Na Malaika” inakanusha mawazo ya baadhi ya wahakiki waliomwona Shaaban Robert kuwa daima aliyanunia maisha. Inashirikiana na mashairi mengineyo, kwa mfano lile la “Cheka Kwa Furaha” (uk. 15) kuonyesha upande wa pili wa safaru ya maisha; upande ambao watuusia kuwa maisha si ya kununiwa; kwamba ijapokuwa yamejaa huzuni huweza kuwa ya furaha iwapo mtu atacheka kwa furaha:
Quote:Cheka sasa kwa furaha; dhiki ingawa usoni,
Dhiki ni kama mzaha, asiyecheka ni nani?
Haya cheka ha! ha! ha!, ndiyo ada duniani:
Cheka mwanadamu cheka, mtu kaumbwa acheke,
Msiba kwake dhihaka, kicheko mtu mwenzake.
Katika shairi hili hili la “Cheka Kwa Furaha” tunagundua mambo makuu matatu yahusuyo falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha. Kwanza kunao msisitizo Juu ya umuhimu wa juhudi na ari maishani, msisitizo ambao hata katika shairi la “Mtu Na Malaika” unajitokeza. Mistari kadhaa ya “Cheka Kwa Furaha” inaonyesha msisitizo huo:
Quote:Cheka upone jeraha, yaepuke na mashaka
Na mwili kupata siha, ukianguka inuka
Inuka juu inuka, chini usigaegae
Inuka na kisha cheka, kucheza uendelee
Jambo la pili tuligundualo katika shairi hili ni moyo wa matumaini mema kuhusu maisha; kwani mshairi anatuambia kuwa cheko ni dawa inayotia nguvu mwilini na inayoleta matumaini katika mioyo ya watu.
Hata hivyo, humuhumu katika sbairi hili upo upande wa pili wa falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha. Huu uko katika jambo la tatu tulionalo shairini: hofu ya mauti. Japokuwa mshairi kashauri watu wacheke, hapohapo anawatahadharisha wajiweke tayari, ndiyo maana anamalizia shairi zima kwa kipande cha: “Cheka usiwe na shaka, itakuja zamu yako”. Hii tahadhari kuhusu kifo ilijitokeza sana katika baadhi kubwa ya maandishi ya Shaaban Robert; kwa mfano, katika riwaya yake ya Siku ya Watenzi Wotekashughulikia zaidi tahadhari hiyo ambayo kimsingi ilinuia kutatua matatizo ya jamii kwa mahubiri na vitisho vya dini.
Kidogo falsafa yote itolewayo na mshairi katika shairi la “Cheka Kwa Furaha” inatatanisha na hata kuchekesha. Inakuwa vigumu kuelewa jinsi mtu mwenye dhiki ya njaa atakavyoweza kuamua kujichekea tu na njaa yake. Kicheko atushauricho Shaaban Robert ni cha kilevi ambacho hutolewa kusahaulisha matatizo yaliyopo kwa muda mfupi tu wakati kitolewapo, na mara baada ya hapo matatizo huwa palepale. Kucheka hakuondoi dbiki, matatizo wala huzuni, kama sababu na msingi wa dhiki, matatizo na huzuni hiyo haijashughulikiwa kiukamilifu: kwa hakika kicheko hakitoki katikati ya dbiki na matatizo!
Shaaban Robert alisisitiza pia kuhusu umuhimu wa mabadiliko katika maisha na umuhimu huu unajitokeza vizuri sana katika shairi la “Ukaidi” (uk. 18-19) anaposcma:
Quote:Nashikilia ukale ambapo hapana budi,
Na huacha vile vile iwapo haunifidi,
Nitabadili milele siwezi kuwa abidi,
Wa kutenda yale yale kuizuia juhudi
Kale sina huba nayo nawachia wakaidi
Na watu wenye mioyo yenye hasira shadidi,
Kupinga mambo yajayo; eti waledi zaidi
Wao na washike yao, nami naridhi fuadi
Umuhimu huu wa mabadiliko twaweza kuupanua na kuuelekeza katika uwanja wa ushairi kwani Shaaban Robert anasema kuwa hatakubali kufungwa na minyororo ya sheria zinazoshikiliwa tu bila sababu muhimu na nzito. Ndiyo sababu hata katika mashairi mengi ya diwani hii, kwa mfano, Shaaban Robert katumia aina mbalimbali za miundo toka katika urefu wa beti (badala ya kushikilia tu tarbia) hadi katika wingi wa mizani. Mkabala huu twaweza kuudondolea ubeti mmoja muhimu katika shairi hili (ubeti wa 11):
Quote:Sasa nawajitoge kwa sanaa kusanidi,
Majoho yao wavae na vielbe wale Idi,
Na ufundi uzagae kwa marifa kuzidi;
Mazonge wayazongoe kwa kazi siyo madadi.
Mashairi mengi katika diwani hii na katika diwani zinginezo za Shaaban Robert yameyaona maisha kuwa ni msukosuko na fujo tupu. Kwa mfano, katika shairi la “Kinyume” (uk.26) anasema (ubeti wa 7):
Quote:Masikini akipata, matako hulia mbwata
Na tajiri hutafuta, kamari, bima, karata
Maisha yana matata, na dakika ikipita
Umri umeshakata, kovu kubwa ya kufuta.
Shaaban Robert si mpweke katika ushairi wenye mkabala huu kuhusu maisha. Hata baadhi ya washairi wa leo wanayaona maisha hivyo, kwa mfano E. Kezilahabi ambaye katika diwani yake ya Kichomi (Heinemann, 1971) ana mashairi yanayochukua mkabala huo (angalia, mathalani, shairi la “Nimechoka”). Kila kazi ya sanaa huathiriwa na kufinyangwa na wakati, nayo huwakilisha mawazo, matazamio na mahitaji ya watu katika wakati maalumu wa kihistoria. Kwa Shaaban Robert inakuwa rahisi kuelewa sababu za mkabala wake kuhusu maisha, hasa kwa vile hata kiwango chake cha elimu na cha mwamko wa kisiasa hakikuwa cha juu tukilinganishapo na cha Kezilahabi. Kezilahabi aelekea kuongozwa na falsafa iliyojengwa na athari za elimu aliyoipata (kutoka kwa akina Satre na wengineo) zaidi ya hali halisi za jamii yake. Shaaban Robert yeye anaongozwa na falsafa iliyojengwa na kufinyangwa na kiwango cha mwamko wa jamii yake na hali halisi za jamii hiyo kisiasa, kiutamaduni na kiuchumi; japokuwa hii haimaanishi kuwa wakati huo hapakuwa na waliokuwa wameamka na kupevuka zaidi kimsimamo kuliko akina Shaaban Robert.
Zaidi ya kutuelcza kuwa maisha ni vurugu tupu na kwamba kitu hiki ni cha kupita tu, hakidumu (angalia shairi la “Umri,” uk. 29), Shaaban Robert katoa utatuzi mwingine wa mashaka hayo ya maisha. Ikiwa wakati mwingine aliouona utatuzi huo katika siku ya ufufuo (angalia shairi la “Mbioguni,” ul. 32), kwa hiyo akaona kuwa kila tendo jema ni daraja ituongozayo kwenda mbinguni; na kama wakati mwingine dawa ya mashaka hayo ya maisha aliiona katika kicheko; sasa katika shairi la “Kinyume” anatueleza dawa nyingine: mapenzi, ambayo alikwishaiandikia diwani nzima ya Mapenzi Bora (Nelson, 1967). Katika ubeti wa 11 wa shairi la “Kinyume” anatuambia:
Quote:Watu wanachukiana, hawataki kujivuta,
Pamoja wakapendana, kama mimea na tuta
Hawataki kupatana, kama maji na mafuta
Naghafula wawaona wenyewe wanajiseta
Ni wazi kwamba, ijapokuwa “dawa” ya “mapenzi” inasikika vizuri sana masikioni, hatimaye udhaifu wa “dawa” hii ni sawa na ule tuliouona katika “kicheko”.
Maadili (kuadibu)
Daima katika uandishi wake, Shaaban Robert alikuwa sawa na babu na bibi waliowaketisha wajukuu zao na kuwapigia hadithi kwa madhumuni ya kuwatolea maadili yaliyobeba amali za jamii. Kwa hiyo itaonekana wazi kuwa mashairi mengi ya Shaaban Robert ni ya kimaadili yamfanyayo aonekane kama mwalimu wa walimwengu; na baadhi kubwa ya maadili hayo hutokana na uzoefu wa maisha aliyoyapitia yeye mwenyewe.
Kati ya maadili hayo amesisitiza kuhusu umuhimu wa watu kupatana na kuepuka ugomvi (angalia shairi la “Ubora Wetu” uk. 42, hasa ubeti wa 2), umuhimu wa kuepuka moyo wa kijicho na chuki (“Sumu” uk. 51), na pia umuhimu wa kuoa. Katika shairi la “Jina” (uk. 54) twaelezwa kuwa furaha huletwa na vitu vikuu vitatu: akili ya kufikiri na kutambua jema na baya, fikra ya kutafakari mambo, na matendo yenye maana nzuri maishani mwa watu.
Sifa nyingine iibukayo mara kwa mara katika maadili ayatoayo Shaaban Robert ni ile ya uchaguzi bora wa maneno. Katika shairi la “Maua na Maneno” (uk. 13) mshairi anasema:
Quote:Maua huchaguliwa, ndipo nyuki akaweza,
Asali kuyachujua, tamu naya kupendeza,
Mpaka katika mew, warembo wanayaweka,
Ni yakung’ariza, siyo yale ya kunuka,
Ua lolote porini, nyuki shida kuchukua,
Unga uliyomo ndani, ama mnato wa ua.
Kitu gani achelea? Maua mengine sumu,
Kwa nyuki kuyatumia, na pia kwa mwanadamu,
Licha nyuki hata ndege, wana maua wahofu
Panzi pamoja na nzige, wakiyala huwa wafu.
Palipo ua dhaifu, rw hapakaribii,
Mlaji kila uchafu, huhofu nanwa hii!!
Ubeti huu pamoja na wa pili hujenga taswira inayohusu aina mtrili za maua; picha ambayo kwa muda huweza kumchota na kumdanganya msomaji kuwa shairi linahusu maua. Halafu baada ya kuijenga na kuikamilisha taswira hii, ndipo katika ubeti wa 3 wa shairi mwandishi anatoa kauli:
Quote:Hali ikiwa hivi, na maneno kadhalika,
Watu wasiwe walevi, wakati wa kutamka.
Wakati ambapo neno zuri limefananishwa na ua zuri, neno baya limeitwa risasi, kinywani likishatoka. Kwa hiyo basi, watu watakapo-weza kuchagua maneno mazuri, watafaulu kutengeneza uhusiano mzuri kama asali ya nyuki itokanavyo na maua mazuri.
Huenda kwa baadhi ya wasomaji wa shairi la “Udhia Wa Mali” (uk. 2), Shaaban Robert ataonekana kuwa anapinga kuwa na mali kwa vile tu yeye mwenyewe hanayo mali. Lakini kwa wasomaji wanaochambua kwa undani, wataona kuwa shairi hili ni la kimaadili lituasalo kuwa ili mali isiwe na udhia yafaa wote wawe nayo; na kwamba ni udhia mtupu ikiwa una mali nyingi na wenzako wakuzungukao hawana. Twaweza kupanua maana hii na kuipa welekeo wa kisiasa kuwa shairi hili linatetea usawa baina ya watu.
Mashairi mengine katika diwani hii ambayo tunaweza kuyaita ya kimaadili ni “Cheka kwa Furaha,” “Ukaidi,” “Heshima.” “Woga,” “Fitina,” na “Kweli.”
Siasa
Masuala mbalimbali ya kisiasa yaliishughulisha sana kalamu ya Shaaban Robert. Kwa vile mshairi huyu aliishi nyakati za ukoloni ni wazi kuwa asingeweza kukwepa uhalisi wa maisha ya kikoloni yaliyokuwa yakiwaonea na kuwadhulumu wananchi.
Katika shairi la “Kashata na Ladu” (uk. 37), mshairi anaongea kuhusu serikali mbovu ziongozwazo na watu; serikali ambazo ni duni kuliko zile za wanyama, ndege na wadudu.
Kama luunavyu kutika diwani yake ya Maisha Yangu Baada ya Miaka Hamsini (Nelson, 1968), Shaaban Robert ameonyesha ubaguzi wa rangi uliokuwepo katika jamii yake ambapo Wazungu walipewa (au walijipa) nafasi yajuu wakifuatiwa na Wahindi, halafu Waarabu, na wa chini kabisa wakiwa Waafrika. Katika diwani hiyo Shaaban Robert aliilalamikia vikali hali hii iliyowagawagawa watu katika mafungu kufuatana na rangi zao. Katika Kielezo cha Fasili jambo hili amelisisitiza katika shairi la “Kama Upindi wa Mvua” (uk. 44) ambalo linatueleza kuwa rangi mbalimbali alizoziumba Mungu si za kuletea ubaguzi bali ni kama mapambo tu ya kuongezea uzuri wa dunia.
Shairi la “Vivuli” (uk. 55) linakumbusha yale yasemwayo na mshairi huyuhuyu katika shairi lake lingine la “Gharika” (lililoko katika diwani ya Masomo Yenye Adili, uk. 62). Mashairi haya mawili yanaongea kuhusu uhasama na machafuko ya kisiasa yaliyoko duniani. Sehemu ya mwanzo ya “Vivuli,” kwa mfano, inaeleza kuhusu migongano ya mataifa makubwa ambayo imeleta machafuko na maangamizo makubwa duniani. Mshairi anasema:
Quote:Wenye kuchana magando, na sumu ya kuulia,
Wamo katika mkondo, na tufani ya tabia,
Na ghasia ya matendo, uhalifu na hatia,
Hapana chembe upendo, kwa ualili na ria,
Pamebakia uvundo kila pembe ya dunia.
Picha tuipatayo katika shairi hili ni ile ya wasiwasi na ‘ghasia tupu pamoja na vitisho viletavyo maangamizi makubwa hadi woga umewaingia hata simba na nondo. Picha hii ya wanyama wakubwa-simba na ndovu-walioingiwa na woga na hali kwa kawaida si waoga, na ile ya nondo – mdudu ambaye ana ujasiri mwingi wa kuchezeachezea ndinu za moto ila sasa yu aogopa-ni taswira ikamilishayo mabadiliko mabaya yatokanayo na mivutano kati ya wenye kucha “na sumu ya kuulia.”
Shairi lingine la kisiasa ambalo limewahi kuzusha ubishi kati ya wanazuoni kuhusu maana aliyokuwa nayo mshairi alipolitunga ni la “Kufua moyo.” Kimsingi linaongea kuhusu ushujaa wa askari apiganaye vitani na ambaye hata kama atauawa hafi kwani huendelea kuishi katika kumbukumbu za watu wote, wazee kwa watoto. Hata “uvundo wa mashujaa’ mwandishi kaufananisha na manukato kuonyesha jinsi ambavyo, kama asemavyo mwandishi mwenyewe katika fasili yake, “uvundo wa maiti ya mashujaa ni sawasawa na mafuta ya uturi na marashi usio na harufu ya karaha wala fukuto.”
Kijuujuu shairi hili huweza kusifiwa sana kuwa linasisitiza kuhusu ushujaa na uzalendo. Lakini, kimsingi hili ni shairi ambalo halitupeleki mbali sana kwani linaongelea kijumla tu kuhusu vita na ushujaa wa kufa katika vita hivyo bila kutueleza hasa ni vita gani, vya kumtetea nani na kumsuta nani, na kama ushujaa huo ni kwa jicho la nani. Huu basi ni uzalendo na ushujaa usio na welekeo kamili.
Shairi la “Kuondoana Njiani,” sawa na la kupinga ubaguzi wa rangi, linatetea usawa baina ya watu, nalo linakemea wanyonyaji wanaofanyiza watu kazi bila ujira:
Quote:Kazi za sasa hasara, kwa jamii wafanyao
Nyingi kukuru kakara, hazitimizi chajio;
Wenye nguvu wadodora, wako wapi wachumao?
Fanya kazi kwa imara, tajiri apate cheo,
Kichwa kiote kipara, macho uvae vioo;
Huzidishwi mshahara, wala huna fanikio,
Tutatenda ndivyo sivyo tuondoane njiani.
Mvutano baina ya waajiri, wanyonyaji na waajiriwa wanyonywaji, umeonyeshwa jinsi unavyowadidimiza watu wa chini huku wanyonge hao wakiandamwa na ghera, hasira na matusi ya waajiri.
Hata hivyo, kama kawaida, baada ya kueleza maovu ya waajiri kwa waajiriwa, Shaaban Robert anatoa suluhisho lilelile la kidini la kuwaambia watu kuwa maamuzi yote yatatolewa huko ahera. Haya anayaeleza katika ubeti wa 10:
Quote:Kutumiwa kama nyara, mimi furaha sinayo,
Takwenda nayo ahera, machungu niliyo nayo;
Kuna maamuv bora, ya dhuluma kama hiyo.
Ni wazi kuwa hapa Shaaban Robert kaitumia dini kuwa kimbilio la mnyonge ambaye kakata tamaa; kimbilio ambalo halimsaidii mnyonge huyo kumuondolea unyonge uliomzingira. Ndiyo sababu hata yasemwayo katika sbairi la “Sala na Saumu” inakuwa vigumu kuyakubali moja kwa moja kwani aghalabu sala na saumu pekee bila vitendo muhimu vilivyohusishwa na mizizi ya matatizo ya jamii ni bure tu!
Shairi la “Muadhama Richard Turnbull” limetajwa kuwa moja ya mashairi aliyoyaandika Shaaban Robert yanayotatiza na yanayotufanya tuushangae msimamo wake kwa wakoloni. Hatuoni sababu hasa – zaidi ya kujipendekeza kwa watawala – ya kumwombea afya njema kiongozi huyu wa kikoloni!
Mambo Mengiaeyo
Zaidi ya falsafa kuhusu maisha, maadili na siasa kwa jumla, diwani hii ya Kielezo cha Fasili imeshughulikia pia masuala mengine ingawa si kwa kirefu kama hayo tuliyoyachambua. Kati ya hayo, kubwa ni suala la “ukweli” wa maisha linalohusu hatua mbalimbali za maisha ya mtu tangu kuzaliwa, kuzeeka na kufa. Hapa yapo mashairi ya “Umri,” “Fumbo,” “Sichelei Kufa,” “Uzee,” na kadhalika.
Katika hatua hizo mbalimbali za maisha ya mtu, hatua ya ndoa imepewa uzito na nafasi kubwa zaidi ya zingine katika diwani hii. Katika ubeti wa mwisho wa “Sichelei Kufa” mshairi anasema:
Quote:Ndoa kitu ashrafa utumwa wajia nini?
Ndoa jambo mzofafa huwaje umajununi?
Ndoa ni lulu nadhifa nimehuni kifu gani?
Ushairi wa Shaaban Robert ulithamini mno taasisi ya ndoa, na ndiyo sababu hata katika malumbano mengi tuyakutayo katika diwani nyingine ya nashairi huyuhuyu ya Ashiki Kitabu ffiki (Nelson, 1967), anatetea sana ndoa. Shairi la “Ndoa Ni Kanuni” Kielezo cha Fasili (uk. 70-71), laielezea ndoa kuwa ni kanuni na ni amri ya Mungu. Ubeti wa 7 wasema:
Quote:Ndoa rutuba ya A llah, kuoa ubaya gani?
Ndoa hukuza mahala, mmoja huwa theneni,
Kuoasi mghafala, kuoa kwetu kanuni
Hivyo basi, ndoa kwa Shaaban Robert ni wajibu kwa watu wote. Mkabala huu unajitokeza si katika ushairi tu wa Shaaban Robert, bali hata katika baadhi ya riwaya zake, kwa mfano katika Utubora Mkulima na Siku Ya Watenzi Wote,
Wakati ambapo kidini huenda mkabala huo ukakubalika, kimaisha halisi inaonyesha kuwa taasisi ya ndoa haina budi kuangaliwa sambamba na hali halisi za jamii amazo ndizo zilizoizaa na ndizo zinazoilea ama kuiua taasisi hiyo. Si kila ndoa ni nzuri; na mara kwa mara katika jamii ambayo haijawa na usawa kati ya watu kiuchumi na kimaisha kwa jumla, taasisi hii hujazana mafarakano na ugomvi mwingi ambao kuibuka kwake kunahusiana na maisha mabaya yatokanayo na mfumo mbaya wa jamii. Hii ndiyo sababu talaka zimejazana sana katika jamii za kibepari kwani taasisi hii, sawa na zinginezo za jamii hiyo, hukuzwa katika mismgi ya kibepari.
MATUMIZI YA VIPENGELE VYA FANI
Tumekuwa tukitaja hapa na pale kuhusu matumizi ya vigezo mbalimbali vya fani katika diwani hii, hasa kigezo cha taswira. Taswira zimejitokeza mahali pengi sana katika mashairi haya, nazo zimetumiwa vizuri kuyajenga maudhui ya ashairi. Katika shairi la “Maua na Maneno” kwa mfano, Shaaban Robert katujengea kwanza taswira kamili ya maua mbalimbali, taswira ambayo iunganishwapo na kauli aitoayo mshairi kuhusu umuhimu wa kufanya uchaguzi mzuri wa maneno msomaji huupata ujumbe kwa uwazi zaidi.
Shairi la “Mtu na Malaika” pia limetumia taswira nadto ya dira kusisitiza falsafa ya Shaaban Robert kuhusu maisha yalivyo mzunguko usio na mwisho.
Vile vile shairi la “Kama Upindi wa Mvua” ni mfano mzuri wa uundaji wa taswira ambao unalitoa wazo kuu la shairi kwa njia inayonata vizuri sana akilini mwa msomaji.
Zaidi ya mbinu hii ya fani, mashairi mengi humu hutumia pia miundo mbalimbali ambayo hutofautiana katika wingi wa mizani, aina za vina, urefu wa beti, na kadhalika. Jambo hili limeyafanya mashairi haya yasichoshe na yasomeke vizuri zaidi.
Ni dhahiri kuwa kwa Shaaban Robert hatuna haja ya kutaja sifa ya matumizi bora ya lugha kwani anayo tangu mwanzo mpaka mwisho. Ni sifa ambayo humweka msomaji katika hali ya kutaka kusoma zaidi kwani uchaguzi wake wa maneno ni mzuri mno hata ni vigumu kuona neno lolote lile lililochomekwa tu au lililolazimishwa kutokana na kanuni za vina na mizani, kama ilivyo kawaida ya washairi wengi wa leo wajitokezao hasa katika magazeti.
Kwa upande wa lugha pia yapo matumizi ya tamathali mzo mzo za usemi ambazo zaidi ya kuyapamba mashairi haya zimeongeza uzito wa maudhui yaibushwayo. Baadhi ya tamathali bizo zimejikita katika taswira au ishara kama zile tuzionazo katika mashairi ya “Mtu Na Malaika,” “Maua na Maneno,” na kadhalika. Katika shairi la “Ushairi” (uk. 23) twaona vile ambavyo Shaaban Robert anauthamini sana ushairi kwa jinsi anavyoupamba kwa tamathali nyingi. Anauita “hirizi ya sudi,” “malaika,” “madini za shani,” “huba,” “johari na mvua yenye samadi,” na kadhalika. Kijicho na chuki vimeitwa kuwa ni “sumu” katika shairi la “Sumu” kuonyesha jinsi ambavyo hudhuru uhusiano mzuri baina ya watu. Vivyo hivyo shairi la mwisho, “Kweli” (uk. 93-94), limedhihirisha ufundi wa Shaaban Robert wa kutumia tamathali zinazosadifu sana jambo aliongelealo. Kweli imeitwa “kito mahabubu,” “siri ya ajabu,” “chimbo la johari,” “maadeni nzuri,” “vunjo la kiburi,” “jambo ashrafu,” “nuru takatifu,” “nguvu ya imani,” “kitu cha thamani,” na kadhalika.
Ufundi wa Shaaban Robert wa kutumia tamathali za usemi, hasa za sitiari na tashbiha, na matumizi mazuri sana ya lugha pamoja na ya ishara na taswira, ni baadhi ya vigezo muhimu vya fani vinavyofaulisha maudhui ya mashairi yake, na ndivyo vimpavyo sifa ya ushaha wa malenga na kumweka sambamba na washairi wengine maarufu kama vileMuyaka bin Haji wa Mvita.
Maswali
1. Chunguza nadharia ya fasili aitoayo Shaaban Robert katika “Utangulizi” na ujadili uhusiano wake na uchambuzi wa mashairi.
2. Cbagua dhamira kuu mbili alizozishughulikia Shaaban Robert katika Kielezo cha Fasili ujadili zilivyoibushwa kwa kuzitolea mifano mahsusi.
3. Yajadili matumizi ya lugha taswira na isbara katika mashairi ya Kielezo cha Fasili.
4. Je, “vivuli” ni nini katika shairi la “Vivuli”?
5. Chagua shairi moja kati ya “Mfua Bati,” “Kufua Moyo,” na “Kweli” ujadili ujumbe wake na jinsi taswira zilivyotumiwa kuuibusha.
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (13) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 09:28 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
12. Mwanakupona (Nana): Utenzi wa Mwanakupona
SURA YA KUMI NA MBILI
Kwa sababu utenzi huu wa Mwanakupona hubainisha vile ambavyo fasihi huwa katika jamii ya kimwinyi, yatubidi tuanze na maelezo ya jumla kuhusu fasihi ilivyo katika mfumo huo wa jamii. Maelezo hayo yatatusaidia katika kuupa utenzi huu uzito wa kiuchambuzi.
Fasihi Katika Mfumo wa Kimwinyi
Mfumo wa kimwinyi unabainishwa na mahusiano ya jamii ambayo ni ya kiutwana na ubwana, ambayo yamefikia hatua mpya ya juu zaidi, na tabaka tawala (la mamwinyi) hutawala njia zote za kiuchumi na za kitamaduni. Katika makala yake ya “Ushairi wa Kiswahili ni Nini” (Lugha Yetu, 26 – uk. 12), M.M. Mulokozi amelielezea tabaka hali kama ifuatavyo:
Quote:Uozo na ubaradhuli wa maisha ya kiumwinyi, hasa wakati mfumo huu unapoanza kutetereka kutokana na nguvu za jamii na za uchumi, huwafanya mamwinyi, katika maisha yao ya kizembe na kifasiki, wapendelee sana mambo ya kuvutia macho na kuliwaza pua, kama vile mapambo aina aina, wanawake wazuri, nakshi, na marembo ya rangi za kuvutia katika makazi na malazi yao… marashi, manukato, udi na ubani na kadhalika.
Maisha ya namna hii aliyoyaeleza Mulokozi vilevile hujitokeza katika fasihi itokanayo na mfumo huu (na inayopata udhamini kutoka kwa tabaka tawala). Si katika Utenzi wa Mwanakupona tu, bali pia katika kazi zingine kama vile utenzi wa Al Inkishafi ulioandikwa na S.A.A. Nasir (Oxford, 1972). Katika Al Inkishafi, utaona maelezo yatolewayo kuhusu uzuri wa majengo na makazi ya masultani wa Pate, na pia ule wa wanawake ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwaimbia wakubwa hao, kuipepea usiku kucha, pamoja na kuwatumikia. Beti za 43 hadi 57 za Al Inkishafi ni vielelezo vizuri vya mapambano yaabatanayo na ufasiki wa kimwinyi.
Kabla ya kuchunguza ni kwa vipi mambo yote hayo na mengineyo ya kimwinyi yamejitokeza katika Utenzi wa Mwanakupona yafaa kwanza tujikumbushe historia ya utenzi huu.
Historia fupi ya Utenzi wa Mwanakupona
Kama tuelezwavyo katika Utangulizi ulioandikwa na Ahamad Sheikh Mohamed Nabhany Mtamwini, Utenzi wa Mwanakupona ni utenzi maarufu sana ambao mwanzoni ulitungwa na mwanamke mmoja aliyeitwa Nana. Baada ya kutungwa hivyo ulisambazwa kwa njia ya masimulizi, huku ukizidishwa ama kupunguzwa jumla ya beti kufuatana na kumbukumbu za moyoni za wapokezi na wasambazaji.
Mtaalamu mmoja wa fasihi na lugha J.W.T. Allen alizifanyia utafiti nakala mbalimbali za utenzi huu akachagua nakala moja ambayo aliiona kuwa inaingiza mambo mbalimbali yajitokezayo katika nakala zote.
Nana ni jina la utani tu la Mwanakupona aliyeishi katika nusu ya kwanza ya karne ya kumi na tisa. Mume wa Mwanakupona alikuwa mtu maarufu katika historia ya Waswahili. Aliitwa Bwana Mataka, Shehe wa Siu. Huyu yasemekana kuwa alipigana vita vya msituni kwa muda wa miaka ishirini akipinga utawala wa Sultani wa Zanzibar, Seyyid Said.
Mwanakupona alikuwa na watoto wawili, wote wa Bwana Mataka. Wa kwanza alikuwa mwanamumc aliyeitwa Muhammad bin Sheikh, na wa pili alikuwa binti aliyeitwa Mwana Hashima binti Sheikh. Huyu wa pili ndiye ambaye anahusika katika wasia utolewao kwenye Utenzi wa Mwanakupona, utenzi ambao ulitungwa na Mwanakupona alipokuwa anakaribia kufariki.
DHAMIRA KUU
Tutaanza kwa kuchambua vile ambavyo wasia utolewao juu ya wanawake na jukumu lao la kifamilia na kijamii lilivyoshikamana na misingi ya kimwinyi ambayo tuliitaja hapo awali.
Tulisema kuwa amali za kimwinyi husisitiza sana juu ya mapambano na uzuri wa juu juu. Katika Utenzi wa Mwanakupona msisitizo huo unajitokeza waziwazi. Tunauona katika “uzuri” ambao Mwanakupona anataka binti yake awe nao. Uozo wa mfumo wa kimwinyi husisitiza kuhusu mambo yanayovutia macho, na athari ya mkabala huu twaiona hata katika wasia utolewao. Tuangalie beti zifuatazo kama mifano ya dai hilo.
Quote:38. Na kowa na kiuisinga
na nyee zako kufunga
na asmini’ kutunga
na firashini kutia
39. Nawe ipambe libasi
ukae kama arusi
maguu tia kugesi
na mikononi makoa
40. Na kidani na kifungo
sitoe katika shingo
mwili siwate mwingo
kwa marashi na dalia
41. Pete sikose zandani
hina sikome nyaani
wanda sitoe matoni
na nshini kuitia.
Katika kiwango hiki mwanamke anaonekana kuwa pambo tu, sawa na mapambo mengine mazuri mazuri. Kwa sababu ya athari hii basi, nafasi ya mwanamke katika jamii ya kimwinyi huwa ya chini na duni mno. Naye mwanamke hufanywa na mazingira haya aikubali nafasi hiyo duni. Ndiyo sababu twaambiwa kuwa watu wengi, hasa wanawake, walivutiwa mno na utenzi huu nao wakaamua kuuhifadhi “kwa moyo na wakawahifadhisha watoto wao wa kike” (Kitangulizi). Twaelezwa pia kuwa wengi wao hadi leo wanaujua utenzi huu kwa moyo.
Iko mifano mingi ya beti zinazodhihirisha nafasi duni aliyopcwa mwanamke katika janui na vile ambavyo mwenyewe kaikubali (zima kalazimika kuikubali). Tuangalie beti zifuatazo:
Quote:28. Keti naye kwa adabu
usimtie ghadhabu
akinena simjibu
jitahidi kunyamaa
31. Kilala siilcukuse
mwegemee umpapase
na upepo usikose
mtu wa kumpepea
34. Mnyoe mpalilize
sharafa umtengeze
na udi umfukize
bukurata wa ashia
35. Mtunde kama kijana
asiyojua kunena
kitu changalie sana
kifokacho na kuingic.
Zaidi ya kuwa uhusiano baina ya mume na mke ni sawa na ule wa bwana na mtwana, mume hapa yu bwege kabisa, na ubwege huu wa kimwinyi umesisitizwa kwa mume kulinganishwa na mtoto mdogo (kijana asiyejua kunena). Zaidi ya kuwa mke kaambiwa aketi na mumewe kwa adabu na hata akionewa asijibu, ubeti wa 36 nao unasisitiza nafasi hiyo duni ya mwanamke:
Quote:36. Mpumbaze apumbae
amriye sikatae
maovu kietayeye
Mngu atakulipia.
Mistari miwili ya mwisho ya ubeti huu wa 36 inatuleta katika suala lingine lihusulo amali na maisha ya kimwinyi. Zaidi ya kuamua kuwa mwanamke amtumikie mwanamume, anaaswa asimbishie wala asimjibu ila amtii na amwogope, na unyonge huu unahalalishwa kwa vitisho vya dirii. Vitisho vya dini hufikia kilele katika mfumo wa kimwinyi, nayo dini hutumiwa kuwa taasisi kubwa ya kudumisha na kuhalalisha mgawanyiko wa jamii katika matabaka ya watu wa juu (mamwinyi) na ya wa chini (watwana); hutumiwa kuhalalisha unyonge si wa wanawake tu bali wa watu wote wa matabaka ya chini. Ubeti huo wa 36 unaonyesha vile ambavyo dini hapa inatumiwa kumgandamiza zaidi mwanamke ambaye anaaswa kuwa maovu yoyote yale atakayotendewa na mumewe asiyashughulikie kwani Mungu atamlipia. Beti za 24-27, zinasisitiza msimamo na mtazamo huu:
Quote:24. Naawe radhi mumeo
siku zote mkaao
siku mukhitariwao
awe radhi mekuwea
25. Na ufapo wewe mbee
radhi yake izengee
wende uitukuzie
ndipo upatapo ndia
26. Siku ufufuliwao
nadhari niya mumeo
taulizwa atakao
ndilo takalotendewa
27. Kipenda wende peponi
utakwenda dalhini
kinena wende motoni
huna budi utatiwa.
Misingi ya dini katika mfumo huo iliwekwa katika hali ambayo humdunisha mwanamke. Mwanamume kapewa hata madaraka ya kuamua siku ya ufufuo kuwa mkewe aende ahera ama motoni. Mwanamke basi, anapaswa afuate yote anayoamriwa na mumewe kwani yote hayo ni amri ya Mungu. Hapa tunazigundua dhahiri athari za kitabaka zilizojikita mizizi yake katika taasisi ya dini – athari ambazo zinanuia kumgandamiza mtu wa chini zaidi na zaidi.
Kutokana na mkabalatuuonao katika wasia utolewao katika Utenzi wa Mwanakupona kwa wanawake, tunaweza kusema kuwa utenzi huu umetudhihirishia vile ambavyo zaidi ya mwanamke kufanywa aonekane kuwa ni pambo, hapohapo maisha ya kimwinyi yanamfanya kuwa chombo cha kutimizia haja za mwanamume, na pia kuwa mtwana wa mwanamume.
Dhamira Zinginezo
Mambo yote hayo ambayo tumeyahusisha na mfumo wa kimwinyi yanatokana na wakati ambapo utenzi huu uliturigwa pamoja na mazingira ya kitamaduni, kiuchumi na kisiasa yaliyoongozwa na maadili ya kimwinyi. Ndio sababu hata kudunishwa kwa watu wa chini hakuishilii kwa wanawake tu bali kwa watu wote wa tabaka la kitwana. Kwa mfano katika beti za 15-19 mwanamke anaaswa awaheshimu “maqabaili”:
Quote:15. Tena mwanangu idhili
mbee za maqabaili
uwaonapo mahali
angusa kuwainukiya
16. Wangiapo wenukiye
na moyo ufurahiye
kisa uwapeke mbeye
watakapokwenda ndiya
17. Ifanye mteshi teshi
kwa maneno yaso ghashi
wala sifanye ubishi
watu wakayatukiya.
Lakini, zaidi ya kuambiwa awaheshimu na kuwaabudu hao mamwinyi, anaaswa asifanye hivyo kwa watu wa chini, tena hata asiwakaribie, Haya tunayaona katika ubeti wa 20, kwa mfano:
Quote:20. Silangane na watumwa
ile mwida wa huduma
watakuvutia tama
labuda nimekwambiys.
Katika utenzi huu yanajitokeza pia maadili mengine. Mwanamke anaaswa kuwa maisha hayana maana, na kuwa mtu si kitu mbele ya muumba wake:
Quote:6. Mwanadamu si kitu
na ulimwengu si wetu
walau hakuna mtu
anibao atasaliya.
Kwa hiyo basi anaambiwa kuwa jambo la kwanza ashike dini:
Quote:12. La kwanda kamata dini
faradhi usiikhini
na suna ikimkini
ni wajibu kuitiya.
Pia utenzi huu unafunza kuhusu umuhimu wa usafi nyumbani kama tusomavyo katika ubeti wa 37 na wa 42 kwa mfano:
Quote:37. Mwanangu siwe mko’o
tenda kama uona’o
kupea na kuosha choo
sidharau mara moya.
42. Nyumba yako inadhifu
mumeo umsharifu
wakutanapo sufufu
msifu ukimweteya.
Baadhi ya wahakiki wa utenzi huu wamesema kuwa beti tulizokwishazitaja zinazomuasa mwanamke ajirembe na kujipamba zinasisitiza kuhusu umuhimu wa usafi wa mwili zaidi ya kujipamba tu. Ili kuweza kutoa tafsiri ya beti hizo labda itambidi msomaji binafsi aamue mwenyewe. Ila ni wazi kwamba usafi uliotajwa pamoja na urembo na kujipamba kunakosisitizwa katika beti hizo – vyote hivi vimeeiekezwa katika kumpendezana kumfurahisha mwanamume kuliko kuwa na manufaa kwa mwanamke mwenyewe.
Sasa tuuchambue utenzi huu kwa kuulinganisha na kuulinganua na baadhi ya kazi za fasihi ya Kiswahili ambazo zimeshughulikia pia masuala sawa na haya ya utenzi huu. Tumetaja utenzi wa Al Inkishafi kama mfano wa kazi ambazo japokuwa haziambatani na wasia kwa wanawake tu bali kwa watu wote, hapohapo unaonyesha athari za baadhi ya amali za maisha ya jamii nzima. Suala la msisitizo kuhusu mapambano na pia nafasi ya dini katika jamii ndilo hasa tulilolihusisha na yaelezwayo katika Utenzi wa Mwanakupona.
Kazi ambayo inafanana sana na Utenzi wa Mwanakupona ni ile ya Shaaban Robert ya Utenzi wa Hati ipatikanayo katika kitabu chake cha Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini (Thomas Nelson, 1966). Katika Utenzi wa Hati ni mzazi pia ndiye katunga ili kumuasa binti yake kuhusu maisha na wajibu wake katika jamii. Tofauti hapa ni kwamba, mawazo kuhusu mwanamke katika Utenzi wa Hati ni ya kimaendeleo zaidi na yamepevuka zaidi kuliko yale ya Utenzi wa Mwanakupona.
Japokuwa kupo kushabihiana katika baadhi ya mawazo ya tenzi zote mbili kwa mfano katika wasia kuhusu umuhimu wa kushika dini – lakini sehemu nyingi za tenzi hizi zinatofautiana sana na hata kupingana. Kwa mfano, tulionajinsi beti za 15, 16, 17 na 20 zinazomuasa binti wa Mwanakupona asiwapende na kuwaheshimu watu wa tabaka la chini. Shaaban Robert anamuasa bintiye tofauti kabisa na mawazo hayo. Kwa mfano katika beti za 65 na 66 za Utenzi wa Hati Shaaban Robert anaasa:
Quote:65. Kupenda watukufu,
Kwa kumiliki sarafu,
Na fukara kukashifu,
Hatiyasema vibaya.
66. Penda wenye cheo,
Na wanyonge uwe nao,
Hayo ndiyo mapokeo,
Mema mtu kutumia.
Tenzi zote mbili zinamuasa mwanamke kuhusu umuhimu wa kuchunguza na kuyaelewa mambo (angalia ubeti wa 19 wa Utenzi wa Mwanakupona), na pia kuhusu umuhimu wa urafiki mwema na tabia nzuri. Lakini katika Mwanakupona sifa hizo zimeelekezwa zaidi katika nafasi duni ya chini aliyo nayo mwanamke katika jamii. Katika Utenzi wa Hatisifa hizo zimejikita katika ukombozi wa mwanamke ambaye ametakiwa atoke jikoni na kitandani, ashiriki katika mambo ya kujielimisha-hata anaambiwa kuwa ni jukumu lake kujifunza namna ya kujitegemea. Angalia ubeti wa 76 kwa mfano:
Quote:76. Tena kujitegemea
Ni ngao ya ukiwa
Siku ya kubakia
Peke yako hufaa.
Kinyume na mwanamke huyu wa Utenzi wa Hati, yule wa Utenzi wa Mwanakupona hapewi wasia wa kujikomboa bali anaaswa kuwa aendelee kuikumbatia nafasi yake duni na ya chini kabisa katika jamii-nafasi ya kutumiwa kama chombo na pambo, na pia kutumwa kama mtwana.
Tenzi mbili hizi tulizozichunguza zinatudhihirishia ukweli kwamba mwandishi na mturigaji wa kazi ya fasihi, sawa na fasihi yenyewe, ni zao la mazingira maalum kwa wakati maalumu. Tofauti za mifumo ya jamii na mwamko wa kisiasa kwa jumla katika jamii, aghalabu huleta tofauti pia baina ya waandishi wa mifumo itofautianayo. Mwanakupona alizaliwa na kulelewa na jamii ya mfumo wa kimwinyi, na jamii hii ndiyo iliyozaa na kulea mtazamo wa kilimwengu wa kimwinyi tuuonao katika wasia autoao. Shaaban Robert alizaliwa na kukulia katika mfumo wa kibepari chini ya ukoloni, mfumo ambao umepevuka zaidi ya ule wa kimwinyi. Katika mfumo huu wafanyakazi hudai haki zao kwa njia dhahiri, na hata wanawake hudai haki zao kwa kuunda vyama vyao – na nafasi yao katika jamii si jikoni na kitandani tu bali twawaona katika harakati za kupigania uhuru katika nyanja za elimu, sayansi na kadhalika; sambamba au hata juu zaidi ya wanaume. Haya yote aliyaona, aliyasoma na aliyasikia Shaaban Robert, na si ajabu kuona kuwa mkabala wake kuhusu nafasi ya mwanamke katika jamii ni wa kimaendeleo zaidi ya ule wa Mwanakupona.
MATUMIZI YA VIPENGELE VYA FANI
Yako machache sana tuwezayo kusema kuhusu fani katika utenzi huu. Labda hili linatokana na ukweli kuwa wasia utolewao umetolewa kwa njia ya moja kwa moja bila matumizi mengi ya picha ama tamathali za semi.
Kwa jumla utenzi huu umefuata muundo wa kimapokeo wa tenzi za Kiswahili. Sawa na ule wa Shaaban Robert wa Utenzi wa Hati, utenzi huu unaanza kwa kumwita mhusika mkuu, binti yake, halafu unaeleza kwa njia ya dibaji kuhusu madhumuni ya mwandishi au mturigaji, halafu maudhui kuhusu dini na Mungu yanajitpkeza, na baada ya hapo maudhui yenyewe yanatolewa kwa kirefu kabla ya utenzi kufungwa kwa mambo ya sala, Mungu na dini. Huu ni muundo uliozoweleka katika tenzi za kimapokeo zaKiswahili.
Utenzi huu una “urahisi” wa kifani anibao hata hivyo haimaanishi kuwa unapwaya. Katika “urahisi” huo kuna faida ya kueleweka kwa maudhui ya utenzi huu bila shida kubwa kwa msomaji, japokuwa kwa baadhi ya wasomaji msamiati mwingi wa lahaja itumiwayo humu ni mgeni na mgumu kwao.
Maswali
1. Eleza historia fupi ya Utenzi wa Mwanakupona. Je kuna umuhimu gani wa kuielewa historia hiyo?
2. Eleza uhusiano uliopo baina ya fasihi na jamii ya kimwinyi. Ni kwa vipi uhusiano huo umetokeza katika Utenzi wa Mwanakupona?
3. Yachambue kwa undani maudhui ya Utenv wa Mwanakupona. Upe uchambuzi wako uzitpo kwa kuyalinganisha maudhui hayo na ya kazi nyirigine au zingine za fasihi ya Kiswahili ambayo au ambazo zime-yashughulikia pia masuala yajitokezayo katika utenzi huu.
4. “Katika wasia utolewao na Mwanakupona tunagundua jela na silasila za maisha ya mwanamke zaidi ya uhuru na utu wake.” Ijadili kauli hii kwa kuitolea mifano dhahiri kutoka katika Utenzi wa Mwanakupona. Katika jibu lako ihusishe kauli hiyo pia na baadhi ya mashairi yaliyomo katika kitabu cha Shaaban Robert cha Ashiki KitabuHiki.
5. Je tunaweza kusema nini kuhusu fani katika Utenzi wa Mwanakupona?
|
|
|
USHAIRI: NADHARIA NA TAHAKIKI (14) |
Posted by: MwlMaeda - 01-10-2022, 08:58 AM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
13. Muhammed S. Khatibu: Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar
SURA YA KUMI NA TATU
Historia ya visiwa vya Zanzibar ni historia ya harakati, harakati hizo zikiwa dhidi ya tawala za kinyonyaji za kitumwa, kimwinyi au kisultani na kibepari; katika umbo la ukoloni wa Mwingereza aliyeshirikiana na sultani; na leo hii dhidi ya ukoloni mamboleo. Kilele cha mwanzo cha harakati hizo kilifikiwa tarehe 12 Januari 1964, wakati wananchi wa visiwani walipojizatiti wakashika silaha na kuupindua utawala dhalimu wa kisultani.
Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar ni zao la historia hiyo ya visiwa vya Unguja na Pemba. Kwa hakika historia hiyo, hasa tukio la mapinduzi ya januari 1964, imezaa wimbi kali la fasihi ya Kiswahili kutoka visiwani ambalo limevipiga kumbo vitabu vilivyokwepa kuyashughulikia mapinduzi hayo, kwa mfano vile vya upelelezi vya Muhammed Said Abdulla vya Mzimu wa Watu wa Kale (EALB, 1960), Kisiwa cha Giningi (Evans: 1960), Duniani Kuna Watu (EAPH, 1974), Siri ya Sifuri (EAPH, 1975). Vitabu hivi, zaidi ya kutokuyagusia mapinduzi hayo, vimetetea na hata kuuombea msamaha ubinafsi wa wanyonyaji.
Wimbi hilo kali la kifasihi limejitokeza hasa npande wa riwaya kama tuonavyo katika riwaya za: Nyota ya Rehema ya M.S. Mohamed (Oxford: 1976), Asali Chungu ya S.A. Mohamed (Shungwaya: 1978), Kasri ya Mwinyi Fuad na Kuli za Shafi Adam Shafi (TPH: 1978 na 1979). Zote hizi zimechota fani na maudhui yake kutoka katika harakati za wananchi wa Visiwani dhidi ya uonevu; nazo zimetoa welekeo wa matumaini mema kwa wanyonge, kinyume na zile za upelelezi za M.S. AbduIIa, ijapokuwa yeye pia sawa na waandishi hao amezaliwa na kukulia Visiwani Zanzibar.
Utenzi huu umetumia mbinu mbalimbali za “mapokeo” ya tenzi za Kiswahili hasa kimuundo. Kwa mfano mwanzo wa utenzi huu ni uleule kama wa tenzi mbalimbali za mapokeo – wa dua. Baada ya hapo utenzi huu umeeleza asili ya watu wa Zanzibar (beti za 27 na 28) na maisha yao kabla ya majilio ya wageni (beti za 69, 84, na 95-106). Sehemu hii twaweza kuiita kuwa ndiyo “Dibaji” ambayo kwa kutuonyesha jinsi maisha ya watu wa Visiwani yalivyokuwa ya kimawafikiano hapo awali, inatupa msingi mzuri wa kujadili ukoloni na athari zake katika maisha ya watu hao.
Baada ya dibaji hii, utenzi umetoa sababu na misingi ya kihistoria ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tumepewa maelezo marefu kidogo kuhusu ukoloni na maovu yake kwa wahanchi kwa kuonyeshwa kwanza jinsi mamwinyi wa Kiarabu walivyowanyonya na kuwanyanyasa wananchi wa visiwani (ubeti wa 110 na 111):
Quote:110 Tawala za Kiswahili
Zikatupiliwa mbali
Wakafika majahili
Watokao Arabiya
111 Walitumia ujanja
Machoni kutia wanja
Na kujifanya viranja
Usahibu kujitia
Lakini hawahawa waliojitia rafiki wa watu walianza kuwanyonya na kuwadhulumu kwa kujipa uongozi na “kuanzisha ujambazi” (ubeti wa 118). Twaelezwa na mtunzi kuwa kati ya mengi yaliyomvutia Seyyid Said aliyewasili pande hizi mwaka wa 1832, ni uzuri na utajiri wa Visiwani ambao ungeishamirisha biashara yake (ubeti wa 125), na pia utumwa (ubeti wa 129 na wa 130). Kwa hiyo basi, kutokana na utawala wa Seyyid Said wananchi wa Visiwani walinunuliwa katika biashara haramu ya utumwa, huku wengi wao wakilimishwa kwa mateso makubwa katika mashamba yaliyoibiwa kutoka kwao, wakalazimishwa kupanda mazao ya biashara kama vile minazi na karafuu, ambayo yote yalizidi kuwatajirisha mabwana wa Kiarabu (beti za 131-137).
Utawala wa Kiarabu ulifuatiliwa na ule wa Kiingereza (beti za 143-146), na tawala hizi mbili zikaenda sambamba kimawafikiano kuwatesa wananchi wa Visiwani.
Kwa hiyo basi, kutokana na maelezo ayatoayo mtunzi, mbinu kuu zilizotumiwa na tawala hizo dhalimu kuwagandamiza watu wa Visiwani zilikuwa za umilikaji wa kimwinyi wa ardhi, pamoja na biashara ya utumwa. Katika biashara hii twaonyeshwa jinsi ambavyo watu walifanywa kuwa bidhaa za kusafirishwa nje (beti za 178 na 183) wakati ambapo Visiwani kwenyewe mateso zaidi ya wananchi yaliendelea (beti za 227-235) huku unyonge wa wananchi ukizidi kuongezeka, kama tuelezwavyo katika beti za 230 na 231:
Quote:230 Wanyonge kitaka kazi
Hufanywa ndio wakwezi
Wanawake vijakazi
Majumbani kueneya
231 Wakipewa kazi ngumu
Asofanya mwanadamu
Kwao iliwalazimu
Viboko kuwalemeya.
Na, ili kuhakikisha kuwa utengano wa wananchi unanawiri, mbinu ya ukabila ilitumiwa, mbinu ambayo ilitumika si Visiwani tu bali katika nchi mbalimbali (kwa mfano, nchi zote za Afrika ya Mashariki) ili kuwafanya watu wachukiane wao kwa wao wasiweze kuungana na kumpinga mkoloni. Ubeti wa 232 unatuonyesha mbinu hiyo:
Quote:232 Alitia ukabila,
Mpaka katika kula
Asohusu utawala
Hana atojipatiya
Hata hivyo hizo hazikuwa mbinu pekee zilizotumiwa na watawala wa Kiarabu na wa Kiingereza. Kulikuweko pia za kodi, biashara, umilikaji wa majumba makubwa ya kupangisha, ubaguzi kielimu, kimatibabu na kiuchumi, na kudhibiti uchumi kwa jumla. Haya yote yamejitokeza katika beti za 233 hadi 269. Pamoja na mbinu hizi, mabenki pia yalitumiwa kuwakamua wananchi huku viwanda vikuu pamoja na usafirishaji na uagizaji wa mazao muhimu ya biashara vikiwa vimewekwa mikononi mwa watawala (beti za 277 – 283).
Haya hayamaanishi kwamba wananchi wa Visiwani hawakufanya upinzani wowote dhidi ya uonevu huo. Katika beti za 135 na 136 tunaonyeshwa wazi kuwa upinzani ulikuwapo tangu awali:
Quote:135 Walokuwa wakaidi
Kutomtii Saidi
Hawakuipata sudi
Viboko liwaingiya.
136 Wengine waliuliwa
Mashimoni kufukiwa
Sababu wamechukiwa
Kutumwa kutoridhiya.
Upinzani huu ambao watawala walijaribu kuuzima kwa vitisho na uonevu zaidi, uhendelea kwa cmnichini hadi baadaye ulipoibuka katika umbo la mwamko wa kisiasa kwa watawaliwa. Mwamko huu ambao twaelezwa habari zake katika beti za 299 na 300, ilibidi uelekezwe katika njia sahihi kwa mbinu. Kwa hiyo twaelezwa kuwa mwanzoni ulielekezwa katika michezo mbalimbali kama tuonavyo katika beti za 303-307 mtunzi anapoongelea kuhusu klabu ya mpira ambayo ilitumiwa kuwa chombo cha kuletea umoja wa watawaliwa – chombo ambacho kilizaa “mwana” kama beti za 307,308 na 309 zituonyeshavyo:
Quote:307. Klabu kazaa mwana
Tena aliye mwungwana
Na hapo kapewa jina
Afrika Asosheniya
308 Ilikuwa jumuiya
Ya Wafrika wa Unguja
Ilofanya kila njiya
Watu kujiingiliya
309 Moja tisa tatu tano
Liundwa umoja huno
Jumuiya ilo nono
Hadharani kutokeya.
Jumuiya hii ilizidi kupanuka huku shughuii zake za ukombozi zikiendelea kueleweka kwa Waafrika; nayo iliomba sasa kutambuliwa na serikali ya kikoloni – jambo ambalo lilipingwa sana na wakoloni. Twazisoma mbinu za mkoloni za kupinga umoja huo wa wananchi katika beti 321-339. Japokuwa walijifanya kuwa wameikubali na kutambua jumuiya, waliendelea kuwagawa watu kitabaka (ubeti wa 322) na kirangi; kwa hiyo Washirazi wakawa pekee na Waafrika pekee, na huku wakiendeleza mateso yao kwa wananchi (ubeti wa 329).
Hayo hayakurudisha nyuma harakati za wananchi za kujikomboa kwani baadaye waliunda chombo imara zaidi kama atuhadithiavyo mtunzi katika beti zifuatazo:
Quote:339 Shirav na Afrika
Wote wakajumuika
Uhasama kuuzika
Kheri kujitafutiya
340 Likiwa tarehe tano
Ni siku ya Muungano
Ni siku iliyo nono
Daima twakumbukiya
341 Mwezi Mfungo pili
Wa Februari kamili
Ziliungana kikweli
Hizi mbili jumuiya
342 Mwaka hamsini na saba
Ni mwaka wa matilaba
Yalipozidi mahaba
Afro na Shiraziya.
Ndipo Afro-Shirazi Party kilipoundwa, chama ambacho kiliongoza harakati za ukombozi wa Zanzibar tangu wakati huo kilipoundwa kwa kupigania haki za watu na kuwaeleza watu kuhusu umuhimu wa kuungana ili kumtokomeza adui.
Hata hivyo, kwa mara nyingine tena mkoloni bakusita kutumia mbinu za kuyapinga maendeleo hayo ya harakati za ukombozi wa wananchi wa Visiwani. Sasa aliandaa na kuendesha uchaguzi wa bandia ambao ulishindanisha vyama vyta Hizbu (cha Sultani) na Afro-Shirazi (cha Wananchi). Maelezo kuhusu hila hii tunayapata katika beti za 351-410. Japokuwa Afro Shirazi walijipatia ushindi katika uchaguzi huu, bado mkoloni (Mwingereza akishirikiana na Mwarabu) alifanya juu chini kukiua chama hicho cha wanyonge kwa kuwagawa mafungu mafungu wanachama wake. Ndipo walipotokea akina Shamte anibao waliunda chama cha ZPPP; ukaitishwa uchaguzi mwingine baina ya ASP, Hizbu na ZPPP. Ingawa matokeo ya uchaguzi huo yalionyesha dhahiri ushindi wa ASP bado mkoloni aliufitini ushindi huo kwa kuitisha tena uchaguzi ilimradi tu ajaribu kukitoa chama cha Afro Shirazi katika uongozi. Jitihada hizi zilifaulu kwa muda wakati Hizbu na ZPPP zilipounganisha kura zao, na kwa hiyo Sultani akapewa “madaraka” ya kuiongoza serikali huku akishirikiana na Mwingereza. Hata hivyo baadaye wananchi wa Visiwani waliamua kuwa njia pekee ya kuuondoa kabisa udhalimu wa mkoloni ni ya kutumia nguvu.
Udhalimu na hila za mkoloni ulichemsha hasira ndani ya mioyo ya wananchi wa visiwani, ambazo zililipuka na kufikia kilele walipofanya mapinduzi mnamo Januari 12, 1964. Maelezo juu ya mapinduzi haya tunayaona katika beti za 344-452. Katika beti hizi matumizi ya nguvu katika ukombozi wa jamii yamehalalishwa.
Matunda ya mapinduzi haya yameelezwa, baadhi yake yakiwa ni wananchi kupewa madaraka (ubeti wa 457), kuondolewa kwa rahani na poni (ubeti wa 460), lugha ya Kiswahili kupewa hadhi yake kama lugha rasmi ya shughuli zote za sefikali (beti za 465-567), kutaifishwa kwa ardhi (beti za 478-479), wazee kujengewa nyumba (beti za 480-484), na kadhalika.
Baada ya maelezo yote hayo hatua mpya ya muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa kwa Tanzania imcelezwa na kuonyeshwa jinsi ambavyo iliupevusha zaidi ukombozi wa Waafrika kwa kuimarisha umoja baina yao. Hatua hii ilizidisha pia matunda ya uhuru yaliyoleta mambo kama vile elimu kutolewa bure kwa wananchi, na kadhalika. Vilevile twaelezwa na mtunzi kwamba ubaguzi wa rangi, utabaka, uboi na udhalimu mwingine wowote ule ulifutiliwa mbali huku ujenzi wa jamii mpya ukiimarishwa katika nyanja zote za maisha ya watu za utamaduni, uchumi na siasa kwa jumla. Kutokana na hatua hizi, twaelezwa na mwandishi katika ubeti wa 643:
Quote:Uovu kila namna
Nchini haupo tena
Watu wote wapendana
Imani imeeneya.
Ubeti huu kidogo unapingana na beti zinazoufuatia ambazo zinaeleza juu ya jaribio la kuiangusha serikali ya Zanzibar ambalo matokeo yake yalikuwa kuuawa kwa Sheikh Abedi Karume. Tukio hali linaonyesha dhahiri kuwa uovu bado ulikuwapo na si kweli kuwa watu wote walikuwa wakipendana.
Mwishoni, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar unamalizika kimapokeo, kwa sala na dua za kuiombea roho ya marehemu Karume ilazwe mahali pema peponi, na kuwaombea hen viongozi wa sasa wanaoendeleza mbele ukombozi wa Tanzania.
Maoni kwa Jumla na Hitimisho
Uko ugumu wa kuandika uhakiki wa tenzi za kihistoria hasa ikiwa zimeandikwa kama huu tulioutazama. Mara kwa mara mhakiki wa tenzi kama hizi hujikuta akifasili zaidi kuliko kuhakiki; hujikuta kwa mfano, akieleza historia hiyohiyo iliyoelezwa kwa njia tofauti cu ya nathari. Jambo hili hutokana na sababu kuwa watunzi wengi, zaidi ya kuzisifu pande waziungazo mkono katika historia wanazozieleza katika tenzi zao, mara nyingi hawayachambui na kuyahakiki matukio wayaelezayo. Huwa wanatoa mlolongo tu wa matukio kama yalivyoelezwa na kama yalivyojitokezakatikahistoria, japo wanatumia ushairi kufanya hivyo.
Tatizo jingine lijitokezalo katika Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar linahusu fani. Ni kweli kuwa utenzi huu unaeleweka haraka kwani rugha yake ni ya moja kwa moja. Hata hivyo sifa hii hapohapo imeonekana kuwa ni udhaifu kutokana na kukosekana kwa msisimko wa kishairi wakati msomaji asomapo utenzi huu. Ikiwa tunakubaliana kuwa lugha ya kipicha ni muhimu sana katika ushairi, basi ni dhahiri kuwa lugha nu haikujitokeza sana humu. Jambo hili, pamoja na uchache wa tamathali za usemi, limeufanya utenzi huu uwe mkavu mno kisanaa. Huenda yote haya ndiyo yameongezea ugumu wa kuuhakiki utenzi huu kama kazi ya sanaa.
Njia mojawapo nzuri iwezayo kuuondoa ugumu huo ni ile ya kuuchambua utenzi huu sambamba na kazi zingine zilizoshughulikia suala la ukombozi wa jamii, au walau zile ambazo zioa mshabihiano wa aina fulani na utenzi huu. Kwa mfano, Utenzi wa Jamhuri ya Tanzania wa R. Mwaruka, (TPH, 1969); Utenzi wa Vita vya Uhuru wa Shaaban Robert (Oxford University Press, 1967); Utenzi wa Uhuru wa Kenya wa Salim A. Kibao (Oxford University Press, 1972); na Utenzi wa Ukombozi wa Msumbiji wa J.M.M. Mayoka (Oxford University Press, 1976); ni baadhi ya kazi ambazo mhakiki huweza kuzilingamsha na kuzilinganua na Utenzi wa Ukombou wa Zanzibar kwa upande wa fani na maudhui. Hapa mhakiki huweza, kwa mfano, kuchambua dhana za ukombozi na uhuru jinsi zinavyofanana au kutofautiana katika tenzi hizo.
Siyo lazima kulinganisha na kulinganua utenzi huu na kazi za ushairi tu. Twaweza kuuchunguza utenzi huu sambamba na kazi kama vile za riwaya tulizozitaja mwanzoni: kazi ambazo zenyewe mizizi yake imejikita katika historia ya watu wa Visiwani, hususan katika tukio la mapinduzi ya Januari 12,1964.
Pamoja na kazi hizo, kazi mbalimbali za fasihi simulizi ya watu wa Visiwani zinazolieleza tukio la mapinduzi huweza kuwa kianzio kizuri cha kuuchunguza Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar kwa kuulinganisha na kuulinganua nazo. Nyimbo za taarab za makundi kama ya Mila na Utamaduni, Zanzibar; Kwahani Social Branch, Zanzibar; na mengineyo, huweza kuwa kazi nzuri za kulinganishwa na kulinganuliwa na utenzi huu.
Kwa ujumla, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar unaeleza kwa uwazi mlolongo wa matukio ya historia ya huko Visiwani; lakini kutokana na udhaifu wake wa kisanaa si rahisi sana kuutofautisha na maelezo ya vitabu vya historia wakati wa kuuhakiki.
Maswali
1. Jadili dhamira ya ukombozi kama ilivyojitokeza katika Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar,
2. Je ni kwa vipi Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar huweza kuhusishwa na Mashairiya Saadani ya Saadani A. Kandoro?
3. Jadili matumizi ya lugha, picha na tamathali za usemi katika Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar.
4. Jadili kauli isemayo kuwa japokuwa Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar umeshughulikia masuala muhimu ya historia ya jamii ya Visiwani, udhaifu wake kisanaa umeufanya uonekane mkavu mno kwa wasomaji.
5. Yajadili mapendekezo yaliyotolewa kuhusu njia nzuri za kuchambua Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar,
Kinyume
Wanafunzi, walimu na hata baadhi ya wanafasihi, hulalamika kuwa ushairi wa Kiswahili ni mgumu kueleweka. Kikwazo hiki huwafanya wapenzi hao wa fasihi ya Kiswahili wachelee kusoma na kufaidi uhondo uliomo katika utanzu huu.
Ushairi: Nadharia na Tahakiki ni kitabu kinachorahisisha usomaji wa ushairi huo na kuimarisha sana mbinu za uchambuzi wake. Hiki ni kitabu pekee kinachochambua vigezo muhimu vya ushairi huku kikielezea nadharia iambatanayo na vigezo hivyo. Baadhi ya vitabu ambavyo vimechambuliwa kwa kutumia vigezo hivyo ni Raha Karaha, Mashairi ya Saadani, Teuzi za Nafsi, Kielezo cha Fasili, Kichomi, Sauti ya Dhiki, n.k.; vitabu ambavyo aghalabu hutumika sana katika masomo na mitihani ya fasihi.
F.E.M.K. Senkoro ni Mhadhiri Mwandamizi wa somo la fasihi katika Idara ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ana shahada za B.A. na M.A. za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na pia shahada ya M.A. ya Chuo Kikuu cha Alberta, huko Canada. Yeye pia ni mwandishi wa riwaya na vitabu mbalimbali vya taaluma ya fasihi. Vilevile makala zake mbalimbali ni maarufu katika majarida kadhaa ya kitaaluma.
DAR ES SALAAM UNIVERSITY PRESS
Bibliografia Teule
Abdalla, Abdilatif. “Ushairi wa Kiswahili: Na Uhuishwe, Usiuliwe,” Makala, Dar es Salaam: Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (1973).
Abdalla, Abdilatif. “Tanzu za Ushairi na Maendeleo Yake,” Makala isiyochapishwa. Inapatikana Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Abeid, Amri. Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya Amri. Nairobi: East African Literature Bureau (EALB), 1965.
Bascom, W.R. na Melville J. Hcrskovits, (Wahariri), Continuity and Change in African Cultures. Chicago na London: University of Chicago Press, 1959.
Cane, M. Making A Poem: An Enquiry into the Creative Process. New York: Harcourt Brace, 1962.
Chiraghdin, S. na wenziwe, “Tarehe ya Ushairi,” Mulika (1975).
Ciardi, J. How Does A Poem Mean? Boston: Houghton Mifflin, 1960.
Deutsch, B. Poetry Handbook: A DictionaryofTerms. New York: Funk & Wagnalls, 1957.
Finnegan, R. Oral Poetry. Cambridge: Cambridge University Press, 1977.
Graham, D. Introduction to Poetry. London: Oxford University Press, 1968.
Harries, L. Swahili Poetry. London: Oxford University Press, 1962.
Hichens. W. “Swahili Prosody,” Journal of the Easl African Swahili Committee (1941).
Holman, C.H. A Handbook to Literature. Indianapolis. Odyssey, 1975.
Jones, A.M. “African Rythm,” Africa. 24 (1954).
Judson, J. Poet and the Poems. Cindnnati: Writers Digcst, 1974.
Kahigi, K.K. “Ushairi (Mtazamo wa Kisayanri),” Kiswahili. Tol. 45/1 (Machi, 1975).
Kahigi, K.K. na Mulokozi, M.M. Mashairi ya Kisasa. Dar es Salaam, Tanzania Publishing House, 1973.
Kahigi, K.K. na Mulokozi, M.M. Malenga wa Bara. Arusha: East African Literature Bureau, 1976.
Kahigi, K.K. na Mulokozi, M.M. Kunga za Ushairi na Diwani Yetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House, 1982.
Kandoro, S. Ushairi wa Mashairi ya Kiswahili. Nairobi: Longmans, 1978.
Kezilahabi, E. Kichomi. Nairobi: Heinemann, 1974. “Ushairi wa Mapokeo na Wakati Ujao,” katika J.M. Mbonde, (Mhariri), Uandishi wa Tanzania: Insha, Arusha: East African Literature Bureau, 1976, kur. 121-135.
Kezilahabi, E. Ushairi wa Shaaban Robert. Kampala/Nairobi/Dar es Salaam: East African Literature Bureau, 1976.
Kezilahabi, E. “Ushairi na Nyimbo,” katika C.K. Omari na M. Mvungi, (Wahariri) Urithi wa Utamaduni Wetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House. 1981.
Knappert, J, Traditional Swahili Poetry. Leiden: E.J. Brill, 1967.
“The Appreciation of Swahili Poetry,” Kiswahili, 44/2 (1974) kur. 19-29.
Lambert, H.E. “Some Initiation Songs of the Southem Kenya Coast,” Swuhili. 35/1. (1965), kur. 49-67.
Mayoka, J.M. Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House, 1986.
Mnyampala, M. Diwani ya Mnyampala. Nairobi: East African Literature Bureau, 1965.
Mnyampala, M. Waadhi wa Ushairi. Nairobi: East African Literature Bureau, 1965.
Mulokozi, M.M. “Revolution and Reaction in Swahili Poetry,” katika Kiswahili 45/2 (1975).
Mulokozi, M.M. “Ushairi wa Kiswahili ni Nini?” Lugha Yetu, 26 (1975).
“Ushairi wa Kiswahili na Ubantu Hadi 1700,” Tasnifu ya Shahada ya B.A., Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1975.
Mvungi, T. Raha Karaha. Dar es Salaam: Continental Publishers, 1982.
Mvungi, T. Chungu Tamu: Dar es Salaam: Tanzania Publishing House, 1985.
Nicholson, R.A. Literary History of the Arabs. Cambridge: Cambridge University Press, 1969.
Omari, C.K. na Mvungi, M. (Wahariri), Urithi wa Utamaduni Wetu. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House, 1981.
p’Bitek, O. Wimbo wa Lawino. Nairobi: East African Publishing House, 1975.
Perrine, L. Sound and Sense. New York: Harcourt Brace Jovanovich, 1982.
Perry, J.E. (Mhariri), Approaches to the Poem: Modern Essays in the Analysis and Interpretation of Poetry. San Francisco: Chandler Publishing Co., 1965.
Ramadhan, J. “Ushairi,” Mulika, Na 3 (1975), Kur. 1-8.
Richards, I.A. Practical Criticism. New York: harcourt Brace
Robert, S. “Hotuba Juu ya Ushairi,” Journal of the East African Swahili Committee, Na. 28/1 (January, 1958).
Robert, S. Kielelezo cha Fasili. London: Nelson, 1968.
Scully, J. (Mhariri), Modem Poets on Modern Poetry. London: Fontana, 1966.
Secondary English Editorial Staff. A Book ofPoetry, l & 2. New York: Harcourt Brace Jovanovich, 1983.
Senkoro, F.E.M.K. Fasihi. Dar es Salaam: Press and Publicity Ccntre, 1984.
Senkoro, F.E.M.K. Fasihi na Jamii. Dar es Salaam: Press and Publicity Centre, 1987.
Sherman, G.S. Poet and the Flea: On Beat, Image, and Milieu of Poetry. San Jose: Cobra Press. 1971.
Synder, R. Poet to Teacher to Student. Ashland Collcge, Ohio: Ashland Poetry, 1971.
Taylor, H. Poetry: Polnts of Departure. Englewood Cliffs, N.J.: Winthrop, 1974.
Thomson, G. Studies in Ancient Greek Society: The Prehistonc Aegean. London: Lawrcnce & Wishart 1961.
Topan, F. “Swahili Textual Variation.” Kiswahili. 39/142 (1969), kur. 91-110.
“Dibaji” katika E. Kezilahabi, Kichomi. Nairobi: Heinemann, 1974 kur. vii – xii.
Topan, F. (Mhariri), Uchambuv wa Maandishi ya Kiswahili: 1 & 2. Dar es Salaam/Nairobi/Lusaka: Oxford University Press, 1971 & 1977.
Turco, L. Poetry: An Introduction Through Writing. Englewood Cliffs, N.J: Reston. 1973.
Untermeyer, L. Poetry: Its Appreciation and Enjoyment. New York:
Hareourt Brace Jovanovich, 1934.
Velten, C. Desturi za Wasuaheli. Gottingcn, 1903. – Prosa und Poesie der Suaheli. Berlin, 1907.
|
|
|
|