ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI' (/showthread.php?tid=2098) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI' - MwlMaeda - 01-11-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'RIJALI' Neno rijali katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. Nomino: [Ngeli: a-/wa-, wingi: marijali ] mwanamume mwenye nguvu nyingi za kiume. 2. Nomino: [Ngeli: a-/wa-] mwanamume shujaa katika jambo. Mshairi mmoja alipata kutongoa: Ufukara jambo zito, aliloumba Qahari, Mkubwa huwa mtoto, na rijali huwa thori, Asemalo huwa ndoto, hakubaliwi shauri. Katika lugha ya Kiarabu, neno hili rijali(soma: rijaalun/rijaalan/rijaalin رجال ) ni nomino wingi wa neno rajuli (soma: rajulun/rajulan/rajulin رجل) lenye maana zifuatazo: 1. Mwanamume mwanadamu aliyebalehe. 2. Mtu anayeshughulika na jambo fulani, rajulu Al-Aamaal (soma: Rajulul Aamaal رجل الأعمال mfanyabiashara. 3. Hali ya kutembea kwa miguu, rijaalan رجالا. 4. Wafanyakazi wa kikosi cha kuzima moto, rijaalun رجال. 5. Wakongwe, wakubwa wa ukoo au jambo. Kinachodhihiri ni kuwa Waswahili badala ya kuchukuwa neno rajuli رجل lililo katika umoja, walichukua neno rijaali رجال lililo katika wingi na wakalipa maana ya neno rajuli رجل lililo katika umoja. Shukran sana. Khamis S.M. Mataka. |