MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: NA NIKIFA WASICHANGE
#1
NA NIKIFA WASICHANGE

Ewe mwanangu taali, Njoo hapa kwenye mwanga
Njoo usiketi mbali, Kisha na mlango funga
Nataka kupa kauli, ishike kama usinga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Ndiye wewe wa awali, rika si mwana mchanga
Timamu zako akili, huna chembe ya ubunga
Ninakupa uwakili, usikubali matanga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Sinazo nguvu za mwili, kwa maradhi kunizonga
Mwanangu wajidhalili, mikono kwao kukinga
Hupati japo kalili, wote wakupiga chenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Leo ni dhoofu hali, ndiyo kisa wanitenga
Niliwalea azali, maisha yao kujenga
Sasa nipo muhimbili, Dawa za kuungaunga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Huu ni mwaka wa pili, toka nipate majanga
Moyo unatundu mbili, yangu moja imefunga
Dhati nateseka kweli, wafumba yao maninga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Daftari na bakuli, wakipitisha kuchanga
Piga teke vyende mbali, usishiriki ujinga
Nakuomba wakabili, usihofu zao ngenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Mauti yakiwasili, ombi nizikwe Mkinga
Moa kijiji aali, sitaki kuzikwa Vanga
Mwanangu wosia mali, wapuuzao hutanga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

Hapa natia kufuli, na hotuba kuifunga
Wewe wangu abtali, tayari nishakuganga
hima fanya kulihali, yangu usijeyatenga
Nikifa wasijechanga, ishike hii kauli

MBARUKU ALLY
MOTO WENU Jr
(FAHARI YA TANGA)

Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)