MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI : SINA BAHATI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI : SINA BAHATI
#1
Mtunzi:RamaB.
Hivi hawa matajiri, walifanya kazi gani?
Kuondoa ufakiri, wakawa mamilioni.
Nipeni yao siri, iniingie kichwani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.

Nikalikamata jembe, panga na shoka begani.
Nikautoa uzembe, mpunga panda kondeni.
Ukajaliwa na ng’ombe, nikabaki kichwa chini.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaitwaa mashua, nikaitweka baharini.
Samaki kwenda kuvua, mingisi si saladini.
Wimbi kubwa la bamvua, chombo kikenda mwambani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Carina nikanunua, teksi bubu kituoni.
Abiria nangojea, ilala na buguruni.
Trafiki kaniotea, shitaka mahakamani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikauza vitumbua, asubuhi na jioni .
Wateja walinijua, ni gwiji la mtaani.
Mgambo wakang’amua, nauza bila leseni.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaenda mgodini, kujichimbia madini.
Nikaona sa nawini, naunga umasikini.
Magufuli kabaini, ninauhujumu uchumi.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Bunduki yangu begani, nikaingia porini.
Kuwawinda hayawani, kwenda uuza sokoni.
Wakaja nisweka ndani, segerea gerezani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikalipiga kabumbu, golikipa namba wani.
Nikawa kama mzungu, Ronado haoni ndani.
Nikavunjika mguu, nipo hoi taabani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Nikaicheza singeli, asiyejua nani?
Wote walikubali, si Tandika si Mtoni.
Nikazushiwa kejeli, navuta bange kizani.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Bora nirudi nyumbani, ni Mafia kisiwani.
RamaB ni mashakani, sijui nifanye nini.
Zaharia na kinyemi, mwenzenu nisaidieni.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Rabana nipe sahali, mja wako Ramadhani.
Mikiki nilo himili, na bado ni masikini.
Beti hizo ni kamili, peni naweka chini.
Sina bahati mwenzenu, kuchuma najitahidi.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)