MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: JAMANI SINA BAHATI

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: JAMANI SINA BAHATI
#1
MTUNZI: IBN MAJOR ABDUL OMARY
Jama nanena jamani, mja nisokuwa jumu,
Jua naweka jamvini, waja msinihujumu,
Msijifanye jinuni, mkakosea hukumu,
Najishutumu jamani, Sina bahati janjuzi.
Janjuzi sina bahati, tokea kwangu zaoni,
Mama hakwisha jamati, kubembeleza manani,
Apate moja gameti, toka mwake fumbatyoni,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Ikamfikia zama, niwe la kwake pakato,
Pumzi ikawa zahama, mfumbati kwa fumbato,
Kinywa wazi akihema, akatoa mgong’oto,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Mgong’oto alotoa, pakato li hadharani,
Tabasamu akatoa, tabasamu la mwishoni,
Neno tena hakutia, furungu kawa kooni,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Kwenye gao la mkunga, nikawa najililia,
Sauti kama kipenga, za dunga kama shazia,
Nikafungwa mitulinga, nisiweze jihemea,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Hatima kwangu ikawa, kunyonya uji mseto,
Domo likafanywa bwawa, nikajifia kingoto,
Ikanijaa shakawa, kama lo ndani ya puto,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Jamaa waso maono, tuhuma wakanitia,
Mtoto asomavuno, jina baya wanitia,
Kumweka mama kibano, ikawa yangu hatia,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Mungu aso athumani, nuru akanangazia,
Vidato kwangu gambani, mabuku nikabukua,
Badala ya kauleni, digri nikachukua,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Japo njia so laini, wengi walinieleka
Sasa nala kilaini, ila roho yasongeka,
Majonzi tele mbonini, vile mama akopeka,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Masikitiko kibao, leo naitwa Janjuzi,
Mengi mazuri mafao, nala peke kama jizi,
Sikumpa kizibao, mama yangu wa kipozi,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.

Ila namwomba rabuka, mola wa zote sayari,
Yalo mema kutunuka, mama yangu wa sahari,
Aishi bila upeka, adumu kwa ufahari,
Najishutumu jamani, sina bahati janjuzi.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)