Hadithi hadithi…….
Hapo zamani za kale, palikuwepo na mwanaume mmoja jambazi aliyeoa mwanamke mwizi. Basi mwanamke alibeba mimba ,na wakati wa ujauzito wake, mume na mke waliketi kusemezana…. Mwanamke alimuuliza mumewe, “Hivi mume wangu, tunatarajia kuzaa mtoto wa aina gani?”
Mwanaume alijibu “sijui”.
Hadithi hadithi……
Hapo zamani za kale palitokea kundi la wanyiramba waliokuwa wamepanda gari la wazi wakielekea safari ya mbali,
basi wakiwa katika mwendo, walifika sehemu iliyokuwa na miba iliyotanda, juu, kondakta akawaambia
” inama”
wao wakaitikia inama ikole wakimaanisha nyama iko wapi? Sasa wakati wakiendelea kupepesa macho kutafta wapi kuna nyama,
Basi ,muda wa kujifungua ukafika, na mkunga akamsaidia yule mwanamke kuzaa, baada ya mtoto kutoka, alionekana kufumbata kiganja kimoja cha mkono wa kushoto.
Walipokifungua kiganja walikuta pete ya ndoa ya mkunga aliyokuwa ameikwapua wakati akitoka.
Ghafla walijikuta wakiraruruwa na miba usoni, wengine wakabaki vifua wazi kutokana na nguo zao kuchanwa chanwa.
Hadithi yangu inaishia hapo
Hapo zamani za kale palitokea binti aliyekua na kunawili, alikuwa mtoto wa mfalme Matata.
Binti huyo aliitwa Majivuno, basi wazazi wake walipenda nayeye alijivuna kutokana na sura, au umbile zuri alilokuwa nalo.
Vijana kadhaa waliowahi kujitokeza kutaka kumuoa ,aliwakataa kutokana na wao kuwa na kipato cha chini, ama kweli penzi la maskini ni sawa na chai isiyo na sukari.
Hayawi hayawi yakawa, kijana mmoja aitwaye Mgeni, alijitokeza kumchumbia, kutokana na utanashati wake na kuonekana mzee wa pochi, msichana alikubali na akaolewa.
Wakiwa katika maisha, vituko vilianza kupishana, harufu ya uvundo ikazidi kujonga, kila wakati mumewe alikuwa akidamka usiku kwenda kulima,
Bunti majivuno alijiuliza, hivi kwanini mume wangu huenda shambani usiku tu?
Kama kawaida, siku inayofuata mumwewe alimuaga mkewe kwenda shambani, ili kujua nini kinaendelea juu ya mumewe, Binti majivuno aliamua kunyatia mpaka karibu na shamba,
Alipoangaza macho, kwa mbali aliona moto mkubwa sana, na kundi la minyama mikubwa, aliposogelea alimuona mumewe akiwa na mkia huku moto ukitoka mdomoni wakati huohuo miti ikitetezwa mithili ya majani makavu shashikapo moto,
Kuona hivyo Binti alitimka bio mpaka kijijini kwa wazazi wake huku akitwet, walipomuuliza ,kulikoni? Alijibu “Mume wangu ni Zimwi
Wazazi wakamwambua mwananetu, ulikataaa palipo pema, ukanaswa pabovu,
Ama kweli Ndege mjanja hunaswa na tundu bovu, na mkataa pema ,pabaya panamwita
HADITHI YANGU INAISHIA HAPO,
Hapo zamani za kale, palikuwepo na mwanaume mmoja jambazi aliyeoa mwanamke mwizi. Basi mwanamke alibeba mimba ,na wakati wa ujauzito wake, mume na mke waliketi kusemezana…. Mwanamke alimuuliza mumewe, “Hivi mume wangu, tunatarajia kuzaa mtoto wa aina gani?”
Mwanaume alijibu “sijui”.
Basi ,muda wa kujifungua ukafika, na mkunga akamsaidia yule mwanamke kuzaa, baada ya mtoto kutoka, alionekana kufumbata kiganja kimoja cha mkono wa kushoto.
Walipokifungua kiganja walikuta pete ya ndoa ya mkunga aliyokuwa ameikwapua wakati akitoka.
Hadithi hadithi……
Hapo zamani za kale palitokea kundi la wanyiramba waliokuwa wamepanda gari la wazi wakielekea safari ya mbali,
basi wakiwa katika mwendo, walifika sehemu iliyokuwa na miba iliyotanda, juu, kondakta akawaambia
” *inama*”
wao wakaitikia *inama ikole*wakimaanisha nyama iko wapi? Sasa wakati wakiendelea kupepesa macho kutafta wapi kuna nyama,
Ghafla walijikuta wakiraruruwa na miba usoni, wengine wakabaki vifua wazi kutokana na nguo zao kuchanwa chanwa.
Hadithi yangu inaishia hapo
Hapo zamani za kale palitokea binti aliyekua na kunawili, alikuwa mtoto wa mfalme Matata.
Binti huyo aliitwa Majivuno, basi wazazi wake walipenda nayeye alijivuna kutokana na sura, au umbile zuri alilokuwa nalo.
Vijana kadhaa waliowahi kujitokeza kutaka kumuoa ,aliwakataa kutokana na wao kuwa na kipato cha chini, ama kweli penzi la maskini ni sawa na chai isiyo na sukari.
Hayawi hayawi yakawa, kijana mmoja aitwaye Mgeni, alijitokeza kumchumbia, kutokana na utanashati wake na kuonekana mzee wa pochi, msichana alikubali na akaolewa.
Wakiwa katika maisha, vituko vilianza kupishana, harufu ya uvundo ikazidi kujonga, kila wakati mumewe alikuwa akidamka usiku kwenda kulima,
Kama kawaida, siku inayofuata mumwewe alimuaga mkewe kwenda shambani, ili kujua nini kinaendelea juu ya mumewe, Binti majivuno aliamua kunyatia mpaka karibu na shamba,
Alipoangaza macho, kwa mbali aliona moto mkubwa sana, na kundi la minyama mikubwa, aliposogelea alimuona mumewe akiwa na mkia huku moto ukitoka mdomoni wakati huohuo miti ikitetezwa mithili ya majani makavu shashikapo moto,
Kuona hivyo Binti alitimka bio mpaka kijijini kwa wazazi wake huku akitwet, walipomuuliza ,kulikoni? Alijibu “Mumewangu ni Zimwi*
Ni hadithi ambayo maana yake ya wazi inawakilisha maana nyingine isiyo ya wazi. Ni masimulizi ya kiishara yenye kutumia wanyama au taashira za aina mbalimbali zinazowakilisha wanyama hao.
Hadithi kama za sungura,majitu na kobe huwa zinawakusudia watu. Hadithi hizi hutumia wanyama kama vielelezo vya sifa na tabia za binadamu. Baadhi ya wataalamu wa sanaa waliotumia sana Istiara ni Shaaban Robert katika Adili na Nduguze, Kufikirika na Kusadikika.
Katika kazi hizo vitu,watu na wahusika vinasimamia mawazo na adili fulani maalumu.
(b) Mbazi
Ni hadithi fupi yenye mafunzo itolewayo kama mfano wakati wa maongezi au kumwonya mtu. Mwalimu aliyevunja rekodi katika matumizi ya aina hii ya hadithi alikuwa Yesu Kristo.
Alitumia mbazi kwa kiasi kikubwa kuwaelekeza wanafunzi wake na walimwengu katika mafundisho yake.
Mfano wa mbazi ni huu:
Kiongozi mmoja wa kitaifa alikuwa akisisitiza umuhimu wa kila mwananchi kushiriki katika kulinda usalama na amani nchi badala ya kuona suala hilo ni la watu fulani tu hasa vyombo vya ulinzi na usalama. Katika msisitizo wake huo akatoa mbazi ifuatayo…………. siku moja katika nyumba fulani panya aligundua kuwa ametegewa mtego na kwa kuwa hakuweza kuutegua alienda kuomba msaada kwa ng’ombe lakini ng’ombe alikataa akidai kuwa huo ni mtengo wa panya yeye haumuhusu. Panya hakuchoka akapiga hodi kwa mbuzi na kumlilia shida yake, mbuzi naye akamjibu kama alivyojibu ng’ombe kuwa huo ni mtego wa panya wala haunihusu. Hatimaye panya akamwendea jogoo na kueleza yote lakini jogoo naye alimkatalia panya na kumkejeli kuwa huo mtego hamhusu yeye jogoo. Baada ya kugonga mwamba panya akakosa amani akihofia mtego ulioitwa.. “ …wa panya..” kwa kweli siku nzima ile panya hakuweza kujipatia riziki akihofia mtego. Usiku ulipofika baba mwenye nyumba alishituliwa na mkewe akiambiwa kuwa mtego umefyatuka na bila shaka panya atakuwa amenaswa. Baba yule akakurupuka na kuuendea mtego huku akipuuza hadhari ya mkewe kuwa asiende giza giza, alienda huku akijifariji kuwa panya hawezi kumdhuru chochote……alipoufikia mtego ule akapeleka mkono ili auchukue na kumsulubu panya aliyewasumbua kitambo. La haula! Kumbe hakuwa panya, mzee yule akarudi nyuma haraka huku akiagiza mkewe amletee taa haraka. Baada ya taa kuletwa ikabainika mtego ulinasa nyoka na hivyo mzee yule aliumwa na nyoka yule…..ghafla hamkani ikaingia ndani ya nyumba kutafuta dawa ya kumponya mzee mwenye nyumba. Muda si muda mzee yule alikata roho kwa kuzidiwa na sumu ya nyoka na nyumba ikawa na tanzia. Siku ya kwanza wageni wachache ikabidi achinjwe jogoo kupata kitoweo. Siku ya pili wageni ni wengi kiasi ikabidi achinjwe mbuzi ili kukidhi mahitaji. Baada ya maziko siku ya tatu na kumaliza tanga akachinjwa ng’ombe.
Funzo:
Hivi ule mtego ulikuwa wa panya,ng’ombe,mbuzi,kuku au baba mwenye nyumba? Mbazi hii inasadifu umuhimu wa kushirikiana kuokoa mambo ambayo yakiharibika yataathiri wengi.
Ni masimulizi mafupi yanayohadithia tukio moja bila ya kulifafanua kwa mfano; kidahizo cha nyani na mtoto wake.
Nyani na mtoto wake walikwenda kula mahindi katika shamba,wakala,wakala,wakala,halafu mtoto aliuliza,…… “mama tunakula tu,je mpaka uko wapi?” mamaye akamjibu …. “we kula tu mpaka wataweka wenyewe.”
Kidahizo chaweza kutokana na tukio la kweli lenye kuchekesha.
Hapo zamani za kale, palitokea Simba mwenye njaa, katika pitapita zake za kuwinda, alimkuta Sungura akiwa amelala fofofo. Alishusha pumzi, akatabasamu na kumshukuru sana Mungu kwa ukarimu wake wa kutambua taabiko lake na kumtunuku chakula pasi na haja ya kukitolea jasho. Taratibu alimsogelea Sungura ili asije akamwamsha, akalala yeye…Alipoinua miguu yake kutaka kumkamata, mara akatokea Ayala mnono ambaye alipita akikimbia karibu naye, akielekea upande wa kaskazini kwenye uwanda wa nyasi fupi. Simba alimwacha Sungura na akakurupuka kumkimbiza yule Ayala. Vishindo kelele na purukushani za Simba na Ayala vilimgutusha na kumwamsha Sungura ambaye aliamka na kutimua mbio kuelekea upande wa kusini. Baada ya kumkimbiza Ayala kwa muda mrefu Simba alishindwa na kuamua kurudi ili akamle yule Sungura. Alipogundua kuwa Sungura naye alikuwa ameamka na kukimbia, Simba alisema kwa kujilaumu, “ama kweli nimepata nilichostahili; kwa kuwa nilikiacha chakula nilichokitia mkononi tayari kwa tamaa ya kutaka kupata zaidi.”
Hadithi hii inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi hii;
Mbweha alikuwa akijigamba mbele ya Paka kuwa yeye ana mbinu nyingi sana za kuwakwepa maadui zake. “Nina fuko zima la mbinu na ujanja,” alisema, “ambalo lina mamia ya njia za kujiepusha na maadui zangu wakati wa hatari.” “Mimi ninayo mbinu moja tu,” alisema Paka; “lakini ninaiamini, na inanifaa hiyo hiyo.” Wakiongea maneno hayo, punde wakasikia sauti za Mbwa wawindaji zikielekea upande wao, na Paka alichupa akauparamia mti haraka na kujificha juu kwenye matawi. “Hii ndiyo mbinu yangu,” alisema Paka. “Je mwenzangu wafanyaje?” Mbweha akafikiri kwanza kutumia njia hii, mara njia ile, na kabla hajafanya maamuzi, Mbwa walimkaribia na kumkaribia, na mwishowe Mbweha akiwa katika mkanganyiko huo, alikamatwa na kuuawa na Wawindaji. Paka ambaye alikuwa akishuhudia kinachotokea, alisema; “Heri njia moja salama kuliko njia mia ambazo huwezi kuzitumia.”
Hadithi hii inatufundisha nini?
1……………………………………………………………………………………………………………………
2……………………………………………………………………………………………………………………
3……………………………………………………………………………………………………………………
Taja methali, nahau au msemo wa Kiswahili wenye maana inayofanana na maudhui ya hadithi hii;
………………………………………………………………………………………………………………………
………………………………………………………………………………………………………………………
JIVI
Sema yote umalize,kwa hili sidanganyiki
Zipige nari na zeze,fahamu sirubuniki
Funga moyo ujikaze,Nkwazi hanusuriki
Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa
Haya sikuhadithiwa,niliwafuma pahala
Wawili mithili njiwa,kwa mahaba raha mwala
Ukanipata ukiwa,usingizi sikulala
Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa
Wanawake muna mbinu,mufichapo yenu Mambo
Hufutikwa kwenye kinu,jitu lenye kubwa umbo
Mume akose fununu,kuna jivi lala vyombo
Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa
Sina mashaka na Njau, ni njema zake tabia
Hana tamaa ya nyau,vya watu kuwaibia
Hata pesa kisahau,mbio hukurudishia
Yameona yangu mato,haya sikuhadithiwa
Na like jekundu ua,Jana alokutumia?
Wacha uongo kuzua,Filieda naumia
Hivi kweli watambua,kuwa ninaangamia
Yameona yangu mato,haya sikuhadithiwa
Hapa vema kuishia,mengine soni kunena
Usambe ninatishia,najichunga muungwana
Mengine nabakishia,vyuma visije umana
Abdul Ndembo(Wingu zito)
Mburahati sekondari