SHAIRI: JIVI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: JIVI (/showthread.php?tid=759) |
SHAIRI: JIVI - MwlMaeda - 08-03-2021 JIVI Sema yote umalize,kwa hili sidanganyiki Zipige nari na zeze,fahamu sirubuniki Funga moyo ujikaze,Nkwazi hanusuriki Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa Haya sikuhadithiwa,niliwafuma pahala Wawili mithili njiwa,kwa mahaba raha mwala Ukanipata ukiwa,usingizi sikulala Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa Wanawake muna mbinu,mufichapo yenu Mambo Hufutikwa kwenye kinu,jitu lenye kubwa umbo Mume akose fununu,kuna jivi lala vyombo Yameona mato yangu,haya sikuhadithiwa Sina mashaka na Njau, ni njema zake tabia Hana tamaa ya nyau,vya watu kuwaibia Hata pesa kisahau,mbio hukurudishia Yameona yangu mato,haya sikuhadithiwa Na like jekundu ua,Jana alokutumia? Wacha uongo kuzua,Filieda naumia Hivi kweli watambua,kuwa ninaangamia Yameona yangu mato,haya sikuhadithiwa Hapa vema kuishia,mengine soni kunena Usambe ninatishia,najichunga muungwana Mengine nabakishia,vyuma visije umana Abdul Ndembo(Wingu zito) Mburahati sekondari |