MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: LALA

Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
SHAIRI: LALA
#1
LALA
Lala mwendani ulale, lala nakupepelea,
Lala mpenzi silile, uache kuniwazia,
Lala wangu usinzile, lala nakukumbatia,
Lala Nkwazi wangu lala, kabisa lala sinzia.

Lala nakuomba lala, lala nakubembeleza,
Lala siwaze suala, siku utanipoteza,
Lala nakupenda lala, lala ninakutuliza,
Lala Nkwazi wangu lala, kabisa lala sinzia.

Lala nakuchumu lala, mwaa! Lala honey wangu,
Lala waache mafala, hawana lolote kwangu,
Lala ulale pahala, palipo kifua changu,
Lala Nkwaziwangu lala, kabisa lala sinzia.

Lala baba nani lala, lala usitese moyo,
Lala mjuani lala, lala sijali yajayo,
Lala siende Mbagalla, lala na wako kimoyo,
Lala Nkwazi wangu lala, kabisa lala sinzia.

Lala ninakufunika, tulale sote wawili,
Lala acha weweseka, niote mama wawili,
Lala usijeshituka, usingizi wende mbali,
Lala Nkwazi wangu lala, kabisa lala sinzia.

Limetungwa na Filieda Sanga, Kama lilivyoombwa na Malkia.
Mwl Maeda
Reply

Forum Jump:

Users browsing this thread: 1 Guest(s)