TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi andishi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=7) +---- Forum: Riwaya (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=52) +---- Thread: TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA (/showthread.php?tid=1029) |
TASWIRA YA MWANAMKE KATIKA RIWAYA - MwlMaeda - 08-27-2021 Taswira ya Mwanamke Tunaposema taswira ya mwanamke, tunamaanisha picha ya mwanamke inayojitokeza baada ya matumizi mbalimbali ya semi na ishara katika kazi ya fasihi. Waandishi wa riwaya za Kiswahili wamewachora wahusika wa kike katika taswira mbalimbali. Katika utafiti huu, mtafiti amechunguza uchorwaji wa taswira hizo katika kazi chache ziitwazo Rosa Mistika, Nyota ya Rehema, Shida na Hiba ya Wivu ambazo ni riwaya za Kiswahili. Waandishi wa riwaya hizi ambao ni wa jinsia tofauti, wamewapanga wahusika wanawake wa riwaya hizo katika taswira za uzinifu, ubidhaishaji (mali), vyombo vya kuwastarehesha mwanamume na wapenda fedha. Aidha baadhi ya waandishi wamediriki kuwatenga wanawake wasifanye shughuli nyingine muhimu za kuzalisha mali katika jamii zao kwa kuwapangia kazi za malezi ya watoto na kuwatumikia wanaume. Mwanamume ndiye anayeonekana kuwa mwuamuzi, msimamizi na mpiganaji wa majukumu muhimu katika jamii ilhali mwanamke akiwa mzalishaji. Wakati mwingine, mwanamke amechorwa katika riwaya kama mtekelezaji wa yale yanayoamuliwa na kuamuriwa na mwanamume. Mahali pengine mwanamke ameonekana akiwa na uwakilishi finyu au hakuna kabisa katika uongozi wa juu ndani ya jamii. Uwasilishwaji wa kina wa taswira ya mwanamke katika sura hii umerejelea riwaya hizo nne teule, zilizotajwa hapo juu. |