Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 90 online users. » 0 Member(s) | 89 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
MATUMIZI YA NAFSI KATIKA USHAIRI |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 04:26 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
Washairi wengi sana tuchanganya nafsi katika kazi zetu za ushairi katika namna ya kumvuruga msomaji.
Nafsi ziko tatu,
Ya kwanza, mimi na wingi wake sisi
Ya pili,Wewe na wingi wake nyinyi
Ya tatu, yeye na wingi wake wao.
Sasa wengi wetu hujikuta tunachanganya, na matokeo yake wakati mwingine tunamvuruga msomaji.
Mfano.
Ndugu yenu nikilala, ati ninawachunia,
Nikiamka ni ila, vurugu namfanyia,
Kwangu hakuna aula, la kuweza wavutia?
Mshororo wa kwanza.
Neno “Yenu” na “ninawachunia”
Huashiria msemaji katumia nafsi ya pili wingi kusema hisia zake. Hii humaanisha walengwa wa ujumbe wake wako na yeye sehemu moja na anaweza kuwaelekezea macho au kidole, na hao walengwa wake wanamsikia na kumuona.
Mshororo wa pili.
Neno “Namfanyia”
Huashiria msemaji katumia nafsi ya tatu umoja kusema hisia zake. Hii humaanisha mlengwa wa ujumbe wake hayuko naye sehemu hiyo wakati akiweka wazi tuhuma zake.
Kwahivyo hapa utaona ubeti mmoja jinsi matumizi ya nafsi yalivyotumika vibaya, na matokeo yake, msomaji hubaki na viulizi ambavyo si vya msingi na visivyokuwa na natija yoyote.
Kwa mfano, hatujuwi kama msemaji lawama zake anazielekeza kwa mtu mmoja au kundi la watu, na hatujuwi kama mlengwa wake yuko naye sehemu moja au hayuko naye sehemu moja.
Kwa maoni yangu, nadhani shairi moja kutumilia nafsi zaidi ya moja si tatizo, ila tatizo ni mchanganyiko huo wa nafsi kukosa mantiki, kama tulivyooona katika ubeti huo wa mfano. Nadhani hii ni kasoro tusiyoijuwa au twaijuwa lakini twaipuuza kwa kudhani haithiri kazi zetu.
Kwa maoni yangu hii ni kasoro na yafaa kuepukwa na washairi, ingawa wapo baadhi ya washairi wanaona huu ni ufundi. Nimeona mashairi mengi, tena mengine ya watunzi wazuri kabisa yakiwa na kasoro hii.
Hayo ni maoni yangu na yanaweza kuwa si sahihi, ila kama lipo la kujifunza basi na tujifunze sote. Nawaacha na shairi langu hili nililolitunga tarehe 01 Aprili 2017 Jumamosi 03:37am
SHAIRI
Nianze wataka radhi,
Kwa huu wangu waadhi,
Huenda ukawaudhi,
Ingawa si yangu nia.
Wako wenzetu baadhi,
Wamejivisha kubadhi,
Zilizo na kubwa hadhi,
Kwenye hii tasnia.
Wanajiita malenga,
Na hawajuwi kulenga,
Leo wajijuwe chenga,
Si mchele nawambia.
Uchao wanapotunga,
Vina huviungaunga,
Pasi mizani kuchunga,
Tungo hutuandikia.
Makosa yanakithiri,
Tungo zao sio nzuri,
Waambiwapo ni shari,
Nzi wanakujazia.
Haya yetu mashairi,
Yawapo sio mazuri,
Lazima tutafakari,
Wapi tulipokosea.
Kwa kuitazama fani,
Vina na yake mizani,
Tuone namna gani,
Yataweza kuvutia.
Aula kila fanani,
Aweke kando utani,
Anapokuwa ugani,
Kwa kufuata sheria.
Tuyachunge maudhui,
Kama maziwa na tui,
Kama haya hatujui,
Tungo hazitatimia.
Sivyo katu hatukui,
Na tija hatuambui,
Kabisa hatuchanui,
Haya sipozingatia.
Lipo la muhimu hasa,
Mtiririko wa visa,
Siviweke kwa makosa,
Pindi ukijipangia.
Na hoja za kibubusa,
Mithili yake garasa,
Wachana nazo kabisa,
Tungo kuziandikia.
Tungo ziwe za mfano,
Zisilete farakano,
Bali zikuze usono,
Pamwe na udugu pia.
Kama kingali cha mno,
Ni kuchezesha maneno,
Pasi na kumwaga wino,
Na maguvu kutumia.
Kwani hakutaki nguvu,
Kuwa mtunzi angavu,
Tungo nyingi huwa mbovu,
Nguvu tunapotumia.
Zinataka utulivu,
Pamoja na uzamivu,
Kusoma siwe mvivu,
Sivyo hazitavutia.
Ili tungo ziwe tamu,
Mithili yake ya jamu,
Basi inatulazimu,
Kutunga kwa kutulia.
Hawi mtunga nudhumu,
Kuinuka alaumu,
Karatasi na kalamu,
Ambazo azitumia.
Na pia haiwi kwake,
Afure aghadhibike,
Kisa kiwe tungo zake,
Hadhira kumsusia.
Hata watu wamcheke,
Wamwite mwana mteke,
Hainuwi kinywa chake,
Mawi kuwarudishia.
Bali atakaa chini,
Tena akiwa makini,
Apate kuyabaini,
Ya ganda na kokwa pia.
Atazama vitabuni,
Kuzirejea kanuni,
Ili asitunge guni,
Na kuiudhi jamia.
Atatunga za maana,
Zenye mizani na vina,
Asifike kila kona,
Kwa tungo za kuvutia.
Katu hawezi tukana,
Watu wanao mguna,
Ila atawaza sana,
Wapi alipokosea.
Na hata wakimgomba,
Ujuzi atawaomba,
Na kwao atajikomba,
Yake yapate timia
Yashike ninayoamba,
Uende nayo sambamba,
Sikio sitiye pamba,
Upate kuyasikia.
Mithili ya asumini,
Mwenye ujuzi rasini,
Mpigiye goti chini,
Kama wataka nukia.
Hapa sasa tamatini,
Naweka kalamu tini,
Nawaaga kwaherini,
Kikomo changu natia.
MISAMIATI
Kibubusa….mtu anayekubali jambo pasina kulitafakari
Usoni……….usuhuba
13 Agosti 2018 Jumatatu 21:58
Jina la Mtunzi Dotto Rangimoto
Jina La Utunzi Jini Kinyonga
Simu +255762845394 Morogoro.
|
|
|
SHAIRI: HAMUNISHINDI |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 04:11 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
HAMUNISHINDI
Mkusanyike makundi,
Wa Bara na Visiwani,
Mje pia na mafundi,
Wa Lamu na Mombasani,
Juweni hamunishindi,
Kwa uwezo wa Manani,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Machagina toka Lindi,
Na wa Tanga Ngamiani,
Mje na wenu ufundi,
Wa sasa na wa zamani,
Haitokwisha raundi,
Mtakuwa taabani,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Nawataka wa Malindi,
Muulete ushindani,
Mchinje na wenu bundi,
Mlopawa ugangani,
Mtaishia stendi,
Mzikwe ughaibuni,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Wakongwe kwenye vilindi,
Mtambao baharini,
Walimu wenye vipindi,
Vyuoni na mashuleni,
Mfike na zenu tendi,
Ninawangoja dimbani,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Taslimu siyo hundi,
Nawapa zipokeeni,
Mnausaka ushindi,
Kwa nguvu ziso kifani,
Taishia kwenye lindi,
Musitoke maishani,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Ushairi siyo ndondi,
Ama gozi uwanjani,
Kwa maguvu hauendi,
Hata uwe Tysoni,
Ndiyo ma’na hampandi,
Tungo hazitaki kani,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
Si shairi si utendi,
Nawashinda hini fani,
Hata kama hampendi,
Mpawa hawezekani,
Hapa mwisho mbele sendi,
Tukutane ulingoni,
Nawaita uwanjani,
Nione wenu ufundi.
9Machi2017Alhamis13: 11am
Jina la mtunzi: Dotto Rangimoto
Lakabu JiniKinyonga.
Simu: 0762845394
|
|
|
SHAIRI: SICHO |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 04:02 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
SICHO
Sicho kisokuwa ndicho, sicho nitakeni sicho?
Sicho sikitaki hicho, sicho kisokuwa ndicho,
Sicho nilisikinacho, na kuwa nacho sinacho,
Sicho chambiwacho sicho, sicho nipani kilicho.
Sicho mwanenani ndicho, sicho kisokuwa hicho?
Sicho nipani kilicho, mwa vilivyo kuwa ndicho,
Sicho nilopiga jicho, kilicho ndicho chambwacho,
Sicho chambiwacho ndicho, sicho nipani kilicho.
Sicho nilokuwa nacho, ningaliwambia ndicho,
Sicho mukajuwa ndicho, na pia ambacho sicho,
Sicho pimani kwa macho, mupambanuwe kiwacho,
Sicho chambiwacho ndicho, sicho nipani kilicho.
Sicho mushajuwa sicho, kipi kingine kilicho?
Sicho kisiwape ki'cho, mukataka kuwa nacho,
Sicho mimi nili nacho, ila hakikuwa hicho,
Sicho chambiwacho ndicho, sicho nipani kilicho.
Sicho tamati si hicho, sicho muloshika ndicho,
Sicho kingekuwa ndicho, basi singegomba kwa'cho,
Sicho nikitefutacho, sicho atanani nacho,
Sicho chambiwacho ndicho, sicho nipani kilicho.
Utunzi wa: Ibrahim Hemed (sema nao)
SLP - 1019 - 80200.
MALINDI/KENYA.
© 26/11/2019.
|
|
|
USHAIRI NA UTOFAUTI WA MAWAZO JUU YA MAANA YA USHAIRI |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 03:34 PM - Forum: Fasihi kwa ujumla
- No Replies
|
|
Ni kweli kwamba tofauti ya mawazo baina ya mabingwa wa Ushairi wa Kiswahili kuhusu maana ya ushairi ni msisitizo tu kutokana na wataalamu mbalimbali wa ushairi kufasili maana za ushairi kwa utofauti.
Kwa mujibu wa Wamitila (2010) anadai kuwa Ushairi ni utanzu ambao una historia ndefu katika Fasihi ya Kiswahili ingawa mpaka leo hakuna makubaliano kuhusu utungo wa kwanza uliandikwa lini. Wataaalamu wanakubaliana kuwa utanzu huu una historia ndefu. Anaendelea kusema kuwa Ushairi wa Kiswahili umegawanyika katika makundi makuu mawili amabayo ni mashairi ya kijadi au ya kimapokeo ambayo hutungwa kwa kuzingatia arudhi au kaida za utunzi kama vina, mizani, idadi maalumu ya mishororo katika ubeti na vipande. Pia Mashairi ya kisasa au huru ambayo hukiuka kaida hizo na badala yake kutegemea mbinu nyingine za kishairi kama uruwazi wa kimuundo kuwasilisha ujumbe wake.
Wataalamu mbalimbali wa Ushairi wa Kiswahili hutofautiana katika maana zao za Ushairi. Kwa kiasi kikubwa wataalamu hawa wamegawanyika katika makundi mawili ambayo ni wana Mapokeo na wana Usasa. Kwa kuanza na Wanamapokeo wanatoa maana za ushairi na kuonesha msisitizo pamoja na kutofautiana katika maana zao kama ifuatavyo.
Kwa mujibu wa Shaban Robert (1968) anafasili Ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na utenzi. Ushairi una ufasaha wa maneno machache au muhutasari. Anaendelea kusema kuwa Shairi ni wimbo mkubwa, wimbo ni shairi dogo na utenzi ni upeo wa Ushairi. Anazidi kufafanua kuwa kina ni mlingano wa sauti za herufi, kwa maneno mengine huitwa mizani ya sauti na ufasaha na uzuri wa lugha, mawazo, maono na fikra za ndani zinapoelezwa kwa muhutasari wa ushairi huvuta moyo kwa namna ya ajabu.
Katika fasili ya Shaban Robert anasisitiza kuwa shairi lazima liwe na urari wa vina na mizani na hutumia maneno machache yenye ufasaha. Pia anadai kuwa mtu anaposoma shairi huguswa ndani ya moyo kutokana na lugha ilivyotumika kwenye shairi hilo.
Kwa mujibu wa Abdilatifu Abdalah (2003) anafasili Ushairi kuwa ni utungo ambao katika kila ubeti wake kuna ulinganifu wa vina vitukufu vilivyopangwa kimoja badala ya chenzie wenye vipande vilivyo na ulinganifu wa mizani zisizopungufu wala zilizozidi. Vipande hivyo viwe vimetandwa na maneno ya mkato maalumu na lugha nyoofu, tamu na laini, lugha ambayo ni telezi kwa ulimi kwa kuitamka, lugha ambayo ina uzito wa fikra, tamu kwa mdomo na yenye kuathiri moyo uliokusudiwa na kama ulivyokusudiwa.
Hivyo Abdilatifu kama mtaalamu wa kimapokeo pia anasisitiza kuwa shairi huwa na ulinganifu wa vina na mizani, pia anasisitiza kuwa shairi lazima liwe tamu na utamu huo hutokana na maudhui yaliyopo kwenye shairi lenyewe.
Mathias Mnyampala (1970) anafasili Ushairi kuwa ni maneno yenye hekima tangu kale, ndicho kitu bora sana katika maongezi ya dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari na vina maalumu kwa shairi.
Anasisitiza katika urari wa vina na mizani huku akiegemea kwenye maneno yenye hekima yenye lugha ya mkato na lugha nzito zenye kunata. Maneno yenye hekima ni maneno yenye kufundisha, kuasa, kuonya na kuburudisha jamii. Lugha nzito ni lugha ambayo hutumia misemo, nahau, tamathali za semi katika kufikisha ujumbe.
Kwa mujibu wa Amri Abeid (1996) anafasili Ushairi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana. Tunaona kuwa mtaalamu huyu msisitizo wake mkubwa katika Ushairi ni uimbikaji wa shairi kuwa kama shairi haliimbiki basi shairi hilo halina maana kabisa.
Mathalani wanausasa pia wamefasili maana ya Ushairi na kuonyesha msisitizo pamoja na tofauti katika maana zao kama ifuatavyo.
E. Kezilahabi (1975) anadai kuwa Ushairi ni tukio au wazo ambalo limeonyeshwa kutokana na upangaji mzuri wa maneno ya ili kuonyesha ukweli fulani wa maisha. Hivyo tunaona kuwa msisitizo wake mkubwa uko katika maudhui ambayo yanaonesha uhalisia Fulani wa maisha. Pia anasisitiza katika upangaji mzuri wa maneno.
Kwa mujibu wa Mulokozi (1976) anafasili Ushairi ni mpangilio maalumu wa maneno fasaha yenye muwala, kuwa lugha ya mkato katika usemi, maandishi au mahadhi ya wimbo ili kueleza wazo au mawazo, kufunza au kueleza jambo au hisi Fulani kuhusu maisha ya binadamu kwa njia inayoburudisha na kugusa moyo.
Tunaona kuwa msisitizo wa Mulokozi katika fasili yake uko kwenye kufundisha watu na kuburudisha watu. Pia anasisitiza kuwa shairi hugusa moyo kutokana na maudhui au mambo yanayozungumzwa na kuamsha hisia.
Kwa mujibu wa Wamitila (2010) anafasili shairi kuwa ni utungo wa sanaa ya lugha na mpangilio maalumu wa mishororo au wa kisauti na kwa maneno mateule kwa kutumia mbinu za kibalagha na kimtindo zinazomwezesha mtunzi kuwasilisha ujumbe kwa ufupi na kwa mkokotozo mkubwa unaoeleza kisa, hisia, tukio au hali kwa lugha ya mvuto.
Tunaona kuwa katika fasili ya Wamitila anasisitiza zaidi katika vipengele vya fani na maudhui kwani utumiaji wa lugha zenye mnato na mbinu nyingine ni sehemu ya vipengele vya fani na maudhui. Pia anadai kuwa shairi hutumia lugha ya mvuto ili kuweza kumvutia msomaji.
Pia Njogu na Chimera (1999) wanafasili Ushairi kuwa ni sanaa ya lugha inayoeleza jambo kwa njia ya mkato na kwa namna inavyoteka hisia za msomaji au msikilizaji. Hivyo tunaona kuwa wataalamu hawa wanasisitiza katika usanaa wa lugha kwenye Ushairi na utekaji hisia na lugha ya mkato katika Ushairi.
Ingawa wataalamu wa ushairi wamefasili maana ya ushairi kwa msisitizo, pia washairi wanatofautiana katika vipengele au mambo mbalimbali yanayohusu ushairi. Yafuatayo ni mambo mengine yanayohusu ushairi;
Muktadha.
Kwa mujibu wa Wamitila (2010) Muktadha ni kipengele kinachosaidia kufasili maana ya ushairi, maana ya ushairi inaweza kutazamwa kwa kuchunguza muktadha wa wasomaji, wakati au eneo na mwandishi au kazi yenyewe ya fasihi. Muktadha huo huo unaweza kuwa asili ambao ni wa kiusemaji au muktadha pokezi ambao ni wa kulipokea tamko ni wa kuipokea tamko. K-Marx na Georg Lukas wanasema kuwa maana ya kazi ya kifasihi lazima itilie maanani uhalisia wa kijamii. Mfano mabadiliko ya kijamii, mivutano ya kitabaka, mifumo ya uzalishaji mali na mivutano ya kihistoria. Muktadha wa ushairi umegawanyika katika sehemu tatu, kuna muktadha wa mahali huu unaonyasha mabadiliko ya mahali au mazingira. Mfano kuna ushairi uliotungwa kabla ya wakoloni, kipindi cha ujima, wakati wa ukoloni na ushairi uliotungwa kipindi cha harakati za kupigania uhuru. Pia kuna muktadha wa mahusiano kibinasfi huu unaelekeza kwenye wahusika wa utungo maalum. Utungo wa kishairi unaweza kuangalia matumizi ya nafsi yaani inaweza kuwa nafsi ya kwanza au ya tatu.
Muktadha mwingine wa ushairi ni wa kimwingiliano matini huu unavuka mpaka wa ushairi mmoja maalum na kuhusisha muktadha wa shairi au utungo mwingine ambao unadokezwa au kuelekezwa kwa njia moja au nyingine katika shairi linalohusika. Muktadha wa kimwingiliano matini unapanua muktadha finyu wa ushairi na kuonyesha jinsi ambavyo shairi lililotangulia kwa kukamilishana, kujihusisha kwenye usemezano wa aina fulani au hata kuukana au kuukanusha mwelekeo, mtazamo na mwonoulimwengu wake.
Utamaduni.
Ni kipengele kingine kinachoelezea ushari, wataalamu wengi wa ushairi wameelezea utamaduni au asili ya ushairi. Mfano Knappert (1979) “Four centuries of Swahili verse” anasema; ushairi wa Kiswahili ulichipuka kutokana na nyimbo na ngoma za waswahili na ulianza katika karne ya 17. Na Jumanne, M. N (1993) anasema ushairi umetokana na jamii ya wanadamu wenyewe na umesheheneza ukwasa mkubwa wa lugha ambayo imekuwa ikitumika tangu enzi za kuishi mapangoni, enzi za ujima, uvamizi wa wakoloni na harakati za kupigania uhuru. Pia kwa mujibu wa Senkoro (1987) anadai kuwa Ushairi asili yake ni watu wa pwani.
Msisitizo
Ni kipengele kinachoelezea ushairi. Wataalamu wengi wa ushairi wa kimapokeo wanasisitiza matumizi ya vina na mizani na wanamamboleo wanasisitiza kuwa shairi lazima liimbike. Pia wanazuoni wa kimapokeo na wanamamboleo, mfano Shaaban Robert (1958), Topani (1974) na Kahigi (1982) wote wanasisitiza kuwa ushairi lazima uilenge jamii kwa kuibuia hisia za jamii hiyo husika.
Kanuni
Wanamapokeo wao wamejikita katika kufuata kanuni na sheria za ushairi. Mfano Shabaan Robert (1968) anasisitiza katika kufuata urali wa vina na mizani huku wanausasa hawafuati kanuni hizo za utunzi wa mashairii. Mashairi ya kimapokeo yote yanazingatia kanuni za uandishi wa mashairi. Mfano matumizi ya urari wa vina na mizani, kuwepo na kina, bahari au mshororo. Mashairi ya kisasa hayazingatii kanuni hizi za matumizi ya vina na mizani bali yanaangalia matumizi ya arudhi yaani shairi ili liwe shairi lazima liimbike.
Kwa ujumla wataalamu wote wanamapokeo na wanamamboleo wanafanana katika maana zao za ushairi kwa kiasi fulani kwa kuwa wote wanasema kuwa shairi lazima liibue hisia kwa jamii husika na shairi lazima liimbike. Hivyo mashairi yawe ya kisasa au yakimapokeo ni mashairi tu kwa kuwa yote yanalenga kunufaisha jamii kwa lengo la kuelimisha jamii, kuburudisha jamii na kutunza amali za jamii.
MAREJELEO
Abeid, A. (1954). Sheria za Kutunga Mashairi na Diwani ya AMR. Nairobi: EALB.
Abdilatifu, A. (1973). Sauti ya Dhiki. Oxford London.
Kezilahabi, E. (1975). Ushairi wa Mapokeo na wa Wakati ujao. Katika Mbonde J.P 121-137
Knappert, J. (1979). Four centuries of Swahili Verse. Heinemann. London.
Mayoka, J.K. (1993). Mgogoro wa Ushairi na Diwani ya Mayoka. Ndanda Mission
Press.Tanzania.
Mulokozi, M.M. (1976). Fasihi ya Kiswahili. Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam. Dar-es-Salaam
Mnyapala, M. E. ( 1970). Ngonjera za Ukuta. Dar es Salaam: Oxford University Press.
Robert, S (1968). Kielelezo cha Insha. Nelson London.
Senkoro, F.E.M.K. (1987). Ushairi, Nadharia na Tahakiki. Dar-es-Salaam: DUP.
Topan,F. (1974). “Dibaji” katika Kezilahabi, ukurasa:x
Wamitila, K.W. (2010). Misingi ya Uchanganuzi wa Fasihi. Nairobi Kenya: Vide-Muwa.
|
|
|
SHAIRI-NJE ANAFATA NINI |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 03:28 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
1.Galacha si m'bashiri,kujua lilo yakini
Siuwezi utabiri,ukweli kuubaini
Imekuwa desturi,japo ni sumu ndoani
MKE WA MUME TAJIRI,NJE ANAFATA NINI?
2.Wingi wa nyumba magari,ndio wengi hutamani
Maisha ya kifahari,mke kwake burudani
Usishangae kiburi,pesa ni lugha laini
Mke wa mume tajiri,nje anafata nini?
3.Ukitazama uzuri,kasoro hauzioni
Hujinyunyiza uturi,tena ule wa thamani
Utamuhisi kigori,atokaye unyagoni
Mke wa mume tajiri,nje anafata nini?
4.Au ya mume shughuri,haimkidhi mbilini,
Ndo kuona afadhari,atafute afuheni
Hivi haoni hatari ,kwa ndoa kutothamini
Mke wa mume tajiri,nje anafata nini?
5.Wanavyoepwa fakiri,kwa yao maisha duni
Dharau kwao dhahiri,kutwa kushushwa thamani
Kumbe wamefanywa siri,ni ngumu kuibaini
Mke wa mume tajiri,nje anafata nini?
6.Nilisikia hodari,ndilo jina la utani
Nikawa natafakari,uhodari wao nini?
Hapo ndipo nikakiri,ndoa ziko mashakani
Nje mke wa tajiri,anafata kitu gani?
7.Mume aona shubiri,ndoa kutoitamani
Mbona yaliyo mazuri,mke hakosi nyumbani
Hubaki kutahayari,mapenzi ni kitu gani
Mke wa mume tajiri,nje anafata nini?
8.Ukiweza mshauri,atende lipi jamani
Chunga liwe ni la heri,mke atulie ndani
Mume ameshahiyari,kubwaga manyanga chini
MKE WA MUME TAJIRI,NJE ANAFATA NINI?
|
|
|
SHAIRI: MKE NA MUME |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 03:22 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
MUME:?
Mke wangu umenuna, nambie tatizo nini
Toka juzi nakuona, umechukia rohoni
Pia nikaona jana, umejawa kisirani
Mumeo furaha sina, kwa sababu yako hani
MKE:?
Ni kweli nimechukia, tena moyo waniuma
Mume wangu naumia, mpaka napata homa
Mambo ulonifanyia, nishachoka ninasema
Kila siku kuumia, bora nirudi kwa mama
MUME:?
Mke wangu we funguka, nijue tatizo nini
bado wanipa mashaka, Huongei kwa yakini
Sema nini unataka, nikupatie mwandani
Nieleze kwa hakika, nasikiza kwa makini
MKE:?
Sana nimevumilia, ila sasa nimechoka
Mume ninakuambia, unipe yangu talaka
Kutwa kukufumania, mpaka kwenye vichaka
Umempanda rukia, ukimwi ushauteka
MUME:?
Lini wewe umeona, ya watu unasikia
Mambo hayo mimi sina, elewa nayokwambia
Mke nakupenda sana, wengine napuuzia
Maneno yaso namana, watu wamekuletea
MKE:?
Usijifanye wajua, mimi mwenyewe naona
Mwajuma nae asia, mara mbili kwenye kona
Ashura pia maria, hao wote nimeona
Majumbani mwaingia, mimi chonjo najibana
MUME:?
Mke wangu nisikie, haya ninayoyasema
Wale sio wangu mie, wale ni wa bosi juma
Na simu tumpigie, asikie akisema
Chaji moja niletee, simu yangu imezima
MKE:?
Mda chaji nimeleta, mpigie huyo juma
Usije leta utata, mengi sana sitosema
Kitu kitakachofata, kunijua utakoma
Mbona simu inaita, hapatikani wasema
MUME:?
Tatizo ni mtandao, nielewe mke wangu
Nenda hata kalete, kibao niweke miguu yangu
Unisikie mwenzio, nalonena mke wangu
Hebu we achana nao, tulizana mke wangu
MKE:?
Kichwani unanipanda, mume wangu nakuona
Hata kama nakupenda, ila kwa sasa hakuna
Roho yangu ishapinda, ulofanya unakana
Mbali nawe nitaenda, daima hutoniona
SULUHISHO?
MUME:?
Mke wangu ninakili, hayo yote ulosema
Usemayo ni ya kweli, nimelala na fatuma
Zaidi ya mala mbili, nikalala na rehema
Mke wangu tafadhali, kwako naja nalalama
MKE:?
We mwanaume malaya, Mimi bora niondoke.
Huso umejaa haya, Sitaki nihudhunike.
Umenitenda vibaya, Acha peka niteseke.
We mwanaume m,baya, Nipe changu niondoke.
MUME:?
Mke wangu ninatubu, napiga magoti kwako.
Nimelipata jawabu, sitaenda michepuko
Nimejifunza adabu, mi nakupenda mwenzako
Mke wangu mtabibu, nisamehe mume wako
MKE:?
Sawa nimekuelewa, hayo yote yameisha
Nataka kuheshimiwa, tuanze upya maisha
Usije kushaiwishiwa, thamani ukanishusha
Wewe ndiyo maridhawa, mume wangu wa maisha
M W I S H O
Mtunzi:Sefu Makanyila
Location:Jaribu Mpakani-Kibiti
Mawasiliano:+255787 141414
|
|
|
SHAIRI : UJINGA |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 03:14 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
Si neno la kukataa, kiambwa ufanye zani,
Fikiri japo kwa saa, ukweli utabaini,
Kwa ikhiwani hukaa, ndiyo mwake maskani,
Nyumbanikwe ni kichwani, ujinga unapokaa.
Amepambwa insani, ujinga pambo ajaa,
Kwake haukosekani, aliyeumbwa khasaa,
Vipimo hatufanani, ujazo ulivyojaa
Ujinga unapokaa, nyumbanikwe ni kichwani,
Ulojaliwa karaa, muumbwa na Rahmani,
Haukwepi ujohaa, hata fani asheheni,
Mwanga ulipotangaa, aweza kuwa haoni,
Nyumbanikwe ni kichwani, ujinga unapokaa.
Usipate usononi, ukaingiwa kilaa,
Ni kifunguzi cha mboni, ukinenwa ukatwaa,
Kwetu sote mtihani, hako wa kusema laa,
Ujinga unapokaa, nyumbanikwe ni kichwani,
Ambaye hajaukwaa, atokeze hadharani,
Bali tutamshangaa, kuwa na kichwa mwilini,
Ni sawa na motokaa, iliyokosa sukani,
Nyumbanikwe ni kichwani, ujinga unapokaa.
Natamatisha mneni, neno lifae asaa,
Hili msifanye deni, mkanilipa mawaa,
Ningalimo ujingani, ila shikeni makaa,
Ujinga unapokaa, nyumbanikwe ni kichwani.
MKANYAJI
HAMISI A.S KISSAMVU
? 0715311590
kissamvujr@gmail.com
kutoka (Baitu shi’ri)
MABIBO * DSM.()
|
|
|
UTENZI: KAMARI |
Posted by: MwlMaeda - 11-11-2021, 12:18 PM - Forum: Ushairi
- No Replies
|
|
1. Kamari jama kamari,
sione kama futari
kiliwa watahayari,
soni kukaba kabari,
2. Chezao fanya uradi,
tena kwao uradidi,
nasema siyo mradi,
nini mwazidi kaidi?,
3. Kamari tengewa muda,
sidandie kama uda,
taishia kula bada,
kuisahau ibada,
4. Kamari siyo waridi,
wala si maji baridi,
wajiona maridadi,
umeitoa burudi,
5. Mawazo tele kichwani,
huna moja akilini,
waiona kichaani,
meangukia mibani,
6. Wengine sema kubeti,
nani alowapa vyeti,
mwaiharibu bajeti,
kamari yashika chati,
7. Yaidumaza akili,
yaiondoa fasili,
na wengi wananakili,
mwisho waanguka chali,
8. Kamari kwako kificho,
kwa chote ukipatacho,
kipi kisikitishacho,
na umechagua hicho!,
9. Mekuwa kama kisiki,
kipata ishi mikiki,
ya muda hiyo kikiki,
kamari siyo rafiki,
10. Kamari ni uzandiki,
na tena siyo stahiki,
ladhaye isimuliki,
sijipe hatimiliki,
11. Kamari kwako habiba,
tena inazidi haba,
kama madini ni shaba,
mebeba kama mkoba,
12. Imekuwa sandarusi,
ijulikani nyeusi,
mbona mwaona wepesi,
kupata kwa ukakasi,
13. Panue yenu mawazo,
gitaa na micharazo,
yatupeni ya uwozo,
fuateni miongozo,
14. Mnavyo vingi vipaji,
lukuki kama vijiji,
iendea mifereji,
twamsahau Mpaji,
15. Tena hina kamandoo,
na huwezi jaza ndoo,
kakitafute kioo,
usije jibana koo,
16. Umeifanya koongo,
tena yazidi korongo,
ninakujuza ni fyongo,
hebu tumia ubongo,
17. Na uutoe utongo,
kwa huu wangu utungo,
uufungue mlango,
itafute yako wengo,
©Mary G. Marcus, 2019
Mbezi Louis,
Dar Es Salaam
Email: marymarcusg@gmail.com
|
|
|
|