SHAIRI: HAMUNISHINDI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: HAMUNISHINDI (/showthread.php?tid=1466) |
SHAIRI: HAMUNISHINDI - MwlMaeda - 11-11-2021 HAMUNISHINDI Mkusanyike makundi, Wa Bara na Visiwani, Mje pia na mafundi, Wa Lamu na Mombasani, Juweni hamunishindi, Kwa uwezo wa Manani, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Machagina toka Lindi, Na wa Tanga Ngamiani, Mje na wenu ufundi, Wa sasa na wa zamani, Haitokwisha raundi, Mtakuwa taabani, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Nawataka wa Malindi, Muulete ushindani, Mchinje na wenu bundi, Mlopawa ugangani, Mtaishia stendi, Mzikwe ughaibuni, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Wakongwe kwenye vilindi, Mtambao baharini, Walimu wenye vipindi, Vyuoni na mashuleni, Mfike na zenu tendi, Ninawangoja dimbani, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Taslimu siyo hundi, Nawapa zipokeeni, Mnausaka ushindi, Kwa nguvu ziso kifani, Taishia kwenye lindi, Musitoke maishani, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Ushairi siyo ndondi, Ama gozi uwanjani, Kwa maguvu hauendi, Hata uwe Tysoni, Ndiyo ma’na hampandi, Tungo hazitaki kani, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. Si shairi si utendi, Nawashinda hini fani, Hata kama hampendi, Mpawa hawezekani, Hapa mwisho mbele sendi, Tukutane ulingoni, Nawaita uwanjani, Nione wenu ufundi. 9Machi2017Alhamis13: 11am Jina la mtunzi: Dotto Rangimoto Lakabu JiniKinyonga. Simu: 0762845394 |