SHAIRI-NJE ANAFATA NINI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI-NJE ANAFATA NINI (/showthread.php?tid=1462) |
SHAIRI-NJE ANAFATA NINI - MwlMaeda - 11-11-2021 1.Galacha si m'bashiri,kujua lilo yakini Siuwezi utabiri,ukweli kuubaini Imekuwa desturi,japo ni sumu ndoani MKE WA MUME TAJIRI,NJE ANAFATA NINI? 2.Wingi wa nyumba magari,ndio wengi hutamani Maisha ya kifahari,mke kwake burudani Usishangae kiburi,pesa ni lugha laini Mke wa mume tajiri,nje anafata nini? 3.Ukitazama uzuri,kasoro hauzioni Hujinyunyiza uturi,tena ule wa thamani Utamuhisi kigori,atokaye unyagoni Mke wa mume tajiri,nje anafata nini? 4.Au ya mume shughuri,haimkidhi mbilini, Ndo kuona afadhari,atafute afuheni Hivi haoni hatari ,kwa ndoa kutothamini Mke wa mume tajiri,nje anafata nini? 5.Wanavyoepwa fakiri,kwa yao maisha duni Dharau kwao dhahiri,kutwa kushushwa thamani Kumbe wamefanywa siri,ni ngumu kuibaini Mke wa mume tajiri,nje anafata nini? 6.Nilisikia hodari,ndilo jina la utani Nikawa natafakari,uhodari wao nini? Hapo ndipo nikakiri,ndoa ziko mashakani Nje mke wa tajiri,anafata kitu gani? 7.Mume aona shubiri,ndoa kutoitamani Mbona yaliyo mazuri,mke hakosi nyumbani Hubaki kutahayari,mapenzi ni kitu gani Mke wa mume tajiri,nje anafata nini? 8.Ukiweza mshauri,atende lipi jamani Chunga liwe ni la heri,mke atulie ndani Mume ameshahiyari,kubwaga manyanga chini MKE WA MUME TAJIRI,NJE ANAFATA NINI? |