SHAIRI: MKE NA MUME - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: SHAIRI: MKE NA MUME (/showthread.php?tid=1461) |
SHAIRI: MKE NA MUME - MwlMaeda - 11-11-2021 MUME:? Mke wangu umenuna, nambie tatizo nini Toka juzi nakuona, umechukia rohoni Pia nikaona jana, umejawa kisirani Mumeo furaha sina, kwa sababu yako hani MKE:? Ni kweli nimechukia, tena moyo waniuma Mume wangu naumia, mpaka napata homa Mambo ulonifanyia, nishachoka ninasema Kila siku kuumia, bora nirudi kwa mama MUME:? Mke wangu we funguka, nijue tatizo nini bado wanipa mashaka, Huongei kwa yakini Sema nini unataka, nikupatie mwandani Nieleze kwa hakika, nasikiza kwa makini MKE:? Sana nimevumilia, ila sasa nimechoka Mume ninakuambia, unipe yangu talaka Kutwa kukufumania, mpaka kwenye vichaka Umempanda rukia, ukimwi ushauteka MUME:? Lini wewe umeona, ya watu unasikia Mambo hayo mimi sina, elewa nayokwambia Mke nakupenda sana, wengine napuuzia Maneno yaso namana, watu wamekuletea MKE:? Usijifanye wajua, mimi mwenyewe naona Mwajuma nae asia, mara mbili kwenye kona Ashura pia maria, hao wote nimeona Majumbani mwaingia, mimi chonjo najibana MUME:? Mke wangu nisikie, haya ninayoyasema Wale sio wangu mie, wale ni wa bosi juma Na simu tumpigie, asikie akisema Chaji moja niletee, simu yangu imezima MKE:? Mda chaji nimeleta, mpigie huyo juma Usije leta utata, mengi sana sitosema Kitu kitakachofata, kunijua utakoma Mbona simu inaita, hapatikani wasema MUME:? Tatizo ni mtandao, nielewe mke wangu Nenda hata kalete, kibao niweke miguu yangu Unisikie mwenzio, nalonena mke wangu Hebu we achana nao, tulizana mke wangu MKE:? Kichwani unanipanda, mume wangu nakuona Hata kama nakupenda, ila kwa sasa hakuna Roho yangu ishapinda, ulofanya unakana Mbali nawe nitaenda, daima hutoniona SULUHISHO? MUME:? Mke wangu ninakili, hayo yote ulosema Usemayo ni ya kweli, nimelala na fatuma Zaidi ya mala mbili, nikalala na rehema Mke wangu tafadhali, kwako naja nalalama MKE:? We mwanaume malaya, Mimi bora niondoke. Huso umejaa haya, Sitaki nihudhunike. Umenitenda vibaya, Acha peka niteseke. We mwanaume m,baya, Nipe changu niondoke. MUME:? Mke wangu ninatubu, napiga magoti kwako. Nimelipata jawabu, sitaenda michepuko Nimejifunza adabu, mi nakupenda mwenzako Mke wangu mtabibu, nisamehe mume wako MKE:? Sawa nimekuelewa, hayo yote yameisha Nataka kuheshimiwa, tuanze upya maisha Usije kushaiwishiwa, thamani ukanishusha Wewe ndiyo maridhawa, mume wangu wa maisha M W I S H O Mtunzi:Sefu Makanyila Location:Jaribu Mpakani-KibitiĀ Mawasiliano:+255787 141414 |