UTENZI: KAMARI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6) +---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50) +---- Thread: UTENZI: KAMARI (/showthread.php?tid=1459) |
UTENZI: KAMARI - MwlMaeda - 11-11-2021 1. Kamari jama kamari, sione kama futari kiliwa watahayari, soni kukaba kabari, 2. Chezao fanya uradi, tena kwao uradidi, nasema siyo mradi, nini mwazidi kaidi?, 3. Kamari tengewa muda, sidandie kama uda, taishia kula bada, kuisahau ibada, 4. Kamari siyo waridi, wala si maji baridi, wajiona maridadi, umeitoa burudi, 5. Mawazo tele kichwani, huna moja akilini, waiona kichaani, meangukia mibani, 6. Wengine sema kubeti, nani alowapa vyeti, mwaiharibu bajeti, kamari yashika chati, 7. Yaidumaza akili, yaiondoa fasili, na wengi wananakili, mwisho waanguka chali, 8. Kamari kwako kificho, kwa chote ukipatacho, kipi kisikitishacho, na umechagua hicho!, 9. Mekuwa kama kisiki, kipata ishi mikiki, ya muda hiyo kikiki, kamari siyo rafiki, 10. Kamari ni uzandiki, na tena siyo stahiki, ladhaye isimuliki, sijipe hatimiliki, 11. Kamari kwako habiba, tena inazidi haba, kama madini ni shaba, mebeba kama mkoba, 12. Imekuwa sandarusi, ijulikani nyeusi, mbona mwaona wepesi, kupata kwa ukakasi, 13. Panue yenu mawazo, gitaa na micharazo, yatupeni ya uwozo, fuateni miongozo, 14. Mnavyo vingi vipaji, lukuki kama vijiji, iendea mifereji, twamsahau Mpaji, 15. Tena hina kamandoo, na huwezi jaza ndoo, kakitafute kioo, usije jibana koo, 16. Umeifanya koongo, tena yazidi korongo, ninakujuza ni fyongo, hebu tumia ubongo, 17. Na uutoe utongo, kwa huu wangu utungo, uufungue mlango, itafute yako wengo, ©Mary G. Marcus, 2019 Mbezi Louis, Dar Es Salaam Email: marymarcusg@gmail.com |