Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 233 online users. » 0 Member(s) | 232 Guest(s) Bing
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
UHAKIKI WA TAMTHILIYA YA KWENYE UKINGO WA THIM |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 05:17 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
KITABU: KWENYE UKINGO WA THIM
MWANDISHI: IBRAHIM HUSSEIN
MCHAPISHAJI: OXFORD UNIVERSITY PRESS
MWAKA: 1988
UTANGULIZI
Kwenye Ukingo wa Thim ni tamthiliya inayoonesha na kuibua mgogoro uliopo katika hali halisi ya maisha. Mvutano uliopo baina ya mahitaji ya mila na ya kisasa (ukale na usasa) na maonevu yaliyopo-maonevu ya mwanamke na upendeleo wa mwanaume katika sheria za taasisi za utamaduni wa Mwafrika. Aidha mwandishi amenonesha jinsi mvutano huo unavyoleta athari katika jamii.
Maudhui
Dhamira Kuu: Ukombozi wa kiutamaduni
Katika kuijadili dhamira hii mwandishi anaonesha wazi kasoro zinazojitokeza katika utamaduni wa Kiafrika, kama asmeavyo katika utangulizi wake wa kitabu …
“Katika kutumia na kufasiri kipengele cha utamaduni wa Mwafrika kama nilivyofanya mimi katika mchezo huu nimehisi kuna wlakini”.
Walakini anaouzungumzia mwandishi katika utamaduni wa Mwafrika una athari mbaya kwajamii, kwani unasababisha mvutano kati ya ukale na usasa ambao ndicho kiini cha tamthiliya hii.
Ndoa ya Herbert na Martha ambao wameoana watu wa kabila tofauti imechangia kwa kiasi kikubwa juu ya mvutano huu. Jamii nyingi za Kiafrika, mila na desturi zao haziruhusu mwanamke kuolewa au mwanaume kuoa njeya kabila lake. Kutokana na mila hizi kushikiliwa na jamii zetu za Kiafrika, inazua mvutano kati ya vijana na wazazi. Vijana hawaoni sababu inayowazuia kuoa au kuolewa na mtu asiye wa kabila lake wakati wao wanapendana. Kwa upande mwingine mvutano huu umechangiwa na mabadiliko ya jamii kiuchumi, kiasia na kiutamaduni na mabadiliko haya hayajawakumba wazee ambao hayo ndio wanaoshikilia mila hizo zilizopitwa na wakati. Vijana wanaona mabadiliko hayo ni mkombozi kwa upande wao juu ya mila na desturi hizo kama anavyosema Lydia;
“Ndiyo ukweli wenyewe siku hizi mambo ya kisasa. Kila kitu cha kisasa. Mtazame Herbert au Martha. Hii habari ya kuoana kabila moja imekwisha kila unayemuona hivyo hivyo hata Chris” (Uk. 9).
Hivyo mwandishi anaonesha kuwa ili tujikomboe kiutamaduni lazima tufutilie mbali mila kama hizo, kwani zimepitwa na wakati. Hazina nafasi katika kizazi hiki. Masuala ya ndoa yaamuliwe na wale wanaopendana na sio mila na desturi za jamii. Athari hii ya kushikilia ukale kwa upande mwingine hata kwa wasomi haifai kwa kumtumia mhusika Ben, ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu, anaamini kuwa mke wa kweli lazima awe ni wa kutoka kabila lako. Haya yanadhihirishwa wazi na mazungumzo ya Ben na Herbert juu ya ndoa ya Herbert na Martha (uk. 11).
Ben: “Toka huyo mke ameolewa na wewe mimi simjui kama dada yangu labda ni bibi yako tu”
Herbert: “Wewe huoni aibu kuwa mkabila…..wewe umesoma halafu bado mkabila kiasi hicho”
Ukabila unapoota mizizi katika jamii una athari zake kama vile kuuana hovyo kama ilivyotokea Burundi na Rwanda. Na ni kutokana na ukabila huo ndio unaosababisha kifo cha Herbert (uk. 14).
Kwa upande mwingine mwandishi anaonesha kuwa, utamaduni wa Mwafrika unamgandamiza na kumuonea mwanamke. Utamaduni huo unamnyima haki za kuamua mambo yake mwenyewe, unamnyima haki ya kurithi mali alizochuma na bwana wake anapokufa. Mwandishi katika utangulizi wake anasema kuwa mwanamke anaonewa na taasisi za utamaduni wa Mwafrika.
Vilevile mwandishi anaonesha kuwa, baadhi ya watu hasa waliosoma na kubahatika kupata kazi mijini wanasahau vijijini kwao ambako walizaliwa. Mfano halisi ni Herbert ambaye baada ya kupata kazi mjini alisahau kabisa kijijini kwao kiasi cha kushindwa hata kujenga nyumba au kibanda cha kujisetiri kama asemavyo mwandishi (uk. 17);
Mzee: “Herbert alikuwa mtu mjinga hakuwa mwerevu, si vizuri kusema maiti kwa vibaya lakini Herbert aliishi chini ya matakwa ya mkewe hata kibanda kimemshinda kujenga?”
Lydia: “Kwa nini Herbert hakujenga kibanda?”
Mzee: “Dharau….!”
Hii si tabia ya Herbert tu katika jamii yetu. Tunao watu wa namna hii ambao hawataki kurudi kwao kwa ajili ya anasa na starehe za mjini (Rejea Mtawa Mweusi na Ngugi wa Thiong’o).
Dhamira Ndogondogo
Nafasi ya mwanamke katika jamii
Katika tamthiliya hii mwanamke anaoneshwa kwa pande mbili. Kwanza kama mwanamapinduzi na pili kama kiumbe duni anayeonewa na kunyanyaswa na mwanaume.
Mwanamke kama mwanamapinduzi ameoneshwa jinsi Martha alivyoshiriki vita vya msituni vya Mau Mau huko Kenya bega kwa began a wanaume katika kuutokomeza ukoloni wa Kiingereza nchini Kenya (uk. 26). Mwanamke kama kiumbe duni ameoneshwa jinsi sheria za taasisi za utamaduni wa Mwafrika zinavyomwonea na kumgandamiza mwanamke. Sheria hizo zinamnyima haki anayotakiwa kupata kama mke. Mwandishi anaonesha wazi kuwa mwanaume anapendelewa na mwanamke anaonewa na kunyanyaswa na sheria hizo. Anasema hivi…. (uk. 30)
“Mwanamke utakuwa na pesa uliyopata kwenye kibarua na kufunga ndoa na kuanzisha familia….ukipatana na mme basi hiyo ni bahati yako……”
Hapa mwandishi anaonesha kuwa, mwanamke ananyanyashwa juu ya hata kile alichonacho mwenyewe. Hali hii ipo katika utamaduni wetu wa Kiafrika ambao mwandishi anaona una walakini. Vilevile mwandishi anaonesha kuwa, wanaume wana uhuru wa kufanya jambo lolote watakalo bila kipingamizi. Ana uwezo wa kutafuta mke mwingine kijana zaidi, anakwenda kilabuni na mwenzie bila matatizo yoyote. Lakini mwanamke kufanya hivyo hawezi kwa sababu ya sheria zilizopo. Martha anasisitiza hivi (uk. 30)….
“Kwa mwanaume mambo ni rahisi ndani ya nyumba hayamwelemei…..mwanamke kufanya hivyo ndio mwanamke kupewa talaka jina baya! Unaona?”
Hapa mwandishi anaonesha wazi jinsi wanawake wanavyonyimwa uhuru wao wa kufanya mambo watakayo wenyewe. Hili ni zao halisi la maisha ya jamii nyingi zenye mwenendo na taratibu za namna hiyo za kumwonea, kumgandamiza na kumnyanyasa mwanamke. Licha ya hiyo, mwandishi pia anaonesha jinsi mwanamke anavyonyimwa haki ya kurithi mali waliyochuma na mumewe pindi bwana wake anapoaga dunia. Hii inadhihirishwa wazi jinsi Martha alivyolazimishwa kutoa kila kitu kwa George na Umma Klan baada ya mume wake kufa. Mwandishi anasema (uk. 25)…
“Basi baba yako katuachia kichwa cha tembo. Tumewinda pamoja…..unavyotuona hapa sisi ni maskini…..unapoteza mume, maisha na kila kitu!”
Mwandishi anaonesha kuwa, mwanamke anapofiwa na mume wake anapoteza kila kitu cha mume wake. Martha alikataliwa kumzika mume wake Herbert kwa madai kuwa yeye ni mwanamke. Mila na desturi za Kiafrika zinamnyima haki mwanamke hata kama vyombo vya sheria vimeamua (uk. 23). Ili kujikomboa kiutamaduni mwandishi anaonesha kuwa jamii haina budi kutupilia mbali baadhi ya mila hizo zinazomnyanyasa, kumuonea na kumgandamiza mwanamke.
Malezi
Malezi ni dhamira mojawapo inayojitokeza katika tamthiliya hii. Mwandishi anaonesha kuwa malezi mabaya yana athari mbaya hapo baadaye kwa wanaohusika.
Malezi aliyopewa Chris na baba yake wa kumlea, Herbert, bila kumwambia baba yake halisi ni kinyume na taratibu za malezi bora kwa watoto. Martha na Herbert hawakumfahamisha Chris ukweli wa mambo ulivyo hadi anakuja kujua kuwa Herbert sio baba yake baada ya kifo cha Herbert. Hali hii ilitaka kuzua mvutano kati ya Chris na mama yake Martha (uk. 24-25).
Vilevile kitendo cha baba na mama kucheza kwa kukumbatiana mbele ya watoto wao ni kinyume na desturi za Kiafrika. Huo ni mwigo kutoka kwa wageni ambao unazidi kushamiri katika jamii yetu. Mwandishi anatutahadharisha kuwa, hali hii ina athari kubwa kwa malezi ya watoto wetu kwa sababu tunawafundisha watoto mambo ya kigeni badala ya kuwafundisha utamaduni wetu (uk. 12).
Ndoa
Katika kujadili dhamira hii mwandishi ameonesha wazi jinsi mila na desturi za Kiafrika zilivyo na athari mbaya katika suala la ndoa. Vijana wengi wanashindwa kuoa/kuolewa kutokana na sheria mbalimbali zinazowazuia vijana, ambazo zimekumbatiwa na jamii zetu nyingi.
Mfano mzuri ni ndoa ya Herbert na Martha ambao walioana kutoka kabila tofauti. Hii iliwafanya watengwe na jamii yao kwa madai kuwa wamekiuka taratibu za jamii kama anavyosema Martha (uk. 26-27);
“Jamaa zangu damu moja walinitenga siku ya ndoa. Ben peke yake ndiye aliyekuwa na mimi; jamaa za mume wangu pia walinitenga siku hiyo…..”
Katika dondoo hii, mwandishi anaonesha kuwa, baadhi ya mila zinawanyima vijana uhuru wa kuamua ni nani awe mke au mume. Na hii ina athari zake kwa jamii, kwani mara nyingi inazua mvutano kati ya ukale na usasa.
Mwandishi anapendekeza kuwa ili kujikomboa kiutamaduni lazima tutupilie mbali baadhi ya mila hizo ili kuwapa vijana uhuru wa kuchagua wenzi wao wanaowapenda wenyewe. Vijana wakipewa uhuru huo itazuia kutokea kwa mivutano baina ya wazee na vijana. Mawazo haya yanajadiliwa pia na A.J Safari katika Harusi, H. Mwakyembe katika Pepo ya Mabwege, N.Balisidya katika Shida na E. Hussein katika Wakati Ukuta, n.k.
Dhana potofu
Kuna baadhi ya watu wana dhana potofu akilini mwao kuhusu uonevu na unyanyasaji wa akina mama katika jamii. Mojawapo ya dhana hii potofu inatokana na imani kuwa uonevu na unyanyaswaji wa akina mama ni mpango wa Mungu. Hali hii inadhihirishwa wazi na mazungumzo ya Pasta na Martha (uk. 30-31).
Vilevile kuna wengine wanaamini kuwa hali zote za watu wawe matajiri au maskini ni mipango ya Mungu. Pasta anaonesha kuwa utajiri wa Martha na Herbert ni Mungu kawapa na hata baada ya Martha kupokonywa kila kitu na George pamoja na Umma Klan ni mipango ya Mungu, Pasta anasema (uk. 31);
“Unakumbuka uliponunua nyumba hii…..ulijiona umefika sasa……hii ni kazi ya Mungu ambayo haina makosa”
Mawazo kama hayo ni potofu na hayana ukweli wowote ndani yake. Mhusika anayetamka haya anaamini kuwa Mungu huwapendelea baadhi ya watu ili wawe matajiri na wengine masikini. Kwa ujumla, utajiri au umaskini hautoki kwa Mungu bali ni matokeo ya mfumo wa siasa wa jamii unaotawala jamii hiyo, ndiyo unaosababisha utajiri au umaskini wa mtu. Kwa upande mwingine. Pasta anaamini kuwa, kunyanyaswa na kuonewa kwa mwanamke ni maamuzi ya Mungu na mwanamke hawezi kutafuta suluhu bali ni kumwachia Mungu ambaye ndiye mwenye mipango yote, Pasta anasema (uk. 30);
“Wewe huwezi kujua la kufanya mwachie Mungu”.
Msanii anaitahadharisha jamii juu ya mawazo kama haya kuwa ni mawazo potofu. Vilevile anaonesha kuwa kunyanyaswa na kuonewa kwa mama kunatokana na sheria za taasisi za utamaduni wetu pamoja na mfumo wetu wa maisha unaomfunga mama kama kiumbe duni katika jamii. Msanii anaonesha kuwa ili kujikomboa kiutamaduni hatuna budi kufuta mawazo hayo, kwani hayana nafasi kwa jamii ya sasa.
Utekelezaji mbaya wa mipango ya maendeleo ya taifa
Licha ya kujadili dhamira ya ukombozi wa kiutamaduni, vilevile mwandishi anajadili juu ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya taifa.
Katika tamthiliya hii msanii anaonesha wazi jinsi viongozi wanavyopingana wao kwa wao juu ya utekelezaji wa maamuzi yanayohusu ujenzi wa taifa. Msanii anaonesha kuwa kiongozi fulani anaagiza wananchi wafanye kitu fulani na halafu kiongozi mwingine anakataza jambo hilo lisifanyike. Wananchi wanapoacha anakuja mwingine na kuwahimiza kufanya kitu hichohicho. Kutokana na hali hii viongozi wanaleta mkanganyiko kwa wananchi wakati wa utekelezaji wa mipango hiyo ya kimaendeleo (uk. 19-20). Hapo swali la kujiuliza ni kuwa, wananchi washike la nani na kuacha la nani? Hapo ndipo unapokuja mkanganyiko wa mawazo yanayokwamisha maendeleo ya jamii kwa ujumla. Na ni kutokana na hali hii ya viongozi wetu kupingana wao kwa wao ndiyo maana wanashindwa kuinua hali ya uchumi wan chi yetu na matokeo yake ni kudidimiza zaidi uchumi.
Migogoro - Mgogoro kati ya Herbert na George
- Mgogoro kati ya Martha na George (Umma Klan)
- Mvutano kati ya ukale na usasa
- Mgogoro kati ya Chris na Martha
Ujumbe
- Mabadiliko ya kiutamaduni ni lazima katika jamii nan i lazima yaende sambamba na mabadiliko ya jamii nzima kiuchumi na kisiasa
- Suala la ndoa ni jukumu la wale wanaopendana na sio la kulazimishana kwa kufuata kanuni na taratibu za mila, ambapo baadhi yake zimepitwa na wakati.
- Ukombozi wa mwanamke ni muhimu sana katika jamii, kwani mwanamke akijikomboa atathaminiwa na kupewa haki zote anazostahili.
- Baadhi ya mila za Kiafrika zimepitwa na wakati, hivyo jamii haina budi kutupilia mbali mila hizo.
- Mipango mizuri na utekelezaji mzuri wa mipango hiyo ni kichocheo cha maendeleo nchini.
Falsafa ya mwandishi
Mwandishi anaamini kuwa ili kujikomboa kiutamaduni ni lazima tufutilie mbali baadhi ya mila ambazo zimepitwa na wakati kama vile kumwona mwanamke kama kiumbe duni. Suala la ndoa kuachiwa wale wanaopendana na mawazo potofu juu ya kunyonywa na kuonewa kwa mwanamke kuwa ni mpango wa Mungu. Vilevile mwandishi anaamini kuwa mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji wake mzuri utaleta manufaa nchini.
Msimamo wa mwandishi
Mwandishi ana msimamo wa kimapinduzi, kwani anaonesha wazi kasoro mbalimbali zinazojitokeza katika utamaduni wetu wa Kiafrika na anashauri jamuu kuziondoa kasoro hizo kwani zinawanyanyasa na kuwaonea baadhi ya watu katika jamii hasa wanawake na vijana.
Fani
Muundo
Muundo wa tamthiliya hii ni wa moja kwa moja. Mchezo unaanza kwa kuonesha juu ya ndoa ya Herbert na Martha hadi vifo vya wote wawili na matokeo yake. Mchezo umegawanyika katika sehemu kuu nne na kila sehemu ina onyesho moja lenye kichwa cha habari. Mfano Onyesho la I Nyumba, Onyesho la II Nyumbani, Onyesho la III Chira, Onyesho la IV Msingi uliobomoka.
Mtindo
Mwandishi ametumia dayalojia (majibizano) katika tamthiliya hii, na nafsi zote tatu zimetumika katika mchezo huu.
Matumizi ya Lugha
Lugha iliyotumika ni ya kawaida yenye sentensi fupifupi na yenye mbinu mbalimbali za kisanaa.
Tamathali za semi
Tafsida
- Mwisho una chuma dhambi (uk. 30)
- Wakati walipomzika marehemu Martha alikuwa hayupo duniani, alikuwa ameshafariki (uk. 34)
Tashihisi - Vyura jana vilisema mvua inayokuja ni mvua ya rehema (uk. 22)
Mbinu nyingine za kisanaa
Takriri - Si rahisi Pasta! Si rahisi kwa mwanamke si rahisi hata kidogo (uk. 29)
- Hey! Shshshsh!toka.. Toka Elsa nje (uk. 1)
- Tegemea! Tegemea mti! Hivi tu utaanguka (uk. 19)
Mjalizo - Nataka pesa za ndoo mbili, mfagio, chumvi na mbao (uk. 19)
- Kila kitu nyumba, viwanja, gari, fanicha kila kitu (uk. 25)
Mdokezo - Huko siko…..na huko siko….siko kokote (uk. 25)
- Mwache aje hanijui mimi sini…. (uk. 9)
- Vilivyo shikamana vitakuwa vitapo…. (uk. 6)
Lugha ya Kishairi - Kwa kiasi kikubwa katika tamthiliya hii mwandishi ametumia lugha ya kishairi mfano (uk. 21-22, 30,34, n.k)
Vilugha - Vilevile mwandishi ametumia Kiswahili kisicho sanifu katika tamthiliya hii mfano (uk. 19, 20)
- Kutengeneza, itasikwa, mbovu, mujini, mutu mukubwa.
Wahusika
Herbert na Martha
Hawa ndio wahusika wakuu wa mchezo huu ambao maudhui yote yanawazunguka wao. Hawa ni mume na mke ambao kuoana kwao kumesababisha kutengwa na jamii, kwa sababu ya kuoana watu wa kabila tofauti. Herbert ni msomi ambaye ana kazi nzuri mjini na kutokana na kuathiriwa na kazi mjini anasahau kijijini kwao kiasi cha kutowatembelea ndugu zake.
Martha ni mke wake Herbert ambaye alipigana vita vya Mau Mau na baaba ya kifo cha mumewe ananyang’anywa kila kitu na Umma Klan kwa kisingizio cha kuwa yeye ni mwanamke ambaye hastahili kurithi chochote. Herbert na Martha ni mfano wa watu wanaopenda mabadiliko katika jamii nan i vielelezo vya watu wanaopinga ukabila katika jamii. Hivyo ni mfano bora wa kuigwa.
Chris
Ni mtoto wa Martha anayesoma Columbia (Amerika ya Kusini). Ni mtoto aliyetegemewa kuwa mrithi wa Herbert, lakini kutokana na kitendo cha kuwa mtoto wa nje anakosa urithi huo.
George
Huyu ni ndugu wa Herbert aliyemdhulumu Martha, shemeji yake, mali zote baada ya Herbert kufa. George ni kiwakilishi cha watu wanaoshikilia mila za kizamani zilizopitwa na wakati. Hivyo hafai kuigwa na jamii.
Lidya, Jean na Stella
Hawa ni wawakilishi wa vijana wa kike wanaoona umuhimu wa mabadiliko katika jamii hasa katika kipengele cha utamaduni. Hawa wako mstari wa mbele katika kufutilia mbali desturi zinazowagandamiza wanwake katika jamii.
Ben
Mwalimu wa Chuo Kikuu anayeshikilia ukabila katika jamii, Ben ndiye aliyesababisha kifo cha Herbert nan i mtu asiyefaa kuigwa.
Mandhari
Mandhari ya kitabu hiki ni nchini Kenya mjini na kijijini. Uthibitisho ni vita ya Mau Mau na ukabila ambao umekithiri nchini Kenya, na neno “chira” lenye asili ya Kijaluo kabila lililopo mpakani mwa Tanzania na Kenya. Vilevile kuna mandhari ya nyumbani, msituni wakati wa Mau Mau, barabarani, ofisini, mitaani, shuleni, n.k
Jina la Kitabu
Jina la kitabu Kwenye Ukingo wa Thim linasadifu yaliyomo ndani ya kitabu. Kwanza Thim kwa Kijaluo ni Msitu. Kitaswira Kwenye Ukingo wa Thim linaashiria kuwa ukingoni mwa msitu (mila na desturi zilizopitwa na wakati) kwa maana ya jitihada za jamii kutoka katika kifungo cha mila na desturi zilizopitwa na wakati. Vilevile inaashiria kuwa baadhi ya wahusika kama vile Herbert, Martha, Chris, Lydia, Jean na Stella nao wako pembeni mwa mila hizo.
Kufaulu kwa Mwandishi
Kimaudhui
Mwandishi amefaulu sana katika kuonesha kasoro mbalimbali zinazojitokeza katika jamii za Kiafrika kama vile kumwona mwanamke kama kiumbe duni katika jamii, kung’ang’ania ukabila na kupendelewa kwa wanaume katika jamii za Kiafrika.
Kifani
Mwandishi amefaulu pia kutumia lugha rahisi yenye sentensi fupifupi na yenye kueleweka. Ujenzi wa wahusika ameugawa katika pande mbili, wanaopenda mabadiliko na wasiopenda mabadiliko.
Kutofaulu kwa Mwandishi - Amechanganya lugha ya Kiingereza na Kiswahili; kwa mtu asiyefahamu Kiingereza atashindwa kupata ujumbe.
- Ameweka wahusika wengine ambao hawana umuhimu.
|
|
|
MBINU ZA KIFANI ZINAZOJICHOMOZA KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 05:07 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
MBINU ZA KIFANI ZINAZOJICHOMOZA KATIKA RIWAYA ZA KISWAHILI
Kwa kiwango cha kozi yetu, tutavidodosa vipengele vifuatavyo:
o Naratolojia (usimulizi, mwendo wa riwaya)
o Msuko wa vitushi na motifu
o Uhusika na wahusika
o Lugha
o Mianzo na miisho ya riwaya
Naratolojia
Ni taaluma inayohusu suala la usimuliaji katika kazi za kiuandishi. Hudokeza masuala muhimu yafuatayo:
o Usimulizi (aina, sehemu alipo msimuliaji n.k)
o Kuhusiana kwa vitushi na matukio (kusababisha, kuathiriana na kuendelezana).
o Suala la wakati/muda katika riwaya.
o Mwendo wa kazi husika.
Aina za Usimulizi katika Riwaya
Kuna aina kuu mbili za usimulizi. Nazo ni: Usimulizi shahidi (huitwa pia usimulizi wa nafsi ya kwanza) na Usimulizi maizi (huitwa pia usimulizi wa nafsi ya tatu).
Usimulizi Shahidi
Huwa na sifa zifuatazo;
o Hutumia nafsi ya kwanza.
o Huwa na umakinifu zaidi katika usimuliaji.
o Hudondoa yale yashuhudiwayo na mwandishi/msimuliaji tu.
o Hufaa zaidi katika kazi za kitawasifu na kazi za fasihi pendwa.
o Humrahisishia msomaji dhana ya masafa ya kiwakati na kijiografia katika kazi husika.
o Ni rahisi zaidi kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili.
o Dhana ya wakati huenda taratibu.
o Hujenga uhusiano wa karibu kati ya msomaji na kazi husika (msomaji huweza kujiona yu ahusika zaidi; hivyo, kuweza kwenda hatua kwa hatua samba na mapigo/mihemko ya kazi, hususan kama maudhui yenyewe ni chanya).
o Mwandishi hana uwezo wa kuona mambo yote kwa wakati mmoja. Hivyo, husimulia jambo hili kisha lile.
o Huibua kwa karibu kuwapo kwa dhana ya msimulizi ― mwandishi na/au mhusika msimulizi. Rejea usimulizi wa Willy Gamba katika NJAMA.
o Aina hii ya usimulizi huwa na athari kubwa sana kwa wasomaji (kutokana na ufupi wa masafa ya kijiografia na kiwakati).
Usimulizi Maizi
dhana ya umaizi humaanisha uwezo wa mtu kufahamu mambo mbalimbali, ya wazi na ya siri; tena kwa wakati mmoja. Katika uga wa kifasihi, dhana ya umaizi hutumiwa kumrejelea mtunzi/mhusika mwenye uwezo wa kuona, kufuatilia ma kufafanua mambo mbalimbali kwa wakati mmoja. Hata hivyo, ni vema dhana hii ya umaizi ikatazamwa kwa jicho hili tu la kifasihi. Hii kutokana na ukweli kuwa kwa hakika, dhana yenyewe inafungamana sana na uwezo wa KI―UUNGU (uwezo alionao MUNGU). Kuna ukinzani mkubwa wa kimantiki kuhusu usahihi na uwezekano wa utokeaji wake. Hivyo, umaizi unakubalika tu katika muktadha wa kifasihi kutokana na ukweli kuwa mtunzi hujua yote ayatungayo, hujua kila kitu kuhusu wahusika, mandhari n.k. kikubwa akifanyacho ni kuamua tu ni wakati gani (katika tukio/sura gani) na kwa namna gani ayatongoe matukio yake. Kwa hali hiyo, mtunzi huweza kuonekana kuwa ni mmaizi.
Sifa chomozi za Usimulizi Maizi
o Hutumia nafsi ya tatu.o Huwa na uhuru zaidi katika usimuliaji (huweza kuteua la kusimuliwa na lakuachwa).
o Humruhusu mtunzi kurukaruka katika usimulizi wake (huweza kusimulia hili mara lile).
o Huruhusu usimulizi wa hata mambo yasiyoshuhudiwa na mwandishi/msimuliaji.
o Hufaa zaidi katika kazi za kiwasifu.
o Dhana ya masafa ya kiwakati katika kazi husika huweza kukimbizwa au kurushwa―rushwa, kwa mfano usimulizi katika Kusadikika (rejelea suala la safari na umri wa wajumbe).
o Ni vigumu kupenyeza matumizi ya nafsi ya pili ikilinganishwa na usimulizi shahidi.
o Uhusiano kati ya msomaji na kazi husika huwa wa kando 9msomaji hujiweka kando), hivyo hufuatilia mtiririko mtiririko wa vitushi kwa utulivu na mtuo.
o Msimulizi huweza hata kuchupa hadi ndani ya fikra za watu na kutoa kifikiriwacho.
Vijitawi vya Usimulizi Maizi
Usimulizi maize huweza kufanywa kwa namna tatu ambazo ni: Usimulizi Penyezi, Usimulizi Tinde na Usimulizi Horomo.
(a) Usimulizi Penyezi: Ni Usimulizi ambao msimuliaji hujitokeza na hata wakati mwingine kuwashirikisha wasomaji. Huweza kusimulia kisha akajiingiza mwenyewe. Kwa mfano, “hata mimi niliona aibu, sijui wewe”.
(b) Usimulizi Tinde. Huu ni usimulizi ambao hutumia kaida za ki―hisia/ki―dhana. Huweza pia kuitwa kwa jina la usimulizi nusu―nusu au usimulizi shinda. Hii ni kutokana na hiyo hali ya msimulizi kutokuwa na hakika ya akisimuliacho. Aghalabu, hutumika katika vitushi vinavyotakiwa kutafuta jawabu/ufumbuzi wa utata fulani. Kwa mfano, vitushi vya riwaya pendwa 9hususan riwaya za kipelelezi).
© Usimulizi Horomo. Usimulizi wa kurukia―rukia matukio na miktadha tofauti. Usimulizi huu ndiyo unaoruhusu uchanganyaji wa matukio yanayosimuliwa. Ni kama vile mtunzi/msimulizi huwa juu akimulika matukio yatokeayo kote duniani na ndani ya akili za watu kisha kuyasimulia. Ni vigumu sana kwa mtunzi kutumia aina noja tu katuka kazi yake. Mtunzi huweza kuchanganya aina zote za usimulizi katika kazi yake. Hii itategeneana na msuko wa kazi yenyewe pamoja na malengo ya mtunzi.
Mwendo wa Riwaya
Maana
Dhana hii hurejelea suala zima la kasi, mtiririko na mshindilio wa usimulizi wa vitushi vya riwaya kwa kuzingatia vigezo vya Msuko, Maudhui, Masafa ya Kiwakati na Masafa ya Kijiografia. Suala hili la mwendo huuathiri usomaji na msomaji mwenyewe katika ujenzi wa uelewa. Riwaya huwa na viwango tofauti vya mwendo kutokana na kuwepo kwa tofauti katika usanaji wa vigezo vilivyotajwa hapo juu. Kuna zenye mwendo wa kasi, nyingine zina mwendo wa kati/wastani na nyingine zina mwendo wa polepole.
Riwaya zenye mwendo wa kasi ni zile ambazo mtunzi huzisana kwa namna ya kurusha matukio. Aghalabu, riwaya zenye maudhui ya kusisimua au kufurahisha huwa na mwendo wa kasi. Kwa upande mwingine, riwaya zenye maudhui ya kitanzi (ya kuhuzunisha) huwa na mwendo wa polepole. Riwaya zenye maudhui yenye mseto wa kusisimua au kufurahisha pamoja na kuhuzunisha huwa na mwendo wa wastani.
Kwa mfano, riwaya yaweza kusimulia habari za mtu aliyeko Tunduru; kisha mtu huyo hupanga safari ya kwenda Tanga. Katika riwaya yenye mwendo kasi, twaweza kumuona mtu huyo Tunduru kisha ghafla twaambiwa yuko Tanga. Bali kama mwendo wa riwaya ni wa wastani au polepole, tutaweza kuchanganua jinsi atakavyosafiri safari yake yote pamoja na misukosuko mingine ya safari atakayokumbana nayo.
Mifano ya riwaya zenye mwendo wa polepole ni: riwaya nyingi za Shaaban Robert na Kezilahabi kama vileKusadikika, Adili na Nduguze, Mzingire, Nagona, Uhuru wa Watumwa. Mifano ya riwaya zenye mwendo wa wastani ni: Utata wa 9/12. Mifano ya riwaya zenye mwendo wa kasi ni: riwaya pendwa nyingi, mfano, Njama.
Hitimisho kuhusu mwendo wa riwaya
Kwa jumla, riwaya za Kiswahili zimekuwa zikibadilisha miendo yake kulingana na maudhui ya nyakati mbalimbali. Mwendo wa riwaya nyingi za wakati wa vuguvugu la kudai uhuru ni wa polepole. Hii ni kwasababu ya maudhui yaliyotamalaki kwa wakati huo yalijaa huzuni na jitimai kwa kiasi kikubwa. Baada ya uhuru, mwendo wa riwaya ulibadilika kidogo, ulikuwa wa wastani kwa kuakisi maudhui na msuko. Mwendo wa kasi katika riwaya ulishamiri katika miaka ya 80 ambapo kulikuwa na riwaya zilizoiga kazi pendwa za magharibi. Hizi zililenga kusisimua na kuburudisha zaidi.
Mtagusano
Ni mwingiliano wa vipengele mbalimbali katika kazi ya fasihi. Kwa namna fulani, huweza kuhusishwa na kaida za mwigo au uathiriano. Twaweza kusoma kazi fulani ya fasihi na kuona kuwa ina mwingiliano mkubwa na kazi nyingine. Mtagusano au mwingiliano huo waweza kuchagizwa na hali ya kuiga au kuathiriwa. Mtagusano huweza kujidhihirisha kupitia maudhui (mwingiliano wa kaida za maisha ya watu au jamii tofauti), lugha, mandhari n.k. dhana hii inajitokeza sana katika riwaya za Kiswahili kutokana na sababu zifuatazo: mosi, ni waswahili kuwa na mwingiliano mkubwa na watu wa jamii nyingine, hali ambayo husababisha pia wanariwaya kusawiri maisha hayo ya kimwangiliano katika kazi zao. Pili, ni utandawazi. Kupitia maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia, dunia imedogoshwa na hivyo, kukuza mwingiliano wa wanaulimwengu.
Msuko wa vitushi katika riwaya za Kiswahili
Riwaya za Kiswahili zimekuwa zikitumia motifu za namna mbalimbali katika kuvisuka vitushi vyake. Motifu ni msuko au mwegamo mkuu autumiao mtunzi kujenga fani na maudhui alengayo kuyawasilisha. Yaani; kupitia motifu husika, sehemu kubwa ya mambo mengine kama vile maudhui na fani. Aghalabu, motifu katika kazi za fasihi huwa na mrudio wa kiwango kikubwa katika ujitokezaji wake; kiasi cha hata kuweza kuathiri fikra za msomaji au mhakiki kwasababu huweza kumeza kiini cha dhamira halisi.
Baadhi ya motifu maarufu zitumiwazo na waandishi wa riwaya ya Kiswahili ni:
o Mapenzi
o Safari
o U ― jini
o Mauaji
o Upelelezi
o Uhusika wa wanyama
o Usihiri (umazingaombwe)
o Ufutuhi (sherehe, raha na vichekesho)
o Utanzia (mateso, vifungo, mabaa/majanga kama vile njaa na ukame).
o Starehe (pombe, sigara, disko na kamari).
Riwaya za mwanzo zilitumia motifu ya safari katika kuvisuka vitushi vyake. Aghalabu, safari hizo zilihusisha bahari. Hivyo, motifu hizo ziliakisi pia misukosuko ya kibaharia. Mifano: riwaya za mwanzo za Shaaban Robert kama vile Adili na Nduhuze, Kusadikika. Pia Uhuru wa Watumwa. Riwaya nyingine zilitumia motifu ya u― jini au ki―jini. Hizi pia ziliakisi mazingira ya upwa wa bahari. Kama ilivyo kwa motifu ya safari, hii nayo ni miongoni mwa nduni za fasihi simulizi. Nduni nyingine maarufu ya fasihi simulizi ambayo inajitokeza katika vitushi vya riwaya za Kiswahili ni uhusika wa wanyama. Hali hiyo ya matumizi ya wahusika wanyama katika vitushi vya riwaya ni miongozi mwa ithibati ya kuwako kwa ufungamano wa karibu kati ya riwaya na fasihi simulizi; kwani hiyo ni kaida maarufu katika hekaya, visakale, visasili na ngano. Wanyama maarufu wajitokezao katika riwaya za Kiswahili hususani zile za mwanzo ni kama vile nyani (Adili na Nduguze), Paa (Nagona).
Mabadiliko makubwa ya msuko wa vitushi katika riwaya za Kiswahili yanadhihirika katika usahili na uchangamani wake. Dhana hii ya usahili na uchangamani wa vitushi yarejelea mpangilio wa vitushi vyenyewe katika kazi. Katika riwaya za mwanzo, kulikuwa na usahili. Kwa sasa, wasanii huviweka vitushi katika hali ya uchangamani. Riwaya pendwa, kwa upande wake, zilimezwa na motifu za mauaji, starehe, upelelezi na mapenzi.
Mianzo na miisho ya riwaya za Kiswahili
Mianzo
Namna mbalimbali za mianzo ya riwaya za Kiswahili:
o Ya kisira
o Ya kifomyula au kijadi au kihafidhina
o Ya kifalsafa
o Ya kifumbo
o Ya ki ― swali
o Ya kiufafanuzi
o Ya kimajazi
Miisho
Kwa upande wa miisho, riwaya nyingi za Kiswahili huwa na miisho ya:
o Kifomyula au kijadi
o Ya kifalsafa
o Ya kiutatuzi
Maelezo ya jumla kuhusu mianzo na miisho ya riwaya za KiswahiliKuna tofauti kubwa ya riwaya za mwanzo na za sasa. Zile za mwanzo ziliakisi kwa kiasi kikubwa mianzo ya nathari simulizi. Mianzo na miisho hiyo twaweza kusema ilichukua matumizi ya vifungu vya kifomyula. Dhana ya vifungu vya kifomyula hapa yamaanisha utunzi wa neno, tungo au aya kwa namna ya kuirudia katika kazi moja au miongoni mwa waandishi tofauti. Mathalani, kulikuwa na matumizi ya vifungu kama vile:
o Hapo zamani za kale, palikuwa na….(mianzo)
o Paukwa pakawa (mianzo)
o Hadithi hadithi (mianzo
o Na hadithi yangu yaishia hapo (miisho
o Waliishi raha mustarehe (miisho)
o Hatimaye alifanikiwa sana (miisho)Baadaye, mianzo na miisho ya hadithi ilibadilika. Mathalani, kukawa na mianzo ya ki ― taharuki, hususani katika riwaya ramsa. Hizi ni zile zinazotawaliwa na msisimko au burudani. Pia, riwaya za kifalsafa.Kuhusu miisho, ingawa wanariwaya waliowafuatia wale wa awali wamejikwepesha na miisho ya kifomyula; bado miisho yao inalandana kimaudhui. Hii ni kwa sababu, kwa jicho la jumla, riwaya nyingi bado zinaisha kwa namna ya kuonesha msfanikio. Mafanikio haya ni yale yatokanayo na mivutano baina ya ama ubaya na wema, ukale na usasa na kadhalika. Mathalani, katika Haini, twaona tutakosa, alifikiria, na kweli leo ametoka! Na hata hao waliobaki, pia watatoka tu! Alisema Hamza. (uk.267). Mwisho huu unamrejelea yuleyule mhusika mkee aliyedokezwa pia katika mwanzo wa kazi hiyo, Hamza.
MUELEKEO WA JUMLA JUU YA MAUDHUI YANAYOJICHOMOZA KATIKA RIWAYA YA KISWAHILI
Dondoo muhimu kuhusu mielekeo ya maudhui
Maudhui ya riwaya ya Kiswahili yalibeba mitazamo na mielekeo ya sera na mipango ya vipindi mbalimbali vilivyobeba mshindo wa fikra za Waswahili. Vipindi hivyo ni:o Kabla na wakati wa ukoloni (wakati wa vuguvugu la kudai uhuru)o Baada ya uhuru/wakati wa Azimio la Arushao Wakati wa vuguvugu la vijiji na vijiji vya ujamaao Wakati wa vita ya Kagerao Wakati wa didimio la uchumi wa duniao Wakati wa sera za mpango wa kuhuisha mfumo wa uchumi barani Afrika na Duniani.o Wakati wa vuguvugu la kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingio Wakati wa vuguvugu la utandawazi (ubinafsishaji)
Maudhui ya riwaya za Kiswahili kabla na wakati wa Ukoloni
Riwaya za Kiswahili kama mojawapo ya kazi za fasihi ya Afrika, zilikuwa na maudhui yaliyojaa manunguniko, jitimai na huzuni kutokana na hali halisi iliyokuwa inawakabili waafrika wengi. Katika wakati huu ndipo hasa yalipokuwa yanajidhihirisha maudhui yaliyolenga kuamsha urazini wa Waafrika kuhusu maovu waliyokwa wanatendewa. Aidha, maudhui yalikuwa yanawakumbusha kuhusu suala la ukombozi. Baadhi ya mifano ya riwaya zilizotungwa kabla ya uhuru ni: Uhuru wa Watumwa, Kusadikika, Kufikirika, Kasri ya Mwinyi Fuad n.k.
Maudhui ya riwaya za Kiswahili Baada ya Uhuru
Hapa, riwaya zilizotungwa zilibadili mkondo wa kimaudhui. Ziliwahimiza watu kuzijenga upya nchi zao na maisha yao kwa jumla. Aidha, kimaudhui zilichanganyika na zile zilizotungwa baada ya muongo mmoja kupita toka uhuru wan chi za Waswahili. Hizi ziliakisi hali halisi ya maendeleo yaliyofikiwa na jamii husika baada ya kupata uhuru. Zilimulika pengo la mafanikio baina ya malengo ya kupigania uhuru na kiwango cha kufanikiwa (matunda yaliyojitokeza). Kutokana na kuwako kwa kiwango kidogo cha maendeleo, maudhui haya yalijaa kejeli, malalamiko na manungu‘uniko. Malalamiko haya yalitoakana na mambo mengi kama vile tofauti ya kimaendeleo kati ya vijiji na mijini na umasikini wa kupitiliza. Mifano ya riwaya hizo ni: Shida, Njozi iliyopotea, Kichwamaji na Dunia Uwanja wa Fujo.
Baada ya hapo, kilifuata kipindi cha anguko kuu la uchumi wa Dunia. Anguko hilo lilifuatiwa na kipindi cha ufufuo wa uchumi wa dunia (sera za mpango wa kuhuisha mfumo wa uchumi wa dunia, hususani barani Afrika). Riwaya ya Kiswahili pia iliakisi hali hii.
Maudhui ya jumla yanayojichomoza
Maudhui yanayojichomoza sana katika riwaya ya Kiswahili ni pamoja na:o Historia au uhistoriao Mapambano dhidi ya ukoloni (vita vya uhuru/kujikomboa)o Ujumi wa kiafrikao Utabakao Sera za nchi na za kimataifao Utu na maadili (riwaya za sira)o Falsafa na itikadi ya kiafrikao Nafasi ya asasi za dinio Usihirio Epistemolojia ya Waswahili
Ujumi katika riwaya ya Kiswahili
Dhana ya ujumi
Ujumi ni tafsiri ya neno la kiingereza “Aesthetics” lililotokana na neno la Kigiriki “Aisthetikos”. Dhana hii iliasisiwa na Alexander Baumgarten mwaka 1735. Ujumi ni taaluma inayoshughulikia falsafa ya uzuri, ubaya na ladha. Taaluma hii hujibu maswali kama vile:
o Uzuri/ubaya ni nini?o uzuri/ubaya hutokana na nini?o Nini hutuongoza kuamua uzuri/ubaya wa kitu?Maswali haya yakijibiwa, itakuwa rahisi kwetu kutoa maamuzi kuhusu ujumu unaojitokeza katika riwaya za Kiswahili na Fasihi ya Kiswahili kwa ujumla. Dhana ya uzuri au ubaya huweza kufafanuliwa vema kwa kuhusisha mambo makuu matau ambayo ni:
o Ufahamu/akili/hisio Idili za jamii husikao Malengo au matumizi
Idili ni jumla ya nguzo―msingi au vigezo ambavyo jamii hujiegemeza kwavyo kama vipimo vya kuhakikia au kulinganishia uzuri au ubaya wa jambo. Kila jamii na kila kipindi kina idili zake ambazo hutumika kupimia thamani ya vitu mbalimbali. Kigezo kingine (ambacho ni sehemu ya idili) kinachotuongoza kufanya maamuzi ya uzuri/ubaya wa kitu ni malengo au matumizi ya kitu husika. Kitu chochote huweza kuwa kizuri/kibaya kwa watu wa jamii tofauti kutokana na kuwa na malengo au matumizi tofauti.
Kwa mfano: Kalamu yaweza kuwa nzuri kwa mwanafunzi na ikawa mbaya kwa mkulima, mwanamke mnene aweza kuwa mzuri kwa Mwafrika na mbaya kwa mjapani. Katika muktadha wa kozi hii, maarifa haya ya ujumi ni kiunzi muhimu kwetu katika kufanya aamuzi ya kiulinganisho kuhusu falsafa za jamii mbalimbali.Hivyo, uzuri ni matokeo ya kuafikiana au kuwiana kwa uhalisi wa kitu (kadri kinavyoonekana) na idili za jamii husika. Ubaya (ambao ni kinyume cha uzuri), ni kutokuwapo kwa uwiano baina ya uhalisi wa kitu hicho na idili za jamii.Udhihirikaji wa ujumi katika riwaya za KiswahiliKatika kazi mbalimbali za fasihi, ujumi huweza kudhihirika kwa kuchunguza vipengele vifuatavyo:o Usawiri wa wahusikao Mtindo wa sanaa yenyewe kwa jumlao Uumbaji wa maumbile ya vitu (mandhari)o Ukweli na uthabiti wa maudhuio Katika riwaya za Kiswahili, ujumi wa kiafrika hujitokeza kupitia vipengele mbalimbali. Baadhi ya vipengele hivyo ni:o Dhana yenyewe ya U―Afrikao Utamadunio Vyakula na mfumo ― mloo Mgogoro wa mwingiliano wa ujumi wa Kiafrika na ujumi wan chi za kigeni.
Historia au uhistoria
Kwa jicho hili, riwaya huweza kutazamwa kama:o kama kazi ya historia ya waswahilio kama nyenzo ya kufundishia historiao kama sehemu ya historia yenyewe
Riwaya huweza kubeba vionjo vingi vya kihistoria. Kwa namna fulani, riwaya huweza hata kutumika kufundishia historia kwa jamii fulani. Hata hivyo, kwa yeyote aamuaye kuzitumia kwa lengo la kufundishia historia lazima awe na uelewa wa kutosha kuhusu dhana ya riwaya na historia.
Riwaya, kwa kawaida, zina vipengele vya ubunifu, hivyo uhistoria uweza kuwapo kwa malengo ya kiyakinifu (kuakisi uhalisia wa mambo) au kwa lengo la kisanaa. Hivyo, kupitia riwaya hizo, jamii hupata nafasi nzuri ya kujitambulisha na kujifunza mambo mengi yaliyotokea katika nyakati zilizopita. Baadhi ya mifano ambazo zaweza kutupatia maarifa ya kihistoria ni: Miradi Bubu ya Wazalendo, Gamba la Nyoka, Ndoto ya Ndaria, Uhuru wa Watumwa na Moto wa Mianzi.
Utabaka katika Riwaya za Kiswahili
Maudhui haya yalitokana na kuwako kwa wakoloni katika jamii za waswahili kwa muda mrefu. Hata baada ya uhuru bado jamii ilitawaliwa na matabaka. Riwaya ya Kiswahili haikuwa nyuma katika kuisawiri hali hiyo. Katika riwaya mbalimbali waandishi waliwajenga wahusika katika namna ya kujipambanua na kuyapambanua matabaka mbalimbali yaliyokuwapo katika jamii. Aidha, waandishi wenyewe walipaswa kuwa makini kwani walimulikwa na jamii. Hii ni kutokana na ukweli kuwa jamii ilikuwa inajiuliza:
o mwandishi au wahusika wa kazi husika ni nani?o Wako katika tabaka gani?o Wanamsemea nani?
Suala la mipango na sera za nchi na za kimataifa katika riwaya za KiswahiliSuala hili pia limezungumziwa sana na riwaya za Kiswahili. Suala la sera na mipango kadha huwenda sambamba na vipindi mbalimbali vinavyoshuhudia kuanzishwa kwa sera hizo. Kila kipindi kilikuwa na mipango na sera zake.
Epistemolojia ya waswahili katika riwaya za Kiswahili
Epistemolojia ni tawi la falsafa linalishughulikia maarifa. Kila jamii ina duara lake la maarifa na ujuzi. Riwaya za Kiswahili zinamchango mkubwa wakuwasilisha maarifa mbalimbali kwa wasomaji. Dhana ya maarifa hapa yafaa itazamwe kitofauti na dhamira za kawaida. Hii ni kwasababu, maarifa hayo si lazima yawe wazi kwa wakati mwingine huwa fiche. Jambo hili la kuwasili epistemolojia huweza kufanywa na mtunzi kwakukusudia au bila hata kukusudia. Vilevile, miongoni mwa wasomaji wa riwaya, lazima pawe na utofauti katika kuibua epistemolojia inayopatikana katika riwaya husika. Hii inatokana na ukweli kuwa suala la kubaini mafunzo, maarifa na ujuzi linauhusiana pia na utambuzi na tajiriba ya msomaji.
Falsafa na itikadi ya kiafrika katika riwaya za Kiswahili
Maana ya falsafa na itikadi
Falsafa: kweli ambayo mtu anaiamini, anaisimamia na anaiishi au anaishi nayo.
Itikadi: ni njia mkondo au nyenzo ambayo mtu anaishikilia na kuitumia ili kuifikia kweli anayoiamini (falsafa). Dhana hizi mbili zinakanganya na zinachanganya wanazuoni wengi.
Falsafa na itikadi za kiafrika katika riwaya za Kiswahili
Kuna riwaya kadhaa zenye maudhui ya kifalsafa katika riwaya za Kiswahili. Baadhi ya wanazuoni wa kifalsafa wanadai kuwa hakuna mtu anayeishi bila falsafa. Hivyo, hata waandishi wa riwaya ni ngumu kusema huyu hana falsafa: kwamba, takribani kila riwaya kuna falsafa inayoshadidiwa na kupigiwa mbiu. Baadhi ya falsafa zinazojitokeza sana katika riwaya za Kiswahili ni:
o Uduara wa maisha
o Ujuala (kuwapo kwa Mungu na kani za Kiuungu)
o Usihiri na ushirikina
o Thamani ya mtu na utu:
o Udugu na mbari/ukoo (thamani ya uzazi n.k.)Baadhi ya itikadi zinazojitokeza sana katika riwaya za Kiswahili ili kushadidia falsafa hizo ni:
o Dhima ya dini na asasi zake
o Ujadio Sera mbalimbali kama vile ujamaa na kujitegemeao Dhana ya kijadi kama vile uganga, matambiko n.k.
Suala la nafasi na asasi za dini katika riwaya za Kiswahili
Maudhui yake yanamulika masuala yafuatayo: maana na asili ya dini: dini zinanafasi gani katika jamii? Umuhimu wa watu kumcha Mungu, unafiki wa wacha Mungu, udhaifu wa asasi za dini au viongozi wa asasi za dini n.k. mifano ya kazi au riwaya: Siku ya Watenzi Wote, Pete n.k.
Suala la Usihiri katika riwaya za Kiswahili
Ni miongoni mwa nduni maarufu zinazojitokeza katika baadhi ya riwaya za Kiswahili. Suala hili uhusisha dhana za ushirikina, uchawi, wanga na uganga.
Uchawi: ni ufundi au utaalamu wa kutumia dawa na mbinu nyingine za uganga kwaajili ya kuleta madhara kwa watu na viumbe. Pia uhusisha maudhui yanayoakisi uhalisia ajabu au uhalisia mazingaombwe. Kuna migongano kuhusu kuwa au kutokuwapo kwa dhana ya uchawi hapa duniani. Wapo wanaoafiki kuwapo kwake na wengine wanapinga na kudai kuwa hizo ni imani tu. Hata hivyo, kuwapo kwa jambo hili kunadhihirishwa na hata vitabu vitakatifu vya dini. Mifano ya riwaya zenye imelea vya usihiri ni: Babu alipofufuka, Utata wa 9/12, Dunia Yao, Miradhi ya Hatari, Walenisi, Bina —adamu n.k.
Riwaya ya Kiswahili na kumbo la maendeleo ya kiteknolojia
Sayansi na teknolojia kwapamoja zimesaidia kukuza utanzu huu wa riwaya. Sayansi na teknolojia zimeshadidia katika ukuaji wa mambo kadhaa katika maendeleo ya riwaya, baadhi ya mambo hayo ni pamoja na:
o Utunzio Uchapishajio Usambazajio Usomajio Urejeleaji n.k.
UHAKIKI WA RIWAYA TEULE ZA KISWAHILI
Dondoo muhimu katika uhakiki wa riwaya teule
o Vitabu vinavyopaswa kusomwa
o Vitabu vinavyopaswa kuzamiwa
o Mambo ya kuzingatia katika uhakiki
Mambo haya matatu yanaendana sanjari na:
o Kuijua nadharia ya uhakiki
o Nadharia za kuhakikia
o Kufanya uhakiki (wajumla na ule mahususi, uzingatia
o vipengele mahususi).
o Ushahidi katika suala la uhakiki
o Kufanya uhakiki linganishi
Nadharia za kuhakikia fasihi
Ni jicho la kurunzi ya kufikia lengo fulani. Uhakiki mzuri ni ule utumiao nadharia. Zipo nyingi sana bali huweza kugawanywa kutokana na lengo la uhakiki. Hakuna nadharia bora wala dhaifu. Kati ya nadharia hizo nyingi hukamilishana, hutegemeana na kuathiriana. Makundi makuu au maaru ni:o Zilengazo masuala bia (Ya kiulimwengu)o Zilengazo masuala ya kijamii (za kisosholojia)o Zilengazo kazi husika (Umbo au muundo au maana)o Zilengazo msomaji wa kazi za fasihi.
Baadhi ya nadharia hizo ni:
o Uhemenitiki
o Usemezano
o Uhalisia
o Uhalisia ajabu
o Ualisia
o Umatini au semiotiki
o Urasimi
o Urasimi mpya
o Ulimbwende
o Undhanaishi
o Uana au Ufeministi
o Umaumbo
o Umuundo
o Udenguzi au uumbaji
o Upokezi
o Udodosinafsi au saikolojia changanuzi
o Mwingiliano matini
o Usimulizi au Naratolojia
o Mwitikio wa Msomaji
o U — Bakhtini au Ukanivali
o Ungitamaduni au Ubaada Ukoloni
o U — Foucault
o Umaksi
o Uyakinifu wa kitamaduni
o Uakisio Unegritudi
o Usasao Usasa leo
o Uhistoria
o Uhistoria mpya
o Uhakiki mpya.
Vitabu vya riwaya vinavyopaswa kusomwa
Angalau riwaya za kila kundi au kijikundi zisomwe na kupata picha ya jumla ya maudhui na fani yake (usomaji huu wa jumla pia uzingatie riwaya zilizotungwa na waandishi kutoka kanda kubwa za waswahili ambazo ni Tanzania bara, Tanzania visiwani na Kenya).
Mwongozo kwa watakaowasilisha uhakiki
Madondoo muhimu yapaswayo kuwemo katika uwasilishaji ni:
o Ikisiri (taarifa za mtunzi na utunzi, aina ya riwaya)
o Dhamira chomozi
o Mbinu chomozi za kibunilizi
o Hitimisho (kituo au mkolezo, riwaya zinazofanana nazo).
|
|
|
UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 04:35 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
UHUSIANO WA FANI NA MAUDHUI KWA MUJIBU WA WATAALAMU MBALIMBALI
Uhusianoa wa fani na maudhui umekuwa ukiangaliwa na wanazuoni wa fasihi katika mitazamo tofauti, mtazamo mkuu unaoangaliwa na wanazuoni katika uhusiano wa fani na maudhui umo katika makundi makubwa mawili ya kimtazamo. Makundi hayo ni ya mtazamo wa KIYAKINIFU na mtazamo wa KIDHANIFU.
A: Mtazamo wa kidhanifu.
Wanazuoni wanaoegemea katika mtazamo huu hudai kuwa fani na maudhhui havina uhusiano wowote. wanaagalia uhusiano wa vijenzi katika utengano ambao fani inaweza kujikamilisha bila ya kutegemea maudhui na maudhui pia huweza kujikamilisha bila ya kutegemea fani.
Wanaeleza uhusiano wa fani na maudhui kuwa ni sawa na ule wa kikombe na maji au chai iliyomo ndani ya kikombe hicho. Baadhi ya wananadharia hao wanahusisha mahusano haya na yale ya sehemu ya ganda la chungwa lililo nje ya nyama ya chungwa. Wanazuoni wanaoungana mkono na nadharia na mtazamo huu ni hawa.
Fr.F.M.V NKWERA
Nkwera anadai kuwa fani na maudhui havina uhusiano wowote kwa kufananisha na maziwa na kikombe. Kikombe anakiona na kukichukulia kama chombo kinachotumika kuhifadhi maziwa. Hivyo kikombe anakifananisha na fani kuwa ni umbo la nje la kazi ya fasihi. Maziwa anayafananisha na maudhui kuwa ni umbo la ndani la kazi ya Fasihi. Kwa madai yake ni kuwa maziwa yanaweza kutenganishwa na kikombe na kila kimoja kubaki peke yake.
S.D. KIANGO NA T.S.Y. SENGO.
Wanazuoni hawa pia wanaunga mkono mtazamo wa kidhanifu, wanadai kwamba fani na maudhui havina uhusiano wowote katika kazi ya fasihi.Wanazuoni hawa wanafananisha fani na maudhui sawa na chungwa kwa madai kwamba chungwa linaweza kutenganishwa na nyama ya ndani ya chungwa inayoliwa ambayo inafananishwa na maudhui ambalo ndilo umbo la ndani la kazi ya Fasihi. Aidha wanafananisha maganda ya chugwa yanayomenywa ili kupata nyama ya ndani ya chugwa sawa na fani ambalo ni umbo la nje la kazi ya Fasihi.
Madai hayo ni kwamba kwa kuwa magamda ya chugwa yanaweza kutenganishwa na nyama ya ndani ya chugwa basi hata fani na maudhui katika kazi ya fasihi vinaweza kutenganishwa na kila kimoja kusimama katika upekee wake. Hivyo, wanadai fani na maudhui havina uhusiano.
PENINA MUHANDO NA NDIYANAO BALISIDYA
Wanazuoni hawa nao wamo kwenye kundi hili la wenye mtanzamo wa kidhanifu, madai yao makubwa kuhusu mahusiano ya fani na maudhui ni kwamba fani katika kazi ya fasihi ni umbo la ndani basi kwa hali hiyo fani na maudhui vinaweza kutenganishwa kwa hiyo fani na maudhui havina uhusiano kwa vile kila kimoja kinaweza kusimama peke yake.
UDHAIFU WA MTAZAMO HUO
Udhaifu unaojitokeza katika mtazamo huu ni ule wa kutazama fani na maudhui kwa mtazamo wa utengano hili ni kosa kubwa sana kwa kutenganisha vile ambayo havitenganishwi.
B : Mtazamo wa kiyakinifu
Wanazuoni wa fasihi wanaoegemea katika mtazamo huu wanadai kwamba fani na maudhui hutegemeana, huathiriana na kukamilishana. Wanazuoni wanaounga mkono mtazamo huu ni kama vile;
M.M.MULOKOZI NA K.K.KAHINGI
Wanazuoni hawa wanadai kuwa fani na maudhui haviwezi kulingana na kuathiriana unaposoma kazi ya fasihi kwa kupata miundo, matendo, madhari, wahusika na matumizi ya lugha. Hivi ni vipengelele vilivyomo ndani ya fani ndipo msomaji anaweza kupata maudhuni ya kazi ya mwandishi kama vile dhamira, ujumbe (fundisho), falsafa ya mwandishi, msimamo na mtazamo wake kwa hivyo basi huona kwamba fani hutegemea maudhui na maudhui ya fasihi hutegemea fani hivyo, fani na maudhui haviwezi kutenganishwa kwani hutegemeana na kuathiriana kama tulivyoona hapo juu.
F .E.SENKORO.
Mwanazuoni huyu pia anaungana na wanazuoni wa mtazamo wa kiyakinfu wanaodai kwamba fani na maudhui haviwezi kutenganishwa. Senkoro katika madai yake anafananisha uhusiano wa fani na maudhui kama sarafu yenye sura mbili mfano wa sarafu ya shilling 200 yatanzania ili iweze kukamilika na kuwa yenye matumizi halali katika serikali halali ya tanzani inalazimika kuwa na picha ya karume na kuwa upande wa pili kuwa na picha ya simba na mtoto wake kutokuwepo au kukamilika sura moja ya sarafu hiyo basi sarafu hiyo haziwezi kutumika kama sarafu halali.
Kwa hali hiyo inamaanisha kwamba upande mmoja wa sarafu huwa ni sawa na kufananisha na maudhui katika kazi ya Fasihi. Hivyo basi ili sarafu ikamilike ni lazima pande mbili zikamilike na hiyo ndiyo hali iliyopo katika fasihi kwamba ni lazima fani na maudhui kukamilishwa ndipo kazi ya fasihi hukamilika na huwezi kutenganisha fani na maudhui.
Mambo muhimu yanayojitokeza katika fani ni. - Muundo – mtiririko wa mawazo na matukio.
- Wahusika
- Mtindo – mbinu za kiuandishi
- Uteuzi wa maneno
- Picha za ishra
Wakati katika maudhui vitu vinavyojitokeza huwa ni:- - Dhamira
- Ujumbe
- Falsafa
- Migogoro
- Mtazamo
- Msimamo wa mwandishi.
Kwa kuhitimisha basi fani na maudhui haiwezi kutenganishwa kwani hutegemeana, huathiriana na kukamilishana. Fasihi kama tunavyoona inajegwa na maumbo mawili ambayo ni fani na maudhui.
|
|
|
RIWAYA TEULE ZA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA NA UDURUSU WA NADHARIA ZA FASIHI |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 04:19 PM - Forum: Riwaya
- No Replies
|
|
Utangulizi
Sifa bainifu ya baadhi ya kazi za fasihi ya Kiswahili za karne ya ishirini na moja ni matumizi makubwa ya mbinu za kiuandishi za kimajaribio. Msomaji wa kazi hizi aghalabu hujikuta ameghumiwa na wingi wa urejeleo matini, uhalisia mazingaombwe pamoja na vipande vidogo vidogo vya visa ambavyo hutumika kuungia simulizi hizo zilizochupwa huku na huko (Bertoncini 2006: 93; Khamis 2003: 78). Kwa jinsi hali ilivyo riwaya hizi zinaelekea kutangaza upenuni kwamba enzi na dola ya uandishi wa kazi za kihalisia imepitwa na wakati na umefika muda wa kutoa wasaa kwa majaribio haya mapya. Ni maoni ya makala kuwa fauka ya mbinu hizi kuwa na natija pamoja na dosari zake bado kuna baadhi ya waandishi ambao bado wanaongozwa na misingi ya kihalisia.
Mbali na uwezekano wa kazi hizi za kimajaribio za kuitenga sehemu ya hadhira (wakiwemo wale wasiozifahamu nadharia za fasihi) kwa kumkumbatia zaidi msomaji aliyesoma na kuzamia fani adimu za kijamii, fasihi ya karne ya ishirini na moja ni njia jarabati ya kumkomaza msomaji ashiriki kikamilifu katika kufuatilia viini vya simulizi mbalimbali anazozikuta humo. Ndani ya riwaya hizi, msomaji anapambana na fikra za wanafalsafa, wanasiasa mashuhuri pamoja na vitimvi vyao, maswala ya utandawazi na athari zake, madondoo ya vitabu vya kidini, visa(a)sili, mighani,
majinamizi, na hata kazi nyingine za kifasihi za wasomi watajika. Makala hii inazamia kipengele kimoja tu cha mafunzo ya nadharia za fasihi ambazo huwa muhimu hasa kwa wanafunzi wa vyuo vya ualimu na hususani vyuo vikuu pale inapowabidi wazungumzie kitaaluma kazi za fasihi. Makala imetumia riwaya ya Musaleo! (2004) ya Kyallo WadiWamitila na riwaya nyingine mbili za Said Ahmed Mohamed za Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010) kama mifano mahususi ya namna waandishi wanavyozungumzia kwa dhahiri nadharia za fasihi. Nadharia katika Uhakiki wa Fasihi: Kipi kwanza? Katika jadi ya uhakiki wa kazi za fasihi, swala mojawapo lililozingatiwa kwa makini ni iwapo wahakiki wanastahili kuzingatia kile kinachosemwa na matini ili kielezwe kwa misingi ya kinadharia au kufanya kinyume chake.
Ingawa kuna kila ithibati kuwa wapo wataalamu waliofuata mojawapo kati ya njia hizo, ushahidi umeonyesha kuwa wengi wa wahakiki hupendelea kufuatiliwa zaidi kwa matini na kisha kuamua nadharia mwafaka itakayofafanua kwa uwazi kile kilichomo ndani ya matini. Said Khamis (2008) amelizungumzia hili kwa mapana na ametoa sababu ambayo naona niitaje hapa kwa kuwa inawafiki nadharia-tete inayoendelezwa na makala hii. Anasema: Nadharia zinabadilika taratibu zaidi kwa sababu mabadiliko ya nadharia mara nyingi huongozwa na mabadiliko ya mitindo na tanzu za fasihi yenyewe. Kinyume cha mambo kilichopo ni kwamba kila siku nadharia hujaribu kama inavyowezekana iwe na uwezo wa muda mrefu wa kuchambua na kuzieleza kazi za fasihi mbalimbali.
Lakini, kwa upande mwingine, hakuna nadharia inayoweza kufaa katika resi ambamo utoaji wa kazi za kubuni situ una wepesi zaidi, lakini mara zote unazingatia upya na mabadiliko. Hii ina maana nadharia fulani moja au zaidi zinaweza kufaa kwa muda fulani tu mpaka pale zinapojikuta, kwa sababu moja au nyingine, zinakumbwa na matatizo ya kutoweza kuzichambua vyema kazi zinazoibuka na upya na mabadiliko.
Wakati huu ndipo nadharia mpya inapohitajika. (Khamis 2008: 12) Nimemnukuu Khamis kwa mapana kutokana na kile anachokiona kama umuhimu wa nadharia za fasihi kuizingatia matini ambayo kama anavyosema daima imo mbioni kuzua mabadiliko.
Katika vitu viwili hivi vinavyotegemeana, matini inayobuniwa ndiyo inayosababisha zaidi haja ya mabadiliko katika nadharia ambayo huenda ikashindwa kuzizungumzia kazi mpya za kifasihi, hususani zile za kimajaribio. Pamoja na kuwafiki hoja anayoitoa Khamis, makala inazamia nadharia-tete ambayo inahusu uhakiki wa nadharia kama msingi huo wa ubunifu wa kimajaribio ambao unahitaji uteguliwe na nadharia.
Riwaya Tatu Teule kwa Muhtasari na Misingi ya Uteuzi wake Mbali na Euphrase Kezilahabi, wanariwaya Said Ahmed Mohamed na Kyallo Wadi Wamitila wametajwa kama waandishi wanaoongozwa na fikra mpya za kiuandishi, yaani uandishi wa kimajaribio ukiwemo ule wa kihalisia-mazingaombwe (Waliaula 2010: 143; Bertoncini 2006: 93; Khamis
RIWAYA TEULE ZA KARNE YA ISHIRINI NA MOJA
Makala inatambua kuwepo kwa sifa hizo za uhalisia mazingaombwe ndani ya riwaya miongoni mwa mambo mengi yaliyofumbatwa humo. Aidha, riwaya hizi zina sifa za kiusasabaadaye ambamo mna vipande vidogo vidogo vya simulizi zisizokuwa na muwala wala zisizochukuana vyema kama zilivyo hadithi za paukwa pakawa zinazoishilia na harusi au wahusika wanaoishi raha mustarehe. Kwa utaratibu wa sifa hizo, nimeteua riwaya husika za Musaleo! (2004), Dunia Yao (2006) na Nyuso za Mwanamke (2010) kwa kuwa zote zinaagua nadharia za fasihi kama sehemu mojawapo ya dhamira zilizomo ndani ya matini hizi. Musaleo! (2004) inajumuisha simulizi inayoenda mbele na nyuma na iliyofichama hadithi mbili tofauti na umazingaombwe usioweza kutabirika.
Ni hadithi inayomsukuma msomaji mbele na nyuma na mwingiliano matini uliokithiri unaohitaji umakinifu ili msomaji apate kuelewa fikra mbinu, njama, vitimbi na hila wanazotumia wakoloni mamboleo katika kuwazuga wale wanaosimama kidete kuzitetea haki zao katika jamii. Nyuso za Mwanamke (2010) nayo inamwendeleza nguli wa kike, Nana, na jinsi anavyojinasua kimawazo kutokana na wavu wa ulimwengu wa kiume kwa kufuata kile kinachoridhiwa na moyo wake.
Ni safari ya msichana, mwanagenzi wa maisha, anayeabiri kujua utu wake na sifa zinazomfafanua binafsi kama mwanamke, tofauti na wanavyotarajia wahusika wengine wa kike na wa kiume wa riwayani. Dunia Yao (2006), kwa upande wake, imesheheni mijadala ya kifalsafa inayozamia fani mbalimbali za sanaa na swala zima la ubunifu. Ninachokiona zaidi ni swala la uendelevu wa sanaa ukiwemo uhai na ufaafu wake katika kuzungumzia visa visivyowaelea watu katika ulimwengu mamboleo.
Dunia, inavyosema Dunia Yao, ni bahari isiyotabirika kina chake na sanaa haiwezi kuwekewa mipaka tunapoabiri kuizungumzia. Kama ilivyoparaganyika dunia, sanaa nayo haina budi kufuata mkondo huo kwani kuifuatilia dunia kwa mstari ulionyooka kama zilivyo kazi za kihalisia ni kuishi katika njozi.
Kuelewa nadharia za fasihi ni miongoni mwa njia adimu za kuelewa mafumbo ya kisanii na ya kimaisha yaliyoatikwa katika riwaya hizi. Makala imezamia baadhi ya nadharia za kifasihi ambazo zimejitokeza wazi wazi katika riwaya hizo tatu. Uhakiki wa Nadharia ya Mwigo Katika kitabu chake maarufu cha Poetics, Plato anaelezea asili na chanzo cha sanaa. Miongoni mwa mambo mengine, Plato humo anaelezea uhusiano wa karibu uliopo kati ya msanii na Mungu ambaye anachukuliwa kuwa mfalme wa sanaa zote. Hususani, Plato anamtaja Mungu wa sanaa aitwaye Muse ambaye huwapanda wasanii vichwani na kuwafanya wabubujikwe na mawazo ya kisanii pindi anapowakumba (kufuatana na Plato kama inavyofafanuliwa katika Tilak, 1993: 29).
Kwa mujibu wa Plato, Mungu huyu huwapagawisha wasanii tu na kuwapa ufunuo au wahyi unaowawezesha kuwasiliana moja kwa moja na wasanii (Habib 2005: 24; Wafula & Njogu 2007: 24).
Kwa sababu hiyo, Plato aliwaona wasanii kama watu wenye vipaji maalum vinavyotoka kwa Mungu na kwa sababu hiyo, siyo kila mtu angeweza kuwa msanii. Katika riwaya tatu zilizoteuliwa Dunia Yao, na kwa kiasi fulani Musaleo!, inafuatilia kwa makini nadharia hii ya Plato kuhusu mwigo na imethubutu hata kumchukua mhusika wake mmoja, Muse ambaye anahusishwa na ghamidha na kariha ya utoaji wa sanaa za kiubunifu huko Ugiriki, kuwa mshirika wa kiroho wa mhusika mkuu aitwaye ‘Ndi-‘. Mhusika Bi Muse (wakati mwingine Mize) wa Dunia Yao anazua mjadala mpevu wa swala zima la sanaa na hulka yake kama inavyowasilishwa na Mohamed. Mhusika huyu ambaye amechukuliwa moja kwa moja kutoka kwa maandishi ya wahakiki wa Kiyunani, Plato na Aristotle, anakuwa kiunzi muhimu cha kujadili swala zima la usanii. Haya yanadokezwa ipasavyo katika riwaya hii pale Bi Muse anapoeleza asili yake.
Ufunguzi wa sura ya tanounadokeza asili ya mhusika huyu, Bi Muse, ambaye ni yule yule aliyezungumziwa na Plato tangu jadi, tofauti hapa ikiwa Bi Muse ni mhusika wa hadithini. Sura inaanza hivi: “Mimi ni Muse” […] “Kwa asili hasa, Ugiriki – lakini siku hizi naishi popote. Mara nyingine hujificha katika vina virefu vya ardhi kabla sijachomoza kumzuru niliyemchagua. Na leo nimekuchagua wewe.
Kwa hivyo nimechomozekea chini ya mnazi palipofukiwa kitovu chako, baada ya kupiga mbizi Bahari ya Hindi kuja kukuingia kichwani mwako…” (Mohamed 2006:61) Sawa na anavyopendekeza Plato kuhusu namna wigo wa kisanaa unavyojiri, hapa mwandishi anaendeleza hoja hiyo hiyo ya namna Ndi- anavyosababishwa atunge kazi yake na Bi Muse.
Naye ni kiumbe anayetangaza kuwa asili yake ni Ugiriki (alikotoka Plato) na hamkumbi Mgiriki pekee bali humkumba mtunzi yeyote wa kazi za kubuni. Ana nguvu za kichawi za kumsababisha msanii apagawe kama riwaya inavyodokeza: “Kwa kawaida,” aliendelea, “sina umbo maalum. Ni aina ya jeteta linalochanua jinsi andasa zangu na zako zinavyokubaliana kuchanua. Sikuzaliwa katika dhati na bayana ya mambo.
Mimi ni binti wa Zeus na Mnemosyne. Asili yangu inasimamia kumbukizi na dhana tu. Ndio maana nina majina mengi kwa mujibu wa kazi yangu ya kutia ilhamu. Calliope, Clio, Erato, Euterpe, Melpomene, Polyhymnia, Terpsichore, Thalia, Urania.
Hata unaweza kuniita Bi Mize, kwa jina la kikwenu. Kwani hapa nilipo nimekuja kwa sura ya kikwenukwenu, kipande samaki, kipande mtu na kipande ndege.” (Ivi: 68f) Huyu anayefahamika kama Bi Muse katika riwaya anaeleza namna anavyoweza kubadili umbo na kuwa mwenza wa kila msanii duniani. Ingawa amezaliwa na Mungu Mkuu wa Kigiriki, Zeus, Bi Muse ana uwezo wa kuwa binti wa kifalme au wa kijini kwa kuzingatia utamaduni wa msanii husika. Ndiyo sababu hapa anamwambia Ndi- kuwa akipenda anaweza kumwita Bi Mize ili afahamu kwa ukaribu nguvu zake anapomkumba. Mize au Mwanamize ni mhusika wa Waswahili anayefahamika kwa vitimvi vyake na nguvu za kiuchawi za kugeuka umbo kama inavyosemwa kwenye dondoo.
Muse, kama anavyotangaza, ana nguvu za kichawi za kumzuga mtu na kummiliki pale anapomchagua na kumfanya kuwa kiti chake. Kitendo hiki cha kupandwa na jazba na kupagawa ndicho kinachojitokeza mwanzoni mwa riwaya pale Ndi- anapoeleza namna swala zima la utunzi linavyohusiana na nguvu hizo za Muse ambapo utunzi unakua hatua baada ya nyingine hadi kukamilika kwake: Katika kubuni na kuumba – ‘Bi Muse’ anapokujia na kukuchota kwa uzuri wake – kama koja la ajabu, unatunga sauti na sauti, ileile au tofauti, na kupata silabi. Silabi na silabi, unapata neno! Neno, maneno. Ibara na sentensi. Ibara na sentensi huzaa matini. Na vyote hivyo ni sehemu muhimu ya simulizi – maandishi. (Ivi: 9) Dondoo hili linaeleza kwa muhtasari uhakiki wa ki-Plato na ki-Aristotle unaohusisha uandishi na kujazibika kwa mwandishi. Safari inayoanza na sauti au fonimu moja inakua na kupea hadi kufikia kuwa matini nzima. Inapotokea hivyo, mwandishi na mungu huyu wa sanaa, Muse, huwa kitu kimoja. Ndi- anaelekea kukiri kuwa uandishi hufatwa na ghamidha na kariha inayomjia mwandishi na wala si jambo la vivi hivi tu, chambilecho Ndi- kuwa Muse si kiumbe wa ‘sasambura turore’ au anayejitoa hadharani kuonekana. Ni kana kwamba Ndi- hushindwa kujizuia na kuhamasika kuendeleza kazi yake ya kiubunifu pale anapotawaliwa kihisia na kifikra na Bi Muse.
Hujikuta tu akiongozwa asikokufahamu ingawa anavyokiri mwenyewe huwa ni wakati adimu wa kutamanika. Hii ndiyo sababu Dunia Yao inaufafanua uhusiano wa Ndi- na Bi Muse kuwa wa mke na mume wanaoliwazana na kubembelezana hadi wanapooana na kuwekana nyumbani. Ni taswira ya unganiko la kipekee ambalo hufukuza utasa na badala yake huzalisha kazi za kisanaa baada ya wahusika hawa kusuhubiana na hata kupata mtoto, yaani kazi inayotungwa. Hatua zote hizi zinaelezwa na Ndi- hivi: Ndiyo, jina lake nimekuwa nikilisikia na kulisoma siku nyingi. Kama alivyosema mwenyewe, si kiumbe wa sasambura turore. Hujifichua anapohitajiwa kwa mapenzi ya dhati au kwa kutoa msaada.
Na mimi, nimefikia baleghe ya kusalitika naye. Nina haja naye. Ninamhitaji. Ninataka anisaidie. Anisaidie kuwasaidia wengine ikiwezekana. Anisaidie kuukata ugumba wa utunzi. Nina hamu kurutubisha na kutia mbolea pahala fulani. Nipate kizazi kipya cha sanaa katika ukame wa ubunifu. Nipate kurutubisha kizazi kipya cha utu katika ukame usio na utu. Ninahitajia mtekenyo wake unipandishe jazba. (Ivi:61f) Swala la kupandwa na jazba linajitokeza pia katika Musaleo!. Katika riwaya hii, Kingunge anaonyesha kuwa uandishi wake hutokana na jazba na kariha inayomsukuma kuandika kile ambacho yeye mwenyewe hana maarifa nacho. Tunaelezwa hivi: Lakini mara hii alipomweleza mkewe uandishi wenyewe alilazimika kusikiliza kwa makini. “Mara hii ni tofauti. Inajisimulia mimi naandika tu. Ni kitu kama ndoto. Yaani kazi yangu ni kuandika yanayonijia. Ngoja niimalizapo utajua tofauti yake na nyingine…” (Wamitila 2004: 12).
Tofauti na riwaya ambazo Kingunge anadai amezipa majina, riwaya anayoandika kwa wakati huu ni ya kipekee na imepokea nguvu maalum asizoweza kuzidhibiti. Ni kariha ya kipekee inayomsibu na ambayo inamsukuma kuandika mambo asiyoyaelewa. Si ajabu basi anapodai kwamba riwaya hii itajipa yenyewe jina badala ya yeye kufanya hivyo (k.10f). Nadharia za Umaumbo wa Kirusi na Umuundo katika Dunia Yao Dunia Yao pia inahakiki kwa uwazi dhana za nadharia ya umuundo za uhusiano wamaneno kimfululizo na kiwimawima. Msingi unaochukuliwa na riwaya hii ni ule wa ki-Saussure, na ulioendelezwa baadaye na Roman Jakobson, unaohusiana na dhana zake za uhusiano wa ishara wimawima au kimfululizo (Eagleton 1996: 85f).
Katika Dunia Yao Mohamed anatueleza hivi: Uhusiano wima wa maneno unakuhakikishia uteuzi. Uhusiano mlalo unakuhakikishia mpangilio wa kisarufi.Unatii amri za lugha au unavunja kanuni za lugha wakati mmoja. Unajenga kutoka kipashio cha chini kwenda kipashio cha juu kabisa. Au unaweza kushuka kutoka juu kwenda kipashio cha chini kabisa. Madhumuni ni kujenga maana kwa njia ya kubomoa maana. Kujenga mvuto wa kisanaa. (Mohamed 2006:9; msisitizo wangu) Mohamed katika Dunia Yao anataja na kuzifafanua dhana mbili muhimu za umuundo ambazo anazirejelea kama “uhusiano wima” na “uhusiano mlalo” wa maneno. Mahusiano haya ya maneno, tunaelezwa, yana natija zake hasa kwa mwanafasihi.
Uhusiano wima wa maneno, tunaambiwa, huhakikisha uteuzi. Swala muhimu hapa ni kujua namna uteuzi huu unavyohakikishwa kwani haujabainishwa waziwazi kwenye dondoo. Mwamzandi (2007: 71) ametoa mfano ambao kwa muhtasari unafafanua swala hili la uteuzi: mchuti kiki Abasi aliupiga teke mpira mkwaju Katika mfano huu, neno ‘teke’ limechukuliwa kama neno la kawaida au la wastani ambalo msemaji wa Kiswahili angelitumia.
Maneno yaliyoandikwa kwa mlazo na ambayo yamejipanga juu na chini ya neno ‘teke’ ndiyo tunayoweza kusema kuwa yanahakikisha uteuzi unaozungumziwa na dondoo. Maneno hayo yanaeleza namna na jinsi mbalimbali za kuupiga mpira na mwanafasihi anaweza kuchangua neno mahsusi kwa kutegemea hisia maalum anayotaka kuibua kwa msomaji wake (Mwamzandi 2007: 71). Uhusiano mlalo wa maneno nao, kama unavyofafanuliwa ndani ya dondoo, una uwezo wa kuidumisha au kuivunja sarufi ya lugha, matokeo ambayo yanatokana na jinsi mwanafasihi, kwa mfano, atakavyochagua kuyapanga maneno yake katika sentensi. Katika sentensi, lugha yoyote huwa na matarajio na sheria zake za kisintaksia na kisarufi. Kwa sababu hiyo, kulibadilisha neno
moja katika sentensi na kuliweka mahala tofauti na pale panapotarajiwa na wanalugha husika kuna athari kubwa, ikiwemo ile ya kuzua maana tofauti na ile inayoweza kukubalika. Neno hilo linaathiriana kivingine na maneno mengine ya sentensi na kuzua maana mpya inayoweza kutegua uzoefu wetu wa lugha hiyo. Huu ndio ule mpangilio wa kisarufi unaoweza kutii au kuvunja kanuni za lugha na ambao unaozungumziwa na dondoo hapo juu na tunaweza kuutolea mfano huu: kitabu kizuri mtu mnene Hebu tazama sasa tunapobadilisha na kuanza na vivumishi na kisha nomino, na kuikaidi sarufi ya Kiswahili kama inavyotarajiwa: kizuri kitabu mnene mtu Ingawa maana iliyokusudiwa bado ipo, mabadiliko ya pale zilipo nomino na vivumishi kumesababisha ugeni fulani. Huu si muundo wa wastani wa Kiswahili ingawa unaweza ukakubalika katika miktadha mahsusi, ukiwemo fasihi.
Huku ndiko kujenga maana kwa njia ya kuibomoa kama kunavyozungumziwa na dondoo. Uhakiki wa Kidenguzi: Nyuso za Mwanamke na Dunia Yao Mbali na kushughulikia maelezo ya kinadharia kuhusu nadharia ya udenguzi, riwaya za Nyuso za Mwanamke na Dunia Yao pia zinashughulikia zoezi lenyewe la kuchanganua maana kwa kuongozwa na fikra hiyo ya kidenguzi. Ili tufuatilie kila kinachosemwa katika riwaya hizi mintarafu ya udenguzi ni vyema tuangazie, walau kwa muhtasari, fikra kuu ya nadharia yenyewe.
Udenguzi ni nadharia inayohusishwa na Mfaransa Jacques Derrida (1930-2004). Hapa nitafafanua misingi miwili tu ya nadharia hii kama ilivyofafanunuliwa na wataalamu mbalimbali (taz. Burman & McLure 2005: 284-286; Schmitz 2007: 115f). Mosi, mbinu kuu na muhimu inayotumiwa wa wanaudenguzi ni ukinzani wa jozi za maneno. Tasnifu ya Derrida kuhusu jozi hizo ni kuwa jamii za Kimagharibi zimejenga upendeleo wa wazi pale neno moja katika jozi husika daima linawakilisha utukufu au kile kinachopaniwa kufikiwa kama kitu adili huku dhana ya pili ya jozi hiyo hiyo ikiangaliwa kama ghushi, isiyo safi na ya daraja ya chini. Wanafilosofia wa awali, kama anavyodokeza Derrida, waliuona ulimwengu katika muktadha huo – jambo lililowafanya kuuona upande wa kwanza wa jozi za maneno kama unaojengwa na vitu vya kimsingi na vinavyostahili kupewa kipaumbele kama vilivyo safi, vya wastani na vilivyokamilika huku upande wa pili wa jozi nao ukifafanuliwa na vitu vilivyotandwa na utata, vyenye doa na umahuluti. Kwa sababu hiyo, usanifu wa hoja katika nchi za kimagharibi una tabia ya kuviona vitu na hali mbalimbali kwa namna ya upendeleo.
Pamoja na mgao huo ambao wanafilosofia wa kijadi walipania kuujenga, wanaudenguzi hulenga kufutilia mbali mipaka hiyo na kuonyesha kuwa jozi za maneno ni mfano wa sarafu moja yenye pande mbili. Udenguzi hubainisha kuwa nuru na kiza ni vitu ambavyo wanafilosofia wa kijadi wangevitenganisha kwa kupendelea nuru kuliko kiza. Kwa wadenguzi, nuru sawasawa na kiza vimechangamana na huwezi kukielewa kimoja bila kingine. Hatungeweza kumaizi kile tunachokifahamu kama nuru iwapo lugha tunayoitumia haingekuwa imeratibu ndani yake dhana ya kiza. Pili, udenguzi hushughulikia kwa pamoja jozi ya maneno yanayokinzana na wakati huo huo kubainisha itikadi kuu inayojitokeza na inayostahili kusailiwa upya. Kupitia uchanganuzi makini wa lugha ya matini, wadenguzi hudhihirisha ukinzani na utepetevu wa matini hizo.
Hili ndilo linalowapelekea wadenguzi kudai kuwa matini hujiumbua na kujibomoa yenyewe na wala sio wao wanaofanya hivyo. Wanavyodai, hii ni sifa ya azali na iliyomo katika lugha kwani tangu jadi lugha imejengeka kama mfumo wenye ukinzani na unaotofautisha maana. Lugha yenyewe imejengeka kiudenguzi kwani hubainisha tofauti zilizomo ndani yake – za kimaana na za kiitikadi. Kipengele cha kwanza kinaingiliana moja kwa moja na fasiri inayotolewa na mhusika mkuu wa Nyuso za Mwanamke, Nana, pale anapotoka nyumbani kwao na kuabiri safari ndefu ya kuutafuta uhuru wake binafsi baada ya kuamua kutoroka nyumbani kwao. Anaanza somo lake la kidenguzi kwa kuzamia jozi zilizomo katika dhana mbalimbali zinazokinzana: Kwa kawaida nafsi yangu ilinifanya niamini kwamba hakuna utenganisho mkamilifu baina ya kuwepo na kutokuwepo. Sisi binadamu tupo kama hatupo au hatupo kumbe tupo.
Basi, maisha ya siku hizi ni kama kuwepo ndani ya kutokuwepo au katika kutokuwepo na kuwepo. Ni hali ya kudinda ndani ya ukweli na uwongo. Au baina ya nafsi moja na ndani ya nyingi na nyingi ndani ya moja: utambulisho wetu ni wa weusi na weupe, majilio yetu ni nidhamu na machafuko. Tunavunga ndani maumbile yanayovunjwa na utamaduni wa pupa, katika dunia isiyobagua tena kati ya wema na uovu, uke na uume, kitovu na pembezoni… (Mohamed 2010: 59; msisitizo wangu). Lakini kama Derrida anavyotambua kuwa watu hupania tu kuweka mipaka kati ya vitu, mipaka hiyo kwa hakika huwa ya kufikirika na udenguzi hutuelekeza tuangalie kwa makini ukinzani unaojitokeza ndani ya matini (Carter 2006: 111).
Nana anatutanabahisha juu ya jozi tofauti tofauti zikiwemo kuwepo/kutokuwepo, ukweli/uwongo, umoja/wingi, weusi/weupe, wema/uovu, uke/uume, kitovu/pembezoni ambazo tunastahili kuzifikiria kwa pamoja ili tuone namna jozi hizi zinavyojengana na kuumbuana1. Hii ndiyo sababu Nana wakati mwingine anazibadilisha jozi za maneno kama vile kuwepo/kutokuwepo hadi kutokuwepo/kuwepo, na “moja/nyingi” – “nyingi/moja”. 1 Kwa ufafanuzi zaidi wa fikra ya kidenguzi kama zoezi la uchanganuzi wa jozi za maneno msomaji anashauriwa asome makala ya Mwamzandi (2011: 1-14). Humo ataona namna maneno jozi yanavyoumbuana na pia kujengana kimaana. Aidha, ningependa kuwashukuru wahariri kwa ushauri na mapendekezo yao, hususani kuhusu sifa na hulka ya fasihi ya kiusasa-baadaye.
Mipaka ya jozi za maneno huwa myembamba sana na hili ndilo linaloendelezwa na Nana kwa utaratibu huu: Mkinzano unaishi ndiyo, na kwa kweli lazima uishi kwani mkinzano ndiyo maisha yenyewe. Lakini kila mkinzano una mstari mwembamba usioonekana kwa macho. Ndiyo unatenganisha mambo, lakini ni mwembamba mno kutenganisha kwa ukamilifu kitu kimoja na cha pili. Hapana kitu kimoja na cha pili, pana kimoja kinachoshibishana na kugombana na cha pili. Ndivyo dunia yetu ilivyoanza tokea mwanzo katika hali ya uwili inayotegemeana na kutofautiana […] Pana kuvuka mipaka pande mbili. Hiki cha huku kinaweza kwenda kule na cha kule kinaweza kuja huku. Nguvu za hiki zinajengwa na kile. Kuwepo kwa hiki ni sababu ya kuwepo kile. Huo ndio uwili unaotegemeana, lakini unaovunjana kwa wakati mmoja. Anayejiona ameshinda hatimaye ni yule mwenye nguvu, lakini ukitazama sana, hapana anayeshinda. Kuna kushindwa kwa wote. (Ivi: 59f) Katika dondoo hili, uwili unaozungumziwa na Derrida umekaririwa mno hapa. Kila mahali, kunatajwa kitu kimoja na jinsi kinavyosuhubiana na kuathiriana na kile cha pili.
Dunia, kama asemavyo Nana, imejengwa na uwili huu wa ukinzani. Maneno ya Nana yanadokeza muktadha mahsusi unaohusu ugomvi wake na babake. Baba alidhamiria kushinda kwa kumlazimisha Nana awe chini ya mamlaka yake. Nana naye anajiona ni mtu mzima wa kujiamulia watu anaotaka kutangamana nao. Hili ndilo analosisitiza Nana katika mvutano wake na babake. Baba anapania mwanawe atangamane na watu wa aila ya juu kama alivyo yeye mwenyewe na haelekei kuufurahia uhusiano wa bintiye na Mpiga Gita (Faisal).
Mwishoni, tunaonyeshwa kwamba baina ya kushinda na kushindwa, kushinda kunawavutia wengi ingawa kwa hakika hakuna mshindi. Nana anatoroka nyumbani na katika vita hivi vya baba na mwana, hakuna anayeshinda – kila mmoja anashindwa! Baadaye kidogo, Nana anatueleza waziwazi chanzo cha mawazo haya anapotuambia: Hapo nilimkumbuka Derrida na ubomozi wake anaouita (de)construction. Kila kitu lazima kiwe deconstructed. Naye hakuchukua muda kunijia katika fikra hii ya (de)construction. […] Falsafa si mijineno tu. Si ubingwa tu wa kushindana ili mmoja amwone mwingine duni, ili yeye aonekane bingwa au gwiji. Falsafa ni maisha yenyewe. (Ivi:60) Udenguzi au ‘ubomozi’ kama unavyorejelewa kwenye Nyuso za Mwanamke unahusishwa na usomaji uliopea wa kutazama kila neno katika jozi kwa jicho pekuzi. Usomaji huu umependelewa sana na wadenguzi wanaodai kuwa matini za fasihi zina tabia ya kuzungumzia kile zisichokidhamiria (Burman & MacLure 2005: 284f). Hii ni mianya inayostahili kufuatiliwa na msomaji ili aweze kuidengua kikamilifu matini husika. Dunia Yao, kupitia Ndi- inazungumzia hatua hii muhimu katika usomaji wa kidenguzi kwa kusema:
Madhumuni ni kujenga maana kwa njia ya kubomoa maana. Kujenga mvuto wa kisanaa. Ndiyo, unaweza kujenga maana hata katika mwanya mtupu. Hata ukitaka, unaweza kwa makusudi kupoteza maana kabisa kwa vivuli vya maana. (Mohamed 2006: 9) Katika dondoo hili kile kinachorejelewa kama kivuli cha maana ni ile sehemu ya pili ya neno au dhana katika jozi ambayo aghalabu huenda ikaachwa nje na isizungumziwe wazi wazi na mwandishi. Wadenguzi wanafuatilia maneno kama hayo kama linavyotarajia zoezi la kidenguzi ili kubainisha kile kisichosemwa na athari yake katika uwanja mzima wa maana (Schmitz 2007: 118; Carter 2006: 111). Uhalisia, Sanaa Faafu na Nadharia ya Usasa-baadaye Swala jingine muhimu linaloibuliwa na riwaya zilizoteuliwa katika makala hii ni mazingatio ya kile tunachoweza kukitambua kama sanaa stahiki kwa waandishi na hadhira lengwa.
Kama nilivyotanguliza hapo awali, riwaya hizi zimesheheni majaribio mengi na kwa namna zilivyoandikwa msomaji huenda akatanzwa na mbinu tata zilizomo za kiuandishi. Waandishi wa riwaya hizi wanaelekea kulitambua hilo na Dunia Yao inazamia mjadala huu wa sanaa faafu dhidi ya ile iliyopitwa na wakati, hasa kwa kuzingatia kipindi mahsusi cha kihistoria na mbinu sadifu za kuwasilishia sanaa. Kama tapo la kiuandishi, uhalisia umekuwa na uzuri wake ingawa kile kilichoonekana kitu adimu ndani ya uhalisia kimeanza kutiliwa shaka. Ndi- katika Dunia Yao anadokeza hivi: Alisita hapo. Nilifahamu amekusudia nini. Wakati wa sanaa ya uhalisia nilijua umeshapita.
Kwa kweli wakati ule nilipoanza, nisingeweza kuandika vingine nje ya uhalisia. Kanuni zake zisingekubali. Nani angenichapisha? Nani angenisoma? Jambo moja muhimu lililoshikamana na sanaa wakati ule lilikuwa dukuduku la watu. Tamaa zao za dhahiri. Nusura iliyoonekana iko njiani. Ingefika kesho kama si sasa hivi. (Mohamed 2006: 71) Kama mhusika, Ndi- anaona kwamba yeye pia amekuwa katika hali ya mpito. Uhalisia aliouenzi sasa hauna nafasi kwake kwa kuwa wasomaji sasa wako tayari kuzipokea kazi zake za kimajaribio.
Hapo awali, hakuwa na budi ila kutunga kazi za kihalisia na anazo sababu zake za kufanya hivyo kama inavyoelezwa katika majadiliano haya ya Ndi- na Bi Muse. Jambo la kwanza ni kuwa wasomaji wenyewe walikuwa na matarajio au dukuduku lao kuhusu kazi za fasihi ambazo walitarajiwa ziandikwe kwa mtindo huo wa kihalisia. Pili, wachapishaji nao hawangethubutu kuchapisha kazi za kimajaribio kwa kuwa wanunuzi hawangeziona za manufaa kwao. Hivyo mwandishi wa wakati huo hangekuwa na hiari ya kiuandishi ila kuwatii wachapishaji ambao waliongozwa zaidi na faida inayotokana na mauzo yao kuliko ujasiri wa kisanii wa mwandishi. Swala hili la kuthaminiwa kwa fedha kuliko waandishi limezungumziwa pia katika Musaleo! kama tatizo mojawapo linaloathiri kutolewa kwa sanaa nzuri, tena faafu. Sanaa nzuri, kama inavyoelekea kujadiliwa humo, ni ile
ambayo itakidhi haja za kibinafsi za waandishi na aila zao. Hususani, Musaleo! inalalamikia namna waandishi wanavyopunjwa na kuchezwa shere na wachapishaji. Zamda, mkewe Kingunge, analalamika jinsi mumewe anavyotumia muda wake mwingi kuandika riwaya huku akikosa namna za kuikimu familia yake. Zamda anasema: Sasa huu uandishi nao naona umekuwa kama kufungukwa na uganga. Heri siku zilizopita na hata kulipa haulipi huu! Uandishi! Uandishi! Uandishi wa nini? (Wamitila 2004: 12) Ndi- katika Dunia Yao anaelekea kupendelea fani ya usasa mamboleo au usasa wa kisasa katika maswala ya uwasilishaji wa kazi za sanaa. Sanaa, kwa mujibu wa mhusika huyu, huenda na wakati na mahitaji ya mwanadamu.
Na hapo anaeleza kwa nini uhalisia ulifaa katika kipindi fulani cha uandishi kuliko uandishi wa aina yoyote na ilipodhihiri kwamba uhalisia haungeweza kushughulikia dhamira za kisasa, basi ilibidi nao utupiliwe mbali kama kinavyotarajia kipindi cha hivi leo. Ndi- anasema: “Hii ni bustani iliyopitwa na wakati,” nilimsikia akisema hatimaye, “inafanana na mantiki ya mambo ya miaka ile iliyopita. Ni bustani ya ukame na kifo. Ni ukaukivu wa mambo unaoashiria ufu wa bongo lako lisiloweza tena kusimulia kwa mantiki. Hakuna tena mantiki. Hakuna tena umajimaji wa ubichi wa mambo. Uhai haupo tena mbali na kifo, na kwa hivyo hauwezi kuwepo ukweli, ukweli. Wigo wa ukweli wa moja kwa moja haudindi tena. Na kusema kweli, tokea mwanzo haukuwepo.
Iliyokuwepo ni ndoto. Ndoto ya bustani hai. Kumbe kavu na teketevu namna hii.” (Mohamed 2006: 64) Hapa, Ndi- anaulinganisha uhalisia na kifo cha kiakili, yaani kukosekana kwa ubunifu katika fasihi. Hata kile kilichothaminiwa kuwa uhalisia kiliishi katika njozi za watu na kamwe haukuwa ubunifu kama anavyodai Ndi-. Anachosisitiza Ndi- ni kuwa kuzingatia uhalisia kwa kipindi cha leo ni kuishusha hadhi fasihi. Mawazo sawa na hayo yamezungumziwa pia na Kingunge katika Musaleo! pale anapokutana na mhariri wake ili wazungumzie maendeleo ya mswada wa hadithi yake.
Mhariri anabishana juu ya mwelekeo mpya aliouchukua Kingunge kwa kusema: “Wasomaji wako watalalamika sana mara hii. Mbona usitumie mtindo rahisi ambao wanaufahamu: unajua watu hawapendi mabadiliko bali huyapenda mazoea na ukale…” alilalamika mhariri. “Na hilo ndilo kosa kubwa. Maendeleo hayamo katika ukale!” (Wamitila 2004: 41) Sawa na anavyodai Ndi- wa Dunia Yao, katika Musaleo! naye mhusika Kingunge anayaona maendeleo yakiwemo katika kuhimiza kuwepo kwa majaribio katika uandishi na wala sio katika kuwa wahafidhina. Lakini je, sanaa mamboleo inayopendelewa na riwaya hizi ni ipi?
Waonavyo waandishi hawa wa kimajaribio uhalisia umepitwa na wakati na wamehoji kuwa sanaa kamwe haiwezi kuwekewa mipaka. Mintarafu ya riwaya hizi, sanaa nzuri ni ile itakayojumuisha mbinu za kuelezea dunia ya sasa iliyojaa miujiza na mambo mengi ambayo hayawezi kueleweka kwa njia iliyo rahisi. Uzuri wa sanaa kwao si kuyaeleza mambo yalivyo kihalisia na, chambilecho Dunia Yao, “kuzipata maana kibungabunga” (Mohamed 2006: 9). Msomaji sharti ashiriki kikamilifu katika kuzipekua maana za kazi anazozisoma na kukubali kuzugwa pale inapobidi.
Sanaa nzuri kwao ni ile itakayomlazimisha msomaji kusaili ishara tofauti tofauti atakazotumia mwandishi na kisha kuzihusisha ishara hizo na muktadha wa maisha yake halisi. Hatimaye, ufaafu wa sanaa huamuliwa na namna itakavyomtumikia yule anayelengwa. Haya ndiyo mawazo makuu yanayoendelezwa katika sura yote ya tano ya Dunia Yao. Katika Musaleo! naye mhusika Kingunge anayakubali mawazo haya anaposema: “Siandiki? Naandika sana. Tena mara hii riwaya ya kisawasawa itakayojisoma yenyewe pamoja na kuyasoma maisha yetu. Naandika riwaya itakayojihakiki yenyewe!” (Wamitila 2004: 10) Kingunge, kama inavyodhihirika hapa, anashadidia wazo kuwa kitendo cha uandishi huvuka mawanda ya matini kwa kuhakiki mchakatowenyewe wa uandishi.
Katika muktadha huu, riwaya za kisasa zinamaizi hali hiyo na kuhimiza wingimatini uliomo duniani – jambo ambalo wasomaji hawana budi kuliafiki na kulikubali kama dira inayochukuliwa na fasihi ya kisasa ya Kiswahili. Baada ya kuzungumzia uhalisia na ufaafu wake wa kukidhi matakwa ya binadamu, riwaya teule pia zinafafanua viunzi vilivyotumika kuzijenga.
Riwaya za kisasa, kama inavyopendekezwa, zimejengwa na vipande vya ngano au simulizi fupi fupi zisizokuwa na uaushi, tofauti na simulizi kuu ambazo aliziona kama zilizopoteza uthabiti wake (Lyotard 1984: 37). Simulizi hizi hutokeza kwa muda mfupi ndani ya riwaya na hazilengi kuhodhi ukweli kama zilivyo simulizi za jadi ambazo zililenga kukongomea ukweli kama zilivyouona. Lyotard, kwa mfano, amenukuliwa na Barry (2002: 86) akisema kuwa simulizi kuu hubuniwa kwa azma ya kusawazisha ukinzani na kusababisha urajua ambao kwa hakika hauna mashiko. Mtazamo sawa na huu unachukuliwa na riwaya teule kutokana na kile anachokirejelea Baudrillard (1983: 142-156) kama “kupotea kwa uhalisi” ambapo mpaka kati ya uhalisi na kinachodhaniwa kuwa maana yake haupo. Anachodhamiria Baudrillard (ibid) ni kuwa viashiria vimepoteza uwezo wake wa uashiriaji na kwa sababu hiyo, uhalisi haurejelei chochote kilicho nje ya kiashiria bali kiashiria hutuelekeza katika viashiria vinginevyo. Maana, hivyo basi, hubakia ikiselea kutokana na wingi wa viashiria. Hii ndiyo sababu riwaya za usasa-baadaye zikakosa muungano na muumano wa hadithi tangu mwanzo hadi mwisho ingawa huo unakuwa msingi wa kuchachawiza hadithi yenyewe inayosimuliwa. Katika Musaleo! inadaiwa kwamba sanaa ya siku hizi imefanana sana na uhalisia wenyewe wa maisha na waandishi wanafuata mkondo tu wa uhalisi huo. Mawazo haya yanachukuana
na yale ya Baudrillard, anayedai kwamba mahala pa uhalisi wa siku hizi umechukuliwa na mbinu za uashiriaji au uwasilishaji wa ukweli huo (1983: 142-156). Mjadala wa Kingunge na mhariri unafafanua zaidi uhusiano kati ya uhalisia wa maisha na sanaa sadifu ya kuuzungumzia: “[…] Uhalisi wa siku hizi umevunjikavunjika hauna pa kujishikiza; hauna mshikamano imara. Hakuna njia nyingine ya kuukabili isipokuwa kwa mtindo wa uhalisi wenyewe; hujasikia mjinga hunyolewa jinsi anavyojipaka maji? Lazima tudadisidadisi kila kitu: siasa, uchumi, mapenzi hata miundo ya hadithi pamoja na hata lugha yenyewe. Hii sio dunia ya kuridhika na tulichozoea,” alisema Kingunge. (Wamitila 2004: 41) Msimulizi katika Dunia Yaoanazungumzia hili pia: Katika simulizi na mapito yake, vipandevipande – si lazima vishikane. Unavimwaga tu vipande vyenyewe kama unaatika mbegu kwenye shamba la sanaa. Unafanya hivyo kuwaacha wasomaji waunge wenyewe vipande vya maana zao, huku maneno mengine ukiyajengea vivuli ili kuwategea makusudi watafute maana zao badala ya kuzipata maana kibungabunga. (Mohamed 2006: 9) Kwa kuwa muda wa kimajaribio umefika na kazi zenye sifa hizo kukubalika na kuchapishwa, basi msimulizi katika Dunia Yao anaeleza kile kinachokuwa kiungo muhimu cha kazi kama hizi: Naam, nilikiri. Hii ndiyo itakuwa simulizi yangu mpya katika mchanganyondimi.
Kipande hapa…kipande pale. Vipande vya ‘allegory’. Vipandevipande vya ngano mpya. Ngano ya tafrani-za-kileo katika usogori mpya. Aaaaa, ikiwa zamani sikukujua Bi Muse, sasa nakuhitaji mara milioni moja. Nataka niwe nawe pachapacha. Nikukumbatie unikumbatie, unikoleze ilhamu, nilimwambia. (Ivi: 68) Huu ni mdokezo unaotolewa na riwaya kuhusu kile kitakachopatikana humu. Tunatanabahishwa kuwa riwaya hii itakuwa ni mchanganyiko wa simulizi za kila aina na wingimatini wa “kipande hapa…kipande pale” (ibid.).
Kwa yakini, hii ni sifa inayojitokeza katika riwaya zote tatu ambazo zimenakili kazi mbalimbali za waandishi tofauti tofauti. Mimi/Wengine, Kitovu/Pembezoni: Mazingatio ya Nadharia ya Ukoloni-baadaye Kipindi mahsusi cha kustawi kwa nadharia ya ukoloni-baadayeni katika mwaka wa 1978 baada ya Edward Said kuchapisha kitabu chake cha Orientalism (Said 1978). Nadharia yenyewe inajihusisha na mambo mawili makuu yaani ukoloni-baadaye wenyewe na kazi za kisanaa zinazouhusu. Riwaya teule zinazoshughulikiwa na makala hii zimezingatia mambo yote haya mawili kwa njia tofauti. Musaleo! inagusia mada muhimu ya Said iliyomo katika Orientalism. Riwaya inazunguzmia dhana za ‘mimi’ na ‘wengine’ – mbeya mbili muhimu zinazotofautisha Umagharibi na Umashariki. Umagharibi ulihusu nchi za Ulaya na Marekani ambazo zilihusishwa na ustaarabu pamoja na maendeleo makubwa katika nyanja zote huku Umashariki ukinasibishwa na nchi zilizokuwa na umasikini uliokithiri, maendeleo duni na ushenzi. Kile ambacho Said alikirejelea kama Orient (‘WENGINE’ katika Musaleo!) na kilicholengwa na watu wa Ulaya Magharibi kilijumuisha nchi za Mashariki ya Kati pamoja na zile za watu lugha za Kisemitiki pamoja na mataifa ya Asia Kusini.
Mataifa haya, na hasa yale ya Uarabuni ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, ndiyo yaliyobeuliwa na kuonekana kama yenye dosari mbele ya macho ya wazungu wa Ulaya Magharibi (Said 1978: 99). Umagharibi nao ulichukuliwa kama kitovu cha ustaarabu na maendeleo ya kisayansi na kijamii. Hiyo ndiyo misingi anayoitumia mhusika Ukolongwe katika Musaleo! katika kujitofautisha na wanajamii: “Sasa kuanzia leo, na wala si kuanzia leo ni tangu zama na azali, kuna MIMI na WENGINE tu. Mimi ndimi msingi wa kila kitu. Mimi sio kama nyie!” (inasemwa alikuwa na rangi nyepesi na nywele zake zilikuwa mbuyembuye, ambazo hazikuiva) […] Alisema mengi lakini kufupisha habari kadai rangi yake ilikuwa bora na iliashiria ubora wa akili.
Ukolongwe alishikilia kuwa kauli zake ziliwekewa misingi imara na Sayansi [sic]. Inasemekana siku moja alitokeza hadharani huku ameshikilia kitabu kimoja kiitwacho The Wild Man’s Pedigree. Humo aliwasomea watu sehemu fulani aliyodai kuwa ilizieleza sifa zao. “Weusi: wasiochangamka, watulivu, wenye pua pana, wajanja, wazembe na wanaotawaliwa na ugeugeu!” Ajabu ni kwamba mwenyewe alikuwa na sifa hiyo hiyo ya kubadilikabadilika kama kinyonga. (Wamitila 2004: 26f; herufi za mlazo hivyo hivyo katika matini ya awali) Kinachohadithiwa katika riwaya ya Kingunge ni juhudi za wakoloni za kukuza uwingine kupitia maumbile kama vile rangi na nywele. Aidha, madai ya wakoloni kuwa wao ni bora yanajitokeza pia katika maandiko yao wanayoyaenzi kama vile The Wild Man’s Pedigree ambamo wanaendeleza propaganda kwamba wao ni bora kuliko wanajamii wengine.
Humo, twapata Waafrika wakifafanuliwa kama wenye sifa hasi za uzembe, ujanja, kutokuwa na msimamo na hata walioumbuka kimaumbile kama inavyoashiriwa na pua zao pana. Kwa upande wao, wakoloni wanajiona kama wenye rangi bora inayoashiria akili iliyopevuka, waliostaarabika na wanaofuata maadili ya kisayansi. Pamoja na kutambua hila za wakoloni, Musaleo! inajusurisha kubainisha mbinu mbalimbali zilizotumiwa na wakoloni katika kuwatawala wenyeji Waafrika. Ukolongwe, mhusika mkuu wa riwaya ya Kingunge, kwa mfano, anapiga marufuku kile alichoshindwa kukifahamu na ambacho wenyeji walikifahamu. Pia aliamrisha watoto wafunzwe nyimbo mpya, tofauti na zile walizoziimba hapo awali.
Vilevile, tunaelezwa namna alivyoiteka nyara lugha na kubadilisha maana za maneno kiasi kwamba pale panapozungumziwa ‘uhuru’ au ‘uzalendo’ wenyeji walisikia badala yake ‘kufuru’ na ‘uvundo’ mtawalia (Ivi: 26). Kwa utaratibu huo Musaleo!, kupitia kwa riwaya ya Kingunge, inaingia katika hatua ya utekelezaji wa nadharia ya ukoloni-baadaye kwa kuzingatia namna fasihi ya ukoloni-baadaye inavyoweza kuweka upenuni kwa uwazi au kwa mafumbo hila na hilaki wanazotumia watawala kwa watawaliwa (Tyson 2006: 431). Musaleo! ni zoezi la kina la uchanganuzi wa njama, hulka na athari za ukoloni mkongwe pamoja na ukoloni mamboleo wa viongozi wa zama za leo. Riwaya hii ina zoezi maalum la utekelezaji wa uhakiki wa nadharia ya ukoloni-baadaye. Humu, ukoloni mamboleo unawakilishwa na kina ‘Musaleo’ wa siku hizi, yaani viongozi, wanaotumia njama za kila aina za kuwakandamiza wale
waliowapa madaraka. Hapa na pale, riwaya hii inazungumzia kwa mafumbo namna nchi za Kimagharibi zinavyowazuga wale walioko pembezoni kama inavyobainishwa na kile kisa cha “ardhi kuwa pande kubwa lililovunjika na kuwa Godi-Wana na Huraa-Asi na mengine madogo madogo mpaka yakafikia matano” (Wamitila 2004: 89). Katika kisa hiki, kunatajwa sumaku inayozivuta ardhi mahala pamoja na yule buibui aliyesakini pale kwenye kiini ambaye aliwala nzi waliozongwa na utandu – sitiari ambazo zinafafanua mahusiano hayo ya kitovu (wenye nguvu, wakoloni au mataifa ya ulimwengu wa kwanza) dhidi ya pembezoni (wanyonge, watawaliwa au mataifa ya ‘ulimwengu wa tatu’). Nadharia ya ukoloni-baadaye haiishii katika kumlaumu mkandamizaji kama anavyodhihirisha Said katika kitabu chake Culture and Imperialism (Said 1993). Anatambua kuwa ingawa nchi za Asia, Afrika na Amerika ya Kilatini zina uhuru wa kisiasa bado zinatawaliwa na kutegemea nchi za Kizungu (Said 1993: 20). Pamoja na ukweli huo, Said anaona kwamba haifai kuzimwagia nchi za Kimagharibi lawama kwa kuwa nchi hizo zinastahili kujilaumu zenyewe kwa kutoichanganua vyema mifumo adili ya kuleta mageuzi ya dhati ya kisiasa na kitamaduni katika jamii (Said 1993: 277). Ni hapa ambapo viongozi walioshika hatamu za utawala baada ya kuondoka kwa wakoloni wakongwe waliendeleza na bado wanaendeleza uongozi wa kiimla na kuwanyanyasa wananchi wenzao. Kulingana na Said hali ilivyo baada ya ukoloni wa Kimagharibi ni aina ya mduara wa kibeberu unaoturejesha katika hali iliyokuwa wakati wa mkoloni. Bado kuna tamaa za kichoyo ambapo watu wanataka kujinufaisha kibinafsi na kuwabagua wenzao kidini, kirangi na kikabila (Said 1993: 275-276). Na hapa ndipo Nana katika Nyuso za Mwanamke anavyotaka watu waangazie kitovu na pembezoni kama chanzo cha uovu uliosakini duniani: Sikubaliani nao wanaotilia mkazo kitovu cha duara. Nguvu tunazoambiwa zimeumbwa makusudi ili wanaoishi pembezoni lazima wavutwe ndani kusujudia kitovu.
Nionavyo mimi, lazima ukingo wa duara uvunjwe ili viliyomo ndani vimiminike nje na vya nje viweze kupenya ndani kutafiti kilicho ndani na kitovu chenyewe kinachotoa fikra mbaya na ovu. Bila ya hivyo walioko pembezoni maisha watajikuta wako pembezoni – wamezugwa kabisa na maneno ya kukuza njugu maganda. (Mohamed 2010: 60) Anavyoona Nana, swala la kitovu na pembezoni ni fikra potofu iliyomo vichwani mwa watu na kwa sababu hiyo wakati umefika wa kila mtu kujituma ili kuifanya dunia kuwa mahala bora badala ya kuishi kwa visingizio vya ukoloni na athari zake mbaya. Anima na Mamanchi wa Musaleo!:Wahusika katika Saikolojia Changanuzi Musaleo! imetumia mawazo ya mwanasaikolojia Carl Gustav Jung2 hasa katika ujenzi wake wa wahusika Anima na Mamanchi. Kimsingi, Jung alidai kwamba kila binadamu, awe mke au mume, 2 Carl Gustav Jung (1895-1961) ni mwanafunzi wa Sigmund Freud na kwa mujibu wa Wamitila (2003: 298) ni mwanasaikolojia anayefahamika kwa kuendeleza dhana ya ‘ung’amuzi jumuishi’ ambayo aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo hurithiwa na kufanana kwa kila binadamu. Sehemu hii, anavyoeleza Wamitila, ndiyo huwa amebeba chembechembe za hulka za jinsia tofauti na yake. Hivyo ni kusema kwamba mwanamume huwa na sifa za kike zilizofichika katika ung’amuzibwete wake na aghalabu sifa hizo hujitokeza katika umbo la msichana bikira au mwanamke mwenye sifa za kiungu na ambaye hufahamika kama Anima. Vivyo hivyo, mwanamke naye huhodhi sifa za kiume katika ung’amuzibwete wake na hudhihirika katika umbo la kikongwe mwenye busara aitwaye Animus (Carter 2006: 79). Kudhihirika kwa wahusika hawa huwa katika ndoto na ishara mbalimbali na wanasaikolojia huamini kuwa wahusika hawa huwa njia ya kuimarisha tabia ya mtu binafsi ambayo huwa imeficha mawazo na mitazamo hasi (Schmitz 2007: 200).
Mawazo ya Jung yanabainika ndani ya riwaya hasa tunapozingatia uhusika wa Anima na Mamanchi na jinsi wanavyomdhihirikia Mugogo Wehu. Wote wanatokea pale Mugogo anapokunywa sumu aliyotegewa na watu wasiojulikanana kupoteza fahamu nyumbani mwake, ingawa Mugogo mwenyewe alihisi machovu na hivyo kujilaza kitandani (Wamitila 2004: 8). Yote anayoyafanya Mugogo ndani ya hadithi kwa hakika si mambo yakinifu bali yanatokea ndani ya ‘ndoto’ anayoipata katika ‘usingizi’ huu – yakiwemo kukutana kwake kwanza na Anima, na kisha, Mamanchi. Akiwa katika ndoto yake kuu, Mugogo anakutana kisadfa na Anima (Ivi: 28). Kukutana kwao kwa hakika si kwa kisadfa kama anavyodai Mugogo mwenyewe bali ni njiamaalum inayotolewa na riwaya kwa msomaji ya kuona wasiwasi na hofu zilizofichika katika ung’amuzi bwete wa Mugogo. Tangu mwanzoni mwa riwaya, tayari msomaji ameshamuona Mugogo kama mhusika anayeishi maisha yaliyojaa shauku, hofu na wasiwasi mwingi. Kwa mfano, alikuwa na yakini kuwa aliusikia mlio wa bunduki na kushuhudia kishindo cha vijana waliokimbilia huku na huko ili wazinusuru roho zao. Kisha akawaona vijana waliopigwa risasi nje ya nyumba yake ambao wanatoweka kimiujiza (Ivi: 1). Yote haya yanamfanya atoke kwa azma ya kufanya uchunguzi iwapo aliyoyashuhudia ni ya kweli. Anachohadithiwa huko nje ni tofauti na watu wanamdhania kuwa mwehu.
Anashauriwa apuuze yasiyomhusu kwani hakuna aliyesikia bunduki anazozungumzia Mugogo (Ivi 6). Anaporudi nyumbani kutoka ulevini, ndipo “anapojipumzisha kitandani” (Ivi: 8) ilhali ukweli ni kuwa makali ya sumu aliyokuwa ametiliwa yalikuwa yamekolea na kumfanya apoteze fahamu. Hapo ndipo riwaya inapomdhihirisha Anima kama mhusika ambaye, katika misingi ya Jung, anajitokeza kamanjia mbadala ya kutufunulia wazi wazihofu na wasiwasi aliokuwa nao Mugogo akilini mwake. Mbali na hayo Anima wa Musaleo!, kama alivyo Anima wa Jung, pia ni mwanamke na Mugogo anaelekea kuathirika naye kimapenzi kama anavyolazimishwa akiri hilo na Mamanchi ambaye awali anajitambulisha kama “siri ya Mashamba ya Mawe” (Ivi: 22): inayohodhi vikale ambavyo hujitokeza kwa njia ya ishara na ndoto. Wahusika wake wa kisaikolojia, Anima na Animus, ni vielelezo vya visakale anavyozungumzia na ambavyo vimo katika ung’amuzi jumuishi wa kila binadamu.
“Mugogo, unamjua Anima?” Nitakosaje kumjua mtu kama huyu jamani? Alikuwa rafiki yangu wa kike; mwanamke mwenye ujasiri mkubwa na mapenzi yasiyojua kukimwa. (ibid.) Katika safari yake kwenda katika shamba la mawe, Anima anajitokeza tena – wakati huu katika umbo la mhusika Mamanchi. Katika njozi hii ambayo Mugogo anapata ufumbuzi wa mambo mengi kupitia Mamanchi, Anima sasa si msichana tena bali ni mwanamke mkongwe, mwenye busara na anayejua mambo mengi. Aidha, Mamanchi ana sifa za kiungu, sawa na zile zilizozungumziwa na Jung. Mamanchi, kwa mfano, amezaliwa akafa, akazaliwa akafa, na akazaliwa upya (Ivi: 60). Anamfahamisha Mugogo katika ziara yao ya shamba la mawe hila na vituko vinavyotumiwa na kina ‘Ukolongwe’, jina tunaloweza kulichambua kama kifupi cha ‘ukoloni mkongwe’ na kina Musaleo au viongozi wa siku hizi katika kuendeleza utawala wao wa kiimla. Weledi wa mambo alionao Mamanchi kuhusu vitimvi vya wakoloni wakongwe na wakoloni mamboleo unaelekea kumtanza Mugogo. Mapenzi na ufahamu wa Mamanchi kwake unamkumbusha uhusiano maalum aliokuwa nao na Anima kiasi cha kumfanya Mugogo ashuku kuwa Mamanchi na Anima ni mtu mmoja anapouliza: “Mbona sauti yako inafanana na ya mtu ninayemjua?” Mamanchi: Nani? Anima! Mamanchi: Anima ni mimi pia! Mimi naye ni sawa! (Ivi: 86) Kumbe Anima na Mamanchi ni wamoja ingawa wamejitokeza katika maumbo tofauti: Anima akiwa msichana huku Mamanchi akiwa ajuza. Kinachounganisha umbile lao, hata hivyo, ni msaada mkubwa unaotokana na ukweli na uthabiti wao kwa Mugogo Wehu katika kuuelewa ulimwengu unaoelekea kumtanza.
Kupitia wahusika hawa, Mugogo anatoa harara zake, shida, hofu na kupata mtazamo wa maisha. Mwishoni anaporejelewa na fahamu zake, tunamwona akiwa kiumbe tofauti na vile alivyokuwa hapo awali ingawa hayo yanadokezwa kwa mafumbo na Msimulizi: Ung’amuzi wa mambo wa Mugogo Wehu umepiga hatua kubwa. Macho ambayo alishindwa kuyafungua jana ameyafungua. Ameweza hata kusema mambo kadha. (Ivi: 100) ‘Kufungua’ na ‘kufunga’ macho kunakorejelewa hapa kunahusiana na kule kuzindukana kwa Mugogo Wehu kutoka lindi la kutofahamu (kupoteza kwake fahamu) ambako kulielekea kumtia woga hadi hali ya matumaini (kufungua macho) kama inavyoashiriwa na uwezo wa ‘kusema mambo kadha’.
Hitimisho hili linawafiki uhakiki wa ki-Jung kwa jinsi linavyoagua hofu, wasiwasi na jumla ya mitazamo hasi iliyofichika katika ung’amuzibwete hadi kuleta satua kwa waathiriwa, wakiwemo Mugogo Wehu. Hitimisho Mapitio ya riwaya za Dunia Yao, Nyuso za Mwanamke na Musaleo!yamebainisha wazi kwamba fasihi ni nyenzo mbadala, tena ya kiubunifu, ya kuzizungumzia nadharia za fasihi kwa njia ya ukakamavu zaidi. Uaguzi wa makini wa nadharia za fasihi katika riwaya teule umeziweka kazi hizi katika medani ya kipekee ya kuzungumzia mambo ambayo yangepatikana katika matini mahususi za nadharia za fasihi. Miongoni mwa mambo mengine mengi, riwaya hizi, kwa ustadi, zimeatika mawazo ya wananadharia mbalimbali wa fasihi wakiwemo wanaumaumbo wa Kirusi, wanaumuundo, wanaudenguzi na hata wanasaikolojia changanuzi katika bunilizi za Kiswahili. Wahakiki, walimu na wapenzi wa fasihi wanaweza kuzitumia riwaya husika kama matini za kiziada katika somo la nadharia.
ukakamavu zaidi. Uaguzi wa makini wa nadharia za fasihi katika riwaya teule umeziweka kazi hizi katika medani ya kipekee ya kuzungumzia mambo ambayo yangepatikana katika matini mahususi za nadharia za fasihi. Miongoni mwa mambo mengine mengi, riwaya hizi, kwa ustadi, zimeatika mawazo ya wananadharia mbalimbali wa fasihi wakiwemo wanaumaumbo wa Kirusi, wanaumuundo, wanaudenguzi na hata wanasaikolojia changanuzi katika bunilizi za Kiswahili. Wahakiki, walimu na wapenzi wa fasihi wanaweza kuzitumia riwaya husika kama matini za kiziada katika somo la nadharia.
Marejeleo - Barry, Peter. 2002. Beginning Theory. Manchester: Manchester University Press.
- Baudrillard, Jean. 1983. Simulations. New York: Semiotext(e).
- Bertoncini, Elena. 2006. Globalization Unmasked in Two Kiswahili Novels. Makala ya Kongamano la Kimataifa la Jubilei ya TUKI – 2005, ed. by Seleman S. Sewangi & Joshua S. Madumulla. Dar es Salaam: TUKI, pp. 84-94.
- Burman, Erica&Magie MacLure. 2005. Deconstruction as a Method of Research. Research Methods in the Social Sciences, ed. by Bridget Somekh & Cathy Lewin. New Delhi: Vistaar Publications, pp. 284-292.
- Carter, David. 2006. Literary Theory. Reading: Cox & Wyman.
- Eagleton, Terry. 1996. Literary Theory: an Introduction. Oxford: Blackwell Publishing.
- Habib, Rafey M.A. 2005. A History of Literary Criticism. Malden: Blackwell Publishing
- Khamis, Said A.M. 2003. Fragmentation, Orality and Magic Realism in Kezilahabi’s Novel “Nagona”. Nordic Journal of African Studies 12(1): 78-91.
- Khamis, Said A.M. 2008. Nadharia, Ubunifu, Uchambuzi na Taaluma ya Kiswahili. Nadharia katika Taaluma ya Kiswahili na Lugha za Kiafrika, ed. by Nathan O. Ogechi, Naomi L. Shitemi & K. Inyani Simala. Eldoret: Moi University Press, pp. 3-23.
- Lyotard, Jean-François. 1984. The Postmodern Condition. A Report on Knowledge. Trans. Geoff Bennington and Brian Massuni. Minneapolis: University of Minnesota Press.
- Mohamed, Said Ahmed. 2006. Dunia Yao. Nairobi: Oxford University Press.
- Mohamed, Said Ahmed. 2010. Nyuso za Mwanamke. Nairobi: Longhorn Publishers.
- Mwamzandi, Issa Y. 2007. Utandawazi na Teknolojia ya Mawasiliano katika Umalenga wa Waswahili: Mfano wa Sitiari za Taarab. Kiswahili na Elimu Nchini Kenya, ed. by Kimani Njogu. Nairobi: Twaweza Communications, pp. 68-82.
- Mwamzandi, IssaY. 2011. Derridean Thought in Practice: an Examination of the Kiswahili Proverb. Journal of Intra-African Studies 5: 1-14. Said, Edward. 1978. Orientalism. New York: Pantheon Books.
- Said, Edward. 1993. Culture and Imperialism. London: Chatto and Windus.
- Schmitz, Thomas A. 2007. Modern LiteraryTheory and Ancient Texts: an Introduction.
- Malden: Blackwell Publishing. Tilak, Raghukul. 1993. History and Principles of Literary Criticism. New Delhi:
- Rama Brothers Educational Publishers. Tyson, Lois. 2006. Critical Theory Today. New York:
- Routledge & Taylor and Francis. Wafula, Richard & Kimani Njogu. 2007. Nadharia za Uhakiki wa Fasihi. Nairobi: Jomo Kenyatta Foundation.
- Waliaula, Ken W. 2010. Uhalisia na Uhalisiamazingaombwe: Mshabaha kati ya Dunia Yao na The Tin Drum. Swahili Forum 17: 143-157.
- Wamitila, Kyallo W. 2003. Kamusi ya Fasihi: Istilahi na Nadharia. Nairobi: Focus Books. Wamitila, KyalloW. 2004. Musaleo!. Nairobi: Vide-Muwa.
|
|
|
UHAKIKI WA KITABU: ADUI WA UMMA |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 03:44 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
UHAKIKI WA KITABU: ADUI WA UMMA
1.REKODI ZA KIBIBLIOGRAFIA
Jina la kitabu kinachohakikiwa hapa ni: Adui wa Umma.
Kitabu hiki ni tafsiri ya “Enemy of the People”, kilichoandikwa na Henrik Ibsen, miaka zaidi ya miamoja iliyopita. Kimetafsiriwa na Elias K. Maarugu.
Mchapishaji wa tafsiri hii ya kiswahili ni EK International Publishers na amekipa namba ifutayo katika sekwensia ya vitabu duniani (ISBN): 9987 8824 12.
Kimechapishwa 1992 kikiwa na kurasa 95.
Na anayekihakiki sasa hivi ni mimi Padri Privatus Karugendo.
II. UTANGULIZI
Adui wa Umma ni tafsiri ya mchezo wa kuigiza ujulikanao kwa jina la “An Enemy of the People”. Mchezo huu ulitungwa mnamo mwaka 1882 na Henrik Ibsen wa Norway, na umetafsiriwa katika lugha ya Kiswahili na Ndugu Elias K.Maarugu, mnamo mwaka 1982; miaka mia moja baadaye. Mchezo wenyewe una maonyesho matano. Onyesho la kwanza ni sebuleni mwa Dk. Stockmann, onyesho la pili ni kama lile la kwanza. Onyesho la tatu ni Ofisini mwa mhariri wa Gazeti la The Herald.Onyesho la nne ni chumbani katika nyumba ya Kapteni Horster na onyesho la tano ni chumba cha faragha cha Dr.Stockmann. Wahusika katika mchezo huu ni: Dk.Thomas Stockmann, ambaye ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji, Bibi Katherine Stockmann, ambaye ni mke wa Dk. Stockmann, Petra, ambaye ni binti wa Dk.Stockmann na ni mwalimu wa shule, Eilif na Morten, ambao ni watoto wa kiume wa Dk.Stockmann, Peter Stockmann, ambaye ni kaka wa Dk.Stockmann na ni Meya wa Mji, Mkuu wa Mgambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Hamamu, Morten Kil, ambaye ni mmilikaji wa Viwanda vya ngozi na ni babamkwe wa Dk.Stockmann, Bwana Hovstad, ambaye ni mhariri wa gazeti la “The Herald”,Bwana Billings, ambaye ni mhariri msaidizi, Kapteni Hoster ambaye ni Kapteni Mkuu wa meli, Bwana Aslaksen ambaye ni mchapishaji mkuu wa mitambo ya magazeti na kuna kundi la wanaume na wanawake wa mchanganyiko kimaslahi na wanafunzi wachache. Maonyesho ya mchezo yanachukua siku nne mfululizo za mwanzoni mwa majira ya vuli mwaka 1882, Mji mmoja kando ya Bahari Kusini mwa Norway. Katika aya zifuatazo nitatoa muhtasari na tathmini ya mchezo, lakini baada ya kudokeza mazingira yanayoitangulia tafsiri hii ya kiswahili.
III. MAZINGIRA YANAYOKIZUNGUKA KITABU. (TAFSIRI YA KISWAHILI).
Bwana Elias K.Maarugu, alifanya kazi ya kutafsiri kitabu hiki mnamo mwaka 1982, lakini kwasababu ya kushindwa kupata pesa za uchapaji, alikaa na muswada kwa kipindi cha miaka 10! Mwaka 1991, Bwana Maarugu, aliombwa na Mama Keti Kamba, ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa UWT enzi hizo, amwakilishe katika warsha ya Elimu ya Mazingira.Warsha hiyo ilimwezesha Bwana Maarugu, kukutana na Bw.Peter Martin, ambaye alikuwa Afisa Elimu Mfawidhi (World Wide Fund WWF for nature UK). Bw.Peter Martin, katika risala yake ya kuelezea umuhimu wa warsha hiyo ya elimu ya mazingira, kwa wanawarsha, aligusia maudhui yanayojitokeza katika kitabu cha Isben “An Enemy of the People”, kwa kutoa mfano jinsi ambavyo maslahi binafsi ya wanasiasa wenye uroho wa fedha, yanavyoweza kuvuruga mipango ya miji na kuleta maafa kwa masuala ya mazingira siku za uzoni. Bwana Maarugu, alitumia mwanya huo kuongea na Bw.Peter, juu ya mswada wa Adui wa Umma, alikokuwa amekaa nao zaidi ya miaka kumi bila kuchapishwa. Kuanzia hapo mwanga mpya wa kukichapisha kitabu ulipatikana.Bw.Peter, kupitia WWF, alitoa pesa za kuchapa kitabu cha Adui wa Umma. Pesa zilizotolewa, ziliweza kuchapisha vitabu elfu tano. Ingawa kitabu hiki kilichapishwa mwaka 1992, sasa ni zaidi ya miaka kumi, kitabu hiki hakijasambaa nchi nzima. Hakipatikani kwenye maduka ya vitabu.Bwana Maarugu, nafikiri aliamua kukisambaza yeye mwenyewe na bila shaka kazi ilikuwa ngumu kwake. Hivyo anayekitaka kitabu hiki, amtafute Mheshimiwa Maarugu, Mkuu wa Wilaya ya Mishenye –Kagera. Nami nilipata bahati ya kukipatakitabu hiki nilipomkuta Bwana Maarugu, Magu, akiwa mkuuu wa Wilaya. Lakini pia kwa vile sasa hivi watu wanajadili mswada wa Habari, ni vyema watu wakakisoma kitabu hiki wakaona jinsi mapambano na Ya Jamii, Serikali na Waandishi wa habari, yalivyo ya siku nyingi. Pia mtu anaweza kuona vizuri ugumu wa kuwa mhariri wakati mwenye gazeti anatetea maslahi binafsi.Mchezo huu umetungwa zaidi ya miaka miamoja iliyopita lakini ujumbe wake ni waleo hii! Baada ya maelezo haya sasa tuone kitabu chenyewe kwa muthasari.
IV. MUHTASARI WA KITABU
Adui wa Umma ni mchezo wenye vitendo vitano.Ni mchezo wenye dhamira za kisiasa.Aidha unatokana na mgogoro kati ya msema kweli mmoja aitwaye Dk.Stockmann, na Meya wa Manispaa, Peter Stockmann.Kwa kifupi ni kwamba, Manispaa hii ilikuwa imejenga “hamamu” kwa ajili ya shughuli za starehe na utalii.Mradi huu ulibuniwa na Dk. Stockmann na Peter Stockmann, Meya wa Manispaa.Matokeo ya mapato haya yalikuwa makubwa kwa wakazi wote wa jiji: kulikuwa na nafuu ya kodi kwa wananchi, na viongozi walifurahia matunda ya kazi yao. Kwa bahati mbaya, kulijitokeza magonjwa Fulani ambayo, Dk.Stockmann, Bwana Afya wa Manispaa, alidhani kuwa yanatokana na maji ya “Hamamu”. Alifanya uchunguzi na kuthibitisha jambo hilo.Uchafu uliokuwa unatoka kwenye kiwanda cha ngozi ulikuwa unaingia kwenye mabomba yaliyokuwa yakielekea kwenye “hamamu”. Dk.Stockmann, alichukua hatua za kuwaeleza viongozi wenzake. Meya wa jiji hakupendezwa na ukweli huo.Dk Stockmann pia, alishauri mabomba yatolewe yalipo na yatandikwe upya.Hali kadhalika ushauri huu haukukubaliwa na Meya.Basi watu hawa walikubaliana kutokukubaliana. Dk.Stockmann alisimama upande wa utaalam wake na ukweli.Naye Meya Peter Stockmann aliuona ushauri na msimamo huo wa ukweli kama shambulizi la moja kwa moja kwa uongozi wake na yeye binafsi. Mvutano huu ulisababisha mapambano kadhaa.Dk.Stockmann, alitarajia kuchapisha ripoti ya uchunguzi wake katika gazeti la “The Herald”.Hakufaulu kwani gazeti hili lilimilikiwa na kufadhiliwa na ongozi wa manispaa.Kuchapisha ripoti hiyo kungesababisha kufungwa kwa gazeti hilo. Uwanja mwingine wa mapambano ulikuwa mkutano wa hadhara. Pande zote mbili zilieleza tatizo hili. Dk. Stockmann alikuwa akisema ukweli.Hakusikilizwa na badala yake alizomewa na kudhihakiwa, kitu ambacho kilisababisha kugawanyika.Upande wa Peter Stockmann ulikuwa ukimshitaki Dk.Stockmann, kuwa ni shabiki, mchafuzi wa amani ya umma na kwa hiyo ni adui wa umma. Swali ambalo lingekuwa la kwanza kuulizwa ni hili: ni nani kweli adui wa umma? Dk. Stockmann au Peter Stockmann? Je adui wa umma ni yule anayeamua kusema ukweli na kufichua aibu na mizizi ya magonjwa katika jamii, au yule ambaye ni mnafiki, anayeficha uozo kwa ajili ya kulinda maslahi yake binafsi ya kikazi.Je adui wa umma anaweza kuwa ni yule mwenye nia ya kuondoa maovu, rushwa, ujinga na uongo, umaskini na uchafu uliomo katika Jamii? Hadi mwisho wa mchezo tunamwona Dk,Stockmann akisimama peke yake na akisimamia ukweli mtupu bila ya kujali kama anaungwa mkono na watu wengine au la!Kwa maneno yake mwenyewe anasema hivi: Dk, Stockmann: “ Ndiyo,- uvumbuzi wenyewe ni huu –mwanaume shupavu duniani ni yule anayeweza kutetea msimamo wake peke yake hata kama haungwi mkono… uk 92” Katika kusema na kutetea ukweli Dk. Stockmann,alikuwa na changamoto nyingi.Yeye na kaka yake Peter Stockmann, walibuni hamamu.Na kweli zikawa kitegauchumi cha mji.Mapato ya mji yalipanda sana na wenyeji wa mji walipunguziwa kodi.Ukweli kwamba hamamu hizo zilikuwa na wadudu wanaosababaisha magonjwa ya binadamu kungesababisha kufungwa kwa hamamu, Na kuporomoka kwa mapato.Meya wa mji ambaye alikuwa kaka yake Dk.Stockmann, angeingia matatani na labda kupoteza umeya.Alimtaka mdogo wake kuuficha ukweli ili kulinda cheo chake!!Na kulinda kipato cha mji.Mabishano yao yalikuwa hivi: Peter Stockmann: Ndiyo maana unafanya juu chini kuhakikisha kuwa unapokonya mji huu chanzo pekee cha kujipatia mapato,sivyo? Dk. Stockmann: Hi huelewi? Chanzo chenye sumu, bwana! Umekuwa mwehu? Tunaendesha shughuli za utalii kwa kuuza uchafu na maradhi; kwa nini ustawi wa maisha yetu utokane na uongo… uk36. Peter Stockmann: Hizo ni ndoto tupu na za hatari.Mtu ye yote ambaye anaweza kutoa ushauri wa kupotosha kama huu kuhusu mji wake si mtu wa amani, bali ni adui wa umma…uk36 Meya wa mji ambaye ni kaka yake Dk.Stockmann, alimtishia kumfukuza kazi kama angefichua ukweli wa vijidudu kwenye maji ya hamamu. Alimshauri akae kimya kuwasikiliza wakubwa zake: Peter Stockmann: Kwa kuwa u mtumishi wa kamati, huna haki ya kufuata mawazo yako binafsi…. Si katika wadhifa wako wa kikazi.Ungalikuwa mwananchi wa kawaida, hili lingekuwa jambo jingine. Lakini maadamu u mfanyakazi mwenye madaraka ya chini, huna haki kutoa mawazo ambayo yanapinga na yale ya wakubwa wako..uk.33 Changamoto nyingine kubwa iliyokuwa mbele ya Dk.Stockmann, ni kwamba vile viwanda vya ngozi vilivyokuwa vikizalisha uchafu uliokuwa uaingia kwenye mabomba ya hamamu vilikuwa vya Baba mkwe wake, Bwana Morten Kil. Kufichua ukweli wa uchafu huo ilikuwa ni kupiga vita viwanda vya Baba Mkwe wake.Bwana Morten Kil, alikuwa ameandika urithi wake kwenda kwa binti yake; mke wa Dk Stockmann na watoto wake. Sasa alikuwa akitumia urithi huo kumzuia Dk. Stockmann, kusema ukweli: Morten Kil: Na jana usiku ulisema kwamba kiwanda chagu cha ngozi ndicho kinaongeza uchafu. Kama hivyo ndivyo iliyo, basi baba yangu, na babu, wamekuwa na wanautia mji huu uchafu kwa karne nzima.Kama malaika watatu waharibifu.Huwezi ukafikiri kwa dakika moja tu kwamba sitavumilia kashafa ya namna hiyo ikivumishwa dhidi yangu bila kuchukua hatua yoyote- unafikiri hivyo?… uk 84 Morten Kil: Vema, sina budi kuondoka.Lakini lazima unifahamishe kwa njia moja ama nyingine.Na iwapo hutafanya hivyo, hisa zote zitakwenda kwenye misaada ya huru mchana huu…uk 85. Pamoja na shinikizo la Baba Mkwe, kwamba Dk,Stockmann, akae kimya ili apate urithi wa viwanda vyenye kuzalisha uchafu na vijidudu – alikataa na kuendelea na mpango wake wa kusema ukweli.Mke wake alijaribu kumshawishi.Alimkumbusha kwamba wana watoto watatu.Wawili walikuwa bado wanasoma shule. Akifukuzwa kazi – wangeshindwa kuwasomesha. Lakini Dk.Stockmann, alisimama kidete: Dk. Stockmann: Kate! Umepagawa! Yaani kwa sababu mtu ana mke na watoto watatu aongope kutangaza ukweli, kuwa raia wa manufaa- asitimize wajibu wake katika maisha..uk.50 Marafiki zake wahariri wa gazeti la “The Herald, waliogopa kuchapisha makala yake.Gazeti hili lilimilikiwa na kufahdiliwa na uongozi wa manispaa. Wangechapisha makala ya Dk. Stockmann, hamamu zingefungwa na uchumi wa mji ungekwenda chini.Kodi ingepanda.Watu wangeacha kununua magazeti.Na gazeti lingefungwa.Hivyo wahariri hawakuangalia ukweli.Walizingatia mishahara na maslahi yao binafsi! Binti mkubwa wa Dk. Stokmann, Petra, alifukuzwa kazi, kwa sababu ya ukweli wa baba yake.Alikuwa anafanya kazi ya ualimu.Watoto wake wawili wavulana walifukuzwa shuleni walikokuwa wanasomea.Yeye mwenyewe Dk.Stockmann, alifukuzwa kazi na kufukuzwa kwenye nyumba na kupachikwa jina la Adui wa Umma. V. Tathmini ya kitabu. Bwana Elias K.Maarugu, alifanya kazi nzuri ya kuutafsiri mchezo wa Ibsen, “An Enemy of the people” katika lugha ya kiswahili. Ni imani yangu kwamba watu wakiusoma mchezo huu wa Adui wa Umma.Tutagundua kwamba Adui wa Umma si Dk.Stockmann, bali kaka yake Peter na viongozi wengine wa Manispaa.Adui wa Umma ni wahariri wa magazeti wanaoogopa kuandika ukweli ili kulinda biashara yao. Mchezo huu ni wa maana kwetu, ukizingatia kwa sasa hivi viongozi na wanasiasa wanatanguliza maslahi binafsi na wanakuwa na uroho wa fedha, hii inaweza kuvuruga mipango ya miji yetu na kuleta maafa kwa masuala ya mazingira siku za usoni.Watu wanagawiwa viwanja vya kujenga majumba ya makazi na mahoteli bila kujali hifadhi ya mazingira.Vyanzo vya maji vinaharibiwa.Mahoteli yanajengwa bila mpango kwenye ufukwe wa babari. Ingawa mchezo huu umetungwa zaidi ya miaka 100, lakini unafaa sana kwenye mazingira ya leo na hasa hapa Tanzania, kama nilivyodokeza mwanzoni, ni kwamba sasa hivi kuna muswada juu ya vyombo vya habari.Pia tumeshuhudia kila siku matumizi mabaya ya vyombo vya habari, tumeshuhudia jinsi wahariri waliyotumiwa vibaya ili kulinda maslahi ya wenye vyombo hivyo. Tunalilia uzalendo.Mchezo huu, unaonyesha mfano wa mtu mzalendo.Mtu huyu ni Dk.Stockmann, anasimama kidete, hadi anapoteza kila kitu kwa kusimamia ukweli.Watoto wake walipofukuzwa shule, aliamua kuwafundisha yeye mwenyewe akisaidiana na binti yake mkubwa Petra: Dk.Stockmann: Na tutaanzisha shule yetu katika chumba kilekile walimoniita mimi adui wa Umma.Lakini nyinyi wawili tu hamtoshi hatuna budi tuwe na vijana kama kumi na wawili wa kuanzia… Vema! Baadaye mtaenda mitaani mkawalete mtakao waona.Kwa majaribio tutaanza na watoto wa ombaomba – kwa safari mmoja tu – matokeo yanaweza yakawa ya kufurahisha-uk.92 Mtoto mmoja aitwaye Morten, aliuliza swali kwa baba yake: Lakini Baba tutafanya nini baada ya kukua na kuwa wenye mawazo mapana na walio mashujaa..Uk 92, Dk.Stokmann: Wafukuzeni hawa mbwa mwitu wote…92.
Hata hapa Tanzania, kazi ya wanamapinduzi, kazi ya wazalendo na kizazi cha leo, ni kuwafukuza mbwa mwitu wote. Wale wote wanaoshughulikia maslahi binafsi bila kuaanglia maslahi ya taifa zima, ni lazima wafukuwze kabisa! Hivyo mchezo huu ni muhimu kwetu sote maana anayesema viongozi wanakula rushwa ndiye anaonekana kuwa adui wa umma.Kila msema kweli hapa kwetu ni adui wa umma. Na wasema ukweli wote wanapata mashinikizo kama ya Dk. Stockmann.Mashinikizo ya kaka, dada, mjomba, wanandugu, wanaukoo, wakwe, kabila, ukanda hadi kwa wanamtandao.Na yeyote anayetoa shinikizo kwa msema ukweli, anaangalia maslahi yake na tumbo lake.Haweki mbele maslahi ya watu wengine na ustawi wa taifa zima.Kwa maneno mengine Adui wa Umma, ni adui wa matumbo ya watu wachache wanaopenda kuneemeka kwa gharama ya maisha ya watu walio wengi.
VI. HITIMISHO.
Pamoja na pongezi zangu kwa Bana Maarugu, ningependa kuwahimiza watanzania kukizoma kitabu hiki, maana kuna mengi ya kujifunza na kulinganisha na yale yanayotokea katika taifa letu. Mfano mtu akifanya utafiti juu vipodozi, akasema vipodozi ni hatari kwa ngozi, kwamba vipodozi vinasababisha magonjwa ya ngozi na hata kasa.Wenye viwanda vya vipodozi, wenye maduka na wenye salooni, watamnyoshea kidole mtafiti huyo na kumpachika jina la adui wa umma.Wenye salooni, viwanda na maduka ya vipodozi wanashirikiana kwa karibu sana na viongozi wa serikali – na wakati mwingine ni mali za viongozi.Hivyo ukweli wa usalama wa vipodozi hautegemei mtafiti.Unategemea tamko la serikali.Mtafiti akikazana kuonyesha ukweli- atanyoshewa kidole na kupachikwa jina la Adui wa Umma. Gongo ni pombe ya hatari.
Ni sumu tupu na hatari kwa afya ya binadamu.Inatengenezwa kienyeji na vyombo vinavyotumika kuitengeneza kama mapipa yenye kutu na mirija iliyotengenezwa kwa vyuma si salama.Hapa Tanzania, tuna sheria ya kuzuia pombe hii ya gongo.Sheria hii imekuwa kama pazia la maafisa watendaji wavijiji na mapolisi kujipatia hongo.Watu wanaendelea kunywa gongo na kujaza sumu mwilini.Mtu akijitokeza na kupendekeza sheria ya kuzuia gongo ifutwe- atanyoshewa kidole na kupachikwa jina la Adui wa Umma.Kuzuia gondo ni kuziba riziki: polisi ameangalia hapo, mtendaji pia!Watu wanasomesha watoto, wanajenga nyumba na kumili mashamba makubwa kwa kutumia pesa ya gongo.Wanastawi kwa kuuza na kueneza sumu katika jamii. Kuna mifano mingi inayoonyesha jinsi maadui wa Umma, wanavyoshughulikia maslahi binafsi na kulitelekeza taifa. Wao wanajiona wanafanya vizuri, na kuwageukia watetezi wa ukweli kuwa wao ndo maadui wa umma.Pia ningependa kumshauri Bwana Maarugu, afanye mipango ya kukisambaza kitabu hiki.Kukiacha vunguni mwa kitanda, ni sawa na kusema alifanya kazi bure maana kitabu kilicho vunguni hakiwezi kusambaza maarifa katika jamii.
|
|
|
UHAKIKI WA RIWAYA YA ROSA MISTIKA |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 03:35 PM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
Hakiki riwaya ya Rosa Mistika (Euphase Kezilahabi) kwa kutumia nadharia ya U-Marx.
Katika utangulizi tutaanza kuelezea maana ya nadharia kutokana na wataalam mbalimbali walivyoielezea, tutaangalia maana ya U- marx kutokana na wataalam mbalimbali. Na tutajikita katika kuelezea misingi ya uhakiki wa ki-marx, kwa kutumia misingi hiyo tutahakiki riwaya ya Rosa Misitika na mwisho tutamalizia nahitimisho.
Nadharia ni dhana iliyofafanuliwa na wataalam mbailimbali kama ifuatavyo:-
Wafula na Njogu(2007) wanaeleza kuwa nadharia ni “jumla ya maelekezo yanayomsaidia msomaji au mhakiki kuifahamu kazi ya fasihi kwa kufuata utaratibu maalumu.” TUKI (2004) wanasema nadharia ni “mawazo, maelezo au muongozo ili kusaidia kueleza,kutatua na kutekeleza jambo fulani.” Hii ina maana kuwa msomaji kupitia nadharia anapata uwezo wa kufahamu mambo mengi kwa undani ambayo anaweza kuyatumia katika kazi yake ya kifasihi.
Hivyo basi nadharia ni taalumu inayojishughulisha na uchambuzi na uchanganuzi juu ya asili au mwazo wa kitu au jambo fulani.
Dhana ya U-marx imeelezwa na wataalamu mbalimbali kama ifuatavyo;Wamitila (2006) anasema U-marx ni falsafa ya kiyakinifu hasa kwakuwa pana msisitizo mkubwa kwenye msingi wa hali za kiyakinifu za maisha kama mazingila ya kuishi kuliko mawazo katika maisha ya binadamu. Ikimaanisha kwamba mawazo yake hayategemezi kwenye dhana dhahania kama urembo,ukweli au ndoto bali anayategemeza kwenye uhalisia unaonekana. Nadharia ya U- marx ilianzishwa na Karl Marx mwaka 1818-1863 na Fredrick Engles mwaka 1820-1895.
Katika kutekeleza nadharia ya U-marx kuna misingi ya kufuata ili kuhakiki kazi za kifasihi kwa ufasaha. Moja, misingi hiyo ni historia ya maisha ya binadamu inayoweza kuelekeza katika misingi yakinifu ya kiuchumi; ambayo itachunguza njia ya uzalishaji mali pamoja na miundo ya kiuchumi inayo athiri uzalishaji mali na usambazaji wa mali hizo. Pili, kuamini kuwa historia ya kibinadamu inadhihirisha au kuakisi harakati zinazo endelea katika matabaka ya kiuchumi-jamii; matabaka hayo yapo katika ngazi ya familia, dini na elimu na tatu, ubepari kama njia ya uzalishaji mali na mara nyingi huharibiwa na tabaka la chini.
Kulingana na misingi ya kimarx, tunaweza kuhakiki Riwaya ya Rosa Mistika iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi kama ifuatavyo:-
Suala la dhuluma na unyanyasaji; unyanyasaji ni kitendo cha mtu mwenye nguvu au shirika fulani kuwakandamiza watu wasio na nguvu katika familia au jamii fulani inayowazunguka nadhuluma ni kitendo cha mtu au watu kunyimwa haki zao za msingi. Kupitia msingi wa nadharia ya ki-marx inaonesha suala la ubepari kwamba ni jumuisho katika suala la dhuluma na unyanyasaji. Mwandishi anawatumia wahusika Flora, Stella, Honorata, Sperantia na Emmanuel walivyodhulumiwa kwa kunyang’anywa vitu vyao vyote baada ya wazazi wao kufariki. Katika uk.96, msanii anasema:-
“Hawa jamaawalirithi. Walirithi hawajamaa. Walirithi, walirithi. Jamaa waligawanavitu. Walirithi kila kitukilichokuwa ndani ya nyumba. Walirithi michungwa namiembe. Walirithi migomba yote. Walirithi paka nambwa. Walirithi majaniyaliyokuwa juuya paa, namiti yote, iliyofanya nyumba isimame. Walirithi mashamba yote. Walirithi kuku, kweli walirithi. Lakini hapakuwa namtuhata mmoja aliyeweza kusema atamchukua mtoto fulani amtunze.”
Vilevile msanii anaonesha suala la unyanyasaji kwa kumtumia mhusika Regina anavyonyanyaswa na mumewe. Mfano katika riwaya ya Rosa Mistika suala la unyanyasaji limejitokeza katika sehemu ya kwanza uk. 3 mwandishi anaposema:
‘‘Lakini Regina tanguaolewe hakuwa na raha ;alikuwa akisumbuliwa nakuteswa na mumewe kwa kosalisilo lake.”
Wanawake wengi katika jamii zetu wamekuwa wakinyanyaswa na waume zao kwa kupigwa na kupewa majukumu yote ya familia bila ya kusaidiwa na waume zao.
Nadharia ya u-marx inazungumzia suala la unyanyasaji na dhuluma kuwa ni tatizo kubwa katika jamii hasa katika kufanya maendeleo ya kijamii ili jamii iweze kujikomboa kiutamaduni, kisiasa na kiuchumi. Vilevile suala la uongozi mbaya, uongozi mbaya ni kitendo cha viongozi kushindwa kukidhi mahitaji ya watu wake. Pia suala hili la uongozi mbaya ni moja kati ya suala zima la ubepari ambalo huleta mikururo katika jamii, hivyo mwandishi anaonesha uongozi mbaya kwa kumtumia mhusika Deogratias pale anapo kuwa anatumia cheo chake vibaya kwakuwa kandamiza watu. Uk. 41mwandishi anasema:-
“Zaidi ya hayo,Deogratias alikuwa mmoja katiya wale watu watumiaovyeo vyao napesa kwakutaka chochote wapendacho.” “…Nasikia alikwisha wapa mimba watoto wawiliwa shule? Ndiyo, lakinialiwapa shilingi wasimseme. Walitaja vijanawengine waliokuwa wakisoma nao.” Pia suala la uongozi mbaya lipo hata katika jamii zetu kwani kuna baadhi ya viongozi ambao hutumia nafasi zao kufanya vitu visivyostahili katika jamii mfano rushwa ya ngono, matumizi mabaya ya fedha za serikali. Katika nadharia ya U-marx inasema kwamba ili jamii iondokane na uongozi mbaya ni lazima jamii ipambane kuondoa uongozi mbaya.
Pamoja na hayo suala la migogoro mwandishi amelionesha; migogoro ni mvutano au ukinzani baina ya mtu na mtu au pande mbili. Migogoro imegawanyika katika makundi mbalimbali mfano migogoro ya kinafsi, mtu na mtu, mtu na serikali au jamii yake. Katika riwaya hii mwandishi anaonesha jinsi jamii ya watu wa Ukerewe wanavyokumbwa na mikururo katika jamii hiyo. Mwandishi anamtumia mhusika Rosa anavyokua na mgogoro na baba yake kutokana na malezi aliyokuwa anapewa na baba yake. Katika uk. 58 mwandishi anasema:-
‘’Zakaria alipata maneno yote: maneno aliyopaswa kuambiwa siku ile……Rosa tangu leo wewe simototo wangu. Tangu leo wewesi baba yangu. Rosa alidakia bilakukawia. Aliingiamara moja ndani ya motakaana kwendazake Beach. Siku hiyo Rosa hakurudi nyumbani.”
Suluhisho la mgogoro huu ni Rosa kuondoka na kutokurudi nyumbani.
Mgogoro mwingine ni kati ya Regina na Zakaria kutokana na suala la ulevi wa Zakaia ambae ni mume wa Regina. Uk. 4. Mwandishi anasema:-
‘’Mwanzoni haya yalikuwa yakizunguka kichwani mwake aliposikiasauti kwa mbali: Hoi! Hoi! Hoi! Alifahamu. Alifahamu huyo mtu alikuwa naninaalikuwa katikahali gani: sauti hiyo alikwishaizoea.’’ Mgogoro huu haukupatiwa suluhisho kwani Zakaria aliendelea na tabia yake ya ulevi mpaka mauti yalipomchukua.
Vilevile mwandishi anaonesha mgogoro wa nafsi kwa kumtumia mhusika Rosa, baada ya kukataliwa kuolewa na Charles. Mwandishi anasema; “Ha! Rosa, kweli wewe ulikuwa bikira! Unafikiri baada ya kufahamu kwamba ulichezewasana huko Morogoro,na baada yangu mimi mwenyewekuona bonde la ufanakuliona hilo sikio,unafikiri mimi ninaweza kukuoa! Ha! Dada yangu,sahau.’’uk 90
Suluhisho la mgogoro huu ni Rosa kuchukua maaamuzi ya kujiua.
Kwa mujibu wa ki-marx migogoro haina budi kuwepo katika jamii na ni lazima pawepo migogoro ndani ya jamii yeyote, hivyoni lazima itafutiwe suluhisho ili kuleta maendeleo. Vilevile suala la matabaka; matabaka ni utofauti uliopo kati ya mtu na mtu au jamii na serikali.
Katika jamii kuna matabaka ya aina mbili ambayo ni tabaka la juu na tabaka la chini katika mfumo wa uzalishaji mali yaani kiuchumi,kisiasa na kiutamaduni. Mwandishi anaonesha suala hili jinsi linavyojidhihirisha wazi kati ya wenye nacho na wasio nacho mfano familia ya Zakaria hawa ndio wasionacho uk.38, mwandishi anasema:-
‘’…Walianza kufikiri, akija atalala wapi? Mgeni-mkubwa na mwenye heshima namna hiyokulala naye ndani ya nyumba moja isiyo na vyumba vingi lilikuwajambo la aibu.” Pamoja na hayo wapo wenyenavyo ni kama vile Mkuu wa wilaya Deogratus uk.41, “Nasikia alikwisha wapa mimba watoto wawiliwa shule? Ndiyo, lakinialiwapa shilingi wasimseme. Walitaja vijanawengine waliokuwa wakisoma nao.” Watawala mfano kiongozi Mkuu wa wilaya uk. 58 na watawaliwa ni Zakaria na Ndalo.
Tatu,matabaka kati ya wasomi na wasiosoma, wasomi kama Rosa,Stella na Charles, wasiosoma ni Regina uk. 46. Suala hili la matabaka katika jamii zetu bado linaendelea, hivyo kwa mtazamo wa kimarx unatoa pendekezo kuwa ili jamii ijikomboe na matabaka lazima ifanye mapinduzi. Vilevile suala la uzalishaji mali, uzalishaji mali huo unaweza kuwa katikanyanja za kiuchumi,kisiasa, kiutamaduni na kijamii .Mfumo wa uzalishaji mali kwaujumla huzingatia katika uletaji maendeleo ya mtu binafsi au nchi kwa ujumla. Katika riwaya hii mwandishi anaonesha jinsi mhusika Zakaria navyoshindwa kufuatilia vitu ambavyo vinaweza kumkomboa yeye pamoja na familia yake badala yake anaendekeza ulevi ambayo siyo njia sahihi ya uzalishaji mali. Katika uk. 17, mwandishi anasema:-
‘’Aaa! Aaa! Pombe ilikuwa ya kutuua. Hivi tulikunywa chupa ngapi? Zakaria aliuliza. Mimi nakumbuka tulikunywa chupa kumi.” Kitendo hiki hata katika jamii zetu bado kipo kwani watu wengi hujihusisha na masuala ya ulevi kuliko kujihusisha na masuala ambayo ni tija katika uzalishaji mali.
Hivyo ili mhakiki wa kazi za kifasihi aweze kufanya kazi yake vizuri ni lazima atumie nadharia zaidi ya moja ili aweze kuhakiki vipengele vyote vya fani na maudhui, kwani kipengele kimoja hakiwezi kujitosheleza katika kuhakiki kaziya kifasihi.
MAREJELEO
Kezilahabi, E. (2011). Rosa Mistika. Nairobi: KenyaLiterature Bureau
TUKI. (2014). Kamusi ya Kiswahili Sanifu. Dar es salaam: O.U.P East Africa Limited.
Wamitila, K. (2002). Uhakiki waFasihi, Misingi na Vipengelevyake. Mombasa: Phoenix Publishers Limited.
|
|
|
ODC : MUHADHARA WA KUMI NA NANE : FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 03:32 PM - Forum: Nukuu
- No Replies
|
|
MUHADHARA WA KUMI NA NANE
FANI NA MAUDHUI KATIKA FASIHI
18.1 Utangulizi
Katika muhadhara huu utasoma vipengele vya fani na maudhui na jinsi vinavyohusiana.
Madhumuni ya Muhadhara
Baada ya kumaliza kusoma muhadhara huu, utaweza : - Kufafanua vipengele vya fani na maudhui.
- Kuhusianisha vipengele vya fani na maudhui
18.2 Fani na Maudhui
Fani katika kazi za fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia mwandishi kufikisha ujumbe kwa jamii aliyokusudia. Fani inahusisha mambo yafuatayo; Muundo, Mtindo, Matumizi ya lugha, Wahusika naMandhari. Maudhui katika fasihi ni yale mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu mawazo hayo. Nayo,yaliyomsukuma mtunzi kutunga na kusana kazi fulani ya sanaa. Pia katika maudhui kuna falsafa ya mwandishi.
Kuna mitazamo miwili inayojadili uhusiano wa fani na maudhui. Mitazamo hiyo ni mtazamo wa kidhanifu na mtazamo wa kiyakinifu.
Mtazamo wa kidhanifu ni ule unaoona kuwa fani na maudhui ni vipengele ambavyo havina uhusiano wowote, kwamba vinaweza kutenganishwa. Wataalamu kadhaa wanalinganisha fani na maudhui na kikombe cha chai. Kikombe kinachukuliwa kama ndiyo fani na upande mwingine chai iliyomo ndiyo maudhui. Mnywaji wa chai hiyo analinganishwa na wasomaji wa kazi ya fasihi.
Vilevile wanafafanua kuwa fani na maudhui hulinganishwa na chungwa ambalo lina sehemu ya nje na ndani. Maudhui ya kazi ya fasihi yanalinganishwa na nyamanyama za chungwa na fani ni sehemu ya nje (ganda). Kwa ufupi hawa wanaona kuwa fani ni umbo la nje la kazi ya fasihi na maudhui ni umbo la ndani.
Mtazamo huu una udhaifu wake (mkubwa) na unaweza kuwachanganya wasomaji. Kwa sababu hauonyeshi ama kuwakilisha ukweli wa mambo juu ya uhusiano uliopo kati ya fani na maudhui katika kazi ya fasihi.
Mtazamo wa kiyakinifu unaeleza vizuri ukweli wa mambo ulivyo. Ni kwamba vitu hivi viwili hutegemeana na kuathiriana na wala havitazamwi katika utengano.
Wanafasihi wenye mtazamo huu, wanalinganisha fani na maudhui na sura mbili za sarafu moja, na si rahisi wala sahihi huzitenga na kuzieleza katika upweke, bila kuhusisha upande mmoja na nyingine. Sura moja ya sarafu ikikosekana, basi sarafu hiyo haiwezi kuwa na hadhi ya kisarafu. Jambo la muhimu ni kuona jinsi kitu kimoja (fani) kinavyoweza kukikamilisha kingine (maudhui).
Wanafasihi hawa wanaonesha kuwa kila kimoja cha kigezo cha fani na maudhui kimo ndani ya chenziwe, kushirikiana na kuathiriana katika ama kijenga vizuri au kubomoa kazi ya sanaa.
Kama kazi ya fasihi itakuwa na fani duni, lakini maudhui yake ni mazuri basi hata maudhui yaliyokusudiwa hayatatoa ujumbe unaokusudiwa ipasavyo. Mfano mzuri ni riwaya ya kikasuku zilizoandikwa baada ya Azimio la Arusha zinazojadili dhamira ya ujenzi wa jamii mpya kama vile Shida, Mtu ni Utu, Ufunguo Wenye Hazina, Njozi za Usiku, Ndoto za Ndaria n.k. zilisisitiza zaidi maiudhui na kuupuzia kipengele cha fani.
Vile vile kama maudhui ni duni na fani ni bora, pia jamii itapata hasara ya kufikiwa na maudhui yasiyo na maana. Mfano mzuri ni riwaya pendwa zote zimeweka msisitizo kwenye fani na kusahau kipengele cha maudhui. Katika riwaya pendwa kama vile riwaya za upelelezi , mapenzi na uhalifu, zina wahusika ambao hawaaminiki kwani wanapewa sifa ambazo si rahisi kuziona kwa binadamu wa kawaida. (Toa mifano ya riwaya hizo).
Fani na maudhui ni vitu viwili ambavyo huwiana, hutegemeana hatimaye kuathiriana. Uhusiano huo ndio unaojenga kazi bora ya fasihi. Msanii hutumia vipengele mbalimbali vya maudhui katika kuijenga fani na hutumia vipengele mbalimbali vya fani katika kujenga maudhui.
18.3 Vipengele muhimu vya fani na maudhui vijengavyo kazi ya fasihi andishi.
Katika fasihi andishi, fani hujumuisha vipengele vifuatavyo:
Kwanza ni muundo ambao ni mpangilio na mtiririko wa matukio toka mwanzo hadi mwisho. Hapa tunaangalia jinsi msanii alivyounda na alivyounganisha tukio moja na linguine, kitendo kimoja na lingine sura na sura, ubeti na ubeti n.k. Katika hadithi na Tamthiliya muundo unaweza kuwa wa moja kwa moja (Msago), wa Kioo (Rejeshi) au wa rukia. Katika ushairi muundo unaweza kuwa wa Tathnia, Tathlitha, Tarbia au Sabilia.
Pili, Mtindo, ambao ni upangaji wa fani na maudhui katika kazi ya fasihi andishi kwa njia ambayo hatimaye huonesha nafsi au labda upekee wa mtungaji wa kazi hiyo. Katika riwaya, mtindo unaweza kuwa na masimulizi, monolojia au doyolojia na katika tamthiliya mtindo wake ni dayolojia (majibizano). Katika ushairi mtindo unaweza kuwa wa kimapokeo au wa kisasa.
Kipengele cha tatu ni wahusika ambao hutumiwa na msanii kufikisha ujumbe kwa jamii yake. Katika hadithi na Tamthiliya kuna wahusika wakuu, wadodo (wasaidizi) na wajenzi. Wahusika wakuu na wadogo wanaweza kuwa wahusika bapa, mviringo (duara) au shinda (wafoili).
Kipengele kingine ni matumizi ya lugha, ambayo mwandishi hutumia kuyaibusha mawazo yake katika kazi hiyo. Vipengele vya lugha wanavyotumia sana ni: - Matumizi ya semi – Misemo, Nahau, Methali, Misimu, Mafumbo n.k.
- Matumizi ya tamathali za semi
- Matumizi ya mbinu nyingine za kisanaa
- Matumizi ya taswira
- Matumizi ya ucheshi
Pia kuna Kipengele cha Mandhari hii ni sehemu ambapo matukio muhimu ya kazi ya fasihi hutokea. Mandhari inaweza kuwa ya kubuni au ya kweli. Katika masimulizi mengi ya kihistoria mandhari yake ni ya kweli na kazi za kubuni mandhari yake ni ya kubuni.
Kipengele kingine ni jarada kazi za fasihi huwa na michoro au picha na hata rangi kwenye majarada yake.Inawezekana majarada hayo yakawa na uhusiano na dhamira au maudhui ya kazi zinazohusika.Picha hizi huweza kuwa kielekezi muhimu cha fani kwenye uchambuzi wa kazi ya kifasihi.mfano picha za majarada ya Nyota ya Rehema ya M.S.Mohamed,Kufa Kuzikana ya K.Walibora,Babu alipofufuka ya M.S.Mohamed na Bina-Adamu ya K.W.Wamitila na nyingi nyinginezo Hata hivyo ni muhimu kutambua kuwa sio kazi zote za kifasihi ambazo zinaonesha uwiano kati ya majarada yake na yaliyomo.
Vipengele vya maudhui, kipengele cha kwanza ni dhamira.
Dhamira ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi andishi. Dhamira hutokana na jamii. Katika dhamira, kuna dhamira kuu na dhamira ndogo ndogo.
Kipengele cha pili ni mtazamo wa mwandishi. Hapa ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe. Mtazamo wa msanii unaweza kuwa wa kiyakinifu au wa kidhanifu.
Kipengele kingine ni msimamo wa mwandishi ambayo ili hali ya mwandishi kuamua kufuata na kushikilia jambo fulani. Jambo hili linaweza kuwa halikubaliki na wengi, lakini yeye atalishikilia tu.
Msimamo wa msanii ndio unaosababisha kazi ya sanaa iwe na mwelekeo maalum na hata kutofautiana na kazi za wasanii wengine.
Kipengele cha nne ni falsafa ya mwandishi. Ambao huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza kuamini kwa mfano “Mungu hayupo”.
Maadili na ujumbe ni kipengele kingine cha maudhui.Katika fasihi andishi, ujumbe ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kusoma kazi Fulani ya fasihi andishi.
Mwisho, migogoro, ambayo ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi. Katika migogoro tunapata migogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao, matabaka yao n.k. na migogoro hii mara nyingi hujikita katika mahusiano ya jamii. Migogoro yaweza kuwa ya kiuchumi, kiutamaduni, kisiasa na kinafsia.
18.4 Wahusika katika Fasihi ya Kiswahili
Wahusika ni watu, ama viumbe waliokusudiwa wawakilishe tabia fulani za watu katika kazi za fasihi ..
Mitazamo mbalimbali juu ya Mhusika ni nani?
Jonathan Culler katika kitabu chake cha Structural Poetics anasema kuwa uhusika ni kipengele cha msingi katika riwaya, kwani kila tukio lipo ili kumfafanua mhusika na maendeleo yake. Naye Barthes katika kitabu hichohicho anasema kuwa mhusika ni kitu kilichochorwa kwa fikra (maneno) kwa msingi wa vielelezo vya kitamaduni, kwa maana kwamba mhusika wa fasihi ya jamii fulani ataeleweka vizuri na kwa urahisi zaidi na jamii hiyo husika.
Nao Kasper na Wuckel wanasema kuwa mhusika ni picha ambayo huchorwa na fasihi, na ni kiini cha vyote vipya, dhamira na mada za fasihi: Wanaendelea kudai kuwa katika mhusika kuna uwili: kwanza kuna usawiri wa kisanaa na mtu kwa upande mmoja, na sura ya mtu kwa upande mwingine. Yaani, katika mhusika kuna hali ya welekeo binafsi (subject) na uhalisi (object). Aidha, dunia ni ghala ya wahusika wa namna mbalimbali kwa fikra, hisia na utendaji, na hayo ndiyo yanayosababisha maendeleo tofauti.
Aristole akizungumzia mwigo katika utanzu mkuu wa zama zake, yaani tanzia, alisema kuwa mhusika hufunua uadilifu na kuonyesha lipi zuri baya, kwani tanzua tanzia ni mwigo wa watu.
Naye Hegel, alisema kuwa mhusika ni kitovu katika usawiri wa kisanaa, na anapaswa kutazamwa katika utatu huu:
- Kama mtu binafsi mkamilifu;
- Kama mtu katika upekee;
- Kama mtu mwenye tabia maalum iliiliyojijenga ndani yake.
Karl Marx na F rederick Engels, kwa kutumia upembuzi wa kiyakinifu, walikubaliana na Hegel kuhusu umuhimu wa mhusika, isipokuwa utatu wake usiangaliwe katika ombwe, bali katika mazingira yake kama ifuatavyo:
- Kama mtu binafsi, kwa sababu ni zao la upekee usioweza kujirudia;
- Kama mtu tabaka, kwa sababu ni kiwakilishi cha kijamii kinachosimamia tabaka, au kikundi maalum na maendeleo maalum ya kipindi cha historia;
- Kama mtu jamii, kwa sababu ni mtu mwenyewe sifa za mtu na za kijamii.
Sifa mbili ni bayana, kwani hujionyesha kupitia matendeo. Lakini sifa ya tatu ni ya kidhahania, au ya kufikirika.
Kutokana na ufafanuzi huu mhusika, tunaona kuwa wahusika ni watu au viumbe katika kazi ya fasihi waliokusudiwa kuwakilisha tabia za watu katika maisha halisi. Wahusika katika hadithi za mapokeo na baadhi ya hadithi fupi, kwa kawaida huwa ni wanyama, wadudu, mimea, mashetani, miungu, n.k. kama ndio wahusika wakuu. Kitabia, wahusika hawa hugawika katika makundi makubwa ya ubaya na wema. Katika riwaya, hasa zile za mwanzomwanzo (za akina Shaaban Robert, Mathias Mnyampala na Faraji Katalambullah), uundaji wa wahusika uliathiriwa na ule wa hadithi za kimapokeo. Lakini wahusika katika riwaya halisi huwa ni wahusika halisi wanaoendana kwa karibu sana na maisha ya kila siku kwa sura yao, mavazi yao, lugha yao, na hulka yao kwa ujumla. Na kitabia, hawagawanyiki kwa urahisi katika makundi mawili, bali huwa na tabia mchangamano: hawana sifa za uungu na kuwa wazuri moja kwa moja, wala hawana sifa za shetani wakawa wabaya mia kwa mia.
Je, ni jambo gani huwezesha mabadiliko ya mhusika? Sababu ya msingi ni kule kujitokeza kwa wajibu mpya wa fasihi kutoka kipindi kimoja hadi kingine unaotelekezwa na ukweli wa maisha, kwa njia ya mahusiano ya kijamii. Mhusika wa kipindi cha ukoloni hawezi kuwa na wajibu sawa na mhusika wa kipindi cha baada ya Azimio la Arusha; wala kamwe hawezi kuwa sawa na Yule wa baada ya kufia kwa uchumi huria.
AINA ZA WAHUSIKA KATIKA FASIHI
Hawa ni wale ambao wanajitokeza kila mara katika kazi ya fasihi tangu mwanzo hadi mwisho. Wahusika hawa hubeba kiini cha dhamira kuu na maana ya hadithi yote. Vituko na matendo yote hujengwa kuwahusu ama kutokana nao. Mara nyingi jambo hili limewafanya wahusika wakuu wa kazi za fasihi wawe “midomo” ua wasanii. Wawe vipaza sauti vya Watungaji. Wahusika Wakuu hasa wa riwaya na tamthiliya huchorwa na Wasanii kwa mapana na marefu ya maisha na tabia zao ili kuukamilisha unafsi wao. - Wahusika wadogo/wasaidizi
Hawa hujitokeza hapa na pale katika kazi ya fasihi ili kuukamilisha ulimwengu wa kazi hizo. Hawa husaidia kujenga dhamira flani katika kazi ya fasihi, lakini mradi dhamira hiyo ni ndogo, basi hata wahusika hao tutawaita kama ni wadogo. Wakati mwingine husaidia kuijenga dhamira kuu ya kazi ya kazi ya fasihi, lakini, kwa sababu nafasi yao ni ndogo sana katika kuutoa msaada huo, basi hawa tunawaita wahusika wadogo.
Hawa ni wahusika ambao wamewekwe ili kuikamilisha dhamira na maudhui fulani, kuwajenga na kuwakamilisha. Wahusika hawa wawili; yaani wahusika wakuu na wahusika wasaidizi.
Wahusika wakuu na wadodo tunaweza kuwaweka katika makundi makuu matatu:
Hawa ni wale wasiobadilika kitabia au kimawazo kulingana na mazingira au matumio ya wakati wanayokutana nayo. Wahusika bapa tunaweza kuwagawanya kwenye makundi mawili:
Wahusika Bapa – Sugu – hawa wanakuwa sugu katika hali zote, kiasi amacho hata tunapowaona mahali pengine hali zao ni zilezile, hawahukumiwa bali wao huhukumu tu, hawashauriwi bali wao hushauri tu, madikteta, mfano Bwana Msa katika riwaya za M.S. Abdalla ni mmoja wa wahusika hawa.
Wahusika Bapa – Vielelzo – Ni wale ambao pamoja na kutobadilika kwao, wamepewa majina ambayo humfanya msomaji aielewe tabia na matendo yao. Shaaban Robert alikuwa fundi sana katika kuwaumba wahusika wa aina hii, akina Majivuno, Adili, Utubusara n.k. Hapa msanii anatilia mkazo tabia moja inayotawala, kiasi ambacho anaondoa sehemu nyingine zote za sifa za mhusika huyo.
Hawa ni wahusika ambao wana desturi ya kubadilika kitabia, mawazo au kisaikolojia. Maisha yao yanatawaliwa na hali halisi za maisha. Hivyo wanavutia zaidi kisanii, kwani wanasogeza hadithi ielekee kwenye hali ya kutendeka au kukubalika na jamii. Mfano ni: Rose (Rosa Mistika), Josina (Pepo ya Mabwege).
Hawa wako katikati ya Wahusika bapa na wahusika duara. Hawakuja kama wahusika duara, lakini ni hai zaidi kuliko wahusika bapa. Tofauti kubwa kati ya wao na wahusika wengine ni kwamba wahusika shinda wanawategemea wahusika duara au wahusika bapa zaidi ili waweze kujengeka. Wanaendeshwa na mawazo ya wahusika wengine. Kwa mfano, katika riwaya za M.S. Abdalla, Najum ni mhusika shinda.
|
|
|
ETIMOLOJIA YA MANENO 'ADUI', 'ADAWA' NA 'UADUI' |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 03:30 PM - Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili
- No Replies
|
|
HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO 'ADUI', 'ADAWA' NA 'UADUI'
Neno adui (wingi: maadui) katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo:
1. Nomino: Mtu, mnyama au kiumbe chochote kinachofanyia kiumbe kingine uovu.
Kuna methali: adui wa mtu ni mtu, adui mpende, adui aangukapo mnyanyue.
2. Nomino: Mtu unayekabiliana naye katika mchezo.
3. Nomino: Jambo, kitu au hali inayokuletea madhara.
Kuna msemo: Ujinga ni adui wa maendeleo.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adui (soma: aduwwun/aduwwan/aduwwin عدو ) ni nomino yenye maana ya "mwenye uadui, chuki au hasama dhidi mwengine."
Neno adawa katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana ya:"hali ya kufanya chuki dhidi ya mtu mwengine."
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili adawa (soma: adaawatun/adaawatan/adawaatin عداوة ) lina maana zifuatazo:
1. Nomino: Hali ya kufanyianana uadui, chuki na hasama baina ya pande mbili au zaidi.
2. Nomino : Chuki,
Ama neno ' uadui ' limetoholewa kutoka neno ' adui ' na kupewa maana zifuatazo:
1. Hali ya kufanyiana mambo mabaya baina ya watu wa pande mbili.
2. Hali ya watu kuchukiana na kutendeana maovu.
3. Ukosaji huruma, tabia ya kutenda mambo ya ukatili.
Neno hili uadui kwa maweko yake, si neno la Kiarabu.
Kinachodhihiri ni kuwa maneno adui (soma: aduwwun/aduwwan/aduwwin عدو) na adawa (soma: adaawatun/adaawatan/adaawatin عداوة) yalipoingia katika lugha ya Kiswahili na kutoholewa kuwa maneno adui na adawa maana zake za msingi katika Kiarabu hazikubadilika.
Shukran sana.
Khamis S.M. Mataka.
|
|
|
ODC : MUHADHARA WA KUMI NA TISA: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 03:26 PM - Forum: Nukuu
- No Replies
|
|
ODC : MUHADHARA WA KUMI NA TISA: UHAKIKI WA KAZI ZA FASIHI
19.1 Utangulizi
19.2 Mhakiki ni nani?
Mhakiki ni mchambuzi na mfafanuzi wa maandishi ya sanaa hasa yale ya kifasihi. Ni jicho la jamii kwa vile katika kazi za fasihi anagundua mazuri pamoja na hatari iliyomo. Huyu ni bingwa wa kusoma na kuchambua maudhui, maadili na ujumbe uliomo katika maandishi ya fasihi.
19.3 Sifa za Mhakiki
Mhakiki anatakiwa ajue historian ya mazingira yaliyomkuza mwandishi. Mhakiki ili aweze kuifanya kazi yake anapaswa aelewe vema historia ya mwandishi na jamii yake inayohusika. Aelewe asili ya mwandishi, historia yake na utamaduni wake kwa ujumla. Kutokana na hali hii, mhakiki anaweza kuelewa kama mwandishi amefanikiwa kueleza ukweli wa maisha ya watu yaani jamii inayohusika.
Mhakiki anatakiwa kuelewa histori na siasa ya jamii inayohusika. Hii itamwezesha kuyaelewa matatizo ya jamii hiyo. Mhakiki lazima aifahamu barabara jumuiya ambayo mwandishi aliandika juu yake ili aweze kuandika uhakiki imara, ama sivyo atakwama na kuandika uhakiki dhaifu. Mhakiki anapaswa kuelewa historia ya watu ambao maandishi yao hayo yanawahusu, bila kuifahamu historia yao, itakuwa vigumu kwake kueleza bayana baadhi ya mambo ambayo mwandishi aliandika na kwa nini aliandika hivyo. Uhakiki wake ukisomwa na watu wanaoishi katika jamii hiyo si ajabu kusema yeye si mhakiki. Mhakiki, huangalia jinsi gani mwandishi ameiwakilisha hali halisi ya jumuiya na historia ya watu hao.
Mhakiki ni muhimu awe amesoma kazi mbalimbali za fasihi na siyo ile tu anayoifanyia uhakiki. Hii itamsaidia kuwa na ujuzi zaidi katika uwanja wa uhakiki.
Mhakiki anatakiwa asome tabakiki za wahakiki wengine katika uwanja wa fasihi na hata nje ya jamii yake ili kupata upanuzi zaidi katika kazi ya uhakiki. Hii itamsaidia kutoa tahakiki bora zaidi kwani atakuwa amejifunza yale yaliyo mazuri na kuepuka makosa waliyofanya wengine.
Mhakiki lazima awe na akili pevu sana ili aweze kung’amua mambo na akishayang’amua ayaandike kwa lugha rahisi ili mawazo yake yasomeke na kila mtu kwa urahisi, yaani atumie lugha ambayo itawatumika wasomaji wake.
Mhakiki lazima ajiendeleze katika taaluma mbalimbali ili aweze kuwa na mawazo mengi ambayo yatamsaidia kuhakiki maandishi mbalimbali.Mhakiki hodari huichonga jamii yake kimawazo. Huiimarisha isitetereshwe au kupofushwa na waandishi wapotoshi.
Mhakiki anapaswa kuwa na uwezo wa kuchambua mambo kisayansi bila kutonesha hisia za wasomaji. Asiwe na majivuno na awaheshimu anaowahakiki na anaotaka wasome uhakiki wake, asichukie au kusifia tu kazi za waandishi kwa sababu zake binafsi bila kueleza ukweli wa kazi hiyo. Mhakiki ni rafiki wa mwandishi na wasomaji. Kwa hiyo, mhakiki lazima awe fudi katika kutoa hoja zake na lazima ziwe zinagonga, zenye kuibua udadisi na kuathiri.
Mhakiki anapaswa asiwe mtu wa kuyumbishwa na maandishi au maeneo ya wahakiki au watu wengine. Tunategemea asme kweli kuhusu kazi hiyo. Mahusiano baina ya mhakiki na mwandishi yasiathiri uhakiki wake.
Mhakiki anapaswa awe na uwezo wa kutumia mkabala sahihi kulingana na kazi anayoifanyia uhakiki. Mikabala humwongoza mhakiki kuchambua vema kazi za fasihi.
19.4 Dhima za Mhakiki
Kuchambua na kuweka wazi funzo linalotolewa na kazi ya fasihi. Hapa mhakiki anatoa ufafanuzi wa kimaudhui wa kazi ya fasihi. Mhakiki husoma kwa uangalifu kazi ya fasihi, baada ya kusoma kwa makini, hutafakari na kuchunguza maudhui, Maadili , na ujumbe ambao mwandishi amekusudia kuwafikishia wasomaji wake na jamii inayohusika.
Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi. Mhakiki huwasaidia wasomaji ili wasishindwe kuyaelewa maudhui barabara kutokana na kukakanganywa na usanii, matumizi, mathalani ya Ishara na baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kumkanganya msomaji ambaye hajapata utaalamu mkubwa wa kuchambua. Mhakiki kwa kufichua ishara Fulani ina maana kuwa amemsaida msomaji kupata ujumbe kikamilifu.
Kuhusu matumizi ya picha, kwa kawaida, lugha ya picha ina mguso sana na huibua hisia aina na hata kuchekesha au kuwafanya watu walie machozi. Mhakiki sharti awambie kwamba, matumizi ya picha ni mbunu mojawapo inayosaidia maudhui kuwaganda wasomaji. Picha inayochekesha, kufurahisha, kukejeli n.k. haikomei pale tu kwani baada ya kucheka n.k. msomaji huathiriwa sana kinafsia na aghalabu huachiwa funzo fulani. Hivyo mhakiki lazima achambue na kuiweka wazi funzo ambalo linatolewa na picha hiyo.
Mhakiki ana dhima ya kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora zaidi. Mhakiki anamfundisha mwandishi juu ya yale anayoyasema yanavyoweza kupokelewa na jamii. Humwonesha msanii uzuri na udhaifu wa kazi aliyosaini kitendo hiki humfanya anavyoelekezwa na mhakiki, na hivyo humfanya awe na nafasi nzuri ya kuirekebisha kazi hiyo atakapoishulikia kazi nyingine. Kwa msingi huo mhakiki anaweza kulaumu au kusifu/ kumpongeza mwandishi wa kazi yoyoe ya kisanaa.
Mhakiki ana dhima ya kumwelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila dira ya mhakiki. Mhakiki huifunza jamii (wasomaji) namna ya kupokea na kuifurahia kazi ya sanaa. Vilevile mhakiki huwasaidia wasomaji kuyabaini maandishi yaliyo sumu kwa jamii. Mhakiki lazima ayafichue maandishi hayo ili yasieneze sumu kwa jamii inayohusika.
Mhakiki ni kiungo muhimu kati ya jamii na msanii. Mhakiki ndiye anayeitambulisha na kuelezea kazi ya msanii kwa hadhira. Vile vile mhakiki huchukua mawazo ya wasomaji na kuyapeleka kwa mwandishi. Humtahadharisha msanii kuhusu makosa aliyoyafanya katika kuikabili kazi yake na wakati huo huo anaionesha jamii udhaifu uliomo katika kazi hiyo ya fasihi.
Mhakiki ana dhima ya kukuza kiwango cha utunzi na usomaji wa kazi ya fasihi. Kutokana na ushauri anaoupata mwandishi kutoka kwa mhakiki, humfanya awe makini zaidi wakati wa kushughulikia kazi nyingine. Vile vile wasomaji wanakuza kiwango chao cha usomaji kwa kufuata mawaida ya mhakiki.
Mhakiki ana dhima ya kusema wazi kuhusu kiwango cha maandishi anayoyahakiki.Akisema wazi kwamba maandishi hayo yako katika kiwango cha chini, mara mwandishi huyo asilia atakapoamua kutunga tena, atashawishika kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu zaidi. Na waandishi wengine watapatiwa msukumo wa kuandika maandishi yaliyo kwenye kiwango cha juu pia. Na hivi ndivyo mhakiki anavyosaidia kukuza na kuendeleza maandishi ya taifa lake.
Mhakiki ana dhima ya kumsaidia msomaji kuyabaini maandishi yaliyosumu kwa jamii. Mhakiki sharti aseme wazi ayafichue maandishi ya namna hiyo. Kuna maandishi ambayo huwachekesha na kuwaburudisha wasomaji sababu yameandikwa kwa namna hiyo, na kumbe yaneneza sumu, na maandishi haya yanazorotesha maendeleo ya jamii, hivyo mhakiki huyafichua maandishi kama haya.
Mwisho, mhakiki anatakiwa kuheshimu na kuthamini kazi za waandishi na kuzifanyia haki. Jambo la msingi (lazima) kuzingatia ni kwa mhakiki afayapo kazi yake huwa vitani. Mhakiki anapaswa kujua namna ya kuwanasa wasomaji bila wao kujitambua na kuwa na uwezo au kuchambua kisayansi mambo bila kutonesha hisia za wasomaji. Anatakiwa asiwe na majivuno na aheshimu anaowahakiki na anaowataka wasome uhakiki wake, awachukue hatu kwa hatua kifalsafa hata waone vigumu, na haiwezekani kupingana naye.
Kwa kuhitimisha, mhakiki ni mtu muhimu sana katika kazi za fasihi. Kazi ya sanaa ya uandishi ni kama chakula kilichokwishapikwa na kuungwa vizuri. Uhakiki ni sehemu mbalimbali za ulimi zenye kuifanya jamii ikubali utamu wa chakula hicho; uchungu au ukali wa chakula hicho na igundue uchungu wa chakula hicho au ukali wake.
19.5 Uhakiki wa Fasihi
Nkwera (2003) amechunguza na kuona kwamba mara nyingine mhakiki hulazimika kulinganisha kazi za kifasihi. Kazi hizo zinaweza kuwa zinafanana au zinatofautiana. Ulinganisho huo utazingatia vipengele vyote vya fani na maudhui. Mhakiki anatazamiwa aone ubora au upungufu katika kazi na jinsi zinavyozidiana.
Vigezo vinavyotumiwa katika kulinganisha kazi za fasihi ni vile vile vya ukweli, uhalisi na umuhimu. Vigezo hivyo vitapima dhamira, ujumbe, falsafa, wahusika na matumizi ya lugha.
Uhakiki wa kazi za fasihi unajumuisha kuzingatia kazi hiyo kwa kuisikiliza au kuisoma; kuchambua vipengele vya fani na maudhui vinavyoijenga kazi hiyo. Hatimaye mhakiki atatoa maoni kuhusu ubora au ubaya wa kazi hiyo na hukumu ya kazi ipi bora kuliko nyingine.
VIPENGELE VYA UHAKIKI 1. MAUDHUI
- FANI
Katika kuyahakiki maudhui ya fasihi, zingatia yafuatayo:
(i) Soma na uielewe habari nzima, kisha uieleze kwa muhtasari.
(ii) Itambulishe hadhira au wazo kuu la mchezo husika kwa sentensi mbili au tatu.
(iii)Onesha mapendekezo au mawaidha ya mwandishi, msimamo na mtizamo wake wa mambo kutokana na mchezo huo.
(iv) Chunguza falsafa ya maisha ambayo mwandishi anaielezea: k.m. Je, mwandishi anaelezea hali halisi ya maisha au ni nadharia tu za uchawi au ni maisha ya njozi yasiyo na ukweli ndani yake?, nk.
(v) Ainisha matatizo na migogoro inayojitokeza katika mchezo huo na sababu zake.
(vi) Mtambulishe mhusika mkuu katika mchezo mzima.
(vii) Onesha njia/mbinu zilizotumika ili kumuinua au kumuangusha mhusika mkuu.
(viii)Onesha njia/mbinu zilizotumika ili kuyakabili na kuyatatua matatizo hayo na migogoro iliyojitokeza katika mchezo huo.
(ix)Onesha majibu/matokeo ya juhudi zote alizotumia mwandishi ili kulikabili suala au tatizo linalozungumziwa katika mchezo huo.
(x)Fanya tathmini ya kupima kama mwandishi amefanikiwa, katika maelezo yake, kulifikisha lengo alilokusudia kwa hadhira lengwa.
(xi)Na kama hakufanikiwa kulifikisha lengo lake kwa hadhira husika, eleza kwa nini kashindwa.
19.5.2 Uhakiki wa Fani: Wahusika
Uhakiki wa Fani Wahusika unatakiwa ushughulikiwe kwa kuzingatia na kuchunguza mambo mawili makubwa:
Yuko mhusika mkuu au wako wahusika wakuu.
Mhusika mkuu au wahusika wakuu hutambulishwa kwa maswali matatu:
(a)Hadithi imejengwa juu ya nini?
(b) Je, mhusika huyo hutokea mara nyingi akitenda mambo, kuongea au kuzungumziwa na wahusika wenzake?
© Je, mhusika anatoa uamuzi unaofikisha mchezo kwenye kilele au upeo wa weledi wa hadhira yake?
Wahusika wadogo nao huunda makundi matatu:
(a) Wahusika wadogo walio maarufu au muhimu.
(b) Wahusika wadogo walio maarufu kidogo.
©Wahusika-Wadogo wanaofanya mazingira katika mchezo ambayo yanamsukuma Mhusika-Mkuu aamue au asiamue jambo kama alivyokusudia hapo awali.
Jinsi wahusika walivyoundwa na kulelewa mambo muhimu ya kuchunguza katika kipengele hiki ni:
(a) Sura, tabia, kazi zao maishani katika jamii, na katika mchezo.
(b) Uhusiano wao katika Jamii: - Je, wanaendelezana kimaisha, au kila mmoja kivyake?
- Je, wanagongana kitabaka, kifikra, kiuchumi, kielimu, nk?
- Je, wanasadikika na kupokeleka na jamii yao, au na hadhira kwa jumla?
19.5.3 Uhakiki wa Fani: Muundo
Kipengele hiki kinachunguza jinsi mchezo wenyewe ulivyotengenezwa. Maswali ya kujiuliza ni haya:
(a) Mwanzo wa mchezo ni wapi na unakomea wapi?
(b) Kilele cha mchezo ki wapi; kimeanzia na kuishia wapi?
© Sehemu za mchezo ni zipi? Yaani mchezo una vitendo vingapi (sehemu ngapi) na maonesho mangapi?
(d)Ni mandhari gani yaani sura ya mahali na mzingira ya wakati yanasawiriwa katika mchezo?
19.5.4 Uhakiki wa Sanaa: Kufaulu Kwa Mtunzi
Uamuzi wa kwamba mtunzi amefaulu ama hakufaulu katika utunzi wa mchezo wake, hatuna budi kuchunguza au kujiuliza mambo yafuatayo kuhusu sanaa aliyoitumia katika mchezo wake.
(a) Je, lugha aliyoitumia mwandishi ni fasaha, (yaani ni lugha sahihi kisarufi, na ni rahisi kueleweka kwa watu wengi waliokusudiwa wauelewe mchezo wake?
(b) Je, viashiria au ishara na mifano iliyotumika ili kulijenga wazo kuu; kuunda visa, mazingira ya wakati na mahali; kubainisha ukale dhidi ya usasa (mapinduzi); nk. yamechangia kufanikisha azma ya mchezo?
© Je, ukubwa wa hadhira au jamii inayoweza kufikiwa na ujumbe wa mchezo na ikauelewa fika na kuathirika nao vibaya au vizuri, unaridhisha?
(d) Je, maudhui yatokanayo na mchezo huu yanatoa jawabu au suluhisho la kufaa kuhusu migogoro inayojitokeza katika jamii hiyo? Je, yanachochea zaidi vurugu akilini kuhusu mgogoro uliopo?
(e) Je, semi zimetumiwa katika mchezo ili kusisitiza au kukejeli mambo yanayosadikiwa na kufuatwa kama kanuni au desturi katika jamii?
(f) Je, suala linalojadiliwa linawagusa watu wa kiwango gani kielimu katika jamii hiyo?
(g) Je, suala la wachache katika jamii, yaani ni tabaka dogo tu la watu?
(h) Je, suala la watu wengi katika jamii, yaani ni tabaka kubwa la watu?
(i) Je, suala la watu wote katika jamii?
(j) Je, suala linalojadiliwa lina umuhimu gani kwa jamii kwa wakati huu?
(k) Je, mwandishi amewatumia wahusika wake ipasavyo katika kuliweka bayana wazo kuu kwa hadhira husika, na uwe mfano bora kwa hadhira kuwaiga au kutowaiga kwa vile alivyowamulikia kwa undani maisha yao kwa vitendo na maneno yasemwayo mchezoni?
19.5.5 Uhakiki wa Kichwa cha Mchezo
Kichwa cha mchezo ni kama nembo. Kwa hiyo, nacho pia inafaa kihakikiwe. Maswali ya kujiuliza kuihusu ni kama ifuatavyo:
(a) Je, kichwa kilichowekwa kweli kinawakilisha wazo kuu, au
kiini cha habari?
(b) Je, ni wazo mojawapo tu linalojitokeza katika mchezo huu katika jumla ya mawazo? au
© Ni neno tu la kuamsha udadisi wa msomaji na labda la kuwavutia wanunuzi wa kitabu chake?
|
|
|
Dhana ya Uhuru wa Mwandishi |
Posted by: MwlMaeda - 12-25-2021, 11:23 AM - Forum: Uhakiki wa kazi za fasihi
- No Replies
|
|
Dhana ya Uhuru wa Mwandishi
E. Kezilahabi
Dhana ya Uhuru
Tunapozungumzia uhuru kama dhana ya kifalsafa mara nyingi huwa tunafikiria uwezo wa mtu binafsi wa kufanya uamuzi, kujijua, kujiendesha kujirekebisha. Lakini pia huwa tunatia maanani mkondo ambao uko nje ya nafsi. Mkondo huu wa nje huwa na uwezo wa kuathiri na wakati mwingine huongoza moja kwa moja na kutoa kauli ya mwisho kuhusu jambo la kutenda. Wakati mwingine nguvu za ndani au utashi wa nafsi ya mtu huweza kuwa na nguvu zaidi ya mkondo wa nje.
Kwa muda mrefu katika historia ya falsafa ya Kimagharibi kulikuwa na imani iliyotawala – kwamba uwezo wa kutoa sababu au utumiaji wa akili ndilo jambo limtofautishalo binadamu na mnyama. Kufuatana na falsafa hii binadamu anatakiwa kuzitawala hisia zake kwa kutumia akili. Hisia zikiachwa peke vake haziaminiki kwa sababu mara nyingi huoneoza kwenve njia ambayo hatima yake ni madhara. Kwa sababu hii mwanafalsafa wa Kiyunani, Plato, hakuwa na imani na ushairi.
Lakini, je ni kweli kwamba kwa muda wote huu katika historia binadamu amekuwa akitumia akili? Swali hili linakuwa gumu tunapokumbana na ukweli wa mambo kama: utumwa, vita vya dunia, ubaguzi wa rangi, nafasi finyu aliyonayo mwanamke katika jamii, hatari ya kuteketezwa kwa dunia na silaha kali za nyukliya, na njama za ubeberu.
Ukweli wa mambo haya umeleta fikra mpya katika mijadala ya kifalsafa na kielimu jamii. Wanafalsafa wa existentialism ndio waliokuwa wa kwanza kufikiria upya misingi ya falsafa iliyopita. Waliona kwamba mambo haya yote yanaambatana na uhuru pamoja na mtazamo rahisi kuhusu maisha aliokuwa nao mwanadamu. Waliona kuwa masuala yote yanahusiana na kuwako (existence au being there) au kutokuwako (nothingness). Haya ni maswali muhimu yanayomkabili binadamu wa leo. Kwa hiyo uhuru ni katika kuwako na kutokuwako (being & nothingness) na uamuzi (choice) anao binadamu mwenyewe. Katika aya zinazofuata nitajaribu kueleza zaidi dhana hii ya uhuru.
Tunaweza kusema kwamba binadamu katika kuusaka uhuru ni kama mtoto mdogo ambaye ameanza kufurahia uwezo wake wa kutembea. Mtoto huyu anaona kipepeo mwenye rangi nzuri ametua juu ya ua. Anataka amshike kwa mkono. Kila anapomkaribia anaruka. Mtoto, bila kukata tamaa, anaendelea kumfuata hadi anapojikuta msituni; mwishowe giza linaingia, haoni njia ya kurudi, woga unamwingia, anatoa kilio kuomba msaada akifikiri wazazi wake wako karibu. Uhuru basi haushikiki. Ubora na umuhimu wake vimo katika kutoshikika au kutopatikana. Tungekuwa nao tusingeishi maana maisha yasingekuwa na kitu kijulikanacho kama telos, yaani kile kinachosakwa au nia. Tunaweka juhudi katika shughuli zetu za kila siku kwa sababu ya utupu (nothingness) ambao hutakiwa kujazwa lakini haujaziki. Ni kama kujaza maji ndani ya pakacha. Katika kufanya hivyo tunaishi. Uhuru basi umo katika utupu, katika kutokuwa nao.
Ni kweli tunaweza kupata uhuru wa bendera, tukashangilia sana. Mara tunajikuta katika mfumo wa jitihada – jitihada ya kufanya hali ya uchumi iwe nzuri zaidi. Kubadilisha hali ya maisha ya watu. Kwa hiyo tunakata mirija yote ya unyonyaji. Tunajikuta katika mfumo mwingine – mfumo wa kukata na kukatwa. Katika vita hivi mkulima anaumia zaidi. Polepole neno ushindi linabadilishwa kuwa kujaribu. Kila kiongozi anayekuja anasema atajaribu, atajitahidi kubadilisha hali. Kwa hiyo tunaweza kuongezea kwamba uhuru umo katika kujaribu na kujitahidi, na tunasukumwa mbele na mabadiliko ambayo yana rangi ya kipepeo.
Tunaweza pia kufanikiwa maishani, tukapata mali na vinginevyo. Tunaweza kutamani kujenga nyumba, tukapata pesa tukajenga. Baada ya muda tunasahau kuwa hata hiyo nyumba moja hatukuwa nayo awali, tunajenga ya pili. Katika kusahau, tunajisukuma mbele. Tunatamani kitu kingine, na katika kutamani tunajisukuma mbele. Tunaishi. Katika mtazamo huu kutamani na kusahau si ila. Si vibaya kusahau unakwenda wapi. Inapasa kuwa hivyo. Unaweza kusema unakwenda mjini. Hakuna mtu, wakati anakwenda mjini, akumbukaye kila sekunde kwamba anakwenda mjini. Unafika mjini kwa kusahau kuwa unakwenda mjini. Ni vizuri kusahau marehemu uliowafahamu, la sivyo vivuli vyao vitakutokea mara nyingi na utajiona huna uhuru. Utahama nyumba na nyumba. Ni vizuri kusahau makosa tuliyotenda. Kama binadamu angekumbuka daima makosa yake yOte, asingeishi. Hata mwaka mmoja. Kwa hiyo tunaweza kusema kuwa uhuru umo katika kusahau (forgetting). Tunasahau hata majina yetu; tunayakumbuka tunapoitwa. Katika kusahau mambo hupeana nafasi katika kichwa cha binadamu.
Tunaweza kujiuliza swali moja muhimu. Nini kitusukumacho mbele? Jibu ni utashihuru (free – will). Hapa utashihuru hauna maana ya kufanya upendalo bali linalotakiwa kuwa. Gurudumu ukilisukuma kutoka juu kilimani linatakiwa au lazima litajiviringisha lenyewe. Muundo wake, pamoja na misingi ya kisayansi, vinafanya lizunguke lenyewe bila mkondo wa nje. Hapa sina nia ya kusema kuwa gurudumu lina utashihuru bali hali ya gurudumu inalinganishwa na utashihuru wa binadamu. Utashi huu unaambatana na kutamani (desire) pamoja na mahitaji (need(s). Utashi ni moja kati ya nguzo muhimu zilizopo katika dhana ya uhuru wa mwandishi ambako mjadala huu unaendelea.
Dhana ya Uhuru wa Mwandishi
Bila utashi mwandishi atakuwa mwoga na mwepesi wa kukata tamaa. Atayumbishwa haraka kutoka kwenye msingi ya falsafa yake na imani aliyonayo juu ya mabadiliko yatokeayo katika nchi yake. Makombora ya wahakiki na wanasiasa huweza sana kuyumbisha; lakini kwa mwandishi mwenye utashi makombora haya hukomaza. Nitatoa mifano miwili ya waandishi wawili wa Kiafrika ambao wameonyesha dhahiri utashi wao. Waandishi hao ni Wole Soyinka na Ngugi wa Thiong’o. Hapa Afrika hakuna mwandishi ambaye amepata kushambuliwa na wahakiki kama Soyinka. Lakini msimamo wake ni uleule, na si mtu wa kuyumbishwa na makala. Tukumbuke kuwa amepata pia kufungwa, na alipotoka kifungoni hakubadili msimamo wake. Misukosuko iliyompata Ngugi wa Thiong’o watu wa Afrika ya Mashariki twaijua. Ngugi hajatetereka na hajayumbishwa. Waandishi hawa wawili wameweza kuwa hivyo kwa sababu ya utashi na falsafa zao.
Tunaweza kusema kwamba uhuru wa mwandishi kwanza kabisa umo katika utashi. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi wenye utashi wapo? Bila kutaja majina nafikiri wapo. Na msingi wa kuwako kwao ni kutoyumbishwa na matamshi ya jukwaani na wahakiki ambao hawajapevuka. Msingi wa pili unawahusu hasa wale waandikao katika lugha ya Kiswahili. Kwa muda mrefu hapa nchini pamekuwa na wazo potovu linalotawala: kwamba maandishi ya Kiswahili hayana hadhi. Nimeona wanafunzi wasomao Kiswahili Chuo Kikuu wakifichaficha vitabu vya Kiswahili wasionekane kuwa wanasoma Rosa Mistika, Nyota ya Rehema, n.k. Ila wakiwa na The Interpreters, ingawa hawakielewi, watatamba nacho. Licha ya hadhi ya chini ambayo maandishi ya Kiswahili yamepewa, waandishi wa Kiswahili wanaendelea kuandika kwa sababu ya utashi walio nao. Msukumo huu ndio unaoendeleza mbele fasihi ya Kiswahili.
Tumetoa hoja kwamba, kwanza kabisa uhuru wa mwandishi umo katika utashi. Tuone sasa nguzo ya pili. Nguzo hii ya pili imo katika kuwa na falsafa moja inayoeleweka, falsafa ifanyayo maandishi yaonekane kama kazi moja yenye mwelekeo maalum. Falsafa ndiyo kamba ifanyayo maandishi yote ya mwandishi yawe kazi moja, siyo jina la mwandishi. Falsafa ndiyo ifanyayo maandishi ya mwandishi mmoja yawe na kitu kijulikanacho kama terminus ad quem, yaani lengo. Waandishi niliowataja hapo juu, Wole Soyika na Ngugi wa Thiong’o (na hapa nitamwongezea Leopold Senghor), ndio wanaoongoza katika kuwa na falsafa zao zinazojulikana. Katika fasihi ya Kiswahili tunao waandishi wenye falsafa inayojulikana? Wapo wachache. Wengi tulio nao wanaandika kufuatana na jambo au tukio la wakati huo bila kiunganisho. Leo ataandika juu ya mapenzi, kesho juu ya upelelezi, na kesho kutwa “mapinduzi” – mwishowe anakuwa na orodha ndefu ya vitabu visivyokuwa na terminus ad quem. Waandishi wachache tulio nao ambao waelekea kuwa na falsafa inayoongoza maandishi yao ni kama Shaaban Robert na Mohammed Suleiman. Bila kuwa na falsafa maahum ni rahisi kwa mwandishi kuyumbishwa. Tunaweza kusema kuwa uhuru wa mwandishi umo katika falsafa yake.
Hoja ya tatu itatufikisha kwenye sanaa yenyewe. Hoja hii.inasema kwamba uhuru wa mwandishi umo katika kuitawala vema sanaa yake. Kama unaandika tamthiliya na hujui misingi ya sanaa ya aina hiyo utajikuta katika kikwazo. Utajikuta huna uhuru kisanaa. Unaweza kujaribu, lakini kazi utakayoitoa itakuwa hafifu. Tunaweza kusukuma wazo hili mbele kwa kusema kuwa kazi nzuri ya kisanaa ni ile inayounganisha vema ubunifu na uhalisia. Mwandishi akielemea sana katika uhalisia kunakuwa na matatizo, na aelemeaye sana katika ubunifu anazua matatizo mengine. Kazi ngumu aliyo nayo mwandishi ni katika kuupatia barabara msitari huo. Mwandishi mwenye vitabu vingi anaweza kuwa na kitabu kimoja tu kilichoupatia vema msitari huo. Katika fasihi ya Kiswahili waandishi walioupatia msitari huu tunao: Ebrahim Hussein, Penina Muhando, Muhammed Suleiman, C.G. Mung’ong’o na A.J. Saffari. Hawa ni miongoni mwa waandishi ambao ningewataja bila kusita. Mwandishi anayeweza kuitawala vema sanaa yake anaunganisha vizuri sanaa na maudhui yake.
Lakini mwandishi hawezi kuitawala vema aina ya sanaa anayoitumia kama msingi wa lugha anayoitumia ni mbovu. Lugha ndicho kiungo maalum kati ya sanaa na kazi za kifasihi. Kama hujui vema lugha unayoitumia utajikuta huna uhuru wa kusema unachotaka kukisema. Kwa hiyo lugha ndiyo nguzo ya nne katika uhuru wa mwandishi. Waandishi wa Kiswahili niliokwisha wataja wanakitawala vema Kiswahili sanifu. Hapa nitasisitiza kwamba Kiswahili sanifu ndio msingi wa fasihi ya Kiswahili.
Tutamalizia sehemu hii kwa kusema kuwa uhuru wa mwandishi umo katika utashi, falsafa, aina ya sanaa aitumiayo mwandishi, na katika lugha.
Mashetani Kama Mfano
Mashetani ni tamthiliya inayofikiriwa na wengi kuwa ya kiwango cha juu kisanaa. Ni tamthiliya ya kwanza ya Kiswahili ambayo inapenya na kujaribu kuufikia urazini. Labda ni tamthiliya ya kwanza ya Kiswahili ambayo imejadili mvutano wa kisaikolojia ulokuwa katika vichwa vya Watanzania kuhusu muungano kati ya Zanzibar na Tanganyika miaka michache baada ya Azimio la Arusha. Azimio la Arusha na Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo matukio makubwa yaliyobadilisha maisha ya watu wa tabaka la juu katika nchi hizi mbili zilizoungana.
Wahusika wakuu katika tamthiliya hii ni Kitaru na Juma. Wote ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kitaru anasomea uwanasheria na Juma anasoma historia. Ni wanafunzi “wanamapinduzi,” wanausaka uhuru ambao umo katika ukweli. Lakini kutokana na matukio ya kihistoria pamezuka “chuki” ambayo imevuruga uhusiano kati yao. Baba yake Kitaru ambaye anatoka Bara ni bepari, na baba yake Juma ambaye mali yake ilitaifishwa Zanzibar kabla hajahamia Bara, sasa ana kijiduka. Uanamapinduzi wao unajigonga juu ya mwamba uliojikita katika tabia ya baba yake Kitaru ambaye anawachochea na mawazo ya kuchuma pesa; na katika bibi yake Juma ambaye anawachochea kwa hadithi za fahari iliyopita.
Ukweli wataupata wapi? Katika historia. Kwa hiyo historia halisia inachezwa kisanaa. Mchezo ndani ya mchezo. Hii ni mbinu ya kisanaa aitumiayo mwandishi katika kuipa historia uhai. Hadhira inapewa nafasi ya kuishi tena historia iliyopita. Sehemu ya pili ya tamthiliya hii pia ni mchezo ndani ya mchezo, lakini mchezo huu unatokea kichwani mwa Kitaru. Mchezo huu unahusu matukio yaliyotokea baada ya uhuru wa bendera na matatizo ya ukoloni mamboleo ambao lengo lake ni kichwa na uchumi. Hali ya nguvu za mkondo wa nje tunaiona katika mcheko. Baada ya maonyesho haya ya kisanaa Hussein, katika sehemu ya tatu na ya nne, anairudisha hadhira katika hali halisi.
Katika tamthiliya tunamwona mwandishi akijaribu sana kuutafuta msitari kati ya ubunifu na uhalisia. Ili kuupata msitari huu anatumia mchezo ndani ya mchezo; anatumia lugha inayowiana na wahusika, na mwanga wa spotlaiti na ndoto. Katika tamthiliya hii tunauona mvutano uliopo kati ya mkondo wa nje na nafsi. Mkondo wa nje tunauona katika sitiari ya chewa na jahazi inayofuata mkondo wa maji. Mvutano huu unawakilishwa na Binadamu na Shetani. Inavyoelekea Hussein anatoa wazo kuwa uhuru uliomo katika ukweli unapatikana katika hali ya nusu ndoto na katika hali ya nusu kichaa (neurosis), na kwamba tunaukaribia ukweli katika kazi za kisanaa kwa sababu katika sanaa tunaishi tena na tena maisha yetu. Katika sanaa tunacheza mchezo tena na tena hadi ukweli unapojidhihirisha. Wazo hili tunaliona katika maneno ya Kitaru anaposema, “Lakini katika ule mchezo, na katika ndoto, nimeona mengi niliyokuwa siyo nikiyaona” (uk. 47).
Katika Mashetani Hussein anaanza kuachana na uhalisia rahisi tuuonao tangu Wakati Ukuta hadi Kinjeketile. Anaanza kuachana na fasihi rahisi yenye nia ya kufunza (didaclic) na kuingia katika mfumo wa sanaa unaoelekea katika dhana ya uhuru wa mwandishi. Hussein anakuwa si mwandishi wa kurudia nyimbo za jukwaani. Mfululizo wa tamthiliya zake zilizofuata zimekuwa katika kiwango hicho. Mwandishi anaitawala aina ya sanaa anayoitumia, na anaonyesha dalili za kuwa na utashi thabiti.
Hitimisho
Nia ya makala haya ni kuondoa mawazo rahisi juu ya uhuru wa mwandishi. Kati ya kuwako na kutokuwako tumo katika kujaribu, katika kusahau, katika kuieleza vema falsafa inayotawala uandishi wetu, katika kuitawala lugha, na wakati huo tukisukumwa mbele na utashi. Uhuru, huo hatunao, katika kutokuwa nao tunaandika.
|
|
|
|