ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU' - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Majadiliano ya Wadau wa Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=16) +--- Thread: ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU' (/showthread.php?tid=2090) |
ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU' - MwlMaeda - 01-10-2022 HII NDIYO ETIMOLOJIA YA NENO 'KUNTU' Neno *kuntu* katika lugha ya Kiswahili lina maana zifuatazo: 1. *Kihisishi:* Neno linaloonyesha ukubalifu wa moja kwa moja katika moyo wa mtu; sawasawa, barabara, hasa. (Chanzo: Kamusi Kuu ya Kiswahili). 2. *Kielezi:* Sawasawa, bila ya shida yoyote. (Chanzo: Kamusi ya Karne ya 21). 3. *Kielezi:* Kwa ufupi, kweli, hakika; hasa; kabisa; ndivyo. (Chanzo: Kamusi Teule ya Kiswahili). Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *kuntu *(soma: kun + tu كنت* ) ni kitenzi cha Kiarabu cha wakati uliopita *fiilu maadhwi فعل ماض* kwa nafsi ya kwanza, chenye maana ya: nimekuwa/nilikuwa. Kitenzi hiki kimenyumbulika kutokana na kitenzi cha Kiarabu *kaana كان* amekuwa/alikuwa. Kinachodhihiri ni kuwa neno hili *kuntu كنت* lilipoingia katika Kiswahili lilipewa kategori ya kihisishi/kielezi na kupewa maana mpya tofauti na maana yake ya awali katika lugha ya Kiarabu ya kuwa kitenzi chenye maana ya: nilikuwa/nimekuwa. *Shukran sana.* *Khamis S.M. Mataka.* |