MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: NDOTO - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: NDOTO - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: NDOTO (/showthread.php?tid=783)

SHAIRI: NDOTO - MwlMaeda - 08-07-2021

NDOTO
Kufasiri mejaribu, kwa ndoto niiotavyo,
Hakika napata tabu, kwa ndoto inijiavyo,
Sasa nipeni jawabu, nitambue maanavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Azukapo afiriti, anitende atakavyo,
Nalikwepa varangati, vile juu nipaavyo,
Atahaha hanipati, vile mbali niendavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Ni nini kinanizinga, kwa ndoto niiotavyo?
Au ndoto yanikenga, nijione ndivyo sivyo?
Kukicha siwezi ringa, mbawa zinipotevyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Kigutuka ninawaza, ndotoni nipepeavyo,
Linazidi nitatiza, siku mbele ziendavyo,
Nimeona kueleza, mashaka yanijiavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Pengine nanusurika, vile anikimbizavyo,
Lizidivyo patashika, ndivyo juu niendavyo,
Nikimwepa namcheka, chini nimtazamavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Ndoto yanipa tatasi, na hivyo irudiavyo,
Yanijia wasiwasi, na ndivyo niandikavyo,
Nipeni majibu basi, ndoto niwaambiavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Nane beti sio kenda, shairi niishiavyo,
Swali nalituma nenda, majibu nisubirivyo,
Ili nije pata wanda, niepuke nikondavyo,
Vile juu nipaavyo, hivi ina maana gani?

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704