Welcome, Guest |
You have to register before you can post on our site.
|
Online Users |
There are currently 68 online users. » 0 Member(s) | 66 Guest(s) Bing, Yandex
|
Latest Threads |
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
|
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
|
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
|
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
|
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
|
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
|
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
|
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403
|
|
|
SWALI: ELEZA KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA LEKSIKOGRAFIA NA LEKSIKOLOJIA KATIKA LUGHA |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 03:44 PM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
SWALI: ELEZA KUFANANA NA KUTOFAUTIANA KWA LEKSIKOGRAFIA NA LEKSIKOLOJIA KATIKA LUGHA
UTANGULIZI
Wataalamu mbalimbali wameweza kutoa fasili ya Leksikografia baadhi ya wataalamu hao ni;
Mdee (1985) Leksikografia ni usawiri wa kamusi, huu ni utaalamu au utaratibu wa kukusanya msamiati pamoja na tafsiri yake na kuupanga katika kitabu cha maneno ambacho huitwa Kamusi. Fasili hii ya Mdee ina udhaifu kwani Kamusi siyo lazima iwe imeandikwa katika kitabu pekee, bali kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia siku hizi kamusi zimeweza kuandikwa katika elektroniki mfano kompyuta na simu za mkononi.
Wiegand,(1984) akinukuliwa na Mdee, (2010) anasema Leksikografia ni kazi ya kisanyansi ya kutunga kamusi.Leksikografia hujumulisha uorodheshaji wa msamiati wa lugha inayotungiwa kamusi pamoja na maelezo yenye kufafanua kila neno lililoorodheshwa kadri ya mahitaji ya watumiaji wa kamusi aliyewalenga.
Oxford dictionary, (2001) Leksikografia ni kitendo cha kuunda kamusi. Hivyo basi kutokana na fasili tulizoziona hapo juu tunaweza kufasili leksikografia kuwa ni sehemu ya isimu inayojihusisha na uundaji wa kamusi.
Leksikografia inafafanua maneno na kuweka wazi matumizi na miundo ya maneno. Katika taaluma hii ya leksikografia tunaweza kuigawa katika sehemu kuu mbili ambazo ni leksikografia ya vitendo na leksikografia ya kinadharia.
Leksikografia ya vitendo ni sanaa ya kukusanya, kuandika na kuhariri kamusi wakati leksikografia ya kinadharia ni mwongozo wa kitaaluma wa kueleza na kufafanua uhusiano wa semantiki, sintagmatiki na pragmatiki katika leksikoni ya lugha, kuendeleza nadharia zinazounda kamusi na kuhusianisha data katika kamusi. Kwa ujumla leksikografia inajihusisha na kubuni, kukusanya, kutumia na kutathimini kamusi kwa ujumla.
Hali kadhalika leksikografia inajihusisha na fonolojia, mofolojia, semantiki au maana pamoja na miundo ya maneno kwa ujumla.Leksikolojia hii inahusu mfumo, maana na tabia za maneno (Oxford, 2001).Leksikolojia ni tawi la isimu linaloshughulikia mofolojia na maana ya maneno (Ullmann, 1962 akinukuliwa na Mdee, 2010).Leksikolojia ni tawi la isimu linalochunguza etimolojia, maana na matumizi ya maneno.
Hivyo Leksikolojia ni sayansi ya maneno na ni msingi wa nadharia ya leksikografia (Doroszewski, 1973 akinukuliwa na Jackson, 1989 katika Mdee, 2010).Hivyo basi kutokanana fasili tulizoziona hapo juu tunaweza kusema leksikolojia ni tawi la isimu linalojishughulisha na maneno, asili na maana, mofolojia ya maneno, mahusiano ya maana ya maneno, makundi ya maneno na leksikoni kwa ujumla.Hali kadhalika katika kufasili leksikoni huu ni msamiati wa mtu, lugha au tawi la maarifa.
Ni ule msamiati wote uliopo kichwani mwa mzungumzaji wa lugha. Leksikoni ndio nguzo au chanzo cha data za wanaleksikolojia na wanaleksikografia katika mchakato mzima wa uandaaji wa kamusi.
KIINI CHA SWALI
Baada ya kuangalia fasili za dhana mbalimbali hapo juu, sasa tujikite katika kufafanua ufanano na utofauti uliopo baina ya leksikografia na leksikolojia katika lugha. Ufanano uliopo baina leksikografia ya na leksikolojia katika lugha ni kama ifuatavyo:-
Leksikografia na leksikolojia zinajihusisha na msamiati wa lugha.
Leksikografia hukusanya msamiati na maana zake na kutunga kamusi ambayo hutoa ufafanuzi juu ya misamiati ya lugha hali kadhalika leksikolojia hujihusisha na msamiati katika kuelezea maana na matumizi ya maneno husika kwa jamii husika (Ndumbaro, 2013). Leksikolojia na leksikografia hutegemea watumiaji wa lugha katika kukusanya data zake kwani zote hujihusisha na leksikoni.
Hivyobasi leksikografia na leksikolojia hutegemea leksikoni iliyopo kichwani mwa mtumiaji wa lugha (Mdee, 1985).Leksikografia na leksikolojia zimetokana na maneno ya Kigiriki ambayo ni “lexico” likiwa na maana ya maneno. Leksikolojia limetokana na neno “lexico” (maneno) na logos (sayansi) ikimaanisha sayansi ya maneno wakati leksikografia imetokana na neno “lexico” (maneno) na “graph” (kuandika) ikiwa na maana ya kuandika maneno (Ndumbaro, 2013).
Zote zinahusika na uwanja wa kiisimu ujulikanao kama semantiki. Leksikografia licha ya kujihusisha na nyanja nyingine kama vile fonolojia na mofolojia pia inajihusisha kwa kiasi kikubwa na semantiki kwani hata hapo mwanzoni kamusi ziliandikwa kwa kuzingatia semantiki. Huangalia maana ya msamiati katika kutunga kamusi, hali kadhalika leksikolojia pia hujikita katika maana na matumizi ya msamiati (Ndumbaro, 2013).
Zote zinahusu etimolojia ya maneno katika kupata data za kimofolojia na kisemantiki za leksimu, kamusi pia hutusaidia katika kupata taarifa za kimuundo zinazohusu asili ya maneno na taarifa za kihistoria kuhusu mabadiliko ya maneno na matumizi ya maneno (Mdee, 2010).
Baada ya kufafanua ufanano uliopo baina ya leksikografia na leksikolojia sasa tugeukie katika kufafanua utofauti uliopo baina ya leksikografia na leksikolojia katika lugha, utofauti huo ni kama ifuatavyo.
Leksikografia inafikiriwa kuwa ni kongwe kuliko leksikolojia kwani utungaji wa kamusi inasadikika kuwa ulifanywa na wayunani tangu karne ya kwanza hata hivyo maandishi hayakuwa kwenye kamusi kama tujuavyo leo hii bali yalikuwa orodha ya maneno na maana zake. Wakati leksikolojia ilianza miaka ya 1820 ingawa inasemekana kuwa kulikuwa na wanaleksikolojia kabla ya neno leksikolojia kupatikana(Mdee, 2010).
Tofauti nyingine ipo katika malengo, malengo ya leksikografia kiujumla ni kubuni, kukusanya, kutumia na kutathimini kamusi au kuunda kamusi wakati leksikolojia malengo yake ni kuchunguza etimolojia, maana na matumizi ya maneno (Mdee, 1985).
Tofauti nyingine ipo katika mabadiliko, katika leksikografia mwanaleksikografia anapounda kamusi yake hubaki kama ilivyo hadi hapo atakapounda kamusi nyingine iliyobora kupita ile ya kwanza. Hivyobasi ni vigumu kamusi kuweza kupokea mabadiliko ya msamiati na maana zake mara kwa mara kuendana na mabadiliko ya jamii. Kwa upande wa leksikolojia kwa kiasi fulani huweza kupokea mabadiliko kwani leksikolojia ipo katika nadharia (Ndumbaro, 2013).
Tofauti nyingine ni kuwa leksikolojia hujihusisha na sifa za jumla, sifa ambazo zinaweza kuonekana katika mpangilio maalumu wakati leksikografia inajihusisha na sifa ya maneno kiupwekeupweke yaani maana zake nyingi ni fafanuzi ambapo maana ya maneno hutegemeana na wazungumzaji wa lugha siyo mwanaleksikografia (Mtengenezaji wa kamusi) (Ndumbaro, 2013).
Tofauti nyingine ni idadi kamili ya maneno, katika leksikografia idadi ya msamiati uliopo katika kamusi huweza kujulikana na kubainishwa wazi wazi. Hii inatokana na ukweli kwamba kamusi huwa na idadi ya misamiati kulingana na aina ya kamusi ambayo mwanaleksikografia amedhamiria kuiandaa lakin kwa upande wa leksikolojia yenyewe haijihusishi na idadi ya maneno katika kamusi bali inajihusisha na mofolojia na maana na tabia za maneno katika kamusi (Mdee, 2010).
Tofauti nyingine ni kwamba katika leksikolojia maana ya maneno ni elekezi ambayo yanaongozwa na nadharia ya kisemantiki na muundo wa maneno wakati katika leksikografia maana nyingi ni fafanuzi ambazo hutegemea wazungumzaji wa lugha na sio watunga kamusi yaani wanaleksikografia (Mdee,1985).
HITIMISHO
Hivyo basi tunaweza tukasema kuwa licha ya tofauti zilizofafanuliwa hapo juu dhidi ya dhana hizi mbili, ukweli ni kwamba dhana hizi mbili zinahusiana kwa karibu sana hasa katika mchakato mzima wa kukusanya na kuandaa kamusi. Hivyo ni vigumu sana kuzitenganisha dhana hizi mbili kwani zinaonekana kama pande mbili za shilingi ambapo upande mmoja usipokuwepo haiwezi ikaitwa ni shilingi tena.
MAREJEO
Mdee, J.S. (1985). Ukusanyaji wa Data ya Leksikografia naMatatizo yake; Mifano kutoka Kiswahili katika Mulika na.17: Dar-es-Salaam.TUKI
Mdee, J.S. (2010). Nadharia na Historia ya Leksikografia: Dar-es-Salaam.TUKI
Ndumbaro, E. (2013). Kusigana na Kulandana kwa Msamiati; Kufanana na Kutofautiana kwa Leksikografia, Leksikolojia na Leksikoni: Imenukuliwa kutoka www.chomboz.blogspot.com tarehe 1.4.2015 saa 2:30 usiku
Concise Oxford Dictionary.(2001).London: Oxford University Press.
|
|
|
TOFAUTI KATI YA SARUFI MIUNDO VIRAI NA SARUFI GEUZI |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 03:00 PM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
Tofauti kati ya Sarufi miundo virai na Sarufi geuzi
SWALI: Sarufi miundo virai inatofautianaje na Sarufi geuzi?
Sarufi ni nini ?
Kihore na wenzake (2008) wakimnukuu Gaynor (1968:88) wanaeleza kuwa sarufi ni sayansi ya muundo wa lugha pamoja na sheria, kanuni na matumizi yake ambayo kwa kawaida hukubalika kwa watumiaji wake.
Massamba na wenzake (2009:31) wanaeleza kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu za uchambuzi zinazotawala lugha.
Saluhaya (2010:72) anadai kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha katika matumizi yake ambayo hujumuisha matamshi, maumbo, miundo na maana. Taaluma hii husisitiza kanuni zitumikazo katika uchambuzi wa lugha katika viwango vinne vilivyotajwa hapo juu.
Sarufi miundo virai
Hiki ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa(Matinde, 2012:233).
Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinavyoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neon moja moja lililokiunda kirai.
Sarufi Geuzi
Sarufi geuzi ni utaratibu wa kubadili maumbo ya maneno kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu. Sarufi hii hujengwa kwa wazo kwamba katika lugha kuna sentensi ambazo huwa ni za msingi, ambazo kutokana na kaida mahususi sentensi zingine huweza kuzalishwa na sentensi hizo (Matinde, 2012:231). Ugeuzaji huu huathiri muundo wa sentensi na wala si maana ya sentensi. Kwa mfano;
(a) John amemchapa Bigile.
(b) Bigile amechapwa na John.
Hivyo basi, ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuta sheria au kanuni maalumu.
Kwa mujibu wa Habwe na Karanja (2007), Matinde, (2012) wanaonesha utofauti uliopo kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi kama ifuatavyo:
Tofauti katika maana, sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo mengine kwa kufuata kanuni maalumu. Ilhali sarufi miundo virai ni kitengo cha sarufi geuzi maumbo zalishi ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na ukomo.
Tofauti katika uchanganuzi wa sentensi, sarufi geuzi huweza kuchanganua sentensi zenye maumbo tofauti. Kwa mfano sentensi sahili, changamano au ambatano ilhali sarufi miundo virai hujikita katika kuchanganua sentensi sahili peke yake.
Mfano; Rajabu ni mwana wangu.
Tofauti katika uchopekaji wa viambajengo, sarufi geuzi huweza kuchopeka viambajengo katika sentensi na kuifanya sentensi hiyo kuwa tenda au tendwa. Kwa mfano, sentensi ya kauli ya kutenda inapogeuzwa na kuwa katika hali ya kutendwa kuna elementi ambazo huchopekwa.
Mfano; (a) Changwe anampiga mtoto
(b) Mtoto anapigwa na Alpha.
Hapa tunaona mofu {-w} na kihusishi {na} huchopekwa katika sentensi (a) na kuifanya sentensi hiyo kuwa ya kauli ya kutendwa katika (b). Ilhali sarufi miundo virai uchopekaji huo haujitokezi na hivyo kutokuonyesha mahusiano kati ya kauli tendi na tendwa.
Tofauti ya waasisi, sarufi geuzi iliasisiwa na mwanasarufi aitwaye Noam Chomsky (1957) ambaye anadai kuwa nadharia hii ya sarufi geuzi ilizuka ili kurekebisha taratibu za sarufi za awali. Yeye alidai kuwa sarufi za awali hazingeweza kuonyesha kuwa sentensi ya kauli ya kutenda na ile ya kauli ya kutendwa zinatokana na muundo mmoja wa ndani. Pia sarufi za awali hazingeweza kuonyesha mahusiano ya sentensi zinazotofautiana kwa ndani lakini ambazo zilikuwa na muundo wan je mmoja. Kwa mfano; Herman alinunuliwa shati na mwanawe.
Sura hii ya nje ya sentensi huwa ina sentensi kadhaa katika muundo wake wa ndani. Wakati sarufi miundo virai iliasisiwa na Bussmann (1996) ambaye anafafanua kwamba sheria miundo virai ni sheria zinazoonyesha mpangilio na ujenzi wa virai katika lugha, hivyo sheria hii huonyesha kuandikwa tena kwa viambajengo. Sheria kama,
S = KN+KT
yaani S = sentensi
KN = kikundi nomino/kirai nomino
KT = kikundi tenzi/kirai kitenzi
Inamaanisha kuwa sentensi inaweza kuandikwa kama Kikundi Nomino kikifuatwa na Kikundi Tenzi. Wakati mwingine sheria miundo virai huonyesha uhusiano wa utawazi hivi kwamba nomino hutawala Kikundi Nomino (KN). Kwa mfano sentensi kama; Amina ni mke wangu.
Suala la msingi ambalo wanaumuundo walisisitiza ni kutazama na kuchunguza lugha kisayansi. Hapa walisema kuwa masuala ilibidi yachunguzwe kwa uwazi na kuonyesha vitu, kategoria na elementi kwa uwazi zaidi. Ilhali sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao unaomwezesha kutumia lugha. Huu ni ujuzi wa kutunga sentensi kwa njia iliyo sahihi na vilevile namna sahihi ya kutamka na kueleza maana za maneno na sentensi. Mfano mmilisi wa lugha ya Kizinza anaweza kutunga sentensi zinazoeleweka na kutamka maneno ya lugha hiyo kwa usahihi kabisa.
Kwa ujumla, sarufi miundo virai na sarufi geuzi hufanana sana katika kuchunguza miundo ya lugha husika japo katika utendaji wake hujitokeza baadhi ya tofauti ambazo husababisha nadharia hizi za sarufi miundo kutofautiana katika vipengele kadha wa kadha kama vile uchopekaji wa viambajengo, maana zake pamoja na mfumo wa namna ya kuchanganua sentensi.
MAREJELEO
Habwe, J. & Karanja, P. (2004). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili.Nairobi: Phoenix Publishers.
Kihore, Y.M. na wenzake. (2008). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Sekondari na Vyuo. Dar es Salaam: TUKI.
Massamba, D.P.B na Wenzake (1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu (SAMIKISA); Sekondari na Vyuo. Dar es Saalam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha, Isimu na Nadharia; Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) LTD.
Saluhaya, M.C. (2010). Nadharia ya Lugha Kidato cha Tano na Sita. Dar es Salaam: CHILDREN EDUCATION SOCIETY (CHESO).
|
|
|
Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi? |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 11:35 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
DHANA YA SARUFI GEUZI NA SARUFI MIUNDO
Swali: Sarufi miundo virai inatofautianaje na sarufi geuzi?
DHANA YA SARUFI
Sarufi ni taaluma ya lugha inayochunguza na kuchanganua vipashio na kanuni mbalimbali zinazotawala muundo wa lugha, (Matinde, 2012.
Sarufi ni utaratibu wa kanuni ambazo humwezesha mtumiaji wa lugha kutunga tungo sahihi zinazoeleweka mara zinapotamkwa. (Kapinga, 1983).
Dhana ya sarufi inatafsiriwa katika mitazamo tofauti lakini yenye kuhusiana. Mtazamo wa kwanza tunaweza kusemaSarufi ni taaluma ya uchambuzi walugha inayojumuisha viwango vyote vya uchambnuzi yaani kiwango cha umbo sauti (fonolojia), kiwango cha umbo neno (fonolojia), kiwango cha miundo maneno (sintaksia) na kiwango cha umbo maana(semantiki), (Massamba, 1999).
DHANA YA SARUFI MUUNDO VIRAI
Sarufi muundo virai ni mkabala wa kimapokeo ambao haujihusishi na sarufi miundo katika marefu na mapana yake, ambapo zilijihusisha sana na sentensi sahili, (Massamba 1999).
Sarufi muundo virai ni kitengo cha sarufi geuza maumbo zalishi, ambacho hujikita katika matumizi ya sheria chache kuzalisha sentensi nyingi zisizo na kikomo, ambazo zina usarufi na hata zile ambazo hazijawahi kutungwa, ( Matinde, 2012).
Sarufi muundo virai ni mpangilio wa vitu vidogo vilivyowekwa pamoja na kujenga kitu kikubwa zaidi. Sarufi miundo virai ni mkabala wa kuchambua lugha kwa kuigawa sentensi katika virai vinayoiunda na kasha kuvichanganua zaidi hadi kufikia neno mojamoja lililokiunda kirai, (Massamba, 2001).
DHANA YA SARUFI GEUZI
Ugeuzi ni utaratibu unaotumiwa kubadili umbo la tungo kuwa umbo jingine kwa kutumia kanuni maalumu. Kwa hiyo ugeuzaji ni mbinu ya kisarufi ambayo hutumiwa katika sarufi geuza maumbo zalishi kuzalisha sentensi lukuki kwa kufuata sheria mahususi, (Matinde, 2012).
Sarufi geuzi hueleza ujuzi wa lugha ambao msemaji mzawa anao ujuzi anaomwezesha kutumia lugha (Habwe na Karanja,2007).
Sarufi geuzi maumbo ni utaratibu wa kubadili maumbo kuwa maumbo meng kwa kufuata kanuni maalumu (Matinde,2012).
Zifuatazo ni tofauti kati ya sarufi miundo virai na sarufi geuzi:
Hutofautiana katika lengo. Lengo la sarufi muundo lilikuwa halifahamiki zaidi ya kutumia taratibu za kijarabati zinazohusu ukusanyaji wa data na kuzichambua pamoja na kuunda kanuni kwa kutumia data hizo. Lakini,
Lengo la sarufi geuzi liko bayana, hujitokeza dhahiri. Lengo la sarufi hii ni kufafanua umilisi wa ujuzilugha ambao huwa mwanalugha anao. Umilisi huo humfanya mwanalugha kutambua viambajengo kati ka tungo, katika mtazamo wa ndani yaani muundo wa ndani.
Hutofautiana katika miundo. Sarufi miundo virai, hii huwa inajikita katika miundo ya nje, ambayo huchunguza na kuchambua sentensi katika umbo la nje.
Mfano; Mama anakula ugali
Hivyo huonyesha tu aina ya maneno husika katika sentensi au tungo kama vile: Mama- Nomino, Anakula- Kitenzi, na Ugali- Nomino. Ilihali,
Sarufi geuzi, hii huwa imejikita katika kuchungaza sentensi kama umbo la ndani na umbo la nje. Muundo wa ndani ni uchopekwaji katika miundo hiyo ambapo muundo wan je lazima upitie katika muundo wa mofofonemiki na kuweka katika kitengo cha fonolojia.
Hutofautiana katika vitengo. Sarufi geuzi ni sarufi ambayo inafumbata vitengo vyote vya lugha ambavyo ni fonolojia, sintaksia, semantiki, na mofofonemiki ambapo kitengo cha fonolojia hushughulikia sauti za lugha, kitengo cha kisintaksia hushughulika na uundaji wa sentensi, kitengo cha semantiki hushughulika na ufasili wa maana, na kitengo cha mofofonemiki huwa na kazi ya kuibadili njeo za wakati. Ilihali
Sarufi miundo virai hufumbata kitengo cha mofolojia ambapo sentensi iligawanywa katika kiunzi cha aina za maneno kama Nomino, Kitenzi, Kivumishi, Kielezi na kihunzi hicho kilijulikana kama utaratibu wa uchanganuzi wa viambajengo.
Hutofautiana katika uhusiano wa sentensi. Sarufi geuzi ilipiga hatua kubwa, kwanza huonyesha uhusiano uliopo kati ya maumbo mbalimbli ya sentensi au tungo. Na pia kuonyesha uhusiano unaoweza kuwepo baina ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Mfano: (1) Mtoto mrefu anacheza, na si kusema kuwa Mtoto anacheza mrefu
Huu ni uhusianao kati ya maumbo.
Mfano: (2) Juma alipiga mpira
Mpira ulipigwa na Juma
Huu ni uhusiano wa sentensi moja na sentensi nyingine. Ilihali
Sarufi miundo virai haionyeshi uhusiano kati ya sentensi moja na sentensi nyingine.
Hutofautiana katika uwazi. Sarufi geuzi huonesha sentensi sahihi na ambazo sio sahihi pia huonesha sentensi ambazo zinakubalika na sentensi zisizokubalika kwa msemaji mzawa. Ilihali
Sarufi miundo virai yenyewe haina uwazi huo.
Hitimisho ni kwamba, Sarufi geuzi ilianzishwa kutokana na mapungufu katika sarufi muundo virai. Sarufi iliyokuwepo, sarufi miundo virai, ilishindwa kuonyesha mahusiano yaliyokuwepo baina ya sentinsi zinazo husiana kimaana. Hivyo kutokana na upungufu huo kulikuwa na haja ya kuonyesha uhusiano huo.
MAREJELEO
Kapinga, M.C.(1983). Sarufi Maumbo ya Kiswahili Sanifu (SAMAKISA). Dar-es-Salaam:
TUKI.
Massamba, D.T., Kihore,M.Y.& Hokororo.(1999). Sarufi Miundo ya Kiswahili Sanifu
(SAMIKISA). Dar-es-Salaam: TUKI.
Matinde,S.R.(2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia. Mwanza: Serengeti Educational
Publishers (T) LTD.
|
|
|
OSW 224: FASIHI SIMULIZI : MTIHANI WA MWAKA – ODEX – MASWALI NA MAJIBU –FEBRUARI,2016 |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 11:21 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
OSW 224: FASIHI SIMULIZI : MTIHANI WA MWAKA – ODEX – MASWALI NA MAJIBU – FEBRUARI, 2016
- Kila jamii ina Fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Kwa vipi?
MAJIBU
Ni kweli kila jamii ina Fasihi simulizi yake tofauti na jamii nyingine. Utofauti huo unatokana na mambo mbalimbali kama vile. - Mila na desturi
- Mazingira
- Amali
- Historia ya jamii husika
- Misingi ya asili ya jamii husika
Misingi ya jamii ndio msingi wa Fasihi ya jamii husika na utofauti wa misingi hiyo ya kila jamii hufanya kila jamii iwe na Fasihi simulizi yake.
- “Fasihi simulizi iko Afrika tu! Ulaya hakuna Fasihi simulizi!” Jadili kauli hii.
MAJIBU
Jamii za Ulaya haziamini juu ya kuwepo kwa Fasihi simulizi, wao wanaamini kuwa maandishi “litera” ndiyo Fasihi pekee. Fasihi za kiafrika huchukuliwa kuwa ni ushenzi (kutostaarabika) na ushamba. Fasihi simulizi ya Afrika kwa asili haiwekwi katika maandishi kutokana na uwasilishaji wake na umuhimu wake. Miongoni mwa Fasihi simulizi za Afrika ni:
Jando na unyago, haya ni mafundisho ambayo hutolewa kwa vijana wa kiume na wa kike mtawalia. Mafundisho haya humjenga kijana wa kiafrika kuwa mchapakazi, mwadilifu na mtetezi wa jamii yake. Mambo haya kwa jamii za ulaya hayapo na huyaona kama ushamba.
Matambiko, ni ibada zinazowapa waafrika fursa ya kuwasiliana na miungu yao na kuelezea mahitaji yao ili kupata ufumbuzi.matambiko husaidia jamii kudumisha umoja na mshikamano na kutatua changamoto zao za kiimani. Jamii za Ulaya huona matambiko kuwa ni dhambi kutokana na imani za kimagharibi.
Ngoma, ni Fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hutumiwa kuburudisha, kuelimisha na kuleta jamii pamoja katika matukio mbalimbali ya kijamii ya furaha au huzuni. Kila jamii huwa na ngoma yake ya asili na hutambulishwa kwayo.
Hadithi za kimapokeo, hutumiwa kupitishia maarifa ya kijamii kwa vizazi chipukizi kupitia masimulizi ya mambo hayo kwa vijana na watoto. Hadithi kama ngano, vigano, tarihi na visasili hubeba amali mbalimbali za jamii.
Miviga, ni Fasihi simulizi ya kiafrika ambayo hufanyika msimu wa mavuno na huambatana na sherehe za kijamii kama kusimika viongozi, kumtoa mwali au kuwapeleka vijana jandoni. Miviga hutumiwa pia kuwaleta watu pamoja na kuwasahaulisha watu madhila mbalimbali.
Kwa ujumla Fasihi simulizi inapatikana Afrika kwa kiasi kikubwa kutokana na mazingira na mahitaji ya jamii husika.
- “Wa mbili havai moja na maskini akipata matako hulia mbwata”. Eleza maana na dhima ya semi hizi.
MAJIBU
Katika maisha kila mtu amepangiwa bahati yake. Kuna ambao kupata ni kawaida na kuna wale ambao kupata sio kawaida. Makundi haya mawili ya watu ndiyo huzaa methali ya “Wa mbili havai moja” na “Maskini akipata matako hulia mbwata”. Methali hizi zinafafanuliwa kama ifuatavyo.
Wa mbili havai moja, methali hii inamaana kuwa alichopangiwa mtu na Mola ndicho atakachopokea hata kama patatokea watu wenye chuki na husuda dhidi yake. Kuna watu huwa hawafurahishwi na mafanikio ya watu wengine kiasi cha kufanya mipango ya kukwamisha mafanikio ya watu wengine.
Dhima ya methali hii ni kuwahamasisha watu kuongeza bidii katika kutafuta mafanikio yao badala ya kuhangaika kuzuia mafanikio ya wengine ambayo hasa ni mipango ya Mungu.
Masikini akipata matako hulia mbwata, methali hii inaelezea tabia ya baadhi ya watu kuonesha ufahari pindi wanapopata mafanikio kidogo maishani mwao. Watu hawa hasa ni wale ambao hawaamini kama wanastahili kufanikiwa ndio maana wakipata kidogo tu hujisahau na kuonesha ufahari.
Dhima ya methali hii ni kuwatahadharisha watu kutoonesha ufahari wanapofanikiwa kwa kujua kuwa mafanikio huweza kuwa ya muda nay a kupita lakini utu na uhusiano mwema hudumu daima.
Kwa ujumla methali ni kipengele muhimu cha semi chenye kuhifadhi na kurithisha hekima na busara za jamii.
- Fasihi simulizi huchapuza kazi. Mfano: kilimo n.k.! thibitisha dai hili.
MAJIBU
Chapuzo ni Fasihi simulizi itumiwayo sana kuchochea na kuhimiza kazi katika jamii. Nyimbo za kuchapuza hutofautiana kulingana na kazi husika. Kwa mfano:
Chapuzo za wavuvi, hizi huimbwa na wavuvi wawapo majini katika shughuli zao hasa usiku. Nyimbo hizi huitwa kimai. Hutumika kuwaondolea wavuvi ukiwa na unyonge.
Nyimbo za vita, hizi huimbwa na wanajeshi msimu wa vita ili kuwapa morali wanajeshi wawapo vitani. Chapuzo huwafanya wanajeshi wasiwaze sana kuhusu madhara ya vita na kujiondolea woga na hofu ya kufa.
Chapuzo ya watwanzi, huimbwa na akina mama wakati wanapotwanga kikoa hasa vijijini ambapo huwa hakuna maendeleo ya mashine za kuzalisha unga, kukoboa mpunga au kupwaga ulezi. Kazi ngumu za utwanzi zinapofanywa na akina mama basi huanzisha nyimbo mbalimbali ambazo huwafanya wasichoke wala kuhisi uvivu.
Katika kazi za udobi pia hutokea chapuzo pale ambapo mfuaji hujiimbia wimbo aghalamu usio na maneno ya kusikika sana ilimradi tu hujifariji na kujisaulisha ugumu wa kazi yake na hatimaye hujikuta amemaliza kazi bila kuhisi uchovu sana.
Kwa hali hiyo ni dhahiri kuwa chapuzo ni kipengele muhimu sana cha Fasihi katika kuifanya kazi yoyote au mazingira ya kazi kuwa mepesi na yasiyochosha.
|
|
|
OSW 224: FASIHI SIMULIZI : MASWALI NA MAJIBU – JARIBIO KUU MAALUMU – FEBRUARI, 2013 |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 11:09 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
OSW 224: FASIHI SIMULIZI : MASWALI NA MAJIBU – JARIBIO KUU MAALUMU – FEBRUARI, 2013
- Hakiki kwa kutoa mifano ya nchi moja mbili zinazotoa picha halisi ya hadithi.
MAJIBU
Hadithi ni miongoni mwa kazi za Fasihi simulizi zenye kuonya, kuadibu na kuadilisha jamii hasa watoto. Hadithi kwa asili husimuliwa kwa watoto nyakati za jioni baada ya kazi ili kuwafunza maadili mema.
Tanzania ni moja ya nchi zenye kutumia hadithi kwa kiasi kikubwa sana kama ifuatavyo:
Hadithi za kimapokeo kama ngano hutumiwa kuwakumbusha watoto matukio ya asili yaliyowahi kuikumba jamii. Hadithi hizi hushabihiana na maisha halisi ya jamii kwa mfano masimulizi juu ya habari za maisha ya Mfalme na Malkia wa nchi fulani jinsi walivyoishi maisha ya raha mustarehe.
Hadithi za visasili, hizi hutumiwa kuelezea jinsi matukio au maumbile na tabia fulani zilivyoanza katika jamii, mfano kisasili cha “Asili ya Jogoo kuwika”, “Asili ya kiboko kuishi majini” ni mifano ya hadithi za kitanzania zinazosaidia watoto kupata majibu ya maswali ya kisayansi kwa njia isiyohusisha usayansi.
Hadithi za tarihi, ni hadithi za kitanzania ambazo husimuliwa kuhusu matukio ya kihistoria yaliyowahi kutokea katika jamii na wakati wa kutokea kwake, mfano tarihi za njaa, ukame, vita na majanga mbalimbali yaliyowahi kuikumba jamii.
Hadithi za vigano, hizi hutolewa kwa lengo la kukemea tabia na mienendo isiyofaa kwa jamii kama vile ulafi, uchoyo, udokozi, mfano kigano cha “Mtoto aliyeficha kitumbua” kwenye sanduku la nguo na kukisahau, kisha panya akala kitumbua pamoja na nguo yake mpya ya sikukuu. Hadithi hii hukemea tabia ya uchoyo kwa watoto.
Hadithi za soga, haya ni masimulizi yatumiwayo na watu kupoteza muda. Soga huwa na visa zaidi ya kimoja na huwa kisa kinaweza kusimuliwa nus utu na kisiendelee. Kupitia soga watu hupashwa ukweli na kujirekebisha kitabia.
Kwa ujumla Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosheheni hadithi mbalimbali zenye kuvutia na kutia hamasa.
- Kwa kutumia Fasihi simulizi jadili suala la mipango ya kizee ya kuandalia ndoa vijana wao.
MAJIBU
Ni fikra potofu kudhani kuwa mipango ya wazee kuandalia ndoa vijana wao imepitwa na wakati. Ukweli ni kuwa ndoa zilizoandaliwa na wazee zilidumu sana kuliko hizi za siku hizi ambapo vijana huchaguana wenyewe. Faida za wazee kuandalia ndoa vijana wao ni nyingi kama zifuatazo:
Kwanza, vijana hasa wa kike walijitunza na kujiheshimu kwa kutambua kuwa wanachunguzwa na wazee nap engine wakakosa sifa za kuposwa iwapo hawatajiheshimu na kujitunza.
Pili, uhusiano wa vijana haukuleta madhara kama ilivyo sasa kutokana na uhuru. Vijana walijiepusha na mahusiano kabla ya ndoa ili kulinda heshima ya familia nzima. Kubeba ujauzito kabla ya ndoa lilikuwa ni kosa la kulaanika.
Tatu, ilisaidia kudhibiti mmomonyoko wa maadili tofauti na ilivyo hivi leo ambapo wazee kujihusisha na vijana wadogo kimapenzi kwa sababu ya uhuru wa kujichagulia na kujiamulia.
Vilevile, wazee walikuwa kinga ya kuvunjika hovyo kwa ndoa kwa sababu vijana walioozwa na wazee zoezi la kuachana lilitakiwa kuwahusisha wazee na waridhie, hii ilichangia uvumilivu na kuheshimiana ndani ya ndoa.
Ndoa za kuandaliwa na wazee zilizuia kuzaliwa watoto wasio na malezi au kukataliwa kwa watoto kwa sababu ndoa zilisimamiwa na wazazi wa vijana.
Kwa ujumla ndoa zilioandaliwa na wazee zilikuwa ndoa bora sana na zilidumu sana kuliko hizi za kuchaguana ambazo huleta migogoro isiyokwisha.
- Kizuka kwa mfiwa, aliolewa na ndugu mkubwa wa marehemu kwa ajili ya kuendeleza na kulea kizazi nani kwa hiari kwa wanaooana. Jadili na toa mifano hai.
MAJIBU
Kizuka kurithiwa na ndugu wa mume ni mila za jamii nyingi za kiafrika na hata Tanzania. Jambo hili kwa sasa linatazamwa tofauti kulingana na maendeleo ya mila za kigeni zilizovamia na kuziteka nyara mila za kiafrika. Hebu tuangalie faida zake na kisha hasara zinazoelezwa na wanaopinga suala hilo.
Faida ya kwanza ni kuwa familia ya marehemu hutunzwa na kuendelezwa na mrithi wa familia hiyo na hasa watoto hupata malezi yanayostahili.
Pili, huepusha migogoro ya mirathi za marehemu kwa sababu uamuzi wa nani arithi familia hufanywa na kikao cha familia au ukoo na kuheshimiwa na wote.
Husaidia kuepusha uchanganyaji wa damu iwapo mke ataolewa na mtu wa nje ya ukoo wa mume wake wa kwanza.
Pia humpunguzia machungu kizuka haraka tofauti na kama ataachwa na pengine kufukuzwa kwenye nyumba ili ajitafutie maisha.
Pamoja na faida hizo pia zipo hasara zinzoelezwa hasa na makundi ya watetezi.
Kwanza inasemwa kuwa ni kinyume cha haki za mwanamke hasa inapotokea kizuka huyo hakuridhia jambo hilo.
Pili inaonekana kuwa ni hatari kiafya endapo mrithi atakuwa na maradhi ya kuambukiza huweza kumuambukiza kizuka.
Kwa ujumla zipo mila na desturi ambazo pamoja na faida zake jamii inaziona kuwa zimepitwa na wakati na hivyo kufanya juhudi kuziacha.
- Nyimbo za harusi zinafundishaje wari?
MAJIBU
Nyimbo za harusi ni sanaa ya kifasihi simulizi ambayo hutumiwa kuwafunda wari katika sherehe yao ya ndoa. Miongoni mwa mambo yanayofundishwa ni:
Kuhusu utii, wari hufundwa kutii waume zao katika ndoa, kupitia nyimbo za makabila mbalimbali.
Vilevile, wari hufundwa kuhusu kazi na majukumu yake kama mama wa familia, kupitia nyimbo hukumbushwa majukumu yake kama kupika, kumuandalia mume na namna ya kutunza nyumba.
Masuala ya usafi pia huzungumzwa katika kumfunda mwari. Usafi binafsi pamoja na mazingira yanayomzunguka. Mwari mchafu hutia aibu familia iliyomlea na kumkuza.
Mwari hufundwa pia kuhusu namna ya kulea watoto pindi watakapobarikiwa kuwapata. Sehemu kubwa ya malezi kwa jamii za kiafrika huachiwa mama na watoto wanapokosa malezi bora hulaumiwa mama.
Utanzu wa nyimbo ni kipengele kinachogusa sehemu kubwa ya maisha ya jamii katika kuadibu na kuadilisha.
- Dhana ya R. Finegan Afrika haina Fasihi ni ya kweli? Jadili kwa mifano dhahiri kwa kumrejelea R. Finegan 1970.
MAJIBU
Finegan, 1970 ni miongoni mwa wataalamu wa kigeni waliopotosha sana historia ya Kiswahili na Fasihi yake kwa kudai kuwa Afrika ni bara la giza na haina Fasihi. Mawazo hayo potofu yalijengwa na imani yao juu ya maandishi kwamba kisichoandikwa hakiwezi kuwa Fasihi.
Ukweli ni kwamba Afrika ina Fasihi na tena wazungu waliitumia sana kuiga mambo mengi yanayowanufaisha hadi sasa.
Mfano wa kwanza ni kuwepo kwa ngoma ambazo hutambulisha makabila mbalimbali ya kiafrika hususani Tanzania. Mpaka leo wageni toka nje ya Tanzania hupokelewa na ngoma za asili.
Utanzu wa hadithi ni kielelezo cha kuwepo Fasihi Afrika. Zipo hadithi za kimapokeo zinazohusu matukio ya zamani sana kama masimulizi ya Fumo Liyongo, hadithi za Ng’wanamalundi ni baadhi ya hadithi za zamani sana na zinazohusu watu wa Afrika waliowahi kuacha historia kubwa katika jamii zao.
Jando na unyago ni sehemu ya Fasihi ya kiafrika itumiwayo kama darasa la kutolea elimu kwa vijana wa kike na kiume na kuwaandaa kwa maisha ya utu uzima.
Matumizi ya ala za muziki za asili, kama marimba, zeze, zumari, ni miongoni mwa vyombo vingi vya muziki toka jamii za watu wa Afrika na baadhi yavyo wazungu wameiga kwa mfano zeze (gitaa), marimba (kinanda) kutaja kwa uchache.
Kazi nyingi za Fasihi kwa lugha ya Kiingereza zilizotungwa na waafrika kama Wole Soyinka, Chinua Achebe, Ngugi wa Thiong’o na E.Kezilahabi na bila kumsahau Shaaban Robert ni ushahidi wa wazi kwamba Afrika ina Fasihi tena kongwe.
- Fasihi simulizi ya kabila lako ina msaada gani katika kujenga maadili ya nchi yetu?
MAJIBU
Maadili ya nchi hujengwa kwa ushirikiano wa jamii nzima. Katika Fasihi makabila hutoa mchango tofautitofauti katika kuadilisha jamii na nchi kwa ujumla. Mchango huo ni kama ufuatao:
Nyimbo mbalimbali za makabila huweza kutumiwa kuhimiza maadili ya jamii nzima na hatimaye kuisaidia nchi kwa mfano nyimbo za kazi toka makabila mbalimbali huhimiza uadilifu katika kuchapa kazi.
Kutoa maonyo kwa jamii huweza kufanywa kupitia methali mbalimbali mfano methali hii ya kipare “Kivuke cha ibwe kimanywa ni igondwa” maana yake ni “ siri ya kaburi huijua maiti” methali hii hutoa maonyo kwa jamii kutohamakia mambo kwa kuyaona kwa nje tu.
Kuhimiza nidhamu na utii katika jamii kwa mfano methali kama, “asiyesikia la mkuu huvunjika guu” inahimiza utii kwa wakubwa.
Kuhimiza kazi kama uti wa mgongo wa maisha ya jamii, kwa mfano majigambo huhimiza ushiriki wa kila mwanajamii katika uzalishaji mali na kujiondolea umaskini.
Masuala ya ushirikiano wa kijamii ni suala muhimu sana kwani umoja ni nguvu. Suala hili husisitizwa kupitia ngoma, utani na matambiko ambapo watu huletwa pamoja kupitia matukio hayo na kuwa kitu kimoja katika shida na raha.
Yote kwa yote Fasihi simulizi ya kabila lolote la kibantu huchangia sana katika kujenga maadili ndani ya nchi yetu.
|
|
|
SWALI: Jadili dhana ya ubunilizi katika Kufikirika na Mirathi ya Hatari |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 09:35 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
SWALI:
Jadili dhana ya ubunilizi kama inavyojitokeza katika riwaya ya Kufikirika na Mirathi ya Hatari.
Kazi yetu imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi, kiini cha kazi na hitimisho. Katika utangulizi kuna maana ya riwaya na maana ya ubunilizi, katika kiini cha kazi kuna vipengele vya ubunilizi kama vilivyojitokeza katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI na KUFIKIRIKA, na hitimisho ni mawazo kuhusu dhana na vipengele vya ubunilizi kama ilivyojikeza katika riwaya hizo.
Riwaya ni kazi ya kinathari au kibunilizi ambayo huwa na urefu wa kutosha, msuko uliojengeka vizuri, wahusika wengi walioendelezwa kwa kina, yenye kuchukua muda mwingi katika maandalizi na kuhusisha mandhari maalumu (Wamitila, 2003).
Riwaya ni utungo wenye sifa ya ubunifu, usimulizi, mpangilio au msuko fulani wa matukio, ufungamano wa wakati, mawanda mapana na uchangamano (Mulokozi, 1996).
Kwa ujumla, riwaya ni masimulizi ya kinathari yenye ubunilizi na yenye kutumia lugha ya mjazo katika kuwasilisha mawazo yake.
Ubunilizi ni ubunifu aliyonao mtunzi kwa kubuni na kuingiza au kutumia kazi yake ili ilete mvuto na manato kwa hadhira. Mbinu hii huakisi kipawa cha utunzi alichonacho mtunzi na kumtofautisha na watu wengine.
Kwa kutumia vitabu viwili vya riwaya KUFIKIRIKA kilichoandikwa na SHAABANI ROBERT, na MIRATHI YA HATARI kilichoandikwa na C.G MUNG’ONG’O, vifuatavyo ni vipengele vya kibunilizi vilivyojitokeza katika riwaya hizi;
Dayalojia, ni kitendo cha mtunzi kutumia kauli za majibizano katika kuwasilisha mawazo yake au kazi yake katika jamii husika. Katika kipengele hiki mwandishi hutumia vinywa vya wahusika katika kuwasilisha maudhui aliyonayo katika jamii husika. Kwa mfano katika kitabu cha KUFIKIRIKA mwandishi ametumia dayalojia ndani ya masimulizi kama inavyojidhihirisha katika (uk… 27),
Mfalme anasema: “nimetumia fedha nyingi kwa mafunzo yako lakini mwalimu wako wa kwanza hakufanya kitu ila upotevu…” Mtoto wa mfalme anajibu “wajua baba kuwa mimi sichukii mtu ambae amekubaliwa na utukufu wako. Lakini mwalimu huyu ni bora?…”
Vilevile, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI dayalojia imejitokeza katika (uk. 19), mazungumzo kati ya Gusto na Mzee Mavengi yanayohusu usihiri;
Mzee Mavengi: “unaziona shanga hizi? Gusto: ndio
Mzee Mavengi: na manyoya haya?
Gusto: ndio
Mzee Mavengi: Basi hili baba yako alilitumia kama ndege ulaya akiwamo kazini”.
Ujadi, ni utumiaji wa kauli, matendo au mazingira ya asili yanayofungamana sana na jamii inayoandikiwa. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia kipengele cha ujadi katika kazi yake kama vile methali, misemo na mazungumzo mbalimbali ya jamii husika; mfano katika (uk. 5), mwandishi ametumia methali isemayo “nyumba ya mgumba haina matanga”, vilevile mwandishi ametumia misemo mablimbali kwa mfano (uk. 37), “maisha ya mwongo ni mafupi”, pia mwandishi ametumia matendo mbalimbali ya kiganga katika kusawiri maisha halisi ya jamii husika kama ilivyoelezwa katika sura ya pili (uk. 8) na kuendelea ambapo mwandishi ameonesha makundi mabalimbali ya waganga pamoja na shughuli zao, makundi hayo ni:
“waganga wa mizizi,
waganga wa makafara,
Waganga wa mazinguo,
waganga wa hirizi,
waganga wa mashetani,
waganga wa utabiri”
Waganga wote hao wanatumia dawa mbalimbali za asili kama mitishamba, dawa za wanyama, makombe, mashetani na ramri za kila aina.
Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia methali, nahau, matambiko, na vyakula vya asili mfano, kiapo katika matambiko (uk. 16-17) anasema;
“nye misoha gya vakuhu
Nye vasehe yemwalonguwe
Nye vayangu yetulilumwi”
Pia mwanndishi ameonesha ujadi kwa kutumia vyakula vya asili kama vile maboga ya kuchemshwa na viazi vya kuchomwa, (uk. 3).
Utomeleaji, ni muingiliano wa tanzu, utanzu mmoja kuingilia au kuwekwa kwenye utanzu mwingine, mwandishi wa riwaya ya KUFIKIRIKA ametumia shairi katika (uk. 18) kama usemavyo;
“MFALME na MALKIA,
Katika KUFIKIRIKA,
Siku ya kuzaliwa,
Mtoto tuliyetaka….”
Halikadhalika, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia mbinu hii kwa kutumia barua, nyimbo, na simu ya maandishi mfano simu ya maandishi (uk. 9) anasema;
“GUSTO BABA MAHUTUTI NJOO HARAKA KITAMBI”
Pia picha inayoonekana juu ya kitabu pamoja na nyimbo (uk. 16,17, 32 na 33),
mfano katika (uk. 33) Mavengi anaimba,
“Gende ve dadna, gende
Umvipwawo apigile uwivina
Avedze lukule
Gende, yane danda gende…”
Tanzia, ni mbinu ambayo mwandishi hutumia vipenegele mbalimbali ambavyo huibua huzuni, masononeko, masikitiko au mateso na majonzi kwa hadhira yake. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi anasema; “Mimi na malkia tumefadhaishwa mno na ugumba na utasa katika nyumba yetu wala hatujui tufanye jambo gani litawezaa kutufanya kuwa wazazi wa mtoto ambaye atarithi ufalme wa Kufikirika” (uk. 5). Pia katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi ametumia utanzia wa majonzi kwa Gusto kutokana na kufiwa na baba yake (uk. 13) ambapo anasema “tulimzika hayati baba…” mfano mwingine ni kutoka kwa mama Gusto ambapo anamwambia mwanae Gusto akisema “sipendi nimpoteze tena hata mmoja wenu kabla sijafa, alikaribia kulia nikamwonea huruma lakini wazo lilikua limekwisha kunivamia akilini..” (uk. 29).
Ufutuhi, ni mbinu ambayo msanii hutumia ucheshi au furaha kwa hadhira yake mfano kejeli, utani, dhihaka, raha, ubeuzi na mizaha. Mfano Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia ufutuhi kama vile dhihaka (uk. 27) anasema; “naona sura yake imechujuka kwa fikra”, pia katika (uk. 17) anasema “Nimefurahi sana kwa kujaliwa kupata mtoto na nimependezwa mno…….”. vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia ufutuhi kupitia utani kati ya John, Gusto na Rajabu (uk. 8), anasema “akamjibu kwa shere hunielewi nini yakhe? Una baridi ya bisi nini kaka?”.
Taharuki, ni hali ya kuwa na shauku ya kutaka kujua juu ya nini kitafuatia katika usimulizi wa kazi ya fasihi. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ameonesha taharuki kwa kutumia jina la kitabu “KUFIKIRIKA” ambapo humfanya msomaji kutaka kujua zaidi nini kilichomo ndani ya kitabu, na masuala ya usihiri (uk. 8), mwandishi ameonesha kwa kutumia mambo ya ushirikina ambapo msomaji hutaka kujua nini kinachofuata katika riwaya. Vilevile, katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia taharuki mbalimbali ikiwemo pale Gusto anapokua anaongea na baba yake kwa mara ya mwisho (uk.12) kuhusu kumrithisha mambo ya usihiri.
Mfano;
Hapo nilishituka nikamaka “Baba…!”“Najua hukulitegemea hili, mwanangu lakini hakuna mwingine wa kunirithi” sauti yake ilikuwa ya kutetemeka yenye amri. Alisema “Jina lako nimekwishalipeleka mbele ya wenzangu watakapokuja usishangae”.
Usawiri wa wahusika, ni kitendo cha kuwachora, kuwafafanua, kuwatambulisha na kuwajemnga wahusika huku wakipewa maneno, matendo, hadhi na uwezo unaolandana au unaouwiana na uhusika wao. wahusika hutumia mbinu kadha wa kadha ili kusawiri uhusika wao katika kazi ya fasihi ikiwemo majazi,uzungumzaji nafsi,kuzungumza na hadhira ,kuwatumia wahusika wengine ,ulinganifu na usambamba wa maelezo. Katika riwaya ya KUFIKIRIKA mwandishi ametumia mbinu ya majazi, mfano, kiongozi amepewa jina la “mfalme”, pia “malkia” ambaye ni mke wa mfalme katika (uk. 1), na “utubusara” (uk. 48) ambaye ni mtu mwenye busara. Vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI, mwandishi amemtumia mhusika Gusto anaposhuhudia mambo ya usihiri (uk.80) anasema;
“Nilimwangalia mzee huyu akienda angani kama kimulimuli”
Ufumbaji, huu ni utumiaji wa kauli zenye maana fiche, Ufumbaji hujitokeza katika kichwa cha habari,majina ya wahusika,sura ya kazi,na hata aya. Mwandishi wa riwaya ya KUFIKIRIKA ametumia kauli zenye kuonesha maana fiche,kauli ambazo huwa na maana tofauti na umbo la nje la kazi au matini husika.Katika riwaya hii ufumbaji umejitokeza katika (uk.28)anasema;
“Kutu huaribu chombo kisichotumiwa.Lazima ubongo wake utengwe na uharibifu wa kutu”.
Vilevile katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia kipengele hiki katika kazi yake, ametumia ufumbaji au fumbo katika(uk.8) ambapo anasema;
“ Gusto kapata simu!”
alitamka rafiki yangu John.
“Atavuta sigara leo”.
Ritifaa,ni hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye, umbali huo waweza kuwa wa kijografia au kufariki. Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI Mwandishi ametumia ritifaa kupitia kiapo cha asili ambapo Gusto anaapa ili arithi mikoba ya uchawi wa baba yake (uk.17). Anaapa kwa mizimu akitumia lugha ya asili ambayo kwa Kiswahili ina maana ya ;
“Enyi mahoka wa mababu,
Enyi wazee mliotangulia,
Enyi wenzangu,
Sikilizeni kiapo change,
Sitasema wala kuwaza lolote,
La ndani ni la ndani,
Nishindwe mara tatu,
Pembe hili linichome moto…!”
Pia katika (uk. 71-72) ambapo Gusto yupo makaburini anaongea na mpenzi wake ambae alishafariki. Anasema; “pokea zawadi hizi za maua mfuto….”
Kisengerenyuma, hii ni namna ya kupangilia vitushi au kusimulia kwa kuanza na tukio-tokeo kisha kufuatia tukio-chanzi ili kuboresha hamu ya hadhira kujua muundo wa vitushi katika kazi husika. Katika riwaya ya MIRATHI YA HATARI mwandishi ametumia mbinu hii katika (uk. 1) ambapo ameonesha tayari Gusto emerudi kutoka chuo lakini katika (uk. 3) ameonesha historia ya Gusto tangu alipozaliwa.
Hivyo basi, watunzi wa riwaya zote mbili wametumia kwa kiasi kikubwa mbinu mbalimbali za ubunilizi ili kuleta mguso pamoja na kuzifanya kazi zao ziweze kuvutia. Lengo kuu la kutumia vipengele vya ubunilizi ni kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa hadhira yake ambapo kwa kiasi kikubwa waandishi wamefanikiwa kufikisha ujumbe kwa jamii husika.
MAREJELEO
Mulokozi,M.M.(1996), Fasihi ya Kiswahili,Dar es salaam:OUT.
Mung’ong’o C.G. (2016), Mirathi ya Hatari. Dar es salaam. Tanzania. Mkuki na Nyota Publishers Limited.
Shaaban R (2013), Kufikirika. Dar es salaam. Tanzania: Mkuki na Nyota Publishers limited.
Wamitila. K.W (2003), Kamusi ya fasihi; Istilahi na Nadharia. Nairobi. Focus publication Ltd.
|
|
|
SWALI: Vipengele vya kibunilizi vimejitokezaje katika Kufikirika na Mirathi ya Hatari |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 09:17 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
SWALI:
Vipengele vya kibunilizi vimejitokezaje katika riwaya ya Kufikirika na Mirathi ya Hatari?
MAJIBU
Kazi hii imegawanyika katika sehemu kuu tatu ambapo sehemu ya kwanza ni utangulizi ambao umebeba fasili ya riwaya na dhana ya ubunilizi, sehemu ya pili ni kiini cha swali ambacho kinaonesha vipengele vya ubunilizi kama vile ufutuhi, utomeleaji,ritifaa,ufumbaji,tanzia,usawili wa wahusika na ujadi jinsi vilivyojitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” iliyoandikwa na C.G.Mung’ong’o na riwaya ya “Kufikirika”iliyoandikwa na Shaaban Robert na sehemu ya tatu ni hitimisho ya kazi hii ambayo imebeba umuhimu wa vipengele vya ubunilizi katika riwaya ya Kiswahili kwa ujumla wake.
Riwaya ni hadithi iliyotungwa ambayo ina urefu wa kutosha, visa vinavyooana na ambayo imezingatia suala la muda. (Mlacha na Madumlla 1991).
Riwaya ni utungo wa kinathari wenye maneno kati ya 35,000 hadi 75,000 ambapo riwaya fupi huwa na maneno kati ya 35,000 na 50,000 na ndefu huwa na maneno kama 75,000. (Mphahlele 1976).
Riwaya ni utanzu unaoweza kuanzia maneno 35,000 na kuendelea. (Muhando na Balisidya 1976).
Udhaifu wa fasili hizi ni kuwa kufasili dhana ya riwaya kwa kutumia kigezo cha maneno haitoshi kwani mtu anaweza kuweka habari yoyote ile katika idadi hiyo ya maneno lakini isiwe riwaya. Hapa jambo la muhimu ni kuwa inapaswa ksuwa na mchangamano wa matukio, ujenzi wa wahusika na dhamira, muundo wake na hata mtindo.
Kwa ujumla, riwaya ni utanzu wa fasihi andishi unaohusu kazi ndefu za kibunifu za kinathari ambazo zina mawanda mapana, (visa, matukio, dhamira, wahusika, muundo na mtindo) na mchangamano wa fani na maudhui yake na kuzungumzia tukio la wakati fulani mahususi.
Ubunilizi ni uwazaji na uundaji wa wazo katika hali inayohalisika. Aghalabu dhana hii imetokana na kitezi “buni” ambalo humaanisha kuunda jambo ambapo jambo hilo huwa katika hali ya kidhahania kabla halijaonekana au kudhihirika kwa hadhira kupitia ogani za fahamu. Kupitia ubunilizi msanii ama mtunzi ana uwezo wa kubuni visa na wahusika kwa njia ambayo haikanganyi katika maisha na kuleta uhalisia.
Vipengele vya kibunilizi vinajitokeza katika riwaya mbalimbali vikitumiwa na waandishi wenyewe kwa madhumuni mbalimbali, hivyo vifuatavyo ni vipengele vya kibunilizi kama vilivyojitokeza katika riwaya ya “Kufikirika” iliyoandikwa na Shaaban Robert na“Mirathi ya hatari”iliyoandikwa na C. G. Mung’ong’o;
Ritifaa, hii ni hali ambayo mtu mmoja hufanya mawasiliano na mtu aliye mbali naye kijiografia au kifikra. Mtu huyo anaweza akawa anazungumza na mtu aliyekufa zamani au mtu aliyesafiri na yuko mbali na hivyo anaongea naye kwa fikra tu. Kwa mfano katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”ritifaa imejitokeza wakati Gusto anaapishwa kule pangoni. Mzee Mavengi anasema katika ukurasa wa (17),“Enyi mahoka wa mababu, enyi wazee mliotutangulia”. Hapa mzee Mavengi anaongea na watu waliokufa zamani (wazee) na mahoka (vitu ambavyo havionekani) kifikra tu. Pia wakati Gusto anakwenda kwenye kaburi la mpenzi wake Dina anaongea peke yake juu ya kaburi kama vile anaonana na Dina akiwa hai, ukurasa wa (72) anasema, “Dina, sina budi kuondoka kesho jioni kurudi shuleni. Itakuwa ni muda mrefu baadaye nitakapokuja kukuona tena, lakini kurudi ni sharti nitaarudi. Hili naahidi. Nachukia sana kukuacha peke yako.” Anayaongea yote hayo akiwa juu ya kaburi la Dina kama anaongea na Dina aliye hai. Piakatika kitabu cha “kufikirika” kipengele hiki kimejjitokeza hasa katika matatizo ya mfalme. Katika Ukurasa wa (3) Mfalme anajisemea mwenyewe,“maskini mwenye mtoto namuona kuwa ni bora kuliko mimi na pengine moyo wangu huona wivu juu yake”. Pia Ukurasa wa (3) Mfalme anajisemea mwenyewe, “lakini ni sikitiko kubwa kwa kukosa mtoto”. Pia Ukurasa wa (25) Mfalme anajisemea,“Kijana safihi na mbumbumbu! Sijapata kuona mfano wake. Namna watu kama hawa wapatavyo ualimu na sifa mimi sielewi”. Hapa mfalme alikuwa akizungumza peke yake yaani anaongea na hadhira ambayo haiko karibu naye bali ni katika mawazo yake tu.
Utanzia, utanzia ni hali ya kuleta huzuni kwa kutumia vipengele mbalimbali kwa hadhira yake. Utanzia hujengwa kwa kutumia mambo mbalimbali kama vile; mateso, ugumu wa maisha, mabaa kama njaa na magonjwa. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari utanzia unajitokeza pale Gusto anapopelekwa kwenye moto na mzee Malipula ili akubali kuwa yeye ndiye aliyemuua Kapedzile. Mwandishi anasema katika ukurasa wa (48),“…Nilipotamka neno hapana tu Malipula alinishika kwapani akanisogeza karibu na moto huo. Miguu yangu ikawa nusu mita hivi kutoka motoni. Maumivu yalliyofuatia yalikuwa hayavumiliki, nikajaribu kujivuta lakini sikuweza.” Utanzia pia unajitokeza wakati Gusto akiwa kwenye njozi anapoona mama yake na dada yake Nandi wakiungua kwa moto na kugundua kweli walikuwa wamekufa kwa kuchomwa na moto. Mwandishi anasema ukurasa wa (78), “Moto uliendelea na uharibifu wake kwa kasi ya ajabu. Mama na Nandi wakateketezwa kwa moto! Dakika ile nilisikia uchungu usio kifani! Moyo ulinusuru kupasuka. Nikalia kilio cha huzuni isiyo tumaini…..uchungu wa mama ukanichoma moto!Pia kifo cha Dina mpenzi wake Gusto kinaleta huzuni ukurasa wa (72).Pia katika riwaya ya “Kufikirika” dhana hii imejitokeza kama ifuatavyo. Ukurasa wa (32), “wakati mtoto wa mfalme akiwa mgonjwa, mfalme alisema “lakini mtoto niliyepata sasa ni mgonjwa sana. Yaonekana kwamba matumaini yangu yote ya kurithiwa na mwanangu karibu yatapondwa chini”. Pia katika Ukurasa huohuo, mfalme anasema “Mwanangu akipatwa na faradhi msiba utanipeleka ahera mara moja”. Kukosa mtoto ni tatizo ambalo lilikuwa linamsumbua mfalme na kujiona kuwa hafai katika jamii yake.Matukio kama haya husababisha huzuni na jitimai kwa msomaji au msikilizaji kwa kumhurumia mhusika.
Kisengelenyuma, ni hali ya kusimulia kwa kuanza na tukio tokeo na kumalizia na tukio chanzi. Mwandishi huanza kuonesha kitu kilichopo tayari kabla kuelezea kilivyotokea. Kwa mfano riwaya ya “mirathi ya hatari” mwanzoni kabisa mwandishi ameanza kuonesha tayari Gusto akiwa chuo kikuu kabala ya kuelezea huku nyuma alisomea wapi shule ya msingi na sekondari. Pia ameanza kuonesha mkasa ambao ulimpata Gusto na familia yake kwa ujumla kabla ya kuonesha ulivyotokea au ulisababishwa na nini? Anasema ukurasa wa (1-2), “….kwa jumla ni hali inipayo ridhisho ambalo sijawahi kulipata mahali pengine tangu nyumba yetu ifarakane katika mkasa ule uliokitikisa kijiji chetu ukaashiria mfarakano mkubwa Zaidi, mkasa uliokiacha kijiji kizima katika mahame”. Pia mwandishi anaelezea mahusiano yaliyopo tayari kati ya Gusto na Lulu na mipango ya kuoana kabla ya kuelezea Lulu na Gusto walianzaje kuingia katika mahusiano ya kimapenzi. Anasema ukurasa wa (2), “kwa yakini ni ridhisho ninaloweza tu kulishabihisha na penzi la Lulu-Lulu yule aliyeniliwaza mawazo akanipa upendo dhahiri hata nikasahau kabisa uzito wa maisha ya ukiwa. Kwa hakika maisha yangu bila yeye sijui yangekuwaje. Mipango yangu sasa ni kumwoa punde tumalizapo masomo yetu hapo mwakani.”
Utomeleaji, huu ni mwingiliano wa tanzu zingine za fasihi katika riwaya. Kwa mfano, mtunzi kuchopeka ushairi kwenye riwaya na matumizi ya barua. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” mwandishi ametumia barua, kwa mfano ukurasa wa (24) Dina anamuandikia barua mpenzi wake Gusto kumpa pole ya kufiwa na baba yake, anasema:
“Gusto wangu,
Nina uchungu wa moyo na masikitiko makubwa juu ya kifo cha mzee wako mpenzi.
Habari hiyo ilinifikia kama pigo kubwa. …..Mara upatapo barua hii njoo haraka. Nina jambo muhimu la kukueleza.
Na …..ah!
Maneno yamenippotea!
Dina.
Pia kuna matumizi ya nyimbo katika riwaya ya
“Mirathi ya hatari”
Mwandishi anaonesha ukurasa wa (33),
“Mavengi aliyachoma yale mawe matatu niliyoyachukua. ….Alikuwa anaimba hivi,
“Gende, ve
dadna, gende;
Umwipao apugile uwuvina;
Avedze lukule; Gende, yane danda, gende…
Maana yake, “Damu tembea mpwao atambalie umwinya. Katika riwaya ya “Kufikirika” kumejitokeza tenzi mfano katika Ukurasa wa (18-19) kuna utenzi wenye beti 4 beti la tatu ni;
“Jina lake Milele. Lazima likumbukwe.
Kama watu wateule. Na yeye anakiliwe. Nchi ijae tele. Watu mfano wa yeye. Daima kwendambele. Mambo yatazaamiwe”.
Pia kuna utenzi mwingine Ukurasa wa 37, utenzi huu unabeti moja tu ambalo ni;
“Kweli kama lebasi. Uongo nao matusi.
Tena Kitu azizi halisi. Uongo pia najisi.
Mtu mwema haaugusi”.
Hizi ni tanzu ambazo zimechopekwa katika riwaya hizo na waandishi hao kama mbinu ya kibunilizi.
Ufumbaji, ni utumiaji wa kauli zenye maana ya uficho. Kauli hizo huwa na maana iliyo tofauti na umbo la nje. Ufumbaji huweza kuwa majina ya wahusika, aya au sura nzima na jina la kitabu chenyewe. Ufumbaji umejitokeza katika sehemu mbalimbali katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”,kwa mfano jina la riwaya yenyewe“mirathi ya hatari” ni la kiufumbaji, kwa kawaida binadamu anaposikia urithi au mtu anaporithi inategemewa kuwa anarithi vitu vya thamani kama vile nyumba, magari au pesa, lakini mwandishi wa riawaya ya “mirathi ya hatari” anaonesha urithi anaorithi Gusto ni uchawi ambaoanaurithishwa na baba yake. Kwa mfano ukurasa wa (12) anasema, “mwanangu, nakuachia kazi kubwa. Ni urithi mkubwa ukiutumia vema, bali pia ni mirathi ya hatari usipojihadhari nayo. Nakuachia dawa zote na milki yangu katika mizungu ya sihiri. …Hapo nilishituka.”
Pia katika katika riwaya ya,“kufikirika” jina lake ni la kimafumbo. Kwa mjibu wa mwadishi jina hili linatokana na jina la nchi ambayo nayo pia haipo katika ulimwengu halisi mwandishi amesema katika utangulizi kuwa,sehemu ya (vii) anasema,“Kufikirika ni nchi moja kubwa katika nchi za dunia. Kazikazini imepakana na nchi ya Anasa. Kusini nchi ya Majaribu, mashariki bahari ya Kufaulu na magharibi safu ya milima ya Jitihadi”.Pia ukurasa huohuo anasema,“Njia ya kwenda nchi hiyo hukanyagwa kwa fikira siyo nyayo”.Vilevile majina ya wahusika yasiyokuwa na umahususi mafano “mfalme, malkia, mtoto wa mfalme, waziri mkuu, makundi ya waganga, mwerevu, mjinga, wanachama, wanachuoni, wanashaeria, waongozi wa dini, mahatibu na mkulima”. Majina haya yametumika kwa lengo la kufanya kazi hii iwe na ufiche.
Taharuki, ni hali ya kuwa na dukuduku la kuendelea kusoma kazi ya fasihi. Taharuki hujengwa kwa kutumia mambo kadhaa kama vile matendo ya wahusika, kisengelenyuma na mabadiliko ya sura. Hii inajitokeza katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” ambapo mwandishi ameanza kuonesha mipango baada ya wanakijiji kuhama. Ukurasa wa (1) anasema, “ni juma la pili leo tangu nifike hapa kuwasaidia ndugu wanakijiji hawa katika operesheni sogeza; operesheni ya kuhamia katika vijiji vya maendeleo.” Pia kitendo cha Gusto kutoroka kutoka pangoni, ukurasa wa (34) anasema, “na mara ile Mavengi alianza kunisogelea nikaona wakati wangu umewadia. Nikakurupuka nikauandama mlango, mbio. ….yule mzee bawabu alinyanyuka kunizuia, lakini nilimpiga kumbo la bega akatetereka.”Katika riwaya ya “kufikirika” imejitokeza sehemu mbalimbali kama vileukurasa wa (38), “kwa sababu hii kila raia alihofu kuwa atakamatwa na kuchinjwa kama mnyama”, pia Ukurasa wa (39) mwandishi anasema “Mwerevu alipokuwa hawezi kuona hata njia ya nyembambaa ya kujiokoa, mjinga aliweza kuona barabara pana ya kujiokoa mwenyewe namwenziwe”. Pia taharuki imejitokeza ukurasa wa (8) wakati waganga walipo tengwa katika makundi katika kudadisi ni kundi gani litafanikiwa kuponya ugumba wa mfalme na utasa wa malkia. Haya matukio yote humfanya msomaji aendelee kusoma riwaya hii ili kujua kitakachotokea au kuendelea baadaye.
Dayalojia. Dayalojia ni mbinu ya majibizano katika kazi ya fasihi, katika riwaya ya “Mirathi ya hatari” mwandishi ametumia dayalojia pale ambapo mzee Mavengi anamchukua Gusto na kumpeleka kwenye mapango. Majibizano yao yanaoneshwa ukurasa wa (19);
“Baadaye mzee Mavengi alilichukua moja la yale mapembe matano akalionyesha
kwangu akisema;
“Unazionashangahizi?
Ndiyo Na manyoyahaya? Ndiyo
Basi hili baba yako alilitumia kama ndege Ulaya akiwamokazini
Lakini mbona ni dogo sana kulinganisha na kimo cha mtu?”
Hayo ni majibizano kati ya Gusto na mzee Mavengi wanapokuwa kule pangoni mahsusi kabisa kumpa Gusto elimu kuhusu uchawi.
Katika riwaya ya“kufikirika” ukurasa wa (4) katika mazungumzo kati ya Mfalme na Waziri, Ukurasa wa (5-7) mazungmzo ya mfalme na waganga, Ukurasa wa (23-26) mazungumzo ya mwalimu na mfalme, Ukurasa wa (27-28) mazungumzo kati ya Mwalimu na mgeni. Kwa mfano katika ukurasa wa (24) Mfalme anasema, “Pia nilikataa kuwa mwanangu asicheze ila asome wakati wote lakini hukutii”na mwalimu anajibu kuwa “umefanya vyema, Mfalme mtukufu, kwa kutangulia kunitoa kazini”. Hapo wanazungumza kwa kupeana nafasi ili mwingine azungumze huku mwingine akisikiliza kabla ya kuzungumza.
Ujadi, hii ni hali ya kutumia vipengele vya fasihi simulizi katika kazi ya fasihi andishi. Hapa mwandishi huweza kutumia mambo kama vile nahau, methali na ama misemo. Hii inajitokeza katika riwaya ya “mirathi ya hatari” ukurasa wa (39), anasema, “majuto daima ni mjukuu”, ukurasa wa (73) anasema pia, “dawa ya moto ni moto.” Siyo hivyo tu lakini pia ukurasa wa (27) anasema, “mtegemea Mungu si mtovu.Pia katika kitabu cha riwaya cha“kufikirika” kuna matumizi ya methali mfano Ukurasa wa(6) mwandishi anasema“mwenye haya hazai”. Piaukurasa wa(26)“milima haikutani binadamu hukutana”. Vilevile Ukurasa wa(5) anasema,“nyumba ya mgumba haina matanga”.Pia matumizi ya majina ya waganga Ukurasa wa(8) ambao ni “waganga wa mizizi, waganga wa makafara, waganga wa mizinguo, waganga wa hirizi na waganga wa mashetani”. Pia Ukurasa wa (4) neno “ramli” na Ukurasa wa (9) neno “makafara”.Pia “makombe, Gilani, Kinani, ktimari, makusuri, shamhariri na ruhani. Huo ni ujadi ambao waandishi hao wamepachika kwenye riwaya hizo.
Usawili wa wahusika, ni kujenga wahusika kwa kuwapa maneno na matendo yanayofanana na uhusika wao. Katika riwaya ya “Mirathi ya hatari”Gusto ni mhusika ambaye jina lake na anavyofanya vinasawili, kwa mfano ukursa wa (1) anashirikiana na wanakijiji kama ishara ya kuonesha kuwa elimu ya chuo kikuu imemsaidia kuwa na kushirikiana na jamii yake. Pia kitendo cha Gusto kutotaka kuwa mchawi ni usawili way eye kama mtu ambaye hataki ukale yaani uchawi. Katika riwaya ya“kufikirika”kuna usawiri wa wahusika, kwa mfano, mhusika “Mfalme” amepewa maneno yanayofanana na wadhifa wake kwa mfano katika sura ya kwanza ukurasa wa (1-3) mfalme anaelezea juu ya vitu vilivyopo katika nchi yake, maneno ambayo ni ya kawaida kwa watawala mfano Ukurasa wa (3) Mfalme anasema “nina majeshi ya askari walio shujaa, waongozi hodari na raia wema na watii”. Pia mhusika Utubusara ujinga hasara ametumiwa kutetea utu kwakuepushaumwagajidamunaalijitahidikuepukananaujinga mfano katika ukurasa wa (40) mjinga anasema “Hapana haja ya kumdharau mwanamke”. Hapa mtu mwerevu hawezi kumdharau mtu mwingine bali mjinga tu ndiye huweza kufanya hivyo.
Ufutuhi, hii ni mbinu ya ucheshi inayotumiwa na mwandishi kutokana na matendo na maneno ya wahusika. Katika riwaya ya “kufikirika”mbinu hii imejitokeza sehemu mbalimbali, kwa mfano; mwandishi ametumia ucheshi katika kutoa kauli za kejeli kama vile ukurasa wa (11) anasema, “mfalme na malkia walilemewa na uzito wa hirizi juu ya miili yao wakashukuru siku walipoamuriwa kuzivua…”, pia katika ukurasa huohuo mwandishi anasema “siku hiyo kuni, makaa na mafuta yote yalikwisha kwa kuchoma hirizi hizo”. Vilevile katika ukurasa wa (45) mwandishi anasema, “kama mkulima si mjinga na mchuuzi si mwerevu”, kauli hii imetumiwa kwa ajili ya kukejeli ambapo inaleta ucheshi. Vilevile majina ya wahusika mfano “Utubusara ujinga hasara” Ukurasa wa (47), ni jina la mhusika ambaye alipinga ujinga na umwagaji damu za watu na jina hilo linaleta hali ya ufutuhi kwa msomaji.
Kwa ujumla vipengele vya kibunilizi katika kazi ya fasihi huweza kusaidia kuonesha uumbaji wa tanzu hizo. Kuainisha maudhui, kuondoa uchovu wa kuendelea kusoma, kuweka msisitizo, kujikaribisha na uhalisia, Kushirikisha hadhira katika kutafakari kwa ukaribu, kujitanibu na ghasia za kufuatwafuatwa na mkono wa dola, kuonesha ufundi wa mtunzi katika kusawili maneno na hadhi ya wahusika. Vipengele vingine vinavyoweza kutumiwa na mwandishi katika kazi ya fasihi ni kama vile muundo, mtindo, ujumbe, vitushi, dhamira, wahusika na ushikamani
MAREJELEO
Mhando, P. & Balisidya, N (1976). Fasihi na Sanaa za Maonyesho, Dar es Salaam: Tanzania Publishig House.
Mlacha, S & Hurskainen, A., (1995). Lugha, Utamaduni na Fasihi Simulizi ya Kiswahili, TUKI na Chuo Kikuu cha Helsinki.
Mung’ong’o, C. G (1977). Mirathi ya hatari. Dar es Salaam: Tanzania Publishing House.
Robert, S (2013). Kufikirika. Dar es Salaam: Mkuki na Nyota Publishers Ltd.
|
|
|
JINSI YA KUJIBU MASWALI KATIKA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE – SWALI LA 15 |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 09:08 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
JINSI YA KUJIBU MASWALI YA KISWAHILI KATIKA MTIHANI WA TAIFA KIDATO CHA NNE – SWALI LA 15 LA LAZIMA
Utangulizi
Kwa mfumo wa utungaji wa mitihani ya kiswahili unaotumiwa kwa sasa, swali la 15 ni la lazima kujibiwa na mwanafunzi afanyaye mtihani wa kumaliza kidato cha nne. Mfumo huu ulianza kutumika mwaka 2008. Swali la 15 lina alama 15, alama hizi ni nyingi sana na zikikosekana zinaweza kuleta madhara makubwa katika matokeo ya mwanafunzi.
Isivyo bahati wanafunzi wengi huliacha swali hili la lazima na kupoteza alama zote 15. Wale wanaojikaza kisabuni kulijibu swali hili hukosa mbinu za jinsi ya kulijibu na hujikuta wakishindwa kulitendea haki na kuambulia alama za simanzi. Wachache hufaulu, pengine ni wale waliopata kusoma muongozo huu.
Muongozo huu unatoa maelezo ya kina juu ya jinsi ya kulijibu swali la 15, mbinu hizi zitawawezesha wanafunzi kufaulu vyema mitihani yao. Pia mada zinazojadiliwa humu, zitaongeza ubunifu wa wanafunzi na kuwafanya waongeze maarifa yao ambayo ndiyo msingi wa kila kitu.
Mambo yanayohusika katika swali la 15.
Swali hili huhusisha mambo matatu tu;
- Utungaji wa hadithi
- Utungaji wa tamthiliya
- Utungaji wa mashairi
Hivyo mwanafunzi atatakiwa awe na mbinu za utungaji wa mambo hayo kwani kila mwaka swali hubadilika, huenda mwaka huu ukaambiwa utunge tamthiliya na mwaka ujao ukatakiwa kutunga shairi.
Mbinu za utungaji wa mashairi
Katika utungaji wa mashairi, yakupasa kufahamu mambo manne muhimu.
- Namna ya kutunga utenzi
- Namna ya kutunga mashairi ya kimapokeo
- Namna ya kutunga ngonjera
- Namna ya kutunga majigambo
Namna ya kutunga utenzi
- Utenzi uwe na vina na mizani nane
- Utenzi uwe na sifa ya tarbia. Tarbia ni muundo wenye mistari minne katika shairi/utenzi
Sasa hebu tazama mfano huu uliojibiwa kutoka swali la necta 2008.
Swali
“Tenzi zina kanuni maalumu”. Tunga utenzi wenye beti tatu (3) unaohusu ugonjwa wa UKIMWI.
Jibu
UGONJWA WA UKIMWI
UKIMWI umevamia,
Jamii o inalia,
Wavuvi mabaharia,
Wote unawachukua.
Hii simanzi jamani,
Heri itupwe motoni,
Tutoke korokoroni,
Tupumue kwa amani.
Kujikinga ni rahisi,
Mwenzenu nimedadisi,
Fundisha yako nafsi,
Ngono haina nafasi.
Namna ya kutunga ngonjera
Ngonjera ni shairi lenye wahusika wawili wanaojibizana. Kwa mfano; ubeti wa kwanza, mwalimu, na wa pili, mwanafunzi.
Unapotunga ngonjera zingatia haya;
- Wahusika wanaojibizana
- Urari wa vina na mizani
- Mwisho wahusika wakubaliane kuhusu jambo moja
Swali la necta la mwaka 2009 limejibiwa vyema kama mfano;
Swali
Umeteuliwa kushiriki katika shindano la uandishi wa ngonjera la Afrika ya Mashariki. Tunga
ngonjera yenye beti nne (4) kuhusu maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2010.
Jibu
MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU 2010
Mzee
Uchaguzi umefika, viongozi kuchagua,
Hakuna kubabaika, kama moto wa mabua,
Rushwa hiyo kwangu taka, busara kuibagua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Kijana
Wala Sitapiga kura, kupoteza muda wangu,
Chagua wauza sura, wasioona uchungu,
Kiona vyao vipara, ni vyeusi kama vyungu,
Nasema kura sipigi, uchaguzi ukifika.
Mzee
Kijana elewa sasa, faida za kuchagua,
Tena si vyema kususa, taja angukia pua,
Na usitoe ruksa, serikali kuiua,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Wote
Kushiriki uchaguzi, ni bora si kulalama,
Hatuachi uchokozi, kwa uchaguzi salama,
Hakuna kumwaga chozi, kwako we baba na mama,
Mzee ama kijana, lazima kupiga kura.
Namna ya kutunga mashairi ya kimapokeo
Unapotunga mashairi ya kimapokeo zingatia yafuatayo;
- Urari wa vina na mizani
- Lugha ya mkato
Swali la necta mwaka 2010 linatumika kama mfano;
Swali
Tunga shairi la kimapokeo lenye beti nne (4) kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.
Jibu
UNYANYASAJI WA KIJINSIA
Kunazo jinsia mbili, ya kike na ya kiume,
Zote hizi ninakili, zastahili falme,
Changamoto ya akili, hii jinsia ya kiume,
Kunyanyasa mwanamke, wote tuseme yatosha.
Yu shambani analima, mume pombe ajinywea,
Yeye baba yeye mama, umri wazidi mwendea,
Kutwa yu kashika tama, kipigo kesha pokea,
Kunyanyasa mwanamke, wote tuseme yatosha.
Mumewe anapokufa, mali anadhurumiwa,
Hachukui hata sofa, mwanamke aonewa,
Mwisho apata kifafa, na kukonda kama muwa,
Kunyanyasa mwanamke, wote tuseme yatosha.
Kalamu nashusha chini, wanaume eleweni,
Dhambi mwajaza pomoni, mwanamke heshimuni,
Haki sawa zipambeni, zienee kooni,
Kunyanyasa mwanamke, wote tuseme yatosha.
Utungaji wa majigambo
Majigambo ni sanaa ya unenaji yenye utendaji na inayotumiwa na wasanii kujigamba ama kujinaki na kutangaza sifa zao.
Tofauti iliyopo kati ya mashairi na majigambo ni kuwa, majigambo yapo kwa ajili ya kujigamba tu kuhusu umahiri au ushujaa wa mtu wakati mashairi huweza kuzungumzia mambo mbalimbali yahusuyo jamii. Vilevile majigambo si lazima yawe na vina na mizani.
Mfano huu toka swali la necta 2012, unafafanua zaidi
Swali
Umeteuliwa kuwa mmoja kati ya waandaaji wa shindano la sanaa za maonesho litakalofanyika wakati wa kusherehekea siku ya walimu duniani mwaka 2013. Andika majigambo yenye beti nne ya mhusika ambaye ni mwalimu.
HAKUNA KAMA MIMI
Mimi ni mwalimu bora, dunia yote yajua,
Na nishikapo bakora, wanafunzi hutambaa,
Nafundisha lugha bora, kiswahili manufaa,
Jamani nasema hivi, hakuna alo ka mimi.
Mi ndo kubwa la vibaka, nilombaka popobawa,
Mchawi we utachoka, mi tabibu bila dawa,
Nguo iso na viraka, ninatinga kama kawa,
Mwalimu mwalimu kweli, ukinigusa tanata.
Nilimfundisha Mudi, leo hii ni profesa,
Pia mwingine Daudi, mpaka kawa na pesa,
Kazi yangu maridadi, naoa bila ya posa,
Jamani nasema hivi, hakuna alo kama mimi.
Kalamu naweka chini, tabasamu li usoni,
Nimenena ya moyoni, yalotoka akilini,
Katu sikai shimoni, mwalimu kazi kazini,
Mwalimu mwalimu kweli, ukinigusa tanata.
Utungaji wa hadithi fupi
Katika utungaji wa hadithi fupi, vipera vingi vya hadithi huhusika, vipera hivyo ni kama, soga, ngano, vigano, tarihi, visasili, visakale n.k. hivyo ni vyema kuvijua vipera hivyo. Hata hivyo katika utungaji wa hadithi kanuni zake ni zilezile hata kama unatunga katika kipera tofauti.
Mambo yafuatayo ni sharti yazingatiwe katika utungaji wa hadithi fupi
- Hadithi fupi inakuwa na mhusika mkuu mmoja ambaye anajitokeza sana kuliko wahusika wengine.
- Wahusika wachache.
- Mandhari finyu.
- Hadithi fupi inakuwa inaongelea dhamira kuu moja tu ambayo inaonekana toka mwanzo hadi mwisho wa hadithi.
Mfano huu unafafanua zaidi;
Swali
Tunga hadithi fupi kuhusu kisa chochote cha kusisimua.
PURUKUSHANI USIKU WA MANANE
Ilikuwa usiku wa siku ya Jumatano, Mowasha alijilaza katika kitanda chake cha teremka tukaze kwa furaha kuu. Ajabu ni kwamba hakukumbuka hata kuvua viatu, alilala navyo!
Kilichompa furaha Mowasha hakikuwa kitu kingine bali fedha aliyoipata baada ya kuuza pamba yake, pamba aliyohangaika kuilima leo ilimpa mamilioni, kweli mchumia juani hulia kivulini.
Akiwa amelala tena hajitambui kwa sababu ya usingizi, ghafla alistushwa kwa kupigwa kofi zito la mgongo, kofi hilo lilimpa simanzi na kumfanya alie kwa maumivu.
“Toa fedha uishi.” Jambazi mmoja alimwamulisha Mowasha, Mowasha akamtazama bwana huyu usoni akagundua ya kuwa jambazi huyu alikuwa mweusi kama kipande cha giza!
Jambazi yule aliendelea kumchapa makofi mazito ya uso Mowasha, kuna wakati jambazi alisikika akisema, “Toa fedha niko kazini!”
Mowasha baada ya kuona anaweza kufa, akainama chini ya mvungu wa kitanda chake akatoa kitita kikubwa cha fedha, jambazi bila kupewa fedha zile akazikwapua na kutokomea kusikojulikana.
Mowasha alihuzunika sana baada ya kuibwa fedha zake, alionekana mnyonge kama mtoto wa panya aliyekutana na paka mkubwa, lakini hakukata tamaa, aliendelea na shughuli za kilimo, safari hii hakulima pamba peke yake, alilima machungwa, nyanya na matikiti. Hivi sasa anamiliki nyumba mbili za ghorofa.
Kwa kuzingatia kanuni zilizotolewa hapo juu, hebu jipime kwa kufanya swali hili la necta mwaka 2011.
Eleza muundo wa soga. Tunga soga ya kusisimua kuhusu kisa cha kubuni.
Utungaji wa tamthiliya
Mambo ya kuzingatia katika utungaji wa tamthiliya
Katika utunzi wa tamthiliya kuna mambo kadhaa ya kuzingatia, mambo hayo ni kama yafuatayo:
- Chagua jambo unalotaka kuandikia
- Panga namna msuko wa visa na matukioa utakavyokuwa
- Buni wahusika wako kulingana na kile unachotaka kukiandika
- Chagua mandhari yanayofaa kulingana na visa vyako
- Tumia mtindo wa majibizano kati ya wahusika
- Gawa tamthiliya katika maonyesho
- Weka maelekezo ya jukwaa. Haya huelezea kile kinachotendeka kwa wakati ule. Maelezo ya jukwaa huwa katika maandishi ya italiki.
Tazama mfano wa tamthiliya hii ambayo imezingatia vigezo vyote vya utunzi wa tamthiliya.
Swali
Tunga tamthiliya fupi kuhusu kisa chochote kinachothibitisha kuwa mwanamke si mnyonge.
Jibu
VITUMBUA VITAMU
ONYESHO LA KWANZA
(Jukwaani wanatokea Kipisi na Mwantumu, Kipisi anatembea haraka na kumkamata mkono Mwantumu)
Kipisi: Habari yako sista…
Mwantumu: salama karibu biashara. (Anashusha chini sufuria lililojaa vitumbua, Kipisi anachukua vitumbua viwili na kuanza kutafuna)
Kipisi: Asante sista, nimetafuna viwili, vitumbua vitamu sana. Kwa heri!!
Mwantumu: Kwa heri hiyo vepee? Nilipe fyeza yangu, shilingi mia mbili.
Kipisi: sikulipi, fanya unachoweza.
Mwantumu: ahaa… kwa kuwa mi mwanamke ndo unanichukulia poa sio? Sasa leo nitakuonesha utamu wa mihogo pilipili.
(Mwantumu anamkunja shati Kipisi, kisha anampiga mweleka na kumfanya kipisi adondoke chini kama gogo.)
Kipisi: we mwanamke nuksi, chukua pesa yako usije niua bure.
Zingatia kuwa swali liulizwapo, huelezea urefu unaotakiwa katika hiyo tamthiliya yako.
Sasa hebu jipime kwa kufanya swali hili la necta mwaka 2014
Tunga tamthiliya fupi kuhusu umuhimu wa elimu kwa vijana wa Tanzania ya leo. Tamthiliya hiyo isipungue maneno mia tatu (300).
TAMATI
Marejeo
Mitihani ya necta taifa somo la Kiswahili mwaka 2008 – 2015
Marejeo mengine hayakuwekwa kwa sababu maalumu
|
|
|
SWALI: Faida ya misimu katika kuhifadhi historia ya jamii. |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 08:58 AM - Forum: Maswali na majibu
- No Replies
|
|
SWALI: Moja ya faida ya misimu ni kuhifadhi historia ya jamii. Toa mifano ya misimu zagao iliyovuma Tanzania katika vipindi vifuatavyo:
MAJIBU
(a) Muda mfupi baada ya kupata uhuru. - Kichele
- Mabeberu
- Uhuru na kazi
- Makabwela
- Walalahoi
(b) Miaka ya Azimio la Arusha.- Kabaila
- Bwanyenye
- Ukupe
- Mchumia tumbo
- Ujamaa
- Kujitegemea
© Njaa ya mwaka 1974/1975.- Unga wa yanga
- Kufunga mkanda
- kumbakumba
(d) Miaka ya vita vya Kagera.
(e) Kipindi cha hali ngumu ya maisha baada ya vita vya Kagera.
(f) Kipindi cha kuanzia 1985 hadi sasa- Ruksa
- Ngangari
- Ngunguri
- Wapambe
- Wafurukutwa
- Wakereketwa
|
|
|
SHAIRI: ADHA YANGU |
Posted by: MwlMaeda - 08-31-2021, 08:49 AM - Forum: Ushairi
- Replies (1)
|
|
ADHA YANGU
Naona kimya chazidi, na madhara hunifuma,
Simi mwana mkaidi, sana napenda kusoma,
Pamwe na zangu juhudi, naona bado nakwama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Ni wengi yetu idadi, mfano Darisalama,
Tuendavyo na kurudi, tatuonea huruma,
Uchovu unatubidi, ndefu safari tu wima,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Konda nao magaidi, daima kutusakama,
Wana zao itikadi, kutuzidisha dhahama,
Chunguzeni kuna budi, madhila yatuandama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Ninawatupia bodi, pia nanyi watu wema,
Serikali ikibidi, litatueni mapema,
Siku hizi imezidi, wanafunzi si salama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Elimu kwetu ni sudi, nalijua jambo jema,
Na wala sileti kedi, kitu hiki kinauma,
Au ndio makusudi, tuende mbele kukwama?
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Heri kwao auladi, wasichana uwi mama,
Vipando bure kukodi, wakafanyiwa unyama,
Maana nimeadidi, shairi mkalisoma,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Beti kadha nina budi, hapa kutunga nakoma,
Ila siku nitarudi, kushukuru watu wema,
Hapo nitasema hodi, kwa sauti ya heshima,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.
Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704
|
|
|
|