MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

SHAIRI: ADHA YANGU - Printable Version
JIFUNZE KISWAHILI
SHAIRI: ADHA YANGU - Printable Version

+- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz)
+-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1)
+--- Forum: Fasihi simulizi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=6)
+---- Forum: Ushairi (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=50)
+---- Thread: SHAIRI: ADHA YANGU (/showthread.php?tid=1080)

SHAIRI: ADHA YANGU - MwlMaeda - 08-31-2021

ADHA YANGU
Naona kimya chazidi, na madhara hunifuma,
Simi mwana mkaidi, sana napenda kusoma,
Pamwe na zangu juhudi, naona bado nakwama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Ni wengi yetu idadi, mfano Darisalama,
Tuendavyo na kurudi, tatuonea huruma,
Uchovu unatubidi, ndefu safari tu wima,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Konda nao magaidi, daima kutusakama,
Wana zao itikadi, kutuzidisha dhahama,
Chunguzeni kuna budi, madhila yatuandama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Ninawatupia bodi, pia nanyi watu wema,
Serikali ikibidi, litatueni mapema,
Siku hizi imezidi, wanafunzi si salama,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Elimu kwetu ni sudi, nalijua jambo jema,
Na wala sileti kedi, kitu hiki kinauma,
Au ndio makusudi, tuende mbele kukwama?
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Heri kwao auladi, wasichana uwi mama,
Vipando bure kukodi, wakafanyiwa unyama,
Maana nimeadidi, shairi mkalisoma,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Beti kadha nina budi, hapa kutunga nakoma,
Ila siku nitarudi, kushukuru watu wema,
Hapo nitasema hodi, kwa sauti ya heshima,
Usafiri kwangu Mimi, adha yangu mwanafunzi.

Mtunzi Filieda Sanga
Mama B
Mabibo Dsm
0753738704

RE: SHAIRI: ADHA YANGU - John John - 08-31-2021

Hongera sana mtunzi kwa kubaini adha hii inayowakumba wanafunzi wengi.