MyBB Internal: One or more warnings occurred. Please contact your administrator for assistance.

JIFUNZE KISWAHILI

Welcome, Guest
You have to register before you can post on our site.

Username
  
Password
  
Search Forums

(Advanced Search)

Forum Statistics
» Members: 5,481
» Latest member: Kundlimatching
» Forum threads: 2,178
» Forum posts: 2,256

Full Statistics

Online Users
There are currently 119 online users.
» 0 Member(s) | 118 Guest(s)
Bing

Latest Threads
Buy Vilitra 60 Mg |【Get E...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-24-2023, 11:45 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce50?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-19-2023, 12:59 PM
» Replies: 0
» Views: 0
About the Vidalista 60 Mg...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-04-2023, 04:07 PM
» Replies: 0
» Views: 0
What Is Vidalista 60?
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
04-03-2023, 10:49 AM
» Replies: 0
» Views: 0
How to take Cenforce 100 ...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Kieth_winsett
03-29-2023, 02:37 PM
» Replies: 0
» Views: 66
How is Vidalista 10 Mg us...
Forum: Watunzi wa Kiswahili
Last Post: Kieth_winsett
03-27-2023, 01:26 PM
» Replies: 0
» Views: 117
Obtain Thesis Paper Assis...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Minny02
03-24-2023, 03:01 PM
» Replies: 0
» Views: 200
SEO services for sports f...
Forum: Historia ya makabila ya kibantu
Last Post: Maria Poland
03-17-2023, 01:51 PM
» Replies: 1
» Views: 223
NUKUU ZA KISWAHILI DARASA...
Forum: Nukuu
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:31 PM
» Replies: 0
» Views: 788
NECTA K4 2022
Forum: Mitihani
Last Post: MwlMaeda
01-15-2023, 05:25 PM
» Replies: 0
» Views: 403

  JUHUDI ZA VYOMBO VYA HABARI KATIKA KUKUZA NA KUENEZA KISWAHILI NCHINI KENYA
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:54 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Mosol Kandagor
Ikisiri
Vyombo vya habari ni asasi muhimu sana katika kukuza na kueneza lugha yoyote ile, hasa katika enzi hii ya utandawazi. Vyombo hivyo ni kama vile idhaa za redio, televisheni na magazeti. Katika nchi ya Kenya kuna vyombo vya habari vinavyotoa huduma anuwai kwa ajili ya kutosheleza mahitaji ya wateja wao. Katika karne hii ya 21, vyombo vya habari vimelazimika kuhakikisha kuwa wateja wao wananufaika kutokana na huduma mbalimbali ambazo hutolewa kila kukicha. Huduma hizo hujumuisha kuwajuza, kuwafundisha, kuwaburudiisha na hata kuelimisha jamii kwa namna moja au nyingine. Makala haya yanatathmini juhudi za vyombo vya habari katika kukuza na kueneza Kiswahili nchini Kenya kwa kujikita katika gazeti la Taifa Leo, Idhaa za redio (Citizen na KBC), pamoja na kituo cha runinga cha KBC.   BOFYA HAPA CHINI KUIFUNGUA KATIKA PDF>>>>>>> 
.pdf   JUHUDI-ZA-VYOMBO-VYA-HABARI-KATIKA-KUKUZA-NA-KUENEZA-KISWAHILI-NCHINI-KENYA.pdf (Size: 7.29 MB / Downloads: 0)

Print this item

  UKUTA
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:46 AM - Forum: Taasisi za kukuza lugha - No Replies

Hiki ni chama cha Usanifu wa Kiswahili na Mashairi . chama hiki kilianzishwa mwaka 1965 na mshairi Mathias Mnyapala kwa lengo la kukuza ushairi wa Kiswahili kwa ujumla.
  Ukuta ilikuwa na malengo yafuatayo:
     a). Kukuza lugha ya Kiswahili na ushairi kwa ujumla kwa njia ya kujishughulisha na kazi tafauti zinazohusiana na maendeleo ya Kiswahili na ushairi kama vile uhariri wa miswada ya Kiswahili, utunzi wa mashairi na uandishi wa vitabu na kutafsiri maandishi mbali mbali katika Kiswahili.
     b).  Kukuza utunzi wa ngonjera na kuhamasisha utunzi wa vitabu katika misingi yenye kuzingatia utamaduni wa Mtanzania.
Mafanikio ya UKUTA.
     c).   Imeweza kuundaa na kuendesha semina na makongamano ya Kiswahili na kutunga kazi za fasihi kwa kushirikiana na vyombo vingine.
     d).   UKUTA imeweza kuandika vitabu mbali mbali vya ushairi hususan vya ushairi, kama vile Ngonjera za  ukuta ( cha kwanza na cha pili – 1968 ), Mashairi ya Azimio la Arusha – 1974 na Mashairi ya miaka kumi ya Azimio la Arusha – 1977.
     e).   Imeweza kutafsiri kwa Kiswahili maandishi mbali mbali . mfano , iliwza kutafisiri majina ya baadhi ya mitaa ya jiji la Dar – es – Salaam kama vile mtaa wa uhuru badala Independence Avenue na mtaa wa Sokoine badala ya Sokoine Drive.
  1. TUKI ( Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ).
     Taasisi hii kihistoria ilianzishwa mwaka 1930 ikiwa kamati ya lugha ya lugha ya Afrika Mashariki na uatwala wa Waingereza , na mnamo mwaka mwaka 1964, ilipandishwa hadhi na kuhamishiwa katika chuo kikuu cha Dar –es – Salaam baada ya kuimarishwa kwa sheria ya Bunge ya mwaka 1964. Na mwaka 1970 kilipoanzishwa chuo kikuu cha Dar –es Salaam taasisi ilikuwa moja wapo wa asasi za utafiti wa chuo, ambapo mpaka leo asasi hii imekuwa ikifanya kazi chini ya Chuo Kikuu,
    Mnamo mwaka 2009, taasisi hii ilibadili jina baada ya kuungana na Idara ya Kiswahili ya chuo na kujulikana kwa jina la Taasisi ya Taaluma za Kiswahili. ( TATAKI ).
    Malengo ya TUKI ( TATAKI ).
       i).  Kuichunguza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika fani zake zote ikizingatia mipango ya muda mrefu katika Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Afrika na mashariki na Katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.

Print this item

  TAKILUKI : TAASISI YA KISWHILI NA LUGHA ZA KIGENI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:23 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Taasisi hii iliundwa mwaka 1979 ikiwa chini ya Wizara ya Elimu  na Mafuzo ya Amali Zanzibar.
 Lengo kubwa ya kuanzishwa taasisi hii ni :Kusimamia na kuendeaha shughuli za ukuzaji wa kiswahli na lugha za kigeni kisiwani humo.
KAZI ZA TAKILUKI:
  1. Kutoa mafunzo na elimu ya Kiswahili kwa kiwango cha juu kwa watumishi wa serikali na viongozi wa chama ua vyama ili kukuza ujuzi wa Kiswahili  na kuzumgumza Kiswahili fasaha
  2. Kufanya utafiti wa Kiswahili , kuandika vitabu vya taaluma mbali mbali za Kiswahili na kutafsiri katika kisahili maandishi mbali mbali yaliyo katika lugha za kigeni.
  3. Kuhimiza matumizi ya Kiswahili fasaha , kuchapisha vitabu vya Kiswahili  na kuwapa waandishi chipukizi miongozo ya uandishi sahihi wa vitabu.
  4. Kuratibu na kusimamia maendeleo ya Kiswahili visiwani Zanzibar pamoja na kuendesha mafunzo ya lugha ya Kiswahili kwa wazawa na wageni
  5. Kuandaa isitalahi za taaluma mbali mbali pamoja na kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwamashirika ,idara wizara kampuni,na watu binafsi , pia hufundisha lugha za kigeni kama vele GR, PR FR ARB CHINA na kuandika vitabu vya Kiswahili.
  6. Hujishughulisha na ufuatiliaji pamoja na usimamizi wa matumizi sahihi ya Kiswahili katika vyombo vya habari katika shughuli mbali mbali za serkali na za kawaida.
  7. Kufanya utafiti wa lahaja na fasihi simulizi ya Kiswahili.
MAFANIKIO YA TAKILUKI.
Takiluki imepata mafanikio kadhaa yakiwemo haya yafutayo:
  1. Kuchapisha vitabu mbali mbali vya Kiswahili kama vile malenga wapya, na tungo zakale.
  2. Kuandaa na kuendesha semina na makongamano mbali mbali ya Kiswahili.
  3. Kuhimiza ufundishaji wa Kiswahili visiwani Zanzibar.kushirikiana na vyombo mbali mbali vyaukuzaji lugha ya Kiswahili katika kutekeleza mipango mbali mbali ya ukuzaji Kiswahili.

Print this item

  TAASISI YA ELIMU YA WATU WAZIMA
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:17 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Taasisi hii ilianzishwa mwaka 1963. Kama chombo cha kuwasaidia wazelendo  katika stadi za kusoma na kuandika ambao hawakupata fursa ya kupata elimu katika ngazi ya msingi na sekondari.
   Baadhi ya mafanikio ya elimu ya watu wazima ni:
  • Kufanikiwa kutoa elimu ya watu wazima katika stadi za kusoma na kuandika wakati wa jioni kwa lengo la kufuta ujinga .
  • Kutoa masomo kwa njia ya posta kwa kidato cha kwanza hadi cha sita katika somo la Kiswahili.
  • Kuanzisha maktaba makao makuu ambayo huwasidia wanafunzi kupata vitabu na majarida mbali mbali ya Kiswahili.
  • Kunzisha idara ya mafunzo ya elimu ya watu wazima ambapo wanafunzi kutoka ndani na n je ya nchi husomea diploma ya elimu ya watu wazima.

Print this item

  UWAVITA ( Umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania )
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:11 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

.pdf   UWAVITA ( Umoja wa waandishi wa vitabu Tanzania ).pdf (Size: 131.47 KB / Downloads: 0)

Print this item

  TATHMINI YA MAENDELEO YA KISWAHILI BAADA YA UHURU
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 08:01 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Lugha ya Kiswahili baada ya uhuru imepata mafanikio kadhaa. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:
  1. Uendelezwaji wa Kiswahili.
    Kiswahili kimeweza kuendelezwa kwa njia mbali mbali kama vile kufundisha kama somo moja wapo katika ngazi zote za elimu nchini, kufanyiwa utafiti, kusanifiwa na kutumika kama lugha kuu ya mawasiliano.
2. Kuongezeka kasi ya ueneaji wa lugha ya Kiswahili.
         Kiswahii kimeweza kuenea hadi nje ya Tanzania katika mataifa mbali mbali na hata kufikia moja wapo lugha ya kimataifa na pia kuongezeka msamiati.
3. Kuongezeka kwa uundwaji wa vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
    Kuendelea kujitokeza vyombo mbali mbali vya ukuzaji wa Kiswahili ndani na nje ya Tanzania  ni mafanikio makubwa kwa upande wa lugha ya Kiswahili kwa sababu vyombo hivyo vimewea kuikuza lugha ya Kiswahili kwa njia mbali mbali.
4. Kutumika Kiswahili katika vyombo vya habari vya nje.
    Kuendelea kutumika lugha ya Kiswahili katika vyombo mbali mbali vya habari vya nje kama viel BBC. Deutchwelle,radio japani, sauti ya amerika na nyinginezo kumeifanya lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha mashuhuri duniani

Print this item

  CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 07:55 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

 Pamoja na mafanikio hayo ,zimekuwapo changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto hizo ni:
  • Upotoshwaji wa lugha ya Kiswahili.
       Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa mfano ni wa uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio yanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
  • Athari za lugha za kigeni.
Tatizo la kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan kingereza.
  • Kutokuwepo uwiano wa kimatumizi.
Hii ni changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha mama.
  • Utafauti wa sera .malengo na mipango ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili.
  Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo,sera, na mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.
  • Uhaba wa wataalamu.
  Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya  na kutekeleza malengo kwa ufanisi.
  • Kutokwepo mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia.
   Ni tatizo jengine linalokwanishwa maendeleo ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa mwanya hasa kwa lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya Kiswahili katika jamii.

Print this item

  MCHANGO WA WIZARA YA ELIMU KATIKA MAENDELEO YA LUGHA (KENYA)
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 07:48 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Kwa Muhtasari
WIZARA ya elimu nchini Kenya ni mojawapo ya asasi mbalimbali zenye nafasi muhimu katika ukuzaji wa lugha ya Kiswahili.
Miongoni mwa majukumu yake ni pamoja na kuhakikisha kwamba kuna sera madhubuti katika viwango vyote vya elimu nchini. 
Pia ina wajibu wa kuhakikisha kuwa viwango vya utoshelevu vya walimu wa Kiswahili vimezingatiwa ili kuboresha ufaafu wa walimu. Ni majukumu haya pamoja na mengine, yanayoifanya Wizara ya elimu kuwa na nafasi muhimu katika kuendeleza na kukikuza Kiswahili nchini. 
Katika kufanya hivyo, bila shaka kuna changamoto ambazo ni lazima zishughulikiwe ikiwa asasi hii muhimu inaazimia kutimiza wajibu wake.
Miongoni mwa changamoto hizo ni sera za elimu, mielekeo ya wadau katika sekta ya elimu wakiwemo walimu, wanafunzi na wazazi pamoja na ukosefu wa fedha za kugharimia mipango yote ya wizara ya elimu. Wizara yenye jukumu la kukuza, kuimarisha na kuendeleza Kiswahili ni ile ya elimu. 
Wizara hii hutoa mipango ya kisera ambayo hutafsiriwa kwenye sera ya lugha, mihutasari ya masomo na kwenye asasi zinazokuza Kiswahili. Kwa kuwa shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu viko chini ya Wizara hii, basi haiwezi kukwepa matatizo yanayoikumba sekta ya elimu humu nchini. 
Hata hivyo, makala haya yamezingatia hasa majukumu ya wizara ya elimu kwani ndiyo inayohusika kwa kiwango kikubwa na masuala ya kisera yanayoathiri taaluma ya Kiswahili. Hivyo basi, ni jukumu la Wizara ya elimu kupanga mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu kuyakabili matatizo hayo. 
Kwanza kabisa, Wizara ya elimu nchini Kenya ina jukumu la kuhakikisha kwamba walimu wanaofundisha somo la Kiswahili ni wale waliofuzu na kutosheleza masharti ya kitaaluma.
Isistoshe, ina jukumu la kuhakikisha kuwa walimu wa kutosha wanapatikana ili kuboresha ufundishaji wa Kiswahili shuleni na hata vyuoni.
Kimsingi, Wizara ya elimu inatakiwa kupanga mikakati ya muda mfupi na ya muda mrefu ya jinsi ya kupata walimu wa kutosha si tu walimu wa Kiswahili bali pia na walimu wa masomo mengine.
Jambo hili linapozingatiwa kwa njia inayofaa, taaluma ya Kiswahili itaendelezwa ipasavyo. 
Fauka ya hayo, Wizara ina jukumu la kuimarisha mieleko ya wanafunzi na wadau wote katika sekta ya elimu. Ukuzaji wa Kiswahili utawezekana ikiwa mielekeo ya wanafunzi katika kuitumia lugha hiyo itakuwa chanya.
Kuhusu mwelekeo wa kutaka au kutotaka kuzungumza lugha ya kigeni, Schooling (1990:71) anaeleza kwamba: Mtazamo chanya kuhusu lugha ya kigeni humchochea mtu kutaka kujifunza na kutumia lugha hiyo pindi nafasi ya kutumika inapopatikana (Msanjila 2005:215). 
Mtazamo
Kwa upande mwingine, mtazamo hasi kuhusu lugha ya kigeni humfanya mtu achukie kila jitihada zinazofanywa za kutaka kuongeza matumizi ya lugha hiyo.
Kinachojitokeza hapa ni ukweli kwamba katika mazingira ya Kenya, Wizara ya elimu, shule na vyuo kwa pamoja vinatakiwa kujenga mazingira chanya kwa wanafunzi ili wao wenyewe wahimizike kutaka kujifunza lugha nyingine kwa bidii kuliko kulazimishwa kutumia lugha ngeni kama Kiingereza bila wao kupenda. 
Isitoshe walimu na Wizara ya elimu wanaweza kushirikiana katika jitihada za kuimarisha mwelekeo chanya kwa wanafunzi katika matumizi yao ya Kiswahili.
Jambo hili lawezekana kupitia midahalo shuleni na hata nje ya mazingira ya shule. Ili kuipa mashiko midahalo hii, walimu wanaweza kuwashindanisha wanafunzi kividato yaani Kidato cha I na II, kidato cha II na III na kadhalika. Hatimaye washindi wa kila kikundi wapewe zawadi.
Kwa kufanya hivyo, Wizara ya elimu pamoja na walimu wa shule za msingi na sekondari watakuwa wanachangia kuendeleza mwelekeo chanya katika matumizi yao ya Kiswahili. 
Jukumu jingine la Wizara ya elimu ni kuhakikisha kuwa sera zinazoundwa na kutekelezwa zinachangia kuimarisha Kiswahili. Japo wizara ya elimu imetambua umuhimu wa Kiswahii, bado inaendeleza sera zinazoikandamiza lugha hii.

Print this item

  MAENDELEO YA KISWAHILI URUSI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 07:33 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Warusi walianza kuifahamu lugha ya Kiswahili mwanzoni mwa karne ya 19, lakini uchunguzi kamili wa lugha ya Kiswahili na lugha zingine za Kiafrika ulianza nchini Urusi baada ya mapinduzi ya Oktoba 1917. Kiswahili ni lugha ya kwanza ya Kiafrika iliyokuwa ikifundishwa nchini humo.
Uteuzi wa lugha ya Kiswahili kuwa lugha ya mafunzo ulitegemea maana na umuhimu wa lugha hii. Kiswahili kilienea sana katika nchi za Afrika Mashariki na kutumiwa na makabila mengi tangu zamani. Idadi ya wazungumzaji wa Kiswahili ilikuwa kubwa zaidi kuliko lugha nyingine za Kiafrika. Uchunguzi wa kinadharia wa Kiswahili ulianza kuendelezwa nchini Urusi katika miaka ya 1930. Mnamo mwaka 1933, Warusi walianza kujifunza Kiswahili. Mmoja wa waalimu wao alikuwa Jomo Kenyatta, Raisi wa kwanza wa Kenya ambaye wakati huo alikuwa anasomea siasa huko Moscow.
Mwaka 1934, kulianzishwa idara ya lugha za Kiafrika katika chuo Kikuu cha Leningrand na kukubaliwa kwa kundi la kwanza la vijana wanafunzi waliojifunza lugha hizi, hasa Kiswahili. Vilevile lilifanyika kongamano la kwanza la elimu nchini Urusi, yaani kongamano la wanataaluma Warusi waliojishughulisha na utafiti wa lugha za Kiafrika. Kongamano hilo liliwashirikisha wanaisimu wa Leningrand na wa Moscw.
Ni katika kongamano hili, wanataaluma waliidhinisha mpango wa kazi za uchunguzi wa lugha za Kiafrika. Miongoni mwa kazi hizo, zilikuwemo Kamusi za istilahi za kiuchumi na za kijamii za lugha zifuatazo: Kihausa (Yushmanov), Kizulu na Kihosa (Snegiryov), Kisotho (Olderoge) na Kiswahili (Danilov). Zaidi ya hayo, wataalamu hawa walipanga kutunga sarufi ya lugha ya Kiswahili na ya Kizulu.
Siku hizi, lugha ya Kiswahili inafundishwa na kuchunguzwa kwenye baadhi ya vyuo vikuu na taasisi za nchi ya Urusi: Taasisi ya nchi ya Asia na Afrika iliyoko chini ya Chuo Kikuu cha Moscow kwa jina la Lomonoscov (tangu mwaka 1960), Kitivo cha Mashariki cha Chuo Kikuu cha Petersburg (tangu mwaka 1934), Taasisi ya uhusiano wa kimataifa (tangu mwaka 1957) na Chuo Kikuu cha Urafiki baina ya mataifa kwa jina la Patrice Lumumba (tangu mwaka 1961). Academia ya kisayansi ya Urusi inajishughulisha vilevile na utafiti wa Kiswahili. Katika taasisi ya isimu kuna idara ya lugha za Kiafrika.
Zaidi ya miaka 70, uchunguzi wa lugha ya Kiswahili pamoja na lugha nyingine za Kibantu uliendelezwa kwa nguvu zaidi. Vilitungwa vitabu vya sarufi ya Kiswahili kikilinganishwa na lugha nyingine za Kibantu. Kwa mfano Lugha ya Kiswahili (E. Miachina), Sarufi ya Kinadharia ya Kiswahili (N. gromov na N. Okhotina), Aina za Maneno katika Lugha za Kibantu na Misingi ya Kuzifafanua (N. Gromov). Kulitolewa makala nyingi zinazohusu mfumo wa kisarufi wa Kiswahili, mnyambuliko wake, utaratibu wa kifonetiki, n.k. Hivyo, wanataaluma wa Kirusi wanachunguza lugha ya Kiswahili katika vipengele vyake pamoja na nyanja zake zote (Fasihi na sarufi).
Walimu wa lugha ya Kiswahili nchini Urusi wametunga vitabu vya masomo kwa ajili ya kufundishia wanafunzi vitabu vya kiada, vya ziada, matini, n.k. vinavyowezesha kufanya ufundishaji uwe bora zaidi. Vilevile kamusi za aina mbili: Kamusi ya Kiswahili-Kirusi na Kirusi – Kiswahili zimechapishwa. Kamusi ya kwanza ya Kirusi – Kiswahili ilitolewa mwaka 1961. Mwaka 1987, ilichapishwa kamusi mpya na mwaka 1996, ilitolewa kamusi kubwa ya kwanza ya Kirusi – Kiswahili yenye zaidi ya maneno 30,000. Nyongeza ya kamusi hiyo ni “Sarufi linganishi ya lugha ya Kirusi na lugha ya Kiswahili”
Aidha, vitabu vya tafsiri vimesaidia sana kukuza na kueneza Kiswahili nchini Urusi. Maandishi ya Kirusi yalianza kutafsiriwa kwenda lugha nyingine miaka ya sabini. Baadhi ya vitabu vya Kirusi vilivyotafsiriwa kwa Kiswahili ni Mama (1980), Tabia ya Mrusi (1964), Ajali ya Mwanaume (1962), Watabakia Vijana Milele (1963) na nyinginezo. Wafasiri wa vitabu hivyo walikuwa Waswahili waliokuwa wakiishi Moscow, wakisomea taaluma fulani, au kufanya kazi redioni. Baadaye, Warusi waliojifunza Kiswahili na kukimudu kikamilifu walishiriki katika kazi hiyo ya kutafsiri.
Fasihi ya Kiswahili ilitafsiriwa pia katika Kirusi. Vitabu vilivyotafsiriwa sana ni vya Shaaban Robert. Vitabu vyake vilivyotafsiriwa katika Kirusi ni: Kusadikika, Adili na Nduguze, Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini, Wasifu wa Siti Binti Saad, Siku ya Watenzi Wote, Utubora Mkulima, mashairi yake mengineyo. Waliotafsiri walikuwa ni Warusi waliojifunza Kiswahili. Maandishi hayo yalitolewa katika vitabu viwili: kimoja kilichoitwa Maisha Yangu kilitolewa mwaka 1969, kwa idadi ya nakala 50,000 na kingine ni Maandishi Yaliyoteuliwa kilitolewa mwaka 1981, kwa idadi ya nakala 30,000. Hivyo wasomi Warusi walipata nafasi nzuri ya kujua kazi hizo za Fasihi ya mwandishi maarufu wa Kiswahili inayoakisi upeo wa juu wa usanifu na utajiri wa lugha ya Kiswahili.
Baada ya Urusi kusambaratika, shughuli zote za fatsiri zimesimamishwa pamoja na kufungwa kwa asasi zote zilizoshughulikia lugha na Fasihi ya Kiswahili. Kutokana na hali hii, shughuli za ukuzaji wa Kiswahili nchini humo zinaenda kwa kusuasua. Wataalamu wa Kirusi wanaojishughulisha na Kiswahili wanakosa uhusiano na asasi za lugha ya Kiswahili zilizoko Afrika ya Mashariki hali hii hukwamisha maendeleo ya Kiswahili nchini humo.

Print this item

  NAFASI YA CHAWAKAMA KATIKA KUUNGANISHA VIJANA WA AFRIKA MASHARIKI
Posted by: MwlMaeda - 09-06-2021, 07:24 AM - Forum: Maendeleo ya Kiswahili - No Replies

Utangulizi

Lugha ya Kiswahili ina historia ndefu hapa Afrika Mashariki kama chombo cha kuunganisha watu wenye tamaduni tofautitofauti tokea enzi za biashara ya utumwa hadi baada ya uhuru. Wafanya biashara wa enzi za utumwa walitumia lugha ya Kiswahili ili kurahisha mawasiliano na kukidhi haja zao za kibiashara, bila kujua, walijikuata wanakieneza Kiswahili kutoka pwani ya Tanganyika hadi bara ya Kongo. Wakoloni nao walipokuja Afrika Mashariki waliona Kiswahili ndio lugha pekee ya kurahisha utawala wao, lakini baadae walikuja kugundua kuwa Kiswahili ilikuwa ni silaha ya kuangamiza utawala wao na hivyo wakahafifisha matumizi ya Kiswahili.
Wanaharakati wa utaifa, wakati wa kupigania uhuru hususani katika nchi ya Tanganyika waliona Kiswahili ndio njia pekee itakayowasidia kupata uhuru bila hata kumwaga tone la damu. Mwalimu Nyerere alitumia fursa hii kuwaunganisha watanganyika wote wenye tamaduni tofautitofauti na waliokuwa wakizungumza lugha tofautitofauti, lakini kwa kupitia lugha ya Kiswahili walikuwa na kauli moja ya kutaka Tanganyika ya watanganyika huru. Umoja huu umedumu hadi leo Tanzania inajulikana kuwa ni nchi ya watu wakarimu na wenye umoja. Isingewezekeana kufukia hapa kama kila mtu angejitukuza kwa kabila lake ila kwa kutumia Kiswahili watanzania sasa ni wamoja, hakuna msamiati katika mazungumzo ya watanzania unaotukuza ukabila.
                                                    [Image: IMG_0226.JPG]
WANACHAWAKAMA KATIKA UFUNGUZI WA KONGAMANO

Chawakama ni NiniKatika makala hii tutaangalia nafasi ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki (CHAWAKAMA) katika kuunganisha vijana wa Afrika Mashariki, tutaangalia kwa kina changamoto zinazokikabili chama hiki na mwisho ni wito kwa serikali za jumuia ya Afrika Mashariki katika kukiwezesha chama hiki ili kiweze kufikia malengo yake.
CHAWAKAMA husimama badala ya Chama cha Wanafunzi wa Kiswahili vyuo vikuu Afrika Mashariki. Chama hiki kilianzishwa mwaka 2004 kwa lengo la kukuza na kueneza Kiswahili katika eneo lote la Afrika Mashariki kupitia wanafunzi wanaosoma Kiswahili vyuoni. Wanachama wa chama hiki ni wale wanosoma Kiswahili na hata wale wenye mapenzi ya lugha ya Kiswahili pia wanaweza kujiunga na chama hiki.
Kama nilivyokwisha sema hapo awali, chama hiki kina nafasi kubwa sana katika kuwaunganisha vijana wa Afrika Mashariki. Lengo kuu la chama hiki ni kueneza Kiswahili lakini sasa wanakienezaje? Wanachama wa chama hiki ambao ni nchi wanachama wa jumuia ya Afrika mashariki wanakawaida ya kuandaa makongamano kwa ngazi ya kitaifa na ngazi ya kimataifa. Kwa ngazi ya kitaifa kila nchi huandaa kongamano kila mwaka ambalo linawakutanisha wanachama wote kutoka vyuo mbalimbali katika nchi husika. Katika kongamano hilo mada mbalimbali zinazohusu lugha ya Kiswahili na mustakabali wake hujadiliwa lakini pia maazimio mbalimbali huchukuliwa juu ya maendeleo ya chama. Sasa katika mijadala kama hii inatoa nafasi ya Kiswahili kukua kwani makala mbalimbali huandikwa ambazo pia husomwa na watu mbalimbali. Makala hizi pia zimekuwa zikichapishwa katika majarida ya chuo husika na pia zimekua zikichapishwa mtandaoni ambapo hutoa fursa kubwa kwa watu wengi zaidi kuzifikia na kusoma, hivyo kwa njia hiyo Kiswahili kinakua kimeenea.
                                                                      [Image: IMG_0267.JPG]
MWANACHAWAKAMA AKIWASILISHA MAKALA

Sasa kwa nini nasema chama hiki kinaweza kuwaunganisha vijana wa Afrika Mashariki. Kwanza kabisa kinachowaunganisha vijana hawa ni lugha ya Kiswahili, kupitia lugha ya Kiswahili kila mtu anakuwa na hisia za kuona kwamba anatoka katika familia moja, anahisi kwamba waafrika mashariki ni wamoja hii ni kwa sababu wanazungumza lugha moja. Na kwahiyo wakiisha jisikia hivyo ile hali ya umoja na mwingiliano inakuwa ni kubwa sana kitu ambacho kinaimarisha mahusiano baina ya vijana hawa wa Arfika mashariki.Kwa upande wa makongamano ya kimataifa, chama kimekuwa kikiandaa kongamano moja kila mwaka na kongamano hili linakua likizunguka katika nchi zote wanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki. Sasa hapa ndipo panapatikana fursa ya kuwaunganisha vijana wengi wa Afrika Mashariki kutoka Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi na Uganda. Vijana hawa wanapokutana kinachowaunganisha ni lugha ya Kiswahili. Mawasiliano yote yanakuwa yakifanyika kwa lugha ya Kiswahili na kila mmoja anahamasika kutumia lugha ya Kiswahili kadri awezavyo na kila mtu huona fahari kuzungumza lugha ya Kiswahili.
Kitu kingine wanapokuwa wamekutana wote wanakuwa na malengo sawa – malengo ya kukienzi na kukieneza Kiswahili Afrika Mashariki nzima. Hili pia ni jambo ambalo huweka umoja baina ya vijana hawa, kwani ili kufikia lengo hili ni lazima wote wafanye kazi kwa pamoja na kwa umoja. Kwa kweli wamekua wakishirikiana kwa ukaribu sana na hata panapokuwa na uaandaaji wa makongamano vijana wote kutoka nchi zote wanachama wanashirikiana ili kufanikisha kongamano hilo. Pia watu wanaohudhuria kwenye makongamano ya CHAWAKAMA ni wengi kiasi cha kutosha. Kwa hiyo hawa vijana wanaporudi nchini mwao wanakuwa mabalozi wazuri wa lugha ya Kiswahili nchini mwao, kwa hiyo kwa kufanya hivyo vijana wengi watakua wamekielewa CHAWAKAMA vizuri na na hivyo watakuwa wameunganishwa na vijana wenzao wa Afrika mashariki.
                                                                        [Image: IMG_0283.JPG]
GAVANA WA JIMBO LA NGOZI

                                                              [Image: IMG_0285.JPG]
WANACHAWAKAMA WAKIONESHA USHIRIKIANO

Kupitia CHAWAKAMA vijana wengi wamehamasishwa kuuthamini umoja wa Afrika mashariki na vijana pia wamekuwa na mwitikio mkubwa sana. Kwa mfano kongamano la mwaka jana (2012) lililofanyika Burundi lilitoa hamasa kubwa kwa vijana wa Burundi na hata taifa zima la Burundi juu ya dhana ya umoja wa jumuiya ya Afrika mashariki. Kabla ya hapo warundi wengi waliamini kuwa lugha ya Kiswahili, si lugha ya kistaarabu – ni lugha ya majambazi, wezi, lugha ya watu wajanjawajanja kwa hiyo sio lugha ya kujifunza na kuifahamu. Lakini baada ya CHAWAKAMA kufanya kongamano Burundi vijana wenyewe wa Burundi walikiri kuwa waliielewa vibaya lugha ya Kiswahili hii ni baada ya vijana wa CHAWAKAMA kushiriki katika shughuli za kijamii ambapo walisaidia kosomba mawe kwa ajili ya jengo la serikali katika ofisi ya Gavana wa jimbo la Ngozi. Gavana huyo alifurahishwa sana na kitendo cha wanaCHAWAKAMA na akaahidi ataaliita hilo jengo kwa jina la “Jengo la vijana wa Afrika Mashariki”. Kwa hiyo kitendo hiki pia kilijenga hisia za umoja ndani ya vijana hawa wa CHAWAKAMA lakini pia kiliacha mawazo mapya juu ya lugha ya Kiswahili, kwamba sio lugha ya majambazi, na watuwasio wastaarabu bali ni lugha ya watu wenye utu, heshima na watu wanaopenda umoja na ushirikiano.
Changamoto katika CHAWAKAMA
Kama tulivyokwisha ona hapo nyuma CHAWAKAMA ni chama kinachowahusisha wanafunzi. Kwa mazingira haya ni dhahri kwamba hata uwezo wa kujiendesha ni mdogo sana. Mapato yake hutekemea michango ya wanafunzi ambayo pia ni kazi sana kuipata, kwa hiyo chama hujikuta kinashindwa kufikia malengo yake kutokana na ukosefu wa pesa za kujiendesha. Na kwa hiyo hali hii inasababisha chama kuwa na maendeleo hafifu sana.
Jambo linguine ni kutotambulika kwa chama katika vyombo husika vya serikali. Kwa mfano hapa Tanzania, CHAWAKAMA hakitambuliki serikalini hii ina maana kwamba chama hakina usajili wa kudumu. Kwa kweli hii ni changamoto kubwa sana, hali hii inasababisha hata chama kinapowaendea watu wa serikalini kuomba misaada kwa ajili ya kufanikisha malengo fulani inakuwa ni vigumu sana kuipata kwani chama hakitambuliki serikalini. Chama kinaposajiliwa kinapata utambulisho rasmi serikalini na hii inakuwa rahisi kwa chama kuendesha shuguli zake ikiwa ni pamojana na kuandaa machangizo na pia kuomba msaada kutoka vyombo vya serikali vinavyohusika na kuweza kusikilizwa au hata kusaidiwa.
Sasa tunaweza kusema tatizo lipo wapi? Kwa nini chama hakijasajiliwa hadi sasa hivi? Mi nadhani viongozi wenye dhamana wa CHAWAKAMA hawajawa makini na suala hili, kusajili chama hakuhitaji pesa nyingi, ni pesa kidogo sana! Na usajili sio wa kuzunguka kiasi hicho, hata pesa za ada  za wanachama zinatosha kwa usajili. Mi ningependa kuwashauri viongozi wa CHAWAKAMA Tanzania, kwamba lichukulieni kwa umakini suala hili, kwani chama kitakapotambulika serikalini hata mtakapokwenda kwenye kongamano katika nchi nyingine mtatambuliwa na balozi na pia atawatendeeni vema kwa kuwa mnaiwakilisha nchi huko. Kwa hiyo hakuna sababu ya kuendelea na changamoto hii, viongozi wakiwa makini chama kitapata usajili wake rasmi na hivyo kutambulika rasmi serikalini.
                                                    [Image: IMG_0313.JPG]
OFISI ZA GAVANA WA JIMBO LANGOZI

Mwamko mdogo wa vijana wengi wanaosoma Kiswahili pia ni changamoto inayokikabili chama hiki katika kukua kwake. Tunaweza sema kuwa vijana wengi hawajawa na mwamko wa kutosha juu ya umuhimu wa lugha ya Kiswahili kama kiungo muhimu cha watu wa Afrika Mashariki.Changamoto nyingine katika chama hiki, ni suala la kujitangaza. Chama hakijitangazi vya kutosha, watu wengi hawajui kama kuna uwepo wa CHAWAKAMA, vyombo vya habari vichache sana ndivyo vinajua kuwa kuna uwepo wa chama hiki na kujaribu kukitangaza. Achilia mbali vyombo vya habari mitandaoni nako chama hiki hakionekani, isipokuwa unapotafuta CHAWAKAMA mtandaoni utakutana na CHAWAKAMA-UDSM  ambalo ni tawi tu la CHAWAKAMA lakini hutakutana na wavuti wa CHAWAKAMA kanda au Afrika mashariki. Hili pia ni tatizo, katika enzi hizi za TEHAMA sehemu nzuri na rahisi ya kukitangaza chama ni mtandaoni. Chama kinatakiwa kitengeneze wavuti ambao kwa kweli utasaidia kukitangaza chama, na katika wavuti huo wanaweza kuweka makala na taarifa mbalimbali za chama ambazo pia kwa kweli zitawavutia watu wengi kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Pia kupitia huo mtandao watu wanaweza kujisajili na chama kwa urahisi. Kwa mfano, hivi sasa kuna chama cha ukuzaji Kiswahili duniani CHAUKIDU  watu wanaweza kujisajili na chama hiki kupitia mtandaoni na hii inasaidia kusajili watu wengi kwa urahisi. Kwa hiyo wavuti ni kitu muhimu sana katika kukitangaza chama. Labda nitoe mfano wa CHAWAKAMA-UDSM, toka blogu hii ianzishwe kwa kweli watu wamekua wakiitembelea kwa wingi kutoka pande mbalimbali za dunia, na wengi wanaonekana kufurahishwa na taarifa mbalimbali zinazohusu CHAWAKAMA na makala zilizojapishwa mle zinazohusu Kiswahili ambazo kwa kweli ndio kivutio kikubwa kwa watu wengi wanaotembelea blogu hii. Kwa hiyo unaweza kuona jinsi mtando ulivyo muhimu katika kukitangaza chama.
Wengi wanadhani Kiswahili ni cha watu duni, watu wenye mitazamo iliyopitwa na wakati, kwa sababu hii hawaoni sababu ya kujishughulisha na na Kiswahili. Wao lugha ya kisasa ni lugha za kigeni hasa kiingereza, ukizungumza kiingereza au ukijishughulisha na lugha ya kiingereza ndio utaonekana msomi na kwamba uko makini na taaluma yako, lakini huyu anayejishughulisha na Kiswahili yeye anaonekana kama kakosa jambo la msingi la kufanya. Hali kama hii kwa kweli huwavunja vijana hawa moyo, lakini kwa upande mwingine pia hawatakiwi kuvunjika moyo kwa sababu wanajua kile wanachokifanya. Wao wanaelewa vizuri manufaa ya Kiswahili, na hawa wanojaribu kuwavunja moyo wanakua bado hawajaelewa kwa nini nyinyi mnajishughulisha na lugha ya Kiswahili. Kwa hiyo jambo la msingi ni kuwaelimisha na kuwaondo huo ujinga.
Sasa unaweza kujiuliza tutawaelimishaje watu wa namna hii? Makongamano na midahalo ifanyike kwa wingi sana. Makongamano yakifanyika kwa wingi sana, kile kinachozungumzwa kitakaa masikioni mwa watu kwa kujirudiarudia na hatimaye wataanza kuzinduka. Hii itawezekana endapo tu chama kitakuwa na uwezo wa kutosha kifedha. Uandaaji wa makongamano na midahalo huhitaji pesa.
Wito kwa serikali za Jumuiya ya Afrika Mashariki
                                                  [Image: IMG_0300.JPG]
WANACHAWAKAMA WAKIWAJIBIKA

Lugha ya Kiswahili inatambulika rasmi katika katiba ya Kenya kama lugha ya taifa na katika rasimu ya katiba ya Tanzania ya 2013 Kiswahili kimetambuliwa sio kama lugha ya taifa tu bali pia tunu ya taifa. Kama tunu ya taifa ina maana kwamba ni hazina muhimu sana ya taifa letu ambayo kwa gharama yoyote ile taifa halitakubali kuipoteza. Na kama kweli serikali hizi zinataka Kiswahili kiendelee kuwa tunu na lugha ya taifa ni lazima kuwekeza katika lugha hii. Serikali zithamini mchango wa CHAWAKAMA katika kuendelza na kukuza lugha ya taifa na hivyo ziwe tayari kuwasaidia vijana hawa pindi wanapowaendea na pia ziweke jitihada za maksudi katika kuchangia maendeleo ya lugha ya Kiswahili.Vijana wa jumuiya ya Afrika mashariki wameamua kuuenzi utamaduni wao kwa vitendo, hamasa ya vijana hawa imekua na mvuto mkubwa sana kwa watu wengi. Hawakusukumwa na mtu yeyote lakini kwa kuona kuwa Kiswahili ni chombo muhimu sana cha kuweka watu wa jumuiya ya Afrika mashariki kwa pamoja ndio wakaamua kuunda chama hiki. Swali langu ni hili; ina maana viongozi wa Afrika mashariki kama kweli nia yao ni kuwa na jumuia ya Afrika mashariki yenye umoja hawaoni kwamba Kiswahili ni njia muhimu ya kutia hamasa kufikia lengo hilo? Watu wakiwa wanazungumza lugha moja wataona kwamba wao ni wa moja na hata itatia hamasa ya ushirikiano na hivyo lengo la Afrika mashariki yenye umoja litatimia. Kama kweli na wao wanaamini Kiswahili ni nyenzo muhimu ya kuwaunganisha wanajumuiya ya Afrika mashariki sioni kwa nini wanashindwa kuwekeza katika vikundi vinavyojaribu kutumia lugha ya Kiswahili kuwaunganisha wanajumuiya. SOMA ZAIDI HAPA >>>>

Print this item