CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI - Printable Version +- JIFUNZE KISWAHILI (https://jifunzekiswahili.co.tz) +-- Forum: My Category (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=1) +--- Forum: Maendeleo ya Kiswahili (https://jifunzekiswahili.co.tz/forumdisplay.php?fid=11) +--- Thread: CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI (/showthread.php?tid=1143) |
CHANGAMOTO ZINAZOATHIRI MAENDELEO YA KISWAHILI - MwlMaeda - 09-06-2021 Pamoja na mafanikio hayo ,zimekuwapo changamoto kadhaa zinazoathiri maendeleo ya Kiswahili. Baadhi ya changamoto hizo ni:
Upotwashwaji wa Kiswahili hutokea kwa namna kadhaa mfano ni wa uchanganyaji wa Kiswahili na kingereza na pia kutumia Kiswahili kwa maneno yasio yanifu na pia utumizi wa Kiswahili ulioathiriwa na sarufi ya lugha za kikabila hususan kimatamshi na kimuundo.
Tatizo la kutokithamini Kiswahili miongoni mwa wanajamii ni changamoto ya kuathiriwa na kasumba za ukoloni ambapo wanajamii huthamini Zaidi lugha za kigeni hususan kingereza.
Hii ni changamoto nyengine ambapo Kiswahili hakina uwiano wa kimatumizi katika nchi nzima, tofauti hizi zipo kutokana na jamii moja na nyingine kuathiriwa na lugha mama.
Juhudi za ukuzaji Kiswahili zinaonekana hazina mashiko kutokana na kuwepo idadi kubwa ya vyombo vya ukuzaji Kiswahili ambayo havina mshikamano wa pamoja kwani kila chombo kina malengo,sera, na mipango ya yake ya uendeshaji wa Kiswahili.
Uhaba wa wataalamu katika vyombo vya ukuzaji wa Kiswahili husababisha vyombo kutofanya na kutekeleza malengo kwa ufanisi.
Ni tatizo jengine linalokwanishwa maendeleo ya Kiswahili kwa kutotekelezwa kwa mpango wa kukitumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia katika ngazi zote za elimu nchini, na hivyo kutoa mwanya hasa kwa lugha za kigeni kama vile kingereza kustawi zaidi na hivyo kuathiri nafasi ya Kiswahili katika jamii.
|