HII NDIYO ETIMOLOJIA YA MANENO ' ALFAJIRI' NA ASUBUHI
Neno Alfajiri katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mwanzo wa muda wa kupambazuka kwa anga katika siku, ambao hudumu kuanzia saa kumi na moja na kabla ya kuchomoza kwa Jua.
2. Muda mfupi kabla ya Jua kuchomoza.
3. Mwanzo wa kitu fulani.
4. Swala inayoswaliwa na Waislamu kati ya saa kumi na moja na kabla ya kuchomoza kwa jua.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili alfajiri ( **fajrun Al-fajr* *فجر/الفجر* ) lina maana zifuatazo:
1. Mwanga wa asubuhi au mawio.
2. Ukarimu au kipawa.
3. Umaarufu.
4. Mali au ukwasi.
5. Hali ya kuondoka kwa kiza cha usiku na kutawala weupe wa asubuhi yaani kupambazuka.
Na neno Asubuhi katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Muda uliopo baada ya alfajiri na kabla ya mchana.
2. Wakati,kati ya kuchomoza kwa jua na kabla ya kuanza adhuhuri.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *asubuhi* ( **subhun/Al-Subhu (soma: As-Subhu* *صبح/ الصبح* ) lina maana zifuatazo:
1. Pambazuko la asubuhi; mawio.
2. Moja kati ya Swala Tano za faradhi kwa Waislamu ambayo huswaliwa kati ya kuchomoza kwa Alfajiri na kuchomoza kwa jua.
Ni dhahiri kuwa, maneno haya yalipoingia katika Kiswahili yalijikita na yale yaliyo mashuhuri katika maisha ya Waswahili nayo ni: wakati na Swala na kuacha maana nyingine katika lugha ya asili - Kiarabu.
Neno *Sakafu* katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Eneo la chini aghalabu ndani ya nyumba lililosakafiwa./eneo la chini aghalabu katika nyumba lakini hata nje ya nyumba ambalo hujengwa kwa mawe na mchanga uliochanganywa na saruji na kisha hutandazwa rojorojo ya saruji.
2. Sakafu moja au zaidi inayojengwa juu baada ya dari ya kwanza ya jengo la ghorofa; horofa.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili *sakafu* ( **saqfun/saqfan/saqfin* *سقف* ) lina maana zifuatazo:
1. Paa la nyumba na mfano wake lililo juu mkabala na ardhi ya sehemu husika.
2. Mbingu/ kitu chochote kilicho juu chenye kufunika.
Kinachodhihiri ni kuwa neno hili ( *sakafu*/ *saqf* *سقف* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili lilichukua maana ya neno ' *dari* ' katika lugha ya Kiarabu wakati neno ' *dari* ' likichukua maana ya neno ' *sakafu* '.
10. Likiongezwa neno 'Al-Harb' kikawa 'Daaru Al-Harbi' (soma: Daarul Harbi': miji ya maadui.
Katika Lugha ya Kiarabu neno sakafu ( *saqfun/saqfan/saqfin* *سقف*) ndio linalobeba maana ya neno 'dari' katika Kiswahili, 'sakafu ya juu ya nyumba iliyo baina ya paa na kuta za nyumba'.
Hii inaonesha kuwa neno hili ( *dari* ) lilipoingia katika lugha ya Kiswahili maana yake katika lugha yake ya asili (Kiarabu) ilibadilika na kuchukua maana mpya zilizobainishwa.
Neno Mrabaha (wingi: Mirabaha) katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Kiasi kinacholipwa na mchapishaji kwa mtunzi wa kitabu kwa kipindi fulani kutokana na mauzo ya kitabu husika.
2. Faida inayopatikana kutokana na biashara fulani.
3. Ushuru anaotozwa mfanyabishara au mwekezaji na mtu aliyemkodisha eneo au mtaji.
4. Malipo yanayotolewa na mfanyabiashara kwa mtu aliyempa mali au mtaji wa biashara.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili mrabaha ( muraabahatunمرابحة) lina maana zifuatazo:
1. Jumla ya rasilimali na ziada maalumu (faida).
2. Kumpa mtu mtaji ili aufanyie biashara kwa makubaliano ya kugawa faida kwa namna mliyokubaliana.
3. Biashara inayolenga kupata faida fulani.
Katika Sarufi ya Kiarabu neno (nomino) muraabahatمرابحة linatokana na kitenzi cha Kiarabu raabaha رابح (amefanya la kumletea faida) na jengo la kitenzi hiki linaashiria kitendo kilichofanywa kwa ushirikiano wa watu wawili au zaidi (mushaarakah).
Utaona kwamba neno hili lilipoingia katika lugha ya Kiswahili halikuiacha ile maana ya lugha yake ya asili nayo ni kufanya muamala kwa lengo la kupata faida.
Neno Maskani katika lugha ya Kiswahili ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mahali kiumbe anapoishi kama vile nyumba au eneo.
2. Mahali ambapo watu aghalabu wafuasi wa chama fulani cha siasa hukutana na kuzungumza.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili (maskani) lina maana zifuatazo:
1. Makazi/Makaazi.
2. Nyumba.
Katika Sarufi ya Kiarabu kinapoongezwa kiambishi 'ma' mwanzoni kwa neno la msingi (mzizi) hutengeneza neno lenye maana ya eneo linapofanyika tendo linalohusiana na maana ya mzizi huo na hasa mzizi wa kitenzi.
Kwa mfano neno la Kiarabu 'darasa درس' (amesoma) kinapoongezwa kiambishi 'ma' mwanzoni kwa Sura ya neno (maf-al/maf-il) yaani (madrasa مدرسة) hutengeneza neno (nomino) lenye maana ya mahali tendo la kusoma hufanyika.
Pia kitenzi cha Kiarabu kataba كتب (ameandika), kinapoongezwa kiambishi 'ma' kwa namna iliyotangulia kuelezwa hupatika neno (maktab/maktaba مكتب/مكتبة) lenye maana ya mahali ambapo kitendo cha kuandika hufanywa. Ndipo neno hili (maktab/maktaba) katika Kiarabu likapata maana ya ofisi, dawati, meza ya kuandikia, mahali panapohifadhiwa vitabu kwa nia ya kujisomea.
Ndipo pia tunapata kutokana na kitenzi cha Kiarabu 'sakana سكن' (amekaa/amefanya makazi) baada ya kuongezwa kiambishi 'ma" mwanzoni mwake neno 'maskani مسكن' lenye maana ya mahali pa kukaa/makazi.
Utaona kuwa neno hili 'maskani' lilipoingia katika lugha ya Kiswahili limeongezewa maana ya mahali ambapo watu hukutana na kuzungumza.
Neno Hayawani (wingi: mahayawani) katika lugha ya Kiswahili, ni nomino yenye maana zifuatazo:
1. Mnyama wa porini, mnyama yeyote yule.
2. Mtu mwenye tabia za kinyama, mtu anayefananishwa na mnyama, aghalabu mtu asiye na aibu.
3. Mwehu, kichaa, mwendawazimu au chizi.
4. Shetani.
Katika lugha ya Kiarabu, neno hili (hayawani) lina maana zifuatazo:
1. Kila kiumbe hai kinachosema na kisichosema.
2. Kiumbe hai kinachojipambanua kwa kuwa na uhai, hisia na harakati. Kwa mfano "mwanadamu" huitwa *"hayawanun naatwiq حيوان ناطق yaani mnyama anayeongea"*
3. Uhai (maisha) kama ilivyondikwa katika Qur'aan Tukufu Sura ya 29 (Surat Al-Ankabuut), Aya ya 64 kuwa: WAINNAD DAARAL AAAKHIRATA LAHIYAL HAYAWAANU وان الدار الآخرة لهي الحيوان ( *Na hakika nyuma ya Akhera ni nyumba ya maisha/uhai (wa milele* )).Hapa "hayawaanun" imekuja kama "maisha".
Kwahiyo,utakuja kuona kuwa, neno hili "hayawani" lilipoingia katika lugha ya Kiswahili limeongezewa maana ambazo hazimo katika ile lugha yake ya asili - Kiarabu kama vile:
1. Mwehu, kichaa, mwendawazimu, na chizi.
2. Shetani.
Ama neno hili la neno 'hayawani' kutumika kwa maana ya 'mtu mwenye tabia za kinyama au mtu anayefananishwa na mnyama yaani aghalabu mtu asiye na "aibu", Waarabu hawalitumii neno hili kwa maana ya moja kwa moja bali hutumika kama *tashbihi baligh* (kutumia tashbihi bila kiunganishi 'kama' - chombo cha kushabihisha) ukasema:
"Fulani ni mnyama" badala ya kusema: "Fulani ni kama mnyama."
Faida :
Katika lugha ya Kiarabu, tashbihi yaani katika Taaluma ya Bayaani- Rhetoric (Utanzu wa Balagha - The Art of Eloquence) ina nguzo nne:
1. Mushabbahun- kinachofananishwa.
2. Mushabbahun Bihi- kinachofananishiwa.
3. Adaatut Tashbiihi- chombo cha kufananisha.
4. Wajhu Al-Shabahi- sura ya mfanano.
Kwahiyo naposema: 'Jemedari wetu ni kama simba' basi:
1. Jemedari ni Mushabbahun.
2. Simba ni Mushabbahun Bihi.
3. Kama ni Adaatut Tashbiihi.
4. Wajhu Al-Shabahi (sura ya mfanano) inaweza kuwa ushujaa, ukali na nyinginezo miongoni mwa sifa bainifu za simba.
(ii) Mofu kapaNi mofu za pekee ambazo hazina umbo. Mofu kapa hazitamkwi wala kuandikwa. Mofu kapa hazionekani katika neno lakini athari zinazotokana na mofu kapa hueleweka.Mfano; Umoja wingi U-kucha – ⱷkucha U-kuta – ⱷkuta U-funguo – ⱷfunguo
Nomino zilizo na kiambishi cha wingi tu cha umoja hakipoMfano; umoja wingi ⱷkasha Ma – kasha ⱷdebe Ma – debe ⱷjembe Ma – jembe
(b) Fasili ya neno kileksika, kimuundo na kisarufi (i) Fasili ya neno KileksikaNeno ni kipashio kidogo cha lugha chenye maana. Kwa maana hiyo neno ni lazima liwe na maana inayoeleweka kwa jamii inayotumia lugha hiyo. (Mdee, 1977).Mfano: Mama- Mzazi wa kike Ndama- Mtoto wa ng`ombeDhana hii ina mashiko kwa sababu maneno mengi katika lugha yana maana ya kueleweka kwa watumiaji wa lugha.
Udhaifu wa fasili hiiSi kila neno linalotumika linaweza kuwa na maana ya wazi au ya kileksika. Mfano baadhi ya maneno hasa viunganishi na vihusishi kama vile ya, kwa, na, wakati ambapo yanakua hayana maana ya kileksika lakini yana uamilifu kisarufi.
(ii) Fasili ya neno kimuundoNeno ni kipengele kidogo kabisa cha sentensi ambacho kinaweza kuhamishwa kutoka nafasi moja hadi nyingine bila kuathiri sarufi ya lugha katika tungo au sentensi hiyo (cruse, 1986) akinukuliwa na (Mdee, 1997). Kwa ujumla hapa kinachotazamwa zaidi ni kategoria za maneno na mpangilio wake katika tungo.
Mfano: Ali alimuua Ahmed N T N Ahmed alimuua Ali
N T NHapa N ni nomino na T ni kitenzi japo nomino zimebadilishana nafasi lakini sarufi hiyo haijaathirika. Utaratibu huu husaidia katika kujifunza sarufi ya lugha hasa miundo ya tungo kama kirai, kishazi na sentensi na pia kujua sehemu za tungo kama kiima na kiarifu.Udhaifu wa fasili hii· Sio maneno yote yanaweza kuhamishwahamishwa bila kuvuruga sarufi ya lugha
Mfano; Ali alisimama kando ya mto Amesimama kando ya mto Ali Kando ya mto Ali amesimama *Mto Ali amesimama kando ya *Mto ya kando amesimamaHivyo sentensi mbili za mwisho hazikidhi haja ya usahihi wa kisarufi.· Vilevile unapohamisha maneno basi maana ya neno pia hubadilika.
Mfano; Zubeda anampenda Zawadi Zawadi anampenda Zubeda
Nomino zimebadilishana nafasi hazijaathiri sarufi ya lugha lakini kimaana imebadilika kwa sababu katika sentensi ya kwanza Zubeda ndiye anatenda tendo na katika sentensi ya pili Zawadi ndiye anatenda tendo.
(iii) Fasili ya neno kisarufi Kwa mujibu wa Katamba (1993:19) ili neno litambulike lazima liwe katika muktadha wa matumizi. Katamba anasema neno moja linaweza kuwa na dhima mbalimbali na dhima hiyo itagundulika tu litakapokuwa ndani ya muktadha wa matumizi kwenye sentensi. Anatoa mfano wa neno la kiingereza “cut” kwamba likiwa kipwekepweke mtu hawezi kutambua linarejelea nini pamoja kwamba neno hilo katika lugha ya kiingereza ni kitenzi yaani ‘kata’ lakini kuna wakati linaweza kutumika kurejelea nomino. Mfano I need my cut na I have cut my fingure. Ukichunguza vizuri mifano hii ‘cut’ katika sentensi ya kwanza hurejelea nomino na katika sentensi ya pili hurejelea kitenzi. Sentensi ya kwanza ilikuwa na maana ‘nahitaji stahiki yangu’ na ya pili ina maana ya ‘nimekata kidole’.
Kigezo hiki huenda mbali kwa kufafanua kuwa pia maneno kama ‘na’, ‘tu’, ‘si’ katika Kiswahili na maneno kama ‘and’, ‘an’, ‘the’ ‘on’ katika kiingereza nayo hayawezi kutambulika yanarejelea nini, lazima yawe katika muktadha wa matumizi ndio tunaweza kusema ni aina gani za maneno na kutambua maana zake.
Udhaifu wa fasili hii Si lazima maneno yote yawe katika muktadha wa matumizi ndipo tuweze kubaini maana zake kwani kuna baadhi ya maneno huweza kutambulika kuwa yana maana gani hata yasipokuwa katika muktadha wa matumizi katika sentensi. Kwa mfano nomino za mahali kama vile Dodoma, Mwanza na Morogoro na majina ya watu kama vile Amina, Omari, Magreth na Ali.
HITIMISHOHivyo basi katika kufasili dhana ya neno ni vyema kuzingatia vigezo vyote vya kisarufi kama vile fonolojia, maana, sarufi ili kupunguza changamoto zinazojitokeza katika kufasili dhana hii kama ilivyobainishwa hapo juu.
MAREJELEO:
Besha, R.M. (2007). Utangulizi wa Lugha na Isimu. Dar es Salaam: Macmillan Aidan Ltd.
Habwe, J. & Karanja, P. (2007). Misingi ya Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Phoenix Publishers.
Katamba, F. (1993). Morphology. London: Macmillan Press Ltd.
Massamba, D.P.B na Wenzake. (2013). Fonolojia ya Kiswahili Sanifu. Dar es Salaam: TUKI.
Matinde, R.S. (2012). Dafina ya Lugha Isimu na Nadharia: Kwa Sekondari, Vyuo vya Kati na Vyuo Vikuu. Mwanza: Serengeti Educational Publishers (T) Ltd.
Mdee, D. (2007). Nadharia za Leksikografia. Dar es Salaam: TUKI.
TUKI. (1990). Kamusi ya Isimu na Lugha. Dar es Salaam: TUKI